Mzee alifika ofisi ya mambo ya usalama, akabisha hodi, na
kuingia sehemu ya maelezo akaelezea shida yake kuwa anataka kuonana na mkuu wa
mambo ya usalama, akahojiwa ana shida gani, akajieleza, lakini hakusema undani
wa kile alichokuwa nacho.
‘Ninaitikia wito wa mkuu, kuwa kila mwenye jambo la kusaidia
kwenye hii vita ya kupambana na mdudu mtu na uchawi wa malegeza ajitokeze ...’akasema
‘Una ushahidi gani..?’ akaulizwa
‘Je ina maana tunatakiwa kujielezea kwako maana nijuavyo mimi
tumeambiwa tukajieleze moja kwa moja kwa mkuu…’akasema
‘Sawa usijali..ni lazima nikuulize hivyo, kwani kujieleza tu
haitoshi, muhimu ni ushahidi..’akaambiwa
‘Usijali….’akasema na yule mdada akaelekea ofisi
iliyoandikwa, ‘Mkuu wa mambo ya usalama, na akaingia humo, baadae akatoka.
‘Haya unaona mlango huo hapo mbele, ingia mle , utakutana na
mtu ambaye atakuelekeza cha kufanya…’akaambiwa, na yeye akafanya kama alivyoagizwa, lakini kila
hatua alihisi moyo ukimuenda mbio, …wasiwasi na mashaka.
Alipoingia kwenye hiyo ofisi akakutana na mtu mwingine
mwanaume kavalia kikazi, akaulizwa maswali machache, ..jina wapi anapotoka,
umri….halafu akaonyeshwa sehemu ya kukaa, na kuambiwa asubirie kidogo, na
haikupita muda mara akaingia huyo mkuu mwenyewe akiwa kavalia mavazi yake ya
kazi,..begani kumechafuka;
‘Samahani ndugu kwa kukuchelewesha kidogo,..najua wewe
umekuja kutoa ushirikiano…..na nafahamu kuwa usingelifika hapa kama kweli huna
taarifa muhimu sana,..sisi ni watu wenu, tunahitajia msaada wowote kutoka
kwenu, …usiwe na shaka kabisa, usalama wako utalindwa…’akaambiwa
‘Ndio mkuu, …mimi siogopi tena kuhusu usalama wangu …mungu mwenyewe
anatosha, ninachotaka ni kusema ukweli,…maana mimi kama mzazi ni mmoja wa waathirika
wa matatizo haya yanayoikumba nchi yetu,…na kwa vile nimeshaumizwa, ..basi
sioni haja ya kunyamaza, kama nikuniua waniue tu….’akasema mzee
‘Usijali kabisa..hakuna mtu wa kukuua…niamini mimi…haya sema
unajua nini na kwa ushahidi gani….yule pale kazi yake ni kuandika kila kitu
unachoongea, na nia ni kuweka kumbukumbu zetu za siri, ..hazitatoka hapa mpaka
tujirizishe…unaelewa eeh?’ Akaulizwa, na kabla hajaanza kuongea mara simu ya mkuu
huyo ikapigwa, na mkuu akaiangalia, na kwa haraka akaizima, huku akiwa kakunja
uso, kuashiria kukasirika hivi...
‘Mkuu…mimi ni mkulima na mfugaji lakini fani yangu nyingine
mimi ni mpiga picha,…..’akaanza kujieliezea kwa kirefu tu, na jinsi gani
alivyoweza kukutana na tukio,…
‘Nililiona lile gari mahali aple, nikajua ni vijana wako wapo
kazini,..….’akasema
‘Lipoje hilo gari?’ akaulizwa
‘Lile gari la landrover lina michirizi mekundu, unalitumia
sana wewe ukitutembelea kijijini…..’akasema
‘Gari langu la kazi, lilifikaje maeneo hayo….Ok, …..ilikuwaje…?’
akaulizwa
‘Ninajua ni vijana wako wanalitumia, nilijua wapo kazini,,….lakini
cha ajabu nilichokiona ni hiki hapa…’akasema na kutoa zile picha alizokuwa
nazo,…
Mkuu, alishikwa na mshituko, …na macho yake yalishindwa
kuficha mshangao,….akasema
‘Shiit…hawa vijana watanitambua, ina maana wanatumia gari la
serikali kwa mambo yao binafsi, sasa kuna nini cha ajabu ulikiona, maana kweli
hili gari letu, mhh,..hebu ngoja, hebu hiyo picha nyingine,…wanaaah,..yap, huu
ni ushahidi safi sana, kumbee, sasa nimewabamba, nilikuwa nahisi jambo kama
hili…ngoja, …’ mkuu huyu, akatoka kidogo baadae akarudi…
‘Samahani ndugu yangu, unajua hili tatizo ni kubwa sana,…na
imenipa changamoto kuwa niwe makini sana, kuna watu wamenizunguka, na ….wanaweza
hata kunichafulia ofisi yangu, sasa ni hivi..huu ni usahidi muhimu sana kwetu,..huwezi
kuondoka na hu ushahidi, nilitaka taaribu zote zifuatwe, hawa vijana wakamatwe
mara moja, ..’akasema akiwa kama anawaza jambo.
Baadae akachukua mfuko wa nailon, akaandika juu yake,…’Ushahidi…no,….kutoka
kwa shahidi….’
‘Tumbukiza humu…..’akasema
‘Mwandishi umeshaandika kila kitu, nipe hiyo nakala aweke
sahihi yake,…’akasema akiongea na yule mtu mwingine aliyekuwa akiandika,…
Mzee akaanza kusoma kilichoandikwa mle,..waliandika kila kitu
alichoongea kwa usahihi mkubwa, alipojirizisha, akaweka sahihi yake kwenye zile
karatasi,.
‘Sasa kazi iliyobakia
ni yetu sisi kulifanyia hili kazi..ninashukuru sana, tukipata watu kama nyie,
basi kazi hii itakuwa rahisi sana…’akasema huyo mkuu.
‘Umesema unaishi wapi…’akaulizwa na yeye akajieleza.
‘Sasa usije kuongea lolote kwa mtu yoyote kuwa ulifika
hapa..tunahitajia usalama wako,..ili wakati ukifika uwepo…wewe ni mtu muhimu
sana kwetu…, nina imani, muheshimiwa akipata hii taarifa utakuwa miungoni mwa
watu watakaozawadia donge nono…’akasema mkuu huyu akitabasamu.
‘Hamna shida mkuu..nimetimiza wajibu wangu….’akasema huyo
mkuu.
Baadae aliaga na kuondoka kwenye hiyo ofisi, …
***********
Ni siku ya pili kilio kikasikika, ….na mara kukaonekana kundi
la watu wakiwa kwenye pori la jirani, kwenye kijiji anachotoka mzee, mpiga
picha, …na taarifa zikazagaa…!
‘Mwili wa mpiga picha umepatikana porini , akiwa kajinyonga…..’
Taarifa zikafika kwa mkuu wa mambo ya usalama….
‘Haiwezekani……’ndio kauli yake ya kwanza alipopokea taarifa
hiyo!
'Vita imeanza…..hawatashinda...tutaona.....'alisema mkuu huyo.
WAZO LA LEO: Vita ya haki hupiganwa kwa haki,..na watakaoshinda
ni wale waliosimamia hiyo haki bila kupindisha, ..watetezi wa haki hawatarudi
nyuma, wakijua kuwa wanachokitetea ni cha haki . Kamwe haki haichanganywi na
batili….!
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
Hongera xaaaaana
Tatizo humaliziii stori zako,....
i like your style, just like a movie...
Post a Comment