Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, January 27, 2017

NI NANI ZAIDI(Kienyeji au Kisasa)



NI NANI ZAIDI (kisasa na kienyeji)
Niliamua kufuga kuku, kwanza nilianza na kuku wa kienyeji, najua kuku hawa hawana gharama sana, na wanazaliana haraka haraka tu kwahiyo nikawa nao wengi.

Baadae nikaona nijaribu na kuku hawa wanaoitwa wa kisasa kama naweza nikapata matunda bora zaidi. Niligundua kuwa kuku hawa wa kisasa wanahitajia gharama kubwa kidogo, utunzaji na ufuatiliaji pia.

Kipindi cha mavuno niliona ubora wake, kuku hawa wa kisasa japokuwa nilitumia gharama nyingi, lkn matunda yake yalikuwa zaidi ya wale kuku wa kienyeji. Kuku waliwakuwa na afya wazito na nyama nyingi tu...achilia mbali mayai.

Nikawa najiuliza nifanyanyeje ili hata hawa kuku wa kienyeje watoe matunda bora. Nikaona niwachanganye, kuleta usawa na ushindani. Ni kujaribu tena.

Mhh ikazuka zogo, kuku wa kienyeji wakawa hawatulii, wanataka kutoka nje kutembea huku na kule na hata ukiwawekea chakula kwenye vyombo vyake, wanavichakarua mpaka vyakula vyote vinaishia chini.. ndio raha yao..wamezoea hivyo.

Nikagundua kitu...ni mazingira yao tokea awali, ni hulka ndio imewafanya wawe hivyo...mhh, ndio maana wanaitwa kuku wa kienyeji. Ni mazingira yamewafanya hata makuzi, uzalishaji wao, gharama na hata matunda yake yatofautiane.

Wakati nawazia kuhusu huu mradi wa kuku, mara nikasikia matokeo ya mitihani ya kidato cha pili. Shule gani zimefanya vyema, na shule gani zimefanya vibaya. Ni yale yale....

Nikajiuliza hivi hawa wanaotathimini wamewekaje mizania sahihi...maana tathimini yao haikujali shule hizo zipoje kimazingara, watoto wote wamechukuliwa kama wanasoma kwenye mazingira sawa,....sijui, lkn kwa hali hii sioni kama kuna usahihi wa kulinganisha.

Nilikumbuka shule zetu tulizosomea, unatoka nyumbani na njaa,unatembea umbali mrefu, jua mvua la kwalo..ukifika shuleni umechoka bado, kuna kufanya usafi, au kumwagilia bustani na mkiingia darasani, mazingira yake mnayafahamu wenyewe.

Haya twende kwa huyu mwalimu, ...jamani walimu wengine wanafika darasani wanapiga miayo ya njaa, kichwani wana madeni lukuki...akili ipo kwenye matatizo, na bado anatakiwa kuwafundisha watoto waliojazana, hadi wengine wanakaa chini..nini kitakachofanyika, mwalimu huyu, kama hana wito, atafundisha tu bora siku ipite. Hapendi lakini atafanyaje!

Nenda shule za wenzetu, wenye uwezo,...ni haki yao, wamejaliwa , maana hata vidole havilingani,...mwalimu huyu anafika shuleni na gari, suti..kashiba, hana shida, akili yake ni kufundisha tu. Na hata watoto wake waliopo darasani wameshiba, wasafi...vitabu nk...kila kitu kipo. Hivi hawa wanavuna matunda gani, ni nini matokea yake, hawa kweli watafeli mitihani?

Mwisho wa siku hawa wanalingwanishwa NI NANI ZAIDI, .SHULE GANI BORA, NI MWANFUNZI GANI KAFANYA VYEMA.

Kwa uoni wangu, tuangalie namna nyingine bora ya kuwashindanisha hawa wanafunzi.
Ni sawa nia ni kuleta usawa, lkn mbona usawa huo hatuuangalii tokea awali, tukaangalia hata mazingira na walimu wake....

Mhh,. jamani mimi NAWAZA TU!


Ni mimi: emu-three

No comments :