Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, January 25, 2017

Muungwana lake MoyoniMuungwana lake moyoni.

‘Ni kweli nimeamua kuoa…na nimemuoa huyo huyo uliyeambiwa..’ilikuwa kauli ya jamaa yangu mmoja, sikuamini niliposikia kaoa, na kumuoa yule yule…., na nilipokutana naye nikamuuliza, hakusita kunijibu, japokuwa mwanzoni hakuonekana na raha.

‘Hongera,..’nikanyisha mkono kumpongea,kwanza akatabasamu na baadaye akatikisa kichwa.

‘Nashukuru, ahsante…’akasema

‘Lakini wengi wanauliza imekuwaje jaje, maana siku zote ulikuwa ukimkashifu huyo mdada, na ulimweka kwenye kundi baya, na ukafikia hata kusema, atakayemuoa huyo kala hasara, je umakubali kula matapishi yako wewe mwenyewe..?’ nikamuuliza

‘We acha tu, …na awali nilikuwa naona aibu sana, lakini baadae nikajirudi , nilijiuliza ni kwanini nione aibu, ni kwanini nijiskie vibaya, hapana, ….sasa nasonga mbele, huyo ni mke wangu, na nimeanza kumpenda, hata yeye haamini…’akasema

‘Mhh hongera, …lakini bado sisi tunajiuliza kulikoni?’ nikamuuliza

‘Kwanza aminini kuwa lipangwalo na mungu halikwepeki, hilo kwangu nimeliamini sasa kwa ushuhuda… ama kwa kujitetea, ni kuwa, ..mmh, ilitokea tu, siku moja, nikaingia kwenye anga zake, na..tahamaki nikanasa, ...’aktulia kidogo.

‘Rafiki yangu mimi siwezi kuongea kwa undani zaidi, lakini siri ya kwanini nimemuoa, ipo ndani ya moyo wangu. …kwani nimeamini uzuri wa sura, umbo,..havina maana sana kwenye ndoa, …muhimu ni nini unachokipata kwake,…nimerizika, na sijuitii tena…na ..we acha tu, nampenda sana mke wangu…hamjui ni nini ninachokipata kutoka kwake…siamini na nashukuru mungu! ’aliyatamka hayo maneno akitabasamu.

‘Sasa mbona awali nilikuona kama  huna raha…?’ nikamuuliza
‘Usoni, sawa…si unajua tena, uso umeumbwa na aibu..kwa yale niliyokuwa nikiyasema, nikawa namkashfu binti wa watu…nimejuta na nimemuomba sana msamaha…usoni ndio hivyo, ,lakini moyoni, nipo ok…muungwana lake moyoni au sio…’akasema na sikupenda kumdadisi zaidi, nikaona niliandike hili  kwenye shajara yangu, kwa nia ya kutoa maadili kwa wanandoa, na wanaotaka kuoa.

Kwani kuna marafiki zangu wanatarajia kuoa na kuolewa, …mimi nawatakia kila la heri, ndoa zao zifanikiwe vyema… na wanaotarajia, kutafuta, wachumba, wafanikiwe kuwapata wachumba wema,..Ila nina ushauri tu. Tukumbuke kuwa kizazi huanzia kwenye ndoa, mkishaoana mjue nyie ni chumbuko la jamii nyingine huko mbeleni, kwahiyo tuweni makini sana hapa kwenye kuchagua wachumba.

Tunapofikia umri, wa kuoa, au kuolewa, tufikirie huko mbele ya safari, ya kuwa, sasa mimi natafuta mtu tutakayejenga jamii ijayo, je nataka jamii yangu iweje, maana nyie ni kizazi, na chimbuko la kizazi chenu ndio jamii ijayo, kikiwa kizazi chema, jamii itakuwa njema, na kikiwa kizazi kibaya, jamiii itakuja kuwa mtihani…Sababu ni nyie!

Vurugu nyingi duniani zilianzia hapo, …watu wanafikia kuchukiana, kuuana, na matokea yake ni visasi visivyokwisha, matokea yake ni jamii yenye ubinafsi,..hakuna upendo, kila mtu anajijali yeye mwenyewe, chanzo ni nini, hukutaka kuchunguza, ..hukutaka kumtafuta mke au mume mwema. Uliyekutana naye ulimuona ‘hakuna mwingine’ kisura mrembo,…nani kama yeye, mrs world,… mwenye mwendo wa tausi, kumbe sura na huo mwendo wa nanihii… ulikuwa ni ulimbo tu. Umenasa.

Sina nia ya kuwakatisha tamaa wale wenye taswira zao na malengo yao ya kufunga ndoa, lakini ushauri wangu ndio huo,..tuweni makini sana kwenye kuwachagua wenza wetu wa maisha, tujaribu sana kufikiria mbali, tukitafakari jamii tunayoiandaa, …


Namuomba mwenyezimungu awape mapenzi mema watarajiwa , na atujalie sisi sote tuwapate wake wema, na waume wema, Aamiyn
Ni mimi: emu-three

No comments :