Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, October 7, 2016

UKITAKA KUMUUA MBWA....2‘Ndugu yangu jinasue..huyo ni mke wa mtu,….usije ukaja kujilaumu…’ 

Nilipigiwa simu na mtu nisiyemfahamu akiwa kajibadili sauti, na hayo ndio maneno pekee aliyoyasema hakusema halloh wala nini, alitamka hivyo tu, aliposema hivyo nilitaka kumuuliza yeye ni nani, na kabla sijamuuliza akakata simu…

Nikapanga kuwa nikifika mezani niage niondoke zangu,…. na kiuungwana ilibidi nifike mezani nimalizie , kinywaji changu- ilikuwa soda tu, tena…, sprite,..nilipoimaliza tu , hapo nakumbuka kabisa nikaanza kuhisi vingine…na muda ulivyokwenda akili ikaanza kupoteza mawasiliano…sijui ni kwanini, sikujua ni kwanini,…

Tuendelee na kisa chetu…

                                **********

‘Mimi siwezi kujua ni nani alinifanyia hivyo, maana ni wazi kabisa kuna mtu aliniwekea kinywaji change ulevi,…sasa alikuwa ni nani, nililiwazia hilo mara nyingi, mwenyewe na hata nilipokuwa nikihojiwa na polisi,

Je alikuwa  ni madam, ..haiwezekani, yeye hawezi kinifanyia hivyo….maana siku ile  alikuwa kalewa, na pale mezani alikuwa kakaa mbali kabisa na pale nilipokuwa nimekaa mimi, ile meza ilikuwa kubwa ya kutosha watu sita, na madamu alikaa upande wa mwingine na mimi upande mwingine mbali .

Na hata niliporudi nilimkuta akiwa kakaa pale pale akiongea na hao wazungu…je aliwezaje kufika pale nilipokaa na kuweka kitu,..labda wawe walikuwa na mpango mmoja na hao wazungu…..na kwanini wanifanyie hivyo..na utakuja kugundua baadae kuwa yeye hakuhusika…

Na tukisema labda ni hawo wazungu, …hapana, ili iweje, mimi nina kitu gani na hao wazungu, ili wapate nini kwangu na muda wote, sikuwaona kabisa wakiwa na habari na mimi, zaidi ya kuongea na madam….

Kwahiyo kwa pale sikuona kama kuna mtu wa kumshuku…’akasema

‘Eehe ikawaje…?’ nikauliza

‘Unajua nilipomaliza kunywa ile soda,..ukikumbuka kuwa, nilishapanga kunywa niondoke… lakaini cha ajabu nilipomaliza kunywa fundo la mwisho tu…nikahisi hali tofauti, akili inanituma kufanya mengine, kunywa zaidi….nilijihisi mtu tofauti kabisa.

Nikawa sasa naagiza kinywaji zaidi…. naongea kilevi , na hutaamini, nilianza kuagiza pombe kuwa na mimi ni lazima ninywe

‘Na mimi nataka kunywa, nipeni na mimi pombe…’nikasema…hayo alisimulia muhudumu mmoja ambaye aliyekuwepo, na aliyazungumza hayo, akitoa ushahidi mahakamani..

‘Ila nakumbuka…unajua kila siku ikipita ndio naanza kukumbuka,… nakumbuka kabisa, madam, aliponiona naagiza pombe,….alinikataza, akijua mimi sio mlevi, sinywagi, na nilikuwa namuendesha mimi , japokuwa na yeye huwa anajindeshaka mwenyewe…., japokuwa madam naye alikuwa keshachangamka, lakini alikuwa makini sana,..yeye si kazoea kunywa,…

‘Lakini mimi sikumsikiliza na alipoendelea kunikataza, nikawa namsema ovyo…..unajua tena mimi sijawahi..kunywa, kuwa hiyo pombe ilinichukua kisawa sawa… ikafikia muda nikawa sijitambui…hata kutembea siwezi napepesuka….kilichotokea baadaye, mimi sikumbuki, zaidi ya kuelezewa mahakamani kama ushahidi, na pia walionyesha video ya tukio hilo….’ Akatikisa kichwa

‘Ina maana yote yaliyotokea hukuwa na kumbukumbu nayo,..?’ nikamuuliza

‘Ndio…..sijui kwanini….’akasema

‘Sasa ilikuwaje, ,..maana hapo inaonyesha kuna siri kubwa,..ulipozidiwa ilikuwaje..mliondoka kurudi nyumbani au ilikuwaje….?’ Nikamuuliza.

‘Nikuambie ukweli….akili ilinipotea pale nilipozidiwa ulevi mengine yaliyotokea nilisimuliwa tu, na kuona kwenye hiyo kanda ya video wakiitoa mahakamani kama ushahidi

Na nilianza kujiambua pale nilipozindukana asubuhi….hapana sio asubuhi, usiku wa tukio…’akasema

‘Usiku wa tukio, tukio gani..kulitokea nini..?’ nikamuuliza

‘Hilo tukio ndio kisa cha matatizo yote haya,..hadi nikasweka jela….’akasema

‘Usiku ule…. nilipozindukana nilijikuta nipo kwenye kitanda, …’akasema

‘Kitanda,..! Kitandani kwako…?’ nikamuuliza

‘Hata mimi nilipozindukana nilihisi hivyo, kuwa nipo kitandani mwangu,…kwa akili ya haraka haraka, niliwaziai hivyo, nilijua nipo chumbani kwangu, na….kuzindukana huko,… ilitokana na sauti za ukelele, za kugonga mlango,… ..’akatulia kama anawaza jambo.

‘Nilizindukana na moyo ukawa unanienda mbio, kama mtu kazindukana kutoka kwenye ndoto mbaya, na kichwa kinauma, na kwa jinsi walivokuwa wanagonga mlango ilikuwa kama wanagonga kichwani mwangu..’akatulia

‘Na hata kabla sijajitambua vyema, mara nikasikia wakifungua mlango kwa ufunguo…wakaingia watu, wakawasha taa,…walikuwa eeh, wanne, mmoka kashika mitambo ya kuchukua video, mwingine simu kaielekeza kwangu kama ananipiga picha, wengine wawili wakawa wamesimama mlangoni kama walinzi...

Kwa muda ule..bado akili ….ilikuwa kama sio yangu, na sikujua humo kitandani nilikuwa na nani, maana bado hapo najua nipo kwangu, si unajua tena…lakini akili ikanijia vingine pia kuwa hao ni majambazi wanataka kunidhuru mimi na mke wangu,,,kwahiyo nikageuza kichwa kumuangalia mke wangu.

Niliona mke wangu kajifunika shuka akijikunyata kama kuogopa, au kuona aibu maana hakuwa na nguo…ndivyo akili ilivyotuma hivyo kuwa huyo aliyekuwepo hapo ni mke wangu, na nipo kitandani mwangu, lakini niliposikia mmoja wapo akisema..

‘Na wewe Malaya acha kujifunika, tunahitaji ushahidi kuwa nyie kweli ni wazinzi…kila siku tunasema nyie ni wazinzi, wanabisha, haya sasa ngoja waone huu ushahidi……’ aliposema hivyo nikageuka sasa kumuangalia huyo niliyekuwa naye.

‘Oh…sasa akili ikaanza kufanya kazi, …kumbe nipo na mwanamke mwingine,…nikageza kichwa sasa kumuangalia kwa makini, na akili sasa imetulia,…alikuwa si mwanamke mwingine ni..oh, haiwezekani, tena yupo uchi, haiwezekani, ilikuwaje

Nilianza kuhisi mashaka, kuwa nipo mtegoni, kuna jambo, ..na wakatii huo huyo mwanamke alikuwa kajikunyata kujiziba, kajikumbatia, kujihifadhi….

‘Unaona eeh, eti tupo kikazi, tunafanya mikutano ya kibiashara..mumeonaaeh, bisahara yenyewe ndio hii…nipo madamu, nipo na.. madam,…’akasema

‘Madam……’nikajikuta akili ikisema

Mmojawapo akasegea hadi pale alipojikunyata huyo mwanamke ambaye sasa nimegundua kuwa ni madamu, akaja kumvuta lile shuka alilokuwa amejizungushia,..madamu akabakia wazi,…alikuwa uchi…mungu wangu,..ilikuwaje, nikawa najiuliza bila kupata majibu..

Niligeuka kwa aibu kumuangalia madamu, nilimuona hata yeye akiwa kama yupo kwenye mshangao, na kutahayari….na alikuwa akijaribu kuuficha uso wake, kwa viganja vya mikono, na pia akijaribu kujifunika kwenye matiti yake, lakini asingeliweza kufanya yote kwa pamoja., akainamisha kichwa chini kama anasujudu,

Mimi kwa muda huo kichwa kilikuwa kinauma sana…mara wale watu wakanijia, na kunivuta nisimame..oh, na mimi nilikuwa uchi……

‘Kwanini kuna nini..kwanini mnatufanyia hivi..?’ nikauliza kwa mshangao

‘Kuna nini..hahaha, mzinzi leo kapatikana…’wakisema wakicheka, huku wakiendelea kuchukau video mpaka walipotosheka, ndio mmojawapo akauliza;

‘Sasa tumfanye nini…?’ mmoja wao akauliza

‘Mtu kama huyu ana aibu, kwahiyo hataki watu wamuone, au sio, …unajua tumfanye nini, tumutoboe haya macho yake…’akasema mmoja, akisogea pale nilipo na peni akitaka kunitoa macho yangu, nikamkwepa.

‘Unanijifanya njamja sio…’akasema huku akinipiga vibao, nilijaribu kujizuia,

‘Oooh, anajifanya mjanja,..unajau tumfanye nini huyu akachomwe moto, na kaba ya hilo tendo, tutamuadhibu, ni lazima tumtoboe macho yake hii ndio adhabu ya wazinzi wenye aibu…na pia tutamkata sehemu zake za siri anazoringia nazo, tumpelekee bosi, anazihitajia…’ akasema mmojawapo.

‘Bosi…’hapo nikashituka,..ina maana kuna mtu kawatuma, ni nani huyo..’nikawa najiuliza

‘Na huyu Malaya wake…?’ wakaulizana

‘Huyo si anawashwa, ngoja midume ya kazi itamshughulikia sasa hivi, ili video yetu ikamilike, wafungulia hao watu wa kazi, ….midume ya kazi ingieni…’wakasema, na haikupita muda wakaingia wanaume watano hivi, mipande ya mibaba, imejazia kifuani, ..walichokifanya sipendi hata kusimulia, …mimi nikawa naambiwa niangalie kila hatua,…

‘Unajifanya unaona aibu eeh, sasa hebu fikiria hivyo anafanyiwa mkeo…utajisikiaje….’wakasema

‘Subiri zamu yako inakuja..’nikaambiwa

NB: Haya zamu yangu ilikuwaje, tuwemo sehemu ijayo


WAZO LA LEO: Mwanadamu huwa na siri zake, siri za kibinadamu hazihitajiki kuweka hadharani, kwa nia ya kuabishana hata kama kakosea, hili wengi twaliona ni jambo la kawaida tu, picha unatumiwa na wewe unaisambaza, kote inapopita ni madhambi unachuma….wengi wetu tumekuwa tukifanya hivi, kama mchezo tu, tukumbuke kuwa, siku hiyo ya hukumu,..hivi viungo vitatushitakia kimoja baada ya kingine, je utajiteteaje,….
Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Malizia za nyuma kwanza, we need them, unatukatishia...