Jamaa yangu kanihadithia ndoto yake ya ajabu …nikaona sio
vyema kuiacha kuiweka ndani ya shajara yangu(diary yangu) , ili kila mtu apate
kuwaadhika nayo.
‘Ndugu yangu, nimekuwa nikimuoata sana mzazi wangu tangia
aondoke hapa duniani,…hutaamini , baba yangu alikuwa mtu wa ibada, mcha mungu
wa vitendo, sio muongeaji sana, na kila siku alikuwa yeye ni wa kwanza kuingia msikitini,
na kuna sehemu yake maalumu alipenda sana kukaa hapo mstari wa mbeel kabisa..kiasi
kwamba kila mtu aliitambua sehemu hiyo kama sehemu yake. Hata alipofariki waumini
wengi walimuombea duwa na kuienzi sehemu hiyo kama sehemu yake.
Basi mimi kila nikilala usiku , ikatokea nikamuota mzazi
wangu huyo , na mara nyingi namuota akiwa sehemu hiyo amekaa, na hapo namuendea
tunaongea ndani ya..na ni pale pale msikitini kwenye sehemu yake…Nashindwa kuelewa ni
kwanini mara nyingi namuota yupo sehemu hiyo na si sehemu nyingine, nikaja
kumuuliza kiongozi mmoja wa dini, akaniambia ina maana mzazi wangu huyo anakuwepo
sehemu hiyo kila muda wa ibada, ni neema kubwa mungu kamtunuku.
‘Sasa basi ikatokea wiki iliyopita nikaota nimefika hapo
msikitini, nikitarajia kumkuta baba yangu sehemu hiyo,…, lakini cha ajabu sehemu
ile nikaikuta ipo wazi, na watu wamekaa sehemu zote ile pale pamebakia wazi,…kama
vile wamemuachia yeye,.. nikaingiwa na mashaka. Ndani ya ndoto, nikageuka ili
kumtafuta, nikamuona baba yangu huyo kasimama mlangoni, huku kainama kwa
masikitiko.
Nikamwendea na kumuuliza, kulikoni, akasema;
‘Mimi nasikitika sana, maana matendo yangu mema hutaki
kuyaendeleza, nilitarajia wewe kipenzi changu ungekuwa ukikaa ile, ukafanya
kama nilivyokuwa nikifanya ili yale mabaya yangu yasafishwe, na mimi nipande
daraja kwa kupata fadhila njema huku. Wenzangu wana watoto wao wanaendeleza
matendo yao mema na wazazi wao hao wamepanda madaraja, …lakini mimi nipo pale
pale…
Basi nilipozindukana nikamuendea imamu, kiongozi wangu wa
dini nikamuuliza, akaniambia huo ni ujumbe , na ni ujumbe wa kweli, unatakiwa
uufanyie kazi,..’akaniambia na kuzidi kuniasa akisema
‘Kuna wengi wetu hatupendi kuyaendeleza mambo mema ya wazazi
wetu waliotangulia mbele za haki kazi yetu ni kusifia tu, baba yangu alikuwa
hivi alikuwa hivi..au kiongozi fulani alikuwa hivi au vile lakini kimatendo
tupo mbali kabisa na tabia hizo njema....hiyo kuongea tu haitoshi kama ni
matendo mema basi tuyaendelezeni, hasa ya wazazi wenu…na kwa kufanya hivyo,
tutayafukuza matendo maovu..
Basi kuanzia siku ile nikawa sasa najitahidi kufika
msikitini mapema, na kukaa sehemu ile ile…hutaamini nikaja kumuota baba yangu
akiwa pembeni yangu sehemu ile ile. Akiwa amefurahi kweli huki akiwa, kava joho
la Hariri…
Jamani ndugu zanguni hivi kweli tunawakumbuka waliotangulia
mbele ya haki kwa matedo yao mema, au ndio tunasubiria siku ya kuwaombea tule
pilau na kuondoka…, kwanini tusijenge tabia njema ya kuwaenzi wapendwa wetu hao
kwa kutenda yale matendo yao mema waliyowahi kuyafanya, ….na tukifanya hivyo
hayo matendo mema ni hakika yatafuta matendo yao mabaya na wao watapanda madaraja.
Tukiacha kuyaenzi matendo hayo mema, ni dhahiri kuwa matendo
mabaya yatashika nafasi, ..ndio maana sasa hivi matendo mabaya ndio yamezidi,
mpaka watu wanayapigia debe,..angalia maangamizi ya kizazi cha nabii
Nuhu,(sodoma na Gomara)…Sasa hivi yameshamiri, na watu wanachekelea, wanapigia
debe, na hata kuyafadhili, nani atayakemea , wakati bwana mkubwa kayafagilia…haya
ndio madhara ya kuacha kuyaenzi metendo mema ya waja wetu wema.
Tumuombe Mungu atusamehe na atusaidie, kutuepushia na janga
hili ovu, kwa ajili ya vizazi vyetu, tusije kupata maagamizi kama hayo
yaliyotokea kipindi hicho, ..tusione hizo ni hadithi, hayo tumeandikiwa ili
tujifunze, na tuweze kujihadhari nayo...maana yaliyokuwepo, yatatokea, na sasa yanatokea….hala
hala mti na macho..
Tumuombe mola awarehemu wazazi wetu, ndugu na jamaa zetu
waliotangulia mbele ya haki, mola awalaze mahali pema peponi. Na tunakuomba ewe
mola wetu, na sisi tuendeleze matendo hayo mema, ili vizazi vyetu navyo viyaendeleze
hivyo hivyo hayo matendo mema na kuyaepuka matendo maovu…na utujaliwe tuwe na
mwisho mwema…Aaamin..
Sote tuitikieni Aaamin…
Ijumaa kareemu
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment