‘Mleteni…’
Hiyo ilikuwa sauti ya ofisa upelelezi, akiagiza kwenye simu, …je aliagiza
nani aletwe?
Pale
tulipokaa tulianza kujiuliza ni nani huyo aletwe, hata hivyo hatukuweza kufanya
kitu zaidi ya kusubiria, tukabakia tumetulia lakini ndani ya nafsi zetu, kwenye akili zetu tukiwa
tunawaza, kumuwazia huyo anayekuja ni nani, nani kwanini lugha hiyo ya ‘mleteni’
itumike…..
Tulifahamu
kama tulivyoambiwa mdada hatuwezi kumuona tena, sijui kwanini, sijui hali yake
ipoje, sijui..labda ndio hayupo duniani..kwahiyo hawezi kuwa ni yeye
anayetakiwa kuletwa…sasa ni nani….
Sote macho
yetu yaliekea mlangoni, tukisubiria kwa hamu, na kila mmoja akiwazia lake, kwangu
mimi nilijua anayeletwa ni Yule jamaa wa kijijini ili aje kuthibitisha yale
aliyoongea huyo mpelelezi, maana kwa mujibu wao huyo jamaa ndiye amekuwa msaada
wao mkubwa, na kwa vile alishajitolea kwa lolote lile amekuwa haogopi kuongea…,wamekuwa
wakimtumia sana kuelezea hali ilivyo kwa kundi hilo haramu, japokuwa bado
walikuwa hawana imani naye sana…
Kulitokea
kuchelewa kidogo na ofisa upelelezi akaamua kufuatilia mwenyewe, akasimama na
kutoka nje, sisi tukabaki mle ndani tukiwa watatu, mimi mwenzangu na dakitari ushauri, na mimi hapo hapo nikawa
na shauku ya kuongea na dakitari huyo, nikaona ni muda muafaka wa kumuuliza
swali kwani hatujui huenda tukarejeshwa tena rumande
Mimi
nikakumbuka kuwa docta huyu wakati anatuelekezea ilivyotokea, alikuwa
hajamaliza maelezo yake aliyokuwa akituhadithia siku ile,
Siku ile
mdada alipataka kunywa hiyo sumu, nikawa na hamasa kujua hilo, nikauliza
‘Docta najua hili halitakwenda kinyume na amri
ya watu wa usalama kuwa usiongee lolote kuhusu huyo mdada, lakini shauku yetu
ni kufahamu jinsi gani mlivyoweza kumuokoa asiweze kunywa ile sumu, ….ulisema
mlibadili na kuweka dawa nyingine lakini nakumbuka ulisema kuwa hamkuwa na
uhakika kuwa kule kwenye bahasha kulikuwa na dawa ngapi…
‘Ni kweli,
lakini sisi tulibahatisha kuwa zitakuwa ndio hizo tu…ndio maana kwa haraka tuliweka dawa zinazofanana na hizo, na zikiwa
na sifa ya kuyeyuka, na kwa kuziangalia usingeliweza kuhisi ni dawa tofauti na
zile, na ambazo hazitaweza kumuathiri mdada kwenye upasuaji wake ulitegemewa kufanyika…..’akasema
docta
‘Tulipohakikisha
kuwa kile kitu kimerejeshwa kama ilivyokuwa kwenye huo mkoba wake, tulifanya
ishara ili nesi arudi na huyo mdada,…lakini wakati tunafanya hilo, ghfla tukasikia nesi akiita kuwa anahitajia msaada….’docta akatulia
‘Kulitokea
nini…?’ tuliuliza maana hapo docta mshauri nasaha alitulia kuendelea kuongea
‘
Tuliposikia hivyo kwa haraka tukakimbilia huko bafuni, na tulipofika tulikuta
nesi akipambana na mdada, nesi alikuwa kashikilia mkono wa mdada ambaye alikuwa
kauweka mdomoni, akiwa kuashiria kuwa
alikuwa anatumbukiza kiti mdomoni,, tukajua ni yale yale….tuliyokuwa tukiwazia,
kumbe kweli mdada alishakuwa na kidonge hicho kabla,….
‘Oh, sasa
ikawaje….?’ Tukauliza pale tulipoona mshauri nasaha akisita kuendelea na
kutuashiria mlangoni, na kweli mara mlango ukagongwa mara moja na kufunguliwa, na
aliyeingia ni Yule askari mpelelezi na
jamaa mwingine na askari mpelelezi akasema;
‘Huyu ndiye
Yule jamaa anayetoka kijiji kimoja na mdada, tunamshukuru sana kuwa amekuwa
msaada mkubwa kwetu, na ameweza kufanikisha tukaweza hata kugundua hilo genge
la wahalifu huko nachi ya jirani…’akasema
‘Kilichosaidia
ni hiyo hali yao waliyotengenezewa bila hata kujuana, wamejengewa tabia ya
kutokuaminiana, kila mtu anamchunga mwenzake, kila kaambiwa huyo mwenzake
mchunge sana, na ukiona dalili za usalitu tuambie, lakini usije kumwambia, na
kwa vile wao ni maaskari waliivishwa na viapo vyao, hufata wanavyoambiwa…
‘Wanaambiwa
na nani, ni nani anayewapa maagizo hayo….?’ Tukauliza
‘Tunapewa
maagizo kutoka huko kwa wakubwa, ….nchi za nje, na mara nyingi maagizo hayo
yaafika kwa ishara maalumu ambazo tumefundishwa, inaweza ikawa kwenye mtandao,
au kwenye simu, lakini kwa alama maalumu ambazo sisi tunakuja kuzitafsiri
wenyewe…’akasema
‘Hizo ishara
au elimu hiyo wote mnaifahamu..?’ tukamuuliza
‘Kwa
viongozi ndio tunaifahamu , lakini sio wote wanaoifahamu…..ni elimu ambayo
inajulikana kwa wacheche sana, na mimi
kama kiongozi wa mtandao, naifahamu, na ….ila kwenye kutafsiri, inategemea
imemlenga nani,…kama ni mtu binafsi inatumiwa kwenye simu yake kama ni kwa
ajili ya kundi inatumwa kwenye mtandao na mimi nitafsiri kwa kuindika kwa
mkono….’akasema
‘Sasa kwa
mfano amri hiyo inamuhitajia mtu kwenye matawi yenu ya sehemu nyingine
mikoani,…mnafanyaje ili iwafikie ili waelewe…, maana umesema alama hizo ni nyeti
na wanaozifahamu ni wachache, hususani viongozi, na wengine hawatakiwi
kufahamu…?’ akaulizwa
‘Mikoani ni
lazima kutakuwepo mtu anayezifahamu, na huyo ndiye atawaelewesha wengine kwa
namna aliyoelekezwa, ni …..namna ya kuhakikisha taarifa haifiki kwa watu
wasiohusika…’akasema
‘Kwahiyo
makao yenu kwa huku kwetu yapo wapi…?’ akaulizwa
‘Hakuna kitu
kama makao makuu, au sehemu maalumu ya kusema hapa ndio ofisi au makao, hii kwa
ajili ya usalama, kwahiyo karibu kila siku ni kuhama kutafuta eneo maalumu,na
mara nyingi inakuwa sehemu zile za starehe au sehemu ambazo huwezi kuhisi
kunaweza kuwepo na kitu kama hicho…’akasema
Nchi ya
jirani tuliweza kukaa vyema, maana hakuna ufuatiliaji sana wa mambo binafsi,
starehe za kila namna zinaruhusiwa, kama makasini, majumba ya ulevi, ukahaba…makumbi
ya starehe, humo ndipo ofisi zetu zinakuwepo, na wakati mwingine hata kwenye
majumba ya Ibada…’akasema
‘Majumba ya
ibada, inakuwaje….!!!?’ Tukaliza
Ili
kufanikisha azma hiyo, wanachama waaminifu walipelekwa mashuleni kwa kila
Nyanja, na wengi waliopelekwa huko ni wateule,wale wenye akili sana,…wakafunzwa
fani hiyo kutegemeana na akili yake, kwahiyo kulikuwa na waelewaji wa dini,
walifunzwa dini hiyo na kufuzu sana,…sasa hao walihakikisha wanakuwa viongozi
kwenye nyumba za ibada,na wanatekeleza majukumu yao kwa njia za siri kabisa,
huwezi kumfahamu….’akasema
‘Na viongozi
hao wanakuwa na karama, watoa mijuiza, wanafanya mambo ambayo jamii inahitajia
sana, ….utakuta majumba yao hayo yanajaa watu, wanakusanya pesa kwa waumini
huku wanatengeneza mambo mengine ndani kwa ndani biashara za kisiri zinafanyka,
ni nani atashuku hilo…’akasema
‘Hata kwenye
siasa kuna watu wameivishwa kwa fani hizo, na wamesoma kweli, wameandaliwa
kushika madaraka sehemu nyeti,…na kwa vile wana elimu, ni wataalamu ni rahisi
kwao kuchaguliwa, na wanajitambulisha kwa wanachi kwa utendaji mwema kabisa,
lakini akilini wana ajemda ya siri…..hawa wanakwenda na wakati, wanajua ni nini
wafanye kwa wakati gani….’akasema
‘Una maana
gani kusema hivyo, maana kama ni wanasiasa mara nyingi huwa wanachaguliwa na
wananchi au kuteuliwa na kiongozi anayeshikilia madaraka kwenye eneo husika,
sasa wao wanajuaje kuwa huyo mtu wao ni lazima atachaguliwa au wanatumia mbinu
gani mpaka mtu wao achaguliwe?’ akaulizwa
‘Kama
nilivyokuambia, hawa watu ni wasomi, sio usomi wa kubahatisha…wana akili za
hali juu, na wapo kwenye kila fani, utaona wengi wamefikia kiwango cha uprofesa
, udocta….sasa utasema nini hapo..na, sio usomi wa kubahatisha…kwahiyo
uwezekana wa wao kuchaguliwa kuwa kiongozi, kushika nyazifa fulani ni mkubwa na
kwa hivi sasa wapo wengi tu, na pia
ikibidi huwa wanatumia mbinu nyingine za ziada za propaganda, ili kufanikisha
malengo yao ….
‘Hebu ni
waulize kwenye kuchagua viongozi wa siasa, au hata kazini, kuna namna yoyote ya kuwachunguza watu au hao viongozi
wametokea wapi….chimbuko lao hasa kiundani, wamesomea wapi kwa vipi,,..walisomeshwa
na nani,….hakuna kitu kama hicho, kuwa mtu anachekechwa kihivyo kujua historia
kwa undani…kweli inafanyika hivyo…?’ akauliza na sisi tukaa kimia
‘Kiukweli
haianyiki hivyo….’akasema
‘Kwahiyo
watu hawa walilifahamu hilo, kuwa kiuhalisia watu huangaliwa jinsi gani
wanavyotoka, wanavyoongea wanavyoshawishi, hasa kwa kutumia midomo yao, lugha
ikipewa kipaumbele,….na fani huja baadaye….’akasema
‘Mimi bado
sijaelewa hapo, maana viongozi wengine wanachaguliwa na mkuu au kiongozi mkuu
husika, unataka kusema kiongozi huyu anayewachagua hawawafahamu hao watu
aliowachagua vyema, ukumbuke kuna watu kama wa usalama wa nchi, unataka kusema
wao hawana uwezo wa kuligundua hilo…?’ tukauliza
‘Nikuambie kitu
makundi haya ni chimbuko la wazo na huyo jamaa aliyetaka kuiweka dunia mikononi
mwake ,…wengi waliliona wazo hilo kama
wazo la mwendawazimu, lakini athari zake ndio hizo, yeye alianza kama muota
ndoto, akalifanyia kazi, …sasa wanachama wake wamelipeleka mbali zaidi na wanamuenzi
hadi kwa mbinu hizo za ishara zake….’akasema
‘Ishara gani
hizo…?’ tukamuuliza
‘Zipo
nyingi, ….muhimu ni kuwa kuna ishara wanatumia kama zile za komputa, herufi
ndogo tu inaweza kuunda kitu…kuna ishara za tarakimu…kuna ishara za vitendo kwa
kuonyesha,…kuna ishara za alama mbali mbali..vyote hivyo vilikuwa ni ndoto za
huyo jamaa…..’akasema
‘Lakini huyo
jamaa alipatikana, na sehemu kubwa ya kundi lake walikamatwa…’nikasema
‘Yeye ni mtu
aliondoka, lakini mfumo wake bado upo na
utaendelea kuwepo,….namna ya utawala, namna ya kuwezesha watu wao kuendelea
kumiliki, kutawala, ili mfumo huo uendelee kuwepo,,namna ya kuwatetea wenzetu,
wanajijua wenyewe wenzetu ni akina nani…kwahiyo watafanya kila njia wao waendelee
kuwepo madarakani na wengine ambao hawana masilahi na wao, wasiepewe
nafasi,….huo mfumo bado upo…sio lazima mtu , lakini muhimu ni mfumo wao…’akasema
Ukumbuke mtu
huyu alichokifikiria kikubwa ni elimu, elimu hii akaiangalia kwa namna ya
ubinafsi, kuwa kumbe unaweza ukaiwekeza kihivyo, kuwatafuta wataalamu,
lakini…wale wenye mleno wao, ubinafsi…, utawagundua tu wakiwa kwenye vyeo vyao,
hata walipwe nini hawataosheki…na zaidi ya hayo, hakuna utu mioyoni mwao,
muhimu kwao ni masilahi….’akasema
‘Kama
mnakumbuka lile tukio la yule jamaa aliyetaka kuiweka dunia mikononi mwake,
alianza kuwasomesha wataalamu, wataalamu hawa walipikwa kinamna,
wakasomeshwa…..mnakumWataalamu hawa walipomaliza kusomesha wakaiva, walitawanywa sehemu mbali
mbali wakiwa wamepewa majukumu, na mtandao ukaenea, mfumo ukashika hatamu,
umimi, umwenzetu ukawa upo kwenye damu…na zaidi propaganda….hata kama Yule
mwanzilishi hayupo lakini mfumo wake bado upo unafanya kazi, kila mmoja kwenye eneo lake aliwekeza na yeye,
akapika watu wake kwa mfumo ule ule……’akasema
Ukimuona mtu
yupo lakini hana elimu,…au utaalamu fulani ujue huyo ni chambo tu…’akasema na
kucheka kidogo.
‘Kwa maana
hiyo unataka kusema hakuna makao maalumu yao na wao hawana kiongozi wao mkubwa,
mfumo ndio kiongozi wao, haiwezekana sasa kwa njia hiyo wao wanawezaje
kujiongoza?’ tukauliza
‘Ni kweli, ….lazima kwa hali kama hiyo kuwepo
na viongozi, viongozi hao wapo, na mara nyingi wao huchaguana kutokana na
ujuzi, yule mwenye ujuzi mkubwa kwenye hiyo fani, na huku juu kabisa wapo wale
waasisi, ambao ni mabaki ya Yule bwana aliyetaka kuiweka dunia mikononi mwake
….
Uongozi wao
ni mfumo, upo tu,…kwahiyo huwezi
kumkamata mmoja ukasema huyu ndiye kiongozi, basi nimemaliza hilo kundi,
unajidanganya, kwasabau wao wanakwenda na mfumo, ambao ni kama imani yao, mfumo huo upo, na nguzo yao ni kipaji, Yule
mwenye uelewi wa hali ya juu, anajikuta ndiye kiongozi,…na kazi yao kubwa ni
kuhakikisha kuwa wao wanaendelea kumiliki njia zote za uchumi, wanakuwa wao ni
watawala…maana wana kipaji cha kuongoza, kushawishi, na wanajua jinsi gani ya
kubadili muelekeo,
Na kitu
kikubwa kinachowasaidia ni propaganda, kuzua mambo na mambo hayo yakaja
kuonekana ni sahihi kwenye jamii,kuhahikisha kuwa mfumo wao unatambulikana, kwa
vile pia wanamiliki mamlaka ya maamuzi makubwa huko juu…kuna mambo jamii iliona
hayafai, lakini kwa propaganda zao, leo yanaonekana ya kawaida…!.
‘Na mara
nyingi wao wamekuwa maadui wakubwa wa dini,misimamo isiyotaka mabadiliko,
wanaipinga sana, na kwanjia ya propoganda, njia ya kuharibu tamaduni za dini,
tamaduni za asili wameweza kupandikiza mifumo yao kila mahali…
Kwa ujanja
wao, wamekuwa wakiwekeza sehemu zile ambazo hazina ufuatiliaji wa sana na hata
kama upo huwezi kuwashuku kabisa.
Wakiwa nchi
ya jirani, ambapo kuna mitambo za kisasa, waliweza kuweka vyombo vyao vya
kisasa ambavyo viliweza kuona sehemu mbali mbali na kunasa matukio wanayoyataka, wakitumia zaidi hizi simu za mikononi na
computa zenye hizo zana…
‘Sasa kwa
ushahidi huo, huyu hapa alikuwa mmoja wa
wataalamu wa kuendesha mitambo hiyo, akiwa nchi ya jirani, jamii huyu ni
mtaalamu sana wa komputa, uone walivyo wajanja, walimgundua na wakamshawishi
wakamuendelea zaidi na kumuwekeza, akawana kampuni yake ya kuweka mikondo ya
mawasiliano, mitandao, na kutengeneza CDs, na humo wakawekeza mambo yao….’akageuka
kumuangalia huyo jamaa
‘Zimwi
likujualo halikuli likakesha,…jamaa huyu anasema tangu awali hali hiyo ilikuwa
inamtesa sana, kuona kuwa anatumika, kipaji chake kinatumika vibaya, lakini
alishaingia kwenye mitego yao angefanya nini..lakini sasa kazindukana na kaiona hiyo hali kwa mbali
zaidi, kaona kuwa dunia hii ni ya kupita, kwanini asijitoe…wenzake
walishamshuku na kwa mbinu zao wakahakikisha kuwa anapandikiziwa hilo gonjwa…’akasema
‘Walishampangia
kuwa mwaka hata maliza, na kwa mahesabu yao wanajua keshafariki….’akatulia
‘Ni kweli kuwahivi
sasa, maisha yake yapo hatarani, kwani kama bado yupo hai ataweza kutoa siri
zao, lakini kwa vile na yeye ni mtaalamu wa mambo hayo ya mawasiliano ya kunasa
matukio, ameweza kuwapiga chenga za hapa na pale na kwa vile alishajitambulisha
kwao kuwa anaumwa, wao wameshamuweka x, kuwa haitachukua muda atakufa,
hawakujisumbua sana kumtafuta…
Utaalamu
wetu nao unazidi kukua, kwani madakitari wetu wamekuwa wakihangaika kutafuta
tiba ya kupambana na hayo madawa yao,…magonjwa yao ya kupandikiza, na sasa tunaweza kusema angalau wataalamu wetu
wamefikia sehemu ambayo wanaweza kupambana na maradhi haya ya kutengenezwa na
wanadamu…
Ni vitu vya
kuogofya kweli ndio maana havitakiwi kutangazwa, lakini kwa hali lilivyo inaidi
wananchi waambiwe, wawe na tahadhari….tatizo ni nani wa kumfunga kengele paka,
wakati huo huo, huenda watalawa waandamizi wapo kwenye hilo kundi…..unaona
ilivyo shida.
ILE NDOTO,
ya dunia yangu bado inatuandama….na wananchi nao ambao ndio waamuzi wa
haya,bado hawajakuwa na utashi wa kuelewa zaidi…kwani kama ni kiongozi wao ndio
wachaguzi, lakini kwa vipi wataelewa hilo,…imebakia kuwa sikio la kufa….
Lakini ndio
hivyo, mwanadamu kujisahau tu, ….na ndivyo ilivyo,mungu humpa mtu ujasiri,
akafanya atakavyo akajenga kiburi, akajiona yeye ndiye mfalme,….mtawala wa
kuogopewa, lakini hajui kuwa yeye ni kiumbe tu, kaumbwa, na mwenye mamlaka
hayo, ya uhai wake anaoringia, mwenye mamlaka ya fya yake anayojivunia, mwenye
mamlaka ya hali ya kipato chake…nk, ni mmoja tu, mwenyezi mungu muumba.
Na kwa
wakati wake ukifika, ataviacha vyote hivyo, na anaweza akaviacha kwa udhalili
wa hali ya juu, akateseka kwa maradhi, au akasubiriwa siku ile anakata roho
akaonana na madhambi yake na vitu atakavyokutana navyo kaburini…..inatisha,
lakini kamwe hatusikii, ..kama hatuoni huko mbali,…maana sisi ni sikio la
kufa…..
‘Hao jamaa
walishagundulikana kuwa watanaswa, wanatafutwa na polisi, sasa iweje, kama
ilivyokawaida yao, wakuu wa kimataifa, wakaona kundi hilo wote waangamizwe, na
wataangamizwaje kabla hawajakamatwa, ikatumika ile mbinu ya kuwa kila mmoja
kupewa agizo la kumuondoa mwenzake,..
Huyu
akaambiwa mwenzako ni msaliti, unatakia ummalize haraka, na huyo mwenzake
akaambiwa hivyo hivyo kwa mwenzake, walichofanyiwa ni kuagizwa kila mmoja kwa
wakati wake, kuwa mwenzake sio mwaminifu, kwahiyo anatakiwa kuondolewa, na huyo
anauetakiwa kuondolewa, naye akapewa maagizo kwa mwenzake kuwa mwenzake sio
mwaminifu kwahiyo anatakiwa kuondolewa..
Kwa mtindo
huo, wakajikuta wote wamelishana sumu zao,na wote wamekutwa wakiwa wamekufa na
hizo hizo sumu zao, na imekuwa mwisho wa kundi hilo hapo nchi jirani…..’akasema
akitikisa kichwa
‘Sasa kwa
kutaka kuondoa ushahidi wote, walitegesha bomu,…mmojawapo mtaalamu wa mabomu
alifanya kazi hiyo, hakujua na yeye ni miongoni wa watu wanaotakiwa kufa, kwani
alipoingia ndani alipigwa sindano ya shingoni na mmojawapo, na kupoteza fahamu,
na baadaye kupoteza uhai,…
Bomu hilo
lilitakiwa kufyatuka baada ya kuhakikisha watu wote wamemalizika na wapo humo
ndani, kwani siku hiyo kulikuwa na kikao kikubwa cha wanachama wenye dhamana,
wote waliitwa kutoka sehemu mbali mbali…wakijua ni kikao, hawakufahamu kuwa
ndio ulikuwa mwisho wao.
Bomu hilo
lilisubiria wakati muafaka, na kiwashio
chake kilikuwa huko huko kwa magaidi wa kimtaifa, ambao walikuwa wakisubiria
wakati muafaka kulifyatua, ili kupoteza ushahdi wote, lakini bomu hilo
likawahiwa kabla hajalipuka,na ndio tukaweza kupata ushahidi mkubwa na mambo
yao waliyokuwa wakifanya yakawekwa hadharani…’akasema
‘Sasa humu
nchini kwetu, kuna sehemu mbali mbali walipandikiza watu wao hao kinamna…,
kwenye fani mbali mbali,na wao wanajiendesha kinamna ambayo hata wao hawajijui
kuwa wanatumiwa,wao wanaona kuwa wanafadhiliwa kufanikisha hizo fani, lakini ni
nini hizo fani, zina faida gani kwa jamii….ndio kitu walitakiwa kujiuliza,
lakini kwa vile lengo lao ilikuwa kupata jina, na kupata ajira, hakuna
aliyejiuliza hilo,…
‘Kuna
ufadhili wa vikundi vya kuigiza, michezo mbali mbali…urembo, sanaa za kila aina
maana wao wamelenga sehemu ambazo zinawagusa vijana, ili baadaye waje kufanya
yale wayatakayo, na vijana wakiambiwa watakubali tu,….mfadhiki bwana mkubwa
kasema, utabisha nini….
‘Umasikini
na hali mbaya za kiuchumi zimekuwa pia silaha za hawa watu, wamejifanya ni
wafadhili wa kusaidia watu wasiojiweza, ….jasho lao lililonyonywa kinamna
linarejeshwa kwao kama misaada,na jamii iliyopo kwenye taabu inapokea kwa
shukurani kubwa,..itafanyaje, hii ndio hali ya unyama unaendelea duniani, wenye
nacho kuzidi kuwanyinya wasio nacho, na kuwadhalilisha……ni mbinu za hali ya juu
sana……sasa haya yote kama jamii tunatakiwa kushirikiana sana kuyabadilisha….’akasema
‘Utajiuliza
ni kwanini, ili iweje…?’
‘Ndoto zao
ni kuitawala dunia,..kuwa na usemi wa kila kitu na dunia iwe na muelekeo mmoja,
kwanza dunia iwe kijiji kimoja, …..hilo limeshafanikiwa, jingine tamaduni za
kiutu zipotee, watu waishi kiunyama unyama, uchi…mtu apendavyo…au sio…..ili
mwisho wa siku, kile kinachoitwa ushetani ndio kitawale dunia…’akaongezea
‘Sasa jamani
nimewaletea huyu jamaa kwenu ili muweze kuamini haya ninayowaambia , ili
mkiandika mambo yenu muwe na uhakika wa kile ninachowaambia,…kuwa hayo yapo na
ndiyo wanayoimaliza dunia…baraka,zinaondoka, na kama mna maswali ya kumuuliza
kabla hatujamalizana, maana baada ya hapa sitaki kuona mkilifuatilia hili jambo tena….’akasema
Tulimuuliza
maswali mengi huyo jamaa na majibu yake yalitufanya hata sisi tuogope ,kwa
jinsi gani wanadamu wenzetu walivygeuka kuwa sio wanadamu tena, ni zaidi ya wanyama,
na kisa ni nini, kupata utajiri, kutawala, ..kuiongoza dunia, …na jinsi
alivyokuwa akielezea, nikakumbuka kile kisa cha dunia yangu…nikagundua ni wale
wale….nii chimbuko lake!
‘Wao wanaamini kuwa kila mtu ana uhusru na
utashi wa kufanya apendavyo, ajisikiavyo, na asiingiliwe, na sheria ziwkwe
kutokana na utashi wa watu,..kusiwe na sheria za kumlazimisha mtu kwa viti
vinavyomfurahisha, na mbora wao ni yule aliye na utajiri, …mjanja, mwenye mamlaka, …kwaho huo ndio ubinadamu
….’akasema
‘Sasa hizo
dawa za kupandikiza magonjwa zina faida gani kwao maana zinawakwanza watu wasifanye
wale wayapendayo…?’nikataka kuuliza na yeye akanikatiza kwa kusema;
‘ Hizo dawa ni
silaha , badala ya kutumia bastola, bomu..vitu vyenye kionekana wao wakaona ni
bora kuwe na silaha za kuua kimia kimia…ina maana bwana mkubwa akisema leo
huishi kweli siku hiyo unaondoka…na hakuna ushahidi, …ukichunguza hivypo
vidonge ukiviweka kwenye ulimi vinayeyuka mara moja kama glucose, na kwa haraka
vinakimbilia kwenye mishipa ya damu na kuathiri mapigo ya moyo, na mtu huyo
haichukui muda,…anakufa! Kama ni maalumu
kwa kuua, kama ni kwa mateso vipo vya namna yake, na kama ni kwa magonjwa vipo
kwa namna hiyo hiyo lakini kwa vipimo vyake, wataalamu wenyewe wanafahamu!
‘Sasa
ilikuwaje kwa mdada, maana hatuoni kama alikuwa tishio, kihivyo, kwanini na
yeye akawa muhanga wa mambo hayo, au alikuwa mmoja wa wanachama wa siri….?’
Tukauliza hapo yeye alikaa kimia mpaka tukaingiwa na wasiwasi kuwa anaogopa
kujibu hilo swali na baadaye akasema
‘Mdada ana
kipaji kikubwa cha uigizaji, ana umbo zuri lenye mvuto,…sura yake kwenye picha
ni zile sura zinavutia sana, na kwa watu kama hawa wanahitaji warembo wa namna
hiyo, kuvutia biashara zao…akina dada, wanatumiwa sana,wananyonywa,
wanazalilishwa kwa urembo wao na nini faida wanapata…hakuna, wanaofaidika ni
wao tu…mdada alitakiwa kuandaliwa hivyo….’akatulia.
Kikwazo
kikubwa ilikuwa wazazi wake…wazazi wake walibobea kwenye dini, ….ikaonekana ni
tatizo, …wakaamua kumtumia mchumba wake,….mchumba wake ukichunguza sana yeye alikuwa na utaalamu wa magari , ana
kipaji kikubwa sana cha ufundi, hata hajaenda shule, lakini aliweza kulifahamu
gari na muundo wake…hawa ndio watu wanahitajika, wenye ufundi wa kipaji, na
wakipewa shule kidogo tu wanakuwa mafundi wa hali ya juu.
Huyu jamaa akiwa
na mdada watakuwa hazina kubwa ya kundi, lakini je wanaelekea, je watakubaliana
na sera za kundi,…walichunguzwa kitaalamu wakaonekana ni vigeugeu…kwamba siku
yoyote wanaweza kuuza siri, lakini bado wanahitajika, …ndio wakapewa kazi za
muda za kufanikisha mambo , na ikifikia muda hawahitajiki tena, wanaishilia
mbali….wakawa wamepandikiziwa magonjwa …..yatakayowatafuna hadi muda
muafaka,magonjwa haya haya tunayoyafahamu sisi..ni nani ataligundua
hilo…’akatulia
‘Mimi
sikuyafahamu hayo,nimekuja kuyagundua hayo ya madawa, nilipogundua kuwa hapo
kuna tatizo, nikaanza kufanya uchunguzi wangu mwenyewe..mpaka nikapata hizo
siri…lakini ni siri zisizo na mshiko, ushahidi upo wapi…huwezi kusema huu ni
ushahidi, wakati kila kitu kinapotea,….sumu iliyofanya hiyo kazi hufutika
kabisa mwilini ,huwezi kuigundua, …wanahakikisha kuwa hakuna maandishi yoyote
ya ushahidi ynabakia , mara nyingi hawatumii maandishi haya ya kawaida
wanatumia maandishi ya ishara….jambo likikamilika kila kitu kinaharabiwa na
hata wahusika, wanapotezwa…
Tukienda kwa
mdada, yeye alikuwa kama chambo tu, japokuwa wakipenda awe mmoja wa warembo
wao, kwani alikuwa na sifa zote, lakini ilionekana ni hatari zaidi kuwa naye
kuliko faida yake, siku zao zikafika..
Kuna kazi
walitakiwa kupewa, majukumu ya kuhakikisha mipango yao inakamilika, lakini ilipoonekana kuna ufuatiliaji, jamii,
imecharuka, na serikali imegundua kile walichokuwa wakikifuatilia,wakaona wote
waliokuwepo wapotezwe…’akasema
‘Serkali
iligundua nini…?’ tukauliza
‘Hawa watu
hawawekezi tu mahali bila ya kujua ni nini watakipata , pamoja na kutafuta
sehemu za kuwekeza, wakitumia rasilimali watu, lakini pia mara nyingi
wanatafuta na mali asili, nchi yetu hii imebarikiwa sana na kuwa na mali asili,…watu
wao walishafanya uchunguzi wakaligundua hilo…’akasema
‘Wao wanajua
jinsi gani watu wao watapata hizo nafasi za uwekezaji,lakini pia hawataki
kupoteza hiyo nafasi ya kutumia rasilimali watu, ambao wanajulikana kuwa
watafika hapo, kutakuwa na mambo ya starehe…biashara, na humo watawekeza mambo
yao mengine pia.
‘Wahanga wa
hayo yote ni akina mdada, wakitumika kama chambo…na ilipoonekana wanaweza kuwa
mzigo badala ya tija, wakatakiwa kupotezwa, ndio wakapewa madawa hayo ya …..kupoteza
kinga….kupungukiwa damu…kwenya jamii ni magonjwa ya kawaida, hakuna
atakayeshuku kuwa ni wao wamepandikiza mambo yao..
‘Kwahiyo…ina maana matatizo aliyo nayo mdada
sio ugonjwa halisia, na ugonjwa wa kupandikizwa, na huenda anaweza kupona..au ukishapewa
madawa hayo ya sumu huwezi kupona tena?’ tukauliza kwa shauku
‘Ni waambie
ukweli,..hawa watu ni wataalamu kweli, wakifanya jambo lao hawakopeshi,sasa
inategemea nia na lengo lao ilikuwa ni nini….kuwamaliza kabisa akina mdada na
wenzake au kuwatesa kwanza hadi hatua fulani, lakini inavyoonekana lengo lao ni
kuwa hao akina mdada waje kufa, kwa namna ionekane ni kifo cha
kawaida,…upungufu wa kinga, na kuishiwa na damu, sasa mimi sijui zaidi labda
madocta wameweza kuisafisha hiyo sumu kitu ambacho sizani kama kinawezekana,….sijui…’akasema
akimgeukia docta ushauri.
‘Kwahiyo na
wewe ulishajifahamu kuwa wamekuwekea hizo sumu, na ulishajua kuwa itafika muda,
utaondoka, au sio, sasa ni kwanini ukajiunga na kundi la kuhamasisha, …kuishi
kwa matumaini, huku ukijua wewe ni mhanga wa sumu hizo, na hauhusiki na ugonjwa
asili wa kupungukiwa kinga za mwili…?’ akaulizwa
‘Najua muda
utafika nitaondoka,..sina jinsi, ndio maana niliona kwa kujipa matumaini hii ndio
njia pekee, ya kujikosha kutubu, na kusaidia wenzangu ili nipate cha kunisaidia
huko ahera….’akasema kwa sauti ya huzuni.
‘Ni kwanini
mkajiunga na makundi haya haramu….sasa mnaona athari zake, mnakuja kuwaumiza na
hata ambao wasio na hatia…’mwenzangu akasema kwa hasira.
‘Nyie
hamuwajuia hawa watu ni hatari,na wakikutaka watakupata tu, kwa mbinu mbali
mbali…wanajua watu wengi wanatafuta, wanatafuta maisha bora, kwa kasi ya hali
ya juu, na kazi hizo wanazijua jinsi gani ya kuzitengeneza, si mnataka kazi,
mtaenda wapi,….’akatulia
‘Kwahiyo
wengi wetu, tuna usemi kuwa ajali kazini, tutakufa tukiwa kwenye nia ya
kutafuta, na tuliobahatika kujitambua ndio hivyo, tunatafuta mema ili yaje
kutusaidia, ..ni kweli tulijiingiza kwenye mabaya, lakini tungefanyaje, sikio
la kufa….’akasema kwa sauti ile ile ya huzuni.
‘Kwa kifupi,
ndio hivyo, mimi niliyebakia, nasubiri hapo sumu hiyo ikifikia kielele chake
basi nitaondoka..japokwua madakitari bado wanajitahidi kupambana, kuendelea
kunisaidia kusafisha damu, sijui…’akasema akitikisa kichwa
Mimi nikaona
muda unakwenda wakati hatujalipata lile tunalolitaka, nikauliza swali hili kwa
kuchokonoa ili nipata huo ukweli
‘Je kwa
mdada mlifikia wapi, hali yake ipoje…mliweza kumuokoa,…?’ tukauliza swali na
jamaa huyo akamgeukia ofisa upelelezi, na ofisa upelelezi akamgeukia docta
ushauri, na baadaye akasema;
‘Najua muna
hamu sana ya kusikia kumuhusu mudada, kwani ndiye aliyewafanya hadi mkafika
hapa…lakini mimi nia yangu ilikuwa kwanza muelewe hali halisi, maana mtu kama mdada
ni mmoja wa wahanga kati ya wengi walionaswa na balaa hili,
‘Inasikitisha
kuwa vijana nguvu kazi ya jamii inaharibiwa,…kwa ajili ya tamaa ya wachache
wenye ndoto za kupata tu kwa vyovote vile,….watu hawa wamejenga mehakalu, wana
miradi mingi lakini bad hawatosheki, …maana laana ya ufisadi ipo ndani ya damu
zao….ukiangalia sasa hivi maisha ya kuishi kama kijana ni machache sana, ..ni kwanini…uwezo wa vijana
kuhimili katika umri wa kijana ni mdogo sana, wanazeeka mapema sana ni
..kwanini…ni athari ya haya yote…’akatulia na kuangalia saa, halafu akasema
‘Sasa kwa
kujibu swali lenu, hebu subirini kidogo…nione kama hawa watu wapo tayari,….’akasema,
akachukua simu na kupiga simu, alisikiliza kidogo halafu akatabasamu na kusema
‘Kumbe
wameshafika , ingieni….’akasema kwa sauti
Mara mlango
ukafunguliwa, …akaingia mwanadada mmoja, shupavu, kwa unekanaji wake,
nilimtambua kuwa huyo hawezi kuwa huyo mdada, bali ni askari, alikuwa kambeba
mtoto mchanga, mikononi, na alipojitokeza tu pale mlangoni alionyesha ishara za
kiaskari, akasema
‘Tumeshafika
mkuu…aingie…?’akasema
‘Mwambia
aingie tu, tunamsubiria yeye…’akasema huyo ofisa upelelezi.
Na mara
akaingia mdada mmoja akiwa akjifunika khanga, ..ile ya kuashiria kuwa huyo ni
mzazi, ilikuwa haijifichi, alikuwa mama wa hicho kichanga, na alipoingia
akaonyeshwa wapi akae,….kwanza alisita kufanya hivyo, akawa kasimama , lakini
dakitari ushauri akasema;
‘Usiogope
mpendwa, mimi ndiye nimekuhitajia,….’akasema
‘Hawa
unaowaona wote hapa ni marafiki wema kabisa, kwa namna moja au nyingine, wamekuwa
wakikuhangaikia wewe, kuhakikisha unafanikiwa, usiwaogope kabisa, lengo lao ni
kukusaidia kila mmoja kwa namna yake, na wote wana kibali cha kufanya hivyo…nitakutambulisha
kwao usiwe na shaka upo salama…’akaambiwa
Lakini mdada
huyo bado alionekana kuwa na mashaka, akageuka kumwangalia Yule askari
aliyembeba mwanae, halafu akageuza uso kumuangalia ofisa upelelezi, halafu
akatugeukia na kutuangalia sisi wawili…sijui kwanini, kwani haikupita muda,
machozi yakaanza kumtoka…
NB: Nilijua
leo tutamaliza, lakini kumbe duuu..bado kuna kitu kidogo cha kumalizia, huyu
ndiye nani , ..najua nyote mumeshapata jibu, lakini ni kwanini analia ?
WAZO LA LEO: Wengi wetu tunatubia makosa yetu
pale tunapoona hatuna jinsi, …muda wa kuishi umekwisha, au tumebanwa kiasi
kwamba hatuwezi kufanya lolote. Na ni wachache wanaoweza kuliona hilo wakafanya
toba,toba ya kweli, kwani mara nyingi madhambi ya kudhulumu yanaziba
ufahamu wetu, ubinafsi unazitawala nafsi zetu, na hata kuyaona yale tunayofanya
ni ujanja wetu…..
Tukumbuke
sisi ni wanadamu tu, wapiti njia, yote tuyafanyayo yanahesabiwa, na ipo siku
yatatuhukumu, kama ni hivyo basi, tujirudi, tutubu toba ya kweli, na tutubie
bado tukiwa na ufahamu wetu, …ili toba hiyo ifike kwa tuliowakosewa, waweze
kutusamehe, ikibidi tufanye jambo, turejesha
mali ya watu tuliowadhulumu, tutende mema, ili hayo mema yaweze kufuta hayo
maovu yetu
Ijumaa njema!
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment