Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, September 24, 2015

IDD MUBARAKAH


Kwanza ni kumshukuru mungu kuipata siku hii muhimu ya kuungana na mahujaji wenzetu waliojaliwa kutimiza nguzo hii muhimu katika dini. Sisi ambao hatujabahatika tumuombe mungu atujalie tuje kuitimiza , kwani kwake yeye yote yanawezekana.

Siku ya leo wengi wana maandalizi , makulaji mavazi na tamasa za hapa na pale, na nifuraha kwa kwenda mbele, lakini tunasahau kuwa kuna wenzetu kwasababu hizi na zile hawawezi kufanya hivyo, hawawezi kula vizuri, hawawezi kusherehekea, ....je wewe uliyejaliwa unawaonaje
Wapo wagonjwa, wamelezwa, au majumbani, na wao walitarajia kuwepo, lakini kutokana na mitihani hiyo ya maradhi wameshindwa, wanahitajii faraja yako, ukila na kusaza wakumbuke , wapitia, wape zawadi wape faraja, utapata jaza zaidi ya hiyo ya kula na kusaza.

Wapo wasiojiweza, kwa ulemavu, wapo wasiojiweza kwa mitihani ya umasikini, wapo mayatima, wazee, jamani jamani, hawa ni vipenzi wa mungu, ukiwakumbuka na wewe utakuwa miongoni waliomjali mwenyezimungu, na imani yako itakuwa kubwa, utakuwa miongoni mwa waumini..

Blog yako ya diary yangu inawatakia IDD EL HAJ NJEMA

Ni mimi: emu-three

No comments :