Ni siku
maalumu kwa Profesa,.....
Ni siku maalumu kwa wenzake, pia,
Profesa alijua sasa ni muda wa kuitwa tajiri, ni muda amao
ataipata pesa ambayo hajawahi kuishika kabla...moyo ukawa unamdunda kwa
uroho...
‘Sasa hawa
watu watanitambua kuwa mimi ni nani....’akawa anaongea, akakuna kichwa
‘Huyu
mtaalamu, anajifaya mjanja, ...hahaha hajui kuwa mimi nimeshika mpini, yeye
kashika makali, ataniliona vumbi langu....’akasema akitabasamu
‘Najua
.....ujanja wake, ....nimeshajua mbinu zake, hajui kuwa mimi ni mjanja....’akaangalia
saa yake...
Akiwa yupo
sehemu yake maalumu,...alikuwa akivuta sigara, taratibu, huwa akivuta sigara
ujue ana tatizo gumu, na tatizo hilo liahitajia kufikiria sana.....
Aliangalia
saa yake, akajua sasa ni muda muafaka, akatembea taratibu, hakuwa na haraka, kwani
kazi hiyo inahitajia umakini sana, kwanza akatafuta usafri hadi mtaa mwingine,
kwenye watu wengi, akahakikisha hakuna
mtu anayemfuatilia
Moja ya
kibanda cha simu kilikuwa kinatumika, alisubiri aliyekuwa kipiga simu
kutoka,...alipotoka tu, akaingia kwenye hicho kibanda cha simu, akaitafuta
namba, akaipiga, na kusubiria,...mara mtu akapokea, akakaa kimia
‘Halloh,....’sauti
ikasema, hakusema kitu, akakata simu
Aliondoka
pale akaelekea kibanda kingine akapiga simu, na mara mtu akasema
‘Halloh,....nani
mwenzangu...’
‘Subiri kuna
mtu anataka kuongea na wewe....’akasema akiigiza sauti ya kike,
Aliondoka
hapo na kutafuta usafiri hadi mtaa mwingine, baada ya kuhakikisha hapo hakuna
mtu karibu, akavaa kitambaa usoni kinachofunika mdomo, akachukua simu na kupiga
namba....
Haikupita
muda akasikia sauti, kama kawaida alisikia sauti ya jamaa akihema, halafu kwa
sauti ya kukoroma, ikionyesha kuchoka akasema;
‘Halloh...mbona
...wewe ni nani .’akaanza uongea
‘Ongea na
....’akaigiza sauti ya kike
Natumai upo
tayari.....’akasema profesa kwa sauti nzito sasa
‘Nani wewe
....mbona namba tofauti tofauti.....’sauti ikasema
‘Wewe
wajifanya mjanja sio,....nilikuambia nini....’akatoa sauti nzito ya vitisho
‘Kwani
nimefanya nini..’sauti ikasema
‘Najua hapo
ulipo unarekodi sauti yangu, hiyo haisaidii kitu, yote haya niliyafanya
kukusaidia, sasa umekiuka masharti, kesho mkeo atapata picha mojawapo kuonyesha
uchafu wako, na baadaye nitatuma kwa mkweo...’akasema
‘Kwani mimi
nimefanya nini, umetaka pesa, pesa nimeshazitafuta, unataka nini zaidi....?’
akauliza
‘Pesa yote
ipo kamili....?’ akaulizwa
‘Ipo kamili,
.....’akaambiwa
‘Wewe si
umetafuta mpelelezi, na unatarajia kuninasa wakati unazipeleka hizo pesa, ....’akaambiwa
‘Mpelelezi,
nani kakuambia nimetafuta mpelelezi...?’ akauliza
‘Nilishakuambia
wahusika wameshajiandaa kwa yote hayo, kila unachokifanya wanapata taarifa....na
hilo ulilolifanya la kutafuta mpelelezi,....na watu wakufuatilia simu
zinazopigwa, kuwa unaweza kuninasa...wanaona wewe huna ushirikiano,mimi ni
mjumbe tu, na hao watu mimi sikutani nao,unajua kwanini wanafanya hivyo....’akasema
‘Ni nani
kakuambia nimetafuta mpelelezi....?’ akauliza
‘Hakuna haja
ya kuongea sana,........ najua hapo unatafuta mbinu za kutafuta wapi
nilipo,...ila nakuambia mkeo akiona huo uchafu wako, ndio utagundua kosa
ulilolifanya, utajutia maisha yako yote....’akasema
‘No,no...usifanye hivyo tafadhali, nambie
nipeleke wapi hizo pesa, na nikampe nani utakayemuamini,au uje uchukue
mwenyewe, tukutane wapi ....nitabadili kila kitu, na ...sijatatafuta mpelelezi,
sio kweli nipo peke yangu....’akawa anaongea kuonyesha wasiwasi mkubwa.
‘Sasa ni
hivi...hizo pesa utazipeleka sehemu ile ile ya awali, ...na utazipeleka wewe
mwenyewe ukifika hapo usubiri maagizo yangu...’akaambiwa
‘Na mzigo
wangu nitaupateje....?’ akauliza
‘Mzigo
gani...?’ akaulizwa
‘Picha ya
hiyo video...tulikubaliana nini.....nataka picha zote na kama mnanidanganya
nawaambia, ninajua kama ni feki au ni sahihi, kama mkitoa kopi nitafahamu ....’akasema
na kutulia
‘Huo mzigo
wako utaupata,....lakini ni mpaka hapo wenyewe watakapohakikisha pesa
imekamilika,huwezi kwenda dukani kununua kitu ukalipa pesa nusu ukakabidhiwa
kifaa, ....umenielewa, pesa kwanza....ikiwa imekamilika.’akaambiwa
‘Ina maana
bado hamjaniamini, nimeshawalipa pesa ya kwanza, ....sasa hii ya pili, bado
hamjanionyesha dalili ya kunipa huo mzigo, nitawaamini vipi, kama sio
mnanidanganya....’akasema
‘Hii yote ni
kwasababu huaminiki tena,na ....kwa taarifa yako kila hatua unayokwenda, kila
mtu unayekutana naye unaonekana....kosa dogo mke wako ataona kila kitu, na
mkweo nasikia anafika huku mjini hivi karibuni....’akambiwa
‘Ni nani kawafahamisha
hilo, mbona hakuna anayefahamu ....?’
akauliza kwa hasira
‘Ndio ujue
kuwa kila kitu mnachokifanya kinajulikana.....sasa nataka kesho peleka huko
mzigo, ukifika hapo usubiri, utaambiwa kinachofuata...’akakata simu, alijua
kuna mtu anafuatilia hiyo simu.
Profesa
akamaliza, na kutoa ile kofia ya kuziba mdomo, aliyokuwa kavaa, na kwa haraka
akatoka pale kibandani na kutembea kuelekea sehemu nyingine akasubiri,
haikupita muda, akaona gari likifika eneo hilo, na mtu mmoja akatoka na
kuonekana akiangalia huku na kule...
Profesa
akaondoka hapo kwa haraka na kwenda sehemu nyingine ilikuwa ni sehemu ya
vibanda vya mitandao, akalipia pesa yake akaingia kwenye mtandao, kwa haraka
akatuma alichotaka kutuma kwenye mtandao,...., halafu akaondoka hadi kibanda
kingine cha simu.
‘Umeona hiyo
picha niliyokutumia....’akasema
‘Picha
gani....?’ sauti ikauliza kwa hasira, na wasiwasi
‘Hii ni
kukuonya tu, fungua simu yako uone, maana huamini kuwa tuna uchafu wako mbaya
zaidi, na picha hiyo ipo tayari kutumwa kwa mkeo...’akaambiwa,
Profesa
hakusubiri, akatoka hapo na kuchukua usafiri hadi mitaaa mingine ya mji, na
kutafuta kibanda cha simu, akapiga hiyo namba tena.
‘Umeiona
hiyo picha...?’ akauliza
‘Kwanini
unanifanyia hivyo...’sauti ikauliza ikionyesha kunyong’onyea
‘Kwasababu
umejifanya mjanja, umeajiri watu wa mitandao kutafuta simu ninazo piga,....sasa
nikiona dalili ya mtu akinifuatilia, naituma hiyo picha mkeo...ipo tayari
kwenye mtandao....’akaambiwa
‘Tafadhali,
usije kufanya hivyo, na tulikubaliana usiweke picha kwenye mtandao kwanini
umefanya hivyo.....?’ akauliza
‘Na
tulikubaliana kuwa hilo ni mimi na wewe na hao watu waliokuwa na hiyo video,
wewe sasa umefaya nini....?’ akauliza
‘Sikiliza mimi nimeshaachana na hao watu, nimewaambia
siwahitaji tena, kama wanafanya lolote wanafanya kivyao, sio mimi siwatai tena...’akasema
‘Mimi hilo
silijui,maana wewe ndiye ulikiuka masharti,. Kwahiyo kitakachotokea baadaye
usije kunilaumu...’akasema na mara akasikia sauti kwenye simu ya kike, akajua
huyo ni mke wake
‘Mume wangu
, upo wapi....Kuna mtu kanitumia ujumbe wa picha lakini haifunguki..’sauti
ikasema na huyo mumewe akasema
‘Ufute huo
ujumbe haraka usije kuufungua, inawezekana ni virus, hujasikia wakisema ukipokea ujumbe kama wa picha uufute
kabisa.....’akasema hakujua simu bado ipo hewani
‘Haufutiki..’sauti
ya kike ikasema
‘Oooh, Hebu
ilete hiyo simu,.....’kukawa na ukimia fulani, profesa hakupoteza muda, akatoka
hapo na kupanda usafiri hadi mtaa mwingine wa mji, na kusubiria muda maalumu.
******
Wakati
profesa akihangaika, mtaalamu alikuwa kwenye mitambo yake akifuatilia
kinachoendelea, akiwa keshajiandaa kwa hatua nyingine na muelekeo mwingine,
alikuwa keshaamua, alihamia kwenye
chumba kingine na kumwambia katibu muhutasi wake, hataki mgeni, hataki
usumbufu,....
Akainua simu
yake na kumpigia jamaa yake....
‘Umemuona,....eeh,?’
akauliza
‘Ndio
nimemuona, yupo mitaa ya kati, ....kavaa kofia pana,...yupo kwenye chumba cha
mgahawa anakunywa maji...na kuvuta sigara,....’akasema
‘Ok,nimeshakuona...sasa
sogea hadi ....ok, hapo hapo, upo karibu naye sasa sio.....?’ akauliza
‘Ndio yeye kavaa
kofia ana mawani meusi,...., na ndevu yes, ndio yeye,ok ok, sawa tatizo kazima simu
yake, angewesha ningemuona, lakini sio hoja, wewe hakikisha unakuwa karibu yake
muda wote....’akasema
‘Kwahiyo
mimi nifanye nini....?’ akauliza
‘Wewe subiri
nitakupa maelekezo....hakikisha unafanya ninavyokuambia, usimsogelee sana,
akagundua unamfuatilia, wewe mfuatilie tu kila anapokwenda, kwa umbali huo....’akasema mtaalamu
Halafu
akakata simu na kupiga sehemu nyingine...huku akisema;
‘Lazima hapa
nitumie pesa kidogo .....bila hivi,....nikitegemea huu mtandao sitakuwa na
uhakika zaidi, hawa ndio watakuwa ishara yangu.....’akasema akisubiria mtu
apokee simu
‘He is too slow,kupokea simu.....’akasema,na
mara mtu akawa hewani na yeye akatoa maagizo
‘Hakikisha
huyo jamaa akitoka unamfuatilia nyuma,...na hakikisha hapotei usoni mwako,wewe
kazi yako ni kumfuatilia tu,na kila
hatua nitakupigia simu.....usije kufanya zaidi ya hapo, ....malipo yako ni kwa
kazi hiyo tu.....’akasema na kukata simu.
‘Huyu ni
rahisi kumfuatilia maana simu yake ipo hewani, nimeshamnasa,...mmh, hata huyu
wa kumfuatilia sio muhimu sana....lakini naona kuna watu zaidi ya
mmoja,....mmh, hapakuna tatizo, huyu mtu ana watu karibu....’akasema
‘Inabidi
niongee na profesa awe makini, lakini profesa kazima simu,....ngoja nione la
kufanya..alisubiria hadi profesa alipokuwa kwenye kibanda cha simu, kwa kutumia
huyo mtu anayemfuatilia, akapiga simu kwenye hicho kibanda akitarajia profesa
atapokea lakini haikufanyika hivyo
‘Hamna shida
...nitaona la kufanya....ni lazima nipata mawasiliano ya hawa watu waliomzunguka
huyu jamaa....ni lazima....ngoja ninase mawasiliano yao.....’akasema akifanya
vitu vyake
‘Ok,
....poa,na hapasawa kabisa simu itakayoingia au kutoka nitakuwa nayo hewani,
...test...akasema na mara akasikia sauti ya mtu akipiga ...
‘Hahaha....this is a crazy profesa...anajua
kuigisa, hahaha....wanacheza na mtaalamu...’akasema na akiwa kaweka vyombo vya
kusikilizia masikioni.
‘Everything now is fine....ni swala la muda...kama profesa
atafanya nilivyomuelekeza,pesa yote itakuwa mikononi mwangu, na hapo ataoana
vumbi langu..hahaha....
Akaangalia
kwenye mtandao wake, akawa anafuatilia kitu...upande mwingine....
‘Na huyu
mpelelezi, anajifanya mjanja,ngoja nione yupo wapi....’akasema akitafuta
jambo....mmmh, .....yupo wapi huyu mtu.....ok,ngoja nitamtafuta baadaye,hana
shida kwangu huyu mtu....’akasema huku akikagua kitu kingine
‘Huyu mtu
vipi mbona hatulii sehemu moja....’akawa anasema huku akiangalia saa yake, akataka kupiga simu kumuulizia mtu wake,
lakini akaona asubirie. Halafu akapiga
‘Mbona hukai
sehemu moja....?’ akauliza
‘Ni mtu
wako, kapanda gari hadi mtaa mwingine ndio namfuatilia....’akasema
‘Ok poa
hakikisha humpotezi, nakuona wewe....akiwasha simu tu nitakuwa naye,
lakini....ok, ok,endelea kumfuatilia....’akasema na kukata simu
‘Mhh, kumbe
mjanja ngoja tuone.....’akasema akiendelea ku angalia kwenye komputa yake,moyoni
akiwa na mipango mingi, akijua leo ni siku ya kupata pesa nyingi , pesa ambazo
zitamfanya anunue mtambo mwingine mpya wa kisasa utakaomfanya aone mbali zaidi,
aone shughuli zote hapo mjini na nje ya eneo lake na hapo ataweza kupanga dili
nyingi za kumuingizia pesa
Alishaona
pesa hiyo itamfaa kwa mambo mengi, na kwahiyo kinachohitajika ni kuhakikisha
inafika mkononi mwake, na yeye ndiye awe na mamlaka nayo, na ikibidi aichukue
yote peke yake...
Akajilamba
mdomoni,kwa uchu, akawa anaangalia kwenye komputa yake, na wakati anataka
kufanya kitu kwenye komputa yake mara
mlango ukagongwa...
‘Who the hell....’akasema kwa sauti
kubwa,na mara mlango ukafunguka...na alipogeuka kuangalia, akajikuta anaangalia
mtutu wa bastola..
*******
WAZ LA LEO: Usije ukajiona mjanja kwenye kazi
za dhuluma, utafanikiwa leo, lakini jinamizi la kudhulumu litakuandama usiku na
mchana, ukumbuke wale uliowadhulumu, wanalalamika, wanaomba, ....familia zao
zinateseka, kwa sababu ya dhuluma zako...
Na wengine
wanakufuatilia usiku na mchana....na japokuwa wewe utawaona hawana lolote
kwako, hawajui kujitetea, sio wasomi.. lakini yupo mwenye uwezo wa kuwasaidia, kuwatetea,...muumba
wa mbingu na ardhi, ..kumbuka dhuluma haidumu, ipo siku utaumbuka tu.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment