Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, July 9, 2015

RADHI YA WAZAZI-16Wawili hawa yaani mke na mume wa mhanga wa mlungula walikuwa na kawaida ya kila mwezi kukaa na kupiga mahesabu ya mwezi, kila mmoja analeta matumizi yake na mahitajio ya nyumbani kwa ujumla.

 Kwahiyo kama kawaida mke akaleta mahitajio yake ambayo hayakuwa na utofauti na miezi mingine, lakini mume alipoleta mahitajio yake ikawa karibu mara tatu ya yale ya kawaida, mke ikabidi ashituke, na kuulikza kulikoni, na mume akatoa mlolongo wa madai yake na yote hayakuwa ya ukweli,ilimradi tu apate fungu lakutosha kulipia pesa anayohitajiwa kuwalipa watu wa mlungula.

 Ni kwanini aje kukubali kulipia pesa zote hizo,na je kweli zitapatikana..mke atakubali,....

Tuendelee na kisa chetu....

*******

‘Pesa yote ya nini....?’ mkewe akauliza akionyesha uso wa kushangaa ,na mume akiwa anamkwepa mkewe wasiangaliane akasema;

‘Nina matatizo mengi kwa kweli mke wangu...sikutaka kukuambia, ila niamini tu....'akasema

'Haa,nitakumini vipi,..wakati unajua hapa tunakwenda kwa mahesabu kama kawaida yatu,mimi siwezi kukubali pesa yote hii itumike kwa mambo yasiyo na msingi....'akasema mke

'Yana msingi mke wangu ndio maana nimeyaleta hapa..viginevyo nisingeyaleta niamini mke wangu....'akasema

'Niambie ni kwaajili ya kitu gani...?' akauliza
'Mke wangu tatizo lilianzia kwenye uharibifu kutokana na tatizo la umeme,na mimi nikaonekana ni mzembe,ili nisifukuzwe kazi nikakubali kubeba hiyodhamana, nilipe...'akatunga uwongo

'Haiwezekani...'akasema mkewe

'Ndio hivyo mke wangu, tatizo hilo liliharibu hadi vitu vya watu, kwa umeme,na ikabidi niingiziwe kwenye deni,na kwa vile vifaa vingi vilikuwa vya wateja, nikatakiwa kulipia kwa haraka, ...nikaona niwakope wenzangu kwa riba, ....unajua tena riba, ....nikachelewesa kulimalizia deni, sasa deni limakuwa kubwa, ila kasema naweza kumlipa kwa awamu mbili, au tatu...’akadanganya

‘Mbona hukuniambia, na ni kifaa gani chenye gharama yote hii....’akauliza mkewe, akionyesha mashaka.

‘Ni kifaa chenye thamani kubwa..usijali mke wangu nitalipa halafu nitaangalia jinsi ya kufidia haya matumzi baadaye...’akasema

‘Hapana tatizo sio jinsi ya kuja kulipia hizi gharama, tatizo ni uhakika..na nauliza kwanini hukuniambia mapema, kama kuna tatizo kama hili..?’ akauliza mke mtu

‘Nilijua nitalimaliza mwenyewe,...huoni nilishaanza kulipa, nikaona mwenzangu atanidai pesa ya kawaida, kumbe kawezeka na riba juu,..kiukweli sikutaka kukusmbua mke wangu, ila sasa hali imekuwa ngumu.....’akataka kujitetea

‘Mume wangu naona kuna kitu unanificha,...kwanini huniambii ukweli, kwani mimi ni nani kwako?’ akauliza na mume akawa mtizama mkewe kwa macho ya kujiiba, na kuuliza

‘Kwani mke wangu kwanini ..ina maana huniamini au...?’ akauliza

‘Nimekuuliza swali mimi ni nani kwako...?’mke akauliza kwa sauti ya msisitizo

‘Wewe ni mke wangu....’akasema

‘Je mke na mume wanahitajika kufichana mambo yao,..?’ akauliza

‘Hawahitajiki kufichana, lakini kuna wakati mwingine unatumia busara kuangalia jambo lenyewe,...kwa mfano hilo la kazini inatokea mara kwa mara, na nasawazisha mwenyewe ,sio lazima mke ajue hayo ya kazini....’akasema

‘Mume wangu...usinione kuwa mimi ni mtoto mdogo,tumeishi miaka mingi, na huwezi kunidanganya kwa lolote lile,...unakumbuka kipindi tunakuja huku ulaya nilikuwambia nini....?’ akauliza

‘Uliniambia nini...mmh, hebu niambie tusizungushane....’akasemahuku akiangalia saa

‘Ok,...hebu niambie hii barua inatoka benki,ni ya kwako,au sio...?’ akauliza mkewe akiwa kashikilia hiyo barua mkononi...na mume wake alipoiona akashituka kidogo,lakini akajisawazisha, na kusema

‘Mhh,nani kaileta hii barua huku nyumbani...?’ akauliza kwa hamaki huku akichukua kwa haraka kutoka mkononi kwa mke wake.

‘Mtu wenu kazini alipitia hapa,akanikuta, akasema ukija nikupe,....’akasema huku akimtathimini mumewe, kwa kumuangalia usoni,na mumewe akijua mkewe haijaifungua akaweka mfukoni

‘Kwanini huisomi hiyo barua, ...na benki nijuavyo, wasingeliandika jina lako moja kwa moja kama sio akaunti yako, ina maana una akaunti yako binfasi,...? Mbona hujaniambia kuhusu hiyo akaunti...?’ akauliza mkewe

‘Nilikuwa nayo zamani, haina pesa, ndio maana benki wanataka kujua kwanini, kama nitaweza kuiendeleza....waifunge tu, nilipokuja, nikaona niiendeleze, kwa kupitishia pesa za kampuni, wakati nikipokea kwa dharura...’akazidi kudanganya

‘Una uhakika na unachokisema mume wangu...’akauliza mkewe,akimuangalia mumewe kwa mashaka.

‘Kwanini unasema hivyo mke wangu, yaonyesha kama huniamini, au...?’ akauliza

‘Nakuuliza una uhakika na unachokisema,...mume wangu kuna tatizo gani, mbona uwongo unazidi siku hizi, tangia tuje huku ulaya nakuona umebadilika, ni nini tatizo lako,niambie nikusaidie...’akasema mkewe

‘Hakuna tatizo kabisa mke wangu,niamini, ni hayo ya kazini, nikiyamaliza, nitakuwa na amani...tusaidiane kwa hilo...’akasema

‘Sawa,....mimi nitakusaidia nitakachofanya, nitapitia kazini kwako niongee na bosi wako nione jinsi gani ya kulimaliza hilo deni, maana ni ajabu mfanyakazi aharibu kitu kwa bahati mbaya, halafu abebeshwe deni...’mkewe akasema

‘Haina shida mke wangu,..., wala usifanye hivyo,hayo ni maswala ya kikazi, nitaonekana natoa siri za kampuni, usifanye hivyonitalimaliza tu, muhimu nipate hizo pesa....’akasema

‘Ok, nimekuelewa,sasa unataka shilini ngapi kupunguza hilo deni...?’ akaulizwa mkewe, akimuangalia mumewe kwa macho ya udadisi

‘Basi angalau nusu ..niweze kupunguza punguza...’akasema

‘Pesa tuliyo nayo tasilimu hapa ni kwa ajili ya kutuma nyumbani, hii haiguswi,  nimeitoa tu kwa vile inahitajika...’akasema

‘Sawa mkewe wangu...’akaitikia lakini akili haikuwa sawa...

 Basi mkewe akakubali hiyo nusu ya kile kiwango alichoomba, na kiwango hicho ndicho alichotuongezea na pesa aliyokwisha kuitoa kwenye akaunti yake na kutupa sisi lakini ilikuwa sio nyingi....’akasema

‘Lakini sasa kilichoharibu, ni kuwa jamaa alikuwa kama kachanganyikiwa, maana na sisi tulishamkaa kooni, ....akawa hatulii, sisi tuliweka shinikizo zito...’akasema

‘Kama hatukupata hizo pesa kwa kiwango hicho mkeo atajua kila kitu kilichotokea huko kwenye bar, kwanza umefanya hata binti wa watu afukuzwe kazi, ...’nikazidi kutilia msumari

‘Lakini...sija..mlazimisha....hata sijui ilikuwaje,...nahitaji kuongea na huyo binti nijue ukweli,nahisi kuna kitu kanifanyia....’akasema

‘Kakufanyia nini,...picha zinaonyesha kila kitu, ukitumia nguvu,...kuna kanda ya video,haifichi kitu,...na kwanini aje kukufanyia sasa hivi, je hukuwahi kumtongoza kabla,je ulipofika hapo siku hiyo, wewe hukua umelewa,halafu ukaongeza pombe nyingine,kama ulikuwa huwezi kunywa zaidi kwanini uliongeza, ina maana ulidhamiria...’sauti ikamwambia kwenye simu

‘Mimi najijua, najua kiasi cha kunywa, ila binti aliniomba nifike kwenye sherehe yao, na huko ndio  nikanywa,...sizani kama kinywaji kile ningeliweza kulewa kupita kiasi....nilikunywa chupa mbili....oh,hata sijui ilikuwaje...’akasema

'Kwahiyo kumbe hukuwa umelewa...?' akaulizwa

'Sikumbuki,ilikuwaje...'akasema

‘Ndio hivyo..ulichokifanya ni kitendo cha aibu,hiyo picha ni moja ya vitendo vyako,na ukatumia nguvu...mtu mzima kama wewe unabaka...huna aibu,una mke na watoto,unatumia nguvu, ina maana mkewe hakutoshelezi,....sasa sikiliza ili aibu hiyo iishie huko huko..sisi tunajua lakufanya, tayarisha dola laki mbili..tulimalize kabisa...tutafuta kila kitu kwenye mitambo ya hapo .....’akaambiwa

‘Dola lakini mbili..!?’ akauliza kwa mshangao

‘Tunahitaji kuondoa picha zote kwenye mtandao wa hiyo bara, unajua wanamitambo yao inachukua matukio yote, sasa kufanya hivyo gharama yake ni kubwa sana...,pia tunahitajika kuwafunga mdomo walinzi...na wale wote walioona hilo tukio...na gharama nyingine ....’akaambiwa

‘Lakini kulikuwa hakuna watu...’akasema

‘Ile ilikuwa sherehe,..au sio..?’ akaulizwa

‘Ndio lakini baadaye nakumbuka tuliondoka na binti ....tukawa peke yetu wawili...’akasema

‘Ehee,umekumbuka eeh,mliondoka na binti,...mkabakia wawili,..mke akisikia hivyo atalichukuliaje, kwanini mliondoka...?’ akaulizwa

‘Oh...sijui....lakini ndio nasema hakuna aliyeona kilichotokea...’akasema

‘Kitu gani ...kiseme hicho ambacho watu hawakuona,au tukutumie  picha nyingine...unaona kumbe ulikua na akili zako timamu unakumbuka ulichofanya, halafu unasema ulikuwa hujitambui, ....’

‘Ni kweli....sikuelewa nilichokifanya...’akajitetea

‘Hahaha, ulikuwa umelewa, siku zote si unalewa wewe...sema ukweli wako,...ulifanya makusudi ...ulikuwa unatafuta mwanya kama huo..ulishamtamani binti wa watu...ndio ukatumia nguvu...au sio...’akaambiwa

 Basi akatishiwa mpaka akaingia kwenye mtego, akawa hana amani, akawa sio muangalifu, na kila baada ya muda fulani akawa anapata barua yenye picha za matendo yake...

‘Wenyewe wamesema watasubiria masaa matatu tu...,baada ya hapo,usije kuja kulaumu, ikifka  kwa wamiliki sio rahisi tena kufuta,...na wao kamaunavyojua, wameshalinakili hilotukio kwenye video, na ndio nikaipata nakala....sasa, kabla barua mojawapo haijafika kwa mkeo,hatutaki kumtumia kwenye simu maana itakuwa ni hatari kwako...’akaambiwa, kumbe sisi wenyewe hatukutaka kutumia simu za mikononi, kwani ikifikia kubaya, simu huku hazina siri.

'Kwani wewe ni nani....?' akauliza

'Usitake kujua mimi ni nani...utaumia zaidi, nikikuambia ni mwandishi wa magazeti ya udaku utasemaje....'akasema

'Sasa nitaaminije kuwa habari hizo hazitakwenda mbali zaidi hadi kumfikia mke wangu..?' akauliza

'Mimi nakuhakikishia ukilipa hizo pesa nakala zote utazipata,vinginevyo kamahuamini sawa,usije kunilaumu....'akasema

Kwahiyo kwa haraka ndio akaenda kuchukua hizo pesa kwenye akaunti yake, na huko nako benki wakamgomea,hadi akamlishe hizo nyaraka zinazohitajika, akaomba sana na kubahatika kupata kisi hicho kidogo,na akajua atamshawishi mkewe, aongezee, angalau ifikie, dola laki moja,lakini hata hiyo haikuwezekana.

‘Usipolipa hizo pesa uchafu wakoutamfikia mkeo...’kauli hiyo ikawa inamuandama
Kwahiyo alipochukua hizo pesa, kwa vile zilikuwa kidogo hakupitiliza moja kwa moja sehemu aliyopangiwa kuzipeleka, sababu mojawapo ni kuwa kiwango kilikuwa kidogo, lakini pia alitaka kucheza na muda, ili ikiwezekana apate kujua jinsi gani ya kujiokoa, hakujua kuwa anapambana na wataalamu.

Alipofika nyumbani kwa haraka mkewe alikuwa hayupo, si yeye anafanyia kazi karibu na kazini kwake,kwahiyo angeliweza kufika nyumbani na kuondoka, bila kuchelewa kazini, na bila hata mkewe kujua, hapo wazo laharaka likamjia...

‘Hii akiba ni kwa ajili ya kutuma nyumbani kwa ajili ya shughuli za huko, usije kuigusa....’akakumbuka kauli ya mkewe, lakini kwa upande mwingine akikumbuka kuwa kuna uchafu utamfikia mkewe,akaona heri fedheha kuliko hiyo kashifa.

 Akalisogelea lile kabati la akiba, akafungua droo ya pesa, na kuongeza kiwango, angalau, ifikie kiwango fulani, alichoona kinatosha japokuwa bado kilikuwa kidog sana, alichukua akijua kuwa benki watamruhusu kuchkua pesa nyingine akikamilisha hizo nyaraka na  atakuja kuzirejesha hizo pesa kabla mkewe hajafahamu...

 Wakati bado anafikiria zaidi, kwani pesa ilikuwa bado ndogo, mara akasikia simu ya hapo ndani ikiita, akajiuliza ni nani anaweza kupiga simu nyumbani kwake,wakati wengi wanajua muda kama huo wote wapo nyumbani, kwanza akaogopa kupokea,...lakini ilipoita zaidi na zaidi, akajua huyo mpigaji atakuwa anafahamu kuwa yeye yupo nyumbani, akaamua kuipokea, lakini kwa mashaka.

‘Wewe mtu, kuna mtu tumemtuma kazini kwa mkeo akiwa na moja ya uchafu wako, si ndivyo unavyotaka wewe, unajifanya kichwa maji, je upo tayari uchafu wako ufike kwa mkeo....’simu ikamwambia

‘Kwanini mbona tulishakubaliana, kuwa nikachukue hizo pesa...’akaanza kujitetea

‘Tulisema ukitoka benki tu, uhakikisha hizo pesa unazipeleka wapi..?’ akaulizwa

‘Ndio nataka kuzipeleka sasa hivi...’akasema huku akihaha...unajua kuhaha,...usiombe ukutane na mtu kama profesa akiwa kwenye hizo anga zamlungula,... hasa akishakufahamu ulivyo..

Na sauti hapo ilikuwa sauti nzito ya jitu kubwa, lakini ukiniona sijai hata kiganjani kama yule mama alivyosema, mwili wa profesa sio mkubwa,ni mwembamba tu,lakini sauti iliyotoka hapo ni ya jitu lamiraba minne...

‘Nakupa sekunde sifuri, ziwe zimeshafika sehemu husika,..na ole wako ufanye makosa, maana makosa hayo yatasababisha siri zako kufichuka, siwezi kubeba dhamana ya kufuta uchafu wako, wakati wewe husaidii lolote, nitaonekana mungo kwa wataalamu wa huo mtandao, ambao wanahangaika kufuta kila kitu,..., wewe unachelewesha...’akaambiwa

‘Japokuwa kuna tatizo kidogo, lakini ndio nipo mbioni kuzipeleka hizo pesa...’akasema sasa akiwa anaangalia kupitia dirishani kama ataona mtu,....angemuona nani.

‘Tatizo...!, tatizo gani,...unataka kuleta mzaha sio...’sauti ikasema,na hapo akaanza kujielezea, ilivyokuwa, kuwa ana tatizo na benki,wanahitajia maelezo, na mkewe aliipata hiyo barua, ...kwahiyo benki wakampa sehemu ndogo tu, mpaka hapo atakapokamilisha hayo maagizo...’akasema

‘Kwahiyo una dola kiasi gani hapo ulipo?...Mimi naona nisipoteze muda wangu na uaminifu wangu, naona niache, maana huo sasa ni utani, ...’nikasema kwa hasira

‘Ni kweli kabisa kama unataka kuthibitisha nenda benki watakuleza maelezo hayo,sasa hivi kuna uhakiki wa dhamana zote ....’akasema, ni kweli hiyo taarifa ilishatoka, nalifahamu hilo, hatujua kuwa huyo jamaa hajalifanikisha hilo.

‘Naona unapoteza muda, hakikisha unafikisha hizo pesa zote ulizo nazo,mimi nakuona hapo nyumbani, na kila unalofanya nakuona...’nikasema ni kweli pale nilipo nilikuwa namuangalia na kiona mbali...tulikuwa tumejiandaa..bro,usinione hivi...’akasema

‘Na..na..zileta...sasa hivi...’akasema na kwa haraka akakurupuka na zile pesa, akawa anatoka hapo nyumbani kuelekea hiyo sehemu,...huku akihaha,..jamaa alichanganyikiwa vibaya kweli, na wakati anatoka ndio hapo mambo yakaanza kumuendea kombo, kwani alikutana na mshituka asioutarajia,....

‘Mshituko gani...?’ akauliza kamamtu alipoona mdogo wake katulia haendelei.

‘Bro....hayo utayasikia sehemu ijayo,ila kwa kukudokezea,...ni kuwa  wakati anafungua mlango,alijikuta akikutana uso kwa uso na mkewe....

‘Mkewe...???’ akauliza kaka mtu


WAZO LA LEO: Jambo lolote lisilo halali, halina amani , tuache kujitafutia magonjwa ya shinikizo la moyo kwa kufanya makosa yasiyo lazima, kwa nia ya kujichumia kipato kisocho halali, kudanganya,..kufisidi..nk.Muhimu ni kujitahidi katika matendo yetu yote kusimamia kwenye kweli na haki.

Ni mimi: emu-three

No comments :