Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeSaturday, June 13, 2015

RADHI YA WAZAZI-3Ikapita miaka kumi na sita baada tukio hilo la kupotea mtoto, na wakati wengi wameshasahau,  isipokuwa mtu mmoja tu...mama wa mtoto aliyepotea, mama huyo alikuwa siku zote akimtaka mtoto wake, akilia...na alikuwa akisema anajua mtoto wake yupo hai,..

'Nina uhakika mtoto wangu yupo hai...kuna mtu kamuiba mtoto wangu...'akawa anasema, lakini tofauti na mawaz yake hayo ndugu na jamaa wao walijua kuwa mtoto huyo hayupo tena duniani, walishakata tamaa na kusema mtoto huyo hayupo hai tena, wakawa wanampuuza huyo mama.

Basi siku moja akaonekana jamaa mmoja anayeitwa profesa, kutokana na utaalamu wake wa madawa, na kuongea lugha nyingi, alionekana akiwa kaandamana na kijana, wakiwa wameteremka kwenye basi na kwa muda huo walikuwa wakitembea kuelekea kwenye nyumba mojawapo, kijana yule alionekaa mtanashati akiwa kavalia kisasa , mawani ya jua, unajua tena vijana....

Dad where are we going...?’ kijana akauliza akiangalia huku na kule huku akikunja pua kuashiria kuna harufu asiyoipenda

‘Nilikuambia nataka kwenda kukuonyesha asili yako,...ambapo baba yako yupo, na ikibidi nitakuonyesha mama yako...’yule profesa akasema

But you told me before, I don’t have a real parents, and even in school, I registered that way, you know what I mean..., then to day....hahaha dad!’akasema akionyesha mshangao

‘Yah, it supposed to be that way,.... but in reality you have your own parents, and me, am not your biological father..’akasema huyo profesa,  na kijana japokuwa alikuwa anafahamu Kiswahili lakini hakupenda kabisa kuongea Kiswahili, ...

Kijana huyu miaka mingi alikuwa akisoma huko nje, kwenye shule maalumu ya watoto mayatima, kuna muda walikuwa wakija likizo, na huwa anapelekwa shule za hapa nchini ili kukijua Kiswahili, lakini hakukipenda, japokuwa alikuwa mwepesi kujua lugha yao, kwani kwa muda mfupi akawa anakijua Kiswahili,, na alishaambiwa kabisa akifika kwao ajitahidi kuongea kiswahili ili aweze kuelewana na jamaa zake.

‘Mhh samahani mzee, ngoja kwanza...’nikataka kumkatiza, msimualiaji, lakini hakutaka kukatizwa akaendelea kuongea

‘Profesa na yule kijana wakaingia kwenye eneo lililozungushiwa miti ya michongoma kama ukuta kuzunguka eneo hilo na ndani yake kulikuwa na nyumba za miti zilizokandikwa kwa udongo,..., na kijana akawa anaangalia yale mazingira kwa macho ya udadisi huku akikwepa asichafuliwe na mavumbi, na uchafu uliokuwa umetapakaa , siunajua tena kijijini.

‘Kuna harufu mbaya....’akasema na kipindi hicho profesa alishapiga hodi na aliyefika kumpokea alikuwa mtu mzima, na wakaanza kuongea

‘Oh, bwana mdogo ndio umefika...nilijua unatania, maana kila mara ukifika unaishia huko mjini, sasa naona umetimiza ahadi yako, haya nambie kilichokuleta, maana huji hapa bila sababu?’ akaulizwa

‘Ndio nimefika kama nilivyokuambia, nimeteremka hapo kwenye bas, na kama nilivyokuelezea kwenye simu, leo nimeamua kutimiza ahadi yangu,  tumefika...’akasema na yule mtu mzima akawa anamkagua huyo mtoto, na mtoto akawa anaangaza macho huku na kule wala hakusalimia

This is your dad,....’professa akasema

My Dad!...gosh....’akasema yule kijana akionyesha ishara ya kukata tamaa, alimtupia jich huyo mtu mzima halafu akageuka kama anataka kuondoka.

‘Huyu ndiye huyo kijana wako niliyewaambia, ana miaka kumi na sita tu hapo, sema li-mwili limekua haraka tu...kachukua mwili wako,....huwezi kuamini kuwa ana umri huo, ...sasa kama unavyomuona keshakuwa mkubwa, msomi, hapo ni kiingereza tu...si ulitaka awe msomi....huyo hapo, kuna kazi kidogo ya kumbadili badili, si unajua muda mwingi alikuwa huko nje...’akasema profesa

‘Sasa mbona hasalimii, ina maana hajui Kiswahili....halafu naona kama katoboa masikio, au macho yangu...hapana, ...mwanaume umetoboa masikio...wewe mtoto hebu kuja hapa...eti au...?’ akauliza huyo mtu mzima huku akikunja uso kwa hasira

‘Hahaha bro, ujana huo...usijali, nimehakikisha havai maherenai, ni kuiga tu, lakini nimeshaanza kumbadilisha, ....na kiswahili anafahamu kwa shida, lakini unajua bro, hawa vijana wakiwa shule, Kiswahili hakitakiwi, kwahiyo kazoea kuongea kiingereza...’akasema huku huyo mtu mzima akiwa anaendelea kumkagua huyo kijana, akaona sura yake kabisa akatikisa kichwa kukubali kuwa hiyo ni damu yake, halafu akasema;

‘Kweli ni damu yangu, ila...mmmh, sijui kama nitaelewana naye, kwa tabia hiyo..mmmh, ...’akatikisa kichwa

‘Atabadilika tu, ...usijali bro...ila kwa vile bado anasoma na natakiwa niwe naye, ..namfudisha fundisha ili akirudi shuleni, awe hajasahau...ualimu kwangu bado upo kwenye damu japokuwa niliamua kuukimbia...’akasema

‘Wewe mtoto hebu salimia, hujui mimi ndiye baba yako...’akasema huyo mtu mzima kwa ahsira akimsogelea kutaka kumshika mkono,  na yule kijana akasogea pembeni kama vile anaogopa kuchafuliwa

Sorry...... ‘ akasema na kugeuka kumuangalia profesa

‘Dad, lets us go...’akasema huyo kijana akimuashiria profesa kwa mkono

‘Hapa ndio nyumbani kwenu, unataka kwenda wapi, ...’akasema huyo profesa

Lets us go dad, I don’t feel well, y’know what I mean, its ....harufu mbaya....’akasema akianza kuondoka

‘Unasema nini, harufu mbaya, huna adanu kabisa wewe, huku ndio kwenu, hata kama kuna kunanuka...wewe bwana mdogo, meniharibia mwanangu...’akasema huyo mtu mnzima akiwa katahayari, katika maisha yake hajawahi kukutana na hali kama hiyo, kijana mdogo kuoyesha kiburi na zarau kiasi hicho, alitamani kuonyesha ukali wake lakini akasita,....

‘Hahaha bro, ndio utandawazi huo, kijana kakulia shuleni...na kabadilika sana tu, ningekuja naye mapema, mbona igekuwa kazi,...tulipokuwa huko nje walikuwa wakifuata taratibu za huko, huko watoto wana haki zao, hawatakiwi kuchapwa..na vitu kama hivyo....,unajua tena, kwahiyo ameshabobea maisha ya huko- kizungu, si unajua tena..., usijali, mimi nitamweka sawa, ila kwasasa mvumilie tu...’akasema profesa

‘Sikiliza, bwana mdgo,  nakupa wiki moja,...mbili,  nataka huyo mtoto abadilike, ajue kuwa mimi ni nani....unasikia, huwezi kuniletea mtoto ambaye ananiona mimi kama kinyaa, ulimuona alivyofanya,..ananikunjia pua mmi....mmmh, yaani hapa ningeshamcharaza viboko....nyie watu nyie ..ondokeni hapa....’akasema akinyosha kidole cha onyo.

‘Sawa bro....lakini...’akawa anajitetea.

‘Sitaki kujitetea,....huyo mtoto hana adabu,  na nakuambia akileta huo upuuzi wake hapa kwangu, nitamuua, unasikia,...’akasema huyo mtu uzima kwa hasira huku akimuangalia huyo mtoto kwa jicho la ukali, na yule mtoto akashika kiuno

Whats,...you want to kill me, go ahead....dad, you hear that, ....lets us go...’akasema huyo kijana akianza kuondoka

‘Umenisikia bwana mdogo, ....nakupa wiki hizi mbili ukija naye hapa nataka ajue kuwa mini ni nani kwangu...vinginevyo, uniachie mwenyewe, kama nikufungwa nifungwe,..na hizo sheria zenu, mtoto nizae mwenyewe halafu nitungiwe shera, ai kakuambia....’akasema na kugeuka kurudi alipotoka, na huyo professa akasimama akishika kichwa.

You..., sikiliza, nilikuambia nini,...ukija huku ukijitahidi kuwa mtoto mwema, nilikuambia ukifanyay hivyo, nitakununulia pikipiki, sasa umeharibu...’akasema huyo profesa

I don’t care, ...sitaki pikipiki yako, sitaki cha huyo baba, lets go...home...’akasema na kweli ikabidi warudi na kwenda kwa huyo profesa....

********

‘Huyo profesa ni nani, na huyo mtoto ni nani?’ nikauliza nilipona jamaa katulia

‘Mhh, huyo profesa alikuwa mtaalamu aliyetokea uchina,...na alishaingia nchini akitangaza dawa zake, alipotea kwa muda,... tangu aliporudi na kipindi hicho ilipita kama miaka kumi na sita hivi ndio akaonekana tena,....’akasema

‘Pale kijijini ndiye aliyekuwa na nyumba ya kisasa, yenye kila kitu muhimu na zahanati yake ya dawa za kienyeji na dawa zake nyingi zlitoka nje, uchina...na nyingine alikuwa akitengeneza mwenyewe....’akasema

‘Alikuwa profesa kweli au ndio jina kutokana na utaalamu wake....?’ akaulizwa

‘Hahaha, kwani uprofesa ni nini, hebu fikiria mtu anajua lugha saba, Kiswahili kiingereza, kifaransa, kichina...eeh, kihindi..kitaliano, kireno na yinginezo, mtu anajua madawa, ...mazingaumbwe....katembea nchi mbali mbali, ulaya , bara asia,...hapo utasema nini, nyie mtu akijua kiingereza kidogo tu mnamuita msomi, sasa mimi ni zaidi ya kiingereza....’akasema

‘Ina maana alikuwa ni wewe...?’ nikauliza

‘Alikuwa profesa...elewa hivyo, sio mimi, ...usitake kuvuruga utaratibu wangu...’akasema

‘Haya endelea....nimekuelewa...’nikasema

‘Ukumbuke kauli ya huyo baba wa huyo kijana, profesa alipewa, wiki moja au mbili ili huyo mtoto abadilike na aweze kumtambua baba yake, awe na adabu, tena adabu zile za kjijini, na profesa aamtambua sana kaka yake, kuwa ni mtu wa namna gani, hawaivani kwa ukali wa kaka yake huyo,....alijua kabisa akimpeleka tena huyo mtoto kwa jinsi alivyo, ataumizwa, kwahiyo akawa anavuta muda, huku akijaribu kumfundisha huyo kijana jinsi gani itakiwavyo, lakini ilikuwa kama kutwanga maji kwenye kinu, kijana akawa mtu wa madharau, ....’

Basi profesa akaendelea kuishi na huyo kjana kwake, huku bado akiendelea kumuelekeza huyo kijana kidogo kidigo, wiki ya kwanza, ya pili , ya tatu, kijana bado hana muelekeo, na hataki kusikia habari za baba yake...ikafika muda akaona huenda sasa kijana atakuwa keshaelekea elekea akaona afanye majaribio, akaona sasa ampeleke huyo mtoto sehemu nyingine sio kwa huko kwa baba yake kwanza

‘Leo nataka ukamuone a real mother of yours...’akaambiwa

My mom, ...mmh, dont tell me, in all years you never told me about a real mother , a mom,,,,leo waniambia yupo mama...kama ni kama yule dad,....never,  I don’t want to see her....’akasema hivyo

‘Unakumbuka nilikuambia usome kile kisa cha `nani kama mama’ ulikisoma ukamaliza...?’ profesa akamuuliza

Its real a hot story....nimesoma, lakini mmmh, ni story tu...unataka kusema nini?’ akauliza

‘Katika hii dunia hakuna kama mama, ..unajua baba unaweza kumchezea, uka...mdharau kwa vile hakuwa na machungu nawe sana, lakini, mama yako ni kitu kingine...usije ukamdharau mama yako....’profesa akasema

‘Nimekaa miaka kumi na sita, simjui mama, wala baba, mama na baba yangu ni wewe...leo ndio waje kunitaka mimi....walikuwa wapi muda wote huo...kwanza niambie kwanini wewe huishi na mama yangu...?’ akauliza swali ambalo profesa hakutaka kuulizwa

I told you before, usiniulize kuhusu mama ....mke wangu...nilikuambia mke wanguu alinikimbia,...eti ...sikuwa na pesa,  nilimpenda sana, na nikaapa kama sitampata yeye sitaoa tena....ndio nikaanza kutembea duniani, ili nimuonyeshe kuwa mimi niazo, nimerudi nasikia eti kaolewa...so, ...tuyaache hayo, hayauhusu...’profesa akasema

‘Hahaha....dad, dad....your real very fun...all mothers wanaokuja na kukaa na wewe, leo huyu kesho huyu, ni nani hao.....si uoe tu mmojawapo....’akasema na professa akashika kichwa akimuangalia huyo mtoto

Profesa na huyo mtoto wamezoeana sana, na wakati mwingine wanakaa pamoja na kuongea maisha ya kawaida, na huyo mtoto amekuwa karibu sana na huyo profesa, ni msiri wake mkubwa, na mengi yake anayafahamu....

‘Sikiliza, ....mimi ni mwanaume unasikia, ulitaka nikae hivi hivi, ...wewe subiri ukue, utayaoa, kwanza hebu kajiandae twende huko kijjijini, nataka nimuone huyo mama yako ana tatizo gani , kama naweza kumsaidia dawa...ni mbali kidogo, tunakwenda kumuoa mama yako,...your biological mother, forget, about this temporary mothers, wanaokuja mara kwa mara hapa kwangu, they are nothing to me, one day I will mary my ....’akasema profesa huku akionekana kuwa mbali kimawazo

Hahaha dad, every time, unasema utamuoa huyo mama umpendaye, yupo wapi huyo mbona haji,....?’ akauliza

One day utamuna, atakuja....’akageuka kuingia ndani, halafu akasimama kama vile kakumbuka jambo, akasema;

‘Ni lazima leo twende ukamuona mama yako....ni muhimu sana, watu wasije kunielewa vibaya.....kabla matokea ya mitihani haijatoka, nataka ujuane na wazazi, ukirudi kusoma huko ujue wapi ulipotoka...wewe sio yatima, ...’akasema

‘Usije ukasema sikukuonya dad, unanielewa dad,...ulinipeleka kwa huyo unayesema ni baba yangu, uliona ilivyotokea...that old man, he is not my dad, ...mimi, naweza kuwa na baba kama yule, hahaha, hebu kwanza angalia hii sura,..handsome boy..hahaha...’akasema akijiangalia

‘Mhh, hapa eeh, tumepoteza mtoto,.nilijua shule itamtengeneza kumbe..oh, sasa hii ni lawama, ..huu ujanja ujanaj mwingine hausaidii...nilimpeleka shule ya misaada akijulikana hana wazazi....kumbe nimeharibu, lakini ningefanya nini..hili sasa ni garasa,garasa....’akasema profesa huyo akimuangalia huyo kijana, yule kijana akiwa anajiangalia kwenye kiyoo cha simu ya mikononi

Be ready..., ni lazima uende ukamuoe mama yako, mama yako anaumwa, na nimesikia siku zote anakutaja wewe, ....’akasema profesa

‘My mother, who one, ok, Ok, dad....siwezi kukataa kwenda, lakini ....usije kunilaumu....’akasema huku akiendelea kubonyeza boyeza simu yake....

Nb Ni nini kitatokea? kidog kidogo, si mnajua tena....


WAZO LA LEO: Ulezi bora wa watoto wetu ndio upendo wa dhati, kama ukimdekeza mtoto, ukaona ndio unampenda, ujue uafanya makosa makubwa, na labda ukataka aishi kijinsi maisha yanavyokwenda...kwenda na wakati, kitu ambacho hukufanyiwa wewe hivyo, ujue unamtengenezea mazingira mabaya huko baadaye. Mtoto alewavyo divo akuavyo.
Ni mimi: emu-three

No comments :