Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, April 15, 2015

NANI KAMA MAMA-58

               
‘Mama alipoulizwa nesi aliyemuona kwenye ndoto ni nani kwanza akaonyesha kama dalili ya kutaka kuinuka na madocta wakamsihi,  na kumshauri kuwa aendelee kulala,….

‘Wewe ongea tu huna haja ya kuinuka,..au umechoka kuongea kama umechoka tunaweza kukuacha upumzika halafu tutakuja kuongea baadaye, utumalizie hiyo ndoto yako.....’akaamabiwa

‘Hapana sijachoka, hasira zilipanda, ….’akasema

‘Kwanini?’ akaulizwa

‘Kuhusu huyo nesi, mimi nilimuona kwa macho yangu, maana alijifunua, sijui alijisikiaje mapaka akajifunua,...au ndio mungu alipanga nimuone ili baadaye uwe ni ushahidi,…kwahiyo sio kwamba namsingizia..mimi nilimuona huyo nesi kwa sura ….na huyo docta mwingine sijui yupo wapi…’akasema

‘Lakini hayo unasema umeyaona kwenye ndoto au sio?’ akaulizwa

‘Ni ndoto ndio…lakini ni ndoto inayonionyesha yaliyotokea, na kutokana na ndoto hiyo ndio nikakumbuka yaliyotokea… na ndivyo ilivyokuwa,….’akasema huyo mama

‘Ehe hebu endelea unasema kulipatikana kiumbe cha ajabu ambaye unahisi alikuwa ni mtoto wako, na hicho kiumbe cha ajabu akapewa jitu mwanamke kutokana na ndoto yako halafu ikawaje….?’ Akaulizwa

‘Ndoto …naona kama hamuaniamini…’akasema

‘Mama unajua sisi tunataka kukusaidia…na mwenzangu hapa ni mtaalamu wa mambo hayo anajua ni nini unachokiongea,….maelezo yako ndiyo yatamsaidia kubainisha ukweli,..mimi ni mtaalamu pia, lakini siwezi kuamua tu..ni lazima kuwepo na mtu mwingine ili niweze kufikia maamuzi yaliyo sahihi…’akasema

‘Nimekuelewa….’akasema

‘Ehe…tuendelee au umechoka…?’ akaulizwa

‘Baadaye wale watu-mijitu wakawa `wameshiba’....huo ni mtizamo wangu kuwa kwa vile walikuwa wanakula nyama zangu, sasa wametosheka, na kwahiyo wameshashiba, na mwili wangu utakuwa umebakia gofu tu…’akaendelea kusimulia huyo mama

‘Uliona wakila hizo nyama?’ akaulizwa na hapo akabakia kimia kwa muda, halafu akasema.

‘Kiukweli sikumbuki kuona wakila hizo nyama,…ni hisia tu kuwa walifanya hivyo…maana kutokana na maumbo yao huwezi kuwaona mwili wote, ila yule aliyekuwa kainama ndio niliweza kumuona kwa uzuri, japokuwa alikuwakajifunika uso…nikawa najiuliza kwanini wajifunike uso kama sio watu wenye nia mbaya kwangu…’akasema

‘Waliposhiba kwa uoni wako, kwenye hiyo ndoto, hao watu-mijitu walifanya nini, waliondoka?’ akaulizwa

Nilimuomba mungu wasiniache pale nikabebwa na mwewe au midege yenye uchu, au fisi maana kwa hisia zangu tulikuwa porini, pori nene lenye miti mikubwa, na mwanga mkali, na baridi kali haliwezi kukosa wanyama wakali…nikawa najaribu kulia , lakini machozi yakawa hayatoki, nikajua kwa vile damu imeshakauka basi hata machozi yameshakauka pia. Nimeshakufa…

‘Umeshakufa,..kwahiyo kwenye hiyo ndoto ulijua kuwa umeshakufa,….?’ akaulizwa

`Niliona ajabu pale walipochukua kitu kama kamba…zilikuwa nene , na zinametameta na kama vile kamba hizo zina maji yanapita ndani yake, wakanifunga mkononi…’akasema na kutokujali hilo swali aliloulizwa, akaendelea kuongea.

`Niliona hiyo kamba ikishikanishwa na kitu huko ..nahis ilikuwa ni mkononi au mwilini, hapo sikuona, ila nikahisi hali kwenye mishipa ya damu, kwahiyo nikajau ni njia ya kuninyonya damu yangu…nikawaza hivyo.. na ikawa kama kumbukumbu zimepotea kwa muda, ni kama nimelala siwezi kuwaza tena…’akasema

`Baadaye kabisa, nikahisi nabebwa hewani hewani au kitu kama gari linanibeba…wananipeleka wapi hawa watu-mijitu, au ndio wanaenda kunitupa, kwani nimebakia mifupa, au gofu la mtu? Nilihisi kama naelelea hivi,...

 Baadaye nikajua kuwa nimehamishwa, nimetolewa pale nilipokuwepo na kupelekwa pori jingine, na zile kamba zikawa zimefungwa kwenye michuma mikubwa iliyotokea huko juu, nisipopaona vyema. Nikawa najiuliza nipo wapie sehemuyanye michuma mikubwa namna hiyo…ubaridi, utulivu ulikuwa vile vile…nipo wapi hapa jamani, nikajaribu kufunua mdomo lakini, ilikuwa kama vile sina mdomo …!

Baadaye wakaondoka , …nakahisi nipo peke yangu, nikajiuliza hapo nilipo ni porini au ni wapi, na mbona kamba niliyofungiwa imefungwa kwenye chuma, ni pori gani hili lina vyuma. Nikajaribu kugeuza macho, yakawa hayageuziki, ina maana hata macho sina, ikawa ni kuhisi tu!

Mara nikaona mtu-jitu akinikaribia,…aaah, ni yule yule mwanamke aliyemchukua mtoto-jitu wangu kutoka tumboni mwangu, alikuwa bado kavaa kitu usoni... kuzuia sura yake isionekane..nilihisi hivyo, nilitaka kumwambia hata ukijificha uso wako mimi nimeshakuona…lakini sikuweza kutamka neno.

Baadaye kwa mshangao…akakiondoa kile kitambaa usoni, …..mungu wangu, nilitamani niinuke nikimbie, macho ya huyu mtu-jitu yalikuwa makubwa kama mpira wa miguu,meno yalikuwa makubwa kama majembe ya trekta kubwa sana, na aliptabasamu kuyaonyesha hayo meno yalitisha sana..meupee, makubwa..!

‘Woga, wasiwasi vikanizidi…nilihisi kuwa huyu sasa katumwa kuja kunimalizia, huenda yeye alikwenda kumla mtoto wangu…akili iliwaza hivyo, kuwa  huyo waliyemchukua  `ni mtoto wangu’ maana walimtoa tumboni mwangu…japokuwa alikuwa mkubwa kama wao...lakini kwa namna fulani nikajua ni mtoto wangu..kwahiyo ni lazima nifanye kitu…ni lazima nijitetee hata kama kuna mabaki ya mtoto wangu niyapate…lakini kwa vipi?

‘Kila mara huyo mwanamke-jitu, alikuwa akija karibu yangu na nilihisi kama alikuwa akiniongelesha jambo..lakini, sikuelewa anaongea, nini, …lakini nilisikia maneno yakipaa kama mwangwi...nahisi kuna neno kama mtoto....halafu  baadaye yule jitu mwanamke akaondoka . Nilitamani nipige kelele kuwa anirudishie angalau mabaki ya mtoto wangu, lakini sikuweza.

‘Baadaye huyo mwanamke-jitu akarudi akiwa na kitu, nikataka kutoa kauli , kumuulizia kuwa kampelekea wapi mtoto wangu, lakini sikuweza.

‘Alikuja hadi pale nilipolala, sijui ni kwenye nini,…akashika ile kamba nene iliyotoka nahis ni mkononi mwangu na kufanya kitu nisichokielewa, akawa amashika kitu kama gunia , yeye kwake kwasababu ni jitu kashika kama kapaketi  ….sijui hata kuelezea, kwani akili hukumbuka itakavyo…lakini kile kitu, ambacho mimi nilikiona kama gunia la plastiki, lilikuwa limejaa maji ndani yake, akalitundika kwenye chuma na …sijui alikuwa analitoboa ili maji yanimwagikiea u vipi, lakini maji niliyoyaona mle ndani hayakumwagika!

Yule mtu-jitu mwanamke akasogeza kiti na kukaa karibu na nilipolala mimi, akawa ameshika karatasi kubwa kama shuka linalojaa eneo lote nililoweza kuliona, kama vile limejaa chumba kizima,kulikuwa na maandishi makubwa ajabu nafikiri alikuwa akisoma kitu! Nikajiuliza. Huenda anasoma, kwa vile ni mijitu mikubwa lazima hata vitabu vyao vitakuwa vikubwa. Muda ukawa unapita tu, siwaoni wale wengine na huyu haondoki hapo alipokuwa kakaa pembeni yangu!

‘Nilihisi kama kusubiri kukubwa tu,..sasa subira ikawa inanishinda, niliomba mungu wangu wasinimalizie sehemu iliyobakia, angalau yabakie mabaki ili ndugu zangu waweze kunizika. Na pia yaweze kupatikana mabaki ya mtoto wangu…Nikaomba sana, na kila mara nikitulia na kumwangalia yule mtu-jitu mwanamke , namuona habandui macho yake kunitizama mimi, na macho yake ni makubwa yanatisha, naogopa hata kumuangalia.

‘Kuna muda alikuja yule mtu jitu amabye alikuwa mgawa nyama yangu…, nilijua ni yule aliyekuwa akinikata nyama, yule aliyetoa mtoto wa ajabu tumboni mwangu, alikuja akawa anaongea na huyo mwanamke....alipofika alijifunua uso nikamuona vyema uso wake ...baaaye alikuja kunikagua, maumbile yake ni yale yale...macho makubwa....meno makubwa, yaani kila kitu chake ni kikubwa cha kutisha...alifanya kama ananikagua akaleta kidole chake kikubwa na kufanya kitu kwenye jicho langu..baadaye akaondoka na kumuacha huyo  mwanamke-jitu...

‘Akili ikiwa imechoka kufikiri na kitu kama usingizi kikawa kinaninyemelea na hatimaye nikahisi kulala maana akili ilikuwa kama imeingiwa na giza,sikuweza kufikiri tena.

‘Baaaye ile hali ya kichwa kutokufikiri tena kama mtu umelala ikaisha na, akili ile ya kuwaza ikanirejea tenaa...ni kama kulala na kuamuka, lakini kwa hisia tu...

‘Kwa mbali nilimuoana yule mtu-jitu –mwanamke akishika ile kamba nene na kufanya kitu fulani, halafu akainuka na kunitizama machoni, alileta kidole chake kwenye jicho langu kama alivyofanya yule mwanamume-jitu mwanzoni,…sijui walikuwa wakifanya nini kwenye jicho langu..nahisi walikuwa wakilifunua. Halafu nikamuona akiondoka.

‘Anakwenda wapi tena…au ndio anakwenda kuwaita wenzake waje kunimalizia…? ‘ nikawa nawaza hivyo…

‘Hapa, hapa, ndipo pakutorokea, hapa hapa, jitahidi mwanamke, jitahidi utoroke, kabla hawajarudi tena….’ Nikahisi sauti ikitoka sijui wapi, sijui ni akilini au nihisia zinaniamurisha hivyo, ila kuna sauti ilikuwa ikiniamrisha hivyo.

‘Sijui ilikuwaje, nilihisi hali ya kupata nguvu…,nikahisi nguvu za ajabu zikinijia, nikaweza kuinua mabaki ya mwili wangu na nikajitutumua na kuweza kukaa, nilihis nimekaa sehemu ya juu, na mbaki ya mwili wangu umening’inia chini,..nikaona kuna kitu kinanizuia, nikakumbuka ile kamba yenye maji ndani yake,…nilitumia nguvu kutoa ule mnyororo au kamba niliyofungwa mwilini mwangu.

Ulikuwa kama huo mnyororo umezamishwa ndani ya mwili wangu, kwani kila ulipokuwa ukitoka nilihisi mwili mzima ukihisi maumivu ya aina yake, na nahisi ulikuwa umeanzia kwenye moyo….., lakini sikujali hatimaye ukatoka…nikajitutumua  na kujiondoa iel sehemu niliyokuwa nimelala, na kukaa,sasa nikawa nahis nimekanyaga chini.

Nilijaribu kuinama kutizama mabaki ya mwili wangu yaliyobakia kwa chini, lakini kichwa kilikuwa hakiwezi hata kuinama, mwili hauwezi hata kujipnda, ni kama jitu limenyooka tu…nilikuwa kama roboti. Kichwa kinaangalia mbele tu…!

 Nikasema hivyo hivyo, lazima nitoroke hapa kabla hawajaja kunimaliza…
Nikatoka pale nilipokuwa nikajikongoja na niliona sehemu kama upenyo wenye mwanga, ni kama upenyo mkubwa kama mlango, lakini ni mkubwa sana…nikauendea na kuona upande huo mwingine kuna mwanga mkali…

Nikauendea huo mwanga, nikijua kuwa huko ndio kwenye uzima,….nikawa natembea, kuna muda nilihisi kitu, sijui ilikuwaje, nikainua kumbe ni mkono angu, ooh, mkono ulikuwa mkubwa….

Ooooh...kumbe....hata mimi ni jitu..., ina maana hata mimi ni jitu –mtu…nikacheka, kumbe naweza kupambana na hawa-watu –mijitu…nikawaantembea kuelekea huko kwenye mwanga mkali, ulioenea kote…mwili wangu ulikuwa kama umetoka kwenye barafu na kuingia kwenye moto…

‘Bora nikafie kwenye huu moto kuliko kuliwa na haya majitu-watu…bora…bora…lakini nakumbuka walitoa kitu mwilini mwangu kama mtoto-jitu…wamekiweka wapi! Nikawaza, nikaanza kusogea huku naangaza macho huku na kule mithili ya roboti, linageuka mzima-mzima…’mtoto wangu yupo wapi....mtoto wangu yupo wapi…’nikawa najiuliza

Baadaye nikawa najiona kama napaa, au natembea, lakini mwendo wa kiroboti. Hadi nikafika mahala kuna nguo zimeanikwa, nguo ni kubwa ajabu…nani anavaa nguo kama hizi, lazima ni hii mijitu watu. Nikaona kitu kama kitambaa, kimeshonwa nikakisogelea na kuona kinaweza kunisaidia kuficha macho uso wangu usiungue na mwanga huu mkali na kujikinga na joto. Nikakivaa, bahati nzuri, kilifunika kichwa chote na kuweza kuacha sehemu ya macho tu…

‘Safii kabisa, haya majitu-watu hayataniona kamwe, nikaingiwa na nguvu nakuanza kutembea kwenye eneo lilojaa mwanga mkali unao-unguza. Nilihisi kuona watu-mijitu wakitemebea, lakini walikuwa hawaji ninapotembea mimi, ilikuwa kama kila mtu-jitu ana njia yake. Nikaongeza mwendo, nikawa naondoka nisipopajua….joto, ..joto…likawa kero, lakini nashukuru usoni pamefunikwa!

Unajua natembea kama roboti, lakini mwendo ni wa kupaa, kuna mtu kama unavushwa waaaaah, kama unapaa vile na kujikuta sehemu nyingine kabisa….

Sasa sijui ilikuwaje kwani wakati natembea nihisi kitu kimenigonga na kujikuta nikielea hewani juu kwa juu kama mtu anayepaa juu kwa juu..na mwisho nilijikuta nikidondokea kwenye vitu kama matakataka, kunatoa harufu mbaya…!

‘Umeua, umeua…’ nikasikia sauti kama mwangwi ikisema hivyo…Nilijaribu kuinuka pale nilipodondokea, sikuweza.

‘Ina maana mimi wameshaniuaa…?’ Nikawa nawaza hivyo… kama nimekufa, mtu anakufa mara ngapi!...maana ile hali niliyokuwa nayo awali nilihis kama mfu  sasa hapo imakuewaje tena..

 Mara kelele zikasikika toka mbali zikisema `hajafa bado mzima, …’

 ‘Ina maana kumbe mimi sijafa bado, haiwezekani, nikajitutumua na kujiinua na nilipogeuka kama roboti, niliona watu….au niseme mijitu watu imejaa kwa mbele, lakini ilikuwa kama kilima, mimi nipo chini wao wapo juu. Kila walipofunua meno ya ilikuwa inatisha, nikaona hapo hakuna heri nikimbie tu..

Wale watu wakanisogelea wakanishika sijui ilikuwaje maana nilihisi tupo kwenye kitu tunakwenda kama tunapaa baadaye nikajua hawa watu wana nia mbaya na mimi, nikainua mkono sijui ilikuwaje, nilihisi napaa na kudondokea sehemu nyingine…nikawa nimetulia sikuona watu tena…nikasikia sauti

‘Karuka kwenye gari…hayupo, twendeni zetu….’nikasikia hivyo

Mimi nikatulia kidogo na baadaye nilipoona kimia nikajau hapa hakuna amani watakuja tena hao majitu watu…nikajitutumua kama roboto inayopaa, nikaanza kukimbia kiroboti….

 Hali hiyo iliendelea hivyo kukimbia kutokea sehemu sehemu…na baadaye nikawa kama mtu amezama ndani ya giza nene, sikuweza kufikiri tena! Nikawa kama nimelala , akili haikumbuki, haijui, imetulia kimia..ni kama umelala bika kuota ndoto…

 Nilipoamuka kwenye huko kulala, nikasimama, na mbele yangu kukawa kunakuja mtu jitu, kajifunika kama mimi, ni mwanamke..alioniona akawa kama ananiogopa,akanisemesha...mimi nikaona nifunua uso wangu nimuone vyema vyema labda kule kujifunika ndio kunaleta hiyo hali….mamamamama...

‘Yule mwanamke jitu alipoona uso wangu sijui ilikuwaje....aligeuka kutaka kukimbia, hakujua nyuma yake kuna kitu kinakuja kinatoa mngurumo….akilini hapo sikujua ni nini, hkitu hicho kikubwa kikamgonga huyo mama, na kudonoka chini.....akawa katulia kimia, ...

Baadaye kulipokuwa kimia, mimi nikamsogelea huyo mama aliyegongwa na kitu nisichokielewa kinachotoa mngurumo,...nilimuona katulia kimia...nikajaribu kumchunguza mapigo yake ya moyo…alikuwa amekufa....oh jitu mwanamke alikuwa amekufa nitaambiwa mimi ndio nimemuua …nikakumbuka kuwa hata mimi ni jitu kwahiyo…hahaha, nikajikagua mkono…ulikuwa mkubwa, nikajua hata mimi huenda nipo hivyo hivyo.

Sijui kwanini nilifanya hivyo....ila niliona nguo nilizovaa sio stahiki yangu….ni nguo zitakazonionyesha kuwa mimi ni nani…, nikija kutafutwa na mijitu ile iliyokuwa ikitaka kunila nyama yangu itanigundua haraka nikiwa na nguo zile zile..nikajiwa na wazo, kama huyu jitu mwanamke kafa, hana haja n nguo zake ....nikamvua nguo zake na mimi nikavua nguo zangu, nikavaa zile nguo zake, nikamvalisha zile nguo zangu...

Sikusahau kujifunika usoni maana mwanga ulikuwa ni mkubwa kwangu

Nikaanza kutembea,...natembea kama roboti lakini nahisi kama ni mwendo wa kupaa….nilitembea hadi nikachoka, mwili unauma,…nahisi tumbo linuma, sina nguvu… nina kiu...natafuta maji siyapati hadi nikafika sehemu nikaona maji nikayanywa, ....na nilipokunya hayo maji ilikuwa kama dawa ya kunipa usingizi nikalala usingizi....akili ikawa haifikirii tena.

Ilikuwa kama vile nililala kwa muda, nilipoamuka, nikajikuta nimetokea sehemu  kama dunia nyingine vile....

Yaani ile hali ya kuona vitu kwa ukubwa ikawa imeondoka kidogo kidogo, mpaka ikafikia mahali sasa naona hali ya kawaida,..na hali hiyo ilitokea kwenye hiyo dunia nyingine… lakini akili inakuwa gizani bado,..ni kama umaingia dunia nyingine ya vitu vya kawaida.

Cha ajabu kwenye hiyo dunia nyingine hukumbuki huko ulipotoka akili haijui imetoka wapi au inakwenda wapi…nikafikia sehemu sasa sikumbuki yote ya nyuma...sikumbuki ilikuwaje mimi ni nani, yaani unakumbuka hicho unachokiona mbele yako tu.... yaani sijui nielezeje….ohooo kichwa kinauma..’huyo mama akasema

‘Unahitajika kupumzika mama umeongea vya kutosha, …chukua dawa hii kunywa itakusaidia..’akasema docta na kumpa huyo mama dawa, na baadaye wakaondoka, Nesi akawafuata nyuma, na ilionyesha wazi kuwa huyo mama ameshikwa na usingizi

‘Nesi umesikia,…?’ aliyeuliza ni docta wakati wameshaondoka eneo hilo wakiwa wanaingia ofisini kwa mkuu wa hiyo hospitali, nesi hakusema kitu kwani alikuwa amezama kwenye mawazo.
‘Ina maana huyu mama ndiye yule mama……hapana mimi sijaamini , mbona alikufa, akazikwa, na nesi mkuu wa kipindi kile alithibitisha hayo…haiwezekani, basi mimi sijaamini…huenda haya kayatunga tu akilini mwake,..ngoja tumsikie akiendelea na uwongo wake, nitamtega,..’akasema kimawazo hakujua mabosi wake wanamuuliza nini

‘Nesi nesi, kweli upo nasi…’ akaulizwa

‘Ndio bosi nahitaji kupumzika ila nahitajia pia kumsikia huyo mama akiendelea kutoa uwongo wake..’akasema

‘Uwongo wake…hayo anayoongea ndiyo yaliyotokea huko nyuma, ila ni hali ya ubongo inavyoweza kurudisha kumbukumbu, inakuwa kama njozi, lakini ikionyesha yale yaliyotokea, huo sio uwongo…’akasema docta

‘Kwahiyo mnataka kusema nini, kuwa mimi ni muongo…’akasema

‘Hautajafikia huko,…muhimu kwa vile wapo watu wa usalama, na wao watatusaidia kwa hilo, kamaikibidi, ila tunakuomba kama mwenzetu ushirikiane nasi, kwani kuna kitu gani kibaya kilitokea unachoogopa kuwa ukisema ukweli utapata matatizo…?’ akaulizwa

‘Ndio maana nawashangaa nyie, kwanini niwafiche, mimi ninayemtambua aliyekuwa siku hiyo ni marehemu, huyu ni mwongo..mwizi na mwanga…si mliona wenyewe pale nilipomkemea, mungu akamzalilisha….’akasema

‘Sikiliza nesi tutarudi tena kwa huyo mama, lakini hatutaki huyo mama akuone ..najua akikuona moto utawaka..na itakuwa mwisho wa kupata habari za hiyo ndoto yake, ni muhimu sana kuisikia yote..’akasema

‘Sawa lakini kwangu hakitabadilika kitu….’akasema

‘Na huyo mtoto uliyemchukua ulimpeleka wapi,…alikufa, au ilikuwaje…?’ akaulizwa na docta bingwa wa mambo ya kili


Nb….tuishie hapa kwa muda


WAZO LA LEO: Haki ya mtu ni lazima ifike kwa mlengwa, hata kama huyo mlengwa hajui,..na wewe una dhamana na hiyo haki  usitumie ujanja kuifisidi hiyo haki ya watu. Sasa hivi kuna ujanja wa wale waliopewa dhamana ambao wana elimu, wanawadhulumu wale wasiokuwa na ufahamu wa sheria, au haki hiyo, hii ni dhuluma, huu ni ufisadi, huu ni wizi,….


Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

cialis for impotence [url=http://tadalafilfor.com]canadian pharmacy mall[/url] cialis for everyday usehow long does it take for levitra to work [url=http://fastshiplevitra.com]is it safe to buy levitra on line[/url] levitra high heart ratepropecia results months pictures [url=http://healthcarerxusa.com]Buy Finasteride[/url] subaction showcomments propecia smile olderpropecia and pregnancy [url=http://acheterpropeciafrance.com]propecia prix 2008[/url] can you take cialis and propeciadoes cialis 5mg daily work [url=http://cialisfor.com]Buy Cialis[/url] cialis ed dosage