Siku ile ilitokea hivyo,
wakati nesi anaongea na docta wakibisha kuhusu jambo ambalo nesi alishinikizwa
kulifanya na akahisi kuwa huenda docta kamshitakia na mara alipogeuka
kumuangalai mgonjwa akamuona kasimama….lakini alionyesha hana nguivu
anatetemeka, nesi akamuashiria docta kwa mkono ageuka kumuangalia huyo mgonjwa,
….
Docta alipogeuka akamuona yule mama ndio anadondoka, na hakuwa
kumshika, wakasaidiana na nesi na kumrudisha kitandani….
‘Hebu tulia, tulia…nesi
hebu saidia huko….’docta akasema alipomuona nesi akisita kusmhiak huyo mama.
‘Unaona…, anaonekana ana joto kali sana huyu mgonjwa…hebu tumpime
joto mshike mkono asidondoeshe hiki kipimo…’ akasema yule dakiatri huku
anahangaika kumkamata.
‘Wanataka kunichoma moto…nakufaaaa, nakufaa…majambazi hawa, hawo
wanataka kuniua eti mimi mwanga….oooh, niache, niache…..’ ilikuwa sauti kubwa
iliyomfanya yule mgonjwa mwingine aliyekuwa kalala, kuzindukana na kukaa
kitandani kutizama nini kinachoendelea.
Baada ya shughuli za kidakitari za kumweka huyo mama sawa na
kumpa dawa za kushusha homa, yule mama akalala.
Leo tena imetokea vile vile… na ilitokea tu pale nesi alipoingia
kwenye hiyo wodi nia ni kutaka kuongea na huyo mgonjwa lakini akamkuta dakitari
naye ndio anaingia.
Ile wanamsogeela huyo mama, wakahisi kitanda kikitetemeka,
kuashiria huyo mama anatetemeka homa
Docta akamsogelea huyo mama, akamtizama kwa uangalifu sana. Na
kumkagua kila panapowezekana,…akamweka kipimo cha joto, joto likaonekana lipo
juu,…. halafu docta akaangalia kumbukumbu za usiku, walipompima, maana ilitakwia
kumchunguza joto kila baada ya masaa sita, akaona usiku joto lilikuwa kawaida,
‘Mpe hizi dawa sasa hivi….akinywa talala, itasaidia….’akasema
docta akimpa nesi vidonge viwili na yeye akawa anazidi kumkagua huyo mama.
Akakagua taratibu za dawa alizomuandikia siku za nyuma, na
alipoona kila kitu kipo sawa akasogea pembeni na kumuuliza nesi;
Tukio hilo naona ni mara ya tatu sasa….na likitokea mgonjwa
anakuwa na homa kali sana…’akasema
‘Majuzi yale ndio ilitokea hivi, sijui kwanini..’akasema nesi
‘Ni kawaida, na …..itakwisha ni dalili za kuonyesha kuwa mwili
sasa umeanza kufanya kazi, ubongo unafanya kazi zaidi….hana tatizo la ndani,
tatizo kubwa limeshakwisha sasa tunapambana na marejeo kwenye ubongo…’akasema
‘Kwaweli lakini lile la juzi na leo…, naona hii imezidi….anatetemeka
hadi kitanda kinatingishika….’, akasema
nesi
‘Hizo ndio dalili za kuonyesha kuwa kumbukumbu zinarudi….na muhimu
kuhakikisha hali kama hiyo ikitokea kuna watu karibu wa kumsaidia, vinginevyo
anaweza kukimbia na hata kujiumiza….’ Akasema docta.
‘Kama ilivyowahi kutokea….’akasema nesi na kukatisha akajifanya
kama anakohoa.
‘Yah..huwa iantokea..’akasema docta akiwa hamjali sana nesi
alichokuwa kitaka kukisema mawazo yake kwa kipindi hicho yalikuwa kwa mgonjwa,
akawa anaweka vyema kadi ya huyo mgonjwa….mara yule mama akiinuka kutoka
kitandani. Ile dawa aliyopewa ilitakiwa huyo mama alale, kwani ni ya usingizi,
lakini inavyoonekana haikufanya kazi haraka…
Docta kamsogelea kumshika ili asije kuanguka, yule mama akawa kama
anaukwepa huo mkono wa docta kama vile ni kitu cha kumdhurua, akasema;
`Wewe ni nani..?’ akauliza huyo mama kwa sauti inayoashiria
kuogopa
‘Mimi ni dakitari wako…umeshanisahau.’akasema docta
‘Ndio wewe eeh…eeh nimekukumbuka….oh, unakumbuka , nilikuambieje…?’
akauliza huku akiwa anamuangalia docta, japokuwa kajifunika kichwani lakini
ilionyesha dhahiri kamkazia docta macho.
‘Ulisema unamtaka mtoto wako ….’akasema docta
‘Sasa yupo wapi ndio huyu….’akasema akimuelekezea mkono nesi, na nesi alikuwa pembeni akiwa tayari kutoa
msaada, lakini alipoona anaelekezewa mkono kumbukumbu za kuwa huyu mama sio mtu
wa kawaida zikatanda ubongo wake akajiandaa kutafuta nafasi kama itabidi
kukimbia.
‘Huyu ni nesi anayekusaidia kila siku umeshamsahau, humkumbuki?’
akaulizwa na huyo mama taratibu akageuza kichwa kumuangalia nesi, akatulia kwa
muda, halafu akawa kama anataka kumsogelea nesi, na nesi akajiweka katika hali
ya tahadhari
‘Usikimbie..sina nia mbaya na wewe….ila ninachotaka ni mtoto wangu
tu..mtoto wangu ,…’akasema na nesi akawa kimia
‘Mtoto wako, hivi kila siku unasema mimi nin mtoto wako, …mimi
nilimchukuaje mtoto wako?’ nesi akaona alimalize hata kama hakutakiwa kuongea
na huyo mama kwa muda huo, na doct akamtupia jicho la kumkanya huyo nesi, kuwa
huo sio muda mafaka wa kuongea na huyo mama.
‘Unakumbuka ile siku…wewe mkiwa na wanzako mlimchukua mtoto
wangu,,…mkijua mimi nimekufa, unakumbuka…sasa nimerudi….namtaka nani, namtaka
mtoto wangu….nakumbuka kila kitu…..’akasema na nesi akawa kimia
Docta akabaki kaduwaa akimwangalia nesi na tena akimuangalia
huyo mgonjwa….docta hapo alitaka kumuuliza kitu, lakini kwa utaalamu wake huo
sio muda muafaka wa kumsumbua huyo mama, alitakiwa kulala na kutuliza kichwa.
Kama alivyotarajia, akamuona huyo mama anayumba, anataka
kudondoka, akajua kuwa ile dawa imeshfanya kazi, huyo mama anaweza kudondoka
sakafuni na hata kuumia, akamsogelea huyo.
‘Sasa pumzika, nesi ameshakusikia,…. tutalishughulikia hilo tatizo
lako, usijali, niamini mimi…’akasema docta
‘Na-na---se…ma …na hivi, na—mtaka mtoto…wangu…docta , nataka
mtotoooo…wa—wa—nguuuuh, unasikia, vi-vi-ngine-vyo, yatawakuta makubwa,msije
kunilaumu…..’akasema maneno ya mwisho kwa nguvu, halafu akawa kama katulia
lakini mara akainua kichwa na kusema;
‘Nesi ..natum-mai ume-ni-elewa---mtoto-wangu…unakumbuka..yule…namtaka
haraka…saaa-na’akasema
‘Mtoto wako yupi wewe mama, mbona hakuna maelezo ya kuonyesha kuwa
uliwahi kujifungua hapa…? Akauliza docta
‘Muulize huyu nesi wako anajua mtoto gaaani, anajuuu-a-a
wapi alim-mm-mm-peleka mtoto , mto-to-to…waaa-ngu, yeye na wenzake
walipa-pa-pa-suuu-a tumbo langu na kum…m..mt-oa mtoto ..toto..wangu waka…waka….’
akakaa kimya kidogo
Ilionyesha kuwa huyo mama keshalala,…lakini baadaye kidogo kwa
sauti ya kufifia akasema;
‘Nesi nikirudi…nataka uniambie mtot o wangu yupo wapi…namtaka
mtoto wangu, na hiyo ndio itakuwa salama yako, sina ubaya na wewe, ubaya wangu
kwa hao…hao…walionifanya hivi…’ akanyamaza kimya, na hatimaye wakasikia sauti
ya muhemo wa kulala, huku anatafuna-tafua maneno, kama vile anaota!
Docta akawa anawazia kauli hiyo `…namtaka mtoto wangu, na hiyo ndio itakuwa salama yako, sina ubaya na
wewe, ubaya wangu kwa hao…hao…walionifanya hivi…’
Akikumbuka mazunguzmo yake ya ofisa usalama, akageuka kumuangalia
nesi, halafu akachukua karatasi na kunadika melekezo kwani alihitajika kwenda
chumba cha upasuaji, akatoa maagizo kuwa vipimo vingine vya damu vichukuliwe,
ili iijulikane ni kitu gani, isije ikawa ana ugonjwa mwingine kama malaria…
‘Mchukue vipimo hivi, tuangalia tena…’akasema docta na nesi
alikuwa kama kapigwa na butwaa, akawa kasimama akimuangalia huyo mama kwa macho
ya kuogopa kabisa, na docta akamsogelea nesi na kumshika bega, akasema;
‘Natumai wakati umefika wa wewe kusema ukweli….kama hali
unavyoiona, je hayo anayoongea huyu mama ni ya kuchanganyikiwa? ,…hapana nesi
hayo anayoongea huyu mama yana ukweli ndani yake…na, wewe inavyoonekana unajua huo
ukweli,….sasa naona htuna muda tena wa kupoteza....’akasema docta na nesi
akabakia kimia.
Docta alimtizam yule mgonjwa kwa makini,..huku akiendelea
kukumbuka mazungmzo yake na ofisa usalama, jinsi alivyoambiwa huko kijijini
kuwa mama huyo sio mama wa kawaida;
‘…. kama tukikubaliana nayo ina maana
tunaamini ushirikina,..na tukiamini hayo tutakuja kuamini kuwa huyu mama..mgonjwa
ni shetani, sio mwanadamu...kaja kulipiza kisasi….’
Hapana huyu ni mtu kamili,
..hayo mengine ni imani tu…’akajikuta akisema na nesi aliyekuwa bado kaduwaa,
akamtupia macho docta akakumbuka kile alichokisia akiwa dirishani,
‘Tunarudi kule kule..ndio maana nikakuambia
hapa hakuna kesi....ni bora tuyaamini maneno ya nesi,..kuwa huyo mama
alikufa...maana kaburi lake lipo...ila kuna kitu kingine kilinitia mashaka..ndio
maana nikakuambia kuna utata..’akasema
‘Kitu gani...?’ akauliza docta
‘Kaburi la huyo mama..kule kwenye kijiji
nilipokwenda awali lilikuwa limefukuliwa....sikukuambia awali ili nije
kuoanisha na sehemu hii ya pili..’akasema
‘Limefukuliwa na nani, uligundua siku ile
ile, au baadaye…..na je maiti ipo?’ akauliza
‘Haijulikani ni nani kalifukua....na maiti
haipo...ni siku ile ile nilipokwenda, hata wao waligundua siku hiyo, wakawa
wanashangaa….’akasema
‘Docta…una uhakika huyu ndio huyo mama….?’ Akauliza nesi
‘Mama yupi?’ akauliza docta
‘Huyo aliyekuwa amekufa…?’ akauliza na docta akamtizama huyo nesi
kwa macho ya kumshangaa, akasema;
‘Wewe hayo umeyatolea wapi?’ akamuuliza
‘Aaah, nataka kujua tu….maana wewe ni docta, una uzoefu na haya
mambo ni kweli kuwa mtu anaweza kufa akafufuka ….?’ Akauliza nesi.
‘Sikiliza nesi, muhimu ni wewe kuniambia yote yaliyotokea huko
nyuma, na mimi nitakuwa tayari kukusaidia kwa hilo…lakini kama utabakia an siri
yako, sijui, unasikia kauli ya huyo mama kasemaje?’ akauliza
‘Kwani kasemaje..?’ akauliza huku mwenyewe akikumbuka alichoambiwa
na huyo mama;
‘Nesi nikirudi…nataka uniambie mtot o
wangu yupo wapi…namtaka mtoto wangu, na hiyo ndio itakuwa salama yako, sina
ubaya na wewe, ubaya wangu kwa hao…hao…walionifanya hivi…’
‘Docta lakini huko ni kuchanganyikiwa tu, sizani kama ……huyu mama
ndiye yule aliyekuwa amekufa,mimi nina uhakika huo, hawafanani kabisa….au docta na wewe...unaamini hayo mambo, mtu afe afufuke haiwezekani….?’ akauliza
‘Chukua vipimo vya damu , na …nitaongea na wewe baadaye,
ngoja nimalizie wagonjwa wengine…’ akasema yule dakitari akielekea kwa huyo
mgonjwa mwingine, lakini kichwani mwake alikuwa anadadisi mazungumzo yake na
ofisa usalama kuhusu huyo mama!
***********
Nesi akiwa hana nguvu, alifanya alichoagizwa na docta,
akachukua sindano na kuchukua mkono wa huyo mama kwa tahadhari huku akiwa kama
anatetemeka akajitahdi na kuchukua damu ya huyo amma,
Alipomaliza, akasimama pembeni akimkagua huyo mama kwa macho,
alishindwa hata afanye nini, alitamani amfunue kichwa amtizame usoni lakini
akaona hilo halitawezekana kwani docta bado alikuwa hapo akiongea na yule
mgonjwa mwingine
Basi nesi akachukua vile vupimo vya damu na kuanza kutoka navyo
nje huku akiwaza kauli ya huyo docta;
‘Sikiliza nesi, muhimu ni wewe kuniambia
yote yaliyotokea huko nyuma, na mimi nitakuwa tayari kukusaidia kwa hilo…lakini
kama utabakia an siri yako, sijui, unasikia kauli ya huyo mama kasemaje?’
Halafu akakumbuka kile alichokisikia pale dirishani;
‘Kwa huyo nesi naona ama anapotezea muda,au
na yeye anahusika kwa namna moja au nyingine...sasa nilikuwa nakusubiria wewe,
kama utatoa kibali, ....tumfikishe kituoani, nahisi ana mambo mengi anatuficha,
na hili litatutafanya tushindwe kutimiza wajibu wetu...’
`Ina maana huyu docta anafanya kazi mbili, ya udakitari na
ushushu..kaja kunichunguza mimi…lakini anichunguze mimi kwa kosa gani, kwa
ajili ya matukio hayo ya huko nyuma, lakini mimi sina hatia, ni kuhusu mtoto…..hapana,….’
‘Kwanza nivifanyie kazi hivi vipimo, nitamuomba docta wa zamani
avichunguze vyema, na ikibidi nipate vipimo vya DNA, nipo tayari kugharamia…..siwezi
kumtoa mtoto kwa shetani..hapana….’akawa anazidi kuongea kwake hadi alipofika
chumba cha maabara.
‘Unasiki achukua vipimo vya damu hii haraka…na nahitajia zaidi,
hivi wewe unaweza kutumia ile mashine ya DNA,….?’ Akauliza
‘Naweza lakini kwa kibali cha mkuu wa kitengo hiki, ….si
unamfahamu mambo yake..’akasema
‘Nitaongea naye ni muhimu sana, nipata hivyo vipimo,..’akasema
nesi akielekea kwa huyo dakitari wa zamani, na bahati nzuri alimkuta hata
wagonjwa akamuelezea shida yake na dakitari akamtizama huyo nesi kwa muda,
halafu akamuuliza
‘Hebu niambia ukweli, kwani siku ile mlifanya nini ..mpaka
uhangaike hivyo, hayo hayakuhusu
yanawahusu wale waliokuwa wamepewa dhamana, kwani wewe kuna kitu
chochote kinahusu pale….?’ Akauliza
‘Aaah, docta nakuombaunisaidie kwa hilo, nitakuja kukuelezea
mengine ambayo hustahili kuyasikia kwa sasa, wewe niamini tu..’akasema
‘Sawa mimi nitafanya hivyo, ila ujue ile mashine inasoma na
gharama, sasa itabidi ugharamie japo kidogo…’akasema
‘Nitafanya hivyo docta…’akasema nesi
‘Kwahiyo itachukua muda gani?’ akauliza
‘Mhh…ngoja nikaone kwanza, ….’akasema na kusimama kuelekea huko
maabara
Wakati anasubiri vipimo, simu yake ya mkononi ikaiita,
alipoitizama akaona ni dada yake anayepiga, akaipokea haraharaka. Hakutaka
kuwaambia nini kinachoendelea hapo hospitalini, kwa sasa hivi, aliona sio
muda muafaka wa kuwavunja moyo, Hakuwa tayari kuamini kuwa huyo mama anaweza
kuwa huyo mama aliyekuwa kafa, na sasa kafufuka, halikumuingia akilini.
‘Tunataka kukupa habari njema, …na tumeona tufanye sherehe fupi ya
kumshukuru mungu…’ dada yake akawa anaongea kwa raha.
Nesi akatabasamu na kusema moyoni, nyie mna raha, lakini mwenzenu
nipo taabuni, mngelijua nini kinachoendelea huku msingekuwa kwenye raha hiyo…nahis
mngeliahirisha hiyo raha yenu..nesi aliyesema hayo mawazoni tu, lakini hakujua
wenzake wanazungumzia raha gani….!
`Habari gani hiyo njema, …na raha gani hiyo..?’ akauliza nesi
akiwa anatizama saa yake kwani aliona hao watu wa vipimo wanachelewa.
‘Nikuambie kitu mdogo wangu, jana tumetoka kuthibitisha kwa
dakitari,… ‘akaanza kusema
‘Ehe..ndio ..vipi una malaria tayphoid…?’ akauliza
‘Sina matatizo hayo bhana….unajua nilipima mara ya kwanza,
sikuamini…, lakini safari hii ya pili , dakitari kasema maneno yale yale,
kuonyesha kuwa ni kweli ..’akasema na nesi kwa vile alikuwa na mawazo yake
kichwani hakuwa na akili ya kuweza kugundua dada yake aantaka kumuambia nini.
‘Mhhh, docta akasemaje…?’ akauliza
‘Mdogo wangu nikuambie nini…ni, kweli kabisa, sikuamini maneno
yake…maana nilitamani nipige ukulele dunia nzima isikie…yaani nina furaha
isiyoelezeka…kama inawezekana kesho njoo…’ akasema dada yake huku akionyesha
furaha.
‘Dada unajau sijakuelewa….’akasema, ni kweli kwa hali aliyokuwa
nayo, hakuweza kuelewa kabisa kuwa dada
yake anamaanisha nini, kwani kwa mara ya mwisho kuwasiliana na dada yake
aliambiwa kuwa dada yake hajisiki vyema, akamshauri aje mjini wampime vyema. Lakini leo anamsikia kwenye simu akicheka kupitiliza, akajua labda anaongea akichwza na mtoto wake, lakini kasema anafurahia kitu alichoambiwa na docta...
Au kaambiwa anaweza kushika mimba tena...au...hapana mbona hilo alishaambiwa siku nyingi tu...'akawa anajiuliza bila jibu, akauliza.
‘Kwani ulipofika kwa docta uliambiwa nini ?’ akauliza huku
akitizama saa yake, na dada yake akawa anaongea kitu huku anacheka, mpaka mdogo mtu akaona hiyo imezidi tena, alitamani sana kujua anachofurahia ndugu ayake, lakini wakati huo huo, akaingia nesi na katarasi mkononina kumuongelesha kwasauti ikabidi asimsikilize dada yake kwanza
akaiondoa simu sikioni na kusema
‘Unasema, vipimo….eeh,?’ Akaumuuliza yule nesi aliyekuja kumpa ujumbe
'Ndio..'akasikia sauti ya dada yake, lakini wakati huo simu ipo mbali na sikio
‘Nesi unaitwa wodini, na vipimo hivi vyako hivi hapa…’ akaambiwa,
‘Sawa…wodi gani?’ akauliza
‘Ya yule mama, mgonjwa wako…’akasema na nesi aliposikia hivyo
akajua kuna jambo, kuna kitu kimetokea tena huko, basi kwanza akavipokea vile vipimo na kuirudisha simu sikioni,
lakini aliona ipo kimia, kumbe mwenzake hayupo tena hewani..hakuwahi kujua ni
furaha gani aliyokuwa nayo ndugu yake.
Kwasababu ya huo muito ulionyesha wazi kuwa kuna dhahrura, ikabidi
nesi aachane na hiyo simu, kwaharaka akaelekea wodini. Wodi ya mgonjwa maalumu,
mama wa mitaani…
NB; Leo tuishie hapa
WAZO LA LEO: Ni muhimu mara kwa mara tuwe na tabia ya
kujichunguza afya zetu, hii sio tabia yetu kwani mara nyingi tunasubiria mpaka
tuone tunaumwa, na huenda huko kuumwa tungekuzuia mapema kama tungekuwa na
tabia hiyo ya kuchunguza japo mara moja kwa mwezi. Najua ni hali za kiuchumi,
lakini kinga (kujipima) ni bora zaidi kuliko tiba.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment