Kikosi
maalumu cha kupambana na kundi haramu kiliundwa, na majukumu makubwa
akakabidhiwa Inspecta Maneno, japokuwa lifanyika kwa njia ya mtego zaidi, na
muda huo mrembo Jembe akawa safarini kwenda masomoni.
‘Uliniambia
Insepecta Moto amepatikana mbona sikumuona nlipoitwa makaoni?’ akauliza
Inspecta Moto alipokutana na Inspecta mwenzake ambaye sasa ndiye atakayeshikilia
nafasi yake.
‘Ilikuwa
njia ya kukufanya ufike huko ukiwa hujajiandaa, ndivyo nilivyoambiwa..’akasema
‘Hawa
watu hawana akili kweli, badala ya kuniacha nimalize kazi niachane nao kwa
amani, wanafikiri mimi nitakuwa nao maisha yangu yote, hilo halipo. Sasa kazi
umeachiwa wewe, kituo hiki sio kirahisi kama unavyofikiria wewe na hao
waliokutuma, nimepata taabu sana, lakini ngoja ujionee mwenyewe..’akasema
‘Usijali
hiyo ndiyo kazi yangu na wajibu wangu, nitaitimiza kama ipasavo, usiwe na
wasiwasi mkuu…’akasema
‘Vipi
yule mrembo niliyakuonyesha siku ile..?’ akamuuliza
‘Achana
na mambo hayo…mimi sipo huko kabisa, najua hiyo ndio mitego ya watu wabaya,
kazi yangu ni moja tu kupamabana na wahalifu….’akasema
‘Haya
tutaona hata mimi nilikuja hapa nikiwa na hamasa kama zako, lakini baadaye mmh,
ngoja ujionee mwenyewe….’akasema
‘Hamna
shaka mkuu,..hiyo ndio kazi niliyoisomea cha muhimu ni kujua ni nini wajibu
wangu…’akasema
‘Yah,
wewe huna tofauti na Moto, sasa yupo wapi……kampoteza mke, na sasa hajulikani
wapi alipo,…..’akasema
‘Ndio
mitihani ya hii kazi….katimiza wajibu
wake….’akasema
‘Mnanikera
nyie watu…..hivi mnataka muishi maisha hayo mpaka lini…hebu angalieni wenzenu
wanavyotesa, magari nyumba nzuri, mnafikiri vimepatikana kirahisi
hivyo…’akasema.
‘Kwahiyo
mkuu wewe ulitaka mimi nifanya nini…?’ akamuuliza
‘Tutaongea
ngoja nikamalizie kazi moja, nikihakikisha hiyo imekwisha, hamna mtu
atakayeniweza…maisha safi kabisa….mtajifunza kutoka kwangu…’akasema
Inspecta
Maneno akachukua pikipiki yake ambayo huwa anaitumia kwa kazi maalumu za haraka
haraka, akaendesha hadi nyumbani kwa Inspecta Moto, alipofika alikutana na
mlinzi , yule mlinzi aliyekuwepo mwanzoni ambaye wanafahamiana alikuwa
kaondolewa
‘Umeletwa
wewe hapa, mwenzako kaenda wapi?’ akauliza
‘Yupo
likizo mkuu….’akasema
‘Sasa
kuna mambo nataka kuchunguza huko ndani, sitaki usumbufu,..akija mtu usimruhusu
kuingia, …’akasema.
‘Sawa
mkuu, lakini…..’akaitikia na alipotaka kusema jambo, inspecta akasema;
‘Hamna
cha lakini…umenielewa…’akasema
‘Sawa
mkuuu....'
Inspecta
Maneno akaingia ndani, akiwa anajiamini kabisa, akijua ni kitu gani alichokifuatilia,
akafungua mlango, hadi mlango wa chumbani, akaendelea na kuchunguza huku na kule
bado akiwa na imani atakipata hicho kitu anachokitafuta.
‘Haiwezekani,
nina uhakika badi kipo humu humu ndani…’akasema akivurumua kila kitu
kuhakikisha kila sehemu kaipitia.
Alipohakikisha
hakuna hicho kitu akakumbuka, ….juu ya kabati!
Akatoka
na kwenda barazani, akachukua kiti, maana lile kabati ni refu, akaweka kiti na
kusimama juu yake na hapo akaweza kufikia mwisho wa lile kabati na kuanza
kuangalia pale juu, kile kitu hakikuwepo..
‘Nina
uhakika niliona kitu hapa juu…’akasema.
‘Ni
hiki unakitafuta mkuu….’akasikia sauti, iliyomshitua hadi kutaka kudondoka
kwenye kile kiti. Sauti anayoifahamu, na sauti hiyo ni ya watu wawili,
wanaofanana wakiongea, mmojawapo ni yule muuaji wa kundi ambaye akitumwa kwako
ujue wewe ni maiti, na wapili… akagwaya….
*********
Kesi
maalumu ya kiaskari ilifanyika, na kama ilivyotegemewa, Maneno hakuweza kutoa
ukweli wote, japokuwa alijua Mrembo Jembe anaweza akawa kawaelezea mengi,
lakini kwa jinsi anavyofahamu yeye, mrembo huyo asingeliweza kujua zaidi,
kutokana na nafasi yake kwenye kundi, kwahiyo akacheza patapotea kuficha baadhi
ya mambo kwasababu zake binafsi.
‘Mimi
naona nikatafute ushahidi ambao nahisi upo kwa Inspecta Moto,kama nitaupata huo
ushahidi, tutaweza kuwashinda hao watu kirahisi….’akaomba kibali.
‘Una
uhakika na hilo?’ akaulizwa.
‘Ndio
mkuu, katika kazi ya hao watu, kila sehemu walikuwa wakipandikiza vifaa fulani
vya kunasia matukio, na nyumbani kwa Moto kulikuwa na hicho kifaa, ni kidude
kidogo sana, lakini kinachukua vitu vingi,picha za video, muda tukio
lilipofanyika, na hata kama utajaribu kudurufu baadaye kunakuwa na kumbukumbu,….’akasema
‘Kwanini
mwanzoni polisi hawakukiona, unahisi hapo
kilipowekwa awali kiliondolewa na nani mpaka msikione wakati mnfanya
uchunguzi....?’ akaulizwa
‘Inawezekana
ni mke wake Inspecta, ….’akasema akionyesha hana uhakika
‘Kwani
mke wake Inspecta, alikuwa anafahamu mipango hiyo?’ akaulizwa
‘Yeye
kama mwanachama, kuna baadhi a mipango alikuwa akiifahamu kwa nafasi yake, lakini
hiyo ya kuweka vitu kama hivyo, hakutakiwa afahamu,..ila kama alikuja kuhis
hivo…’akasema.
‘Kwanini
mume wake asihisi kuwa kuna kitu kama hicho ndani ya nyumba yake..?’ akaulizwa.
‘Kama
nilivyosema ni kifaa kidogo sana, na unaweza kuweka kwenye kitu kingine,
kikafanana na hicho kitu, kinaashiri rangi ya kile kitu, kimeengenezwa kwa
tabia a kinyonga, na hakuna chombo cha kugundua vitu kama hivo kinachoweza
kukigundua…’akasema
‘Tunachojiuliza
hapa ni jinsi mke wa Inspecta alivyoweza kugundua…maana kama ulivyosema
inahitajia mtaalamu sana kukigundua, au sio?’ akaulizwa
‘Kama
shemeji yangu huyo alitafakari kwa makini angeliweza kuligundua hilo, hasa
baada ya kutishiwa kwa kuonyeshwa mambo yake binafsi ambayo hakupenda mume wake
ayafahamu, ambayo pia yalitumiwa awali kwa yeye kuingizwa kwenye
kundi….’akasema
‘Mambo
gani?’ akaulizwa
‘Mara
nyingi kundi hilo huwalazimisha watu kujiunga kwa kuwanasa kwenye kashfa nzito,
kwa wanandoa wanaweza kutafuta matendo yako machafu ya nje ya ndoa, na
ikishindikana kabisa wanakupandikizia mtu, ufanye naye uchafu, na kuchukua hayo
matendo kwenye kanda za video…’akasema.
‘Kwahiyo
kwa huyo mama walifanya hivyo?’ akaulizwa
‘Mhh,
ndio, nahisi hivyo….na nahisi pia kuwa huenda, ndio sababu ya kuja kujiua kwake,
kwani yeye alitakiwa kutoa maelezo ya mume wake ambayo hakuweza kuyatoa,
wakaona njia rahisi ni kumtishia kwa kumuonyeshea machafu yake zaidi yaliyokuwa
yamefichwa…’akasema.
‘Lakini
si umesema huyu mama alikuwa mwanachama toka awali, kwanini haya yaje baadaye, hadi
afikie kujiua, kwanini ashindwe kushirikiana na kundi kama alivyofanya toka awali?’ akaulizwa.
‘Uwanachama
wake ulikuwa sio wa ndani zaidi, ni ule wa kawaida tu kwa kutumiwa, mwanzoni
walimuingiza wakati anashikirikiana na yule dada mwenye kampuni ya urembo,na
akanaswa kwa kutegwa akiwa na mwanaume aliyetegewa naye….’akasema
‘Huyo
mwanaume alitegewa kwake, sio kweli kuwa huyo mama alikuwa na tabia kama hiyo y
akutembea na wanaume wa nje…?’ akaulizwa
‘Yule
mama alikuwa mwaminifu sana kwa mume wake, ni mwanamke aliyekuwa akijitahidi
sana kutimiza wajibu wake wa ndoa…hilo mimi namtetea. Lakini watu hawa wana
mbinu za kila namna, wakapitia kwa wanawake wenzake..kwenye vikundi, sherehe,
na huko wakamwekea madawa kwenye kinywaji, akajikuta anatembea na huyo
mwanaume, na hapo wakaweza kuchukua picha zake mbaya…’akasema
‘Hapo
ni wakati walipomtaka kujiunga na kundi au ni baadaye…?’ akaulizwa
‘Ndio
chanzo cha yeye kujiunga na hilo kundi, kwani alipoonyeshwa hakuamini, na
alikuwa kama kachanganyikiwa, nakumbuka kipindi hicho alikuwa mgonjwa sana,
hadi mume wake akaamua ampeleke kwako kwa muda, na aliporudi akatulia, na ndipo
alikuja mtu kumshauri ajiunge na hayo wanayotaka hao watu, akakubali, akaamua
kufanya hivyo watakavo hao watu.
‘Unafikiri
kwanini alikubali..na kwanini hakumuambia mume wake?’ akaulizwa
‘Asingeliweza
kabisa kumuambia mume wake..sio rahisi, maana kinachofanyika hapo ni kitu
ambacho hutapenda mume wako au mtu mwingine unayemuheshimu akione….wanajua ni
nini wanachokifanya…’akasema
‘Kwahiyo
na wewe ulifanyiwa hivyo?’ akaulizwa
‘Ni
kama hivyo,…maana walijua kuwa sitakubali kirahisi, wakanitegea wanawake na
kuninasa, na kwangu haikuwa vigumu sana kunitegea wanawake maana wananifahamu
udhaifu wangu, na kiukweli niliwagomea sana, ila pale waliposema wanaupeleka
huo ushahidi kwa baba mkwe wangu, hapo, nikashindwa…
‘Kiujumla
mkuu, watu hao wana mbinu za kila namna, hata za kukushawishi kuwa muwekezaji
na humo wanaweza kukutegea bidhaa bandia, ukaja kukamatwa na polisi, na hao
polisi ni watu wao…..’akasema
‘Je
katika hilo kuna muda walikuchukua picha zako ukiwa na mke wa Inspecta?’
akaulizwa
‘Mhhh,
yaah…ni kweli hilo walilifanyia, lakini….mmmh, haikuwa mbaya ya kuweza
kunishawishi, zipo nyingine za wanawake wengine, ndizo zilikuwa mbaya zaidi, na
ndizo sikupenda zije kuonekana na familia yangu…’akasema
‘Mahusiano
yako na mke wa Inspecta yalikuwa toka awali au ni katika kumshawsishi mke huyo
kujiunga au kutoa taarifa za mume wake?’ akauliza
‘Hapana
yule mama ni mtu aliyekuwa akijiheshimu sana, na nikuambie ukweli, hata kama
ingelikuwa ni wewe kwa mbinu wanazozifanya utakubali tu kujiunga na hilo kundi,
wana mbinu za kila namna ikishindikana ndio wanatumia mbinu za kukupandikizia
makosa..’akasema
‘Mbona
Inspecta Moto walishindwa kumshawishi?’ akaulizwa
‘Alikuwa
mbioni,angepatikana tu,….na hata hivyo, yeye hawakumuhitaji sana, maana mke
wake alishanaswa, kwahiyo kila walichokitaka kwake,walikipata kupitia kwa mke
wake..ila baadaye walianza kumuona kuwa ni tatizo, kwani alishaanza kugundua
mengi kuhusu hilo kundi, ndio maana wakaanza kumuandama...’akasema
‘Kwahiyo
mke wake aliweza kutoa taarifa zote kuhusu mume wake?’ akaulizwa
‘Za
muhimu ndio..kuna muda alikuwa anaogopa,…unajua tena mapenzi ya mume na mke,
kuna muda unamuonea mwenzako huruma, lakini akiogopa wanamuonyesha uchafu wake, na
wakimlewesha kidogo tu, anaongea kila kitu…akilewa hana ujanja, ataongea kila wanachokitaka….’akasema
‘Je
hadi kuwa na mahusiano na shemeji yako, walifanya hivyo, wakiwa na lengo la
kupata hayo wanayoyataka kutoka kwa Inspacta Moto ?’ akaulizwa
‘Sio
mara kwa mara, maana wananifahamu msimamo wangu, mimi walinitumia tu kwa kazi
nyingine, na hata hivyo, kwanini wanitumie mimi kwa kazi hiyo ndogo huyu
shemeji hakuwa mgumu kiasi hicho, hasa walipogundua kuwa akilewa, anaongea yote
wanayoyataka….’akasema
‘Wewe
huwa walikutumia kwa kazi kama zipi?’ akaulizwa
‘Zinazohitaji
utaalamu wa kujua jambo lisilopatikana kwa urahisi, kama wanataka kujua jambo
ambalo hawawezi kuwatumiwa watu wengine, ndipo wananitumia mimi, lakini sio
kazi ndogo ndogo hizo ambazo wangeliweza kufanya watu wengine, kama mrembo
Jembe, ….’akasema kwa kujisifu.
‘Na
mwishoni ndio maana wakakutumia wewe kumpata au kumuua Inspecta Moto?’
akaulizwa.
‘Ni
kweli waliposhindwa wakaniita mimi kuwa nikabiliane na mwenzangu huyo, kwakweli
hapo walinivunja nguvu, nilijaribu kuwashawishi kuwa huyo mtu waachane naye ,
mimi nitajua jinsi gani ya kumuweka sawa, lakini hawakukubali, wakasema ni
lazima ama tumshawishi ajiunge na kundi, au apotozwe kabisa, kwani kwa sasa
yeye ndiye tishio..’akasema.
‘Kwahiyo
ukafanyaje?’ akaulizwa.
‘Nikawa
natumia mbinu zangu kupoteza muda, maana kiukweli inspecta ni rafiki yangu na
tumetoka naye mbali, kwahiyo ingeniuma sana, sikupenda na baadaye waliligundua
hilo, ndio wakampa kazi hiyo mtu wao maalumu, huyo akipewa kazi, hana
mzaha…’akasema
‘Ni
vitu gani hasa wanavyovitumia kuwaangamiza watu wasiowataka..?’ akaulizwa
‘Mara
nyingi wanatumia madawa, kuna sindano zinawekwa kwenye bastola akma risasi,kwenye
hizo sindani wanaweka sumu..au hata kwenye dawa kama hizi za capsule,hata kwenye panadon, ukienda kutibiwa wanakupa
basi kazi imekwisha, ..au hata kwenye vinywaji, soda pombe, wao wanakuwa na
chupa zao tayari, zinaweka sehemu za manunuzi, ukija kunywa mtu wao,..ukinywa
umekwenda na maji….’akasema
‘Ni
hatari…huoni kuwa wanaweza kufanya makosa vinywaji hivyo vikaenda kwa watumiaji
mitaani?’ akaulizwa
‘Hilo
hawafanyi makosa, vnywaji hivyo hutengenezwa siku hiyo na kuhakikisha vinatumiwa
siku hiyo kwa walengwa, na kama vimebakia vinaharibiwa haraka sana….hakuna
ushahidi unaobakia, nakuambia hao watu ni wataalamu sana, na kila tukio
wanalifuatilia kwa kamera za video…’akasema
Inspecta
Maneno alihojiwa kwa siku mbili, ili kupata hizo taarifa, lakini mara kwa mara
aliachiwa kutoka ili aonekane yupo kazini kama kawaida, lakini chini ya ulinzi
maalumu, nia ni kuhakikisha kundi hilo haligundui chochote.
Na
siku iliyofuata ndio Inspecta Maneno akaamua kwenda nyumbani kwa Inspecta Moto,
kukagua kwa mara ya mwisho kama alivyoomba. Na kitu kilichomshangaza ni
kutokumuona Inspecta Moto, huko makaoni ambapo alisikia yupo huko, na alipouliza
aliambiwa huyo mtu hajapatikana.
‘Kwanini
msako usiendelee kufanyika, maana huyo ni mtu wetu..na kama walimpiga hiyo
sindano sizani kama yupo hai, mna uhakika kweli kuwa yupo hai?’ akauliza
‘Hilo
linaendelea kufanyika, usiwe na wasiwasi, wewe kuanzia sasa weka fikira zako
kwenye hii kazi ya kuwajibika, kuhakikisha hili kundi linamalizwa,
usipofanikiwa kwa hili, ujue utawajibika
vibaya sana, umesaliti, na adhabu ya kusaliti unaifahamu..’akaambiwa
‘Naifahamu
mkuu, mimi nitatimiza wajibu wangu nipo bega kwa bega kuhakikisha kundi hili
linapatikana, mkuu….’akasema.
Na
pale alipokuwa kasimama kwenye kiti aliogopa hata kugeuka, akilini akijaribu
kuhakiki, kuwa kweli sauti hiyo ni ya mtu anayemfahamu, akasema;
‘Wewe
ni nani, umetumwa kuniua sio…..’akasema na kwa haraka akaruka hewani na kujiviringisha
kisarakasi hewani kutoka kwenye kile kiti na kutua chini tayari kwa mapambano….
WAZO LA LEO: Siku hizi ubinadamu
umekwisha, watu wapo tayari kufanya lolote, ili wapate mali, wamefikia hadi
kuua,umesikia visa vya kuua wenye athari za ngozi-Alibino,..achlia mbali hao majambazi ambao wameamua maisha yao yawe hivyo, lakini
pia hata kwenye sehemu zetu za kazi, maofisini, mitaani, ndugu marafiki,
wanaposhawishika kuwa wakifanya hivyo watapata mali, hawajali tena ubinadamu.
Hivi
tukiwa na tamaa hivyo ya mali isiyo halali hata kufikia kuua, ina maana tunajiona
kuwa tutaishi milele, …hapana, huko ni kujidanganya, kwani kiujumla mali,
utajiri huo ni wa kupita tu, siku yako itafika, na mali hiyo utaiacha kwa
fedheha na mateso makubwa, maana adhabu ya dhuluma mateso yake huanzia hapa
hapa duniani.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Ujumbe Wa Leo murua natamani wapite wasome
Post a Comment