Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, September 9, 2014

DIARY YANGU-30




 Siku ya kwanza ya kusikilizwa kesi ya mauji ya mke wa Inspecta, watu walijitokeza kwa wingi, utafikiri ilikuwa kesi iliyotangazwa sana, na ilivyoonekana kujaa kwa watu kulitokana na propaganda nyingi zilizotapakaa kwenye magezetini, na kila mmoja alijua kuwa Inspecta ni muuaji asiyefaa kusamehewa, na baadhi ya magazeti yaliandika hivi;

‘Hatimaye haki itatendeka kuondoa uzalilishaji wa wanawake wanao zalilishwa na waume zao hadi kufikia kuwawa…

Jingine likaandika, ‘hatimaye serikali yasalimu amri na kumfikisha mmoja wa watendaji wake mahakamani, baada ya kubainika ukweli wa kuzalilishwa kwa wanawake hadi kuuwawa…

Haikutosha jingine likaandika;

‘Kigogo wa polisi aliyemuua mkewe kwa sababu ya wivu, atinga mahakamani,..

‘Kesi iliyotaka kupindishwa ionekane kuwa mke kajiua mwenyewe, yatinga mahakamani huku mshitakiwa wake akiwa mmoja wa wakuu wa idara ya usalama…

Ilimradi kila gazeti liliandika kivyake, na hakuna gazeti liliweka bayana ukweli wa tukio zima, au hata kumtetea Inspecta, habari zote zilionyesha kuwa Inspecta ni mkosaji anayestahili hukumu nzito, na amekuwa akilindwa na wakubwa ndio maana kesi yake ilicheleweshwa kufikishwa mahakamani.

Siku kabla ya kesi hiyo, Inspecta alitembelewa na mtu asiyemtegemea kabisa na hakutaka kabisa aje kuonana naye kwani ingelileta picha mbaya..na hata yeye moyoni alimuona mtu huyo kama mmoja wa watu ambao wamechangia kumuharibia mpangilio mzima wa maisha yake….alipoambiwa kuna mgeni, akajua ni rafiki Inspecta amefika, akihitajia jibu lake, lakini alipotoka hakumuona huyo rafiki yake..na akitaka kugeuka kuondoka mara akasikia sauti nyuma yake.

‘Baby, pole sana…..’akashituka, akashindwa hata kugeuka, alichofanya ni kusema…

‘Ni wewe umekuja kufuata nini hapa…?’ akauliza Inspecta.

‘Nimekuja kukushauri jambo, na kupata jibu lako, maana nimekutana na rafiki yako, akasema yupo mbioni kuhakikisha kuwa ukweli unabainika, kuwa mke wako alijiua yeye mwenyewe, na mimi nikaona hakuna hilo halina ubaya akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli, au sio…, sasa basi mimi, nimekuja kupata jibu lako, je upo tayari tulifanyie kazi…?’ akauliza huyo mdada akionyesha uso wa huruma.

Inspecta alipoambiwa hivyo,akakumbuka mazungumzo yake na rafki yake, siku alipokuja kumtembelea, ambaye alisema anahitajia jibu kesho yake, lakini kesho yake hakufika zikapita siku mbili, na siku ya kutajwa kesi ikawa anakaribia, na Inspecta Moto, akajua mwenzake keshaghairi, kaona hana hoja.

‘Sitaki kuongea na wewe, nataka kuongea na huyo aliyekutuma, nakuomba tafadhali uwe mbali na mimi…’akasema bila kugeuka kumuangalia.

‘Sikiliza kati ya watu wanaoweza kukuokoa katika hiyo kesi, mmojawapo ni mimi, mimi naweza kukiri mambo mengi sana, na yakaja kukusaidia, mwenyewe unafahamu hilo, na pia mimi ndiye ninaweza kukuangamiza, na hakuna ushahidi wowote utakaoweza kukutetea kama nikiamua kufanya hivyo…kweli si kweli…’akasema

Inspecta akageuka kuangaliana na huyo mdada, kwanza akakunja uso kwa hasira, lakini macho yake yalipkutanana huyo mdada, akajikuta akinywea, …na kwa mbali akaiona taswira ya mkewe akilia,…..alipoiona hiyo hali, akainama chini na kutulia.

‘Unakumbuka mazungumzo yenu na rafiki yako, je umeshafikiria vya kutosha maana kesho kesi inaanza kutajwa rasmi, na ukikubali tu, kila kitu kitageuka, hata hayo magazeti unayoona yakiandika ubaya, yatagezwa na kukuandika wema, kuwa kweli kumbe, mkeo alijiua….hilo niamini mimi…

Akasema huyo binti, na Inspecta akakumbuka walivyokutana na raiki yake Inpsecta mwenzake, japokuwa siku hiyo, hakupenda kabisa kukutana na huyo mtu, lakini baadaye akaamua kwenda kuongea naye tu ili ajue ni kitu gani kilichomleta, na mazungumzo yao yalikuwa hivi…

***********

‘Rafiki yangu, najua utaona nimekutupa, hasa baada ya hili tukio, ni kweli sitakuwa mbali na sheria, kwani ulichofanya hata mimi kimeniuma sana,…sikuamini hadi nilipofanya upelelezi wa kina, nikagundua mengi na moja wapo eti wewe ulinishuku kuwa huenda mimi natembea na mke wako, …siamini, na sutakusamehe kwa shutuma hiyo..mimi rafiki yako nikusaliti, hivi imekuwaje hadi kufikiria hivyo….’akaanza hivyo.

‘Ndicho kilichokuleta hapa au kuna zaidi ya hilo?’ akauliza Inspecta Moto.

‘Kilichonileta hapa ni upelelezi wa mauaji ya mke wako, nataka sheria ichukue mkondo wake, lakini kwa haki,…sasa nataka kujua ukweli kwanini ulifanya hivyo, licha ya madai yako kuwa hizo ni njama za sijui dunia yangu, na porojo zisizo na maana, hivi kwanza ulikuwa na maana gani kusema hivyo, ….’akasema Maneno

‘Nakuomba kama huna la maana lililokuleta hapa, rudi kwa hao mabwana zako waliokutuma, waambie nitapambana nao kwa kila hali,..nitahakikisha hadi tone la mwisho la damu yangu linamwagika ..hadi nyote mlioshirikiana kuyafanya haya hadi kufikia kumuua mke wangu na kunisingizia mimi, yanabainika,..hilo nakuhakikishia, nafahamu unanifahamu vyema nilivyo , nikiahidi jambo ni lazima litendeke….’akasema

‘Unajua mimi sikuelewi, kwanini unanishinikiza kwenye makosa yako, mimi nahusika vipi, kwanza hebu tuwekane wazi, ilikuwaje hadi unishuku na mauchafu hayo, tumeishi miaka mingi bila kusikia hilo imekuwaje sasa…hivi kama ningekuwa mtu wa kukushuku kwanini mimi nisingelikushuku wewe uliyekuwa unatoka na mke wangu hata  bila ya mimi kujua, eeeh, acha wivu usio na tija, na sasa unaona matokeo yake….’akasema

‘Nakufahamu ulivyo siku zote ukiahidi jambo ni lazima ulitende, ndio maana ulivyoahidi kumuua mke wako ukafanya hivyo, au sio….’akaongeza Inspecta Maneno

‘Pandikiza fitina uwezavyo, ongeza na chuki juu yake, lakini nakuambia ukweli hutafanikiwa kwangu mimi, najua kila jambo lilivyotengenezwa, ni swala la muda tu, nakusikitikia kwa jinsi ulivyojiingiza kwenye mitandao ya kijasusi, na kuacha kazi yako ya kuwatumikia wananchi…’akasema

‘Kwa vipi maana sikuelewi unachoongea, hayo maneno yako, unayatoa wapi hayo, ….?’ Akauliza

‘Utakuja kuyasikia mahakamani hatua kwa hatua,…..ngoja kesi ifike mahakamani, siwezi kukuambia lolote kwa hivi sasa, haya niambie umekuja kufuata nini, au unataka kujua nafahamu kiasi gani kutokana na njama zenu…’akasema

‘Nina maswali nataka kukuuliza…’akasema, na Inspecta Moto akatulia, hakusema neno la kukubali au kukataa

‘Ukinijibu vyema huenda na mimi nikatafuta njia njema ya kukusaidia,…mimi nina njia ambayo inaweza kukusaidia sana, lakini nataka kujua ukweli wako, niambie ulipofika siku ile kwa mkeo, usiku, mliongea nini mpaka ukafikia kukasirishana kiasi hicho?’ akauliza, na Inspecta moto akabakia kimiya

‘Wakati mpo hotelini ya yule mpenzi wako, ulisikika ukisema , tena mbele ya wahudumu wa mle ndani, kuwa utamuua mke wako,…kuna nini kilikushinikiza hadi kufikia kutoa kauli kama hiyo nzito, tena ya kuapiza, na wewe kawaida yako ukiapiza kitu hurudi nyuma, kwanini hadi kufikia kumuua mkeo,,..?’ akauliza lakini Moto akawa kimiya

‘Je wewe na mkeo mlikujaje mkawa hamuelewani, na kwanini hukuniambia , maana mimi ndiye rafiki yako mkubwa ningelikusaidia kutoa muafaka, unakumbuka siku mkeo alipofika kutoka kijijini kwa wazazi wake…wewe hukuwepo, nikajaribu kukusaidia ili sijue kuwa upo na huyo mpenzo wako, kwa nia njema nikajaribu kumliwaza , maana alishafikia kukasirika,..’akasema

‘Kuliwaza eeeh, nafahamu sana, unajua jinsi gani ya kuliwaza wake za watu…ndio ukamchukua mkaenda naye hapo hotelini, na hiyo kumbe haikuwa mara yenu ya kwanza au sio?’ akauliza Inspecta Moto

‘Ndio sio mara ya kwanza, na sio mara ya kwanza kutoka na shemeji kumpeleka popote alipotaka, kama ilivyo kawaida ya wewe kumchukua mke wangu, na yote hayo tuliyafanya kwa kuaminiana, au sio, sasa kuna kitu gani kilitokea hadi ukafikia hatua ya kutokuniamini mimi?’ akauliza, na inspecta akabakia kimiya.

‘Nilipofika usiku ule pale hotelini nilimkuta mke wako akiwa kalewa sana…sio kawaida ya shemeji kulewa hivyo, mimi namfahamu sana, kafanya hivyo kutokana na wewe au sio,… na alikuwa na wanaume, ambao sikuwaamini, nikaona nimchukue shemeji kumrejesha nyumbani, ….nakueleza haya ili nikuondoe wasiwasi wako, kuhusu mimi…’akasema na Inspecta akbakia kimiya.

‘Nilimshauri sana shemeji kuwa anayofanya sio mazuri, ni vyema turudi nyumbani na mimi nitakutafuta  maana alisema wazi kuwa anafanya yote hayo akikushuku kuwa upo na huyo mpenzi wako, kitu ambacho ni kweli, …au unabisha hukuwa na mpenzi wako huyo binti mrembo Jembe…?’ akauliza

‘Umemaliza?’ akauliza Inspecta Moto.

‘Ni hivi, nilipoona shemeji yupo katika ile hali, mimi nikamshauri na baadaye kwa shingo upande akakubali, nikamchukua hadi kwenye gari, na ilikuwa vigumu sana, hata hivyo kwa heshima aliyokuwa nayo kwangu,mwishowe alikubali, nikamchukua hadi nyumbani…’akasema

‘Nilipofika nyumbani kwako, akateremka kwenye gari, nikamuuliza kama anaweza kutembea mwenyewe , maana alikuwa amelewa, akasema anaweza, na mlinzi akamsaidia kumuingiza ndani, na mimi nikasubiri hadi mlinzi alipotoka , na kusema ameshamfikisha ndani, …sikuwa na amani, nilitaka nihakikishe kuwa huyo mtu kalala….nikampigia simu nikiwa hapo hapo nje…’akaema

‘Ushahidi wa simu kuwa kweli nilimpigia upo, hata ukihitajia naweza kukuthibitishia hilo,…na yeye alipokea simu yangu, akasema nisiwe na wasiwasi, ameshafika ndani, na muda huo alikuwa akijindaa kulala, aliongea kwa sauti iliyo sahihi kabisa….kama unataka kusikia sauti yake naweza kukusikilizisha…’akasema

‘Kwanini ulirekodi yote hayo….huoni kuwa ilikuwa sehemu ya kujihami , ya kuwa ulkuwa na njama, na kama ikitokea tatizo utoe ushahidi huo…’akasema

‘Mimi nina kawaida ya kurekodi simu zangu zote zenye utata, na hali ilivyokuwepo siku hiyo,nilijua wewe unaweza kuleta utata, nikajihami kihivyo, na utakuja kuona kuwa siku hiyo nilikuwa nimerokodi simu zote nilizopiga maana hata hivyo nilikuwa kazini kufanya uchunguzi wa kesi zinazoendelea..’akasema

‘Baada ya kuhakikisha kuwa kweli shemeji kalala, baada ya kunihakikishia kwenye simu, mimi nikaondoka, nikimuachia maagizo mlinzi kuwa kama kuna lolote litakalo tokea anifahamishe, na mimi nikarudi hotelini kukutafuta wewe..’akasema

‘Niliporudi hotelini nikakutana na hizo shutuma kutoka kwa muhudumu ambaye nilikutana naye mlangoni akiwa anaondoka, na ilikuwa ni Bahati tu, vinginevyo nisingekutana naye, alichelewa akiwa na shughuli nyingine, akaniambia kuwa wewe umetoka hapo ukiwa na hasira, na umeapa kuwa utamfanya mke wako kitu kibaya ambacho hajawahi kufanyiwa…..’akasema

‘Kwa vile mimi nakufahamu sana, kuwa ukilewa wewe unakuwa mtata, ndio maaa hupendi kulewa mara kwa mara, na sijui kwanini umeanza tena kulewa. Kiukweli nilianza kuhisi vibaya, kuwa kama umelewa, lolote laweza kutokea, nikaona nifanye juhudi kuhakikisha kuwa wewe na shemeji hamtazuriana.

‘Lakini nikajiuliza nitafanyaje, maana kwa hali ilivyokuwa na huku umelewa, taswira ya kibinadamu inaweza kugeuka, wema kuwa ubaya,hata hivyo sikukata tamaa, na kabla ya kufanya lolote,nikataka kuhakiki, nikampigia simu mpenzi wako ili nijue jinsi ulivyoachana naye je ulikuwa umelewa sana au la

‘Kauli yake ilinikatisha tamaa kwani haa yeye alikuwa na wasiwasi sana kuhusu hatima yako na familia yako. Yule binti anakupenda kweli, hata hivyo, hapeni kuvunja ndoa yako kihivyo, alitaka wewe mwenyewe uje kuamua, unajua aliniambiaje…’akatulia

‘Nenda kahakikishe kuwa kuna usalama, sitaki baya litokee mimi niwe sababu, sitaki mpenzi wangu aingie matatani kwa mgongo wangu, nenda tafadhali….akanisishi sana, nikamuuliza kwani kumetokea nini..akaniambia;

‘Rafiki yako kalewa….na alipokumbuka yale aliyokuwa akifanya mkewe, kaondoka hapa kwa hasira huku ukiapiza kuwa akifika nyumbani atamfanya kitu mbaya mke wako, nikamuuliza kitu mbaya gani, akasema umetamka waziwazi  kuwa utamuua mke wako,….sasa nakuuliza je kauli hiyo hukuitamka, je umesingiziwa kusema maneno hayo?’ akauliza na Inspecta Moto akabakia kimiya.

‘Unaweza kusema kutamka ni jambo jingine na kutenda ni jambo jingine haya tuseme 
hivyo, twende hadi hapo ulipofika kwako, …ulifanyaje, kwa jinsi inavyoonekana ulifika, na ukaanza kuzozana na mke wako, mkaanza kupigana, yeye akiwa na kisu , namfahamu sana shemeji pamoja na yote …ana hasira za haraka, licha ya kuwa mwanamke mpole sana mwenye hekima, nitamkosa sana shemeji yangu….’akasema na kuinama chini.

‘Umemaliza…’akauliza Inspecta Moto.

‘Nataka kukuonyesha uliyotenda, maana unaweza kusema unasingiziwa, kesi ya mauaji mara nyingi watu hawakubali kuwa wamefanya mpaka ushahidi upatikane, maana ukikiri basi hakuna jinsi ni kunyongwa tu…..’akasema

‘Na ndio lengo lenu, mkijua kuwa mimi nikiondoka, basi hakuna kikwazo kwenye mipango yenu, mumemuondoa mke wangu baada ya wewe kugundua kuwa kagundua mengi  unayoyafanya….au unafikiri hilo sijui…’akasema Moto.

‘Samahani sana, hayo ya kugundua, sijui mimi nahusika na kundi gani hayo ni yako, na sio vizuri kumuhusisha shemeji ya hisia zako, shemeji wa watu yupo mbali kabisa na hisia zako ..hajawahi hata siku moja kuniamboa lolote kuwa mimi ninahusika na lolote…sijui hayao yanatoka wapi, ni kwa vile umeona nimebadilika, nimeamua kujijanga, sasa wewe ulitaka nife masikini…..’akasema

‘Najua kifo cha shemeji kilikuwa bahato mbaya, ni wakati mnapambana, akiwa na kisu, ukitaka kumnyang’anya ndipo bahai mbaya kikamchoma,….sizani kama ulikusudia, na hilo nimekutetea sana….kwahiyo itakuwa mauaji ya Bahati mbaya, …sina jinsi gani nyingine ya kukusaidia…’akasema

‘Sawa nimekusikia, unaweza kuondoka…..’akasema Moto.

‘Ila kuna kitu kingine, hicho ni baina yangu mimi na wewe, tunaweza kufanya hivyo japokuwa ni dhambi, ..wakati mwingine mtu akishakufa ndio basi tena, tugange yaliyopo, hilo ni wazo langu tu, kama utaliafiki, basi mimi nitalifanyia kazi….’akasema

‘Unataka kusema nini?’ akauliza Moto

‘Mkeo kajiua mwenyewe….’akasema Maneno na kumuangalia Moto kwa makini

‘Hayo unasema wewe…’akasema Moto.

‘Ni uamuzi wako, ufe jela, kwa kifungo cha maisha au kunyongwa, au ukubaliane na wazo langu, …’akasema

‘Hayo ni mawazo yako, kama umemaliza unaweza kuondoka…’akasema Moto.

‘Ni hivi mimi nimeshaanza kujenga hoja, na kukusanya ushahidi mwingine, ambao utakusaidia wewe, nimeshaanzia huko hotelini, kusawazisha mambo, na wao wana mitambo yao ya kuweka kumbukumbu, nitakachofanya ni kuhakikisha atukio yote yanahakikiwa, ili ionekane kuwa shemeji, …alikuwa na dhamira ya kijiua mwenyewe….’akasema

‘Wewe una kichaa, wameshakuharibu akili yako, na nikuambie ukweli sitakaa kimia hadi nione haki inatendeka….’akasema Moto.

‘Sikiliza rafiki yangu, hii dunia ina mambo, na ukijifanya wewe una huruma, mpole, mcha mungu, wenzako wanatumia hayo kukudidimiza kwa masilahi yao…ukitaka kujietetea wanakupeleka kwenye mistari, kuwa muogope mungu, usifanye hivyo, uwe na huruma, wakijua kuwa ukifanya hivyo, wao wananeemeka…..’akasema

‘Sikiliza rafiki yangu wakati umefika na wewe kula nao sahani moja…mnabanana hapo hapo…ukijifanya mjanja, utaumia, na hutapata faida yoyote, hao watu unaotaka kupambana mimi siwaoni, ni hisia tu, nilishafanya uchuguzi, mengi ni kuhangaika tu, huwezi kupata lolote kwa hisia hizo, anyway…hilo wazo langu tu,  kaa fikiria hilo wazo hadi kesho nikija unipe jibu, kwani, hata ufanye nini huwezi kumrejesha shemeji duniani, au sio…’akawa kama anauliza

‘Ni kweli tunatakiwa kuona haki inatendeka, lakini kwa hali hii ilivyo, ni wewe au yeye, na yeye hawezi kuja kujitetea kuwa ulifanya wewe hivyo, kuwa ulimuua, haiwezekani hilo, yeye keshaondoka, umebakia wewe,…kwanini umebakia ina maana bado unahitajika duniani, …au sio…’akasema

‘Sasa ukijifanya msamaria mwema, unakiri kosa haya, kwa vile ushahidi upo wazi, basi wewe kiri kosa tujue moja, vinginevyo,mimi nakushauri kama rafiki yako .. tetea shingo yako…hilo ni ushauri wangu tu, kama hutaki haya pambana na ukuta…’akasema akisimama kuondoka.

‘Umemaliza…..’akauliza Moto.

‘Ndio hivyo, kama upo tayari nipe hiyo kazi, nitahakikisha kesi inafutika, na unardi uraiani, uje tujiunge pamoja, ujijenge, uwe kama mimi , wekeza miradi, jiandae vyema kwa familia yako, hizi kazi zina mwisho wake, utastaafu huna hata cha kuanzia.nakuonea sana huruma…’akasema

Inspecta Moto, akasimama na kuanza kundoka, akimuacha rafiki yake akiwa katulia na alipofika mlangoni ambapo kasimama mlinzi akageuka, na akataka kusema neno….


WAZO LA LEO: Wakati wote simamia kwenye haki na ukweli,…vikwazo, vishawishi na tamaa mbaya visikukwaze, na kugeuka nyuma, ukasaliti haki, kwa jina la kuja kujitakasa baadaye, haki ina masharti yake, mojawapo ni kuwa mkweli na mwanifu. Jijenge na tabia hiyo njema, ya ukweli na uaminifu, kamwe hutajuta katika maisha yako.

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

Heʏ there! Someone in my Facebook group shaгed this website
ԝith us so I came to take a look. I'm definitely loving the infοrmɑtion. I'm bookmarking
and will be tweeting this to my followers! Wonderful blog and wonderfսl style and
design.

My weblоg: temp

Anonymous said...

An oսtstanding share! I have just forwarded this onto a coworker who had been doing a little homework on this.
And he actually bought me lunch because I discovered it for him...
lol. So let me reword this.... Thank YOU for the meal!! But yeah, thanks for spending time to talk aƄout this iѕsue here
on your internet site.

Revіew my homepаge :: clothes printables