Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, August 11, 2014

DUNIA YANGU-14





‘Ndio nikampigia simu dakitari wake, ni dakitari wake wa karibu, nikamwambia ajaribu kumpigia simu mume wangu maana anaumwa, na bado anafanya kazi za kumuumiza kichwa, sikumwambia wasiwasi wangu huo kuwa nahisi kuna tatizo kwa mume wangu, lakini mwilini nilikuwa na wasiwasi kweli, sijui kwanini..., na yeye akafanya hivyo....’akasema na kutulia


‘Kweli alimpigia, na baadaye akatupigia simu, akasema amepiga simu lakini haipokelewi, hapo nikahisi kuna jambo..........

Endelea na kisa chetu

*********

Inspekta baada ya kuongea na mjane wa marehemu, aliondoka hapo nyumbani, na hakurudi ofisini, akaona ampitie dakitari aliyekuwa aliyekuwa dakitari wa marehemu wa siku zote, na alikwenda moja kwa moja nyumbani kwake, kwani alishawasiliana naye kuwa anakuja huko nyumbani kwake na kwa vile alikuwa mapumziko docta alimwambia atamkuta nyumbani kwake...sio mbali na hapo nyumbani kwa marehemu.

Alipofika alikimbilia moja kwa moja kuulizia tatizo lilimleta hapo....

Kwa maelezo ya mwanzo, alichoeleza hakikuwa na utofauti na maelezo aliyoyapata kutoka kwa mjane wa dakitari huyu alisema kuwa yeye alipigiwa simu na mke wa mheshimiwa kuwa ajaribu kumpigia simu mume wa mjane kujaribu kumshauri apunguze kazi kutokana na hali yake ilivyo, yeye kama dakitari aliona hilo ni muhimu, kwahiyo akafanya hivyo;

‘Kwahiyo wewe ulifanya hivyo kutokana na ushauri wa mjane wa marehemu, au ni kutokana na utaalamu wako?’ akaulizwa

‘Huyo ni mke wake, wanaishi wote na yeye anamfahamu vyema mume wake kuliko hata mimi katika maswala mengine, japokuwa kiafya na utaalamu wake,mimi namfahamu zaidi marehemu kuliko mume wake, lakini hata hivyo, mimi kama docta utaalamu wangu mara nyingi unategemea maelezo ya mgonjwa, jinsi anavyojisikia na kama sitapata maelezo ya kina, basi nitategemea vipimo zaidi….

‘Kabla ya hata maelezo hayo ya mjane, mimi mwenyewe niliwahi kuongea na muheshimiwa, ukumbuke kuwa tatizo hili hakuwa na nalo kabla, lakini mimi kama dakitari wa mtu, huwa naangalia na mwenendo wa mtu, muheshimiwa alikuwa akijituma sana, kupita kiasi, hili nilikuja kumshauri kuwa kazi ni kazi, na umi unavyokwenda, inatakiwa mtu kupunguza utendani,....

‘Kwahiyo aliponipigia mke wake, nikaona kweli kuna umuhimu wa kufanya hivyo, japokuwa haikuwa ni wakati muafaka, na kwa hisia zangu nikahisi huenda kuna tatizo, na mimi kama dakitari naweza kulisaidia, …’akasema

‘Kwahiyo hukupinga ushauri huo wa kupiga simu, maana kwa muda nahisi kwa mipangilia ya muheshimiwa ungeliweza kumsumbua, na kama ulihitajia kuongea naye ungelimpigia muhusika wake...au..?’ akaulizwa

‘Ni kweli hata mimi nililiona hilo, lakini kwa sauti ya mke wake, nilihisi kuna jambo,...’akasema.

‘Ilashawahi kutokea hivyo kabla, ukawa unampigia simu hata kabla, bila ya yeye kutaka kuongea na wewe, …..maana kama muheshimiwa angelikuwa na matatizo angelikupigia mwenyewe, kwanini wewe ulipoambiwa na mkewe ukalichukulia maanani?’ akaulizwa

‘Kwakeli hata ingelikuwa wewe, licha ya mimi kama docta wake, sauti ya mjane, lionyesha kuna jambo, kwahiyo nikaona nimpigie mume wake nihakiki, na kiukweli kama dakitari wake, niliona hilo ni muhimu zaidi….’akasema.

‘Ulipompigia simu ilikuwaje?’ akaulizwa

‘Nilipopiga simu iliita tu bila kupokelewa…’akasema

‘Ulipiga simu ya mkononi au ya mezani?’ akaulizwa

‘Nilipiga zote mbili, na zote mbili ziliita bila kupokelewa….’akasema.

‘Wewe ulipoona hivyo ulihisi nini?’ akaulizwa

‘Nilihisi kuna tatizo,...sio kawaida ya muheshimiwa, anapoona simu yangu, haaachi kuipokea, atapokea na kunipa udhuru, kuwa atanipigia baadaye kama hana nafasi ya kuongea na mimi....’akasema

‘Kwa maana hiyo kumpigia simu kabla ya yeye kukupigia sio mara ya kwanza, na je uliwahi kumpigia simu kwa sababu gani, au je mkewe alishawahi kukuambia au kukushauri kumpigia simu mume wake kabla..?’ akaulizwa

‘Mimi ni dakitari, lakini pia nautumia udaitari wangu kupata chochote, kwahiyo wakati mwingine nampigia kuulizia malipo yangu, ama kwa upande wa mkewe, hapana,...inatokea kuwa namtfauta mume wake, naamu akupiga simu ya nyumbani na anapokea mkewe, na mkewe ananielekeza wapi alipo mumewe....ni hivyo tuseme...’akasema

‘Wewe ulipompigia marehemu ukaona kimiya, ulimpigia moja kwa moja mke wake na ukamwambiaje?’ akaulizwa

‘Baada ya kuona ukimiya huo, nikahisi kuna migangano ya kifamilia,...ndizo hisia zangu za mwanzo,sikuwa nimewazia sana kuwa marehemu ana tatizo, kwani angelikuwa nalo angelinipigia mimi kama dakitari wake,...na ni muda sijawasiliana nao kuhusu afya ya marehemu, na familia yake kwa ujumla...nilimpigia simu na kumwambia mkewe, simu haipokelewi....’akasema

‘Mkewe alikuambiaje?’ akaulizwa

‘Aliguna, na kukata simu....mimi nikaona ni bora nifike tu nione kama naweza kusaidia, kama jirani , ....’akasema

‘Kwanini unasema kama jirani, na sio kama docta?’ akaulizwa

‘Sikuwa nimefikiria tatizo la kiafya zaidi, japokuwa niliona nifike kwa yote mawili, kama ni kiafya basi nitafanya kazi yangu, lakini kama ni kifamilia basi nitatumia hekima yangu...’akasema

‘Katika mkataba wenu wa kazi, unaweza kufika wakati wowote bila kuitwa?’ akaulizwa

‘Hilo halijasema hivyo, kuwa mpaka niitwe , hapana mkataab wetu unasema mimi ni dakitari wake na nitatoa huduma za kiushauri, matibabu, nk....ushauri hapo ni kwa muda wowote nitakaoona mimi, au yeye....’akasema akitafakari jambo.

‘Ulipofika uliwakuta wanafamilia wanafanya nini?’ akaulizwa

‘Nilipofika nilikuwakuta watoto na mfanyakazi wao wa ndani wakiwa sebuleni, wakionyesha wasiwasi mkubwa, na mkewe hakupo hapo, nikawauliza mama yao yupo wapi, wakanielekeza kwa kidole kuelekea sehemu ambayo naiahamu kama maktaba ya marehemu...’akasema

‘Ukaelekea huko, hukuwauliza kuna tatizo gani?’ akasema

‘Hapana, kama engelikuwepo mkewe ningelimuuliza, mimi moja kwa moja nikahisi wapo pamoja huko makataba na kuna maongezi mazito, kwahiyo bado nikawa na tahadhari nikaelekea huko, na bahati nilimkuta mkewe akiwa mlangoni...’akasema

‘Akiwa nje au ndani...?’ akauliza

‘Ilionekana alikuwa anaingia au anatoka...maana alikuwa kashikilia mlango, nusu wazi, na sehemu ya mwili wake upo nusu nje na nusu ndani...akiwa kachungulia kwa ndani....’akasema

‘Ukafanyaje?’ akauliza

‘Nilimsalimia, akashituka, na alionekana kutoa macho ya uwoga, na waisiwasi kama vile kaona kitu cha kutosha au hakutarajia kuniona mimi, siweza kujua ni kwanini yupo kwenye hiyo hali, lakini akatulia aliponiona na kusmea;

‘Afadhali umekuja....akasogea kuniachia nafasi nipite....’akasema

‘Kwahiyo hakuwa ameingia ndani, huyo mama|?’ akauliza
‘Siwezi kujua hilo,..kama alishawahi kuingia au ndio alitaka kuingia, kwani kama nilivyokuambia alikuwa kati kati ya kuingia au kutoka, ila alikuwa kachungulia kwa ndani, akiwa kashikilia mlango...’akasema

‘Halafu ukakupisha ukaingia ndani,..uliona nini kwa haraka?’ akaulizwa

‘Unapoingia pale kwenye makitaba hiyo huwezi kuona ndani moja kwa moja nafamau unaifahamu vyema, kwahiyo nilifulululiza hadi ndani, na nilipokuwa ndani ndio nikaona hali halisi, marehemu alikuwa kakaa kwenye kiti akiwa kaegema kichwa upande na ulimi upo nje...’akasema

`Ulifanya nini, ulimuambiaje mkewe ambaye nahisi alikuwa bado mlangoni?’

‘Mimi niliharakisha kufanya yale dakitari yoyote angelifanya, kwanza kama mgonjwa kapoteza fahamu na ana uhai unamrejeshe katika hali yake, kwa kumpa huduma ya kwanza, lakini kwa hali niliyoiona kwa marehemu, kiukweli haikuhitajia maelezo, sijawahi kumuona hivyo kabla, na ndio kama dkitari sikutakiwa kumhisi hivyo, ila kwa haraka niliona hali aliyo nayo ni mbaya, kwanza kabisa nikakimbilia kuangalia mapigo ya moyo...’akasema

‘Nilipomgusa mwili, nilihisi ubaridi wa hali ya juu, ..na japokuwa unaweza kusema ni kwa vile kulikuwa na kipozeo cha hali ya hewa, lakini ubaridi wake ulikuwa sio wa kawaida, mapigo ya moyo yalikuwa hayapo,..nikatumia kipimo cha kitaalamu na ilikuwa kama kujirizisha tu....’akasema

‘Katika kazi yako hiyo unaweza kumtambua mtu kuwa hayupo hai kwa kumuangalia tu kwa macho?’ akaulizwa

‘Unaweza kama dakitari, lakini udakitari ni utaalamu, una njia zake za kuhakiki jambo, huwezi kusema kuwa hiki kipo hivi mpaka kuwe na vipimo, na kuna huduma za kwanza nk, ....

‘Je hayo ulimfanyia marehemu?’ akaulizwa

‘Kama nilivyokuambia hali aliyokuwa nayo haikuhitaji maelezo, nilipompima na kipimo cha kitaalamu, niliona hapo hakuna uhai, na kabla sijafanya lolote la ziada nikaona ni vyema waje watu wa usalama.

‘Dakitari, kwanini hukumfanyia huduma ya kwanza...mimi hapo hujaniweka sawa?’ akauliza

‘Sikuwa na haja hiyo, kama dakitari nilishaona kuwa muheshimiwa keshafariki, mtu yoyote hata kama sio dakitari kwa hali ile ungelijua kuwa huyo muheshimiwa alikuwa marehemu....kwakweli sikusumbuka kufanya hivyo...’akasema na Inspecta hakuona haja ya kushinikiza hilo kwani kwa vipimo ilionyesha wazi muheshimiwa alipatwa na umauti kabla ya huyo dakitari hajafika.

‘Ulipoingia mezani uliona nini?’ akaulizwa

‘Mhh, kulikuwa na simu ya mezani na ya mkononi...na ...mafaili na kitabu....’akawa kama anakumbuka

‘Je Simu ya mkononi uliikuta ikiwa inafanya kazi kazi?’ akaulizwa

‘Siwezi kujua, mimi sikuingia kwa ajili ya kuangalia simu, ila nakumbuka wakati nampigia iliita, umuhimu wangu ulikuwa kwa mgonjwa…’akasema

‘Hugusa kabisa simu, au kitu chochote kwenye meza?’ akaulizwa

‘Sikugusa kitu chochote, akili na mawazo yangu ilikuwa kwa mgonjwa…’akasema, na Inspecta akazidi kuwa na hamasa ya kifo cha muheshimiwa huyu, na akili yake ilimtuma kuwa ni lazima kuna jambo limejificha,...ni kwanini simu ile ya mkononi imezimwa na namba zote zilizopigwa siku hiyo zikafutwa , na ni nani mwingine aliingia kabla ya docta, au baada ya docta kuondoka.

‘Hebu turudi nyuma kidogo, mjane anasema mume wake kabla alikuwa hana matatizo kama hayo, na wewe ni dakitari wake wa siku nyingi,je unahisi ni tatizo gani lilimfanya abadilike hivyo , je marehemu hakuwahi kuongea na wewe kuhusu hali yake au kama ana matatizo yote , ya kiakazi au ya kifamilia?’ akaulizwa

‘Ni kweli marehemu hakuwahi kuwa na tatizo hilo kabla, mimi nimekuwa naye kwa muda mrefu, tatizo ni kuwa alipoanza kusikia hali mbaya, hawakuniita mimi kwanza, walikwenda moja kwa moja kwenye hospitali kitu ambacho sio kawaida yao, mara nyingi wananiita mimi, kwahiyo siwezi kujua zaidi walichotibiwa huko…waliponiita jana, niliangalia dawa alizopewa, kwangu mimi niliona kama dawa alizopewa nidozi kubwa zaidi….’akasema

‘Una maana gani kusema hivyo?’ akaulizwa

‘Ni kwa maoni yangu tu, kama mtu ninayemfahamu marehemu vyema,sizani kama hali yake ilikuwa mbaya kiasi hicho, sina uhakika kama shinikizo hilo lilifikia kuwa kubwa hivyo,hadikuandikiwa dozi hiyo kubwa hivyo…. ‘akatulia kama anahakiki maneno yake.

‘Ina maana kwa kutumia hizo dawa, walipandisha shinikizo kwa haraka sana, na hapo unaweza kueleta shinikizo la juu..., sijui ndio kutaka kumponyesha kwa haraka au ni kwasababu gani, lakini kwa vile yupo mtalaamu aliyemuhudumia, siwezi kusema zaidi, yeye anajua zaidi, kwa vile yeye aliona anahitajia hizo dawa ….’akatulia kidogo akionyesha wasiwasi baadaye akasema;

‘Kwahiyo kwa kauli yako unahisi kuna uzembe, kuna mapungufu katika matibabu yake na huenda ikawa ndio chanzo au....?’ akaulizwa

‘Hapana sio kwamba nalaumu,ni wasiwasi wangu tu, maana wanasema huyo aliyemshughulikia ni dakitari bingwa, na yeye ndiye aliyempima akaona dawa hiyo inastahiki, kwahiyo yawezekana kweli huenda shinikizo hilo la damu lilistahiki hiyo dawa…’akasema

‘Inaweza ikawa ni biashara, siku hizi biashara inapewa kipaumbele kuliko taaluma, unahisi ikawa hivyo, kuwa aliandikiwa ili kuingiza pesa kuliko kuangalia atahari zake?’ akaulizwa.

‘Mhh, yote yawezekana au isiwezekane, kama nilivyokuambia aliyemuhudumia ni docta, na nimeambiwa ni docta bingwa, kwa hali hiyo mimi siwezi kutia neni hapo..’akasema na kauli yake ilionyesha wasiwasi

‘Docta wewe ni docta wake wa siku nyingi, unaweza kunipa tathimi zako, maana huyo ni mtu wako, na mlikuwa naye karibu, kama kuna uwezekano wa hujuma, ni vyema ukasema ili haki itendeke, wewe unaonaje kuhusu kifo cha muheshimiwa je kuna jambo, kuna hujuma?’ akaulizwa

‘Sijasema hivyo kuwa kuna hujuma, na siwezi kukimbilia huko kuwa kuna jambo limefanyika kusababisha hayo yote, kwani aliyempima ni mtaalamu na docta bingwa, na hata mahakamani huwezi kumpinga,ila kwangu mimi naona walikimbilia dozi kubwa zaidi sana ….’akasema

‘Je dozi hiyo ni hatari hata kusababisha kifo?’ akaulizwa

‘Dawa yoyote ikizidi kipimo yaweza kuwa sababu, hasa dawa za mashinikizo ya damu, ni dawa zinazohitaji uangalifu wa hali ya juu...lakini aliyemuhudimia ni docta bingwa, siwezi kulaumu au kutia neno.

‘Wewe unamfahamu huyo docta aliyempima?’ akaulizwa

‘Niliangalia cheti cha dawa alizoandikiwa nikaona jina na sahihi ya docta, sina uhakika kama ndiye huyo, ila mjane alisema ni Docta Mashuhuri kutoka Marekani, sikumbuki vyema, lakini kwa kumbukumbu zangu za hospitali zinazomilikiwa na madocta bingwa, sikumbuki kuwepo kwa docta kama huyo kutoka Marekani,....’akawa kama anafikiria, halafu akasema kwa uhakika

‘Sizani kama hiyo hospitali inamilikiwa na mtu kutoka nje, sina uhakika zaidi hapo,na sijapata muda wa kulichunguza hilo, hiyo sio kazi yangu, na sikuwa na sababu ya kufanya huo uchunguzi,japokuwa mimi ni mmoja wa viongozi wa wamiliki wa hospitali, upande wa madocta bingwa ….

‘Unajua mambo hapa yamekwenda haraka zaidi, na japokuwa mimi ni docta wa marehemu, lakini siwezi kuingilia na kusema ngoja nichunguze nione ni nani alimpima na kumuandikia hiyo dawa kama wanafamilia hawajaniambia hilo….’akasema

‘Je wewe unahisi anayemiliki hiyo hospitali aliyopimiwa ni Mtanzani au ni mtu unayemfahamu?’

 ‘Kwa kumbukumbu za madocta bingwa, kuna docta mmoja ambaye kamiliki hospitali hivi karibuni, na kama ni huyo docta ninayemafahamu mimi, basi ni docta bingwa kiukweli,maana alikwenda kusomea nje,kuongeza ujuzi wake zaidi, na ana kipaji cha udakitari licha ya udhaifu wa hapa na pale wa kibinadamu, vinginevyo yeye ni docta bingwa na labda kuwe na mtu mwingine katumia jina lake…sasa sijui huyo Mumarekani ni nani.’akasema

‘Huyo docta bingwa unayemuhisi anaitwa nani huyo unayesema kaanzisha hospitali hivi kaibuni?’ akauliza

‘Anaitwa Docta Chize.....’akasema na kutulia

‘Docta Chezo,Docta Chize …..hili jina kama nalikumbuka...’akasema Inspecta akivuta kumbukumbu zake, na akawa na hamu ya kukutana na huyo mtu, na alipoona docta wa Marehemu hasemi kitu, akasema

‘Na hata hapo kwenye hiyo hospitali yake anatumia jina hilohilo...maana sijawahi kusikia watu wakitaja jina hilo?’ akauliza Inspecta

‘Mhh,sina uhakika sana, ila wengi niliowahi kuwauliza wanasema anaonekana kama mtu mwingine tofauti, sijawahi kumfuatilia sana,…na sijawahi kufika hapo au kukutana naye kama ni yeye, tangu arudi masomoni....’akasema

‘Ok, basi nitakwenda kuonana naye mwenyewe, nashukuru sana docta,kama nitakuwa na zaidi nitakutafuta….’akasema Inaspecta aakagaana na docta huyo na kurudi ofisini kwake.

Alipofika ofisini kwake kuangalia mambo mengine yanakwenda vipi, na hakuweza kumuona msaidizi wake, ajajue mwenzake naye anahangaika kutafuta ukweli wa tukio hilo, akaona haina haja ya kukaa hapo ofisini, akatoka, na safari hii kichwani alijawa na mawazo kumhusu huyo docta asiyetambulikana vyema.

Akaingia kwenye gari kuelekea huko kwenye hiyo hospitali na kila hatua aliona hamasa za kulifuatilia hili swala kwa undani zaidi zinazidi kuongezeka, japokuwa mara kadhaa alipojaribu kumgusia mwenzake kuwa huenda kifo cha Muheshimiwa kina hujuma ndani yake, lakini mwenzake alionekana tofauti na wazo hilo...

‘Kwanini Inspecta mwenzangu haniungi mkono kuwa muheshimiwa anaweza kuwa hakufa kifo cha kawaida...sijui nahisi kachoka na kazi, sijui...., ila namuamini sana, ni mchapakazi mnzuri, na siwezi kumtilia shaka kwa lolote lile, ila lakini tangu aoe, amekuwa tofauti, ...mmh, sijui, ndoa inaweza kuwa sababu, sijui ...ngoja nikikutana naye nitajaribu kuona maoni yake, lakini mimi nataka kulifuatilia hili jambo hadi nione mwisho wake, akubali asikubali....’

NB: Je kuna nini hapa je Inspecta ataweza kuingia kwenye dunia ya bwana Diamu, mtu tajiri, mwerevu mwenye akili ya ziada,....tuone itakuwaje

WAZO LA LEO: Elimu bora ni ile yenye tija, ambayo itamsaidia mtu , na jamii yake kujiendeleza, kutoka hatua moja ya maendelea kwenda hatua ya juu ya maendeleo. Elimu sio ujanja wa hadaa, elimu ni utukufu wenye hekima ya utambuzi wa kipi kizuri na kipi kibaya, kibaya kikaepukwa na kizuri kikaenziwa na kuleta faida(tija).


Mwenye elimu thabiti hana uchoyo wa elimu yake, ataitumia elimu yake, kwa manufaa, kujenga na sio kubomoa, kama elimu itakuwa kinyume chake, basi kuna walakini hiyo sio elimu bali hadaa, na hadaa ni ujinga, ni dhuluma, na kamwe dhuluma haidumu, ikidumu inaangamiza.
Ni mimi: emu-three
Ni mimi: emu-three

No comments :