Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, December 6, 2013

Mkuki ni kwa Nguruwe-42Nilimfikisha rafiki yangu nyumbani kwao, na akapokelewa na shoga yake, na sikutaka kuongea nao zaidi nikaondoka, kwani ilikuwa ni usiku, na wakati natoka, akakatiza mtu, na kuja karibu na gari angu, hakusimama, alikuwa akitembea huku  akisema;

‘Usije ukatutosa bosi, kesho tunakuja kuchukua pesa zetu....tutakuwa tumeshamaliza kazi’sauti ikasema na mimi sikusema kitu nikaingia kwenye gari langu na kuondoka.

Wakati naendesha gari, nilianza kuwaza hicho niichokifanya, hapo hapo huruma ikaanza kunijia, nikikumbuka jinsi gani nilivyohadithiwa na mmoja wa watu waliowahi kushuhudia ndugu yake aliyewahi kufanyiwa huo ukatii na hawo watu, alisema ndugu yao aliharibiwa kabisa, na haikuchukua hata wiki ndugu yao huyo akajiua. 

‘Ina maana mimi nimekuwa na roho mbaya kiasi hicho, japokuwa rafiki yangu amenifanyia huo ubaya, lakini sio vyema, kumtendea hayo, huo utakuwa ni ukatili wa hali ya juu, mbona nimechukua mambo kihasira zaidi, ina maana ubaya nalipiza kwa ubaya wa kiasi hicho, ..kwanza huyo ni mama mtoto , analea, je hicho kitoto kitalelewa nani...’nikajiuliza

‘Nitamchukua mimi, na kumlea kama mtoto wangu,....’nikajipa matumaini, lakini nilikumbuka kauli ya rafiki yangu huyo wakati tunaongea ndani ya gari, aisema;

‘Mtoto huyu ndiye jicho langu, sitakubali kuachana naye hata siku moja...’alisema.

‘Hata kama baba yake akimtaka, akaishi naye utamkatalia?’ nikamuuliza.

‘Kwa misingi ipi, kwani mimi nimekufa, au sina uwezi wa kumlea’akasema.

‘Baba yake ana haki na mtoto wake pia...’nikasema.

‘Hata mimi nina haki na mtoto wangu, hilo sikubaliani nalo hata siku moja, kwasabbu mimi mwenyewe nina uwezo wa kumlea, kwanini huyo anayejiita baba aje kumdai mtoto wangu, ...’akasema.

‘Lakini wakija na hoja kuwa wanamtaka huyo mtoto, wamlee, ikizingatiwa kuwa huyo baba mtoto ana mke wake, na mke wake yupo tayari kuishi na huyo mtoto, utakataa?’ nikamuuliza.

‘Mimi sina cha kuongea, ilimradi kauli yangu ipo wazi, kuwa huyu mtoto sitaachana naye kamwe,labda niwe maiti...’akasema.

‘Hujaniambia baba wa mtoto huyo ni nani, au ni mume wangu kama inavyojulikana na wengi, maana nimeshayafahamu yoye hayo, na wapi mlipokuwa mkikitana?’ nikamuuliza

‘Waache watu waseme wapendavyo, lakini anayefahamu ukweli wa yote ni mimi mwenyewe, na hautabadilika huo ukweli  na nina ushahidi wa kitaaamu, na hujui jinsi gani niivyotaabika na huyo mume wako, hujui tu, vinginevyo angeliishia kutembea na changudoa...’akasema

‘Hahaha, yaani unajisifia kuwa uliweza kuhangaika naye, kuzini na mume wa mtu huoni ni kosa kubwa, na mungu akawadhihirisha kwa kuwapa mtoto, sasa niambie ni ushahidi gani, ndio huo mkataba wa bandia mlioutengeneza, na ambao unaweza kuwa ushahidi mahakamani, siku kesi ya mauaji ya Makabrasha ikianza?’ nikamuuliza

‘Mimi sizungumzii huo mkataba, huko mkataba ni wao walinilazimsha tu, sikuwa nafahamu mambo yao, na sijakaa na kuliwazia hio, mimi nazungumza maswala ya kitaalamu, kuhusu mtoto wangu,...kuwa hana baba,kama wanavyodai watu, na nitalithibistiha hilo hata mbele ya mahakama, huyu ni mtoto wangu mwenyewe....’akasema

‘Kwa vipi,...huwezi kuzaa mwenyewe, hukupandikizwa mbegu, wewe ulizini na waume za watu, ndio ukazaa, kwei si kweli...?’ nikamuuiza.

‘Kuzini ni kitu kingine, wangapi wanazini na hawapati mimba,...sitaki kuyaongea hayo zaidi maana hutanielewa, maana kwa hivi sasa huwezi hata kukumbuka kuwa wewe ndiye uliyekuwa mshauri wangu mkuu, ...ukanishauri yakatokea hayo yaliyotokea basi, sikuwa na wazo hio kabla, sikuwa kukutana na hawo waume za watu kaba, nilianza baada yaw ewe kunishauri, nafahamu hutanielewa, na sina njia nyingine ya kukuelewesha, kwasasa,...sina zaidi, naomba tusiongee, tutakuja kuyaongea siku nyingine....’akasema

‘Hamna shida...lakini kiukwei, sitakuja kukuelewa kamwe, mimi siwezi nikawa mjinga kiasi hicho, eti nikushauri ukazini na mume wangu halafu, halafu kitendo hicho hujafanya mara moja, ungelisingizia kuwa ni bahati mbaye, mikuwa mumelewa....’nikasema.

‘Wewe hujui tu, ...usilolijua ni sawa na usiku wa giza, ...’akasema.

‘Ndio siwezi kukuelewa, hakuna sababu ya msingi ya kuzini na mume wa mtu, tena mume wa rafiki yako, rafiki yako unayemtambua kama dada yako, anayekuamini..mpaka sasa akii inashindwa  kuamini kama kweli wewe ulifanya hivyo,huna sababu ya kusamehewa,  ..’nikasema na kumwangalia, alikuwa kakunja uso na kushika kichwa kuonyesha kukerwa na hayo ninayoongea.

‘Naomba tuyaache, ipo siku nitakuambia ukweli ulivyokuwa,..lakini kwa sasa naomba uniache, sina cha kuongea zaidi...’akasema

‘Haya mimi naisubiri hiyo siku kwa hamu, maana umeshaniahidi mara nyingi kuwa utaniambia, sasa umerudi, ...nataka kusikia huo utumbo wako, wa kujiidhinishia madhambi yenu, mimi nilichotaka ni kauli yako tu, kuwa kweli ulizini na mume wangu, ilimradi umekubali kuwa ulizini na mume wangu, hiyo inatosha... inatosha kabisa...asante sana.’nikasema na kukaa kimiya,kwani hata mimi niikuwa na mawazo yangu kichwani, na hasira nilizokuwa nazo zilikuwa kubwa sana, kwahiyo tukawa tupo kimiya hadi tunafika.

*******

 ‘Je ni haki kumufanyia huyo mama wa mtoto hayo ninayotaka kuyafanya, akili yangu hakukubaliana na huo uamuzi,  niliingiwa na wasiwasi, nikawa na mawazo mengine kuwa niwazuie wasiendelee na hilo zoezi, kwani kama walivyosema, vitendo watakavyomfanyia vinaweza kumuua, na hata kama hatakufa hapo, lakini anaweza kuja kujiua mwenyewe

Nikaamua kuwapigia simu ili wasitishe hilo zoezi, lakini simu zao zikawa hazipatikani, nikaamua kumpigia simu huyo rafiki yangu, ambaye alipokea simu yangu halafu aliposikia sauti yangu, akakata simu.

Muda ukawa unakwenda na na sikujua kabisa nifanye nini, maana muda huo ni usiku, na nisingeliweza kurudi kule kwa rafiki yangu, mara simu ikalia, nilipoangalia mpigaji nikaona ni baba yangu;

‘Baba mbona simu usikuusiku..?’ nikauliza baada ya kusalimia

‘Je kikao cha kesho kipo , kama ulivyotaka?’ akaniuliza

‘Ndio baba nimeamua iwe hivyo, ..’nikasema, maana nilipanga kuwa , tuwe na kikao cha pamoja, kikiwahusisha wazazi wangu. Niitaka kikao hicho kiwe cha hitimisho ya hayo yote, ili hukumu itolewe na kila aliyehusika awajibike.

‘Basi itakuwa vizuri, na uwe na ushaidi wote, kwani sisi hatutaweza kuvumilia hayo yanayotokea kwenye familia yako, nilishakuambia kuwa mimi sitaki kashifa, sasa hicho kinachoendelea hapo kwenu kinaniharibia jina langu...unalifahamu hilo?’akaniuliza

‘Kwanini unasema hivyo baba, kwani kuna nini kimetokea huko kwako?’ nikamuuliza

‘Jana Askari walifika hapa kwangu na kunihoji, ...wanahisi kuna uwezekano mkubwa kuwa mume wako kahusika kwenye mauaji ya Makabrasha..’akasema

‘Kwanini wakuhoji wewe?’ nikauliza

‘Kwasababu wanataka kujua mahusiano ya kampuni zangu za zako, na kwanini kulionekana mikataba miwili, kuna mkataba mwingine uliokuwa ukimpa Makabrasha hisa nyingi kwenye kampuni ya mume wako, ikipingana na mkatana wa awali ambao hata sisi tunaufahamu, je huo mkataba mpya ulitayarishwa lini na kwanini mkampa hiyo kazi Makabrasha, wakati mnamfahamu tabia yake?’ akauliza

‘Baba hilo ni moja ya jambo tutakaloliongea kesho, kuna mengi yamefanyika, nakubali hilo, na nimeamua kesho niyaweka yote wazi,, ili kijulikane kimoja, mume wangu hajambo, na anaweza kujieleza, na lolote linaweza kutokea, sijaamua ni nini cha kufanya mpaka sasa, ukizingatia kuwa mume wangu hajawa na afya ya kutosha, inabidi nitimize wajibu wangu kama mke wake..’nikasema

‘Hujaamua la kufanya hadi sasa, wakati unaishi na mtu anayeweza ku-kuua, kwa ajili ya mali zako, wewe hulioni hilo, kama wamefikia hatua ya kubadili mikataba ya halali...na katika harakati zao, inaonekana walishindwana,  wakauana. Huoni kuwa mkono ukionja damu, inakuwa kama muonja asali, hajai tena kufanya maasi,....hilo sisi hatutalikubali, kama wazazi tutachukua hatua ...’akasema.

‘Baba nafahamu, mnavyojisikia ...lakini...’nikataka kujitetea lakini baba hakukubai kunipa nafasi , akasema;

‘Sitaki kusikia jambo jingine la kupinga maamuzi yangu, kama unanikubali mimi kuwa ni baba yako, kama unamkubali mama yako, basi itabidi ukubaliane na sisi, ....wewe huoni, wameamua kumuua,mtu wao wanayemuamini, na kumtambua kama sehemu ya famiia yao, kwa ajili ya kuficha ukweli, unafikiri watakuwa na huruma na wewe, binti yangu nilishakuambia huyo mume hakufai, mbona unatuweka roho juu...’akasema

‘Baba nilishawaambia mambo yangu nitajua jinsi gani ya kuyatatua, mwenyewe...niachieni,kwanza, nifanye nijuavyo mimi, ...msikimbilie kuchukua maamuzi yenu kwanza,kesho nimewaomba ili muweze kusikia maamuzi yangu, ambayo yatakuwa ni maamuzi yenye muafaka wa kudumu, nimesema sijafikia uamuazi bado, lakini mpaka kesho nitakuwa nimeshaamua ni nini cha kufanya, kwani kuna mambo ambayo nilikuwa nayamalizia...’nikasema.

‘Ulikuwa unamsubiria mpelelezi wako, ambaye keshakusaliti,...usimwamini huyo binti, kesharubuniwa, na kwasababu ya mali ..kwasababu ya tamaa, na kwa vile ana mahusiano na mume wako hatajali lolote itakao tokea kwako....anakufahamu udhaifu wako, anafahamu siri za kwako za nje na ndani, kwahiyo hatasita kukufanyia lolote baya....’akasema.

‘Baba huyo nimeshamweka sawa, hana lolote kwangu, nimeshamfahamu,...’nikasema

‘Sisi kama wazazi, tumeshafikia uamuzi,  sisi kama wazazi, kesho tutatoa maamuzi yetu,kwa masilahi ya familia kuu, hili siwezi kulivumilia tena, na tuijaribu kuongea na mume wako, akaonyesha kiburi cha hali ya juu, inaonyesha anajiamini sasa kupita kiasi, hiyo ndio tabia yao, wameshajua kuwa wamekuweka mkononi mwao, ....’akasema.

‘Baba kwanini mnaongea na huyo mtu wakati yupo kwenye matibabu,...hamuoni kuwa mtakiuka makubaiano yangu nay eye.....’nikasema.

‘Mume wako alishapona, na hayo yaliyotokea baada ya yeye kupona, ni moja ya mbinu zao, sisi hilo tulishaiona, na tumeshaongea na dakitari wake, na ingawaje dakitari wake anamtetea, lakini tuna uhakika kuwa mume wako anafanya hivyo makusudi, ili kufanikisha maengo yake...’akasema

‘Baba naombeni mniachie nifanye jinsi nionavyo mimi,...nisingelipenda nyie muingilie kati kwanza, kwani sijashindwa, ...’nikasema.

‘Ushindwe mara ngapi, kama umekubali, mume wako awe na nyumba ndogo, umekubai mume wako, azae nje, hujashindwa hapo. Hilo lilikuwa ni jukumu lako kubwa sana kuhakikisha kuwa mume wako anakuwa na utuivu wa ndani, ....hukuweza kulifanya hilo, na huo unaonyesha udhaifu, niambie kuhusu watoto wa mume wako ....au unafikiri sisi hatufahamu hilo?’ akaniuliza

‘Watoto gani wa mume wangu,?!’ nikauliza kwa mshangao

‘Unaniuliza, wakati sasa hivi umesema kuwa mambo yako utayaongoza mwenyewe, ..hufahamu kuwa mke wako ana watoto nje..huoni athari zake, wewe unalichukulia kawaida tu, hiyo ndio adabu tuliyokufundisha, huoni hiyo ni aibu kwenye familia yetu, unatuweka wapi sisi,..hebu angalia maisha ya mbele, hao watoto, watakuja kujitokeza na madai yasiyoeleweka, watakuja kugombana na wenzao, ...maana kwa hivi sasa hamuwatambui, mpaka mmoja wenu afariki,..ndivyo ilivyo, ni heri wangejitokeza muda huu, mkiwa hai, ili mjue ni nini cha kufanya, haya tulikukanya, tunaifahamu sana hiyo familia...’akasema

‘Baba hili nimeligundua, lakini nijuavyo mimi , mtoto wa nje mmoja tu, huyo wa pili sio kweli’ nikasema.

‘Huyo wa pili sio kweli, ni yupi wa kweli na yupi sio wa kweli?’ akaniuliza na mimi hapo sikuwa na uhakika wa kumuelezea nikasema.

‘Baba yupo mtoto namfahamu,...japokuwa mume wangu hajanikubalia, na hata huyo mzazi mwenzake hajakubali lakini daily zipo wazi...’nikasema

‘Mimi nina ushahidi, ana watoto wawili,...unamkumbuka yule mfanyakazi wenu wa ndani aliyeondoka hapo bila kuaga,ulifuatilia ukajua ni kwasababu gani,wewe ulisema kuwa aliondoka bila kuaga,...hujui kuwa aliondoka kwa shinikizo la mume wako, ilikuwa siri yao wawili, huyo binti  aliondoka akiwa mja mzito, na mume wako anafahamu, akawa anamtumia pesa za matumizi huko huko kwa siri, alijifungua, mtoto wa kiume, wanafanana na mume wako kama mapacha...’akasema

‘Mhh, hilo kwangu ni jipya, sikuwahi kulisikia, nitamuuliza mume wangu na ikibidi nitamtfauta huyo binti ii niweze kuhakikisha ...na kesho hayo yote yatajulikana, na ingekuwa vyema huyo msichana awepo kwenye hicho kikao, ..nyie mlipata wapi hiyo taarifa?’ nikamuuliza

‘Sio kwamba tumesikia, huyo msichana yupo hapa kwangu, alikuja kulalamika, kwasababu tangu mume wako aanze kuumwa hajatumiwa pesa za matumizi, na ilikuwa bahati tu kumpata, na sisi ikabidi tumchukue aje hapa kwetu, alikuwa mbioni kuja hapo kwako, tumelifanya hilo ili kuepusha kashifa, sasa hili halina siri tena, unafikiri wewe utachukua hatua gani, ii hii hali isifike kwa hawa wadaku...’akasema

‘Oh,..baba naona unipe muda niweze kufikiria, sikulijua hilo kumbe sio mmoja,...’nikasema nikiwa nimeingiwa na wasiwasi, kumbe namuhukumu mtu mmoja, na huyo je atahukumiwa na nani, na je ni hawo wawii peke yao....

‘Huna haja ya kuumiza kichwa, nashukuru kusikia kuwa umeshaupata huo mkataba wenu wa hiari, kati yako na mume wako,...nimeupenda, na ni vyema sasa ukachukua hatua kama mivyokubaliana, na kama utashindwa kuchukua hatua, ujue wewe huwezi kujiendesha mwenyewe...huo ndio mtihani wako, sisi tumeshachukua maamuzi yetu,....’akasema

‘Baba naomba nipumzike, maana akii yangu haipo sawa...’nikasema

‘Haya usiku mwema,..lakini uwe makini, usije ukachukulia hasira, ukatenda mambo kama mtu asiyesoma, ujue kuan sheria,..ujue ni kitu gani unachokifanya usije ukatenda mambo kama watu wengine, ...ukiharibu , sisi hatutakubali...’akasema

‘Sawa baba....’nikasema
Nikachukua simu yangu na kumpigia rafiki yangu, akawa hapatikani, nikajaribu kuwapigia hawo watu niliowapa hiyo kazi, na wao wakawa hawapatikani...sikukubali, nikatoka nje, na kuingia kwenye gari, sikuwa na muda wa kuongea na mlinzi, nikalitoa gari, na wakati nataka kutoka mlinzi akaja kunisalimia

‘Bosi unatoka?’ akaniuliza

‘Ndio kuna kazi nafuatilia, je mambo yapo sawa?’ nikamuuliza

‘Yapo sawa...’akasema lakini nilimuona kama alitoka kulala..

Wakati nimeshafika barabarani, nikahisi kuna mtu nyuma yangu, ndani ya gari, na kabla sijaweka gari sawa, sauti ikasema;

‘Fuata maelekezo yetu, la sivyo, tutakufanya kitu kibaya..’sauti nzito ya kiume ikasema na nikahisi kitu kikali kikigusa ngozi yangu, nikahisi kuwa ni kisu....

NB; Kulikoni...

WAZO LA LEO:Ushauri wa wazazi ni muhimu sana, tunaposhauriwa na wazazi wetu tujaribu kuwasikiliza, hata kama tunajiona tuna uwezo zaidi yao wa kihali na mali, tujue kuwa wao wameona mengi zaidi yako, na wamepitia maisha ambayo wewe hujawahi kuyapitia, hekima zao zinaona mbali zaidi, tuwasikilize, tukae pamoja nao, tuone je mawazo yao na mawazo yetu yanaweza kufikia muafaka wenye manufaa, tusichukulie ubabe kwa vie tunazo, tumesoma sana, nk.

Hata hivyo, na wazazi nao wanahitajika kuwasikiliza watoto wao, wasikie mawazo yao, kwani  huenda kwa elimu yao, na upeo wao wa kuchanganyika na watu wanaweza wakaja na njia mbadala,...hii ni kwa nia njema, kwani  maafa yakitokea ni athari za pande zote.

Ni mimi: emu-three

3 comments :

Nancy Msangi said...

Mmmh, nashindwa hata Ku comment bt nimejifunza mengi, km ndio story inaanza upo juu ndugu.

Nancy Msangi said...

Mmmh, nashindwa hata Ku comment bt nimejifunza mengi, km ndio story inaanza upo juu ndugu.

Nancy Msangi said...

Mmmh, hii ni elimu na burudani tujifunze jmn wote tunaopita hp