Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, November 29, 2012

Uchungu wa mwana Aujuaye ni mzazi-30
Saa kumi na moja, jioni ikaingia na jua likawa linatoa miale yake ya kuaga, na hiyo ndiyo saa waliyotabiriwa kuwa mfalme siku hiyo atatokezea huko miale inapotokea, na utakuwa muda wa jioni, kuisha kwa muongo wa shida, dhuluma na kuingia siku za matumaini, na neema. 

Hili kwa mzee Hasimu alishajiandaa nalo, kwani siku hiyo mtabiri akiwa anaelezea hayo alikuwepo na mzee mwenzake, Mzee mtaule....akaona hilo anaweza akalitengeneza;

Alichofanya mzee Hasimu, ni kumpanga kijana, akamsomesha, na jinsi gani afanye, akawatuma yeye na kikosi cha watu waaminfu,waende upande huo wa machweo ya jua, na muda ukifika wajitokeze na kikundi cha watu wake, huku wakipiga mbinja, au mruzi, na kutoa mlio maalumu wa ndege mmoja wanyemuheshimu sana,. 

Ndege huyo akilia wanasema anabashiria neema. Na kweli kijana wao na kundi la maaskari walielekea huko, na wakawa wanasubiri huo muda ufike.

Mzee Hasimu na wapambe wake walipoona sasa ni jioni ya saa kumni na moja, kwao wao, saa haikuwa makini sana, walichokuwa wakiangalia ni majira, na mwendo wa jua, na mwezi , na waliweza kusema muda huo ni saa ngapi kwa kutumia vitu hivyo vya asili bila hata ya kukosea. Kwahiyo Mzee Hasimu alipoangali jua, na kuona linaelekea kuzama, akawaambia wapambe wake muda umefika, waelekee njia panda.

Njia panda nis ehemu ya mpaka, kati ya koo hizi mbili kubwa, ukifika hapo utakuta njia inayoelekea eneo la mzee Hasimu, na nyingina inaelekea eneo la mzee Mteule, na njia ya kati kato inaelekea sehemu wanayoitambua kama sehemu takatifu. 

Sehemu hiyo na njia panda ndipo vikosi viwili vya mahasimu hawa vilikutana na kuchinjana kama mbuzi, hapo, hakuna aliyejali kuwa huyu ni mtoto wa baba mkubwa na mdogo, wote kila mmoja, alitaka kutwaa utawala, wakauana, na waliobakia walikuwa majeruhi ambao wengi wao walifariki baadaye. Kipindi hicho wazee hawa wawili ndio walikuwa majemedari wa vita kila mmoja upande wake.

Walijikuta wamebakia wawili, na wakaanza kupigana, walipigana mpaka wakaishiwa nguvu, kama vile jogoo, wanaopigana hadi kuishiwa nguvu, na hapohapo ndipo kikosi maalumu toka uko chimbukoni kwao kikafika, na kuwatenganisha.

Kila moja alichukuliwa upande wake, na baadaye wakakutanishwa na maiti zote zilipelekwa sehemu hiyo wanayoiita sehemu takatifu, ambapo ndipo askari wengi waliuwawa kabla hawajafikia hapo njia panda, sehemu hiyo ndiyo iliyokusanywa maiti wote na kila aliyebakia hai, ndugu na jamaa ambao hawakuwepo itani, walifika kuchukua maiti zao.

‘Haya jamani mliyoyataka ndio hayo, hawo ni ndigiu zenu, toka ni toke, baba mdogo na mkubwa, sasa hivi na maiti, ……naona sas amumesuuzika mioyo yenu, …je bado mnataka kuuana, ?’ wakaulizwa. 

Majeruhi ambao walikuwa wakigugumia maumivu, wakaguna, kila mmoja akitaka apate sehemu ya kujipumzisha ili aponyeshe kidonda chake, na wale ndugu waliofiwa na vijana wao, walikuwa wakitoa machozi ya huzuni. Hakuna aliyetaka vita tena, hakuna aliyetaka huo unaoitwa utawala, wa nini kama utawala ndio huo wa kuuana, hakuna amani. Na wengine walidiriki kusema kama ni hivyo ni bora warejee huko walipotoka.

Mzee Hasimu ambaye alikuwa kazingirwa na maaskari kutoka huko chimbukoni kwao, alikuwa katulia, akiuma meno kwa hasira, moyonu alikuwa na kisasi, na alitaka akiachiwa hapo akakusanye tena kikosi chake na kuja kummalizia hasimu wake, lakini kila alipotoka kuinua mguu alitulizwa.

‘Jemedari sikiliza, hivi wewe unataka nini zaidi, …unataka madaraka, unataka kumiliki ardhi , unataka kumiliki mifugo utajiri..au unataka nini cha zaidi,…kama unavitaka hivyo vyote utavipata, haina haja ya kumwaga damu tena, hakuna haja ya kuuna tena, kama mtauana wote, huo utajiri, utapatia wapi, na ni nani utamtawala, ..unataka utawale vilema?’ akaulizwa.

‘Sasa ni wakati wa kushikana mkono, vita  basi…kwanza mshikeni mikono, na pili watakuja wanasheria kuwatungia sheria itakayowatawala,…kila mmoja ni lazima aifuate sheria hiyo, tutawapa kipindi cha mpito, na kipindi hicho kila atakayekiuka hiyo sheria hakutakuwa na msamaha…

Wakapewa hiyo sheria, na sehemu hiyo ikawa inatawaliwa kijeshi na kikundi maalumu toka huko chimbukoni kwao. Kipindi hicho kilikuwa cha sheria ni msimemo, kila aliyekiuka sheria, adhabu kali ilitolewa, na adhabu kali ilikuwa kutupwa ziwani na kuliwa na mamba. Na hapo ndipo kulipotokea imani ya kuamini kuwa mamba ndiye mlaji wa wakosaji. Na imani hiyo ilikuwepo toka huko chimbukoni kwao.

Kipindi hicho kila raia alitakiwa kufanya kazi, kila ikifik asubuhi, maaskari walipita nyumba hadi nyumba kuhakikisha kuwa kila raia yupo kwenye kazi, hakuna kukaa makundi, vijana walitumiwa kwa kazi ngumu, ili wawe mashupavu, hakuna kulewa kipindi cha mchana,…kila mtu alitakiwa kutahamini kazi.

Kipindi cha mpito kilipopita, kila mtu akawa kajengeka na imani, imani ya kupenda kazi, imani  ya kutii sheria, na imani ya kuamini mambo yaliyoelekezwa na wazee wao kutii viongozi wao, na kila mmoja aliogopa kufanya makosa, kwani ukifanya kosa unatupiwa mamba, familia inatengwa, na kupelekwa kisiwa cha umauti.

‘Kipindi cha mpito kimekwisha sasa tunataka kuwakabidhi madaraak yenu, lakini kwa amsharti kuwa yule atakyekiuka sheria, ataadhibiwa,…na adhabu kubwa itakwua ikiwaandama viongozi, …kama kiongozi unatakiwa uwe mfano, uwe wa kwanza kutii sheria, …’wakapewa maagizo na sehemu hiyo ya kumbukumbu ya mauaji ya kivita ikawa ndio sehemu ya kukutania.

Baadaye akaja huyo mtabiri, na kuwaambia sehemu hiyo ni sehemu takataifu, kwani roho za mashujaa waliokufa kwenye vita huwa zinafiaka hapo kila siku, na nyingine bado zinadai haki, na haki ni utawala bora. Kila mmoja atii utawala, atii sheria, mkikiuka sheria, basi janga litawapata.

‘Yupo kiongozi wenu atakuja miaka kadhaa mbele, kiongozi huyo, ndiye ataibadili hi hali hapa na kuwaletea amendeleo ya kisasa. Kiongozi huyo atakutana ndiye atamuoa malikia. Malikia mbaye ujaji wake hapa utakuwa wa miujiza,….malikia huyo hatatokana na nyie, ila alikuwa ni damu yenu.

‘Malikia huyo akija ndiye ataolewa na kijana wenu shupavu,..kijana wenu ambaye ndiye atakuwa mfalme, mfalme wa taifa teule. Taifa ambalo litakuwa kuja taifa lenye nguvu, utajiri, aman na matumaini. Hakuna umwagaji damu tena, hakuna dhuluma, hakuna kuwaonea wanyonge.

Mfalme huyo atatoke  machweo ya jua, atakuja na usafiri wenu wa asili, akiwa na sura ya ajabu….sura ya ajabu kwa sababu ya mavazi yake, kwasababu ya kuwajibiak kwake, atakuwa kachoka, na pembeni yake atakuwa na majeruhi ya walioumia vitani…

‘Na huyo ndiye atakaye waleta taifa la amani, taifa teule, taifa lenye nidhamu, …lakini hayo yote yanahitaji subira, yanahitaji ujasiri, na hayatakuja kirahisi,….mkicheza mnaweza kuingia vitani tena, na kama kutatokea vita tena, taifa hili lote litaangamia.

‘Kumbeni siku hiyo, siku maalumu ya mavuono, ndipo atatokea huyo shujaa, siku hiyoo haitaki kumwagwa damu, siku hiyo, kila mmoja anatakiwa awe mkarimu kwa mwenzake, na kama unataka baraka, na kama una matatizo, na kama unaumwa, siku hiyo ndiyo siku ya kupona, lakini kuweza kufanikisha hayo, inahitaji kwanza ujisafishe moyo wako. Uwe huru, uwe na amani, na kam kuna watumwa, waachiwe wote..ili muwe na amani.

‘Tadhari siku hiyo, kama kutatokea kumwaga damu, laana kubwa itawaandama, ….kama kweli mnataka taifa teule, taifa la amani, …kama kweli mnataka maisha ya raha, kama kweli mnahitaji baraka kwenye familia zenu, vizazi vyenu, siku hiyo ndio siku maalumu, …..pendaneni, ondoeni chuki,….visasi, na kila mmoja amuone mwenzake ni ndugu yake. Na kila mmoja we tayari kupma mwenzake kila alichojaliwa nacho…

‘Mkifanya hivyo, mtafanikiwa, …kama bado moyo wako una uchoyo, hupendi mwenzako apate, kama ulivyo wewe, utakuwa hujafanikiwa siku hiyo. Na siku hiyo ikifika, na miali ya juoa ya kuzama ikiwa ainamulika kuashiria kuisha kwa siku, na kila mmoja akwa huru nafsini mwake,….akajaa upendo, huruma, unyenyekevu…basi pale kiwingu kitakapotanda kutokana na ugeni huo, kama una tatizo, kama una shida, omba, elezea shida zako,….hutaamini, zitaondoka zote kabla siku hiyo haijaisha…

‘Nyie ni ndugu, mkiangalia hapa mlikuja watoto wa babu ba bibi mmoja, ambaye alizaa watoto wengi, lakini kutoka kwa mama mmoja, ndio nyie kutokana na watoto hawo mkazaliwa, kizazi cha babu na bibi mmoja au sio” akauliza, kwani ni kweli watu hawo waliamua kuondoka huko walipokuwepo awali, wakidai kuwa babu yao alikuwa na eneo na inabidi waende wakaishi huko kwenye eneo la babu yao.

‘Sasa kwanini mpigeni, kwanini mjengeani visasi, chuki uchoyo na husuda. Babu yenu na bibi huko alipo kakasirika, roho yake haina amani,…na sasa anataka amani….ole wenu yule atakayekiuka…subirini mpate mtawala bora, ambaye ataweza kuwafikisha huko mnapopataka.

Mtabiri huyo aliongea mengi na kila aliloliongea siku hiyo liliweza kutokea moja baada ya jingine, lililokuwa limebakia ni hilo la kupatikana kiongozi ….mfalme wa taifa teule…na pale alipotokea huyo malikia mtarajiwa wakajua kuwa sasa , kile kipindi walichotabiriwa kimefika, kila mmoja akawa na hamu ya kukifiki hicho kipindi.

Kwa wale wenye pupa….kwa wale walioona siku zinakwenda tu, na huyo mtawala hapatikani, wakaanza kuzusha fitina,…na choko choko za hapa na pale zikaanza kutokea, na hata baadhi ya sheria zikaanza kupindishwa. …na ukoo mkubwa ukawa na haki kuliko ukoo mdogo, sheria ikawa inmsadia yule aliyenacho, na asiye nacho akawa ananyang’anywa hata kile kidogo alichojaliwa…

Leo hii koo mbili hasimu zimekutana , sio hizo koo mbili tu, hata zile zilizoonekana kama koo ndogo, zilizojengwa na familia hizo hizo, zilifika, zilifika sehemu ile ile waliyosuluhishwa , sehemu ile ile waliotabiriwa kuwa mfalme, atakuja, ….je ni kweli mfalme atatokea siku hiyo kama ilivyotabiriwa.

********

Malikia hakuwa na jinsi tena, ilibidi akubali, akainuka pale alipokuwa amekaa, na kunanza kutoka nje, huku akikanyaga maua, maua yaliyodondohwa ardini kutoka hapo nyumbani hadi sehemu sehemu takatifu, sehemu ambayo,atakabidhiwa majukumu ya umalikia, sehemu ambayo atakabidhiwa mume wake…..huenda mume mpya.

Alipowaza hilo kuwa huenda atakabidhiwa mume mpya, akasita kutembea, lakini kauli ya mzee, babu yake ikamsuta kuwa yeye hapo alipo sio malikia wa ukoo huo peke yake, ni malikia wa koo zote, na huko anapokwenda anakwenda kuwa mama wa taifa hilo….akajipa moyo..

‘Huenda nitamkuta mume wangu keshafika huko..’akasema na kutabasamu, na moyoni akakumbuka kuwa siku hiyo hapo ni siku maalumu, siku ya kuondokana na shida, siku ya kuomba shida zako, siku ambayo kila mtu anapata neema, lakini huwezi kupata neema na baraka bila kuwa huru kwenye nfasi yako, uondoe, chuki, uondoe husuda, uondoe uchoyo, uondoe akili ya kulipiza kisasi, uondokane na kila baya, ujawe na upendo, na amani….

Akasafisha moyo, na kujenga tabasamu, na moyoni akajawa na matumaini kuwa lolote linaweza kutokea, na sio kwa mapenzi yake, bali kwa yule aliye na nguvu, ambaye ndiye aliyeumba kila kitu, hana mfano ….hana uzaifu wowote wa kibadamu….mwenyezimungu, yeye alikuwa anajua hilo, …

Akaanza kutembea kutoka nje, akahesabu hatua moja, mbili, tatu..nne,..mara akasikia sauti ya ndege, akakumbuka….mume wake aliwahi kuwambia kuwa nudge huyo akilia ni ishara ya neema, baraka, na hutoke kweli, ….akasimama, na kueguza uso wake kutafuta wapi hiyo sauti ya ndege imetokea, akajikuta akikutana na miale ya jua linalozama…na kiwungi kikatanda, ….

Akakumbuka kuwa muda kama huo alitakiwa kuomba , alitakiwa kulilia hali yake,….akaomba, kuwa anataka mume wake arejee, ili wawe naye kwenye majukumu hayo mazito ya kuliongoza taifa kuwa taifa bora walilolitarajia wanachi wote…..

*********

Wakati hayo yakiendelea eneo hilo, mzee mteule, alikuwa kakaa na kundi la wazee wenzake, ambao bado walikuwa na imani kuwa kijana wao atakuja, na kila muda ulivyopita ndivyo kundi hilo la wazee lilivyozidi kupungua, kwani wengine walishakata tamaa na wakajua kuwa kijana huyo hayupi tena, na iliyobakia ni kusuburi huyo kijana mwingine, na yule aliyekata tamaa akawa anatoa udhuru, anaondoka, wakabakia wazee wachache sana.

Wale wazee wachache wakawa wanaongea ili kupoteza muda na kupena matumaini, na mmoja wao akasema;

‘Kama ni kijana wa mzee Hasim ndiye atakabidhiwa hayo madaraka, basi nahisi mambo yatakuwa bado, nahisi kuwa siku sio leo, pengine hili linatakiwa litokee mwakani, maana huyo kijana hana sifa zilizobashiriwa siku ile’akasema mzee mmoja ambaye alikuwepo siku hiyo mtabiri alipoongea.

‘Mbona malikia ana sifa zote zilizobashiriwa, kwanini kwa upande wa mfalme ishindikane…kuna tatizo hapa, inabidi tusubiri tuone, au mnasemaje wenzangu?’ akasema mzee mwingine.

‘Mara nyingi mambo kama haya ya wanaume ni magumu kuingia kwenye muafaka…ukizingatia huko tulipotoka, ujue kuwa kila ukoo unahisi huenda huyo kijana atatokea sehemu ya ukoo wake. Ni kweli malikia keshapatikana, lakini huenda pia asiwe ndio yeye, huenda kaletwa huyu kama majaribio tu, ili tujindae kwa malikia mtarajiwa’akasema mzee mwingine.

‘Mimi sikubaliani na hilo, malikia mtarajiwa ndio huyu huyu, tatizo ni mfalme,…kwasabaabu sifa zote za malikia mtarajia anazo huyo binti..je hamjaona karama zake, kwa baraka zake amekuwa akiwasaidia watu, mimi mwenyewe nilikuwa naumwa na kichwa, nilikuwa na matatizo ya kifamilia, mimi na mzee mwenzangu mke wangu tulikuwa kama chui na paka, ….mnakumbuka nilivyotaabika,…lakini siku tulipofika kwake, yote hayo yamekwisha…’akasema huyo mzee.

‘Kweli hata mimi….

Na wengi walitoa ushuhuda, kuwa huyo malikia aliweza mengi,mkono wake ulijaa baraka, akikushika kichwa, kama kichwa kilikuwa kikikuuma, kinapona, kama ulikuwa na msongo wa mawazo, yanayeyuka, na kama ulikuwa na shida, inapungua au kuondoak kabisa….kila mtu aliamini kuwa huyo kweli ni malikia matarajiwa.

‘Kama ndio yeye, mbona mume wake haonekani kuwa hivyo, na huyo aliyekuwa ana sifa zinazokubalika tunahisi , kuwa kauwawa na mamba’akasema mzee mwingine.

‘Hizo ni tuhuma,…hazina ukweli, tatizo ni kuwa tuhuma,na propaganda potofu, zinatawala sana akili za mwanadamu. Kitu kidogo kikitokea, kinachotangulizwa mbele na tuhuma, udaku na uzushi na propaganda potofu, …na hili huchukuliwa kwa kasi kubwa sana, kuliko ukweli wenyewe wa jambo. Na huenda hata ule ukweli ukija, unakuwa hauna nguvu tena, watu wanaweza hata wasiuamini!

‘Lakini haki, ukweli, ..vina nguvu, ni kama taa ndogo kwenye giza nene, hata kama, dhuluma, uzushi utagubika dunia, lakini tunaamini kuwa haki, ukweli utaleta nuru yake, hata kama miali yake itakuwa ni midogo, kutokana na propaganda potofu, lakini bado, tutaona nuru yake,….kama unavyoona nuru ya taa ndogo kwenye giza nene, haifichikia…’akasema Mzee Mteule ambaye alikuwa muda wote kainama akiwa kwenye dimbwi la mawazo.

Aliinuka na kuangalia nje, na miali ya kuchwa kwa jua ikawa inaonekana, ikammulika usoni…kuashiria sasa siku inakwisha, na usiku unataka kuingia, na kwa mtizamo huo, ina maana wenzao wameshashinda, akakuna kichwa na kugeuka kuwaangalia wenzake, akasema;

‘Kama imepangwa iwe hivyo, inabidi tukubali….kumbekeni kuwa siku ya leo sio siku ya visasi, sio siku ya tamaa ni siku ya kupendana, na kushirkiana, ….inabidi tutoke nje tukashirikiane na wenzetu, hata kama kijana wetu hatatokea leo, lakini nina imani yupo njiani….twendeni nje tukaungane na wenzetu..’akasema na akawa wa kwanza kuinua mguu kutoka nje,

Wenzake wakabakiwa wakiwa wameshangaa, hawakuamini hilo, wakaona kuwa mwenzao keshakata tamaa na anataka kuwasaliti, wakasita kuinuka, na mzee alipoona wenzake wamekaidi amri yake, kitu ambcaho hakijawahi kutokea, akageuka kuwaangalia, na usoni akatoa tabasamu na kusema;

‘Hamkumbuki jamani, kuwa siku kama ya leo, hatutakiwi kuwa na visasi, kinyongo, husuda na uchoyo,…siku kama ya leo inatakiwa tuwe na upendo , kushirikiana na kusahau tofauti zetu, ili kama una matatizo, una shida, unaumwa, uweze kupona,…kweli sisi hatuna hayo…kama kweli hatuna hayo huenda yameshatatuliwa, lakini hili la kumsubiri kijana wetu hatulioni kuwa ni tatizo…’akasema

Wenzake waliposikia hivyo, kwanza waliangaliana, na wote wakatingisha kichwa, na bila kusema neno wakainuka, na kwa pamoja wakaanza kutembea kuelekea nje wakiinua miguu yao kuanza kutoka, kwenda kukutana na wenzao huko nje, na hatua zao zilikuwa kama zile na askari, yaani kuinua mguu kwa pamoja na kushusha kwa pamoja na walipohesabu hatua tatu ya nne, sauti ya ndege ikasikaka kwa nje..

Ilikuwa sauti ya yule ndege, ndege wanayemuamini kuwa akitoa sauti hiyo anaashiria neema,…kila mmoja akageuza kichwa, kuangalia upande huo wa machweo ya jua ,wakajikuta wanamulikwa na miali ya jua linalokuchwa….kila mmoja akawa na hamasa ya kumona kijana , mfalame mtarajiwa akitokea huko, kwani ishara zote zimeshakamilika, sasa kwanini mfalme mtarajiwa asitokee…

Wazee wale wakaanza kutembea kuelekea sehemu ya makutano ili kukutana na wenzao, na walipokaribia sehemu hiyo, wakasikia sauti tena ya yule ndege, na safari hii sauti hiyo iliongezewa na sauti nyingine ya kutoka kwenye mdomo wa binadamu, wote wakageuka kuangalia huko sauti ilipotokea,

Kiwingu kikatanda, kwani miali ile ilizibwa, na kikundi cha watu waliokuwa wakija kutokea huko kunapochwea jua….watu kwa pamoja kwanza wakatoa macho yao kuelekea huko, kutizama ni nani huyo, na baadaye wakakumbuka, na kila mmoja akaihini na kuanza kulilia shida yake moyoni, na mojawapo ni kupta mtawala bora, kupata taifa bora, taifa teule, walilolitarajia…..

NB: Sijui nimeandika kile nilichokusudia, kwani sikupata muda wa kukupitia tena….lakini naona ipo pouwa, mnasemaje?.

WAZO LA LEO: Najua kila mmoja ana imani yake na anamuamini mungu wake, ...hata hivyo kuomba kwa mungu huyo unayemuamini hakuna tofauti. Ila ili tufanikiwe katika maombi yetu, kwani kila mmoja ana shida, kila mmoja ana tatizo lake, lakini ili tufanikiwe katika maombi yetu, kwanza tusafishe mioyo yetu, tuondoke uchafu uliogubika mioyo yetu, ya chuki, husuda, uchoyo, ubinafsi….na kuzijaza mioyo yetu kwa upendo, na huruma,…na kila lililojema,..na hapo tukiomba kwa mola wetu,..tutafanikiwa.

Ni mimi: emu-three

No comments :