Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, December 6, 2011

akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-58 Hitimisho-2
‘Rose umekuja huku Tanzania na mumeo, au upo peke yako?’ Maua alishituka pale alipoulizwa hilo swali na Inspekta wa polisi, ambaye walikutana naye akiwa maeneo ya hospitalini. Alikuwa kaongozana na mkewe ambaye naye alikuwa mja mzito. Alimsogelea Maua na kusaliamina anye kwa ksuhikana mikono. Maua aliitikia salamu ile bila kuonmyesha hisia zake za kustaajabu kwani hakumbuki kujuana na huyu askari.

‘Huyu ni mke wangu, wakati nikiwa kule Uganda nilikuwa naombea sana mkataba wangu uishe haraka, maana kama unavyomuona alivyo…aliponipa taarifa tu kuwa ana kiumbe tumboni nikasema sasa mambo yameiva, maana mke wangu akiwa mjamzito, namjua mwenyewe… naona hata wewe kama sikosei umeshapandishwa cheo, na wewe ni meneja kama sikosei maana gilo gauni linaeelzea mengi…’akamtizama Maua tumboni, Maua alikuwa hapendi hiyo hali, kwani wengi walishaanza kumsengenya kuwa akolewa akiwa na mimba..

Kwa ujumla hali ya tumbo ilikuwa haijajionyesha vyema, lakini kwa mzoefu angelimgundua ampema sana. Yeye kuja hapo hospitalini, ilikuwa sehemu ya mazoea yake anapijisikia vibaya, …akamtizama yule sakari akijiuliza amewahi kumuona wapi, na kwanini anamuita jina hilo! Na hata hajajua nini amjibu mara akaulizwa swali lililomfanya ashindwe kunyamaza kimiya…

‘Wewe una miezi mingapi vile? ‘akaulizwa swali hilo na Inspecta, huku akimwangalia Maua machoni. Na Maua akaangalia pembeni akitaka kujaribu kulikwepa hilo swali, kwani hakupenda kujitangaza, kihivyo ..
Maua akajivunga hakusema kitu akawa anajibaragua kutaka kuondoka pale alipokuwa kakaa, lakini kabla hajainuka, Inspekta akaja na kukaa naye karibu…

‘Docta Rose una miezi mingapi maana licha ya hilo gauni ulilovaa, lakini hali halisi haijifichi inaonekana umeshakuwa meneja au sio, kama sikosei?’akasema Inspekta kwa utani, na kumufanya Maua acheke bila kupenda, alicjheka kama njia ya kuondoa hali iliyojijenga moyoni mwake, …ilibidi acheke kwa kuitwa jina ambalo sio lake , na pili kuaitwa kuwa yeye ni docta. Toka lini akawa docta, wangelijua kuwa yeye na fani hiyo ni vitu viwili tofauti, licha ya kuwa alipenda kuifanya akzi hiyo wakati anasoma, lakini kutokana na kukosekana na mwalimu wa masomo hayo akajikuta anasomea masomo mengine kabisa.

‘Nina miezi mine, inakimbilia miezi mitano, ..’akasema Maua, huku akionyesha kushangaa, kwani anavyoongea huyu jamaa ni kama vile wanajuana . Maua alitaka kumuulizia huyu askari kuwa wamejuana wapi, lakini aliogopa kumuuliza lolote, kwani hakutaka kuongea na mtu kwa muda mrefu,…hapo alipo tu alikuwa anatafuta mwanya ainuke hapo na kukimbilia chumba cha kunawia akatapike, huwa akiongea na mtu, hasa mwanaume anajisikia vibaya, kichefuchefu…akajitahidi kujizua kwasababu alikuwa kawenye foleni ya kukutana na docta bingwa wa akina mama.

‘Mwenzako ana miezi mitano inakimbilia sita, ndio unamuona hivyo, hatupumui, inabidi niache kazi za ofisini kwa ajili yake, anataka kila mahala tuongozane naye, hata huku klinik, kanilazimisha twende sote, ila tuna miadi na huyu mtaalamu wa akina mama, ni mtu anajua kazi yake vyema, vipi wewe, nilizania kwa vile wewe ni dakitari, ungejitibie mwenyewe nyumbani…’akasema Inspekta kwa utani.
‘Kuhusu hilo swala la kuongozana na mkeo kwenye kiliniki wewe unaonaje hilo, mimi naona ndio vyema,ili kama kuna tataizo au ushauri muusikie pamoja…?’akasema Maua huku akijaribu kujigeuza mbali, lakini hakuweza…akavumilia.

‘Mwambie maana hilo swala limeleta mabishano yasiyo na maana…’akasema mke wa inspekta.

‘Lakini jitahidi ukamuone mume wako, maana nilikwenda mara moja kule, kwa ajili ya ile kesi ya maujai pale hotelini, nilimkta mumeo ana hali mbaya sana, natumai mnawasiliana, aua sio, kwa ujumla hali mumeo sio ya kurizisha..’akasema Inspekta.

‘Mume wangu yupi huyo, mbona sikuelewi wewe askari…’akasema Maua akizidi kushikwa na mshangao.

‘Rose unanishangaza kweli, mumeo yupi, kwani una waume wangapi, …lakini…mmh, name hapa nashikwa na wasiwasi kidogo, ….kule ulikuwa umejifanya mzungu, …tabia yako ya kule ilikuwa tofauti kabisa na ulivyo hapa sasa, nakuona umebadilika kweli au ndio mambo ya nyumbani ni nyumbani na kule ni kazini lazima ufanane na wazungu au sio. Umefikia wapi… , kwasababu nina mazunguzmo na wewe mazito, lazima nije nikutembelee, nina maswali machache ambayo najua ukiwa huku utanijibu vyema, ingawaje lile kundi tumeshalisambaratisha, kabisa, lakini wewe na mumeo mlihitajika mahakamani mkawa hamuonekani, imeleezwa kuwa wewe umeenda kusoma Ulaya na mumeo hajulikani wapi alipo, na alipoonekana tu akashikwa na kuwekwa ndani, walimtoa kwasababu ya afya yake mbaya…kuna mengi yametokea ndio maana nataka tuonane, unaishi wapi…? Akauliza Inspekta.

‘Sasa hivi ninaishi maeneo ya Mbezi, ….’akasema Maua na kumueelekeza huyo askari wapi anaishi, lakini hakupenda kabisa kukutana naye tena, kwani moyoni aliona akizoeana na hawa watu unaweza ukajikuta unaingia mahakamani au jela bila kupenda..

‘Mbezi ….Oooh, mbona mimi nami nina nyumba yangu huko ninahamia huko karibuni, nitafika kwenu,…nina mambo ya kikazi nataka tuongea na wewe kabla hujarudi huko kwenu, unatarajia kuondoka lini, maana kiukweli nenda ukamuone mumeo hali yake sio nzuri, …’akasema huku akimwangalia mke wake ambaye alikuwa kamshika mkono, kama kutaka kumwambia jambo. Maua alibakia kushangaa, na kujiuliza maswali mengi kichwani, ambayo hakuweza kabisa kuyaelewa, na akawa na hamu ya kutaka kumuuliza huyo askari , lakini kwa muda ule alikuwa kamgeukia mkewe kusikiliza nini anachoambiwa, na alipomaliza kuteta na mkewe akamgeukia Maua na kuanza kuongea kabla Maua hajafungua mdomo wake kumuuliza lolote..

‘Kweli Rose umebadilika sana na mabadiliko hayo ni ya haraka kweli, mpaka inanitia wasiwasi kuwa nimekufananisha nini, lakini nina uhakika kua wewe ni Rose, siwezi kukusahau popote pale..na ….;akawa anaongea huyo askari lakini kabla hajaongea zaidi wakasikia jina likiitwa, na kumbe ndio jina la mkewe..

‘Basi Rose nitakuja nyumbani, ….akasema Inspekta akimsaidia mkewe kusimama.

Mkewe akainuka , alionekana ujauito ule ulikuwa umemchosha sana, na kutokana na unene wa mwili tumbo lilionekan kubwa kama vile ana mapacha. Inspekta akainuka naye huku akiomba tafadhali kwa Maua, kuwa wanakwenda kumuona docta, kwahiyo mazungumzo yakakatishwa bila Maua kujua nini kinachoendelea.

Maua akabakia akiwaza mengi, kwanza hilo jina la Rose limetoka wapi, anakumbuka kuitwa jina hilo na Mhuja, wakati wakitaniana …huwa katika maongezi yake alipenda kumuita `Maua , Rose wangu,…’ lakini hajawahi kuitwa na mtu mwingine…oooh, baadaye akakumbuk ipo siku shangazi yake aliwahi kumuita hilo jina na kusema `Maua , Rose, oooh, kwakweli nimejisahau sana…’

‘Kwanini unite Rose, hilo sio jina langu shangazi, mimi sipendi kuitwa majina ambayo siyo yangu..’akalalamika Maua siku hiyo alipoitwa jina hilo na shangazi yake.

‘Ndio maana nikakuambia nimejisahau….samahani maana na wewe huna dogo…’akasema shanagzi yake.na

*****


`Maua umerudi toka kliniki hebu niambie mambo yapo shwari,..’akauliza shangazi huku akimsogelea na kumshika tumbo. Maua akajifanya kama vile hataki kushikwa hivyo, lakini cha ajabu, ni kuwa alikuwa akiona raha kuwa na shangazi yake, lakini sio kuwa na mumewe, wakati mwingine anampigia simu shangazi yake aache shughuli zake aje wakae pamoja.

‘Yapo shwari ila nina mazunguzmo na wewe, ….mazito sana na safari hii sitaki mambo ya kufichana, maana hilo jina ninaloitwa sasa hivi nahisi lina jambo…’akasema Maua.

‘Jina gani tena, …hebu niambie mpenzi, kabla mumeo hajaja, isije ikaleta kisirani, sipendi muwe mnazozana na mume wako, japo kuwa najua huko kuzozaan kwenu kunasababishwa na hiyo mimba, sijui ndio dume linakuja nini, na ningeshauri umuite Mhuja

‘Eti nini shanagzi kwanini unasema hivyo,…?’akauliza Maua kwa kushangaa, kwani kweli akilini mwake alishajiwa na wazo kama hilo kuwa akijifungua mtoto wa kiume atamuita jina la Mhuja, kuonyesha jinsi gani alivyompenda mume wake, na hapo mawazo ya mume wake yakamjia, alimkumbuka sana, licha ya kujitahidi kumuondoa mawazoni.


‘Usipoteze lengo, nina mazunguzmo mengine ya kuhus hilo jina la Rose, maana ulishawahi kuniita hilo jina na sasa leo tena nimeitwa jina kaam hilo na polisi, na tena hakuishia hapo aliniita Docta Rose, toka lini nikawa docta mimi, lazima kuna jambo hapo, na najua wewe unalijua zaidi yangu….’akasema Maua.

‘Wewe mtoto wewee mbona unataka kunileeta balaa, mambo hayo ya zamani yalishaisha, na …hapana unasema nani kakuita hilo jina, polisi gani huyo…

‘Kuna polisi mmoja, nimesikia watu wakimuita Inspekta, mimi nawajulia wapi hawo watu, kwanza mimi na polisi hatuivani, siwapendi hawa watu…’akasema Maua.

‘Unawapenda, sema kwa vile ni mwanaume, na wewe kimimba chako hakitaki wanaume sijui atakuwa dume …atajuwa mhuja huyo..hahahah, hebu niambie anasema anaishi wapi aua nafanya wapi huyo polisi…?’akauliza shangazi

‘Kasema amejenga huku huku na anahamia karibuni…’akasema Maua.

‘Aaah, nimeshamfahamu, huyo ndiye tulizozaan naye kwenye kiwanja chake, kajenga karibu na mimi, akapitisha ukuta wake karibu na eneo langu, halafu analeta mambo yake ya kiaskari, nikamwambia weee, achana na mimi siogopi cha polisi au nani mbele ya haki yangu, alibomoa ukuta wake bila kupenda…’akasema shangazi mtu.

‘Shangazi na wewe, ina maana huogopi polisi, ….tena anaonekana ni mtu ana cheo kikubwa sana…’akasema Maua.

‘Mbele ya haki yako hutakiwii kumuogopa mtu hata kama ni Raisi unapambana naye maana wengine wanataka kutumia vyeo vyao kunyonya wanyonge, lakini sio kwangu, tutapambana hadi mahakamani…haya niambie mliongea nini mpaka akakuita Rose…?’akauliza shangazi.

‘Tulikuwa kwenye foleni ya kumuona dakitari, tumekaa kwenye viti, mara nikamuona huyo polisi akija na kukaa karibu nami, akadai kuwa namba yao ipo mbele yangu, na aliponionyesha hiyo namba ambayo kweli ilikuwa ya mbele yetu, nikawapisha, nikijua kuwa wanatumia ubabe wao wa kipolisi, na baadaye akaja mwanamke mmoja mnene mjamzito na kukaa karibu naye, na kunifanya nirudishwe nyuma tena, kumbe ni mke wake, na amechoka, utafikiri kafika kujifungua, kumbe ndio bado ana miezi mitano tu, je akifikia miezi minane ,au hiyo tisa itakuwaje, jamani sisi wanawake tuna mitihani mikubwa, na kwasababau yupo na mumewe basi anadeka kuliko maelezo, maana mara amuegemee mume wake, mara alale mapajani mwa mume wake, utafikiri yeye pake yake ndiye mwenye mume…’akasema Maua.

‘Sasa kwanini wewe hukwenda na mume wako kliniki ukamdekea kama huyo, siku hizi ni mambo ya kwenda hospitali au kliniki ni lazima uwe pamoja na wanaume zenu, sio sisi , zamani ukienda kliniki unakwenda peke yako,na mwanaume haruhusiwi kufika wodi au sehemu za wanawake, lakini hizi mnaiga wazungu, …siku nyingine mwambie Maneno mwende naye…

‘Eti nini, hapana, sitaki kabisa kuongozana na huyo mwanaume,…’ akasema Maua huku akimuwaza Mhuja, na kilichomshangaza ni kuwa tangu aamuke asubuhi, amekuwa akimuwaza Mhuja, na kujuta kwanini siku ile hakuingiwa na ujasiri wa kumwambia asiondoke, lakini kwa vile hisia zake na wanume zimekuwa hazioani, siku aliomba ile siku iishe haraka, hata kufungishwa harusi kwenyewe alikuona kama mwaka, alizindukana kwenye lindi la mawazo, vigelegele vikitanda hewani, keshakuwa mke wa Maneno, na Mhuja hajulikani alipo. Alikumbuka baadaye alimuita shangazi yake na kumuuliza kuwa Mhuja yupo wapi, …

‘Unasema nini, eti Mhuja, hebu achana naye, kwanza usiseme lolote kuhusu huyo mtu, tmekubaliana hilo…hayupo na hatarudi tena,…wewe sasa mume wako ni Maneno, unafikiri ungelisemaje kama angelikuwepo hapa, hiyo mimba ungembambikia, kila kitu hupangwa na Mungum, huyo sasa msahau….uinasikia…’alisema shangazi yake kwa ukali.

Hapo Maua akakumbuka jisni isiku ile ilivyokuwa, kwani hata kile kisa hakikuweza kuelezewa chote, hakujua nini kilitokea baada ya pale, akakumbuka jinsi Mhuja aliposhikwa na butwaa pale alipomuuliza swali;

‘Maua naona shangazi anafoka huko nje, na kisa hiki sijakimalizia, nikuuulize swali moja, je una uhakika nah ii ndoa, nina maana kuwa je una mpenda kweli Maneno, rafiki yangu awe mmeo badili yangu, na ikizingatiwa kuwa umeniona kuwa nipo hai,,naomba unijibu haraka…?’ akauliza Mhuja, huku akiangalia saa, na nje shangazi alikuwa akiita kwa hasira.

Maua alikuwa akijsikia vibaya, alikuwa akitamani atoke mle ndani na kukimbia, alishangaa, mume aliyempenda kwa moyo wake wote, leo hii yupo mbele yake, lakini hataki hata kumuona, sio yeye tu, hataki sura inayoitwa mwanaume, anaijsikia vibaya kutapika, na alitamani kumwambia Mhuja aondoke haraka mle ndani…

‘Maua muda unakwisha, na kama jibu ndio kuwa umeamua kuolewa na Maneno, nakuomba sana, usije ukamwambia Maneno kuwa uliwahi kuiniona, mpaka siku nitakapotokea tena mwenyewe, kama kweli nitatokea tena, kwasababu yule ni rafiki yangu, hatakubali kukuoa kama atajua nipo, na inaweza ikageuka uadui mkubwa…huyo ni rafiki yangu wa damu, sipendi tukosane…, ninachotaka kwako ni wewe kujisikia huru, mapenzi yangu kwako ni wewe uwe huru, sitaki nikuuzi kwa lolote lile, …’akasema Mhuja kwa sauti ya huzuni.

‘Sikia Maua nipo tayari kuumia kwa ajili yako,…ni kweli nitaumia sana, lakini ni heri niumie mimi kuliko kukuumiza wewe, je unampenda Maneno awe mume wako, sihitaji sababu jibu ni ndio au hapana…’akauliza tena Mhuja, lakini Maua likuwa kimiya, hakuwa anajua anaulizwa nini, kichwa kilishaanza kumzunguka, ilibakia kidogo kudondoka , …ashukuru mnungu kuwa alipojisikia hali mbaya alikimbilia kukaa kwenye sofa, na kwa muda huo kichwa alikuwa kakiegemeza kwenye sofa, na huku kaangalia juu,…na kabla hajasema lolote, mlango ukagongwa na shangazi akaingia na kusema;

‘Wameshakuja waoaji, …’akasema shangazi akiwa keshafungua mlango, na kukawa na kukura kakara, ambazo Maua hakuweza kujua nini kilitokea pale mlangoni, kwani hauwa yeye, akili ilikuwa imesimama, akawa kama mtu aliyepoteza fahamu, kwani alidondokea pale kwenye sofa na kujilaza, na hakuna aliyejua kuwa hali yake imekuwa hivyo, akawa kajilaza pale kwenye sofa kwa muda,alitaka kumwambia shangazi yake ahirishe hiyo harusi maana hali yake sio njema, lakini hakuweza, kauli ilikwisha kabisa, mdomo haufunguki, na alishitukia anaulizwa swali kuwa umemkubali Maneno awe mume wako, na kwa vile hakutaka zaidi akaitikia ndio, ilimradi, watu waondoke na abakie huru,…vikatanda vigelegele, anashitukia keshakuwa mke wa Maneno.

amekuwa sitaki kabisa, bora kama nikwenda na mtu twende pamoja na wewe, lakini sio na Maneno,pale tu alipokuwa akiniongeelsha Yule askari mwanaume nilitamani nimtapikie, sijui kwanini nawachukia wanaume kiasi hicho…sijui kwanini. Sasa shangazi usibadili mada, nilikuuliza swali,…. hebu niambie hilo jina la Rose limetoka wapi?’akauliza Maua

‘Sikiliza Maua, wakati mwingine hutakiwi ujue kila kitu, mengine yanatokana na historia ambayo haitakiwi kujulikana, na mimi siwezi kabisa kujua kwanini huyo askari akuite Rose , inawezekana ni kwasababu yote ni Maua, sikiliza Maua, jambo jema ni wewe kutulia ujifungue salama, sipendi mambo mengine yaingilia kati, hayo hayakuhusu kabisa, na huna haja ya kuyajua, unanisikia vyema…’akasema Shangazi.

‘Hapana usiponiambia kutachimbika, na kutokana na maelezo yako inaonyesha kabisa kuwa hilo jina lina sababu maalumu, kama ulivyosema sitakiwi kuyajua, kwanini sitakiwi kuyajua na wakati mnaniita jina hilo ambalo sio langu, na kama huniambii nitampigia simu baba ajae aniambie, maana sipendi kuitwa majina ambayo siyo yangu na kumbe kuna jambo limejificha, niambie shangazi sasa hivi, kabla sijaanza kutapika…’Kabla Maua hajamaliza kuongea kengele ya mlangoni ikalia,na Maua akashikilia mdomoni, kuonyesha kuwa anasikia kichefu chefu, na kukimbilia chumba cha kunawia…

Shangazi akachungulia nje, kwa kupitia dirishani, wote kwa muda ule, ingawaje sio saa za kawaida, kwa Maneno kurudi nyumbani, lakini walikuwa wakijua hivyo kuwa atakuwa ni Maneno aliyekuja …

‘Huyu sio mume wako, ….wala usijisikie vibaya, nimeona gari tofauti limeimgia getini, na kama sikosei atakuwa. ooh,… mungu wangu…mbona mambo leo…’akasema shangazi mtu huku akionyesha uso wa wasiwasi na kumfanya Maua naye aje kuchungulia dirishani...

NB: Wapendwa nitajitahidi kuwa nanyi kila inapowezekana, hasa kwa kupita internet cafe, ikizingatia kuwa sasa tupo katika hitimisho. Naombeni maoni yenu, ili kama nimesahau kituu niweze kukiweka katika sehemu hii ya hitimisho. Ama kuhusu lile tukio la kule hotelini, linakuja, lipo ...na muhusika atakayetuelezea yupo nchini, ...TUPO PAMOJA.

Ni mimi: emu-three

1 comment :

samira said...

nashkuru m3 kuwa na sisi vipi mauwa alimkataa mhuja akaolewa na maneno au walilazimisha hapa kidogo pame nichanganya nijuzu
na rose imekuwaje nahisi kama utachanganya kuwa sehemu ya hitimisho itafahamika dear
thank you mungu yupo na wewe ndo dunia ilivyo