Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, August 15, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-15‘Nilijua kabisa kuwa huyu mtu mnaye mnajaribu kumficha, na hili limebainisha hisia zangu za siku nyingi kuwa wewe unamahusiano na hawa wahaini, …sijui mtaniambia nini cha kunishawishi vinginevyo, …’ akasema askari yule huku kashikilia silaha yake imara mkononi, huku kichwani akikumbuka maelekezo kutoka kwa mkubwa wake, kuwa huyo jamaa kama watamkuta wawe makini sana, kwani ni mtaalamu , ni komandoo,…alikiweka kidole chake kwenye kifyatulio cha risasi kuzimimina risasai wakato wowote, lakini alitaka kuthibitisha kuwa na yeye ni shujaa, alitaka kuthibitisha kuwa kazi anaijua na huenda akapandishwa cheo kwa ujasiri huo, na kwa hilo anaweza akamshawishi mpenzi wake aliyemkimbia,kwa kudai hana lolote, hana pesa na mshahara wake ni mdogo, eti kwasababu yeye anafanya kazi na analipwa mshara mkubwa kuliko yeye, na amekuwa akimringia sana kuwa yeye si lolote si chochote, sasa atakuwa chochote...
‘Sikiliza afande, musitake kukimbilia mambo kwa pupa, kabla hamjafanya uchunguzi wa kutosha, nikuulize swali, je unamfahamu huyo mtu mnayemtafuta kwa sura, yaani uliwahi kumuona kabla, maana watu wanafanana, watu wanaweza wakafanana kitabia, na hiyo sababu ya kuwa huyo mnayemtafuta alikuwa kachanganyikiwa , kapoteza kumbukumbu…mbona pale hospitalini wanakuja wengi wa namna hiyo, na hata sasa hivi wapo wengine mle, kwanini mnamsakama huyu…?’ akaongea Docta Adam, na kumuuliza yule Afande.
‘Kwanini mnamsakama huyo…! Huoni kuwa umeshajijibu swali langu, …watu wenye matatizo kama hayo wapo wengi, ….hahaha docta unaongea kama hujasoma bwana, …watu kwa ujumla wapo wengi, na hatuwezi kuwakamata wote , eti kwa kuwa wanafanana sawa na mhalifu tuliyeambiwa, tunamkamata mhalifu kwasababu tumefanya uchunguzi wa kina, na kuhakikisha kuwa huyo ndiye mshukiwa, ….sasa hatutaki porojo, tumekuja kwa kazi moja, kumkamata huyo mtu na kumfikisha kituoni, mengine yatafuata baadaye…’ akasema yule askari bado akiwa kamuelekezea bunduki yule jamaa wanayetaka kumkamata na wenzake wakiwa wanafanya hivyohivyo.
‘Tatizo ni kuwa hatukatai mumkamate huyu jamaa kama mnavyodai ni mshukiwa, lakini taratibu zenu ndizo zinazotutia wasiwasi, mkimkamata mtu hata kabla hamjathibitisha kuwa ni mhalafu mnaanza kumuazibu, mnampiga, mnamtesa, kiasi kwamba huyo mshukiwa anakuwa hana kauli ya kujitetea, na anaweza akakubali kosa, hata kama hajalifanya ili aondokane na maumivu ya kuteswa, na hili linakwenda kinyume na haki za binadamu…’ akasema Rose.
‘Oooh, mnajua nyinyi sasa mnataka kutufundisha kazi, sisi hatujaja hapa kujadiliana na nyinyi, sisi sio wanasiasa, sisi ni watendaji, na amri ikitolewa, haina mjadala, hayo ya kuteswa, sijui kukiuka haki za binadamu, …hayana nafasi kwasasa, …hapa ni kazi kwa kwenda mbele, haya, mikono juu, na wote mpo chini ya ulizi kama nilivyosema awali, wote inabidi mfikishwe mbele ya …..pi-la-to….hahahaha, docta nimekuwa na usongo na wewe…leo nimekupata….ok, funga pingu wote…huyu sio yule mnayependa kumchezea, hapa mumefika, lazima mfike kituoni…lazima mmmmh….’ Akaongea huku kaelekeza mtutu wa bunduki kwa huyo jamaa wanayemshuku, alikuwa habandui macho kwake, anachofanya ni kuizungushazungusha ile bunduki katika muelekeo wa mtu mmoja, na kuhakikisha kuwa ikibidi kufyatua risasi hakosi shabaha yake, akilini akiwa anaomba mungu huyu anayeitwa komandoo asije akaanza kashikashi zake.
Wenzake kwa tahadhari walimfunga yule jamaa pingu, na hata docta Adam na Rose walifunga pingu pia na wakatolewa nje waliwa wameshikiwa bunduki kwa nyuma na kuingiza ndani ya landrover, ambayo ilikuwa na king’ora ili kuhakikisha usalama wa barabarani na kuwa hakuna sehemu yoyote watasimama…ilikuwa sio mbali sana na ilipo kambi yao, lakini walihakikisha tahadhari zote zimechukuliwa na moja kwa moja wakafikishwa kambini kwa hawo maasakri, na hata vile docta Adam, alipojaribu kujijittea kuwa kwanini kama wao ni wahalifu hawafikishwi kituo cha polisi lakini wanapelekwa kwenye kambi ya kijeshi, hakusikilizwa,…jamaa walikuwa kama bubu, hawaongei tena,hadi walipofika hapo kambini, walipokelewa kama mpira wa kona,…mara ghfla vipigo vikaanza, simama, ruka tembea, hadi wakafikishwa mbele ya afande wao aliyewatuma.
‘Bosi kazi nimeifanya…kama ulivyoniagiza , huyu hapa mhalfu tuliyekuwa tukimtafuta pamoja na watu waliokuwa wakimuhifadhi...’akasema yule askari aliyewakamata.
‘Oooh, kazi nzuri …koplo,…hiyo ndiyo tunaihitaji, na huo ulikuwa moja ya mitihani yako, …hilo utalishuhudia baadaye…kwani umeweza kumkamata komandoo,….siamini eti wanamuita komandoo, mhalifu mkubwa huyu, umemkamata bila mapaigano, bila kuumizwa, nakuhakikishia umefanya kazi kubwa sana, sasa….mmmh, hata docta amerudishwa hapa tena, nilijua huyu anajambo, na mmm, na huyu mrembo docta mrembo, …sawa hawa wawili wapeleke mahala pao, sisi kazi yetu ni huyu anayeitwa komandoo, mpeleke kule, mahala pake,……’ akasema huku akimwangalia Rose kwa macho ya aina yake ..
Mara yule wanayemuita Komandoo akavutwa kwa nje, na kabla hajajitetea, akajikuta yupo chini, akainuliwa …ilikuwa dakika tano, alikuwa kalegea, na hata alipofikishwa huko mahabusu alikuwa hajiwezi, na kila mara alipotaka kutamka neno alikutwa akifungwa mdomo kwa kofi, na ….
‘Hatutaki kufanya makosa, nasikilia hata kauli yako ni silaha, kwahiyo utafunga mdomo wao na utaongea tu pale utakapoulizwa, wewe sikiliza maagizo yetu, ukiambiwa kaa, unakaa mara moja, simama, unasimama…wewe si komandoo bwana, unajua ziaid yetu, nasikia ukipandisha unaweza kumuinua tembo, …sasa tuone huyu shetani wako yupoje..haya pandisha basi hayo mashetani tukuone, au mpaka tukupigie ngoma, afande mtukutu, komandoo anataka kupandisha, lakini mpaka apigiwe ngoma, piga ngoma…’ basi ikawa kama mchezo wa kuigiza, wanapiga ngoma, na kuimba, `shetani panda..shetani panda..’ na wakimuona huyo jamaa akitikisika tu, anapata kipigo hadi analala chini…
******
Huku nyuma, Docta Adamu, na Rose walifikishwa kwa mkuu, ambaye alikuwa Kapteni wa zamu, na akapewa taarifa na Luteni wake, kuwa vijana waliotumwa kumkamata yule mtu wamefanya kazi yao vyema sana, na huyo mtu yupo mikononi mwao…
‘Kweli, kazi nzuri, unajua bado nina mashaka, aah, labda kwa vile atakuwa hajapandisha, nasikia kama hajapandisha mnaweza mkamkamata bila matatizo, kazi nzuri Luteni, kwasababu huyu mtu amekuwa gumzo, amekuwa anatupa taabu, ila mimi sijaamini kuwa kweli ndiyo yeye, kwasababu namjua sana,ingawaje sikuwahi kuwa karibu naye kipindi hicho, namjua kwa kumsikia, kama ndiyo yeye, basi lile tatizo limekwisha atakuwa kabadilika sana, ila huyu kama ndiyo yeye au siyo yeye anatakiwa kuwa katika mikono yetu hadi tutakapohakikisha kuwa yeye ni nani…, kwasababu kama siyo yeye anaweza akawa kachero, na keshaingia kambini kwetu, lazima azibitiwe…’ akasema Kapteni wa zamu
‘Afande atakuwa ndiyo yeye, kwasababu mimi ndiye niliyeletewa huyu mtu akiwa kaokotwa ufukweni, kwa kweli nilipomkagua nikaona kabisa hana uhai, nikaona hatuwezi kuchukua maiti…na kila mtu aliyeulizwa maeneo yale alidai hamjui,…kwasababu alionekana ni maiti nikaona ngoja tumepeleka kwa wataalamu, kwenye hospitali ya karibu wakampokea,…kwakweli pamoja na makosa yao, lakini nawasifu sana kituo hiki cha Docta Adam, na mrembo Rose…’ akamgeukia Rose, na kutabasamu, halafu akakumbuka yupo kwa bosi wake akakunja uso na kuonyesha ukakamavu…
‘Hawa wataalamu bwana wakasema ngoja kwanza wamuingize kwenye vipimo,…baadaye tunasikia kuwa huyu mtu ni mzima, sikuamini…sikuamini, lakini baadaye, baada ya kusikia sifa zake, kuwa anatabia kama wanavyoita `eti ana mshetani’, …nikakubali..maana niliwahi kukutana na watu kama hawa, wenye hayo yaitwayo mashetani, mimi siyaamini sana….siui kwanini, lakini maajabu yake ni makubwa, mtu mwenye hayo matatizo anaweza akazimia siku tatu…mnajua kuwa huyo mtu kafa, lakini baadaye anaibuka kiajabu…na…huyu..’ akawa anaongea huku akionyesha kuwa ana furaha kubwa sana.
‘Sawa, ilimradi yupo mikononi mwetu, tuhakikishe kuwa tunapata ukweli wote, hakikisha anazungumza kila kitu, kabla ya yote ngoja niwasiliane na wenzangu, kwanza kazi ya huyo mtu ipo mikononi mwa mkuu mwenyewe, kwahiyo ngoja niwasiliane na afande-Meja, yeye atajua jinsi ya kuufikisha huo ujumbe, ila nawaomba mumweke kwa tahadhari, hakikisheni ana ulize wa kutosha, ….’ Amri ikatolewa na huyo askari akaondoka, wakabakia docta Adamu na Rose wakisubiri nini kinachoendelea.
‘Docta Adam, nimesikia sana sifa zako, jinsi gani unavyosaidia wagonjwa, nimesikia sana udhaifu wako pia kuwa unawakumbatia wahalafu, hilo sikulaumu kwani wewe ni docta,hutakiwi kuangalai ni nani unayemtibia,lakini kuna kitu kinaitwa `utaifa’….taifa sasa hivi lipo kwenye vita, kwahiyo tunaposema mtu fulani ni mhalifu, basi ujue ni adui wa taifa, na adui wa taifa ana sehemu yake…huyu jamaa kwa vile tuligundua baadaye kuwa ndiye tunayemtafuta, vinginevyo angeishia kwenye hospitali zetu…’ akasema huyo askari. Na kichwani docta Adamu akasema kimoyomyo, `na kama angekuwa mikononi mwenuu angakuwa sasa hivi maiti…’
‘sidhani kuwa hatuna wataalamu, tuna madocta bingwa , sisi kama jesho tunajitosheleza, na labda wakati mwingine tunapata shida ya vifaa vya kitaalamu, lakini hilo linafanyiwa kazi..kwahiyo kama angefikishwa hapa moja kwa moja, angafanyiwa huduma zote. Jeshi ni sehemu ya usalama, na…ninauhakika kama ngekuwa mikononi mwetu angelikuwa kashapona, …kwasababu nilishangaa kila watu wakija kwako wanadai kuwa hajazindukana…na ndipo tukaanza uchunguzi na tukagundua kwua huyo mtu alishazindukana, …mkawa namkinga, ama kwa kutojua au kwa ujanja ujana wa huyo jamaa, kwani jamaa huyo ni mjanja…’akawa anaongea na mara sauti ya simu yake ikasikiak ikiita.
‘Roja…three four, three four…nimekupata…ndege yupo tunduni, …., sawa, over..’ akakata simu na kuwageukia Adamu n Rose.
‘Sasa sijui niwasaidienije , maana sasa mumeiweka pabaya, siui itakuwaje, maana hata mkuu wa kikosi anataka kuwaona,…na sijui…’ akaangalia nje, na wakati huo gari likawa limesimama nje, na akaja askari mmoja na kutoa salamu zao na baadaye akasema gari lipo tayari.
‘Twendeni ofisini, maana hapa sio sehemu ya maongezi..’ akawaongoza Docta Adam na Rose kwenye gari na kuondoka hado sehemu inayoitwa `utawala’
Walipofika hapo wakakabidhiwa kwa mhusika na kuandikishwa maelezo yao, halafu wakaambiwa wasubiri kwenye ofisi mojawapo ambapo baadaye alikuja askari mmoja akiwa na cheo cha Meja, akawauliz amaswali mengi, kuwa walimjuaje huyo mtu, na maswali mengi, ambayo yaliwekwa kwenye kumbukumbu, halafu, wakaambiwa waweke alama za vidole kwenye yale maelezo.
‘Samani sana kwa haya , lakini ndio utendaji wetu, na lazima kila kitu kiende kitaalamu,na tutahakikisha haki inafanyika, na sioni kwa nini muendelee kushikiliwa , ngoja niongee na wahusika, na …mtaruhusiwa, ila mnaweza kuitwa , ..lakini sio hapa, mtaitwa kituo cha polisi, kwani nyie ni raia, hatuhusiki na nyie, labda ibainike kuwa mnahusiana na wahaini hawo…na hata hivyo bado mtashitakiwa uraiani, sio hapa…’akasema na kuondoka na baada ya muda akaja askari mwingine na kuwaambia kuwa wameruhusiwa kuondoka ,wakachukulia na gari hadi nje ya kambi.
‘Bosi, mbona hawa watu wantushangaza, ….mimi nahisi watakuwa hawan uhakika na hilo kuwa huyu jamaa ndiye wanamtafuta…na hili linanitia uchungu zana, kuwa huyo jamaa atapigika, na wakishagundua atakuwa katika hali mbaya sana, kwanza ni mgonjwa, hajapona vyema,bado akili yake haipo sawa, sasa anapata vipigo..na hivyo vipigo vitazidi kumdidimiza ki-akili….’ Akasema Rose kwa wasiwasi.
‘Hilo nalijua, hilo nimekuwa nikiwaza , lakini baadaye nikaona hatuna jinsi, sisi tumetimiza wajibu wetu,na tumenawa mikono, ingawaje hawa jamaa ndio hivyo wameshafungu akesi kuwa tumemficha mhalafu, lakini hilo tutalimaliza kisheria, halina hoja, hoja ni kuwa tuanpoteza muda mwingi katika mambo ambayo sio kazi yetu, elewa wagonjwa wameshaanza kulalamika kuwa huduma zetu zinazorota, na hospitalini yetu inajitegemea, …hili linanipa shida sana..lakini,..ninataka ufanya maamuzi makubwa, nataka ubadili utendaji…’ akasema Docta Adam.
Docta Rose aliondoka kurudi kwake akiwa na mawazo mengi, alimuwaza sana huyo jamaa anayeshukiwa kuwa ni mpiganaji, yeye kila anapomuwaza alimuona tofauti na wanavyomfikiria na alishangaa kwanini kila anapojaribu kumuondoa akilini anashindwa, anakuwa kama sehemu ya ubongo wake…akasema angalau sasa kwa vile yupo mikononi mwao, labda ataweza kumuondoa akilini, lakini haikuwa hivyo, kwani hata ndoto akawa anamuota yeye!
Siku zikawa zinakwenda, miezi ikapita na hata watu wakaanza kusahau kuwa kulikuwa na mtu kama huyo na haikujulikana kabisa huko jeshini, kambini kunatokea nini. Siku hiyo Rose alikuwa kalala mapema na mara ikamjia ndoto moja ya kutisha…ndoyo hiyo alimuota mtu anayemfahamu…lakini kwenye ile ndoto alishindwa kumtafsiri vyema ni mtu gani, alimuota huyo jamaa akizama kwenye ziwa, na anapiga kelele ya kuomba msaada,…wenzake aliokuwa nao kama Docta Adam, walikuwa wanamdharau na hawakutaka kumsaidia huyo mtu, yeye akaamua kujitosa kwenye maji kuogelea kwenda kumuokoa, lakini kila alivyojaribu kumkaribia, alishindwa, na kwa mbali akaona mijitu ya kutisha ikimjia kutaka kummeza, mijitu hiyo ilikuwa na midomo kama ya mamba, lakini kiwiliwili cha mtu, yenyewe ilikuwa ikitembea juu ya maji bila kuzama, na kabla haijamkaribia akazindukana toka usingizini na hakuweza kulala tena hadi asubuhi yake.
Alipoamuka alijikuta akihema kwa nguvu , moyo ulikuwa ukimwenda mmbio kiasi kwamba akawa anawaza, ni kwasababu ya ile ndoto au ana matatizo mengine ya kiafya, akajichunguza kuwa labda ana malaria au shinikizo la damu, lakini alijiona yupo shwari, akaghairi akijua kuwa na ndoto tu, …kama ni ndoto kwanini impeleke resi namna hiyo, na hapo akajaribu kumkumbuka huyo jamaa aliyemuona kwenye ile ndoto, ooh kumbe ni `Sweetie..’ akamkumbuka yule jamaa aliyezoea kumuita Sweetie, akajaribu kujiuliza moyoni atakuwa wapi sasa hivi, huenda wameshamuua,huenda kagundulika kuwa ndio yeye..lakini kwanini amuote tena…na wakati anawaza hivi mara mlango ukagongwa, na hata kabla hajasema neno la karibu mlango ukafunguliwa.
‘Ni nani wewe unaingia kwa fujo…’ akasema akiwa chumbani kwake, na alipoona kimiya ikabidi atoke chumbani na kuelekea varandani, haraka haraka alisogea pale anapoweka panga lake …halipo…akashanga, kwani jana usiku aliliweka pale pale anapoliweka, hakumbuki kabisa kuliondoa pale, lazima kuna mtu kalichukua, atakuwa nani kama sio huyo mtu aliyepiga haodi na aliskia kabisa mlango ukifunguliwa na kufungwa ka fujo…mwili ukaanza kumsisimuka, kwani alihis harufu..harufu hiyo ilishawahi kuisikia kabla….harufu…harufu, ndio harufu ya wapiganaji wa msituni…mungu wangu kaingiliwa tena…
Alikuwa kageukia mlangoni, lakini alihisi kuwa kuna mtu nyuma yake, ….lazima kuna mtu nyuma, sijui ndio huyo mtu akiwa na panga, anataka kumkata, sijui kasimama nalo, sijui ana malengo gani, naogopa kugeuka kuonana naye, naogopa kuona kifi changu….na kifo cha panga langu mwenyewe, hapana sikubali, lazima nigeuka nipambane naye akajipi moyoo na haraka akageuka, na alichoona mbele yake ni panga likiwa limeinuliwa juu, na mkono..mkono uliojaa manyoya kama ya mnyama…ooh, wapiganaji wa msituni, na ni nani huyu…
‘Samahani docta, nimeichukua silaha, yako, nilitaka kuhakikisha usalama wangu, lakini sikuwa na nia mbaya kwako,….hata hivyo hii silaha ni katuni tu, huwezi kupambana na mtu kama nah ii katuni….’ Akalizungusha zungusha lile panga kama kitu dhaifu kwake. Siku hizi unashika `machine gun..SMG..NA silaha za kisasa, sio kitu kama hiki…ok, sawa ni kwa aili ya kujipa moyo, sio kosa lako…’ akaliangalia lile panga, halafu akamwangalia Rose, nay ale macho, na lile jicho la kutisha, sasa hivi yalifunikwa na mawani makubwa meusi, ila alama ile ya pembeni haikuweza kufichika.
‘Kama unanikumbuka nilikuja hapa mara ya kwanza na kukupa ujumbe, nashukuru uliufikisha, hata kama jamaa yako hakukupa jibu zuri, lakini kimatendo tupo pamoja nanyi…na poleni sana kwa kashkashi za hawo maaskari wajiitao wa serikali, wanaojiona wamefika, kwasababu wanalipwa vyema na wengine wanadanganyika tu ni wenzetu na sisi, wanadanganyika na `posho’ na hicho kinachoitwa mshahara, wakati wenzao wanakula nyama kwa mrija, wapo maofisini kwao kazi yao kuagiza, nendeni mkapigane, nyie mashujaa….masikini hawo wanaodanganyika kwa kuitwa mashujaa wanakufa vitani familia zao zinataabika, hakuna hata mmoja anayeijali ile familia tena, hakuna anayejaribu kwenda kuhakikisha kuwa familia za hawo jamaa waliokufa kwa sifa ya ushujaa zikoje, hakuna…sisi tumeliona hilo ndio maana tunataka mabadiliko….maaskari, wanausalama wathaminiwe, wao na familia zao…’ Akasema yule mtu na huku akilirudisha lile panga pale alipolichukulia.
Rose alimwangali kwa makini na huku kasimama kama kafungwa, hakuna kutikisika au kuhema alikuwa kama roboti, alisubiri ile kauli ya kusema kwanini mumemkabidhi huyo jamaa yetu kwa maaskari wa serikali, kwanini….lakini hiyo kauli ilionekana ipo mbali na hata hivyo alishangaa kuona huyo jamaa haonyeshi kukasirika, anaongea kama vile hakuna tatizo. Hata hivyo alijua kuwa ndivyo hawa watu walivyo, ni kama chui aliyevaa ngozi ya kondoaa, na alishasikia kuwa hawa watu wakija kwako wanaweza wakakuonyesha ukarimu na kujisahau kuwa umeingiliwa, nia yao ni kupata walichokikusudia na wakiona sasa wapo tayari kufanya jambo lao wanageuka ghafla na kuwa wanyama….hasa hawo wabakaji…..
`Rose, naomba usiniogope, nilishakuambia toka awali kuwa wanavyotuhadithia sivyo kabisa tulivyo, sivyo kabisa kuhusu sera zetu, …hizo ni propaganda potofu, sisi tunachotaka ni haki , tunachotaka ni utawala bora, na haki katika maslahi yanayopatikana, utajiri wa nchi na jasho la watu liende mikononi mwa umma sio kwa watu wachache. Watu hawo wachache wanajilimbikizia mali wananeemeka, wanaiwekea sheria za kuwalinda, eti katiba…angalia kwa mfano watoto wao wanasomeshwa Ulaya, na wapi huko sijui,…ndio hata mimi niliwahi kusomeshwa huko ulaya, lakini kwa haki na taratibu zilizokubalika na nilirudi kuijenga nchi yangu, kulitumikia jeshi, angalia watoto wao ndivyo wanavyofanya kweli, je kuna taratibu zilizokubalika za watoto hawo kwenda kusoma nje…angalia watoto wetu wanasomea sakafuni kwenye mavumbi, vitabu hakuna walimu wanalipwa hela kidogo…wao wanalipwa mishahara minono, marupurupu, na kila aina ya ….sijui wanaitaje…`allowance’…kutokana na jasho la walalahoi..haiwezekani, lazima tulete mabadiliko…’ akanyosha mkono juu akiwa kakunja ngumi.
Rose alibakia kumwangalia tu, hakujua aseme nini, alichoomba ni usalama na moyoni haa kumbukumbu za sala yake zilimtoka, hata akili iligandakufikiri, alichokijua na kumuona huyo mtu akiondoka, ilia pate kuvuta pumzi, hewa ilikuwa nzito kwake, ile harufu, harufu ya jasho, harufu ya nguo zilizojaa uvuguvugu, zinafuliwa hazipigwi pasi…kwa hali kama ile alijiona kama shinikizoa la damu linashuka, alishindwa hata kuhema, aliogopa hata kumeza mate na koo lilikuwa limakauka,….
‘Naona unanishangaa kwa maneno yangu, lakini ipo siku utayakumbuka, najua tu ipo siku,…’ akawa kama anaangalia juu kuwaza na akaendelea kuongea kwa kusema `Najua ipo siku kutakuja mabadiliko, sisi ni kianzio tu, lakini nakuhakikishia ipo siku nchi hii itatawaliwa kwa demokrasia ya kweli, ipo siku wananchi wataamuka na kujua kuwa kweli wanahitajika kudai haki zao, kipindi cha kuogopa na kukaa kimiya kimeisha, watu wanateseka ndani ya nchi yao wenyewe, wanagawanywa matabaka….angalia majirani zetu…licha ya kuwa walitusaidia kumuondoa yule wamuitaye nduli, lakini tunaona heri huyo nduli angelikuwepo, maana yeye aliwafukuzilia mbali wahujumu wa mali zetu…’ akakohoa na kusogea mlangoni.
‘Docta, nisikupotezee muda, utaniona labda nimegeuka kuwa mwanasiasa…sisi kama jeshi tunajua kila Nyanja, na mkuu, kiongozi hachaguliwi hivi hivi, anapitia mafunzo ya utawala, anajua nini cha kuongea kama mwanasiasa ikibidi…mafunzo haya niliyapata huko huko seikalini. Lakini hata hivyo kama mambo yatakuwa mazuri labda ipo siku nitakuwa mwanasiaisa wa ujumla na kuachana na jeshi…hii kazi ni ya hatari sana, lakini mimi nimejengeka kama mpiganaji, mimi nimkulia kwenye kambi, baba na mana yangu walikuwa maaskari na wamekufa kwa risasi…na sitaona ajabu hata mimi nikifa kwa risasi…unakufa kama chui sio kama kondoo…ndio maana siogopi kufa, naendeleza damu ya risasi..lakini kwa nia moja ya kuleta haki na usawa….hata kama sasa mtatuona tunavuruga amani, lakini ni kwa manufaa ya kizazi kijacho….’ Akasogea hadi kwenye meza, na kuchukua bahasha iliyokuwepo mezani, Rose hakumbuki kuwa na bahasha kama hiyo na hakumbuki kuiona wakati anaingia, ilionekana kuukuu na chafuchafu, imekunjwa katikati…
‘Nilitaka kuuacha huu mzigo hapa, sikutarajia kabisa kukuta humu ndani, lakini kwa vile nimekukuta, inabidi nikukabidhi malipo ya gharama za matibabu ya wapiganaji wetu…haya na malipo ya gharama za matibabu ya wagonjwa wetu waliowahi kufika hapo kwenu, kama nilivyokuambia awali, hatutatumia gharama zenu bure, tutawalipa na kuhakikisha kuwa kituo chenu kinakuwepo…na kwa niaba ya kikosi chetu tunatoa shukurani kubwa sana, kwa kuweza kuwatibia wapiganaji wetu na karibu wote wamerejea kazini, hasa yule mtaalamu wetu…amerudi akiwa mzaima, tumeshangaa kabisa, kwani amekuja akiwa na mabadiliko makubwa, …..kwa ujumla kapona huwezi amini hilo…na hili tutalifikiria baadaye jinsi gani ya kuwapa hata kizawadi…lazima tuwafikirie, ila kwa hivi sasa hii ni gharama kwa wapiganaji wetu waliokuwa hawajalipiwa…’ akamsogelea Rose na kunyosha mkono kumkabidhi ile bahasha.
Rose aliiangalia ile bahasha ikiwa imechafuka, na hakujua nini kilichokuwe mle ndani, lakini kutokana na kauli ya huyo jamaa inawezekana ikawa na pesa, na hazanii kuwa ni hundi, na hakuelewa kabisa ni nani hawo wapiganaji waliowatibia, aliogopa kunyosha mkono kuipokea ile bahasha kwani mwili ulikuwa kama umekufa ganzi, aliona huenda ni mtego, aliona huenda ni mbinu zao na mwisho wa siku wanaweza wakaanza kumdai kuwa ndiye aliyekuwa akipokea hela na matokea yake ni kuzalilishwa,… mkono ukawa hauna nguvu ya kunyoka na kuchukua ile bahasha….akabaki kama alivyo. Na yule jamaa alipoona Rosi hanyoshi mkono, akageuka pembeni na kuiweka juu ya meza.
‘Usiwe na wasiwasi Rosi, nimeshakuhakikishia hilo…ok, naelewa jinsi gani unavyojisikia, unavyohisi, ipo siku utaelewa tu.Hii hapa ni gharama yote ya matibabu ya wapiganaji wetu, tunakuamini kuwa utaifiksiha kwa wahusika, mhasibu wenu, au huyo mkuu wenu, na msijali, …sisi sio watu wabaya kama tunavyopakaziwa. Tutahakikisha kuwa wema wenu unalipwa, kwani hatukuamini kabisa kuwa yule mtaalamu kapona na sasa akili ipo kama kawaida, anakumbuka kila kitu, anaweza kufanya kazi yake, na kaingia kiwandani, hatuhitaji tena kuagiza maslaha yao, …wameteka silaha zetu wameweka kizuizi kila kona..wameua baadhi ya wapiganaji wetu wa majini…lakini bado tupo imara,…’ akanyosha ngumi juu tena
`Na kwa vile jamaa yetu karudi atawafunza vijana wengine wapya..hatukutaka kumchukulia hatua ya kuwaua wale vijana aliowafundisha, aliwanyonga kama kuku, kwasababu kipindi kile alikuwa siyo yeye, ulikuwa ni ule ugonjwa wa ajabu, sasa tunaimani kapona, kwani anajua nini anachokifanya…tunashukuru sana kwa hilo, ingawaje imechangia na mambo ya kwao huko, wameshamalizana nayo..’akawa anaongea huku anatembea kuondoka hatua moja moja na Rose hakuweza kuvumilia aliposikia kuwa akiambiwa kuwa `jamaa yetu karudi…’ikabidi afunue mdomo kwa mara ya kwanza tangu huyo mtu wa msituni alipoingia.
‘Ina maana yule mtu mliyesema kachanganyikiwa karudi kwenu…toka lini ina maana katoroka jela, kwasababu walishamchukua…na kumpeleka kwenye jela yao huko kambini, jela la wahalifu na sisi tulishajua huenda keshakufa…’ akasema Rose, wakati yule jamaa kasimama karibu na mlango hakugeuka, akacheka kidogo na kusema.
‘Hajawahi kufanya hivyo na hawatawahi kumkamata…yule ni komandoo, huyo unayesema labda ni mtu wao lakini sio huyo tuliye naye, tunajua nini kinaendelea, na …hiyo ni moja ya miujiza kuwa tunapigania haki ….na miujiza kama hiyo itaibuka mingi…watawakata watu wengi watawatesa wakiwadhania tu, ….lakini hakuna kitu, sisi wapiganaji tupo tunasonga mbele….hilo nakuhakikishia kuwa kamwe hawataweza kumkamata yule mtu….labda wamkamate akiwa mfu….sisi tunajiamini, ni wapiganaji wanaolindwa na imani, wenye uzoeufu wa siku nyingi, makomandoo…tumajifunza nje, sio hapa nchini, sasa watu wadogo kama hawo watukamate kirahisirahisi…sizani…kwaheri Docta, hakikisha bahasha hiyo imefika panapohusika, hatutaki madeni….kwaheri…

Ni mimi: emu-three

4 comments :

Yasinta Ngonyani said...

Duh! nimechelewa kweli naona visa vingi vimenipita wakati nilipokuwa safarini..inabidi nifanya jitihada kweli ili nikutana na hiki...Ila nipo nanyi kwa kila hali..PAMOJA DAIMA

emu-three said...

Da Yasinta sina wasiwasi na wewe.Wewe ni mtu wa watu.TUPO PAMOJA DAIMADa Yasinta sina wasiwasi na wewe.Wewe ni mtu wa watu.TUPO PAMOJA DAIMA

Iryn said...

Mmmnh sasa hapo mambo yanazd kuchanganya jaman

Anonymous said...

MASKINI SWEETIE