Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, August 5, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-10‘Mimi nilimuacha hapa akiwa kalala kama kawaida yake…alikuwa hajazindukana,…labda alizindukana halafu akaamua kwenda haja… labda …..akageuka kuangalia chooni…na kabla hajasema zaidi akachepuka hadi kwenye mlango wa chooni, akasita kidogo, halafu akagonga hodi..akatulia, akagonga tena..kimiya..akageuka kuwaangalia mabosi wake, na sura alizoziona alijua sasa hana kazi…akaanza kuwaza akiongea kichinichini, kwa sauti ndogo..

`Mungu wangu, nitakwenda kwanani sasa, wakati mume nilitimuana naye kwa nyodo, kuwa asinibabaishe, …asinibabaishe kwasababa nilijua nina kazi, kazi yenyewe niliipata kibahati bahati tu, vyeti vya kugushi…mshahara wa kutosha, kwanini nimnyenyekee….nikaachana naye licha ya kunibembeleza, mmh wivu, eti ananipenda …nilishachoka naye, kila siku kwanini umechelewa, kwanini, kwanini…nikaachana naye…sasa kipo wapi…ooh, mungu wangu nisaidie huyu mgonjwa apatikane, mbona nitaumbuka mwanamke miye…’akawa anapiga piga miguu chini bila kujijua, huku kashika kichwa, na akajikuta akiongea sasa kwa sauti ’’….na kodi ya nyumba ndio natakiwa kulipia mwezi huu….wowowooo,…nimeumbuka…nimeumbuka…’ akawa anaruka ruka, hakujua kuwa Rose kaja pale aliposimama!

‘Hivi wewe nesi badala ya kufungua huo mlango, ili uhakikisha kwa hicho unachodai kuwa huyo mgonjwa kaingia huko kujisaidia, wewe unatuchezea ngoma za kwenu, unafikiri katika hali kama hii, inahitaji hizo ngoma zenu…muda utafika utaicheza sana, ukiwa mikononi mwa hao askari vichaa..hebu nipishe huko…’

‘Eti nini, maaskari…hapana, mume wangu naye n i askari, akisikia haya atachekelea kuni…’ alasema yule nesi huku akishikilia kichwa, kama mtu aliyepagawa. Mume wake ni miongoni mwa maaskari wanapambana na wapiganaji wa msituni, nan i mmojawapo anayeipiga vita hiyo hospitali kuwa inamvimisha kichwa mke wake, na alishawahi kusema kuwa atahakikisha kuwa inafungwa….
‘Hebi nipishe huko…maana nakuona umepagawa….’ alisema Rose na kuufungua ule mlango wa chooni, nusu na akawa anachungulia kwa kujiiba, isije kweli kuna mtu anajisadia…alichungulia kwa muda huku kashikilia mlango na kichwa kinaangalia ndani ya kile choo, halafu taratibu akaurudishia ule mlango na kuufunga. Aliogopa hata kumwangalia bosi wake, akawa anatembea kurudi aliposimama bosi wake kwa upande upande, naye akijisema kuwa ni zamu yake kuicheza ile ngoma aliyokuwa akiicheza nesi.

‘Hayupo….’akasema Maua kwa wasiwasi, na yule nesi alikuwa akihaha huku na kule kwa kufungua kila eneo mle ndani..., lakini hakukuwa na mtu, na alipohakikisha hilo akarudi pale waliposimama mabosi wake na kusema `Naapa kabisa nilimuacha akiwa bado hajazindukana, na kama kaamuka basi labda kachanganyikiwa na kukimbia, na atakuwa hajaenda mbali maana sijachukua muda mrefu,. Nilikwenda kuchukua shuka nyingine….’ Akasema nesi huku akizunguka huku na kule hata kuchungulia mvunguni mwa vitanda kama vile anahisi huyo mgonjwa kajificha mvunguni…

‘Haraka amrisha msako, ingawaje eneo letu ni dogo sana, kama katoka humu ndani atakuwa keshafika mbali, …waambieni walinzi wazunguke kote hadi mfukweni mwa ziwa, kote haraka haraka ..muite mlinzi na watu wote wamtafute huyu mgonjwa haiwezekani ayeyuke kirahisi namna hiyo….oooh, hili sasa ni balaa, mbona jamani mnanitafutia balaa…mngalijua nini kitakachofuata baada ya hapa, mngelijua kuwa hawa maaskari na polisi wakilijua hili ndio itakuwa mwisho wa kituo hiki, sijui…niwaambie nini …kila siku nawaambia kituo chetu hiki hawakitaki hawa maaskari, kila siku wanatafuta upenyo kama huu ili wakifunge , wao wanadai eti mimi ninalindwa na wakubwa serikalini na siku wakipata ushahidi wa kukifunga hichi kituo hawatasubiri huyo mkubwa wa serikalini, sijui mkubwa gani huyo nisiyemjua…sasa nahisi, wamefanikiwa….hakikisheni anapatikana, vinginevyo nitahakikisha nyote mnajuta…...

Kukawa heka heka, kila mmoja akitafuta huku na kule, lakini mgonjwa hakupatikana kabisa, na mwisho wa siku ikabakia Docta Adamu kuitisha kikao cha dharura kwa madakaitari wote na manesi. Alikuwa kabadilika sura, mwili unamsisimuka kwa hasira, aliwatizama watendaji wake kwa muda akitafuta neno la kutoa hasira yake akalikosa, alichofanya ni kufungua droo ya meza yake akaanza kugawa barua, kwanza kwa yule nesi aliyekuwa zamu.

‘Kazi umiharibu mwenyewe, nenda huko unapoona kuna kazi ya kuchezea, na akawa kashikilia barua moja, na kila mmoa mle ndani akawa anajiuliza itakuwa ni ya nani. Akamgukia Rose,`.. hii barua ni ya onyo namba mbili, kupona kwako kufukuzwa kazi ni kupatikana kwa huyo mgonjwa, vinginevyo wewe lazima ukaisaidie polisi ukishirikiana na nesi wako..’ akamkabidhi Rose ili barua, na kuanza kutoa hatuba iliyojaa vitisho akiwaeeleza nini kilichopo mbele yao, nay a kuwa hata waliobakiawajijue kuwa kazi ndio imeharibika nay a kuwa yeye hatakubali kufungwa kwa ajili ya uzembe wa watu wachache…

‘Tawanyikeni muendelee na msako…’ akasema kwa hasira, na wote wakawa wanatoka kwa haraka na mara gari la maaskari likaingia kwa fujo kama kawaida yao, na mmoja wa askari aliyepewa dhamana ya huyo mgonjwa akafika na kuingia moja kwa moja ofisini kwa Docta Adamu.Alimkuta Docta Adamu kapagawa kwa hasira, …

‘Mumerudi kufuata nini…’ akaanza kpayuka akijua ni mmoja wa madakitari wake alikuja kumwambia kuwa kuna wageni.

‘Unanifukuza leo Docta, hujui kuwa mimi nimeshikilia mpini , una bahati kuwa huyo mkubwa huko serikalini kaweka ngao, vinginvyo kisu hicho kingesakukata mikono yako…sikia docta, kama huyo mgonjwa hajazindukana tutanchukua kwenye hospitali zetu tunajua jinsi gani ya kumzindua, kwanza wa nini kama keshakufa, tunachotaka ni kupata taarifa kuwa yeye ni nani na wakuu zake ni akina nani. Hivi nyinyi hamuoni wanavyotutaibisha , kila siku vita, hamtuaki amani kwenye nchi hii, na wanaosababisha hili ni hawa watu…’ akasema yule askari akiwa kakaa na kuweka mguu juu ya meza ya Docta Adamu.

‘Nimeshakuambia kuwa mimi ni dakitari na nina dhamana kama dakitari, siwezi kumtoa mtu katika hali kama ile,..nyinyi wenyewe mliamua kumleta hapa baada ya kumchukua huko mlikomtoa, sasa mnanilta fujo…sipendi naman hiyo..naijali kazi yenu na nyinyi muiheshimu kazi yangu…na naomba uondoe huo mguu wako juu ya meza yangu, huoni hapo uanachafua kumbukumbu ….; akasema Docta Adamu huku akiwa na wasiwasi.

‘Sawa bosi sitakuingilia kazi yako kwa sasa ila nikija mara nyingine nataka kumuona huyo mgonjwa,na nitaondoka naye, hil nakuhakikishia kama manashirikiana naye mtaondoka naye, mkatibiane huko jela…siunaifahamu ile jela ya wafungwa wa kivita…huko huko utakwenda kuwatibia wenzako…tuone hiyo nyodo yako itaishia wapi..na huyu bwana mkubwa anyekulinda huko juu, ..mapaka apate nafasi ya kuja kukutoa utakuwa sio wewe tunayekujua…’ yule askari akainuka pale kwenye kiti na kuanza kuondoka.

‘Nasikia manesi wako wanajiona , kwa vile unawalipa mshahara mzuri, mzuri zaidi yetu sisi tunaoweka maisha yetu rehani kwa aili ya nchi yenu…sasa tuone tukikifunga hiki kituo watakwenda wapi….kama si watarudi kwentu…sisi tupo muda wote na kimshahara chetu…lakini tuna uchungu nan chi yetu na ndio maana tunapigana na hawa maharamia, wanaotaka kupindua nchi kwa mtutu wa bunduki…nyinyi mnawalinda, wakiumia wanakuja hapa mnawatibia, wakipona wanarudi kwetu kutusumbua…hujui huo ni usaliti wan chi yako….’ akasema huku akiwa anatembea hatua moja moja kutoka nje, na kumuacha Docta Adamu akiwaza hiyo kauli yake kuwa…`tukikifunga hiki kituo….’

Docta Adam aliwaza afanye nini na huyo mgonjwa keshatoweka , atajitetea vipi, ….na mpaka hapa hajasema ukweli, akiwa anadhania kuwa atapatikana kwasababu hali aliyoodnoka nayo siyo ya kuridhisha, labda awe kweli ni mmoja wa hao majangiri au wapiganaji wa msituni kwani hawo wana roho za paka. Akawaza neno hilo kuwa `yeye ni msaliti wan chi yake…’ akatikisa kichwa, na kusema kimoyomoyo kuwa yeye wote ni abiria wake, inapofikia katika hali ya kuokoa maisha ya mtu, awe mtaifa au mpiganaji awe jambazi wote wanapofika katika mkono wake anatakiwa kuhakikisha maisha afya yake ipo salama…akainuka kwenye kiti na kutoka nje, akiwa na nia ya kwenda nyumbani kwa Rose ili ajue nini kinaendelea, ….

Rose alipotoka pale hospitalini alikuwa kachanganyikiwa akijua kuwa yeye sasa ndiye anaonekana mkosaji hakuwajibiak vyema, hakuwapanga vyema watendaji wake, lakini kwa hali kama ile lolote lingeweza kutokea, unatoka kujisaidia , unatoka kwa dharura, huku nyuma huyo mgonjwa anatimuka…
‘Lakini ina maana kweli yule mgonjwa ni gaidi, haramia, mpiganaji wa msituni, mbona hafanani kabisa, …hapa ndio nashidwa kuwaelewa hawa wanaume, unamwamini mpaka mwisho , siku ya mwisho anakusaliti….lakini bado sijakata tamaa na huyu mtu, lazima nimtafute , anijibu kwanini hana shukurani, na kama kazi ndio imekwisha …mmh, na nilikuwa na mpango wa kusoma, zaidi na nilishaongea na bosi akasema atalifikiria hili , sasa ndio basi tena, …..’

Rose akawa kafika eneo la nyumba anapoishi na rafiki yake, akijua kuwa rafiki yake atakuwa keshaondoka kwani yeye alikuwa na zamu ya kuanzia saa nane . Akachukua ufunguo wake na kutumbukiza kwenye kitasa cha ufunguo, akazungusha ufunguo ili kufungua, akakuta hakizunguki, akazungusha tena akakuta hakizunguki, …akawa kama anakilazimisha kuzungusha kwa nguvu, lakini hakikusogea…

‘Aaaah, haiwezekani, nina uhakika niliufunga huu mlango, …au kitasa kimeharibika…’ akazungusha kifungulio cha mlango na kukuta mlango unafunguka…’ badala ya kuufungua akaufunga kwa haraka, akiwa na wasiwasi, nani kaufungua huo mlango…! Kumbukumbu za hawa wapiganaji wa msituni zikamjia, kuwa mara nyingine wanaweza wakaja na kuingia ndani kwako, ukiingia wanakubaka, au wankubeba na kukupelaka huko msituni, ukatumikishwe …na kuzalilishwa…alipowaza hivyo akaanza kurudi kinyumenyume, ili akimbie.

Akakumbuka kuwa wao wanachangia ufungua na rafiki yake huenda alikuja akafungua halafau akasahau kufunga mlango, lakini haijawahi kutokea , kila mmoja anamuheshimu mwenzake , hawezi mmojawapo akaingia sehemu ya mwenzake kama hayupo, labda awe amemtuma kuchukua kitu…haiwezekani, imeanaza lini hii…akageuka na kutembea hadi eneo la mwenzake , na kufungua mlango wake akakuta umefungwa...

‘Atakuwa keshaondoka kazini, mmmh, ningelikuwa na simu ya mkononi ningelimpigia, …lazima ninunue simu ya mkononi, lakini ni aghali sana…’ akasema na kuangalia ule upande wa chumba chake akiwa anakuona kama kituo cha polisi. ‘Sasa nifanye nini, nirudi kazini nikawaambie nimeingiliwa….’ Hapana ngoja nikafungue niona kuna nini, kama nimeandikiwa kufa, basin a iwe hivyo…lakini sio kufa , kuna kubakwa, kuna….aaah, hapana leo siingii humo ndani…’ Alisimama pale kwa muda akitafakari amwambie nani jirani yao anayemwamini…

Mwishowe akaamua kuufungua mlango wake , aliifungua taratibu, kwa tahadhari…na ulipofunguka akaingiza kichwa kwanza na kuchunguza mle varandani,…hakuona mtu, lakini alihisi harufu ya ngeni, lazima kuna mtu kaingia tofauti na ilivyozoeleka, na harufu hii ni ya kiume….akazidi kuogopa, akaufungua mlango wote na kuuacha wazi ili kama kuna mtu akitoka iwe rahisi kukimbia, …

Akaingia ndani, akakagua varanda yote , hakuna mtu…oh,… lakini alihisi kuwa lazima kuna mtu, ukiwa na chumba chako unaishi peke yako, kama kuna mabadiliko utahisi tu, ndivyo alivyohisi Rose, alijua kwa vyovyote kuna harufu asiyoizoea puani mwake..hata hisia za mwili zilimweleza hivyo, zilimwashiria harati tupu, lakini hakukimbia, alitaka kupambana nayo….sasa atakuwa wapi huyu mtu…akaelekea chumbani kwake, akakagua hakuna mtu, au labda kaingia uvunguni…akatoka na sasa hivi akaelekea jikoni na kuchukua panga, ni moja ya silaha zake akarudi nalo…

Alitafuta karibu sehemu zote hakuona mtu, na akawa keshakata tamaa, akidhania huenda huyo mtu aliingia na baadaye akaondoka! Ili kuhakikisha hili akarudia tena kukagua sehemu zote na alipoona hakuna mtu akaamua kurudi chumbani, akiwa hana wasiwasi tena na wakati huo panga kaliacha varandani,na akiwa kajiamini akaingia chumbani kwake na kuanza kuchojoa nguo zake ili achukue khanga akaoge, akiwa kavua nguo zote kasoro nguo za ndani tu, aliinama kutafuta ndala ambazo zilizama uvunguni, wakati anahangaika kumtafuta mtu asiyeonekana, akazipata sasa wakati alipoinuka akaguswa begani, ……

NB. Nawaombeni sana radhi, sehemu hii nimeiandika kwa haraka haraka sikutaka Ijumaa hii ipite hivihivi...kwahiyo kama ningelikuwa nimepata nafasi ya kuipitia tena,...mmh, nahisi ingekuwa bomba zaidi..lakini ngoja twende hivyohivyo, nikijaliwa kuandika kitabu nahisi kila kituu kitakuwa saafi...tuombeane heri na tusaidiane, kama wapo wanaofanya kwenye sehemu wanachapa vitabu wanibonyeze, kwa kupitia e-mail..TUPO PAMOJA

Ni mimi: emu-three

4 comments :

Anonymous said...

DUh we emu3 e mkali wa kutunga.Hivi nikuulize hakuna hawa wasanii wetu wa movie waliokutafuta uwaandikie script maana hadith zako kama filamu.

NB: nimshaanza kuhisi wewe sasa ni wa jinsia gani bado kidogo tu nikamishe uchunguzi wako.

ROGER-uk

emu-three said...

Roger-UK ,Hawa wasanii wetu wengi wanatunga wenyewe kibongo bongo ! Wakiona stori kama hii wataifanyia usanii na mwisho unaona movie inafanana na stori hii! Tupo pamoja karibu sana Roger!007

samira said...

wow nilikuwa bz jana leo ndo nimepata mda nimeisoma nzuri rose bado mitihani
nangoja next week
m3 big up

Candy1 said...

Baada ya muda mrefu na heka heka za hapa na pale, na matatizo ya computer yangu...pia kusoma tokea sehemu ya kwanza ya story hii sasa M3 nimerudi OFFICIALLY! Hahaha, sasa tupo sambamba na sitomiss unless computer ifanye ujinga tena. I am back! na nipo kama kawa! :-)