Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, July 22, 2011

kila mchuma janga hula na wakwao!



Tulikuwa msibani na watu wengi walikuwa wakiulizana huyu jamaa aliyekufa kaumwa lini, mbona hautukuwahi kusikia, na hayo tukiwa tunaulizana jamaa yao mmoja akajibu kwa machungu, akisema, `wanadamu wabaya, wamemfanyia tu huyu ndugu yetu, na haya yote sababu ya wivu, wamemuona kainukia ghafla basi wakaanza kumsakama…’ aliongea mengu kuonyesha kuwa kufa kwa jamaa yao huyo sio bure ni mkono wa mtu.
 Wakati wanasoma wasifu wa huyo marehemu wakaisoma na ile taarifa ya dakitari kuwa marehemu alikufa kwa tatizo la shinikizo la damu, na kisukari….na hapo kauli zikaongezeka toka kwa jamaa zake kuwa sasa hivi wachawi hulogea ugonjwa ule unaojulikana ili mtu aonekane kuwa kafa na matatizo ya kawaida. Hili linatokea sana, hasa jamaa ambaye wanafamilia walimtegemea hata kama walikuwa hawamtegemei sana, lakini kila kifo hakikosi sababu…
Wakati haya yakiendelea mimi nikawaza mengi sana, na bahati nzuri wakati nawaza haya mmoja wa kiongozi wa dini akatuasa kuwa sasa hivi matatizo yanayoikumba dunia ni `dhambi’ ya kuwa binadamu sasa hivi haogopi kutenda dhambi na cha ajabu  anashindwa kujua kuwa dhambi hizo ndizo zinazomuandama katika misha yake, hilo halionekani kwasababu dhambi sio kitu cha kuogopwa tena…tukabaki tukijiuliza dhambi ndizo zinaleta umasikini, …kwa vipi
‘Angalieni maandiko ya dini zote yanasemaje `tusiibe’ tusizini’ tusidhulumu mali ya mayatima, tusichukiane ikiwa na maana tuwapende majirani zetu na kitu kama hicho, dhambi hizi zinatendwa siku hizi kama watu hawayajui hayo maandiko! Ina maana maandiko haya yapo vitabuni kwa ajili ya siku za kukutana, ama ni siku ya Ijumaa au Jumapili, …lakini hayapo katika matendo yetu ya kila siku..
‘Mifano ya tusizini ipo wazo magonjwa yanaibuka ya kila aina, watu wanagombana, ndoa zinavunjika, watoto mayatima wanazaliwa…hebu enedleza hayo mpaka kufikia kuwa  mayatima hawa wanakosa masomo wangeuka kuwa vibaka, …hebu enedeleza haya, kuwa una magonjwa yanaingia ndani huna unahangaika kutafauta madawa huku na kule shughuli zinalala…hebu enedleza majanga hayo kwa mapana, chanzo kikubwa ni uzinzi….!
 Tuangalie zambi ya wizi, hii wengi ukiwauliza wanasema `mimi siibi…’ …..tumeambiwa tusiibe, hivi kweli kuna mtu haibi sasa hivi, na kuiba kunatafsiriwa vipi katika jamii, ndivyo mungu alivyotutafsiria kweli…..,kama wewe ni mfanyabishara ukaongeza bei isivyo halali umeiba, ukaacha kulipa kodi umeiba! Kama wewe ni docta ukaacha kutimiza wajibu wako umeiba, kama wewe ni mwalimu ukaacha kutimiza wajibu wako umeiba, achilia mbali wahasibu wanatenegeneza vocha za uongo, wanatafuta risiti za uongo ili wapate pesa …..hii ni mifano midogo tu ya kawaida Hii ni kuonyesha kuwa `uaminifu’ wa watu katika nyoyo zao haupo tena, kila mtu anajitahidi amdhulumu mwingine ili afaidike yeye, lakini mwisho wa siku inakula kwake, kinamna ambayo haijui, au aianijua lakini hana muda wa kuchanganua anachujua ni kumnoshea kidole aliye juu yake…
Angalia mataifa makubwa hutaamini kuwa yanawaibia mataifa masikini, na hii linatokana na tamaa za viongozi wetu tuliowachagua wenyewe, viongozi wetu wapo tayari kuuza malighafi kwa bei ya kutupa, wapo tayari kuuza mdini wapo tayari kuiba mali ya uma na kuiuza nje kwa bei ya kutupa, wapo tayari kuingia mikataba mibovu ilia apate cha juu  na huu ni wizi wa kimataifa, na nini chanzo cha yote haya ni sisi wenyewe. Sisi ndio tumesababisha haya kwa kuwa tuliwachagua viongozi kwasababu wametupa kitu kidogo, kwasababau ni mwenzetu , kwasababu za kibinadamu tu…na sababu zisizo na tija kwetu,  ilihali tulijua kuwa sio `mwaminifu’…dhambi ya kutokuwa mwaminifu inaturejea sisi wenyewe…..tumalaumu nani?
‘Kila mchuma janga hula na wa kwao’ Janga tumelianzisha sisi wenyewe kwa kuchagua viongozi wabovu, ambao wanasaini mikataba ya uongo, ili kuwe na cha juu . Hiki cha juu kinatuangamiza sote na hicho cha juu ni kwa maslahi ya huyo kiongozi na familia zao, wakasahau kuwa janga likitokea halitaishia tu kwa hawo waliowadhulumu litasambaa na kumrudia mwenyewe …na dhambi hizo hutaamini zitamwandama huyo kiongozi, angalia magonjwa yanayozuka sasa, shinikizo la damu, kisukari nk, kwasababu sasa hivi kila mtu anaishi kwa `presha’ hana amani tena, kadhulumu hapa, ana wasiwasi na hili, hamkumbuki mola wake tena…anakula mali ya dhuluma, mali iliyofanyiwa dhuluma,..mfano mavyakulwa yaliyochakachuliwa, na hujui humo kumepita dhuluma gani, yote tunayatumbukiza tumboni, matokeao yake nini…magonjwa ya ajabu , tatizo ni nini- dhambi ya wizi.
Wewe umempigia kura huyo kiongozi ukijuwa ni mwizi, sio mwaminifu, kawa kiongozi katumia udhaifu wake uliojaa dhambi moyoni, dhambi ya wizi ,…sasa anafanya dhambi ya kulipiza dhambi yako kwa  kusaini mikataba ya ulaghai. Ukumbuke dhambi hii uliitenda kwa mkono wako wakati unampigia kura inakuja kukurejea wewe mwenyewe. ….

Kwasababu gani,  hebu chukulia mfano huu mdogo wa  balaa la umeme, kutokana na umeme watu wanazidi kudidimia kwa umasikini, wengi walikuwa na miradi yao wakitegemea umeme, kutokana na hili inabidi tununue mishumaa ambayo kwa kiasi kikubwa inaathiri afya za watu, …habu fikiria kila siku unanunua mishumaa mingapi, huku ulishalipa kodi yako, ili umeme uwepo, huku ulishalipa LUKU, …sasa angalia athari zake hebu angalia moshi wa mishumaa, makelele ya majenerator na moshi wake yote haya yanaathiri hali ya hewa na mvua zinapungua…tatizo limeanzia wapi kwako wewe uliyempigia kura kiongozi ambaye ulijua kuwa sio mwaminifu. Usiseme ulikuwa hujui, kwanini kama ulikuw hujui ukampigia kura badala ya kuwapigia watu wenye uchungu na eneo lako..
Niwaambie ukweli kila mchuma janga hula na wakwao… kiongozi ni mtu mhimu sana katika maisha yetu, kama ni hivyo lazima tuwe na michakato muhimu ya kumpata kama tunavyofanya kumpata mke mwema, au mume mwema, huwezi ukakutana na mke au mume barabarani ukaamua kuoana naye… lazima ufanye uchunguzi wa maisha ya familia yao, tabia yake toka utotoni , hana magonjwa ya kurithi…haya yalifanywa na wazazi wetu ndio maana ndoa zao zilikdumu…hako ni kamfano ka hali halisi tunayaiona, sasa kwanini kiongozi tumchague tu juu kwa juu eti kwasababbu anajua kuongea vyema jukwaani, kwaninii hatutaki kuwachunguza hawa viongozi mapema kuanzia huko utotoni mwake, kama alikuwa mdokozi, kama alikuwa akiibia maksi, kama alikuwa anachelewa shule, yote haya yanakuja kujitokeza akiwa kazini, …kwasababu kubwa tumesahau maandiko yanatuambia nini na mwisho wa siku tutaanza kulalamika ooh, mungu wangu umetuacha, oooh, tumelogwa …ooh viongozi wabaya, ooh, kuna mkono wa mtu, …chanzo ni sisi wenyewe…
Jamani hili ni wazo la siku ya leo. Kama limegusa nyoyo zetu tunashukuru na kama linakera basi labda ujumbe umefika, na kama tumekosea, tusameheane. Kisa chetu kinaendelea,tuzidi kuwa pamoja


Ni mimi: emu-three

5 comments :

Anonymous said...

Nimesoma mada hii ya leo kwa kweli imenigusa sana na inatia uchungu. Janga tumelichuma wenyewe basi yafaa tulile wote. Yatupasa tuchukue hatua katika uchaguzi ujao. Tusije kula wa chuya tena kwa uvivu wetu wa kuchambua.

Emmy, MZa.

Anonymous said...

Nilikua wapi sijui

Unknown said...

Nimesoma ujumbe huu 2021 umenigusa sana

Anonymous said...

Woe

Anonymous said...

Maana ya hiyo insha nini