Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, June 20, 2011

Dawa ya moto ni moto-24  
  Muhimu: Ili uweze kwenda vyema na sehemu hii inayofuata, ambayo ni ndefu kidogo, rejea kusoma kwanza sehemu ya tatu: Dawa ya moto ni moto sehemu ya tatu.  Halafu endelea na sehemu hii:-

                                                                 ***********
 Docta alibaki ameduwaa, hasa alipomuona Maua akiinuka na kukaa pale kitandani, na macho yamemtoka, kuonyesha hasira, na huyu mgonjwa mwingine katunisha misuli, kuwa yupo tayari kwa shari na macho yamemtoka kwa hasira. Docta alipoona hivyo akasogea karibu kutaka kuwazua, na alipomuana Maua anajitutumua kuinuka pale kitandani akasubiri, kwani huenda ikamsaidia na kumfanya Maua ainuke haraka kuzoesha viungo vyake. Na miujiza kweli ikatokea, kwani Maua aliinuka toka pale kitandani na kujitahidii kusimama, na kweli akasimama, ingawaje alianza kuyumba kutaka kudondoka, lakini baadaye akasimama ….. Na hapo ukaanza ubishi usio na kichwa wala miguu…!.
 Docta akasogea pembeni kuwaangalia, lakini kwa tahadhari, na hakuelewa kabisa nini kinachobishiwa, kwani hata ukiunganisha maneno yao hayaleti maana kabisa. Huyu anasema hiki kabla mwenzake hajamalizia huyu kadakia hivi, ikawa ni kupayuka-payuka!
Ubishi Ukafikia mahali wagonjwa hawa wanasutana,  kila mmoja akimshuku mwenzake jambo ambalo halikuwa wazi kwa Docta, ilivyoonyesha ni kuwa kila mmoja alikuwa akimuona mwenzake ana makosa, na ndiye chanzo …lakini hawakutaka kumalizia ni kuhusu nini. Docta akaona huenda yeye ni kizuizi, ni bora atoke pembeni awape nafasi,…akasogea na kuanza kutoka nje, na hawa wagonjwa walipoona docta kaondoka, kweli wakaanza kuongea kwa usahihi…na wakati huo docta alikuwa akifunga mlango lakini alipokuwa anataka kufunga vyema huo mlango akasikia maneno ambayo yalimvuta kutaka kusikiliza….
‘Nina uhakika wewe uliniwekea madawa yaliyonipoteza ufahamu wangu na kufanya yale uliyotaka niyafanye …’
Docta aliposikia neno `madawa’ kaona hapohapo, …akasikiliza kwa makini nini wanaongalea kuhusu madawa.
'….Ulipoona nimekuwa kama ulivyotaka halafu ukafanya ulichokusudia…ukanidhalilisha…huku unanirekodi…halafu ndio ukaja na huo mkanda kutaka kunishawishi nitoe hela kwa kupitia watu wako…bisha kama hukuwa na lengo hilo…’ akasema Maua.
‘Mimi naona wewe unajifanya kujitetea, nia ni kuonyesha kuwa wewe ni mjanja wa kugeuza maneno, wewe sasa unajifanya mjanja, kwasababu umeshindwa kufanikiwa lengo lako, la kutaka kuniharibia ndoa yangu, sasa unjikosha. Wewe ulipanga haya na kundi lako, unywe madawa yako ili uondoe aibu na kuniingiza kwenye vishawishi ili itokee mlivyopanga, ….’ Akasema Bosi.
Baada ya kila mmoja kuongea kwa jaziba, huyu akimlaumu mwenzake kuwa ndiye aliyepanga hilo tukio na mwenzake akimlaumu hivyohivyo kwa muda bila kuafikiana, ikafikia hatua wote wakakaa kimya wakiwa wameangaliana kama majogoo yaliyochoka baada ya  kupigana kwa muda mrefu na wote walijisahau kuwa ni wagonjwa.  Walikaa kimiya kila mmoja akiafakari, na hapo docta akaondoka, na huku nyuma wagonjwa wale akili zikawajia na kuanza kuulizana kwanini ilitokea hivyo, e ni mmoawapo alipanga iwe hivyo au kuna mkono wa mtu…
‘Kama ni hivyo kuna mtu yupo nyuma ya hili jambo…’ akasema Maua.
‘Hilo ndilo la muhimu, hata mimi nimeliona hilo, kuwa kuna mtu alituchezea huo mpango ili kukidhi haja zao na ndio maana hata huo mkanda uliokuwa huko ofisini umetoweka tena,….na hata mimi sijauona huo mzigo niliokuwa nimeagizwa nikauchukue huko hotelini, kwani mke wangu alikuwa kanibana, na yakatokea haya yaliyotokea…cha muhimu sasa tuwe kitu kimoja, tuweke akili sawa, tuchunguze nani yupo nyuma ya hili jambo…’ akasema Bosi.
‘Sawa, kama kweli ndio hivyo, ila sitaki makosa kama ilivyotokea kama ni kazi iwe kazi, na kama kutakuwa na udanganyifu wowote, mimi nitakuwa wa kwanza kukutna na mkeo kulijadili hili…’ akasema Maua.
‘Mimi nakuhakikishia sijui lolote, …na kama utathibitisha hilo, mlango upo wazi, kamuone mke wangu, kamuone mkwe wangu,…cha muhimu ni kutafuta huyu mtu aliyefanya uchafu huu…kwa faida yako na mimi…kwani ujuavyo likiharibika sio mimi tu nitapoteza kazi , nina imani na wewe utakosa kila kitu..namjua sana baba yako…’ akasema Bosi.
‘Dawa ni moja, tuwe kitu kimoja, ili tuwavunje nguvu, kwani wakituon tupo pamoja hawatapata mwanya wa kumuogopesha mmoja wetu…, cha muhimu ni kuhakikisha kila mmoja anamweka sawa mwenzake wewe mweke sawa mumeo, na mimi nitamweka sawa mke wangu, ili tupate nafasi ya kuchunguza……’ akasema Bosi, na wakakubaliana kwa hilo kuwa wakitoka hapo hospitalini watatumia moja ya nyumba ya Maua aliyopewa na baba yao kama ofisi yao maalumu na huku watahakikisha kuwa hawo jamaa watavutika kufanya jambo lao tena, kama ndio mtindo wao na kama watamtokea mmojawapo iwe nafasi ya kuwakabili kwa pamoja. Waliogopa kabisa kuwahusisha polisi kwani walisema kwa jambo kama hilo hakuna wanayemuamini.
Basi Maua akawa wa kwanzakuruhusiwa kutoka hospitalini, na kesho yake Bosi naye akatoka, na wote walipata  mapumziko ya wiki moja. Maua kwa upande wake, alijaribu kila njia kumficha mumewe tatizo lililowasibu hata kufika hatua ile, lakini kimatendo alishindwa kabisa,…alitawaliwa na mawazo, na hakupenda kudadisiwa na mumewe, kuwa ilikuwaje, alion aheri akae peke yake na kufikiria mambo yake, na sio kuulizwaulizwa maswali.
Maua alikuwa na hamu sana ya kukutana na hawo watu, ikibidi uso na kwa uso kwani alijua kuwa hawo jamaa waliomfanyia hivyo kama hawatajulikana ipo siku wataibuka tena, hasa baada ya kupotea tena ile kanda ya DVD, aliyopewa…aliwaza sana jinsi gani ya kumfanya mumewe asimgande kwa maswali yake, kuwa ilikuwaje…licha ya kumhakikishia kuwa sasa mambo yapo shwari, lakini kichwani alikuwa na donda ambalo kupona kwake kulitegemea hawo watu walioandaa hilo tukio wana malengo gani, na je lengo lao kama ni pesa, na pesa bado hawajapewa, lazima watakuja tena!.  Baada ya kutafari hili kwa makini akaona kuna haja ya kukubaliana na mawazo ya Bosi kuwa wawatege hawa watu kwa kujifanya kuwa wao wana muhusiano ya siri kama awali.
 Basi wiki ya mapumziko ilipoisha Maua akarejea kazini, na kukuta mabadiliko, kwani alimkuta Bosi mpya kwenye idara yake na aliambiwa kuwa bosi wake wa zamani kahamishwa idara. Na taarifa nyingine Bosi wake huyo hawana mahusiano mema tena na mkewe, ingawaje wanaishi pamoja, lakini kila mtula maisha yake. Kwake haikuwa tatizo kwani bado walikuwa katika ofisi moja, na wakawa wanakutana baada ya kazi kujadili mipango yao. Na siku moja wakaa na kujadili jinsi gani ya kuliweka swala lao vyema, kuwa wajifanye wana kutana nyumba ya siri, na hawa watu watakuja kwa nia ya kuwapiga picha…na ikawa  siku nyingine wanakwenda kwenye majumba ya starehe kujichanganya kama wapenzi, ilimradi ionekane wana ajenda ya siri.
Na kwa vile dunia haina siri watu wakaanza kuwashuku kuwa wanamahusiano ya siri na taarifa hizi zikafika kwa Maneno, na Maneno akaanza kuamini maneno ya marafiki zake kuwa Maua anamahusiano na jamaa mmoja ofisini kwake na ndipo siku moja akamjia rafiki yake na kumwambia kuwa kweli amehakikisha hilo kwa macho yake mwenyewe, na ili ahakikishe mwenywe inabidi kufanya uchunguzi, na yupo tayari kumsaidia kwa hilo. Safari hii Maneno hakukaidi kama ilivyo kuwa awali, kwani awali aliwaona kama watu wanaomuonea wivu. Akakubalina na hilo na fumanizi au kutafuta ushahidi kukafanikiwa.
 Siku moja baada ya kazi  Maua aliamua kurudi nyumbani mapema , haikuwa kawaida yake kurudi mapema hivyo, alipofika eneo la nyumba yao, alisimamisha gari na kutoka, akitaraji mume wake angekuja kumpokea kama ilivyokuwa kawaida yake , lakini hakutokea hivyo, akawaza nini kimetokea ndani, akachukua mkoba wake na kuelekea ndani, akafungua mlango na kuingia ndani, na akamkuta mume wake kakaa kwenye kochi kashika shavu. Akamwendea na kukaa pembeni mwa mume wake na taratibu akapitisha mikono nyuma ya mgongo wa mume wake na kuanza kumminya minya.
‘Vipi mume wangu unaumwa…mbona haupo katika hali yako ya kawaida leo,…’ akauliza
‘Hapana siumwi, mke wangu ila..najisikia sina raha , maana najiona kama mume bwege, mume ambaye hana mamlaka na mke wake, mume ambaye anafichwa hata …;’ akanyamaza na kumgeukia mke wake
‘Haya yote yametoka wapi tena, nimeshakuambia kuna jambo nafuatilia…hili halikuhusu kabisa…sasa umeanza tena, kwani kuna nini kinaendelea maana watu kama nyie mnanichanganya kichwa changu, mimi nahangaika kutafuta maisha yetu yawe mazuri, mapaka nahatarisha maisha yangu, yote ni kwa ajili yetu…mbona hunielewi, imefikia hatua nakesha usiku na mchana napigika kwa kazi za watu nia kikukuhudumia wewe, ili baadaye familia yetu iwe na maisha bora wewe unawaza mambo ambayo hayapo,…narudia tena Maneno, hili linaloendelea sasa halikuhusu kabisa , vuta subira kama ni lazima nitakuambia…’ akasema kwa hasira, na alipoona Maneno hamuelewi akasimama
‘Wewe sasa naona kuna mtu anakuvimbisha kichwa… au umeshaanza kunichoka na hutaki kuishi na mimi, …maana kila siku unazua mambo mapya…nishakuambia mabadiliko yangu unayoyaona hayakuhusu kabisa, wewe vuta subira, ipo siku nitakuhaadithia, lakini kwa sasa hayakuhusu….na hta ukiyajua hutakuwa na msaada wowote badala yake unaweza ukaharibu kila kitu…aaah, nimechoka, unajua kuchoka…basi nimechoka na udaidisi wako usio na kichwa wala miguu’ akasema na kuinuka kuelekea chumbani.  
‘Kila siku hayanihusu…lini yatanihusu….aaah, ni kweli umechoka na mimi, na hili nimeliona mwenyewe kwa macho yangu, na…ushahidi ninao hapa …kama unabisha njoo uangali …’ alikuwa kaisema akijua mkewe yupo hapo, kumbe alishaondoka na mwisho akasema `…wewe una lako jambo…kama nimekuchaoka au kama umenichoka…’ alijikuta akisema mwenywe huku akiangalia juu na kujiuliza kichwani hivi ndoa ndivyo ilivyo hivi, au ni kwasababu yeye amekuwa kinyume chake, …ooh, kwasababu yeye ni mume wa nyumbani na mkewe ni mfanyakazi.
 Maneno alikaa pale kwa muda akiwaza mambo mengi akiwaza kile alichokishuhudia siku ile, alipopanga na rafiki yake kuwa wakafanya uchunguzi, baada ya kusikia mengi, hakupenda kabisa kufanya jambo lile , lakini baada ya kuona hayo mabadiliko , na hayo majibu ya mkatomkato na pia kusikia maneno ya watu zaidi ya mmoja kuwa mkewe ana mahusiona na jamaa mmoja huko ofisi kwao, akaona lazima achukua hatua hiyo. Wakafanya huo uchunguzi, na kujionea mwenyewe hicho kiitwacho kiota cha mapenzi, na leo ilikuwa siku maalumu aliyoitayarisha kumuonyesha huo ushahidi mkewe na kuwambia kuwa sasa yeey amechoka, anajitoa…akajiluza amfuate mkewe ndani akamwambie haya maneno, akasema kichwani hapana sio wakati muafaka, ngoja ampe nafasi ya kupumzika halafu atamuita, aua atamwendea huko huko chumbani!
 Aliinuka pale alipokuwa amekaa, na kwenda moja kwa moja hadi kwenye kabati lake, alikumbuka kabisa kuwa aliifunga vyema, na kweli pale alipokuwa kaicha CD, yake aliikuta na kuichukua akaiangalia vyema halafu akarudi kukaa pale alipokuwa amekaa mwanzoni.
‘Huu ndio ushahidi…akiuona atakujua kuwa mimi sio mume bwege kama anavyodhania…’ akasema na kuitizama ile CD,..! Akilini akawaza je alichofanya ni jamabo jema, au kachukua hatua isiyo na maana, akasema hapana jahachukua hatua isiyo na maana, kwani ameshuhudia mwenywe …akakumbua jinsi gani alifikia kuchukua hatua hiyo ambayo aliifanya baada ya ushauri, pia baada ya kuona mambo yanazidi kuwa mabaya.
Kwanza baada ya kuona mabadiliko ya mkewe ambayo kwa kiasi kukubwa yameanzia kipindi mkewe alipoanzwa kuumwa na kichwa na hata kufikia kupoteza fahamu na hata kuwa kama zezeta,…hilo alilichukulia kama ugonjwa, lakini hata kabla ya hapo kulikuwa na uvumi ulienea, uvumi huo hakuuchukulia manani sana, ila ulipozidi alichukua baadhi ya hatua ambazo aliona ni muhimu sana kwa maisaha yake ya baadaye. Aliwaza sana matukio yaliyotokea baada ya mkewe kuja siku ile akilalamika kuwa anaumwa kichwa na kushuhuida watu wakitaka kuhatarisha maisha ya mkewe. Je kama mume unayemjali mkeo ungekaa kimya eti sababu hayakuhusu…!
 Alipofikia hapo akaiangalia ile CD, nakuizungusha kidoleni, akakumbuka jinsi rafiki yake alivyoamua kumsaidia kupata huo ushahidi, na ndio uliomfungua macho na kujua kweli kumbe aliyokuwa akiambiwa na watu sio wivu, kumbe kweli mume wake ana mahusioano na bosi wake huko ofisini …akachukua ule mkanda wa CD, akaisogelea `laptop’ yake na kuiwasha ,kiukweli hakuwa na hamu kabisa ya kuungalia ule mkanda kwani mengi  alishayaona mwenywe. Alipopewa ule mkanda na rafiki yake, aliuchukua na kuuweka kwenye kabati lake na kuhakikisha kuwa amefunga vyema. Hakutaka kabisa mtu yoyote auone, na alitaka kama wataachana na mkewe basi yaishie kivyema, labda kama itabidi aliona ni vyema aufikishe huo ushahidi kwa wazazi wa Maua, kwani hali ilivyo hiyo familia inaweza ikamdhalilisha na kumtupa mitaani tena na hata kumnyang’anya kila kitu. Akaushika ule mkanda mkononi akiwa katika dimbwi zito la mawazo…
Tukio hilo lilitokea siku mbili zilizopita akiwa yeye na rafiki yake ambaye alikuja hapo kwake na walipokuwa maongezini walifikia uamuzi huo kuwa apelekwe huko ambapo inasadikiwa kuwa ndipo kwenye kiota cha mapenzi kati ya mkewe na bosi wake. Alishangaa jinsi rafiki yake alivyoweza kupagundua hapo, hakutaka kumuulizia ilikuwaje mapaka akapagundua mahali hapo, labda ni kutokana na kazi yake ambayo ilimbidi awe anatembea sana kuwapata wateja wake.  
Hakupendela kabisa, lakini hakuwa na jinsi, mabadiliko ambayo aliyaona mkewe ali[porudi hospitalini yalimtia mashaka makubwa. Yeye alifurahia kuwa mkewe kapona na kareja nyumbani, lakini haikuwa hivyo, badala ya furaja iligeuka kuwa maisha ya mashaka na mawazo tele…na kutokana na tukio zima, akashawishika kutafuta nini kinaendela katika maisha yake. Wakatoka usiku huo na rafiki yake na ilikuwa mara yake ya kwanza kufanya jambo kama hilo, sio kwamba alimuamini sana mkewe , lakini hakutaka kumuudhi mkewe kwa kumchunguza chunguza, kwani yeye ndiye anayemuweka hapa mjini, …!
 ‘Hata kama ndiye ananiweka hapa mjini, lakini masharti ya ndoa yapo pale pale…lazima nijue undani wa haili jambo…’ akasema kwa sauti na rafiki yake akamwambia asitie shaka atathibitisha hilo muda sio mrefu!     Na alipoambiwa hivyo akajua kweli huko kuna jambo , na kweli rafiki yake anauhakika na anachomwambia, …. na kweli kama ataona kama laivyoambiwa ndio utakuwa mwisho wake na Maua, kwasababu haoni raha tena …na hata hivyo lazima ajitegemee , atamtegemea mkewe mpaka lini.
 ‘Lakini huenda atagundua jambo jingine ambalo likasaidia kuiokoa ndoa yao, na huenda akathibitisha kinyume na anavyosikia toka kwa watu’ akajisema moyoni, na wakwa safarini na alishangaa kuwa walikuwa wakitoka kabisa nje ya mji…alianza kuingiwa na mshaka , ingawaje aliyekuwa naye ni rafiki yake mkubwa, alakini dunia hii imebadilika anaweza akaingizwa mkenge, na alipooona wanazidi kutoka kutoka nje mji akamuuliza rafiki yake kuwa wanakwenda wapi, mbona wanatoka nje ya mji!
‘Hivi wewe unafikiri viota vya mapenzi vinakuwa katikakti ya mji,..ukumbuke yule ni mke wa mtu nay eye ni mume wa mtu, na wote wanaishi kwa mikono ya matajiri…mmoja ni binti wa tajiri na mwingine ni mkwe wa mtoto wa tajiri…kwahiyo wanachukua tahadhari yahali ya juu, vinginevyo wangetafuta hoteli za kitalii wakamalizia huko huko….lakini ngoja tuone , huenda wana miradi yao mingine, ngoja tufike kwanza, wewe tulia, niamini mimi…usitie shaka kabisa, …kwanza tukifika, usihamanike, wewe kazi kubwa niachie mimi, nitafanya mambo yangu halafu nitakuwekea kwenye CD, …Utakuwa ushahidi wako  wa kutosha kabisa …hakafu utanikatia mshiko wangu, sitakudai nyingi sana, ila lazima kwanza mwenyewe ushuhudie na ukabaliane na hilo, kwanza wewe ni rafiki yangu, tunasaidiana kwa hili sio lazima unilipe kwa sasa….’ Akamwambia rafiki yake huku akiongeza mwendo..
Wakafika maeneo yanye majengo ya kifahari, na kila jengo lina eneo kubwa la wazi na kila jengo na eneo zima limezungushiwa ukuta mkubwa kabisa, akasema Maneno kimoyoni huku ni maneno ya mfisadi nini, akacheka na kusema kweli nchi hii ina matajiri, wakati yeye analia atakula nini , taishije wengine wanafikiria watajenga mjengo gani ….akawa anayaangalia yale majengo mapaka akajisahau kuwa anapekwa wapi.
‘Tumefika, jengo lenyewe ndio hili hapa, wanamalizia ukuta , lakini nyumba ndani safi kabisa, ina kila kitu kama hotelini vile…niliwahi kuingia hapa siku moja wakati wakiwa na sherehe za kifamilia, wakati huo nilikuwa nakutafuta upo wapi, na nilipoambiwa umeolewa na huyu mtoto, nikakuonea huruma sana, kwani hamuendani kabisa…najua mlitoka naye mbali lakini yale mapenzi yalikuwa ya kitoto…kumbe mwenzangu ulikuwa umedhamiria…sawa sasa tunatakiwa tuingie ndani, na kazi kama hii haitakiwi kupitia getini, twende huku kwa nyuma nitakuonyesha sehemu ya kuingilia ndani kuna mti mkubwa sana kwa nje, lakini matawi yake yameingia hadi ndani na kukutana na matawi ya mti mwingine kwa ndani, unapanda huo mti halafu unashuka kwa kutumia matawi yake kwenye mti uliopo ndani, kama unaogopa ningojee huku nje.
‘Hapana lazima nione kwa macho yangu mwenyewe, tutaingia pamoja…’ akasema Maneno
‘Sawa kabisa twende , maana usije ukasema nimeutengeneza huo mkanda, twende haraka…’ akasema rafiki yake, na wakapanad ule mti na kujikuta wapo ndani ya eneo la hilo ambalo aliambiwa ni moja ya majengo ya baba yake Maua. Akaliangalia lile jengo lililopo mebele yake na kuingia na mawazo kuwa kama ni mali ya Maua kapewa na baba yake, basi hata yeye alistahili kuonyeshwa, mbona hajawahi kuonyeshwa hilo jengo…ama kweli yeye kawekwa tu kama mfanyakazi wa nyumbani, sio mume…akajisema moyoni.
 Alimkumbuka rafiki yake ambaye mara kwa mara alikuwa akimtembelea , rafiki yake alimnhauri mengi, na moja wapo alimwambia kuwa ajaribi kuona mbali, awekeze… na katika maongezi yao wakajikuta wanaongela hilo la mkewe, na mwenzake akamhadithia mengi ambayo anayajua kuhusu mkewe, na kuwa yeye amewahi kumshuhudia wakiwa na mpenzi wake huyo, na siku moja alikuwa kalewa sana na aliwaona wakilambana midomo hadharani. Na kama anabisha yupo tayari kumpeleka, wapi wanapokutana. Alikosna kabisa na rafiki yake huyo na ndipo akaja huyu kumwambia swla hilo hilo, aliyakumbuka sana maneno yake ya mwanzoni alimwambia hivi;.
‘Rafiki yangu, sio kwamba naingilia maisha yako, lakini nimegundua kitu ambacho nikikuambia hutaamini, unajua tena kazi yangu hii ya kupiga picha, inanifanya niingie sehemu mbalimbali, basi siku kadhaa nimemgundua shemeji akiwa maeneo nyeti na jamaa, na jamaa huyo kama sikosei ni bosi wa kampuni yao, huwa wanatalii hoteli kubwa kubwa, basi siku mmoja niliwafuma wakiwa wamekumbatiana, ile ya kimapenzi, siunaijua …mdomo kwa mdomo…nilivumilia sana, mara ya kwanza, lakini nilipowaona mara ya pili nikasema nitakuambia tu, kazi iwe kwako…’ akamwambia rafiki yake.
 Na ndipo mambo haya yalipozidi kuwa mabaya ndipo akaamua kumchunguza mtoto wa nyoka, akijua kabisa kuwa akikosea ajue sumu ya nyoka itammaliza, na kama kweli kuna ushahidi ni rahisi kumkwepa nyoka huyu na madhara atayakwepa …na kikubwa alichelea miradi aliyowekeza huenda ikataifishwa kama atakuwa hana ushahidi na wakati huo keshalikoroga. Na kitu kilichomshinikiza zaidi ni hizo kazi za usiku ambazo amegundua kabisa kuwa hazipo, haiwezekani ziwepo na dereva wao asijue, hilo, lazima kuna jambo, akakubalina na rafiki yake huyo kuwa amsaidie kufanya uchunguzi.
‘Sio nikusaidie, twende leo hii hii..ukashuhudie jinsi gani mkewe anavyoliwa kiaina, wewe unakalia kusugua masufuri hapa nyumbani…tatizo lako umeolewa, kama kweli ungelikuwa ume-OA, usingeganda hapa nyumbani, chakarika na maisha huta…’ akasema maneno mengi ambayo Maneno hakuyasikiliza kwani alikuwa katingwa na mawazo…hapo ndipo alipokubaliana kuwa siku hiyo waongozane na akajionee mwenyewe!

‘Unasikia rafiki yangu  `dawa ya moto ni nini?’ akasema huyo rafiki wa Maneno , lakini Maneno hakujibu kwa sauti alijibu kimoyomoyo kwani alikuwa bado hajaamini kuwa kuna ukweli kama huo, haiwezekani kwa mtu kama Maua amfanyie hivyo, lazima athibitishe hilo kwa macho yake menyewe! Wakati wanapanda ukuta akili yake ilikuwa mbali, kwani alikumbuka sana ushauri wa rafiki yake, aliyemshauri kuwa anatakiwa kuona mbele,
 `Kama ulivyosema kuwa humuamini tena mke wako, na hili tulikuambia tangu mapema, ukatuzania kuwa tunakuonea wivu. Kama umeliona hilo, nakushauri kuwa ufanye mambo kia-akili, kwanza  kabla hamjakorofishana, wewe hakikisha unakuwa na vitu vya kuanzia maisha, nunua kila kitu na weka mahali, au panga chumba na hifadhi vitu vyako, wekeza biashara ambayo utamuajiri mtu, ili hata ukitimuliwa hapa unajua wapi pa kuanzia maisha….’ Alishukuru sana ushauri huo wa rafiki yake, kwani asingekuwa yeye, angelikuwa bado hana hata cha kuanzia maisha kama wakitibuana na mkewe.
 ‘Kweli lazima niwe na malengo, kwanza nishawekeza, pili natakiwa kuthibitisha huu uvumi na tatu natakiwa nichukue hatua…, lakini je itakuwa rahisi kama awazavyo
Na kweli Maneno bila ajizi akaanza kuchakarika na wakati huo ilikuwa hali haijafikia tete kama ilivyo sasa, hakujua kabisa nini kinaendelea kati ya Mkewe na Bosi wake, na hata alipokuja huyu rafiki yake aliyemtaka akathibitishe, hakutaka kuwambia kuwa alishafanya mengi sana kwa ajili ya maisha yake ya baadaye,…alikuwa keshaanzisha bishara ambayo alimuajiri mtu , na huyo mtu alikuwa mwaminifu sana kwake akawa anafanya vizuri sana, kiasi kwamba hata Maneno alishangaa, kwani yeye mwenyewe alikuwa kila akifanya biashara inapukutika kama gunzi la mahindi na anabakia hana kitu. Sio kwamba alikuwa kabisa hajui misingi ya biashara, aliijua vyema kabisa, lakini alikuwa hana bahati na biashara. 
 Yeye alichofanya na kumtumia kijana aliyemuajiri, na akawa anamlipa na hili lilikuwa siri yake, na alihakikisha kabisa mkewe hajui hata rafiki zake waliomshauri walikuwa hawajui hilo kabisa.. Na hata hivyo hakuishia hapo , alikuwa na malengo marefu ya kununua kiwanja, ili ikibidi ajenge kibanda chake, nalo likafanikiwa kwa muda mfupi tu…ndio kitu ambacho alimpendea Maua kuwa kila akiomba fedha, anapewea na haulizwi ni za nini…
 ‘Sasa hatua ya pili imefika ni hatua ngumu sana, lakini bila hatua hii siwezi kuachana na huu utumwa, kweli nampenda mke wang, lakini kweli ananipenda kama ninavyomepnda, kweli kuna mapenzi ya namna hiyo, kuwa msiri…na…ngoja lazima leo nikahakikishe mwenyewe…’ akasema huku wanaondoka na rafiki yake kueleeka huko alikoagizwa. Alifanya hilo akikumbuka maneno ya baba mkwe wake ambaye alimwambia familia hiyo haihitaji kashifa, na kama atagundua kuwa mkewe anakashifa mbaya asisite kumpeleka vielezeo kamili. Na hapa yupo mbioni kutafuta hivyo vielelezo.
 Wakawa ndani ya ukuta na wakati huo jamaa yake alikuwa akiangalia huku nakule, huku anajaribu kamera yake, lakini kwa Maneno akili yake ilikuwa mbali kabisa alikuwa akiwaza sana  na sasa likuwa akimfikiria Maua kuwa ni mtu waliyetoka naye mbali, haiwezekani afikie haraka kumsailiti,…au kwasababau yeye ni baba wa nyumbani tu, na huenda hajui mapenzi ya kisasa…basi kama anafanya hivyo…ngoja nitafute vielelezo ili mwisho wa siku abakie na huyo anayejua mapenzi ya kisasa, kwani hivi sasa nitaamuaje kuoachana na yeye bila ushahidi kamili.
 Akarudisha akili yake na kumwangali arafiki yake akiwa anaweka kitu kwenye kamera yake hiyo, alikuwa tayari na kumsogela Maneno akawa anataka kumwambia kitu Maneno lakini akasita kidgo na kusogea mbele kuangalia kitu, alipoangalia kule jengo kwa muda akaridhika kuwa hakuna mtu kwenye hilo jengo, akamsogelea Maneno na kumwambia,
‘Sasa mimi naingia ndani ya ile nyumba, natakiwa niingie nitafute sehemu ya kujificha, na natakiwa kuweka baadhi ya vitu ambavyo vitanasa matendo yao, siku hizi tekinolojia ni pana, unaweza ukaweka vifaa kama hivi halafu ukatulia sehemu moja uakwa unaona yote na kuyarekodi, inaweza ikatoka vyema , kabisa, ila ikibidi itanibidi nifuatilie kila tendo, lakini ni hatari kidogo….wewe kaa hapa, kama ukiona jambo la hatari unatakiwa utafute njia ya kunisaidia …lakini sidhani kama kuna hatari yoyote, wewe tega sikio ….
Maneni akaitikia kwa kichwa na akilini akasema,, `ngoja nitafute vieleze na hata ikibidi ninaweza kumuonyeshe baba ymkwe wake, na kama baba yake ni mkweli kama alivyomwambia siku hiyo, basi atakuwa hana hatia tena…nitasalamika, nitasalamika hata wakigundua kuwa nina bishara zangu na kibanda changu..’ akasema kimoyomoyo. Akawaza pia akiwa na ushahidi mzito, anaweza akamchezea shere mkewe kuwa kama akinimletea nyodo, atampa baba yake huo ushahidi na yeye anaweza kukosa urithi au chochote kutoka kwa baba yake.
‘Kuna kazi moja ya kusubiri, unatakiwa kusubiri sana, kwani sasa ni saa nne, ilitakiwa saa hizi wameshafika, lakini kwa taarifa niliyoipata kwa jama a yetu bado wanaruka majoka, wanacheza mziki, na nina uhakika wakitoka huko watakuwa wamelewa, na wakifika hapa wataishia kulala, au kufanya ….’ Akasita kumalizia akampiga Maneno mabegani na kuongezea kusema, `usijali hayo ndiyo maisha ….’ Na akaanza kuondoka kuelekea huko kwenye jengo, na kumuacha Maneno akiwa kazama kwenye mawazo.
 Haikuchukua muda kwani kweli lipofika saa nne na dakika 40  gari mbili zikafika kwenye ile nyumba zikiwa zimeongozana, na mojawapo ni gari jekundu ambalo mke wake Maua analipenda sana. Kwenye gari hilo la pili akashuka jamaa mmoja, akiwa na mfuko ambao hubeba komputa ndogo, na aliposhuka alikwenda moja kwa moja hadi lile gari jekundu akafungua mlango na akatokea mke wa Maneno akiwa kavaa kagauni kafupi, nafkiri ndio maalumu kwa usiku, kwani kama angevaa ile nguo mchana ingekuwa ni aibu tupu. Maneno aliona hata aibu kumtizama, ina maana mke wake kabadilika kiasi hiki…
Yule jamaa akamkumbatia mke wa Maua huku akitizama huku na kule kama vile anajua kuna watu wanawatizama halafu akambusu shavuni, walifanya vile kwa muda kama vile walikuwa wakionyesha watu kuwa wao ni wapenzi wa kwelikweli. Nafikiri walikuwa hawana wasiwasi kabisa kuwa wapo peke yao na hakuna mtu wa kuwafuatilia. Pale Maneno aliposimama hasira, wivu , na chuki vilinijaa moyoni, alitaka akimbie hadi pale na kufanya kitu mbaya, lakini alikumbuka ushauri wa rafiki yake kuwa asihamanike, pale muhimu ni kukusanya ushahidi…!
 Maneno alimuona Jamaa yake kwa mbali, akiwa mafichoni na alimuona jinsi gani alivyokuwa akihangaika kuchukua picha, huku akiwa mafichoni, na ilivyoonekana alionyesha jinsi gani alivyokuwa mahiri kwa kazi hiyo, na anaonyesha kuwa sio mara ya kwanza kufanya kazi kama ile, kwani alikuwa mwepesi na alikuwa na tahadhari ya hali ya juu. Maneno alikuwa na kazi mbili, kwanza anatupa jicho kwa rafiki yake hakafu anawaangalia wale wezi wa ndoa za watu, ambao walishaanza kuondoka kwenye mgari yao na kuelekea mlango wa ile nyumba na walisimama kidogo kuongea jambo, halafu wakaingia ndani.
Mara yule mwanaume akatoka kurudi kwenye gari, na akaingia kwenye gari lake hapo Maneno akahisi kuwa huenda huyo jamaa alikuwa akiondoka, lakini haikuwa hivyo, alisogeza gari lake maeneo ya ndani , sehemu wanapoegesha magari, halafu akatoka na kuingia gari la mke wangu na kulisogeza hivyo hivyo.
 Kule mlangoni, Maneno alishangaa, kwani jamaa yake alifanya jambo la hatari, alimuona akifungua mlango wa ile nyumba na akaingia ndani. Maneno yeye alikuwa akihema kwa woga,alikuwa akiogopa utafikiri ndiye yeye aliyeingia  kwenye ile nyumba, akiwa na wasiwasi kuwa anaweza kukamatwa. Na baadaye Bosi akatokea kule alipoyaweka magari na kuelekea kwenye mlango wa ile nyumba, na kuingia ndani na kufunga malngo. Hapo Maneno akawa na wasi wasi akijiuliza kama mlango umefungwa jamaa yake atatokaje mle ndani,..akabakia kusubiri…alisubiri mapaka akaingiwa na wasiwasi….
 Mbu, baridi uwoga vikawa vinamuandama Maneno pale alipokuwa kajificha, mwili ulikufa ganzi kwa baridi lakini aliendelea kusubiri hadi ikafika saa sita! Maneno akawa Kahoka kabisa, na usingizi ukaanza kumnyemelea, Lakini mbu hawakumpa nafasi hiyo…., ingawaje kazi kama hizi za kusubiri, kuumwa na mbu alishawahi kuziifanya sana, lakini kwasababu ya kudekezwa na huyu mwanamke, mke wake alishaanza kusahau taabu hizo.
 Akiwa anahangaika na mbu mara ghafla akaona mlango ukifunguliwa, na aliyetoka mle ni Bosi, alikuwa kama anakagua kitu kwani alikuwa akizunguka zunguka , nafikiri walihisi kitu fulani. Nami nikaona nimsaidia jamaa yangu , nikaokota kigogo na kukirusha nyuma ya nyumba, kilitoa kelele na kumfanya jamaa ashituke, na kubaki kaduwaa. Aliangalia huku na kule kama ana wasi wasi fulani na baadaye akaeleeka huko nyuma aliposikia huo mlio.
 Alionekana kuhisi kuwa kuna kitu , kwahiyo akawa ananyemelea kuelekea kule sauti ilipotokea, na wakati ananyemelea hivyo, yule jamaa yangu mpiga picha akatokea mlangoni na harakaharaka akaja kuelekea nje ya jengo, kumbe yule jamaa kamuona, akawa anamfuata kwa haraka kwa nyuma na mpiga alipoona hivyo  ikabidi aanze kutimua mbio.
Wakati anatimua mbio Maneno aliona kuna kitu kimedondoka kutoka kwa mpiga picha, hapo  Maneno akaona kuna haja ya kusaidia tena, akachukua kigogo kingine na kukirusha sehemu nyingine na kumfanya Bosi asimame ghafla, akijua kuwa yule jamaa aliyekuwa akimkimbiza hayupo peke yake, kuna wengine upande mwigine, akaangalia huku na kule kuhakikisha, na alipokuwa akitiza hivyo, bila kuona mtu...akasimama kutafakari, na wakati anatafakari mara macho yake yakatua kwenye kile kitu alichodondosha yule mpiga picha ,akakiokota na kukitizama…huku anaangalia huku na kule kwa kujiiba, na alisimama  pale kwa muda akitafakari la kufanya. Haikuchukua muda, akaanza kufutilia kule aliposikia mlio akatizama kwa muda eneo lote, halafu akarudi hadi kwenye geti la mlango, na alipohakikisha hakuna kweli hakuna mtu, akaamua kurejea kwenye ndani, alisogea hadi mlangoni, akageuka haraka kama vile aliona kitu na kutizama huku na kule  akasimama hapo kwa muda kidogo baadaye akafungua mlango na kuingia ndani….

NB Naomba samahani sana kuwa nimeunganisha sehemu mbili kwa wakati mmoja, niligundua hili nikiwa nimeshaiweka hewani, na nikaona haina haja kuiondoa sehemu hiyo! Naomba maoni yenu kama ipo sawa ...!, ...Tuendelee kuwepo
Ni mimi: emu-three
Enhanced by Zemanta

13 comments :

Anonymous said...

Hamna cha samahani mkuu, hapa umetupa uhondo, ila inabidi tukasomee home kwanza,...safi sana fanya hivi kila siku

emu-three said...

'Anoy' nshukuru kwa kuwa mtu wa kwanza kunipa moyo, maana niliona nimepitiliza...kama ipo poa, basi twende pamoja, kwani ndio tumerudi kule tulipoanzia ili story kuleta lile tukio lenyewe, na baadaye ....mtaona nini kitafuatia..KARIBUNI SANA, TUPO PAMOJA DAIMA

samira said...

m3 hujakosea bil samahani kwani umetukumbushia pia ya zamani tulipoanzia
mimi nakuunga mkono sasa maneno sijuwi atachukua hatua gani
cant wait

Candy1 said...

oooh ndio maana nikawa najiuliza "leo mbona uhondo double double" hahaha its absolutely fine M3, nimependa vile tumeanganishwa na kule mwanzo kidogo na sasa ndio nazidi kuelewa...haya tuone plans za Maneno zitafikia wapi...Maua&Bosi na kundi la hatari...nipo kama kawa

Anonymous said...

Mmm!!! M3 2po pamoja, ya leo ni nzuri sana nimependa ulivyounganisha kama wasemavyo wadau hapo juu.

Kwa kweli Maneno na huo rafikie watafikia kweli marengo yao. Isije wakaonekana wao ndio chanjo cha matatizo? Kwani Maua na Boss wake pia wapo kwenye uchunguzi.

Sasa kazi kwelikweli.

Haya 2po pamoja.

BN

Swahili na Waswahili said...

Huu Moto siwa makaratasi wangu, Pamoja ndugu!!!!!

emu-three said...

Msinione kimiya afya kidogo inaleta mgogoro .

Anonymous said...

Yaan leo nilitaka kujua kulikonin mbona kimya? kufungua kwenye maoni nakutana na jibu lako.

POLEEEEEEEEE MKUU. NI ZAID TENA.
TUNAKUOMBEA KWA MUNGU AKUPONYE UPESI.

TUPO PAMOJA BOSS, TUNAKU-MIS MNOOOO.

GET WELL SOON.

BN

samira said...

get well soon m3 nilikuwa najiuliza kulikoni leo nimeangalia comment ndo nimeelewa
pole sana

SIMON KITURURU said...

Ipo sawa Mkuu!

Na tupo kama kawa!

Candy1 said...

Ooooh ugua pole mtu wangu :-)

SIMON KITURURU said...

Pole Mkuu kwa kuugua!

emu-three said...

NASHUKURUNI SANA KWA POLE ZENU NA DUA ZENU, KWANI SASA NAJISIKIA NAFUU, Na nikiwa kitandani nilikuwa nawaza sana kuhusu tatizo hili la Malaria, kwani wakati nimepumzika alipta jamaa akinyunyuzia dawa za kuua mbu, lakini tunatakiwa kutoa pesa...nii sawa, lazima tuchangie, ila nahisi kama dawa hizo zina ubora unaotakiwa au ndio zimechakachuliwa.
Kwa ujumla KINGA NI BORA KULIKO TIBA. Juhudi kama hizi zingetakiwa sana ili kupambana na hawa wadudu mbu, ni bora hata kuliko kugawa neti...Neti zigawiwe sawa kabisa, lakini juhudi kubwa ipelekwe kwenye kuodnoa kiinii cha mazalia ya hawa wadudu.
TUPO PAMOJA WAPENDWA WANGU!