Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, December 20, 2010

Aisifuye mvua imemnyea-13

  
  ‘Wewe nani…’ Maua akauliza kwa wasiwasi na aliyegonga akawa kimya kidogo halafu akagonga tena. Na maua akarudia kuuliza, na huyo mtu akajibu, alipojibu, Rose akainuka harakaharaka pale alipokaa kwenye kiti na kuonyesha uso wa wasiwasi…


              Je ni nani huyo! Na kwanini Rose ashituke kiasi hicho,tuendelee kuwepo!

            ** Kabla ya kupata jibu hilo, hebu tumrudie doctor, kwani alikuwa kapoteza fahamu**

Alijitahidi kujizuia kwa kufumbua macho, lakini yalikuwa mazito kufumbua, na muda ule akajiona anapaishwa juu kwa juu, na kutoa sehemu yenye majani mengi, na fahamu zilikuwa zikimuelezea mazingira ya mahala hapo, aliona makaburi yakiwa yamejipanga huku na kule nay eye alitua juu ya kaburi moja, lilojengewa vizuri, lakini limebomoka katikakati. Akajaribu kutizama ina la mwenye kaburi hilo lakini maandishi yalikuwa hayaonekani.

Kwa muda ule mwili ulikuwa kama si wake, alikuwa akiyajua mambo kwa hisia kama mtu aliyepo ndotoni, kwani licha ya kuona nilichokiona, sikuweza kutamka kitu..’ akasema docta. ‘ila moyo uliingiwa na wasiwasi, kwani sura iliyokuwepo mbele yangu ilikuwa ya kutisha ajabu na sikujua ilikujaje, ilikuwa ikipanuka kila wakati na kuwa mtu mwenye umbo kubwa na alipopanua mdomo wake na kuacha meno wazi, nilijua kabisa huyu sio mtu wa kawaida. Alikuwa anakua kama mwanamke baadaye anabdilika na kuwa kama mwanaume...!

Meno yake yalikuwa marefu, sura yake ya kutisha na aliyoongea yalikuwa kama wangwi, yaani yanakuja kwa kasi na kufifia kila neno analotamka. Nilitaka kujiinua kwa nguvu, lakini nilikuwa kama mtu aliyefungwa minyororo mikubwa ya chuma. Sikuweza kusogeza hata kidole, zaidi ya hisia tu, kama vile upo ndani ya ndoto!

‘Wewe kijana, usijaribu kuchezea yale yasiyochezewa, nakupa onyo la mwisho, kwani huyu mnayesumbuana naye ni mtu mdogo tu kwetu, na kwa taarifa yako, yeye anayofanya ni yake, hana msaada wowote kutoka kwetu. Sisi hatujafanya lolote hadi sasa, kumsaidia kwani alikiuka miiko ya familia hii. Sisis eneo hili ni letu, tulilorithi miaka mingi na hapa mizimu yetu ndipo inapoishi, na mkilichukua mnataka twende wapi?

Sasa sikiliza, tutakupa hadi mwisho wa mwaka uwe umeuza nyumba hii na utafute eneo jingine, wateja utapata wengi, ukiamua tu hata kesho wateja wapo. Lakini najua kiburi chenu wanadamu, utataka uone nini kitatokea,basi subiri mapaka mwaka uishe, utaona vumbi letu. Kazi kubwa utaifanya wewe mwenyewe, na mwisho wa siku utajiangamiza wewe mwenyewe…’ akacheka na kupenua meno yake ya kishetani, halafu akatoweka.

Nilijaribu kuangaza macho, lakini yalikuwa mazito, na ile taswira ya yule mtu ilikuwa inaonekana kila mahala, sio yeye tu walionekana watu wengi kama yeye wenye sura kama yeye wamemzunguka. Ilichukua dakika chache, sijiwezi, naona maajabu mengi, mara najiona kama nipo makaburini mara yanatoke ahayo masura , mengine yananitishia kunitafuana. Na ghafla nikaona mwanga, na nikaweza kufumbua macho vizurii …

‘Vipi docta, naoan jamaa walikuchukua kidogo, hawo tunawajua, hawana lolote, kazi kubwa tumeimaliza, wao hawo nia yao ni kukuogofya, tutapambana nao. ..’ huyu alikua mtaalamu, akinipungapunga na vitu kama manyoya kichwani, niliisikia ile harufu ya mwanzo, halafu ikapita, nikapiga chafya na haraka nikainuka pale nilipokuwa nimelala.

‘Kwani imekuwaje, mbona nilikuwa kama nimepelekwa makaburini…hata naona ilikuwa ndoto..’ nikapikicha macho na kutembeatembea, nikiwaza yale niliyoambiwa na yule mwanamke, sijui ndilo shetani au ni kitu gani. Nikawaza, kuhusu vile vitisho, nikadharau, nikajisemea, kama wao wanadaikuwa ni eneo lao, wanionyeshe vithibitisho, …mimi sigopi kitu!

Yule mtaalamu na watu wake wakafanya mambo yao, na baadaye aliwaruhusu mafundi wasafishe na kuendelea na mambo yao.

‘Kazi imekwisha, nyumba sasa ni yako, madude yote yaliyokuwepo humu yameteketea, kinachotakiwa ni kumalizia maswala machache na hili tutaliongelea baadaye, kwahiyo baada ya kumaliza hayo mambo machache utaruhusiwa kuingia kwenye nyumba yako. Sisi kazi kama hii tumeifanya sana, na huenda utaendelea kuota manjozi ya ajabu, hiyo ni kawaida ni vitisho vyao, lakini hawawezi kukufanya kitu..’ akasema na kucheka.

Baada ya tukio hilo, tukarudi nuyumbanai na wale wataalmu wakaondoka. Niliwaambia wazazi wangu kuwa lile tatizo limekwisha kwahiyo kinachosubiriwa na kuhamia tu, ila sitahamia mapaka niwe nimempata mwenzangu. Na nilipowatajia hilo na kuwa na mwenzangu wazazi walifurahi sana, na walitaka kujua huyoo mwenzangu ni nani. Nikawaambia siku itafika nitawaeleza ni nani…Turudi kule kwa mabinti wawili. Waliposikia hadi waliduwaa, na Rose akashikwa na butwaa, kwani sauti aliyoiskia ilikuwa nay a mtu aliyemsumbua akili yake, na hakujua kuwa atakuja hapo nyumbani, wakati wameshakorofishana, alikumbuka maneno aliyomwambia Maua, na aliogopa Maua asije akayaropoka.

‘Fungua, aingie, na …naomba tuachie nafasi, wewe kaa huko jikoni mapaka nitakapokuhitaji..’ akasema Rose. Na Maua akataka kufungua malango, lakini akasita na kuondoka kuelekea jikoni, Rose alipoona Maua kaondoka, akainuka akajitengeneza vizuri halafu akauendela mlango na kuufungua.

‘Umemfuta Maua au umekuja kuniona mimi?’ lilikuwa swali la kwanza la Rose, na aliyesimama mbele yake akacheka, na akachungulia ndani, na kuangaza huku na kule, alikuwa akimtafuta aliyemfikiria, lakini aliona mle ndani hayupo.

‘Hivi Rose, niliwahi kuongea na wewe kuwa nakutaka urafiki na wewe?’ Docta akamuuliza, na akawa kaficha kitu nyuma, ambacho hakutaka Rose akione.

‘Ina maana yale yote ul;iyokuwa ukinionyesha haikuwa na maana yoyote kuhusu mimi…yaani wewe ulitaka kunipotezea muda, au..’ akasema Rose.

‘Sikiliza Rose, wewe unasoma, na mimi nisingependa kukupotezea muda wako, mimi wewe nakuona kama mdogo wangu, nitakuwa nafanya kosa sana kukuchanganya na maswala ya kikubwa, wewe soma kwanza mambo mengine yatafuata…’ akasema huku anaangaza mle ndani,

‘Wewe unamtafuta nani , kama ni Maua kehsondoka, kamfuata Docta wake, hapa nipo peke yangu…kama hukuja kwa ajili yangu ondoka…’ akasema Rose. Na jamaa akacheka sana, kwani sauti ya Maua anaijua hata akiwa usingizini, aliyeitikia mwanzoni alikuwa Maua.

‘Tafadhali nakuomba, najua Maua yupo ndani, nina maongezi naye muhimu sana, niitie, nikimalizana naye tutaongea maswala yetu, kwani masomo yanakwendaje, naomba usichanganye masomo na mapenzi, mimi ni mwalimu mwema, na sipendi kukuharibia maisha yako, naomba niitie Maua…’ akasema kwa sauti ya kuamrisha. Na Rose akaona haina maana kubishana naye akainuka na kukimbilia chumbani kwake. Na baaadaye Maua akajitokeza.

Dakitari alimwangalia yule mrembo akasema moyoni, huyu lazima nimpate, lazima nimshawishi hadi awe mke wangu, lazima, kwa udi na uvumba. Akaingia ndani na mkonono akatoa kile alichokuwa amekificha na kumkabidhi Maua. Maua akapokea, hakujua nini maana yake, akauliza apelike wapi mzigo ule.

‘Hiyo nizawadi yako, ni maua yaliyotengenezwa kama moyo, kuonyesha nini namaanisha,…naomba maongezi muhimu na wewe, na ninachotaka kukumabia ni muhimu sana, kwangu na kwako, na naomba ulifikirie sana jambo hili. Maua, tangu nilipokuana siku aile, moyo wangu umekuwa ukitamanai sana uwe mwenza wangu, nimewaona mabinti wengi. Wanawake wengi, lakini moyo wangu umahakikisha kuwa wewe ndio chaguo langu. Sitaki nikupotezee muda wako, ila naomba, unikubalie ombi langu la uchumba…nakupenda sana Maua, na upendo wangu kwako sio wa hivihivi, ila wa kuwa mke wangu…naomba usinijibu sasa, kaa ufikirie, na ujue umuhimu wa jambo hili. Maisha yako kama nilivyosikia yamepitia mitihani mingi, sasa muda wa kuaga hiyo mitihani imefika, huna haja ya kusononeka tena. …kesho nitakuja kusikia kauli yako…’akamsogelea na kumshika mikono yake na kumwangalia machoni kwa muda, alitamani kufanya tendo Fulani lakini akaona huenda akavuruga kila kitu akamwachia Maua na kuondoka zake.

Maua alisimama akiwa ameduwaa, akatabasamu, akaiangalia ile zawadi, na kuifunua akakuta kweli maua ya thamani yaliyotengenezwa mfano wa moyo, akayanusa, na yalikuwa na harufu nzuri, akatabasamu na kusema, kweli labda muda wa matatizo umekwisha, kweli huyu ana nia njema, kweli huyu ananipenda kwa dhati kwani kanitamkia mwenyewe, hakuna mwanamume aliyekua kumtamkia hivyo, kuwa anampenda na zaidi anataka awe…sio mchumba tu awe mke wake.

‘Jamani namshukuru Mungu, hatimaye na mimi naonekana mtu…haina haja ya kupoteza muda akija kesho nitamwambia nimemkubali…. ‘

Akajirusha kwenye kochi na kuiweka ile zawadi kifuani mwake, na kabla hajatulia vyema simu ya mezani ikalia, akasita kuinuka kuipokea…nani huyu tena, jamani anataka kuniharibia furaha yangu. Ilivyoendeela kulia, akainuka haraka na kuiinua kuipokea akiwa na mashaka, kuwa ni nani anapiga mida kama hiyo, na mawazo yake yakawa labda baba na mama mwenye nyumba ndio wanaopiga. Akaiweka sikioni, na kusubiri asikie sauti ya kutoka huko;

‘Halloh….’ Akasikia sauti ikisema hivyo, hii sio sauti ya…ya…, looh, sauti ..ile sauti..looh, akapumua kwa nguvu na kuiweka vizuri sikioni, huku akiwa na kigugumizi cha kujibu, ..!

Ni nani huyu tena, je ataiharibu furaha ya Maua, na nini kitaendelea baadaye, tuendelee kuwepo!

Ni mimi: emu-three

10 comments :

Pamela said...

ni dr wake kama alivyosema Rose hapo watamchanganya tuu marafiki wanampenda mrembo mmoja amekuwa na uwezo wa kusema wakati mwingine domo zege!! nimekifurahia kipande cha leo nasubiri ufumbuzi wa fumbo hili m3 kazi nzuri

chib said...

Ukiweza, andaa tungo zote, weka kwenye kitabu, na kiuze. Mimi mteja namba 1

emu-three said...

Nashukuru sana Chib kwa kunipa matumaini haya, kuwa utakuwa mteja namba moja kama nikitoa kitabu. Nitajitahidi kufanya hivyo, kwani kwenye kitabu nitakuwa na nafasi ya kuelezea kwa undani zaidi kuliko hapa kwenye mtandao, wakati mwingine inabidi ufupishe...
Ahsanteni sana kama kweli mnakubali kazi hii!

elisa said...

mimi nitakua mteja no 2, mimi napenda kusoma mikasa/hadithi sana sana..sijui ulikua wapi siku zote hizo ..lol

emu-three said...

Elisa nilikuwepo, hata ukiangalia blog imeanzishwa muda lakini nilikuwa sijulikani, nashukuru sasa mumeniona, tutakuwa sambamba, tuombe uzima na sehemu ya kujishikiza.
Karibuni sana!

Candy1 said...

Kwanza huyu docta mbishiiii!!! Kha!!!! Sasa ubishi wake sijui ndio vizuri ama vibaya hata sielewi hahahaha...haya, tumuone bibie Maua in loooooove...mi nipo as usual :-)

Pamela said...

nAPENDA VISA NA MATUKIO PIA vikiendana na mapenzi kama inawezekana kuwa na wateja namba moja wawili bac na mie ni namba moja!
Kweli candy1 huyu ni dr wa aina yake ubishi gani huu hata huku kwenye maisha wya kawaida tuna watu wabishi wao hata hatari huwa hawaioni...
Tuwemo tuone mrembo wetu atakavyo chachawa lkn mwisho wa siku atakuwa na Dr wake

Albert Paul said...

Kweli dr ni mbishi, tena ubishi wa kimsimamo, si kwenye mambo yake ya kwaida(twaona namna anavyopambana na ulimwengu wa giza) na hata kwenye mapenzi (Rose nae ni mzuri, mrembo na mwenye elimu angalao, tofauti na Maua ambaye hajapitia vidato lakini ni mrembo). Bila shaka anampendea Maua kwa kuwa alishaishi nae na mbali na uzuri, anajua pia ni mchapakazi, labda na huruma ya historia ya maisha yake.

Anonymous said...

Jamani m3, histori zako ni tamu sana. Masikin Rose, Jina la kizungu. lakini Maua kamzidi bao. Asije akamfanyia visasi mwenzake. Mzuri wake usimponze masikini, maua. Sasa huyo Dr wake, akichelewa atapigwa bao na rafiki yake. Na kule kwa wazazi ndio keshatangaza anamleta mchumba.

Sasa nae huyu Dr. anataka nini tena kwenye ile nyumba si aachie tu ngazi.

Haya dada Rose kazi kwako, angalia usije changanya mapenzi na masomo. Pole sana Rose.

BN

Anonymous said...

Du, nimependa the way you are so creative. Kwa stahili hii, siku moja utauza kitabu. Imenipa wazo, kwa sasa niko katika mazingira mapya ambayo yananitatiza na kunishangaza. Ninaanzisha utaratibu kuanzia mwezi ujao, nitahakikisha hadi mwisho wa mwaka nitakuwa nimetimiza kitabu kitakachogusia masuala ya maendeleo ya elimu yetu Tanzania na matatizo yake.