Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, October 19, 2009

Nitajiajirije-sehemu ya kwanza

Nimekuwa nikijiuliza toka naanza kazi, jinsi gani ya kujiajiri ili niondokane na utumwa wa kuajiriwa. Nauita utumwa kwasababu sijawahi kuajiriwa na kupata malipo halali kutokana na kazi niliyowahi kuifanya. Swali hili sikulipatia ufumbuzi, hadi nilipofikia sehemu ambayo imenilazimu niutafute `uajiri’ na hapo nikaukumbuka `uajiriwa’
 Ilinilazimu kwanza niende ofisi za mitaa ili niombe leseni za makazi ambayo niliambiwa ni lazima kabla ya yote, nilipofika nikaambiwa lazima nipate barua ya mjumbe. Barua kwa mjumbe inahitaji mchango wa mhuri na karatasi, nikasema hewala nikatoa. Siku ya pili nikarejea ofisi za mitaa, asubuhi na mapema ili kuwahi foleni. Nikakuta ni mtu wa tano, wapo waliotangulia. Hadi kufikia zamu yangu masaa matatu yalishapita.
`Hii hati ya manunuzi ya kiwanja chako iliyofanywa na mjumbe haikubaliki, ilitakiwa manunuzi yasimamiwe na serikali za mitaa, na ulitakiwa ulipe asilimia kumi ya malipo ya kiwanja. Lakini kwa vile ni muda mrefu umepita utatakiwa ulipe elifu ishirini tu’.
 Baada ya hapo nikapewa hati mpya ya kurekebisha hati ya zamani ya manunuzi ya kiwanja, baada ya kulipa ile shilingi elifu ishirini, ndani ya hati hiyo ya marekebisho unabandika picha ya muuzaji na wewe mnunuzi, ikiwa na maana, nimtafute muuzaji na mashahidi wangu wote akiwemo mjumbe wa wakati huo. Muuzaji alishafariki, sijui hawa mashahidi wengine nitawapataje!
 Ilinichukua siku mbili tena kuikamilisha hii hati mpya iliyojulikana kama `hati ya marekebisho ’ na kurejea tena kwenye ofisi yetu ya mitaa. Hapo nikaambiwa niwatafute majirani zangu ambao walishapata leseni za makazi ili iwe rahisi kugundua sehemu yangu katika ramani ya makazi, hili nilishajiandaa nalo, na lakushangaza nikakuta jina langu lipo kwenye orodha za wanaomiliki maeneo, sasa sikujua huu mlolongo wa mwanzo ulikuwa wa nini!
 Nikapewa hati ya maombi ya leseni ya makazi ambayo nilitakiwa kubandika picha yangu na wengineo kama wapo, mimi nikaona ili familia isipate shida ngoja nibandike na picha ya mke wangu. Nikaambiwa hati hiyo niipeleke kwa mtendaji kata, ili aidhinishe, na hapo nitapewa maagizo mengine. Kwa mtendaji kata? Kufika huko ilibidi nipande magari matatu.
 Nikaona ili nifanikiwe hili, niamuke asubuhi sana, ili nikipata maagizo mengine niyafanyie kazi siku hiyohiyo.  Nilifika kwa mtendaji kata asubuhi na mapema, kwani foleni ilikuwa bado, na kuwakuta wanaandaa ofisi wengine wakipata kifungua kinywa. Tulisubiri kidogo na mke wangu kwani alitakiwa naye awepo ili kuweka saini yake ikihitajika. Hapo tuliambiwa tulipe mchango wa ujenzi wa sekondari shilingi elifu sita. Hapa nilianza kukuna kichwa, kwani sikujua huko mbele nitatakiwa nilipe shilingi ngapi zaidi, na mfuko ulishaanza kutoboka. Hapo nikaambiwa niipeleke hii fomu makao makuu ya wilaya, makao makuu haya yapo mjini. Kutoka hapo ilibidi nipande magari mengine mawili tofauti.
 Tuionelea tupitie TRA, kwani katika ofisi za serikali za mitaa tulipewa hati ya kulipia kodi za majengo, na gharama yake ni shilingi elifu kumi. Tulipofika makao makuu ya TRA, tukaambiwa tukalipie ofisi za wilayani, zilizopo Mnazi mmoja. Tukaonelea tumalizane na maombi ya leseni, kwanza.
 Wilayani tulikuta watu wengi wakiwa na matatizo tofauti, kwahiyo mpaka kupata huduma ilichukua muda. Ile fomu ilipochukuliwa tukaambiwa jina na picha ya mke wangu haitambuliki, kwani kwenye maelezo ya mwanzo hakuwepo! Nilishangaa kusikia maelezo ya mwanzo, wakati sikumbuki kuyawakilisha hayao maelezo. Ikabidi nimuondoe, kwani tuliambiwa kama tunataka awepo inabidi kuanza maombi upya! Baada ya hapo nikaambiwa niende kulipia shilingi elifu kumi na tano mia mbili na arubaini, kama ada ya maombi(10,000/-) na ada ya serikali (5240/-)

 Baada ya kulipia hiyo hela nikaambiwa nirudi baada ya mwezi mmoja, ili kupata leseni ya makazi. Nilienda ofisi za TRA za wilaya nikalipa elifu kumi baada ya kupewa tini namba isiyo ya kibiashara. Kwahiyo kama ninataka bishara(kujiajiri) inabidi nifuate mlolongo mwingine kama huo au zaidi ya huo
 Changamoto ni kwa mlalahoi ambaye umelipwa na muajiri wako mshahara wa mwezi mmoja nakuambiwa kwaheri , Je nitaweza kweli kujiajiri kwa hai kama hii.
Tuwe pamoja kwenye sehemu ya pili Mungu akipenda.

From miram3

2 comments :

Anonymous said...

Usipoangalia vijisenti vyote ulivyolipwa na hawo mabepari vitaishia kwenye kodi, kuna kodi ya city, usafi, vat na nyingine zisizojulikana

Anonymous said...

Pole sana