Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, October 12, 2009

mwisho mwema

Katika maisha yetu ya kila kila siku tunatakiwa tumuombe Mwenyezimungu, na moja ya dua zetu tukumbuke kuomba kupata mwisho mwema. Hii ni dua muhimu kwsababu tumeambiwa siku ya mwisho, siku ya hukumu, tendo lako la mwisho ndilo utakalofufuliwa nalo. Kama ulifia pabaya utafufuliwa kwenye ubaya wako.
Hii hata katika maisha yetu ya kila siku tunayaona, unaweza ukatenda mema mara mia, lakini siku moja ukatenda ubaya, hayo mema yote yanasahaulika. Hata ukiangalia makazini, jaribu kuwa mchapakazi sana, lakini siku ukivuruga hawatakumbuka ule uchapa kazi wako. Angalia waajiri wanavyowafania wafanyakazi wao siku za mwisho wao, je kweli wanawalipa vizuri. Hawawezi kukumbuka kwasababu unaondoka na kuondoka kwako huenda kukawa kwa wema au kwa ubaya!
Tumuombe mungu sana na tumkumbuke kuomba hii dua, ili mwisho wetu katika kila jambo uwe mwisho mwema
From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Tunamuomba mungu akuzidishie mema uendelee kutoa maneno ya hekima