Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, September 29, 2009

Huu ni utumwa wa nguvu kazi

 Kuna kitu ambacho siku nyingi nimekuwa nikijiuliza, na sasa naona niwaulize wenzangu kuhusu kodi zinazokatwa kwa wastaafu au malipo ya mfanyakazi anayeacha au kuachishwa kazi. Kwangu mimi naona ni kama kumuongezea mzigo mtu huyu ambaye amepata pigo la kutokujua hatima yake, bado badalaya kufikiriwa anakong'otwa kodi, tena kodi kubwa kwani kama kila kitu huchanganywa humo.

 Mimi nilionelea kwamba huyu mtu kwa vile anaenda kuanza maisha mapya ya kujitegemea ingefaa kodi asamehewe, au iwe na punguzo fulani, kwasababu ukiangalia kipato cha Watanzania wengi walioajiriwa ni kidogo, labda kwa wale waliobahatika kuwa katika nyadhifa za juu,ambao ndio hawo wengine wanye uweza wa kupendekeza nini kifanyike kwenye sheria za kazi,lakini watajuaje wakati wao wengine wameshajiwekezea.

 Umasikini ni adui mkubwa wa binadamu, na umasikini huu husababishwa na kipato kidogo. Ukiongelea wafanyakazi, mishahara wanayopata ni wa kupitia mkononi hadi mdomoni, na hata mdomoni kwenyewe ni onjaonja tu. Wengi wa wafanyakazi hawa wanapostaafu hawabahatiki kuishi maisha marefu ,kwasababu kipato alichokuwa akipata hakikumwezesha kuwekeza. Sidhani kama angeweza kuwekeza kama kweli alikuwa muadilifu(muda wa kazi +Kipato halali). Wanaobahatika kuwekeza wanakuwa na njia mbadala, na njia nyingine za kujitolea nje ya kazi.

 Jambo jingine kubwa ni kuhusu sheria za mikataba ya ajira zinazotungwa na makampuni binafsi. Sheria hizi zinatungwa na mwajiri akiangalai maslahi yake na akijua kuwa wewe muomba kazi umekuja mikono nyuma,hutakuwa na muda wa kudadisi athari za sheria hizo pindi anapotaka kukuachisha kazi,na haya ndio malengo yake akishirikiana na mwanasheria wake. Nashangaa kwanini hili serikali hawaliangalii kwa makini,ili kuwalinda wananchi wake,kuwa mikataba yoyote ya ajira lazima ipitiwe na vyama vya wafanyakazi, kama wakili au mwanasheria wa muajiriwa! Mkishinikiza kuwa ni mpaka wafanyakazi wajiunge wawe wanachama kwanza wa vyama hivyo inakuwa ngumu kwasababu waajiri wengi wa makampuni binafsi hawataki hivyo vyama!

 Uone jambo la kushangaza, mtu akifa husafirishwa hadi kwao(mikoani) lakini wakati anaachishwa au kustaafu halipwi gharama ya kumpelekanyumbani kwao na mizigo yake(haya yapo kwenye kampuni za watu binafsi)! Je sheria inasema nini, wakati wafanyakazi toka nje wanalipwa hadi nauli za likizo kwenda nchini kwao, lakini sisi hatuna kwetu , kwetu ni Dar! Mkataba ukiisha mshahara mmoja kwaheri,kafie mbele!

 Tunaomba serikali ijaribu kuwalinda wananchi wake hasa kipindi hiki ambacho makampuni mengi yanamilikiwa na wawekezaji ambao uchu wao mkubwa ni faida, bila kujali athari za wafanyakazi wao, na ngao yao kubwa ni kuwa `kama hutaki kazi kwake uondoke'. Basi na serikali nayo iseme kama hutaki kumuajiri mwanachi wangu kwa sheria hizi mama, basi kawekeze kwingine.

 Wasiwasi wangu mkubwa ni kuwa `utumwa' wa nguvu kazi umeshika hatamu hapa nchini kwetu, kipato kidogo, maisha duni na udhaifu wa elimu ya kutambua haki kunawafanya Watanzania kuwa `watumwa'ndani ya nchi yao wenyewe. Kesi ngapi zimekuwa zikiishia hewani mahakama ya kazi, kwa kukosa sheria mama ya kumtetea mfanyakazi huyu aliyekuja kudai haki yake. Tumuombe mungu wahusika hasa wabunge waliangalie hili na kutunga sheria nzuri za kuwalinda wafanyakazi na wanachi kwaujumla, kwani tusipoziba ufa tutakuja jenga ukuta dhaifu kwa kulea taifa la wananchi masikini ndani ya wawekezaji matajiri.

From miram3

No comments :