Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, June 5, 2015

RADHI YA WAZAZI-UTANGULIZI

‘Mnamuona Yule mama kipofu aliyeongozana na Watoto wake watatu, anaishi karibu na nyumba yangu, ni kipofu wa maajabu’ Aliongea mama mmoja na kwa yale Maneno ilibidi kila mmoja ageuze shingo kumwangalie huyo mama, ambaye alikuwa kamshika mtoto mmoja bega kwa ajili ya kumuongoza na mwingine kamshika mkono, Yule mkubwa alikuwa mbele akiomba kwenye magari yaliyosimama foleni.


‘Maajabu yake ni nini, mbona hatuyaoni, zaidi ya huo upofu  wake‘ akauliza kondakta wa lile daladala.

‘Yule mama anawafahamu Watoto wake hadi sura, ukimuuliza mtoto wake anafanana vipi atakuambia kila kitu kama vile amewahi kuwaona kwa macho’ akasema Yule mama aliyekuwa akituhadithia hiki kisa.

‘Inawezekana alikutwa upofu ukubwai , na pia si amewabeba tagia wakiwa wadogo kwahiy atawajua kwa kupapasa, na watu wakija siwanamuambia kuwa mwano yupoje, mweupe au mweusi mbona hiyo raisi, hayo sio maajabu bwana ’ akasema jamaa mwingine.

‘Basi huyo mama anawajua Watoto wake vizuri ajabu, wakati wakiwa wadogo hadi sasa, kwa mfano ukimleta mtoto aliye sawa na Watoto wake bila wao kutoa sauti atakuambia huyu ni mwanangu na huyu sio mtoto wangu, na sio lazima awashike na mkono. Hali hii mwanzoni tulizania labda anaona kwa mbali lakini haoni kabisa’ akasema Yule mama.

‘Wakati mwingine tulikuwa tukimchezea, tunawachukua Watoto wengine na kuwaficha Watoto wake lakini alikuwa akigundua kuwa huyo sio mwanangu, na hakosei kabisa. Lakini vitu vingine anakosea, hayo sio maajabu jamani, na kama mnabisha siku moja mjaribuni’ akasema yuile mama.

Mimi nilisema kimoyomoyo, huo ni uasili wa mzazi kwa mtoto wake(parental care), kwani hata wanyama kama kuku anagundua kuwa huyu ni mwanae na Yule sio mtoto wake, hata wakiwa wamechangayika katika makundi ya vifaranga vingine. Huyo kuwa kipofu sio kwamba amenyimwa hisia za mzazi kwa mwanae, hizo hisia ni za asili amepewa kila mtu, na ukiona mtu anajifanya kinyume chake ni kujisingizia tu, au ana ubinafsi Fulani.

Nilikumbuka mtoto mmoja ambaye baada ya kufadhiliwa na kupata elimu alimkana mama yake kuwa hamjui kwasbabu ni kipofu na masikini. Alipomaliza elimu alibahatika kupata kazi nzuri, na baadaye akajenga nyumba na kuoa mke mrembo mwenye kuchanganya damu ya kizungu na kiafriika, baba mzungu na mama mwafrika.

Aliifunga ndoa hiyo akiwa bado anaishi Ulaya, na hata wakati alipoulizwa wazazi wake ni nani na wapo wapii alidai kuwa hana wazazi na wazazi wote walishakufa. Hakuhangaika sana kumtafuta mama yake licha ya kujua kuwa alimuacha mama yake kijijini akihifadhiwa na jamaa ambao hata hawana udugu naye.

Aliporudi Bongo na kutulia na mkewe katika jumba la kifahari alilojenga , Jamaa wanaomjua wakaja kumshauri amchukue mama yake aishi naye, kutokana na hali yake kuwa sasa ana uwezo na mama yake anaishia kuombaomba. Akasema yeye hana mama, na anavyojua yeye mama yake alishafariki. Alisema hivyo lakini alikuwa anajua wazi mama yake yupo hai lakini kutokana na ile hali aliyo nayo mama yake aliona kwake ni aibu kumtambulisha kwa wakwe zake na mkewe wa kizungu na huko alishajitambulisha hivyo kuwa hana wazazi.

Mama yake aliamua kuja kumtembelea baada ya kusikia kuwa mwanae anasema kuwa yeye hayupo hai. Alifika kwake kwa msaada wa watu ambao walikuwa wakimsaidia huko kijijini. Walipofika hawakuruhusiwa kufunguliwa geti la nyumba, na hata Yule mtoto alipoambiwa kuwa aliyekuwepo nje amejitambulisha kama mama yake mzazi.

‘Nilishasema mama yangu hayupo hai, huyo anawezi kuwa mama yangu, hebu niangalieni sura yangu na yake zinafanana kweli’ akasema kwa hasira na askari kama ujuavyo, wakatii amri ya bosi wake wakamfukuza huyo mama na msindikizaji wake.

Yule mama hakukubali kuondoka akasema haondoki atakaa hapo nje hadi mwanae amchukue, lakini hakuruhusiwa na walinzi. Ikiwa kila siku Yule mama anakuja pale getini kuomba angalau aonane na mwanae amsikie mwenyewe kwa kimywa chake akimkata.

 Na Yule mtoto alipoambiwa hivyo akaja kweli na kumwambia mbele yake kuwa yeye sio mwanae labda kakosea na huenda kwa vile kasikia kuwa yeye ana nyumba na hali nzuri ndio maana anatafuta mtu wa kumsaidia, akatoa shilingi elifu kumi akasema chukua hiyo iwe nauli urudi kwenu kijijini mimi sina mama kama wewe.

Yule mama aliposikia vile akageuka na kuondoka, na hakuwahi kuonekana tena,

Siku chache baadaye jamaa alianza kuchanganyikiwa na hata baada ya tiba za kila namana jamaa hakupona na hatimaye akawa kichaa wa kufungwa kamba, na mara macho yakaanza kupoteza nuru na hatimaye akawa haoni kabisa akawa kipofu. Kila mara akawa akimtaja mama yake kuwa anamuona mbele yake. Juhudi za kumtafuta mama yake hazikufanikiwa kwani alipotoka pale hakurudi kijijini na hakuna anayejua wapi mama huyo alipokwenda.

Hii ni radhi ya wazazi, radhi ya wazazi haikopeshi, akisononeka mzazi , wewe mtoto upo hatiani hapa duniani na mbele ya muumba, ndio maana hata akiwa kipofu anaijua damu yake, kuwa huyu ni mwanangu na Yule si wangu, hiyo sio ajabu, sasa wewe unayemkataa mzazi wako ulizaliwa kutoka wapi!

Tuwapendeni sana wazazi wetu kwani bila mama kuvumilia miezi tisa na pengine kuwalea kwa shida usingekuwa unatamba hapa duniani. Hiki ni kisa kingine ambacho nikiwazia pindi nikipata wafadhili na mahali pa kujishikiza mugu akipenda tutakiandaa, na jina tutakiita `radhi ya wazazi' kuna visa vingi vipo kwa ajili ya kuviendeleza, na vyote via mafunzo kwa jamii, lakii ndio hivyo, tuombe mungu

Ni mimi: emu-three

No comments :