Wednesday, September 5, 2018

YOTE NI KWA MAPENZI YA MUNGU-43


‘Siamini niliyoyasikia huko mahakamani…moyo wangu unaniuma sana…’akasema

‘Kwanini kwani kumetokea nini…?’ nikamuuliza

‘Ni kwanini wanadamu wanakuwa na roho mbaya kiasi hicho…’akasema mama mjane, na bado nilikuwa sijamuelewa. Nikasubiria maana hapo alikuwa analia.

 Nilisubiria mpaka alipotulia, …na kabla hajaanza kuongea zaidi, ndio akaingia mpelelezi. …akatuangalia,alimuona mama mjane akifuta machozi, hakuuliza kwanini mama huyo analia, yeye akasema;

‘Tatizo ni kuwa…sis hatuna ushahid wa maandishi, na benki wanayo ushahid wa maandishi, japokuw tumejaribu kuleta hoja kuwa maandishi hayo pia yanaweza kuwa yamegishiwa, sasa kwa vipi, kwa vipi ina maana tulete maandishi yaliyo sahihi, yapo wapi…’akasema

‘Mhh…lakini..’nikataka kusema akanikatisha kwa kusema.

‘Hata hivyo, hadi hapo tulipofikia, tuna uhakika, haki itatendeka, hakimu keshaingiwa na shaka, kuwa hukumu ya awali haikumtendea haki mdaiwa…mama mjane usikate tamaa, bado kesi inaendelea…’akasema akimuangalia  mama mjane.

Mama mjane akabakia kimia tu, hakuonyesha dalili ya kukubali au kufurahia kauli hiyo,.

‘Kwani Ilikuwaje…maana mimi mnaniweka roho juu, …?’ nikauliza

‘Muda ulikwisha, …pale alipofika huyu mtu wako…’akasema

‘Mtu wangu gani huyo…?’ nikauliza

‘Chizi…’akasema na kutabasamu, kama vile anaongea kitu cha mdhaha.

‘Oh…sasa mbona mtamfanya arejee kwenye uchizi wake, …kwa jinsi alivyoniambia alipotoka hapa, haitakiwi kucheleweshwa, oh, sasa ikawaje…’nikasema na kuuliza.

‘Ndio hivyo, sheria za mahakama zina muda wake..hata hivyo,  wakili wa benki, alishaanza kuweka pingamizi kuwa mtu huyo ana matatizo ya akili, kwahiyo , yeye hawezi kutoa ushahdi mbele ya mahakamani…’akasema.

‘Kwahiyo…ikawaje, maana naona hamnifanyi niwe na amani…’nikasema hivyo

‘Docta alihitajika, kuthibitisha kuwa kweli, huyo mtu kapona,na  anaweza kuongea ukweli, mbele ya mahakama…’akasema;

Oh….docta yupi huyo aliyekuwa naye hapa,…mimi simuamini sijui kwanini…’nikasema

‘Hata mimi, lakini ndiye anayeweza kulithibitisha hilo…’akasema

‘Ok, kuacha hilo, hakukuwa na ushahid  mwingine wa kusaidia, kabla ya huyo jamaa…wengine hawajasaidia kitu..?’ nikauliza.

‘Wengine waliongea sawa, ikaonekana kweli benki kulikuwa na hujuma, lakini hujuma hizo utaziwekaje kwenye sheria…wakati benki wana ushahid wao wa kimaandishi, ushahidi wa kisheria…’akasema.

‘Ni ushahidi wa kisheria kimaandishi, lakini ushahidi huo, si ulitengenezwa, ..ukapitia sheria, lakini kwa hujuma,..hamkuweza kulithibitisha hilo…?’ nikauliza.

‘Yote hayo yalifanyika, ndio maana hakimu akavutika kuendelea na kesi hiyo, na lile pingamizi la kuendesha mnada huenda likakubaliwa, …japokuwa alisita kutoa kibali hicho,…akasema inabidi kesi hii ya kukubali au kutokukubaliana na pingamizi hilo iahirishwe…’akasema.

‘Safi kabisa…kwahiyo bado kesi hii ya pingamizi inaendelea, kwetu sisi kuchelewa hivyo itatusaidia zaidi, japokuwa shahidi wetu muhimu, huyo wanayemuita chizi, anataka kutoa ushahid wake haraka, swali je ana nini …maana hataki kuliongea hili nje ya mahakama…’nikasema.

‘Mimi naona kuwe na namna nyingine ya kutafuta huo ushahidi wa maandishi, bila huo bado kuna walakini…’akasema mpelelezi

‘Je mimi naweza kuongea na huyo  Chizi…?’ nikauliza.

‘Utaongea naye nini, kasema kutokana na kiapo chake ushahid wake wote atautolea mahakamani…kwani anaogopa akiongea nje ya mahakama, ushahid wake utaharibiwa, na inaweza ikawa ni hatari kwake…’akasema Mpelelezi.

‘Sasa yupo wapi huyo mtu…?’ nikauliza.

‘Yupo kituoni, hospitalini anapotibiwa,  na ulinzi mkali umewekwa, najua unataka kulisema hilo…’akasema.

‘Ni muhimu, huyu mtu anatafutwa na sehemu mbili kwa sasa, tusiwadharau benki, maana wao pia wanataka kushinda, na wakiona kuwa huyu mtu anaweza kufanya wakakosa…kumpata mdaiwa, wanaweza kufanya kila mbinu huyu shahidi ashindwe kufika mahakamani…’nikasema.

‘Hawawezi, hilo tumeshalifikiria mapema…hata hivyo nasikia wakili huyo na benki hawaelewani…kuna mambo hawakubaliani…’akasema.

‘Kwanini…?’ nikauliza.

‘Ilianzia kwenye malipo, sasa imefikia kwenye sura nyingine…benki wanasema huyo mtu, ana kazi nyingi za watu, kwahiyo hayupo makini na kesi hiyo…’akasema mpelelezi.

‘Hilo kwetu ni nanafuu pia…’nikasema na nikajikuta nimeuliza swali jingine …

‘Vipi Dalali naye anaendeleaje..?’ nikauliza.

‘Bado…haeleweki…’akasema.

‘Una uhakika kuwa huyo mtu hawezi kutembea..?’ nikauliza na mpelelezi akaniangalia kwa uso wa kushangaa, akasema

‘Kwanini unauliza hivyo, wewe mwenyewe si ulimuona yupo kitandani kama mzigo, mwili ule umepooza, na docta anasema itachukua muda, hadi aweze kusimama tena…’akasema mpelelezi.

‘Hahaha…’nikacheka hivyo, na mpelelezi akasema

‘Docta kalithibitisha hilo…’akasema akiniangalia kwa uso wa kujiuliza.

‘Sio kweli..huyo mtu ni muongo, anaweza kutembea kabisa, sema labda kwa shida, lakini anaweza kutembea, huyo mtu, aliweza kutembea usiku mmoja hadi huko wanapokutana na huyo mtu wake aliyemfuata, sijui ni nani…’ nikasema.

‘Unasema ukweli au uliota ukiwa kwenye marue rue ya upasuaji..hilo haliwezekani kabisa, …wewe si ulimuona pale hospialini..?’ akauliza mpelelezi.

‘Ukitaka kulihakiki hilo, kamuulize yule mdada wa mapokezi, au ..yule mlinzi, mimi nilijua kakuambia kila kitu..’nikasema.

‘Hawajaniambia kuhusu hilo, na wala sikuwa na wazo la kuwauliza hilo , maana mtu mwenyewe nimemuona kwa macho yangu…’akasema akiangalia saa yake.

********************

Siku nyingine kesi ikaendelea,…na leo akaitwa shahidi aliyesababisha mabishano ya mawakili hawa wawili…

‘Huyu mtu ana matatizo ya akili ushahidi wake hauwezi kukubalika..’akasema shahidi wa benki.

Hakimu akaingilia kati na kuuliza,

‘Je ni kweli kuwa huyo mtu ana matatizi ya akili…?’ akaulizwa

‘Ni kweli huyo mtu alikuwa na matatizo ya akili, alikuwa kweli kachanganyikiwa awali, na kuchanganyikiwa kwake ni kutokana na dhuluma, na moja ya dhuluma ni hii ya kesi hii tunayoizungumzia,…’akasema wakili .

‘Hakuna dhuluma kwenye hili deni, hio ni kauli yako, na mawazo yako, je ushahidi wetu hautoshi kulisadikisha hilo, …kama ulitosha na mahakama ikakubaliana na ushahidi wetu iweje leo uuite ni dhuluma…’akasema wakiliw a benki

‘Ushahidi wenu umegibikwa na sintofahamu nyingi, ambazo, mashahidi wetu wameendeela kuutoa, na huyu shahid anataka kulithibitisha hilo, na nafahamu mnaogopa, kwa vile mnaufahamu ukweli wake …’akasema wakili mtetezi.

Mjadala wa mawakili hawa ukaendelea, kila mtu akivutia kwake, na ikabidi hakimu aingilie kati tena;

‘Ili kuondoa huu mjadala , nataka docta wa magonjwa ya akili aje alithibitishe hilo kuwa kweli huyu mtu anaweza kutoa ushahidi , je kapona,….’akasema hakimi, na hapo ikabidi docta aitwe  , kinyume na walivyotarajia kuwa labda ataitwa docta wake wa awali, sasa hivi  aliitwa docta mwingine bingwa wa magonjwa hayo ya akili

‘Akaulizwa kama aliwahi kumtibia huyo mgonjwa na anamfahamu matatizi yake, docta akasema 

'Nimewahi kumtibia huyo mtu…, niligundua jambo moja, huyu.mtu sio mgonjwa wa akili ya kawaida kama walivyo wagonjwa wengine,.., ugonjwa wake ni kama unapuliziwa, ni kama mtu anayetumia madawa ya kulevya, lakini hajawahi kutumia hayo madawa..’akasema docta

‘Kwanini unamuita mgonjwa wa akili asiye kuwa mgonjwa wa kawaida…?’ akaulizwa

 Mgonjwa huyu anakuwa na muda wake wa kuumwa, ..na ukipita hajambo kabisa na mnaweza kuongea kila kitu…na kama unavyomuona mgonjwa huyu ni msafi sana, huwezi kumdhania kuwa ni mgonjwa…’akaendelea kuongea.

‘Na zaidi mgonjwa huyu ana akili zaidi ya akili za kawaida, anaweza akafahamu unajikiwaza, ana vipaji vingi sana vya kitaalamu, kimadawa,..hutaamini hata dawa zake anazifahamu, akianza kuumwa, atakuambia nipeni dawa hii, na kweli hiyo dawa inamsaidia…’akasema

‘Ila anaonekana ana msomgo wa mawazo, kuna kitu kinamtatizo, ..na huwa na muda wake wa kukifikiria hicho, kitu akikiwaza, analia sana, na hapo hasira humpanda, na kuanza kujipiga au kuwapiga waliopo mbele yake…’akaulia docta

‘Sasa, mwezi huu hali yake ilizidi sana.., na kila mara amekuwa akinisihi kuwa, tatizo lake litakwisha yeye akitubu dhambi zake.na kutubu dhambi zake ..inahitajia safari ndefu, kwanza aanza kujitenga na watu, ..ndio maana alikuwa akipotea, na kuishi sehemu ambayo watu hawafiki fiki…’akasema

‘Sasa wiki hii ndio kasema muda umefika wa yeye kutubua mbele ya jamii, na hasa mbele ya mahakama,…kwahiyo hili la kuto ashahidi ni sehemu ya toba yake, na amesema wazi, isipofanikiwa hivyo, ndio itakuwa mwisho wa maisha yake,…’akasema docta

Hakimi akamuangalia huyo shahidi, na baadae akamuangalia wakili wa benki, ambaye naye alikuwa akimuangalia huyo mgonjwa,…baada akauliza

‘Wewe ni docta, au sio…?’ akauliza

‘Ndio mimi ni docta…’akasema docta

‘Huyo mgonjwa ana matatizo gani…?’ akauliza wakili wa benk

‘Ana matatizo ya akili…’akasema docta

‘Kwenye vifung vya sheria mgonjwa kama huyo anastahiki kutoa ushahidi, ….?’ Akauliza wakili.

‘Kama nilivyosema awali..’kabla hajamaliza wakili akauliza tena

‘Je mgonjwa huyo ana matatizo ya akili au la…’?’ akauliza wakili

'Mimi kama docta wake, naona njia pekee ya kumsaidia huyo mgonjwa ndio hiyo kwani kia alichokiomba afanyiwe tukamkubalia chenye manufaa kimekuwa kikimsaidia kimatibabu…’akasema huyo docta na hapo hakimu akaingilia kati, na kusema;

'Sio jambo la kawaida, na kesi hii imegubikwa na mambo mengi yasiyo ya kawaida, lakini imebidi tuyakubali ili tuone ukweli halisi wa kesi hii,..mimi ninamkubalia mtu huyo atoe ushahid wake, kutokana na kauli ya docta wake…’akasema hakimu.

Yule shahidi akasogea mbele, sehemu ya kutolea ushahidi, kiukweli huwezi amini kuwa jamaa huyo ana matatizo ya akili,…akatulia akisubiria utaratibu wa kimahakama.

Alipomaliza zile taratibu zote akaulizwa jina;

‘Jina lako ni nani…?’ akaulizwa na hapo akabakia kimia, akaulizwa swali hilo mara ya pili, na hapo akageuka kwa hakimu, akasema;

‘Unajua ni kwanini nimeshindwa kulijibu hilo swali, ni kwasababu mbele yangu nawaona watu ambao nyie hamuwaoni, walikuwa wakiniuliza maswali mengi kwa wakati mmoja,..’akasema na hakim akageuka kumuangalia docta, ni kama vile anataka kusema

‘Mbona umetuletea mgonjwa hapa, …’ na kabla hakimu hajasema kitu shahidi huyo akasema;

‘Hii kesi ni yangu, kote huko mumezunguka tu, na kweli ilitakiwa iwe hivyo, …na kama kweli isingelikuwa hao mzimu,…hahaha, msingelimpata mtu…’akasema.

‘Unaniuliza jina langu ni nani…nitakuambia, ila kabla sijajibu hilo swali lako, kwanza nataka niwaambia jambo moja…’akasema.

‘Hivi kweli mtu mwenye akili zake timamu anaweza kumdhulumu yatima…mjane,..au marehemu..?’ akauliza sasa akimuangalia hakimu, hakimu akabakia kimia.

‘Ikimia wenu unasema neno moja, …’hakuna..’

‘Ni kwanini sasa hayo yanatokea,…?’ akauliza

‘Ukimia wenu unaeleza neno moja,..’hatujui..’

‘Basi mimi niwaambie neno moja…mimi nina akili sana, mimi sio kichaa, wenye kichaa, ni hao wasio na akili, ambao, wanayafanya hayo kwa siri wanawadhulumu mayatima wanapuuza wajane…na wengine ni matajiri tu…’akatulia.

‘Mimi nimeliona hilo, ndio maana leo nimeamua kutubia dhambi zangu, ..leo wakili wa benki ananiita mimi ni ‘kichaa’ wakakati yeye amewahi kusaidia watu kushinda kesi ya kuwadhulumu mayatima,…anabisha,..?’ akauliza na watu kimia.

‘Habishi maana ndio kazi yake, je mimi na yeye ni nani kichaa..?’ akauliza watu kimia.

‘Basi mimi nataka nisema ukweli , na ukweli huo utambulikane kuwa unatoka kwa mtu ambaye ana akili sana, sio kichaa, maana vichaa wapo na hamuwatambui kuwa ni vichaa…’akamuangalia wakili wa benki.

‘Je muheshimiwa unanifahamu mimi…?’ akauliza.

‘Sikufahmu ndio maana tumehitajia jina lako…’akasema wakili.

‘Wewe ni muongo…na muongo sana,..mimi na wewe tumesoma shule moja,..wewe ukachukua masomo ya sheria na mimi nikasomea masomo ambayo yamenifikisha hapa nilipo…mimi na wewe tumekuwa marafiki, …hata tukiwa kazini, lakini leo unasema hulijui jina langu…’akasema na watu wakaguna.

‘Je mimi na yeye ni nani kichaa…?’ akauliza, na watu kimia.

‘Mimi naitwa… M.AL.M…’akasema na hakimu akasikiliza kwa makini..na hata aliporeja jina hilo bado haikueleweka…

‘Hebu taja jina lako kwa harufu moja moja…na alipotaja ndio ikagundulikana kuwa ni kifupi cha majina..

‘Majina yako kwa kirefu ni nini..?’ akaulizwa.

‘Maozo..aliyetupwa, majalalani aka, MOTO…’ Akasema na watu wakacheka

‘Mnacheka,…hii inaonyesha kuwa nyie ni vichaa zaidi yangu mimi, jiulizeni lini mlilipata kusikia jina kama hilo, mliwahi kulisikia hilo jina wapi…?’ akauliza

‘Hakuna hatujawahi…’akajibu mtu mmoja.

‘Na wewe wakili wa benki…?’ akamuuliza.

‘Nililisikia kipindi nipo shuleni, lakini mara nyingi hukuwahi kulitaja kwa kirefu hivyo,…’akasema.

‘Kwanini nilifanya hivyo..?’ akauliza

‘Mimi sijui…’akasema

Hapo akatulia, akawa kama anawaza jambo, …halafu akasema

‘Leo sitalia..leo sitabadilika na kuwa kichaa…leo nitaongea, na leo mtanifahamu kuwa mimi ninani, na kwanini niliitwa maozo..ni kweli nilikuwa uozo mbele ya jamii, mbele ya baba yangu aliyenizaa…’hapo akatulia,

Alikaa hivyo kwa muda, hata hakimu ataka kuongea, ndio jamaa akasema

‘Hilo jina alinipatia mama yangu na ndiye aliyeliandikisha …na alitaka sio kwamba alitaka liwe hivyo,..na muda huo mama yangu alikuwa hawezi kuongea vizuri, hawezi kutamka hayo maneno vizuri..jina langu lilikuwa Mansa Majaliwa Moto…’aliposema hivyo, watu wakaangaliana.

‘Docta au aliyeandika kadi hiyo akaandika, MAOZO,AL, MOTO…kwa jinsi mama alivyoshindwa kutamka, ulimi wake ulikuwa kama umemezeka, kutokana na mtindio wa ubongo aliupata,..ndio jina langu likawekwa hivyo kwenye karatasi…hadi nipo shuleni na mimi nikalipenda liwe hivyo…’akatulia.

‘Sasa naanza kuelezea..nyie si mnataka ushahidi, wa hii kesi, au sio ..kuwa je ni kweli hilo deni ni la marehemu au la…, je kweli hilo deni ni sahihi kwake…?’ akauliza na aliyejibu ni hakimu, akasema.

‘Ndio, tunahitajia hilo jibu…’akasema.

‘Kwa  jibu rahisi na la haraka  ni ‘KWELI’’..’akasema

‘Unasema ni nini…?’ akaulizwa wakili wa benki

‘Kwa jibu la haraka ni kweli…’akasema

Aliposema hivyo wakili wa benk, akamsogelea na kutaka kumpa mkono wa shukurani, lakini shahidi huyo hakuupokea huko mkono, …na Wakili wa utetezi, akawa kimia, kama vile hana wasiwasi, na mtu huyu

Huyo shahidi  akasema;

‘Nimesema naongea ukweli mtupu, na haya nitakayoyaongea ndio ukweli, na hilo deni linatokana na ukweli wa maisha yangu…mnielewe hapo, hilo deni ni stahiki ya marehemu kwa sababu…nitakayokuja kuielezea…’akatulia na kikasikika kilio kwa watu waliofika

‘Ninajua anayelia ni nani..ila anivumilie tu, ukweli unauma, na ukweli utasaidia kizazo chako dada yangu,na baada ya kilio, huja nini, huwezi kulia milele au sio mwisho wake atacheka tu,…’akasema.

‘Kwanini unasema hilo deni ni la marehmu…’akauliza wakili mtetezi wa madeni
Huyu shahidi akamuangalia kwa makini huyo wakili kama anamsoma mawazo yake, halafu akasema.

‘Una shaka na mimi..?’ akauliza.

‘Nijibu swali langu…’akasema.

‘ Nitakujibu,…lakini jibu lake siwezi kulielezea kwa jinsi mnavyotaka nyie, jibu la swali lenu litakuja kutokana na kisa cha maisha yangu…naomba muheshimiwa hakimu unipatie wasaa nilielezee hilo jibu, lakini kutokana na kisa cha maisha yangu,….ili haki ije kutendeka…’akasema.

Hakimu akaangalia saa,…

NB: Na mimi nikaangalia saa, bosi anakuja.


WAZO LA LEO:Ukweli wa maisha ni upi..ni jibu la haraka au ni jibu la maelezo marefu. Maisha ya mtu sio jibu la haraka, NDIO AU HAPANA, maana MAISHA yalivyo yana mlolongo wake mrefu, hata kama ni mtoto kazaliwa leo na kufariki leo. Maisha yalivyo, yanatokana na michakato mingi, na zaidi ya hayo anayefahamu zaidi ya hayo ni yule aliyetuumba. Katika maisha tusikate tamaa maana mengi ya yanayotokea ni kwa mpenzi yake yule aliyetuumba.
Ni mimi: emu-three

1 comment:

  1. I'm truly enjoying the design and layout of your website.
    It's a very easy on the eyes which makes it much more pleasant
    for me to come here and visit more often. Did you hire out a
    developer to create your theme? Superb work!

    ReplyDelete

Changia hoja kwa kutoa maoni yako hapa: Au tuma kwa e-mail> miram3.com@gmail.com