Ni mara nyingine leo siku ya Idd nimekuja kuswalia kwa Mtoro , Nimewahi sana ili angalau niswali ndani, na sehemu ambayo nitanuona imamu.
Msikiti huu unajaa sana, sijajua ni sababu ya kihistoria au kuna mengine ya ziada.
Kwangu mimi msikiti huu una historia nyingi kwangu kiimani.
Nakumbuka enzi hizo za harakati za Uislamu, watu wanakamatwa kamatwa, enzi za Mwembe chai nk
Nakumbuka sana enzi hizi sikosi kufika , hata siku za kawaida, hapa msikitini pamoja na yote nilikuwa nakuja kununua kanda za mawaidha mbalimbali. Mojawapo nyingi ya hizo kanda zilikuwa za mawaidha ya sheikh Bachu.
Misikiti sasa imeboreka, ukiwemo huu, sasa hivi msikiti huu ni wa ghorofa, na umezungukwa na majengo ya magorofa,.,
Nilianganza huku na kule, wale wauzaji wa kanda za mawaidha hawapo tena, sasa hivi kuna wauza nguo, kanzu, madawa,...
Sasa hivi hapa kuna hata tv ...tv mtoro
No comments:
Post a Comment
Changia hoja kwa kutoa maoni yako hapa: Au tuma kwa e-mail> miram3.com@gmail.com