Monday, June 30, 2025

AJALI HAINA KINGA, JE KAMA NI YA UZEMBE TUSEMEJE?

Wakati nipo ndani ya daladala nilishtuka watu wakitoa sauti ya kushangaa, kama nje wameona kitu cha ajabu, ...

'Ajali.....mungu wangu, sijui kama wapo hai...' sauti moja ya mmoja ya wabiria ilisema
Nikajua kuwa kuna ajali imetokea

'Yule wa boda boda anaonekana kuwa anatapatapa.....'akasema abiroa mwingine

Yaonekana boda boda kwa haraka zake alitaka kukatisha mbele ya lile loria...

Mengi yalisemwa, kila mtu na maoni yake...
Akilini niliwaza hivi hao watu....eeh, yaani dereva wa boda boda na dereva wa lori hawakuwa na wazo hilo, kuwa tungelifanya hivi ili ajali isitokee.... ndio zipo sheria za barabarani...na watu wanazifuata lakini ajli bado zinatokea!

Niliinamisha kichwa kutafakari.....Kiimani hi imekuwaje, je ajali ni uzembe wa watu, au ndio mola kapanga iwe hivyo, ....

Ni mimi: emu-three

No comments:

Post a Comment

Changia hoja kwa kutoa maoni yako hapa: Au tuma kwa e-mail> miram3.com@gmail.com