‘Ni zawadi gani ilitoka kwa mama…..?’ shahidi
akawa kama anauliza
Akageuka kumuangalia hakimu, kama kuhakikisha kuwa hakimu huyo bado
anafuatilia maelezo yake,…na hakimu naye akawa amemkazia macho. Hapo shahidi
huyu akarizika, na kuendelea kuongea…
‘Najua nilianza kutoa kitabu,
eeh dafutari, hicho ni kitabu sema tu hakijapigwa chapa..na mungu akijalia
nitakitoa kiwe kitabu, maisha halisi ya mama, au nikiite nani kama mama,
‘Huo ni ushahidi hasa,
uliobainisha, …unyama aliofanyiwa mama, na maisha yake baada ya hapo…na kwangu
ndio ushahid ulionisaidia mimi kujijua, nimetokea wapi, watu walisema
nimeokotwa majalalani…sawa..lakini hicho kitabu kimefichua hilo..kumbe mimi
ni..zao la …’hapo akasita kumalizia.
‘Kwahiyo zawadi hiyo
ilikuwa hicho kitabu…’akawa anaangalia lile dufutari pale lilipowekwa.
‘Nilipobaini kuwa ni
kitabu tu, tena cha kuandikwa kwa mkono, mwandiko mnzuri wa kike,….swali la
haraka lilinijia,..kiukweli nilijiuliza mimi mwenyewe, …eeh,… kama mama
alithaminisha hicho kitabu na zawadi kubwa sana kwangu, …thamani yake ni nini
kwangu,…’akahema kidodo.
‘Sawa nilipokisoma
niliona yaliyokuwepo, huenda kwa wengine hayana thamani,,…labda thamani yake ni
hiyo, mimi kuumia moyo,…mama alivyoteswa, na…sawa, nilie, sawa… kupotewa na fahamu, kuwa kichaa..eeh, halafu
nikae kimia, si ndio jamii inataka hivyo, uwe muungwana.’akatulia
‘Jamani baada ya hayo,
baada ya kutambua hayo, hivi, ni binadamu gani ataweza kuvumilia, au kwa vile
sisi ni masikini..au mlitaka mimi nifanye nini, kama mama alifika mahakamani,
akiwa anaumwa, akiwa na ushahidi kamili wa mwili wake…hakushinda kesi, je mimi…jamani
mlitaka mimi nifanye nini, labda niwaulize hilo nyie mnisaidie…’akasema kwa
unyonge, huku akionyesha dalili ya kutaka kulia.
‘Kiukweli…thamani ya zawadi
hiyo ni kubwa,japokuwa mama hakumaanisha hivyo, kipesa, au kimali, .ila bila
hata kauli, thamani yake ilikuwa kama kuuliza ..HAKI YANGU
IPO WAPI, …swali kwenu, JE HAKI HIYO Ilitendeka,
..hahaha, haki kwa mnyonge, lini ikathamaniwa, eeh, niambieni, msiogope kusema
ukweli, mnyonge hana haki hapa…’akasema sasa akiwaangalia watu, na baadhi
wakapiga makofi.
‘Sihutubii mimi, ila
naelezea uhalisia…ili uwe na haki, ni lazima uwe na ushahidi…na ili uupate
ushahid wa kisheria ni lazima uwe na wakili..ili umpate wakili ni lazima uwe na
pesa, masikin ataipatia wapi hiyo pesa…manielewa nina maana gani, hapa
namuongelea mama, masikini ….’akatulia.
‘Haya maswali..nilijiuliza
sana mimi, nilijiuliza..na kujiweka sehemu ya mama.., kichwa kiliniuma,..na
akili zangu zote hapo niligwaya,.sikupata jibu, nikawaza kupitiliza..nikikumbuka
pia kuwa nimenyang’anywa mali halali…kisa, matajiri wape…siwezi kusema kwa vile
ni mali ya familia nyingine…’akageuka kumuangalia wakili.
‘Kama ilikuwa mali ya
mama mlezi, na mimi ndiye mwanae wa kufikia, na mimi ndiye nilihangaika
naye,..hadi..siku ya mwisho…kwanini kauli yake isithaminiwe…niliwaza sana…hadi
nati za kichwa zikakatika, ti-ti-ti, uchizi huooo
‘Uchizi ulinianzia
hapo ndugu wapendwa,…niwaulize tena, nyie, ningelifanya nini hapo…mmh, mimi kwa
udhaifu wangu,…nikaona jibu rahisi,…nitatumia akili yangu, si ndio nimebakia
nayo,…akili,….nitafanya vile akili itanituma, labda hivyo ni ujinga kwa
matajiri, lakini kwangu,…niliamua hivyo …’akahema kidogo.
‘Nakumbuka sana, kauli
ya mama…’…niache ujinga…nitumia akili yangu…’ nami nikaamua kutumia akili
yangu,nilitumia vipi basi…’akageuka kumuangalia hakim
‘Hahaha watu
wanafikiria kuwa mimi labda ndio nikalitengeneza hilo deni, hahaha, kwanini
nifanye hivyo, deni limejileta lenyewe, kulipa deni,..sasa niwaambie wazi, deni
kwa deni, japokuwa deni lao, haliwezi kabisa kulipa hilo deni, la mama, na…walichonidhulumu,
lakini mimi sijatengeneza deni….’akahema na kumwangalia wakili wa benk,
aliyekuwa akikubaliana naye.
Kuwaza sana,
kusononeka, sana, na kuumia kila nikisoma kile kitabu, nikawa sasa mtu mwingine….kichaa.
Mhh,nikaanza
kuchanganyikiwa …kila nikijaribu kusoma kitabu cha mama, ndio nazidi
kuumia,…kulia, kuwaza…unajua kama mama angelijaliwa kuishi, angelikuwa mwandishi mnzuri sana tu, waandishi
wazuri, huandika uhalisia,..na mama aliandika hali halisi iliyomtokea, na
inagusa ndani ya moyo…kiukwel, wema
hawana maisha.
Japokuwa alinza
kuandika kipindi cha baadae, lakini alijitahidi kuwa na mpangilio mzuri tu,
unaoeleweka,.. kwahiyo mengine aliandika kwa jinsi alivyokumbuka. Isipokuwa
yale yaliyoendana na tarehe wakati anaanza kuandika, ndio aliweza kuaandika tukio na tarehe
yake…kama mtakavyoona kwenye hilo dafutari..kumbukumbu halisia, au shajara kwa Kiswahili
fasaha na kwa kiingereza ..diary..
‘HIYO NDIO ZAWADI
YANGU KUTOKA KWA MAMA…
Siku nilipoanza
kusoma, ilikuwa ni usiku,…nakumbuka ilifika muda kichwa kikawa kama sio changu,
nilipiga ukelele, unajua ukelele, huku naita mama, jamani,…ni mateso gani hayo,
..unyama, hadi mtu anachukua bati lenye kutu, anakata ulimi wa mama, mja
mnzito,..hivi jamani,..mnahisi kama ninavyohisi mimi…kama hamna hiyo hisia nyie
sio binadamu wa kawaida..
‘Hapana…msiseme kwa
midomo yenu huku hamumaanishi hivyo, eti nani kama mama, na kawaelezea vyema,
tu, nasikia wakati anaelezea alivyofanyiwa ili bidi awe anaandika,…hahaha, ni
nani angelisoma,…dharau…kwahiyo sasa mnataka na mimi nikae kimia,..dunia
itanishangaa..naomba mnielewe…maana nimeamua kusema ukweli, na ukweli uwekwe
kwenye maandishi..’akatulia
‘Siku nilipomgundua
huyo baba…we acha tu, usione watu wanaua, usione watu wanageuka kuwa
wanyama..inaumiza, kuna watu wamepitia mateso, na unafanyiwa mateso, huku
unakebehiwa, unadharauliwa,…sasa ufanye nini, ujitoe mhanga,…mimi sijui,
niambie nyie…’akasema akiwaangalia watu.
Nikawa sasa nateseka
na maumivu ya kichwa,…kichwa kinauma kama kinataka kupasuka,…usiku huo, nilipoanza
kusoma..ikafika hatua siwezi tena..…sijui kilichotokea nini..kichwa, eeeh, mara
nziiii, giza, hapo tena sikuweza kujitambua, nilipoteza fahamu, sijui.
Baadae,…,..kumbe
majirani walisikia huo ukelele, wakafika, wakagonga, kimiaa…mtu nimeshapotea…sipo
duniani tena…hata walipoamua kuvunja mlango, mimi sikuwasikia,.waulizeni hao
majirani ili mpate ushahidi…kweli walivunja mlango, wakanikuta nipo sakafuni
nimpoteza fahamu…waiteni muwaulize si mnataka ushahidi…’akasema
Taabu ikaanzia hapo…
‘Ndugu zanguni, hali
hiyo ilinitesa sana, tena sana, kila nikijaribu kusoma hiyo zawadi kutoka kwa
mama, naingiwa na hiyo hali…yaliyoandikwa
humo ndani, inataka moyo kuyasoma..ikizingatia kuwa huyo ninayemsoma,.. sio
mwingine ni mama yangu mzazi, aliyekatwa ulimi, na ile hali ikasababisha kuleta
tetenasi na kuzalisha ugonjwa usiopona…hayo maelezo yapo humo na cheti cha
docta kipo humo, na ndio ilikuwa sababu
yake ya kutangulia mbele ya haki, mola aiweke roho ya mama na mama mlezi mahali
pema peponi…’akatulia kwa muda,
Baadae…
‘Niliwahi kupata nafasi ya kwenda kusoma nchi
ya jirani kwa ufadhili fulani, hapo ni kabla sijarudi ..na niliporudi ndio
nikakumbuka kuhusu hiyo zawadi, na ndio nikakuta nyumba imeshavunjwa,..nianda
mbele na kurudi nyuma, lakini najua mnanielewa, au sio…ukichaa ukawa sasa unaongezeka.
Na muda huo natakiwa kuanza kazi…
Usione hivyo, kila
ninapozidiwa natamani nifike ufukwenu kupata ule upepo wa kule..ndio maana nikaweza
kutengeneza ofisi yangu kule, kule..hadi leo sijaweza kulimaliza hilo dafutari,
lote, someni nyie mnaoweza , na labda mtaona ni kisa cha kutunga…’akatulia
Kazi nilishapata kutokana na akili niliyokuwa
nayo, ilikuwa rahis tu, lakini sasa akili, imeshavurugika,..lakini cha ajabu
nikiwa ofisini nikatulia, nafanya kazi za watu vizuri tu, ila ikitokea namna ya
kukumbuka..na kingine kilichonisaidia…, ni karama aliyonipatia mungu, akili ya
kusoma akili za watu wengine,..sijui …lakini ndivyo nilivyokuwa, nasema ndivyo
nilivyokuwa, kwasababu hiyo hali ya kusoma akili za watu wengine ishapotea,
haipo tena.
Ilipotea kwasababu gani,…akili yangu ilikuja
kutekwa na kitu kimoja,…kisasi..kisasi, kitu ambacho mama hakukitaka..lakini
hata hivyo, mimi ningefanya nini, ni lazima nifanye jambo au sio, ..wengine
wanasema ilitakiwa nifungue kesi upya…hahaha, nitaulizwa ushahidi upo wapi…ni
lazima nitaulizwa hivyo…upambane na yule baba mjanja kama nini…hadi leo kakataa
kabisa kukubali kuwa alimfanyia mama hivyo….’hapo akainamisha kichwa chini.
‘Sasa kisasi…’ ikawa
ndio dhamirana mikakati yangu, .. hatua ya kwanza ni kumfahamu vyema huyo baba, huyo
aliyemfanyia hivyo mama, huyo mtu ni nani, kwangu mimi, sio baba tena,
kwasababu kwanza aliikana mimba, na hata nilipozaliwa alinikana kuwa mimi sio
mtoto wake, mimi ni mtoto haramu
‘Sio baba yangu, kwa
kinywa chake na matendo yake..’akasema
Upelelezi ukaanza,
maana mama mlezi hakuwhai kuniambia hata siku moja baba yangu ni nani, yeye, anasema
anayemtambua ni mama, baba yangu hajulikani..kumbe yupo, na kama mama mlezi
angelikiuka maagizo ya mama mzazi, akaifungu ahiyo zawadi, huenda angelimfahamu
baba yangu ni nani.
‘Nasema hivi, mimi
sina baba, kwa mujibu wa matendo yaliyotendeka, na kwa mujibu wa kauli yake…hadi
leo,…kwa mara ya mwishi nilimuuliza, akakataa kata kata…sasa mtu kama huyo
utamfanya nini,..mimi ndio nijipendekeze kwake,..isingelikuwa shida,
ningekubali yaishe,..sio shida,…ila niliposoma hilo dafutari,..thubutu….’akatikisa
kichwa.
Nikafanya upelelezi,
nikamgundua huyo baba..na siku moja nikakutana naye, wakati huo, huwezi kunijua
ni mimi yule niliyekuwa chokoraa..maana sasa ni msomi, na nina kazi,…nilijaribu
sana kuipoteza sura yangu ya asili, yawezekana tu, wala sio kwa kutumia madawa…’akatulia.
Sasa katika uchunguzi
wangu, nikaja kugundua kuwa, kumbee…huyo baba, ana udugu na huyo mtu
aliyenidhulumu ardhi yangu..anayetumia pesa zake kuwasaidia ndugu zake, ambao,
wanadhulumu wengine, pesa zake…ndio sababu, ok…pesa ndio sababu au sio…nikaanza
mikakati ya kupambana na pesa zake…
Nikisema hivyo wengi
wanasema nimekosea, aliyenidhulumu mali yangu, sio huyo, …aliyemfanyia mama
mabaya sio huyo ni mtu mwingine, LAKINI wote lao moja,..kama huyo tajiri
angelinielewa, asingelinunua hilo eneo…asingetoa ushahidi ambao hana uhakika
nao, na hata nilipojaribu kujieleza kwake, hakutaka hata
kunisikiliza,..aliishia kunikejeli, dawa ya kuwamaliza wote hao, ni kudhibiti
mali yao..PESA ndio ilikuwa inawapa kiburi, si ndio hivyo..
Nikaja kugundua kuwa
mzee, yaani, mjomba naye ana udugu na yule msamaria mwema..mtu wa madawa
asilia..…mnamkumbuka eeh, mtaalamu,..lakini yeye sio mtaalamu, utaalamu ule
aliupata zaidi kutoka kwangu, na hata jina hilo, mimi ndiye niliyekuwa
nikimuita wtu wakifika nyumbani kwake, nawachagamkia, mumekuja kwa mtaalamu eeh……hahaha..’akacheka
.
‘Mtu yule pamoja ya
kuwa anafahamu madawa ya kienyeji, lakini wakati mwingine alikuwa anawadaganya
watu kwa ramli za uwongo, baadae akaenda wapi sijui, aliporudi anadai kapata
shetani gani anaeweza kumsaidia kuagua, na kupiga ramli, ushetani mtupu…mimi
nipo mbali na hayo..nikawa najaribu kumfundisha hiyo karama yangu..akanipenda
sana…hakujua lengo langu ni nini…nilifanya hayo, huku jamaa hajui kuwa
namchunguza, na kuwachunguza maadui zangu…ilikuwa kazi yangu ya kwanza.
Yaliyoendelea kati
yangu na huyo mtu,..ni mengi saa,… nitawachelewesha, nikianza kuyaelezea,
muhimu ni kuwa, watu watatu sasa nimeshawafahamu vyema, na iliyobakia ilikuwa
kuangalia, nitawafanya nini..kila hatua nikijaribu nahisi nitafanya
makosa,..sitaki kumdhulumu mtu…sikutaka kuua mtu, .’akatulia.
Siku zikawa zinaenda…sijapata ufumbuzi na
sijui nifanye nini tena…..’akatulia
Siku zikaenda,…ajira
mpya, ikawa inaniliwaza nikiwa kazini, mawazo ya mama , na maisha mengine
yanapungua, hapo…akili ninayo, kazi sasa ninayo, lakini moyo hauna raha,…wazo
likanijia tu, nifanya jambo, lakini wazo hilo linahitajia pesa, na mimi
japokuwa napata pesa, ni ile ya ..kawaida tu,..hapo kwa mara ya kwanza nikaanza
kuingiwa na tamaa ya pesa. Ili nifanikiwe hilo jambo langu.
Alipofika hapo hakimu
akasema;
‘Muda umekwisha sana,
na ..nimekuachia tu, utoe maelezo yako upendavyo,..kinyume na utaratibu, hadi
hapo, tunaweza kusema wewe, ..uliyokuja kuyafanya yalikuwa kulipiza kisasi, sasa nikuulize swali, je
katika kulipiza huko kisasi chako, ndio hapo ukatengeneza hilo deni…?’
akaulizwa
‘Samahani muheshimiwa
hakimu, mimi sijasema nilitengeneza deni…’akasema
‘Deni la marehemu
lilifikaje kwenye akaunti yake,…na kama ni wewe ulifanya hivyo hilo deni lifike
kwenye akaunti yake, mbona unamuadhibu mtu ambaye hakustahiki,…wewe kwa maelezo
yako, baba yake ndiye alimkosea mama yako au sio, ulimfanya nini baba yako,…?’
akaulizwa
‘Muheshimiwa hakimu, mimi
sijatengeneza deni lolote, mnielewe hapo tafadhali, hilo deni wanalijua wenyewe
watu wa benki, huo ni wajibu wao, na msinitupie mzigo ambao sio wa kwangu…’akasema
na watu hapo wakashikwa na butwaa…hakuwajali, akaendelea kuongea.
‘Kwa maelezo yako
umesema wewe na mama yako mnadai pesa nyingi sana , kwa thamani haimithiliki au
sio, ndio ukabuni namna ya kulipiza kiasasi , na kisasi hicho ulifanyaje…?’
akaulizwa.
‘Mimi ndio nadai,…nadai
mali nyingi zenye thamani nyingi, nadai haki ya mama yangu na mama
mlezi…lakini…mmh, habu niliweke hili hivi… akatulia kwanza
‘Hebu fikirieni hilo
eneo, lipo sehemu gani…, na sehemu hizo, maeneo yanauzwa kwa bei mbaya sana,
mnaweza wenyewe kukisia, na eneno lenyewe sio eneo dogo, ni karibu ekari moja,
limeuzwa, na sikupata hata senti moja, je kiukweli , kihalali, hayo malipo, au
hiyo mali, haikuwa ni haki yangu, je thamani
yake ni shilingi ngapi eeh, hapo ni eneo, na je haki ya mama…?’ akawa kama
anauliza.
‘Utasemaje ni eneo
lako, wakati huna ushahidi wa kulimiliki, kwa mujibu wa wanafamilia, wewe sio
mwanafamilia, na eneo lilikuwa na familia, au…au kama mama mlezi alitaka wewe
urithi eneo hilo…, ushahidi upi wa kukuwezesha itambulikane kuwa hilo eneo ni kwako..?’
akaulizwa.
‘Safi kabisa, mumefika
huko ninapokutaka, sasa eeh…nauliza na nyie mnaodai kuwa hilo deni sio la
marehemu, ushahid gani mliokuwa nao, si maneno matupu kama yangu, hata kama ni
kweli, ushahidi wenu upo wapi..eeh,…hapo sasa jibu mnalo, semeni ..ushahid wenu
upo wapi…?’ akauliza akimgeukia wakili wa utetezi wa wanaodaiwa.
‘Ushahidi wetu ni
maelezo yako…maelezo yako yanaonyesha dhahiri hilo deni ulilitengeneza wewe kwa
nia ya kulipiza kisasi…umekiri mwenyewe mbele ya mahakama…’akaambiwa
‘Mimi nimekiri hivyo, …!!
Sijakiri hivyo,…na kiukweli, nyie hamna ushahidi huo kuwa mimi ndiye nimelitengeneza
hilo deni, kwanza kwa vipi hapo mnaongelea benki, ambao wana utaratibu
unajulikana kisheria,…deni halitoki hivii hivi…mimi nitawezaje kufanya hivyo,…hadi
hapo hizo ni hisia zenu tu, au sio..?’
akauliza.
‘Ushahidi wetu ni wewe
na wenzako, mlioshirikiana nao, wewe umeshasema hayo yaliyofanyika hadi kutokea
deni ni kutokana na chuki zako kwa hao watu waliokufanyia mabaya wewe na mama
yako, au sio..?’ akaulizwa.
‘Kama ushahid ni mimi
na wenzangu, basi hata haki yangu ipo..maelezo yangu, na ushahidi wangu
utambulikane, na mashahidi kwa haya niliyoyaeleza wapo,yupo huyo mzee, japokuwa
wengine ni marehemu..lakini hapa yupo, yule mzee, muiteni kama hatathibitisha
haya niliyowaambia,kuwa ni kweli tupu…’akasema
‘Japokuwa huyo aliyempa mimba mama yangu akamfanyia unyama,
hataki kukiri hilo kosa hadi sasa hivi…’akasema
‘Kama ni hivyo
tutaaminije maelezo yako…?’ akaulizwa
‘Maelezo yangu
yana ushahidi mwingi tu..sawa nimejaribu
kumfanya akiri, lakini kagoma…lakini dhambi zake zinamtafuna kidogo
kidogo,..maana .malipo ya dhambi nyingine ni hapa hapa duniani, ile hali
aliyoipata mama, itamtafuna nay eye, na wote walioshiriki, mmoja baada ya mwingine,watawajibika
kwa hilo…’akasema.
‘Kwa kusema hivyo ina
maana kuna jambo umewafanyia,..je ni nguv za giza, na je ndio hilo deni,
tuambie tusipoteze muda …?’akaulizwa.
‘Mimi sio mchawi,
msije kusema, mimi nimewafanyia hao watu kitu chochote, ningelitaka
ningelifanya hivyo kwa kupitia marehemu, mtaalamu, aliwahi kunishauri hivyo,
lakini sikutaka……’akasema
‘Je ni kweli kuwa wewe
na mtaalamu mlitumia nguvu za giza, kuwatesa familia ya marehemu, na hao maadui
zako, je ni kwanini ulifanya hivyo, ni ili wakubaliane na hilo deni, si ndio
hivyo,…na umekuwa ukitumia nguvu za giza kuwatisha, si ndio hivyo, ..?’ akaulizwa.
‘Mimi sikuwa na haja
ya kufanya yote hayo, na wala mimi sina uwezo huo wa nguvu za giza, mimi nina
karama ya kusoma watu, nilikuwa nayo..lakini sikuwa na ..uchawi, hiyo kazi
nilimuachia mtaalamu, yeye alijua ni nini cha kufanya, kazi yangu ilikuwa kwenye
pesa, maana hawa watu ili kulifanikisha hilo walihitajia pesa, ili baadae lengo
lije kutimia na haki ije kupatikana …’akatulia.
‘Haki gani na haki
hiyo ungeipata vipi..?’ akaulizwa
‘Haki ipi, ina maana
hadi hapo, hamjafahamu haki yangu ni ipi, basi kama ni hivyo, ndivyo…ukweli
unakuwa bayana, kuwa watu kama sisi hatuna haki, hata kama tukifanyiwa mabaya,
na kama ni hivyo, kwanini tusitafuta namna ya kulipwa madeni yetu,eeh… leo hii
nimesimama hapa mahakama, nikitambua kuwa haki yangu itapatikana, mbona haki
bado inapingwa,…’akasema.
‘Kwahiyo wewe ulikuwa
hujui kinachoendelea kati ya mtaalamu na familia ya marehemu..kuwa huyo
mtaalamu ndiye alikuwa akiwatesa watoto wasio na hatia na mama yao, kwanini
alikuwa akifanya hivyo, na kwasababu ya deni au tuambie..?’ akaulizwa
‘Nimesema hivi, hiyo
sio kazi yangu, kazi yangu ilikuwa kutoa pesa, wao wafanye wafanyalo ili wapate
pesa kutoka kwangu..aliyekuwa akijua siri yangu angalau kidogo, ni huyo mtaalamu,
…na mambo kama hayo mjuzi wake alikuwa ni yeye, sasa kama aliwatesa watoto wa
watu, muulizeni yeye, kwanini mimi nishiriki kuwatesa hao viumbe wasio na
hatia, eeh.., haikuwa na haja kufanya hivyo..’akasema.
‘Kwanini sasa huyo
mtaalamu akafanya hivyo, au hukubali kuwa alifanya hivyo,..?’ akaulizwa.
‘Kwasababu ..labda,
kwa vile walitaka kuhakikisha wao hawagundulikani, au…hata sijui, maana hata
maswala ya deni, hawakuwa na ujuzi nalo, walikuwa hawalifahamu hilo, si ndio
hivyo…labda kama walifahamu ni baadae sana, lakini hadi hapo, nilipoamua
kuwaelezea walikuwa hawalijui hilo, na hadi ilivyobainika, sizani kama wapo
waliofahamu kuwa kuna hilo deni ni la nan hasa, ila kama benk wanavyodai hilo deni ni la marehemu,
aliyejenga hiyo nyumba sehemu isiyo halali kwake,…’akasema
‘Una maana gani.,
kwanini hutaki kuliweka hilo wazi , kumbuka wewe umesema utakuja hapa kuwa
mkweli, je huo ndio ukweli wote, kwanini hilo deni huliweki bayana.?’ Akaulizwa.
‘Nina maana gani kwa
vipi…hivi kwanini hamuangalii upande wangu..eeh, mnaangalia upande wa ..benki
sijui, au wa…je mimi haki yangu ipo wapi, je mnakubaliana na ..hukumu, kuwa
hilo deni ni la marehemu au mnapinga, na kama mnapinga kwa vipi, na kama
mnakubaliana na hilo deni, je deni langu na waliotangulia, mama na mama mlezo,
atalilipa nani, mnanielewa hapo sasa…?’ akauliza.
‘Fafanua…’akaambiwa
‘Kama mnakubaliana na
dhuluma hiyo kuwa mama yangu alichofanyiwa ni sawa tu kwa vile yeye ni
masikini, eeh..basi, haina haja ya mahakama hii, ..na kuwasaidia tu,..hebu
wekeni hayo madai yangu na marehemu wazazi wangu kwenye thamani ya pesa, …mnaweza kukadria hilo,
mtaona kuwa hilo ni deni kubwa sana, kuliko hilo deni la benki, haya ni nani
anamdai nani hapo, je hadi hapo hamjanielewa mimi…?’ akauliza
Alipoona watu wapo
kimia,akaendelea kuongea…
‘Nawashangaa sana…,
nyie hii leo mnahangaika na shilingi ngapi hizo za deni la benki....ni sawa ni
pesa nyingi kwa hali ya kipesa, lakini je thamani yake inazidi hayo
aliyofanyiwa mama yangu,..?’ akauliza.
‘Haya…achilia mbali, mama
mlezi, je thamani yake inalingana na dhuluma waliofanyiwa, haya je inalingana
na mali niliyotapeliwa,, huenda mali hiyo mkasema ndogo, mimi sijui..kuna thamani
ya eneo na nyumba inathaminika, au sio, hivyo ni bei gani, ..haya pigeni
mahesabu ni shilingi ngapi, kama ingelikuwa kuuzwa, jumlisha na hiyo nyumba
iliyovunjwa,..…’akawa kama anauliza.
‘Acheni jamani, huyo
anayedai, kuwa deni si lake,..ni muongo, hilo deni ni lake,..na benki wanaodai
kuwa ‘niaba’…wanadai deni,…, wanamudai huyo mdaiwa..ni sawa, wafanye hivyo, kwa
vile wao ni wakala tu,…na wao wametumika hivyo, mnielewe hapo, yaani
nawashangaa kwanini vichwa vyenu ni vigumu hivyo…’akasema na kucheka kidogo
‘Una maana gani hapo…?’
akaulizwa
‘Hahaha…mimi hadi hapo
nimeelezea vya kutosha, huo ndio ukweli wote…hilo deni ni la marehemu, kwa maelezo niliyokwaisha kuyaelezea, kama
alikubali, eeh, kubeba jukumu la wanandugu zake, akatumia pesa yake, sasa ni
wajibu wake kubeba hilo deni kwa niaba yao,, waacheni benki wafanya kazi yao…’akasema
‘Bado tu hamjanielewa
hadi hapo eeh…?’ akauliza akiwaangalia mawakili na baadae hakimu.
‘Ndugu usitake
kutupotezea muda hapa…tuambie hilo deni limepatikanaje, na ni nani mwenye hilo deni,
ni marehemu au..na je benki wana haki ya kulidai hilo deni, wamdai nani ambaye
ni halali ya hilo deni, kama wewe ulilitengeneza kwa utapeli wako, kwanini hilo
deni walilipe watu baki, wewe si ulitakiwa umdai baba yako au sio, sasa kwanini
ukalipeleka kwa marehemu..?’ akaulizwa
‘Hahaha, mimi sasa ninaweza
kusema hiyo kazi ni ya polisi, au kama mumeshindwa mtafuteni mtaalamu na
mjuvi,..ataweza kuwasaidia kwa hilo, ila mimi nimeleezea ule upande
wangu,..zaidi ya hapo mnanipa kazi mimi ya polisi, thibitisheni kwa nyaraka,
hilo deni sasa ni la nani..mimi siwezi kufanya kazi hiyo maana mimi sio polisi…’akasema
‘Wewe mtu
vipi,..usitupotezee muda wetu hapa, …ulisema upo tayari kukiri kosa, na upo
tayari kubainisha kuwa hilo deni ni la nani,..hapa unaongea kama mtu
aliyechanganyikiwa, unawachanganya watu,, awali sisi tulikuelewa,lakini sasa
yaonyesha umechanganyikiwa…’akaambiwa
‘Mimi
nimechanganyikiwa kwa maelezo hayo…hahaha,…waulizeni madocta kuhusu akili yangu
mimi,….…tafadhali, nimejaribu kuwalezea kwa namna ya kipekee kabisa, wenyewe
mumeona yaliyotokea, na hayo niliyowaelezea ni ukweli mtupu, sijadanganya, hata
kidogo, mashahidi wapo, je deni la benki na deni la wadhulimuwa ni lipi kubwa,
ni nani anatakiwa kumlipa nani,…na je si hilo deni sio halali kwa marehemu,
chukueni kalama na …mtagundua kuwa, hilo deni bado ni dogo sana.. ..’akatulia
Hakim sasa
akawaangalia mawakili wawili,….
‘Kwa kuwasaidia tu,…wajiulizei,
je hilo jengo lililojengwa lilijengwa kwenye eneo halali, kama sio halali, hilo
eneo ni la nani, walitafute hilo kwanza..na je ni kweli mama yangu aliwhi
kutendewa hayo, huo unyama, na huo unyama una thamani gani, ni nani walifanya
hivyo,..kwanini hukumu haikutolewa, kihalali,..hiyo sio kazi yangu, au sio,
nitakuwa naingilia kazi za polisi, muheshimiwa hakimu, naomba haki itendeke…’akasema
huku akiinamisha kichwa chini kama
kuomba hivi…
‘Wewe ulipoanza
kuongea awali, ulisema umekuja kukiri kosa, na kukiri kosa maana ni kukubali
ukweli….je huo ndio ukweli wa kukiri kosa,..ni nani atakuelewa hapo, au lengo
lako lilikuwa kuongelea kuhusu mama yako, ili hakimu akuonee huruma…?’
akaulizwa na wakili.
‘Nyi mlitaka
kufahamu ukweli wa hilo deni, si ndio
hivyo, ukweli wa hilo deni ndio huo nimeshawaambia…je waliotenda hivyo, hawana
deni…semeni ukweli wenu kutoka moyoni, je ni haki kilichotendeka, hilo deni la
benki ni kigezo cha kuivuta mahakama, ije kuwajibika, na nyie watendaji mjue
wajibu wenu, ..sasa nimewafafanulia…’akasema
‘Tunachotaka kufahamu
kwanza n jinsi hilo deni wanalodai benki, lilivyofanyika, mengine yatafikiriwa
na hakimu, ukweli umeuelezea, amesikia, kuna harakati za kuutathimini, kama ni
kweli au la..ila kwasasa tunataka kujua ukweli kuhusu hilo deni lililopo benki…’akaambiwa
‘Mimi naona ushahid
wangu umetosha, …na kama mtachukua maelezo yangu kama ushahidi basi msisahau
kuchukua maelezo ya mama na ya kwangu, kama ushaihidi kwa ajili ya haki ya wazazi
wangu, kwa ajili ya mali iliyochukuliwa isivyo halali..kwa vile tu, eti mimi ni
mwanaharamu…’akasema na kutulia kimia
Hakimu akageuka na
akawa anaongea na wazee wa baraza, baadae akawageukia, watu na kusema;
‘Mawakili wa pande
zote mbili waje hapa mbele..’akasema hakimu na mawakili wale wawili wakafika,
pale mbele ya hakimu, wakawa wanaongea, kukawa na ubishani fulani,..hasa kwa
mawakili hao wawili, baadae hakimu akawa anawaelezea jambo, na baadae
wakaambiwa warudi sehemu zao.
‘Hii kesi ni ya ina
yake…tumepoteza muda mrefu sana ili kuweza kuipata maelezo y akutosha, ili haki
itendeke… na mengi aliyoongea huyo shahidi, yana mantiki, yanakera na kama
itathibitika kuwa ni kweli, sheria itachukua mkondo wake,..kwa hivi sasa bado
hayana ushahidi wa kutosheleza …,’akatulia
‘Yeye kasema wapo
mashahidi wa kuthibitisha hayo, hebu tumsimamisha mzee mtupe tena, athibitishe
hayo maelezo yake…, lakini baada ya hapo, tunahitaji, wewe ..uliyetoa maelezo
yako hapa utuambie hilo deni limetokaje benki..achilia mbali, ulipizaji wako wa
kisasi, tunataka jinsi gani deni hilo lilivyotoka benki na kwenda kwa marehemu,
je ni kweli marehemu alikopa yeye, au ni hujuma zako wewe mwenyewe au kuna kitu
kilifanyika huko benki…’akaambiwa
‘Sawa muheshimiwa
hakimu…lakini bado tunadai ushahidi upande wa wanaodi kuwa deni hilo sio la
marehemu, ni haki yao kutupatia huo ushahidi, bila hivyo, mimi yangu yatakuwa
ni maelezo tu, na mwisho wa siku benki wana ushahidi wa kisheria, itasaidia
nini hapo…sasa kama maelezo yangu bado hayajaeleweka, mimi nitawatupia mpira
wanaodai vinginevyo, nitaendelea kuongea tu,…’akasema
‘Mzee mtupe aje sehemu
ya mashahidi…’akasema hakimu..
Hakimu aliposema hivyo
sauti yake ikamezwa, na ghasia, kule mlangoni
kukatokea ghasia, kuna mtu alikuwa anataka kuingia, na watu wamejazana..kwahiyo
ikawa kama ghasia fulani ya kusukumana.
‘Ni nani huyo anayeleta
vurugu huko mlangoni…na nyie askari mnafanya nini sasa…?’ hakimu akauliza
‘Ni mimi muheshimiwa
hakimu, ..nimekuja kutoa ushahidi unaohitajika..’sauti ikasema
‘Ushahidi gani huo
unaohitajika, na ni…, nani kakuambia anahitajia ushahid wako kwa hivi sasa…?’
akaulizwa
‘Ushahidi wa deni,
linalozungumziwa hapa, naomba kwa hisani yako niweze kuuonyesha..’sauti ikasema
‘Wewe ni…’kabla hakimi
hajamaliza hiyo sauti ikasema
‘Muheshimiwa hakimu…,
ili tuimalize hii kesi, huyo shahidi aliyepita ni mjanja, anataka kupoteza
muda, ili hilo deni liendelee kueleweka hivyo kuwa benki walilitoa kihalali,
kiu ambacho sio kweli,……’sauti ikasema na hakimu akamuangalia wakili anayetetea
madeni, halafu wakili wa benki.
Huyo mtu sasa akawa
kapewa nafasi ya kupita kwenye kundi la watu…watu wakawa wanampisha kwa heshima
sasa…
‘Ni nani huyo, ..?’
akauliza hakimu akiwaangalia mawakili.., na kabla hajajibiwa, huyo mtu
aliyeongea kwenye kundi la watu akajitokeza,..
‘Ni mim muheshimiwa
hakimu…’akasema
‘Mtu wa jamii…umetokaje
hospitali…?’ aliyesema hivyo, ni wakili wa madeni, akimuangalia huyo mtu
aliyeingia,, halafu akaangalia kile alichokuwa ameshikilia huyo mtu.
‘Ni nini hicho, …?’
akauliza wakili wa utetezi
‘Ushahidi, ule
ushahidi tuliokuwa tukiutafuta ambao ndio utabainisha ukweli wa hilo deni, na
shahidi aliyekuwa akiongea analifahamu hilo,…’akasema na hapo wakili wa kutetea madeni,akamgeukia hakimu na kusema;
‘Muheshimiwa hakimu
naomba muda kidogo nitete na huyu shahidi yangu mpya, alikuwa mgonjwa, katika
harakati za kutafuta ukweli wa hilo deni,…na sasa keshapata nafuu, natumai
baada ya kuongea naye, nitajua kama asimame yeye kutoa ushahid au tumsimamishe
mzee mtupe…’akasema wakili
‘Mzee mtupe
nimemsimamisha mimi, nataka ahakiki maelezo ya huyo shahidi aliyekuwa
akijieleza hapo…maana yeye kaongea mambo mengi, ni lazima hayo maelezo yake yahakikiwe
kwanza, kama kweli watu waliumizwa, kama kweli maeneo yaliyochukuliwa isivyo
halali,..nataka ushahidi wa hilo, na hayo yanahusiana vipi na hilo deni,…’akasema
muheshimiwa hakimu.
Hapo mzee mtupe akawa keshafika kwenye kizimba
cha kutolea ushahidi, na kufuata utaratibu wa kimahakama, baadae akaanza kuhojiwa,..
‘Mzee mtupe unamfahamu
huyo mtu, shahidi aliyetoa maelezo marefu ya maisha yake…?’ akaulizwa
akionyeshewa huyo shahidi aliyepita
‘Ndio ninamfahamu…’akasema
‘Kwa vipi…?’ akaulizwa
‘Kwanza, nilikuwa
simfahamu vyema awali…, kuwa ni nani..kabla hajaniambia ukweli kuhusu yeye,..na
huo ukweli kanielezea siku chache kabla hatujakamatwa, na kuletwa hapa…tuje
kutoa ushahidi ..nilimfahamu kama bosi wangu aliyeniajiri kama mlinzi na
mpelelezi wa mambo yake…’akasema
‘Wewe ulikuwa
ukitafutwa na polis kwa makosa gani…?’ akaulizwa na wakili wa madeni
‘Nilifanya kama
muajiri wangu alivyonielekeza nifanye,…’akasema
‘Muajiri wako ukiwa na
maana gani…?’ akaulizwa
‘Huyo aliyekuwa akitoa
maelezo …’akasema
‘Uliambiwa ufanye nini…?’
akaulizwa
‘Nikanyamazishe nguvu
alizowekeza marehemu, kuhusu ….’akasita kumalizia
‘Kuhusu nini, elezea…’akaambiwa
‘Kuhusu kuwatesa
wanafamilia hao,…’akasema
‘Kwanini wateswe…?’
akaulizwa
‘Hayo anayafahamu huyo
mtaalamu,na huyo mwajiri wangu hakulipedna hilo, alipogundua kuwa kuna watu
wanateseka, akaniamrisha mimi nifanye juhudi za kidawa, ili hayo mateso yakome…’akasema
‘Ulifanyajae sasa…?’
akaulizwa
‘Niliwahi kuongea na
marehemu, mtaalamu, aliwahi kunielezea hizo nguvu zinapatikana wapi, kwahiyo,
ilibidi nifanya safari,…nilifanya, lakini pia kuna mambo nilitakiwa niyafanye
haraka, kala sijaondoka, ,…ili kuwaokoa watu wengine waliotakiwa kuuwawa ..ilikuwa sio kazi rahisi, ..maana mfani kuna mtu mmoja nitakiwa nimuwahi, asije kunywa simu, nikafika nikakuta tayari keshakunywa, ..nikawahi kumpa maziwa na dawa ya kuondoa ile sumu, polis walinielewa vibaya…’akasema
Hakimu akaingilia kati
na kusema;
‘Ngoja kwanza, naona
kuna mambo mengi kumuhusu huyo mtu, nia yangu kumsimamisha sio hiyo, ni kuhusu
deni kwanza…’akasema hakimu, na wakili aliyekuwa akimuhoji akatulia.
‘Je hayo aliyoelezea,
kuwa wewe ulimdhulumu eneo, nyumba, kutoka kwa ndugu yako marehemu, ni kweli,
…?’ akaulizwa
‘Siwezi kulikataa
hilo,…au kulikubali,… ni kweli dada, au mdogo wangu ..aligawa eneo kwa huyo
shahidii, lakini kiukweli, haikuwa ni sahihi, eneo lile lilkuwa mali ya urithi
wa familia…’akatulia.
‘Familia kama familia
inatambulikana.. , na sisi ndio wanafamilia wa hilo eneo.., ni kweli eneo lile
alipewa marehemu kulihudumia, baadae akalimikisha kivyake bila kukubaliana na
wanafamilia,…sisi hatukuwa na ugomvi kwa yeye marehemu dada..kulimiliki maana
yeye alikuwa mwanafamilia,..na kila mwanafamilia alikuw na eneo lake, sasa…’akatulia kidogo, akionekana kusikia
maumivu.
‘Una tatizo gani…mbona
kama unahisi maumivu…?’ akaulizwa
‘Nina maumivu
yananitesa sana, upande huu wa kushoto, na..huku kwenye koo, kuna uvimbe..vyote
hivyo vinanitesa sana,..na siku za karibuni wameniambia eti nina ugonjwa,
ambao…ooh, wanahisi kuwa ni kansa…’akasema na watu wakaguna kidogo
‘Kansa, una uhakika na
hilo…?’ akaulizwa
‘Ni kweli, nimepimwa,
wakagundua hilo…’akasema
‘Ilikuwaje, ina maana
ni kweli alivyosema shahidi..?’ akaulizwa
‘Wameniloga tu hao
watu,…nilikuwa nakula samaki mfuka ukanasa kooni, ukawa hautoki, hadi leo,
unanitesa sana na huku upande wa kushoto, ni mshutuko,..niliupata mshutuko,
basi nikahis kitu kama sindani ikichoma,..na imekuwa ikiendelea hivyo hivyo
hadi leo, nateseka sana…’akasema
‘Sasa kwa kauli yako
ni nani wanakuloga..?’ akaulizwa
‘Hata sijui…nahisi ni
hao watu wanaodai mali isiyo halali yao…’akasema akionyesha kuogopa
‘Sasa tuambie
ukweli..elezea ilikuwaje kama mlikuwa na maeneo yenu kwanini sasa mkataka
kuchukua na eneo la dada yenu wakati mnafahamu ni mali yake halali, je uhalali
wa mali yake ni upi kama haruhusiwi kufanya apendavyo..?’ akaulizwa
‘Ni mali ya familia,
na isingelikuwa ni tatizo , kama angeliendelea kulimiliki yeye, lakini tatizo
ni kwasababu alimrithisha mtu baki, …sasa kila mmoja akifanya hivyo, kizazi cha
familia husika kitapatia wapi eneo, hamuoni kuwa maeneo yataishia kwa watu baki…’akasema.
‘Swali hapo, je ni
kweli huyo marehemu dada yako, aliamua kwa hiari yake, kulimilikisha hilo eneo
husika na nyumba…, kwa huyo shahdii na wewe ulikuwa unalifahamu hilo…?’
akulizwa.
‘Ndio lakini…muheshimiwa
hakimu…’akataka kujitetea, lakini wakili wa benki akasema;
‘Inatosha, jibu lako
limetosha usieleze usiyoulizwa…’akasema huyo wakili, hakimu akasema,
‘Huyo ni mtu
ninamuuliza mimi maswali, nataka uelezee…’akaambiwa
‘Sisi kama familia
tulikaa kikao, tukajadiliana, tukaona sio sahihi, na hayo yalifanyika hata
wakati marehemu yupo hai, lakini yeye aliamua kufanya hivyo, kutokomoa kwa vile
yeye aliona hana matoto na hapendi watoto wa ndugu zake wafaidike na urithi w a
mabau zetu…’akasema
‘Lakini umekubali kuwa
eneo hilo lilikuwa halali kwa dada yenu, kama ilivyo kwenu, kila mmoja ana eneo
lake, haijalishi kuwa ni mwanaume au ni mwanamke.. si ndio hivyo…?’ akaulizwa
‘Ni halali kwake kwa
vile lipo mikononi mwake, lakini bado lilikuwa linatambulikana ni la familia,
yeye ni mmoja wa wanafamilia, …sasa ikitokea yeye kafariki, eneo hilo hurudi
kwenye mikono ya familia, kwa manufaa ya familia,…maana maeneo yote ni haki ya
damu ya familia, sio haki ya damu nyingine za kurithi,..ndio mila zetu
zilivyo…’akasema huyo mzee.
‘Lakini eneo hilo
mlikuja mkaliuza kwa damu nyingine isiyo ya familia, kuna tofauti gani hapo…?’
akaulizwa
‘Limeuzwa kwa
makubaliano ya wanafamilia wote, na kilichopatikana kimegawanywa kwa
wanafamilia wote, ..na tumefanya hivyo, ili isije kuleta fitina baadae..hayo ni
mambo ya kifamilia, na kisheria yanakubalika, …sijui kama nimekosea, kama
nimekosea, naomba nirekebeshwe…muheshimiwa hakimu,…’akasema
‘Unaweza kurudi sehemu
yenu ya mashahidi utaitwa, ukihitajika tena…’akasema hakimu.
Baadae hakimu akaangalia
saa yake…, halafu akamuangalia wakili wa utetezi wa madeni, huku akisema
‘Muda umebakia kidogo,
je wakili umeshamaliza kuongea na shahidi wako mpya..?’ akaulizwa
‘Nimeshaongea naye, muheshimiwa
hakimu…na ningelipenda mahakama yako tukufu, imruhusu shahidi wetu aliyefika, asimame
, ili aweze kutoa ushahidi ambao mahakama inautaka, ushahdi utakaothibitisha
hilo deni ni la nani..’akasema hakimu na wakili wa benk akataka kutoa
pingamizi, lakini baadae akasita.
‘Kuna pingamizi lolote
kutoka kwako wakili wa benki ..?’ akauliza hakimu…wakili wa benki akasogea
mbele, akasimama, na baadae akamuangalia hakimu, akasema;
‘Ndio nina pingamizi…..’akawa
anafungua makabrasha yake
WAZO LA LEO: Kwenye kuitafuta haki,
tusiangalie ile haki inayobeba ubinafsi wetu tu, ya kuwa hilo lifanyike kwa
vile tu litasaidia masilahi yanayoigusa nafasi etu, au masilahi yetu. Haki ya
kweli huangalia pande zote, kuwa lifanyike hilo kwa masilahi ya wote hata kama
kwa muda huo halitagusa nafasi zenye masilahi yetu. Haki iwe kwa wote sio kwa
masilahi binafsi, huo ndio uadilifu.
Ni mimi: emu-three
Way cool! Some very valid points! I appreciate you penning this post plus the rest of the website is very good.
ReplyDelete