Mimi bado nikawa hospitalini, na nilikuwa nasubiria
vipimo vya mwisho, ili niruhisiwe,…kichwa kilikuwa bado kinanisumbua, na docta
ndio akaamua nichukuliwe vipimo vingine waone tatizo lipo wapi.
Na muda huo nikiwa hapo hospitalini, akili yangu
ilikuwa haitulii, kwani nilikuwa nasubiria maelezo ya kesi ilivyokuwa, lakini
siku hiyo hakuna aliyetokea, baadae nikapata ujumbe wa simu kutoka kwa mama
mjane kuwa hali yake sio nzuri, kashindwa, kuja..
‘Nisamehe sana kaka, lakini nahisi sipo vizuri, ila
siumwi tu, naona nikija hapo hospitalini nitaishia kulia, nikiwa mbele yako
nadeka sana…’akaandika, hivyo, ikabidi nimpigie simu, alipopokea nikahisi kama
anataka kulia, kabla sijasema kitu akaanza kwa kusema;
‘Kwani nini umenipigia, waona sasa natakani kulia…’akasema
kweli akiwa kama anataka kulia.
‘Kwani imekuwaje huko mahakamani, leo naona nyote
hakuna hata mmoja aliteyaka kuja kunielezea, kulikoni..?’ nikamuuliza.
‘Hakuna tatizo, ni kuchoka tu,..na jinsi
ninavyojisikia, nikaona nipumzike kwanza, nitakuja kesho tukijaliwa, na wale
maaskari, kuna vitu wanafuatilia, nahis ndio maana wameshindwa kuja huko…’akasema.
‘Najua wewe haupo vizuri kutokana na hiyo kesi, au
sio..?’ nikamuuliza.
‘Aaah ,… hayo ya kesi sasa aah…, nimeshamuachia mungu,…wao
wanafikiri wakimsingizia mume wangu uwongo ndio wameshinda, hawawezi kushinda
kihivyo, na hata kama watashinda kesi, basi hawajashinda mbele ya mungu,…’akasema
‘Ni kweli, hata hivyo mimi sizani kama watashinda
hiyo kesi,..usijali, kesi safari hii itahukumu kwa haki, …’nikasema.
‘Hahaha, Usijali,…utafikiri nacheka kufurahi, unajua
alichosema hakimu, ..hadi sasa hajaona ushahidi wa kumshawishi, kuwa hilo deni
sio sahihi kwa marehemu, ..ina maana ushahidi wa benk bado una nguvu..’akasema.
‘Ni nani aliongea jana..?’ nikamuuliza.
‘Si huyo chizi wanayemuita chizi, sijamuelewa bado ,
yeye ni nani..lakini kila hatua naanza kumfahamu…sasa sijui kama ni kweli
aliyoyaelezea au kajitungia…’akasema
‘Alisemaje kwani..?’ nikauliza.
‘Eti deni hilo deni, ni la kweli na ni deni la
marehemu..’akasema.
‘Alitamka hivyo hivyo ulivyotamka wewe…?’ nikauliza.
‘Hata kama katamka vingine lakini alikuwa na maana
hiyo..’akasema.
‘Unaweza kurejea maneno , kwa jinsi alivyotamka yeye…?’
nikamuuliza na hapo akatulia kidogo kama anawaza, halafu akasema;
‘Aliulizwa hilo deni ni la marehemu, yeye akasema
hivi… ‘Kwa jibu la haraka ni KWELI…’akasema.
‘Hivyo tu..?’ nikauliza.
‘Ndio, mengine ni mawakili waliongezea wakikariri
kauli yake hiyo…’akasema.
‘Kwa neno hilo …’kweli’ bado sio uthibitisho kamili, kuwa kweli
kakubali kuwa ..hilo deni ni la marehemu,…yategemea ni nini atakuja kuongea
baadae, bado, nategemea mengi kutoka kwake kama kweli anaongea kwa nia ya
kutubia…’nikasema.
‘Mhh, mimi nimeshakata tamaa…’akasema.
‘Kwanini ukate tamaa, sib ado kesi inandelea, bado
Dalali, hajaitwa, hujui atakuja kusema nini,..vipi mzee Mtupe, hakuitwa
kuendelea kuhojiwa…?’ nikauliza.
‘Hapana..nashangaa maana alikuwa hajamaliza…’akasema.
‘Unaona, huo ni mtindo wa huyo wakili, atarejeshwa
tena, kukubali, baadhi ya mambo, na baada ya hapo, itakuwa ni nafasi ya hakimu
kuunganisha ushahid wote ili aweze kuhukumu…’nikasema.
‘Haya …ni kwa vile wewe hukuwepo
mahakamani..ungelikuwepo ukasikia …hasa kauli ya hakimu, ungelijua kuwa kweli
kesi, hapo upande wetu,..nahis itakuwa kama ile safari ya kwanza…’akasema
‘Ni kuulize wewe, kutokana na hayo maelezo ya huyo
shahidi, bado unaamini kuwa deni kweli sio la marehemu..?’ nikauliza.
‘Mimi licha ya….sisemi kwa vile nataka nyumba, hapana
naongea kutoka moyoni, hilo deni sio la marehemu mume wangu…nahis kuna njama
zimepangwa…na najiuliza kumbe ni njama za wanandugu..’akasema.
‘Ukiwa na maana mzee mtupe, mtaalamu na yule mtoa
vibali,..lakini wao, hawajaongelewa kuhusiana na hilo deni au sio, wao waliongelewa
kuonyesha jinsi gani watumisi waliopewa dhamana wanavyoweza kugushi, ..au kutoa
vibali isivyo haki, au sio…’nikasema.
‘Lakini hapo tunazungumzia benki,…’akasema mama
mjane.
‘Enzi hizo, hiyo benk, ilitawaliwa na watu wasio
waaminifu…kama watu wa vibali, kama watu waliopewa dhamana wameweza kufanya
hivyo, ..hata huko benki kunawezekana, na imethibitishwa kuwa walikuwepo watu
wasio waaminifu, ndio maana wakawafukuza..huo ushahidi kuwa lolote liliwezekana
kutendeka, kwanini walifukuzwa…’nikasema.
‘mhh..banki wao wanataka ushahid wa makaratasi,…’akasema.
‘Na hakimu je…?’ nikauliza.
‘Sijui yeye, atasimamia wapi…’akasema.
‘Yeye atasimamia kweli ukweli na haki…ataunganisha
ushahdi wote, na kuliangalia tukia zima…na…nikuulize tu, huyo shahidi aliongea
nini zaidi…?’ nikamuuliza.
‘Alielezea maisha yake, yeye alipotokea, na sana sana
alimuelezea mama yake, kumbe mama yake
alizalilishwa, na kubakwa, ..na yeye ni matokea ya huko kubakwa,…’akasema
‘Oh…inasikitisha si ndio hivyo…?’ nikauliza.
‘Kiukweli inasikitisha sana, lakini mume wangu
anaingizwaje huko, yeye sio aliyemzalilisha huyo mama yake, na …nakumbuka mume
wangu aliwahi kuongea kitu kama hicho…’akasema.
‘Alikuambiaje..?’ nikauliza
‘Yeye alikiri kuwa zamani, mdogo wake huyo aliwahi
kufungwa, kisa ni kwa vile alisadikiwa kuwa alimbaka mfanyakazi wa ndani,
lakini kumbe mfanyakazi huyo wa ndani alikuwa muhuni…sasa hivyo ndivyo mume
wangu alivyokuwa akifahamu,..alikuwa hajui undani wa tukio lenyewe..’akasema.
‘Ilitokeaje mpaka akaongea kuhus mdogo wake kufungwa…?’
nikauliza
‘Nakumbuka tulikuwa tunaongea maswala…mmh,
ndio..ilikuwa kipindi namuonya kuwa asimuamini sana ndugu yake kwenye maswala
ya benki, na yeye akawa anamtetea sana…’akasema.
‘Ilikuwaje mpaka ukaongea hilo…nahis hapo kuna jambo,
hebu kumbuka vyema…?’ nikauliza
‘Ilikuwa tunahitajia pesa,…na ilikuwa ni jambo la
haraka, akasema, ndugu yake akimbie benki akamchukulie, na ..muda ulishapita,…akasema
yeye ndugu yake akienda, kama bado wafanyakazi wapo ndani, akimpigia simu..mtu
mmoja, atamruhusu ..na atachukua hizo pesa…’akasema.
‘Huyu mtu ni nanii…?’ nikamuuliza.
‘Hakumtaja, ila alisema huyo ndugu yake ana namba
yake…’akasema.
‘Ok..ok…sasa kwanini wewe ukaingiza maneno ya
kumtahadharisha mumeo dhidi ya ndugu yake…?’ nikamuuliza.
‘Kuna mambo mengi…yakitaka uwepo wake, anasema ndugu
yake amfanyie…’akasema.
‘Mhh..na sahihi yake je…?’ nikauliza.
‘Anaweza kumwambia lete hapa niweke sahihi, anaweka
sahihi hata bila kusoma kilichoandikwa,…’akasema.
‘Lakini …hata kama hakusoma kilichoandikwa, lakini
yeye si anafahamu ni jambo gani, linalohitajika labda, ..hata akiweka sahihi
yake, bila kusoma haitamuathiri kitu…’nikasema.
‘Hapo nimechukulia mfano tu,,….wakati mwingine
aliongea na watu wa benki, huyo ndugu yake akachukua pesa, na yeye mume wangu
ndio akaenda au akaja kujaza karatasi ya kuchukulia pesa,…kifupi ni kuwa
alimuamini sana ndugu yake…’akasema.
‘Hebi nikuulize wewe, kwanini wewe ukatilia shaka
hilo,…wewe si umeishi naye huyo shemeji yako..unamfahamu matendo yake, kwanini
ukamtilia shaka..?’nikamuuliza.
‘Kiukweli kuna matendo ..ya uhuni, anayo tu..uwongo
..anao tu..lakini anajua kuigiza, hasa akiwepo kaka yake, anajiigiza
unyenyekevu, uaminifu, utafikiri mcha mungu fulani, lakini kwa mimi
ninayemfahamu kwa vile nipo naye karibu …na mara nyingi, naona matendo yake…simuamini
kama anavyomuamini kaka yake…’akasema.
‘Samahani lakini…ulisema aliwahi kukutaka kimapenzi,
ukagombana naye,..je hiyo yaweza kuwa ni sababu ya kutokumuamini, kivile…au?...
maana kama anataka kumuibia hata ndugu yake..mkewe, atakuwaje muaminifu si ndio
hivyo..?’ nikamuuliza.
‘Hiyo kwangu niliidharau..nilijua ni ujana tu..sema
niliposikia hayo maelezo ya huyo shahidi ndio nime..mshusha sana, naamini sio
ujana tu……kama ndio yeye alimfanyia mama yake huyu shahdii matendo hayo
machafu, ..sitaweza kumuamini tena…’akasema.
‘Ok…sasa, huyo shahidi kwanini alipize kisasi kwa
mume wako…kwa jinsi ulivyonielezea awali, ni kama huyo shahidi alifanya mambo
kwa kulipiza kisasi, japokuwa hatujaona ni nini alikuja kufanya…na..huyu mtu ni
nani …nikiwa na maana…’nikatulia nikiwaza.
‘Anasema katika sehemu ya pili ndio ataelezea jinsi
ya hilo deni….’akasema mama mjane
‘Sawa, ngoja tuone ukweli wake…lakini mhh…bado
sijamuelewa,…yeye alikuwa akifanya kazi wapi…maana nijuavyo mimi, mtu ambaye …nahisi
…aliyekuwa banki, ni huyo ambaye hadi leo hajapatikana..sasa huyu mtu..kichaa ni
nani…?’ nikauliza.
‘Hadi hapo alipofikia, hajajifichua vyema, sijui
kwanini mawakili hawajataka kumfichua, nahisi ni katika namna ya kujilinda au
kumlinda huyo shahidi maana kesi inaendelea, je wakimuua, …au wanafanya hivyo,…
kulinda ushahid mkuu, ambao, nahisi watakuja kuutoa baadae..’akasema
‘Exactly…upo sahihi…japokuwa mimi
bado, namuweka Dalali mbele, kama mshukiwa mkuu, sijui kwanini..’nikasema.
‘Mshukiwa mkuu wa nini..?’akauliza mama mjane.
‘Wa hilo deni, ajali iliyosababisha kifo cha mumeo,…ikiwa
na maana, yeye anafahamu undani wake..hiyo hali ya kuigiza anaumwa,..hawezi
kutembea, kwanini afanye hivyo…unaona, kwanini, kwanini… hizi ‘kwanini’ bado zinanifanya
nimuone mshukuwa ni yeye, akisimamishwa, kesi itakuwa…’nikatulia maana simu
yangu iliashiria, mtu anapiga.
‘Kuna nini…?’ akauliza mama mjane.
‘Kuna mtu ananipigia, tutaongea baadae, ..’nikakata
simu na kuangalia mpigaji wa simu,…ilikuwa ni namba ya yule mdada wa kule
alipolazwa Dalali…
Nikasita kumpigia, sikutaka kuingiza mambo mengi kichwani,
na hapo tu, kichwa kilishanza kuuma, na wakati nataka kuiweka simu nipumzike,…
mara hiyo simu ikaanza kuita tena,… nikapokea tu,namba ilikuwa ni ile ile…
‘Pole sana, nasikia bado unatibiwa, vipi
unaendeleaje..?’ akauliza.
‘Sijambo, huenda nikaja kuruhusiwa,…’nikasema
‘Mhh…vipi kuhusu hiyo kesi yenu inaendeleaje..?’
akauliza.
‘Bado inaendelea,…mimi sijawahi kufika huko,… vipi kwani
kuna ushahidi unataka kuutoa au…?’ nikamuuliza.
‘Nataka nikutumie picha ya video, kuthibitisha kauli
yangu,…’akasema.
‘Kuthibitisha kauli yako, ipi hiyo…?’ nikamuuliza.
‘Kuwa mtu wako anaweza kutembea, na ni mwanga,
mchawi, nilikuambia hivyo..’akasema.
‘Lakini hadi sasa akitembea si ndio anachukua mazoezi,
kwani hadi sasa hajaweza kuinuka, au kutembea..?’ nikamuuliza
‘Kwa maelezo ya madocta, bado…bado hawezi kutembea na
madocta wanasema hivyo hivyo kuwa huyo mtu ni wa kuhudumia kitandani, hawezi
hata kuinuka mwenyewe…’akasema.
‘Alitembea akienda wapi, ulivyomuona….?’ Nikamuuliza.
‘Kama siku ile….na nikaamua kumfuatilia mimi mwenyewe…’akasema.
‘Wewe haikukutokea kama ilivyotokea kwa mlinzi..?’
nikauliza.
‘Mimi hawaniwezi…nilimfuatilia,…akawa anatembea hadi
barabarani, hapo akaita pikipiki, ikamchukua hadi baharini..’
‘Hadi baharini, kufanya nini…!!!?’ nikamuuliza
‘Mimi nikachukua pikipiki pia, tukawa tunamfuatilia,
huyo dereva wa pikipiki akafika sehem akaniambia anaona maajabu, nikamwambia
aniachie mimi niendeshe,…’akasema
‘Ndio mkafika baharini, ikawaje..?’ nikamuuliza
‘Yeye….akafika sehemu pale alipokuwa anakaa chizi…akaangalia
huku na kule,…alipoona hakuna mtu, akaanza kuondoa maboksi yaliyokuwa yamelazwa
aridhini, kama kitanda…sasa kwa bahati, kukatokea watu…akayarudisha kwa haraka,
…baadae akaanza kurudi…’akasema.
‘Hiyo sehemu waweza kuikumbuka vyema…?’ nikauliza.
‘Ni pale ofisi kwa yule Chizi, unajua watu wanaogopa kufika
eneo hilo,..kila aliyefika hapo anakutwa na majanga, kwahiyo ni sehemu
imejitenga kihivyo…’akasema.
‘Wewe je…?’ nikamuuliza
‘Nifuate nini sasa…mimi nilitaka kuhakiki hilo jambo,
kuwa huyo mtu anatembea lakini anakwenda wapi, mengina hayanihusu, ..sasa
waitaka hiyo video nikutumie au niache tu, maana sijui kama itasaidia kitu…’akasema.
‘Nikuulize tena,..ni nani bosi wa hiyo hospitali..na
je ni kweli yupo nchi za nje..?’ nikamuuliza.
‘Nakutumia…’akakata simu na haikupita muda,aakatuma
hiyo video..
************
Kesi likuja kuanza siku nyingine, na shahidi yule
yule akaitwa,…
‘Vipi khali yako…?’ akaulizwa na hakimu mwenyewe
‘Naendelea vizuri, haijatokea tena ile hali, nahisi
naelekea kuzuri…’akasema
‘Unahisi ni kutokana na jinsi ulivyoongea huo ukweli,..?’
akaulizwa
‘Ndio muheshimiwa hakimu, nataka niongee kila kitu
ili haki iweze kutendeka..’akasema
Hakimu akawageukia mawakili,…
‘Je bado mna maswali ya kumuuliza..huyo shahid kabla
hajaingia sehemu ya pili ya maelezo yake, ila..shahdi usipoteze muda na maelezo
mengi ya maisha yako, sisi tunataka kile kinachohusiana na hii kesi…’akasema
hakimu.
Mawakili wakasema aendelee tu na sehemu ya pili,
lakini kabla hajaendelea wakili wa kutetea madeni akasema;
‘Samahani kidogo…nataka kufahamu, jambo moja kabla hujaanza
maelezo yako,.. wewe unasema kuna mmoja wapo wa watu ambao hukutaka kuwataja,
ulidai yeye alitumia pesa zake kuwarubuni watu watoe ushahdi dhidi ya mama
yako…’akasema na kabla hajauliza hilo swali shahidi akasema;
‘Mimi nimenukuu alivyoandika mama, kuwa, huyo jamaa
ndiye alitumia pesa zake kumtetea ndugu yake, huku akijua kakosea, huku akijua
kuwa ndugu yake alimpa mimba huyo mfanyakazi wao wa ndani....hakutaka kuulizia
zaidi kuufahamu ukweli, hta pale mama alipotaka kujielezea…’akasema.
‘Wewe mwenyewe unamfahamu vyema huyo mtu, marehemu…?’
akaulizwa.
‘Ndio…nimewahi kukutana naye na hata kuongea
naye…’akasema.
‘Alikutambua kuwa wewe ni mtoto wa huyo mama…?’
akaulizwa
‘Hapana..nilipokwenda kusoma, nilihakikisha narudi
kivingine,..hata sura yangu ilibadilika, na hata hawa wazee, yule msamaria wa
kwanza muuza dawa,, ..ambaye sasa ni marehemu alikuja kunifahamu baadae sana,
baada ya kuamua kumwambia,..ndio hapo akaanza kujipendekeza kwangu,. Akasema
yupo tayari kunisaidia kulipiza kisasi..’akasema.
‘Lakini wengine hadi leo hawajakutambua..au na wao
walishakutambua?’ akauliza.
‘Mhh…nitakuja kuliongea hili, kwenye sehemu ya pili
kama hutojali…’akasema
‘Nataka kuwa na uhakika tu, ..jinsi ulivyomuona huyo
unayesema alitumia pesa zake kumtoa ndugu yake, na akafanya hadi ndugu yake
ashinde kesi, je kweli anaweza kufanya tendo kama hilo..?’ akauliza
‘Najua una maana gani, lakini nataka kauli yako
isikike..una maana tendo gani hasa..?’ akauliza.
‘La kuwarubuni watu ili watoe ushahidi wa uwongo..?’
akaulizwa.
‘Kiukweli..hafanani hivyo, na sijasema yeye
aliwarubuni, hapo sina uhakika hata mama hakuandika hivyo, aliandika kuwa, yeye
alikuwa tayari kutoa pesa zake, ushahdi upatikane, bila kujali kuwa ushahid huo
ni wa halali au la…kwa kipindi nilichomfahamu mimi,..huyo jamaa, marehemu,..ni
mtu mwema, mkweli..na watu wanamsema hivyo …’akasita wakili wa benk aliingilia
kati.
‘Usiseme hisia zako, ongea ukweli ulivyo..’akaambiwa
‘Ukweli ndio huo…yupo hivyo ni ,mwema, sasa ni
kwanini alijiingiza huko, mimi hapo siwezi kuelewa…’akasema.
‘Watu wanasema yeye hakufahamu lolote lililotokea
kati ya mama yako, na huyo baba yako..yeye alielezewa kivingine,
..unavyomfahamu baba yako, yeye ni mjanja sana, yeye alitunga maneno ambayo
yalimjaza hasira huyo kaka yake na kuamini kuwa mama yako alikuwa
hivyo…’akaambiwa.
‘Mimi nategemea sana alichoandika mama yangu, mama
yangu namuamini sana, sio muongo, waliomfahmu vyema wanaweza kulithibitisha
hilo..sasa kama alichoandika kina uwalakini,..mim sijui..kwangu mimi huyo na
mdogo wake, wote sawa tu…’akasema
‘Katika maelezo yako..aliyefanya hivyo, kumdhulumu
mama yako na hadi akafikia huko, ni huyo baba yako, lakini hadi sasa tunayeona
kuathirika na kisasi chako, ambacho japo hujaanza kukuilezea, ni ..kaka mtu,…’akaambiwa.
‘Hahaha, huyo baba yupo wapi…?’ akauliza.
‘Hujatuambia baba yako ni nani…’akaambiwa
‘Kutokana na maelezo, yangu, nisingelipenda kuwataja
hao watu majina kwa hivi sasa, ila..huyo baba,..kwangu mimi sio baba, kwani
alinikataa, alimtesa mama yangu,…atapata taabu sana ,..na yeye mwenyewe
atahitajika kuja kutubia hapa mbele..najua hadi sasa anakana…anasema sio kweli,
sio yeye…ngoja tuone,…’akasema
‘Je hiyo
sehemu ya pili, itaeleza lolote kuhusu hilo deni, maana wewe haujathibitisha
kuwa kweli hilo deni ni la marehemu au …la…’kabla hajamaliza wakili wa benki
akasema;
‘ Keshasema bwana…na tunaimani hiyo sehemu ya pili
utaelezea, jinsi deni lilivyotoka kisheria,…hapo ndio tutajua kuwa kweli
umepona..na ushahdii wako hapa una uzito..’akasema wakiliw a benki
‘Naombeni mnipatie nafasi…kwani nahisi hali si nzuri
sana..nahisi kuna kitu kina..kuna matu anataka kuharibu ..lakini hataweza…’akasema
‘Mtu gani…?’ akauliza
‘Mhh…, sehemu ya pili,..nitakayo elezea hapa,..
itatoa ushahidi wangu…ambao ndio ukweli kuhusu hilo deni…’akasema shahidi.
‘Kuwa ni la marehemu au sio…’akasema wakili wa benk.
‘Kuwa kweli limepewa marehemu kwa kulipiza kisasi,…’akasema
wakili wa kutetea madeni na huyo shahidi akatabasamu kidogo, halafu akasema;
‘Wote mpo sahihi,..naomba niendelee…’akasema.
‘Endelea, jaribu kwenda kwa haraka…’akasema hakimu.
NB: Je hilo deni ni la kweli kwa marehemu..….TUTAENDELEA
WAZO LA LEO: Toba ya kweli ni tiba,...tiba ya maradhi ya nafsi, na hata maradhi ya mwilini, na pia ni tiba ya matatizo...kuna matatizo mengine,sababu yake kubwa ni dhuluma.
Ni mimi:
emu-three
3 comments :
Do you have any video of that? I'd want to find out more details.
For most recent news you have to visit web and on world-wide-web I found this web page as a most
excellent site for latest updates.
This is a great tip particularly to those new to the blogosphere.
Brief but very accurate information… Thanks for sharing this one.
A must read article!
Post a Comment