Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Sunday, February 12, 2023

TUTAFAKARI

 


Wakati nakaribia ofisini kati kati ya barabara nilimuona jongoo akiwa anakatisha barabara, akijitahiid Kwenda kwa kasi...kwa mwendo ule sizani kama angeliweza kufika upande mwingine wa barabara bila kukanywaga na gari.  Nikajiuliza hivi mdudu kama huyu anajuaje kuwa atapita hadi upande mwingine wa barabara bila kukanywaga na gari,  je anajua kuwa magari yanapita hapo kila sekunde...hajui anajua sijui..mjumvi wa hayo ni MOLA pekee...

Nilichukua kijiti kwa kuogopa nikawa najaribu kumsogeza, akajikunja kujihami, ikawa ni shida hatimaye nilijitosha nikamshika kwa mkono...na kumfikisha upande mwingine mwa barabara akiwa kajikunja baadae akajikunjua,...nahisi alishajua siwezi kumdhuru....

Nilimweka chini, na kumwangalia kwa muda, baadae alijinyosha vizuri na kuendelea na safari yake, sijui anaelekea wapi...

Swali...Je huyu jongoo alijua ataokolewa, maana ningelimuacha angelikanywagwa na gari...labda..sijui! Je wangapi walimpita huyo jongoo bila kumjali, je ni kwanini mimi nikaingiwa na huruma hiyo, kwani wengine hawana hiyo huruma...?

Wakati nawazia hilo, akili yangu ikarudi nyuma, NIKAKUMBUKA ...wakati nakimbilia ofisini nilimuona mama mmoja akiwa na mtoto mdogo, wamekaa pembeni mwa barabara wakiomba, kwa muda ule wakati napita eneo hilo, yule mama wa huyo mtoto alionekana kupitiwa na usingizi, lakini yule mtoto alikuwa macho

Nakumbuka yule mtoto, alimuangalia mama yake akamuona mama yake kalala, yeye sasa akawa anainua mkono, lakini kwa mashaka, kuomba kwa wapita njia,...nahisi aliiga jinsi mama yake alivyokuwa akifanya... hakuna aliyemjali, hakuna aliyempatia chochote, hata mie, kwa haraka zangu nilimpita nikiwahi kazini, sikumpatia chochote..Moyoni nilijuta...nimejuta sasa wakati nawaza!

Swali...ni kwanini wengi walimpita mama huyo na mtoto wake bila kumpatia chochote,...wakijua huyu mama ni muhitaji, ni ombaomba, ni masikini na ana mtoto mdogo, Je huyu mtoto anaihisije anajijengea hali gani akilini mwake....sijui, unanielewa!

KIUKWELI hakuna anayejua huyo mama kapitiwa na madhila gani hadi kufikia hatua hiyo ya kuwa omba omba, sio jambo rahisi...je kwa siku hiyo anaweza akawa kasidiwa... , je mara ngapi hakusaidiwa...au mara ngapi alisaidiwa na aliyemsaidia labda kwa kumpa chochote kwanini alifanya hivyo, je nihuruma tu au...

Nikakumbuka kisa cha mdudu aliyekuwa akiishi ndani ya bahari, mgonjwa, kati kati ya miamba...kila mara kunguru anatafuta wadudu au chochote huko anapotafuta, na akifika eneo hilo anakidondosha hicho alichobeba, sijui kwa makusudi kwa bahati mbaya!...na kiu hicho huzama hadi pale alipolala huyo mdudu mgonjwa na mdudu huyo mgonjwa hupata riziki yake...Mola ni mwema na muweza wa kila jambo, hutoa riziki kwa kila kiumbe chake kwa jinsi ajuavyo yeye...

TUTAFAKARI KWA MAKINI...Sisi ni nani...na tupo hapa duniani kufanya nini....tuwafanyie nini wenzetu,hasa wenye uhitaji au tuwafanyie nini viumbe vya mola...

NI WAZO TU....

Ni mimi: emu-three

No comments :