Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, September 17, 2018

YOTE NI KWA MAPENZI YA MUNGU-49




‘ Wewe mtu wa jamii, siku zote umekuwa mjanja,lakini kwa hili…hujashinda…na kwa hili unaweza ukabeba lawama,…., wewe unafikiri kwa ujanja wako wa maswali eeh, unitega, eeh…umeugundua ukweli ulivyo…, hahaha…hujaugundua ukweli wote ndugu yangu, ukweli wote naufahamu mimi….hahahaha….’akacheka sana halafu akatulia.


‘Tuambie sasa ili tumalize hili tatizo, tuache kushindana, kwa masilahi ya wenye haki, haki ya mama mjane na mayatima, si unalifahamuhilo, hao watu wanahitajia haki yao, je tukiwadhulumu tutapata nini, eeh, hebu niambie…’nikasema nikimuangalia machoni.

‘Lakini ile sio haki yao….hivi hamuniamini, lile eneo sio haki yao, ni eneo liliporwa, kama ndio unalizungumzia hilo…’akasema

‘Tunazungumzia deni, je hilo deni la benki ni haki yao, je wao wanastahiki kulilipa…?’ akaulizwa

‘Kama wao ndio warithi, wana haki ya kulilipa, maana wanabeba dhamana ya marehemu…’akasema

‘Je ni kweli kuwa merehemu ndiye alichukua pesa hiyo benki , kwa kuomba deni, kihalali,..kuacha hayo maelezo yako, je ni kweli marehemu ndiye alifika na kuweka sahihi kuwa anataka kukopa…tuambie ukweli wako na mwenyezimungu anakusukia,..na mama yako huko alipo anasikia…?’ nikamuuliza


‘Mhhh.. sio kwamba nayafanya haya kwa kukushandana na wewe, hapana ni kwa vile wewe unalazimisha ukweli, kwa jinsi unavyoutaka wewe, …’akasema


‘Tuambie sasa ukweli uliojificha, ukweli hukusu hilo deni, …’nikasema

‘Ukweli …mnaotaka nyie …ndio huo nilioongea mimi,..huo  ndio ukweli wenyewe, kilichobakia labda, ni  kuse-ma, ni nani eeh, mnataka mtu afungwe, mnataka mtu aonekane ana kosa, lakini kosa halikunzia hapo kwenye deni,..hilo la benki hamnielewi…’akasema na kugeuka huku na kule, halafu akainamisha kichwa chini.

‘Majaliwa…..’nikaaita hivyo


‘Niambie, …jamani nimeshawaambia ukweli wote, na vizuri wewe mwenyewe umeuleta huo ushahidi…kila kitu hapo kipo wazi, ni nani alichukua pesa, ..eeh, sahihi ip,o jina lipo, na dole gumba lipo, mnataka nini sasa, eeh…?’ akauliza


‘Ukweli,….ndio ushahidi huo unaonyesha hivyo, lakini je mbona kuna hitalifay nyingi kama nilivyokubaisnishia, inaonyesha kabisa, kuwa malipo hayo, hayakutekelezwa kihalali,…nyaraka zimejionyesha, ..hata polisi wakifuatilia wataligundua hilo, sasa sisi  tunausubiria ukweli kutoka kwako ili tuokoe muda, ili, hukumu iende kihalali, huenda sio wewe, ila wewe uliidhinisha tu, huenda kuna watu walifanikisha hilo kwa kupitia wewe…’nikasema.


‘Hakuna alifanikisha hilo kwa kupitia mimi,…ukweli nilioelezea ndio ukweli unaobainisha hilo, hayo yalitendekea kihalali,…’akasema hivyo halafu akakaa kimia, niligeuka kumuangalia hakimu, nikamuona anaangalia saa.


‘Majaliwa muda umekwisha, unajua ukitoka hapa unapelekewa jela,…’nikasema


‘Hahaha, hivi unafikiri mimi naogopa kwenda Jela, labda huko ndio nitaweza kutekeleza adhima yangu, ili..…hahaha, mimi nimekuwa jela, tokea siku niliposoma ile zawadi kutoka kwa mama….mimi sina tofauti na mfungwa, japokuwa mimi ni tajiri..lakini eeh, utajiri huo una maana gani kwangu eeh,…eeh, hauna maana kabisa kwangu nimekuwa nikiishi kama  masikini, nateseka moyoni, mwilini, akili haipo kabisa hapa duniani…sasa kilichobakia, labda, useme, nimfuate mama yangu, na nawaahidi siku nikikanyaga jela, mtakuja kutoa maiti yangu …’akasema na hakimu akamuangalia kwa uso wa mashaka.


‘Sikiliza ndugu Majaliwa,…kila jambo lina mwisho wake, ..na vyovyote iwavyo, usiku au mchana hauwezi ukaendelea kuwa hivyo, kutakucha na kutakuchwa, ndivyo maisha yalivyo,, yaliyofanyika yamefanyika, na yanamwisho wake…sasa tuone jinsi gani tutayamaliza haya kwa salama na amani…haki iweze kutendeka,…’nikasema


‘Kwahiyo unataka mimi nifanye nini , nikiuke haki, ili haki mnayotaka nyie itendeke, kwani mimi …si nimeshawaambia kila kitu au….?’ Akauliza


‘Hapana…ukweli bado haujakamilika…ushahidi wa kuwa wewe ndiye uliyehusika na hayo madeni tunao ndio huo hapa, je ukifungwa haki itakuwa imetendeka…?’ akauliza


‘Labda kama hakimi hajui kazi yake vyema…au nimekosea muheshimiwa hakimu…’akasema akimuangalia hakimu, hakimu akawa kimia, na jamaa akaendeela kusema.


‘Sikiliza wewe una akili sana au sio, ..mbona kwa hili hutaki kutumia akili yako vyema…’nikasema


‘Naitumia vyema, sema wewe hujui…ungelijua ukweli ulivyo usingelisema hivyo, akili yangu inaona mbali zaidi ya unavyofikiria wewe…’akasema


‘Kwa hilo..sizani kama wewe unaona mbali..maana wewe unataka kuficha makosa, au wewe tuambie..sisi ambao hatuoni mbali, je kwanini ulifanya hivyo, na ulifanya vipi, na…nimekuuliza swali, ni nani aliyekuja kuweka sahihi , kwenye kukamilisha hilo deni liwe deni, …kiukweli sio marehemu, sasa ni nani…?’ nikamuuliza.


‘Wewe ulikuwepo siku ile, unaposema kiukweli sio marehemu…?’ akauliza


‘Ndio maana nakuuliza wewe uliyekuwepo, uliyesimamia hilo,…utuambie,..ukumbuke ukweli wote ndio utamweka mama yako mahali pema peponi, na ukweli wako, ndio ..utasafisha, nafsi yako, ili upone kabisa, na ugonjwa huo ulio nao, niamini hivyo, baada ya ukweli hutateseka tena…na wanaohusika wawajibike,…’nikasema.


‘Ndio maana nilifanya haya ili haki itendeke,…lakini ninavyoona mimi, eeh… haki inaweza isitendeke…’akasema


‘Kwanini…?’ nikauliza


‘Kwasababu nyie mnachoangalia ni deni la pesa, hamtaki kuangalia deni la uhalisia, deni la madhara, madhara aliyopata mama yangu, madhara, ya dhuluma,…je hayo mtayafidia kwa shilingi ngapi…eeh, je hilo sio deni…?’ akauliza.


‘Hayo hakimu atayaangalia,..lakini kwanza tuambie ukweli…ni nani aliyefika hapo benki, na kuweka sahihi, …ili deni litambulikane, ni nani aliyeweka dole gumba, unasema ni marehemu, mbona sio kweli,…’nikasema


‘Unasema sio kweli, dole gumba ni la nani…?’ akauliza


‘Ndio hapo tunataka kufahamu, kama sio marehemu aliyefika kuchukua huo mkopo, kuweka sahihi yake, je dole gumba la …marehemu lilipatikanaje,…na kiukweli merehemu hakuwa na tabia ya kukopa, hilo hamkuliangalia wakati mnatengeneza hilo deni, je marehemu aliwahi kukoa kabla ya hapo…?’ nikamuuliza


‘Mimi sijui…’akasema.


‘Kiukweli hakuwa na tabia hiyo ya kukopa, ..na hilo unalitambua wewe vyema,..ndio maana ukabuni mkakati huo, ambao uliutambua kama mkakati-moto…ukishirikiana na …’kabla sijamaliza akasema;


‘Kwahiyo …ooh…umelifahamu hilo eeh…mkakati moto, ulikuwa ukichoma dhuluma,..matendo ya watu wabaya, ambayo, …wadhamini wa haki hawakutaka wadhulumaji hao wawajibishwe, je ingefanyika nini…ndio nikabuni mkakat huo mkakati moto nashukuru umeligundua hilo…lakini sio moto wa kuangamiza, bali ulikuwa maoto wa kuugunzua dhuluma..’akasema an kutulia.

‘Sasa tuambie…kama ulikuwa mkakati wa kuangamiza dhuluma kwanini ukawa unaunguza ushahidi…ushahidi ambao ungetumika kuipata haki, ushidi ulioficha ukweli kuhusu hayo madeni…?’ akaulizwa


‘Hayo mimi sijui…hayo unayoyasema, ni hadithi zako…moto kwangu ulikuwa kuunguza dhuluma, na deni lilipwe…kama kupitia mahakama lilishinikana, kama kupitia kwa watendaji,…ilishindikana, haya moto utashindwa…’akawa kama anauliza.


‘Bado hujausema ukweli ndugu majaliwa…mimi najaribu kukubembeleza kwa vile ninafahamu kuwa wewe huna hatia, ila umajitumbukiza kwenye hatia kwasababu fulani,…sasa tuambie tujue…’nikasema


‘Hahaha…mtoto wa majalalani…unatakiwa useme ukweli, ambao hata wewe huufahamu, ukweli gani unahitajika zaidi ya huo niliokwisha kuulizea,… hahahaha, naona sasa wakati umefika, labda, nishushe akili zangu ziendane na nyie, labda mtanielewa, …’akainua uso, na kumuangalia hakim.


‘Muheshimwa hakimu, mimi naona tuyamalize haya mambo, na mengine yote nitayaacha mikononi mwako…ukitaka nifungwe sawa,..ukitaka niu-awe sawa, …mama yangu kafa, nani alijali, haki yake ipo wapi, au mnafikiri hayo niliyoelezea, ambayo aliyaandika yeye, ni ya uwongo…eeh, nani anabisha hapa…’akasema akigeuka huku ana kule..


‘Haya mama mlezi kafa na sababu kubwa ni kuteseka kutokana na ndugu zake, mangi aliyoyapitia sikuweza kuyahadithia haya…hicho ni kisa cha mama mgumba,…nani alimjali, kwa vile hakuwa na ndugu wa kumtetea,..eeh,…haya tumuache huyo,….msamaria mwema kafa, yeye alifahamu mengi, lakini kwanini aliondoka bila kuusema ukweli..je.., mimi nina thamani gani zaidi ya hao watu …’akatulia


‘Sasa , nyie mnataka nisema hata yale nisiyotakiwa kuyasema, ili iweje,..ili nije kubeba lawama nyingine,…niliyosema yalikuwa yanatosha, kutenda haki, na mengine tumuachie mungu mwenyewe,….maana huo ndio ukweli wenyewe..…mengine ni kutafutana lawama tu ndugu zanguni…’akatulia


‘Mama aliteseka jamani hivi nyie hamtaki kuliona hilo,…au kwa vile sio mama yenu…inaniuma sana kuwa hata kulipiza kisasi sitakiw kufanya, …angalau haki basi,…najua huko alipo anayasikia haya, au nadanganya,aau mtu akifa basi haki yake haipo ndio maana watu wa haki za binadamu hawataki mtu akiua yeye asiuwawe, ina maana marehemu yeye hana haki, si ndio hivyo...?’ akaniuliza mimi.


‘Ni kweli, …mama yako huko alipo anakusikia…ndio maana unapata taabu hizi unazozipata, ..ungejtubu makosa yako,  kwa kusema ukweli leo hii ingekuwa ni jambo jingine kabisa…’nikasema

‘Nitubu makosa yangu, umeshaona kuwa mimi nina makosa,..haya haki hiyo nitaitegemea kweli….haya ndio nikikuambia huo ukweli unaoutaka wewe unafikiri itakuwaje, je ukweli huo utafanya haki itendeke, siamini hilo..niambie wewe kama hivi sasa umeshasema nitubu makosa yangu, makosa gani hayo eeh, je haturuhusiwi kulipiza,..kama kweli ulitendwa, ndio kusamahe kupo, sawa, …lakini …hebu niambie mimi nina makosa gani…? ‘ akaniuliza.


‘Bila shaka, hapa ni mahakamani, ukisema yote, mahakama itakuhukumu kwa haki…’nikasema.


‘Nihakikishieni kwa hilo, nikuulize swali je  mama hakudhulumiwa, hakuteswa, na ikawa sababu ya kifo chake,…,’akasema akiniuliza


‘Kwa maelezo yako alidhulumiwa…’nikasema


‘Kwa maelezo yangu eeh…!!  Ina maana hata hayo maelezo yangu huyaamini, unaona ilivyo, mimi nimeshawagundua mlivyo, ndio maana siwezi kuwaamini tena, je umeamini kutokana na maelezo yangu au kutokana na ukweli wenyewe…?’ akauliza


‘Nimeyaamini, kutokana na maelezo yako, kutokana na jinsi ulivyosoma mama alivyoandika, …ndio maana bado nahitajia maelezo zaidi, najua yapo mengi hujataka kuyasema ambayo yalitendeka, baadae sisi kwa hayo ya mama yako tumeshayaweka kwenye kumbukumbu, sasa sisi tunataka yale yaliyotokea baadae, na kuleta deni…’nikasema.


‘Sasa kama mama alidhulumiwa kwa hayo maelezo, haki yake ipo wapi, je alitendewa haki…?’ akauliza sasa akigeuka kumuangalia hakimu, hakimu, alikuwa akimuangalia tu


‘Unaona…’akasema hivyo tu,


‘Ina maana huamini kuwa haki itatendeka..?’ nikamuuliza


‘Haki ya mama..ilitendeka…?’ akauliza


‘Hatujui kwanini haikutendeka, lakini kwa sasa itatendeka, muamini hakimu wako, yeye yupo kwa ajili ya kutenda haki , kwa mujibu wa sheria,….na ndio maana mpaka sasa kakuvumilia, japokuwa muda umekwisha, wewe hujaliona hilo…’nikasema.


‘Tunakuhakikishia haki itatendeka, wewe timiza wajibu wako, ….’aliyesema hilo ni hakimu.


 ‘Lakini kwanini mimi ndiye nisumbuke kwa hilo, hiyo ni kazi ya polisi jamani,  au sio, mimi sijafanya kosa , mimi nilitimiza wajibu wangu wakati nipo kazini,nikiwa nafanya kazi benki niliwajibika ipasavyo,…, na kila kitu kipo wazi, nyaraka si hizo hapo, kaleta huyu mtu, sijui zili..sina uhakika kwakweli kama zilipatikanaje, lakini niamini hivyo, kuwa ndio zenyewe…’akatulia


‘Ndio zenyewe …hazina shaka, nimethibitisha hilo huko benki, na waliokuwa nawe wamethibitisha hilo,…na wewe si umeona sahihi yako, au…?’ nikamuuliza


‘Wewe mtu wa jamii wewe…nilijua tu, mwisho wa yote, tutakutana hapa, unakumbuka nilikuambia nini siku ile tulipokutana hospitalini…?’ akaniuliza


‘Uliniambia na kuniahidi pale uliponiacha hospitalini, kuwa wewe unakuja mahakamani kuusema ukweli, na mimi nikakuamini hivyo, nilijua kweli utakuja kuyakiri yote hayo, uliyowahi kuyafanya,…nilijua kweli wewe ulichanganyikiwa kwasababu ya hayo ambayo sisi tulikuwa hatuyajui…’nikasema


‘Ndio…’akasema hivyo na kutulia


‘Sasa…, .kwa ajili ya dhuluma alizofanyiwa mama yako,..nilijua kwa hilo, utakuja kukiri  na kuelezea kila kitu, …na kesi hii ingelikwisha mapema tu, sasa..ni kwanini ulikuja kubadili nia yako…?’ nikamuuliza


‘Sikubadili nia yangu,…ila nataka nikuulize swali moja, je kauli ya marehemu inapingwa, unaweza ukafanya kinyume na matakwa ya kauli ya marehemu…?’ akaniuliza


‘Yategemea, wakati mwingine marehemu anaweza kuongea kwa vile…kapata taabu, akaongea yasiyostahiki, na ambayo huenda hayatamsaidia, lakini sisi tuliobakia tunaweza kuyapima hayo, aliyoyaagiza,..tukisimamie kwenye haki na ukweli… na kama yanafaa, basi tutayafanya , lakini tukiona hayafai, kwa masilahi yake huko alipo na masilahi ya hawa waliopo hai, tunaweza tusiyafanye, sasa ni yepi hayo ili tuweze kuyapima…’kabla sijamaliza akasema.


‘Marehemu…mdaiwa, ..mimi nitamuta hivyo hata kama nyie hamtaki, yeye alisema kuwa au yeye hana  tabia ya madeni, …si ndio hivyo,.?’ Akaniuliza


‘Ndio hivyo, hata wewe walifahamu hilo…’nikasema


‘Lakini je ni kweli…japokuwa yeye alikuwa akiwashauri watu wasipokope,..je yeye hakuwa na deni..maelezo yangu yote nilielezea madeni ambayo kayabeba yeye, kutokana na dhuluma, na alifahamu kuwa kweli kanunua eneo la dhuluma, na alimtetea, mtu aliyemdhulumu mama yangu kwa pesa zake yeye mwenyewe, …je hilo halijaendana na kinyume na kauli yake…?’ akauliza


‘Wewe umesema hivyo…kuwa anadaiwa kwa vile alitumia pesa zake kuwasaidia wakosaji, lakini je una uhakika kuwa kweli alikuwa akifahamu ukweli kuwa hao wakosaji wapo hivyo,…walidhulumu, walimtesa mama yako, je wewe una uhakika na hilo, kuwa kweli alikuwa akifahamu na akafanya makusudi kwa kutumia pesa yake…?’ nikamuuliza.


‘Niliongea naye nikamuelezea kila kitu, lakini yeye hakutaka kunisikiliza, hakuniamini…akaishia kunikebehi, kwa vile mimi …au mama, ..si chochote kwake…yeye si ana pesa bwana, eti twende mahakamani, kwa vipi tena, waakti mahakama ilishahukumu…jamani, hivi, …hamlioni hilo kama ni dhuluma, mama hana mbele wala nyuma, huyu mwenye pesa, anatumia pesa zake kumdhulumu….haki ipo wapi hapo…’akasema na akawa kama anataka kulia.


Hapo nikasema;


‘Kiukweli hakuwa ana ufahamu huo,..marehemu angelijua hilo, asingelifanya hivyo kwa jinsi alivyokuwa akijulikana, ni kweli..yeye aliwaamini sana ndugu zake, yeye alifanya mambo kutokana na ushahidi ulioletwa mbele yake,…’nikasema.


‘Marehemu yeye aliamini mahakama imetenda haki, na mahakama ilihukumu kutokana na ushahidi,  sasa mimi nakuuliza swali,…je una uhakika kuwa kweli marehemu aliufahamu ukweli wa dhuluma za ndugu yake na bado akatumia pesa zake kumtetea,… nijibu kutoka moyoni mwako…?’ nikamuuliza

 Hapo akakaa kimia, halafu akainua uso, na kusema;


‘Mahakama ilitenda haki, kwa mama, lakini mahakama haijatenda haki kwenye hilo deni, mahakama si ilihukumu kuwa deni hilo ni halali, au….angalieni haya mambo kwa usawa…’akasema


‘Ndio maana baada ya uchunguzi hayo yote yanatakiwa kupitiwa upya, huwa inatokea, najua baada ya haya, kila kitu sasa kikiwa wazi, haki itatendeka…’nikasema


‘Kwahiyo nyie mnataka nifanye nini sasa…?’ akauliza


‘Tueleze ukweli ambao bado wewe hujatuelezea,….’nikasema


‘Ukweli uliobakia,…hauna maana, …’akasema


‘Kwetu una maana sana, maana ndio msingi wa hii kesi…’nikasema


‘Kwahiyo nyie mnataka nimuhini mama yangu, niende kinyume na …mama yangu, hapana,…ndio inaniuma sana, kwanini mama afanyiwe hivyo,…inaniuma sana,.. kwa vile mama alimpenda sana mwanaume aliyemtesa…mama, alinipenda sana mimi…mama, hakutaka nije nipate taabu au yoyote yule kutokana na hayo mateso aliyoyapata yeye, …lakini mimi nifanye nini sasa jamani…’sasa akawa analia.


Ikapita muda, maana jamaa alikuwa analia kweli.


‘Majaliwa, nahisi sasa utajisikia vyema, umelia, na umeondoa hisia moyoni mwako kuwa kweli unampenda mama yako, na umediriki kukifanya hicho mama yako alichotaka ukifanye, lakini je, kitamsaidia mama yako huko alipo, je kwa kuuficha ukweli huo, utatenda haki…?’ nikamuuliza


‘Mimi sijui…’akasema


‘Tutakusaidia kwa hilo…mama yako huko alipo yupo mbele ya haki, ambapo, haki haifichwi,…ukweli na matendo mema au mabaya hayafichwi huko, yupo hakimu anayejua kila tendo,..hebu tuambie ni kwanini hutaki kuusema ukweli uliobakia, ili haki itendeke hapa duniani na kesho ahera iwe ni sababu ya mama yako kusterehe…’nikasema


‘Mama yangu hana dhambi, na aliwapenda wote hata wale waliomtendea mabaya, kuna hao  waliomkata mama ulimi wake, na …bati lenye kutu, likampa tetenasi, ikaja kuwa kansa, akafa kwa mateso, aliwapenda wote, hao na hakutaka walippizwe kwanini…mimi hapo ndio….sijui kama ‘hapa akatulia , nahisi kuna kitu alitaka kukisema lakini akakitanisha.


Hakimu akawa anataka kuongea jambo…mimi nikaonyesha ishara ya kuomba muda zaidi.


‘Nia yangu ilikuwa kufanikisha kile nilichokipanga, ili huo ukweli nilioulezea uje kufahamika hapa mahakamani…na ili ikiwezekana haki ije kutendeke, na kama haki haitatendeka hapa, sijui itakuwaje, sasa kama mnataka nikaidi kauli ya marehemu, mimi sijui..unajua jamani mimi sikuwahi kumtambua mama yangu, mama alifariki nikiwa sijamjua vyema,..sasa mimi nampenda sana mama yangu, sitaki niende kinyume na yeye…’akasema.



‘Ina maana wewe hutaki roho ya mama yako itulie vyema huko alipo,…?’ nikauliza


‘Kwanini roho yake isitulie…?’ akauliza


‘Unakumbuka,…, mama yako hakukuagiza ulipize kisasi, mama yako hakutaka uje kudhulumu mtu, au watu wengine kwa madeni, je hilo hakuandika mama yako kwenye shajara yake..je hujayafanya hayo, je kwa kufanya hayo, unatarajia nini, mama yako atakuwa anaumia,, sasa sisi tunakushauri ndugu yetu kwa masilahi ya mama yako, sema huo ukweli ili haya mambo yaishe …’nikasema


‘Roho ya mama yangu ipo peponi, haya yanayotokea sasa, si yake, na wala mimi sijafanya kosa kwa hilo, ila najaribu kuitafuta haki ya mama, pia, najaribu kurejesha haki  zangu, haki alizoniachia mama mlezi…’akasema


‘Ni kweli, kwa mateso  aliyoyapitia mama yako…, haina shaka, yupo peponi,  lakini hakupenda ufanye uliyoyafanya, hebu kumbuka, ulisema nini awali…, kwenye hilo dafutari la mama yako, mama yako alikupa tahadhari, ipi… usije kufanya kufuru…usije kufanya mabaya, ni kweli si kweli…?’ nikamuuliza

‘Ni kweli…’akasema

‘Je umemtii mama yako…?’ nikamuuliza


Jamaa akanywea,…akawa kainamisha kichwa chini, baadae akainua kichwa , sasa akiwa kama anahema kwa nguvu, na kusema kwa sauti nzito..;


‘Nawauliza tena, je tunaruhusiwa kukaidi kauli ya marehemu…nakuuliza na wewe muheshimiwa hakimu, nataka hili liwe mikonono mwako wewe unayetimiza haki kwa uadilufu…?’ akauliza

Hakimu akawa kimia, baadae hakimu akasema;


‘Ukweli hauweze kufichwa, na ukweli ndio utamsaidia marehemu, kama marehemu alisema neno..kwa nia ya kuficha ubaya, …ubaya huo utamuandama huko alipo, lakini kama kauli yake ni njema..basi haina shaka, hatakuwa na lawama, na sisi wajibu wetu ni kuhukumu kwa haki,....sasa je hayo unayoogopa kuyasema yatamsaidia mama yako huko alipo…?’ akaulizwa

*********


‘Sikilizeni sasa niwaambiae   mama alimpenda sana baba, hata baada ya yote hayo, aliyotendewa, kwenye hiyo zawadi, yeye aliandika,…. na hilo nilikuja kulisoma siku ile nilipotoka kule hospitalini, nilipoahidi kuja kuyasema yote haya…jiulize ni kwanini nikaja kuisoma hiyo sehemu…’akasema


‘Yaani ilikuwa ni bahati, tu ….nikapitia sehemu hiyo…’akatulia


‘Mama yako aliandika nini…?’ nikamuuliza


‘Mama aliandika maneno mazito sana…yamenipa shida sana…yeye alindika hivi, sio kwa kunukuu, ila naelezea kwa uelewa wangu, … kuwa kwa vyovyote iwavyo, nisije kumdhuru huyo mwanaume aliyemtenda..,


‘Ukiwa na maana baba yako au sio…?’ nikauliza


‘Kwa vile yeye alimpenda sana, na akaigiza kuwa nikijaliwa nije  kumsaidia, kwa kadri nitakavyoweza, na vyovyote iwavyo, nisije kulipiza kisasi dhidi yake.., sasa nyie mnataka nifanye nini…’akasema kwa sauti ya ukali hapo, bila kujibu swali langu.


Mahakama ikawa kimia…


‘Unajua hayo yataendelea hivyo hivyo, na hatutaweza kufika mwisho, ..ni sawa mama yako aliandika hivyo, lakini kuna haki hapa inatakiwa kutendwa, na…licha ya kuwa tuna ushahidi hapa,..na ushahidi huo kwa hivi sasa unaonyesha kuwa wewe uliwajibika kutengeneza hilo deni, sijui unanielewa hapo…’nikasema.


‘Mimi sijatengeneza deni, kwa ushahidi huo,… utatengenezaje deni wakati wewe unadai pesa nyingi zaidi ya hilo deni, na je kipi kinakosekana kwenye ukamlifu wa hilo deni…’akasema.


‘Hayo yatakuja kufahamika..lakini sisi tunataka utuelezee ukweli ulivyo kuwa kwenye kutokea hilo deni, maana wewe ulihusika huwezi kulikwepa hilo…wewe unalijua hilo deni, chanzo chake na nani walihusika, kama sio wewe …tuambie tumalize hii,kesi, isiahirishwe kabla hujalifichua hilo…’nikasema


Jamaa akageuka kumuangalia hakimu, kwa taratibu akasema;



‘Haya, muheshimiwa hakimu…nitasema …ni hivi, aliyeweka sahihi  kwa mkono wake kuthibitisha hilo deni,  na aliyefanikisha kupatikana kwa dole gumba la marehemu,ni…ni…..DA-LALI…..’akasema


‘Dalali…baba yako…?’ nikauliza


‘Ndi-ndi-o….’jamaa akasema sasa kwa kigugumizi,…


‘Kwa vipi sasa tuelezee…’nikasema


‘Si-ooh, …’ na kabla hajamaliza kule mlangoni kukatokea vurugu, akageuka kuuangalia kule mlangoni, sijui alimuona nani,…maana pale tuliona hali ikimbadilika, jamaa huyu hakuweza kusimama tena, alikuwa kama kaona kitu cha kumtisha hivi..hata nilipogeuka kuangalia kule sikuona mtu, zaidi ya watu wakisukumana kama ilivyokuwa wakati naingia mimi,…na nilishtuka hakimu akisema

‘Vipi imekuwaje…?’ akauliza hakimu, na kwa vile nilikuwa nimeangalia kule mbele, sikuweza kuona kilichotokea kwa jamaa yetu, huku, nilisikia ..puuuh…

Jamaa kadondoka,…


‘Ni..nini…’nikasema na sauti ya hakimu ikawa imezidia sauti yangu,…


‘Askari kuna nini huko, ..na muangalieni huyo…muiteni dakitari na huyu ni nani tane…’


Ilikuwa ni, kigari cha kukukota cha kubeba mgonjwa kilikuwa kinaingia na jamaa mmoja kakaa kwenye hicho kigari,


Muda wa mahakama ulishaisha……



NB: Kwa hapa ndio kisa kiliishia, lakini kuna hitimisho, je ilitokeaje,..je kweli Dalali alifanya hivyo, tuwe pamoja kwenye hitimisho.


WAZO LA LEO: Ukweli unatesa, ukweli wenye kuficha dhuluma ni donda linatekenya, mtu kuuficha ni shida,…itafika sehemu kama jipu, litapasuka tu.

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

I would like to take the opportunity of saying thanks to
you for that professional guidance I have continually enjoyed browsing your site.
We're looking forward to the particular commencement of my school research and the general planning would never have
been complete without browsing your web site.
If I may be of any help to others, I would be pleased
to help through what I have gained from here.