Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, April 12, 2018

SIFA ZA MKE (MJENGAJI AU MBOMOAJI)



Babu aliniambia, katika maisha, tafuta mke mwenye sifa ya kujenga nyumba…

‘Mhh..babu…mimi kuoa bado.. .’nikaguna na kusema hivyo.

‘Unasikia mjukuu wangu…kuoa huanzia sasa kwa kuwaza ni nani mke anayefaa kwako,…’akasema

‘Sawa babu…’nikasema

‘Mke kawaida yake..hubeba dhamana mbili,…mke sio mchezo, ndio maana wao wana daraja kubwa sana…na heshima yao huanzia  pale wanapokanyaga kwenye miliki ya mume wake. Yeye huja kukamilisha familia, bila ya mke familia inakuwa haijakamilika. Tofauti na mwanaume ambaye amekutwa hapo….’akasema babu

‘Mhh, kwanini babu…’nikajikuta nimesema hivyo tu. Babu huanzia mbali kwenye hekima zake.

Mume yeye ana dhamana moja tu kwa vile yeye wajibu wake ndio huo, hana jinsi, yeye anawajibika kujenga na kuongoza familia.lakini hata weza bila ya kuwa na mke ..’akaendelea kuongea na mimi bado nilikuwa sijamuelewa.

‘Unajua mjukuu wangu, mwanamke ndiye anayeweza kujenga nyumba au kuibomoa nyumba kwa mikono yake mwenyewe,..’aliposema hivyo hapo nikashtuka na kumuuliza;

‘Kwa vipi babu…?’ akaniangalia kwa makini kama kunipima uelewa wangu.

‘Unaifahamu nyumba ilivyo, hizi nyumba za kisasa kwa mfano…’akasema

‘Ndio babu , si hizi zinajengwa kwa matofali..’nikasema

‘Haswa…’akasema

‘Sasa mke akija kwenye familia, kaolewa na mume wake, tusema kakuta nyumba, au hajakuta nyumba,sio tija sana..yeye anakuja na sifa hizo mbili, kuwa yeye anaweza kuijenga nyumba au kuibomoa nyumba..’akasema na kunikodolea macho, aakongeza kuniuliza

‘Huyo ni nani …?’ akaniuliza

‘Mke…’nikasema

‘Huyu mwanamke akifika hapo, anaweza kuijenga hiyo nyumba vyema kabisa ikawa nyumba bora, ya kisasa zaidi ikawa na furaha, na maendeleo yakapatikana, …na kizazi bora kikatokea hapo.

Lakini huyo huyo, anaweza akaja kubomoa nyumba, ikabomoka kabisa, kukawa ni chanzo cha uhasama ndani ya familia na jamii kwa ujumla, ndio maana mke anakuwa ni mtu muhimu sana kwenye maisha, bila ya kuwa na wake wema, amani duniani inakuwa ni kitendawili …’akasema

‘Mhh..babu sijakuelewa…’nikasema.

 ‘Nimekuambia hivi mwanamke akifika kwenye familia, anakuwa na sifa mbili, ana sifa ya kujenga au kubomoa…hapo tupo sawa…’akasema

‘Sawa…’nikasema

‘Lakini kwa mwanamume kwa vile ni wajibu wake kuijenga familia, ni wajibu wake kuwa msimamizi wa familia, ni wajibu wake kuwajibika na familia hiyo,…, yeye sifa aliyo nayo ni kujenga sio kubomoa, kwanini abomoe, na wajibu wake ndio huo kujenga, hilo ni jukumu lake, hana ujanja, na akilikwepa jukumu hilo, atapelekwa wapi…?’ akauliza

‘Kwa mkuu wa mkoa…’nikasema….babu akacheka.

‘Sawa kabisa, kwa ustawi wa jamii,...na hapa ndio utaweza kumpata hata kiongozi bora, sifa zake huanzia hapa…kwa mwanamke na mwanaume, hili kwetu hatuliangalii sana, lakini kuna siri kubwa hapa,…’akasema.

‘Mhh…’nikaishia kuguna.

‘Sasa nikuambia kitu,…mwanamke mwenye sifa ya kuvunja nyumba ni yule anayenyofoa zile tofari zilizojengewa nyumba kidogokidogo bila hata ya yeye mwenyewe kufahamu, huku akilalamika kila siku, nyumba ina nyufa, nyumba haifai, mume hanijali, ..na vitu kama hivyo..…’babu akasemana kutulia na mimi haraka nikauliza

‘Babu mke huyu anayanyofoaje matofali ya nyumba, kwani hajui kuwa ni kuharibu hiyo nyumba, na hayo matofali anapeleka wapi..??? ‘ nikauliza

‘Anaweza akajua au asijue kutokana na ufahamu wake ulivyo,..iwe ni kutokana na ufahamu wa elimu au malezi, na muhimu sana hapa ni kutokana na malezi, na malezi huanzia hapo kwa mke, mke ndio chanzo cha haya yote…’akasema.

‘Mhh, babu, mara nyumba, matofali, sijakuelewa babu…’nikasema.

‘Sasa ngoja nikufafanulie, mwanamke mbomoa nyumba, ni yule anayetumia mbinu za ujanja ujanja kupata pato la mumewe, kwa ajenda za siri,…anaweza kila siku akawa anatunga uwongo au ajenda za siri za kumchomoa mume wake pesa…siku hizi kuna hii michezo..au anataka magauni ya harusi, vipodozi vya gharama, na vitu kama hivyo,…na anayafanya haya yote  bila kumshirikisha mumewe, kuwa anataka hizo pesa kwa vitu kama hivyo,…’akatulia

‘Huyu mke,..anafanya hayo akifahamu fika pato la mume wake,..hebu jiulize huyu mke ana jenga au anabomoa nyumba…?’ akaniuliza

‘Ana…ana..bomoa, sijui…’nikasema kwa kusita sita.

‘Huoni kuwa huyu  anachomoa tofari za ujenzi wa nyumba yao,…tuchukulie mfano katika harakati hizi mume akose kazi, hii familia itakuwajem mke si atakimbia, jiulize ni kwanini kusiwe na makubaliano ya pamoja ya matumizi hayo….ili waangalia umhimu wake.
‘Mhh,….lakini…’nikasema
‘Nakuambia hivi…mke huyo hana ufahamu wa mbali kuwa pato hilo ni kwa ajili ya maendeleo ya familia, kusomeshea watoto, matibabu nk…yeye anachojali ni ubinafsi wake, kwanini asimshirikishe mumewe, mume wangu nahitaji kiasi kadhaa kwa ajili ya kufanya hiki, kwa ajili ya kuboresha , muonekano nak…

‘Kama anayafanya haya kwa ajengda ya siri..basi mke kama huyu, ananyoa tofali moja moja kwenye nyumba yao na,..mwisho wake nyumba itakuwaje..?’ akaniuliza babu

‘Itabomoka…’nikasema hapo kwa sauti.
‘Mke kama huyu, kwa vile ni mbinafsi….atatumia mbinu hizo hizo kwa mambo ya anasa, nywele za gharama utafikiri hana nywele…anataka mpaka nywele za maiti…na nimesikia siku hizi kuna asilimia sabini ya gharama hizo za kujirembesha..kukarabati mwili, yatoke kwa mume ..mapambo nak, ni sawa, lakini …haya kwa mke mwema, alitakiwa akubaliane na mume wake au sio, sio kutumia ujanja ujanja…’akasema babu.

‘Mhh, babu kwani kuna wanawake wapo hivyo…?’ nikauliza

‘Wapo, na wake hawa  hawatajali afya za mume, au hata za watoto wao, au kujali umuhimu wa elimu, yeye anachojali ni masilahi yake…matokeo yake , mume atakuwa mdhaifu, watoto halikadhalika, matokeo yake ni kuhatarisha maisha ya familia, ina maana matofali yanazidi kuchomolewa kwenye nyumba.

Kwa namna hii uimara wa nyumba hiyo, utakuwaje..?’ akauliza na mimi sikumjibu.

‘Mjukuu wangu kwa kawaida nyumba kama hiyo inakuwa haina maendeleo, zaidi ni ukosefu wa maelewano, maana kila mtu hapo atakuwa na ajenda yake ya siri,   magonjwa ya mara kwa mara yatakuwepo.., mikopo mingi na maisha ni mashaka mashaka tu…matokeo yake ni nini….’ Akaniuliza na mim nikakimbilia kuuliza hivi…

‘Na sifa ya pili ya mke ni ipi.?’ Nikauliza

 Sifa ya pili ya mke, ndio huyo mke mjengaji…

Mke mjengaji wa nyumba ni yule anayefanya juhudi, kuongeza uimara wa kuta za nyumba…kama nyumba ipo kama haipo atasaidiana na mume wake kuweka matofali, kuendeleza nyumba, na sio kuyaondoa matofali yaliyopo…’akasema

‘Kwa vipi babu…?’ nikauliza.
.
‘Huyu mke, hata kama hana kazi ya kuajiriwa,..yeye atamsaidia mume wake kuongeza kipato kwa mawazo, na wakati mwingine anafanya juhudi za halali kupata kipato, kwa kubuni biashara ndogondogo. Akimshirikisha mumewe kwani hayo yote ni kwa masilahi ya familia.

Mke kama huyu anakuwa na nidhamu ya pesa, hakuna kitu muhimu kwenye maendeleo,kama kuwa na nidhamu ya pesa…pesa kawaida yake hazitoshi, kama pesa hazitoshi ni lazima kuwe na utaratibu mnzuri wa matumizi yake, sio kutumia tu kwa vile zipo, lazima muangalie umuhimu kwa kila tumizi…mke mjengaji, anayafahamu haya kwa utaratibu walioyokubaliana na mumewe na akifanya zaidi, hatasita kumwambia mumewe.

Mke mjengaji,  hujitahidi hupunguza matumiz ya ndani yasiyo ya lazima, hafanyi kwa ajili ya kujionyesha kwa watu wengine, kuwa na mimi ninacho ..yeey hufanya kwa ajili ya wajibu wake na familia yake, kwa ajili ya maendeleo ya familia yake....huyu ana nidhamu, ana maadili mema, mke mjengaji

Mke wa namna hii, huwa mstari wa mbele kutetea kipato cha mumewe kisichukuliwe ovyo nje..kuna jamii, wanafamilia hupenda kufuja mali ya ndugu yao, na sio wanafamilia tu, hata watu wan je, au hata mume mwenyewe, anajitahidi kuongea na mumewe asiwe na tabia za ovyo, kulewa, nak..…mke mwema, hujitahidi kuona mali ya familia inatumika kwa utaratibu maalumu kutegemeana na bajeti yao.

Mke mjengaji, hujali sana afya ya mume wake,..anajua hilo ndilo jembe lake katika kutafuta kipato, basi ni lazima liwe imara,…liwe na afya…kwahiyo yeye atajitahidi kupika chakula bora, usafi wa ndani, ucheshi, ujirani mwema…kujenga mahusiani mema, ndani na nje..hata kimataifa.., ili kuongeza baraka , maana kipato ni pamoja na mahusiano na watu wengine au sio,..sio lazima kila kitu utakuwa nacho, mke huyu huejenga jina jema la mumewe….sio yule wa kutoa siri za ndani, kwa nia ya kumchafua mume wake.
.
Mke kama huyu ndiye yule anayeitwa mke mwema.

Kumpata mke kama huyu ni nadra, na ukimpata shukuru sana mungu wako…na ukimpata  tegemea maendeleo makubwa kwenye familia, na jamii kwa ujumla, tegemea elimu bora  na makuzi mema ya watoto wa familia, maana mke huyu hujali sana familia yake.
 Mke kama huyu ndiye chanzo cha amani duniani,…
Tumuombe mola wetu tuwapate wake wa namna hii, na wanaume wa namna hii pia. Ili tusiishie kupelekwa kwa mkuu wa mkoa….



Ni mimi: emu-three

No comments :