Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeSaturday, February 24, 2018

MKUKI KWA NGURUWE-86


Niliyoyakuta Dar, yalinikatisha tamaa, kwani sikutegemea kuwa kuna watu wamefikia kiwango hicho cha uhalifu wa kimataifa, maana hayo yaliyofanyika sio uhalifu wa kitoto,  na hao watu waliofanya hivyo, wamefanya kwa kujiamini,hawakujali kabisa kuwa kuna usalama, kuna polisi,… sikuamini..

Kama nilivyoambiwa nisigusie huko, lakini nataka muone jinsi gani tukio nzima lilivyotokea, hadi mimi nakaamua kukubali kuingia kwenye makubaliano ambayo baadae nimekuja kulaumiwa na kuonekana kuwa mimi ni miongoni mwao, huenda sitaweza kuthibitisha kwa mia kwa mia, lakini hivyo ndivyo ilivyokuwa, mkiniamini sawa msiponiamini, mimi nimetimiza wajibu wangu…’akasema na kutulia.

Mwenyekiti alikuwa katulia hakusema neno, nahisi mzungumzaji alitarajia mwenyekiti atasema neno…

 Niwaambie ukweli baada ya uchunguzi wangu niligundua jambo, huenda halijagundulikana hilo, huenda limeshagundulikana lakini nia na amdhumuni kwa sasa ni kuwajibishana, lakini kuna mambo ambayo hamjayaweka kwenye mtizamo wa kihekima…samaahni kwa kusema hivyo.

Hamjui kuwa, malengo na mbinu za hili, kwanza ilikuwa ni kuondoa nguvu za ulinzi, akili na mawazo ya kikazo yaondolewe kisaikolojia, kuharibu ulinzi na usalama wa familia, hilo hakuna aliyelifahamu, sijui naeleweka hapa, na…na  pili kuondoa, mshikamano…familia iyumbe, ikose udhibiti, ni nani kiongozi na ni nani wa kutiiwa, hilo lina umuhimu wake.

Lakini la tatu ambalo ndilo huja kuharibu kabisa, ni kujenga chuki…ukiliangalia hili utaona mfano wake, ni nini kilifanyika kwenye familia iliyolengwa,…na je hili halikufanikiwa, chuki ziliandaliwa kitalamu, kukajengwa matabaka mawili ya mume upande wake na mke upande wake..je hili halikufanyika…?’ akawa kama anauliza

Ilihakikishwa kwua hilo lawezekana, chuki ikasambazwa, kwa marafiki, makundi, ..kundi mume n akundi mke, ushabiki ukajengwa, watu hawalioni hili ubaya, wake, ushabiki wenye mlengo wa chuki ni mbaya sana,…haujengi, familia ikawa sasa kila mtu na lake,…sijui naongea na watu wanaolewa, au ndio bado makundi hayo yapo hapa.

Mzee mimi nayaongea haya kwa nia njema, sina nia ya kuwagawa hawa watu sina nia ya kuingilia hii familia na sina nia mbaya ya kuchukua chochote kwenye hii familia, mimi ni mtu wa kuja tu, wenye familia wapo, wenye mali wapo, kwanini mimi nije kujiingiza humo,…sina fani yangu, na sio lengo langu, lengo langu ni kujitegemea, kufanya kazi yangu kwa malengo mema.

Tuyaache hayo, nahisi mtaniona najitetea kwa vile nimeharibu, ni kweli najuta sana kwa hiki lichotokea imeniuma sana,…lakini yameshatokea nitafanya nini…’akaweka mikono kama anamuomba mungu wake.

‘Namuomba mungu sana anisaidie kwa hili….’akatulia kwa muda

‘Ndugu mwenyekiti, …haya yalipangwa kitaalamu sana, na kila tukio lilikuja kutokea baadae lilichukuliwa kwa uzito wake, maana kashfa inaweza kuwa ni ndogo tu, lakini jinsi itakavyokuzwa na vyombo vya habari, midomo ya watu, inaweza ikawa kubwa kuliko kashfa yenyewe, ni kweli si kweli..hili lilipangwa na maadui wa mzee, na kinara wa kulifanikisha hilo mnafahamu wenyewe…’akageuka kushoto na kulia.

Sasa oneni hili,  siku nilipofika uwanja wa ndege kulitokea nini..na onenani ujanja wa mwenzetu, ulivyo, yupo mbali kabisa na hili, na huwezi kabisa kumdhania, yeye anachofanya ni kutia mafuta kwenye ule moto ulioanza kuwaka..kidogo kidogo…

Nasimulia hili nitajitahidi kutokuingilia kazi ya polisi…

*******a

 Nilielezea  kidogo yaliyotokea awali kwa ufupi, lakini sivyo ilivyokuwa kwa undani wake, mimi nilitekwa nyara mapema tu, na nilikuwa ndani ya mikono ya hao watu kwa siku mbili, hakuna anayelifahamu hilo…’akatulia

Nilipotoka uwanja wa ndege kaam nilivyosema awali mtoto wangu nilimkabidhi mtu, nikijua huku huenda kukawa na jambo, na sikutaka kabisa mtoto wangu aguswe, nilikuwa tayari kupigana hadi kufa, kama mtu atamgusa mtoto wangu.

Nilijiamini kuwa mtoto wangu atakwua salama, nikatangulia kutoka, na mtu niliyemuachia mtoto wangu alibakia nyuma, japokuwa hata nilipotoka macho yangu kwa siri yalikuwa yakihakikisha kuwa mtoto wangu kaondoka uwanjani pale salama, nikabakia mim, na yaliyonikuta

Baada ya ukaguzi wa mizigo yangu, sikuwa na mizigo mkubwa, ni kiasi cha nguo za mtoto na zawadi kidogo,  sasa wakati natoka, nje, ..uon ilivypopangwa kumbe …hahaha maana huyu mtu aliyekuwa nyuma yangu sikuwa na ..yaani hapo ndio nasema hawa watu sio wa kawaida, huyu mtu sikuwahi kumuona kwenye ndege,..

Ukitoka pale uwanja wa ndege,unatembea kutoka, huku wapo watu wanasubiria jamaa zao, wamejipanga, mstari, nyie mnapita ile sehemu ya kutembea, huyu mtu alitokea wapi hadi kuwa nyuma yangu na mimi kwenye ndege sikuweza kuiona sura hiyo.

 Sasa namaliza ile sehemu ya kutembea nataka kufika ile sehemu ya watu walijipanga mtu nyuma yangu ndio akanigusa na kitu kikali, ina maana huyu mtu alikwua nyuma yangu wakati wote, haiwezekani akatokea miongoni mwa watu na kuja kuniwahi kwa nyuma ..hapana…sijui naeleweka hapa…’akasema

Ilikuwa ni kisu kikali maana nilihis maumivi yake, sauti ikasema;

‘Fuata tutakavyokuelekeza, kuna taksi ile pale mbele yako, mlango wake upo wazi, ingia, na mizigo yako tutakuchukulia, hatutaki kukuumiza...’akaniambia, na baadaye akanipa bahasha, akaniambia

‘Fungua hiyo bahasha...’kwa mikono ya kutetemeka, nikaifungua,..nilitetemesha ile mikono kwa makusudi, kumteka huyo mtu akili , ili ahisi kuwa mimi nimeogopa, ni ujanja mdogo tu…nikafungua ile bahasha, na kwa mbali nikaona yule mtu aliyekuwa an mtoto wangu akitoka, akawa anaendea gari, sikuona dalili ya watu kuwa nyuma yake

Na kuwa muda huo ndio nimefungua ile bahasha na kuona zile picha  mbaya, le nilizozoea kutumiwa, na huyo mtu  akaniambia

‘Siku hizi hapa bongo kuna magazeti mengi yanazitafuta picha kama hizo, hatutaki kukuharibia jina lako, na kukuharibia maisha yako ya baadaye, na kumpoteza mtoto wako, yote hayo yanawezekana, au sio…ila sisi tunataka kulijenga jina lako uwe karibu na wenye pesa, wewe unafaa kuwa kiongozi mwema, tunataka kulifanikisha hilo…tunaweza…’nikaambiwa

‘Sasa ili uwe salama, ili mtoto wako awe salama, timiza masharti yetu madogo tu, tutakuwa sambamba na wewe...’wakasema na mimi sikutaka kubishana nao, nikaingia kwenye gari, na gari likaondoka, sasa linatoka, na wakati huo niliona gari lililombeba yule mtu na mtoto wangu wakiondoka..

Kwa pale sikuona dalili kuwa na wao wametekwa, na hata wakati tunatoka, wao walielekea njia ya kawaida ambayo nafahamu wanapokwenda, ila sisi tukageuka upande wa kuelekea Pugu…unaona, na gari halikutembea mwendo mrafu tukawa tumeshafika ahpo walipotaka kunipeleka mimi.

‘Tumefika mpendwa, tunachokuomba ni wewe kuwa mstaarabu, hatutaki wewe uonane na mtu mwingine yoyote bila idhini yetu, kwahiyo tutakupeleka mahali maalumu utakaa hapo, hadi lengo letu likamilike, mambo mengine utakuja kuendelea nayo baadae..’wakasema

‘Ama hilo tataizo la kibali chako cha kwenda kusoma, usiwe na wasiwasi nalo, limeshashughulikiwa, utapata muda mdogo tu wa kuweka sahihi yako pamoja na mambo mengine,…utuelewe, sisi hatuna nia mbaya na wewe, ...’akasema huyo mzungumzaji

Mimi sikuongea kitu adi hapo, sikutaka kwanza kuongea chochote,…na wakati huo tulikuwa tunaingia kwenye jengo moja, ni jengo kwa nje linaonekana kama halijakamilika , lakini kwa ndani limeshakamlika, sijui kwanini walifanya hivyo.

Tuliingia ndani kama watu wa kawaida, na jamaa yule akaenda kuongea na mlinzi, na mlinzi akatuelekeza wapi pa kwenda, kumbe pale kuna njia mbili ya kwenda juu na nyingine ya kwenda chini…kuna jengo la chini ya ardhi, humo humo lakini huwezi kuligudnua hilo .

 Unajua mimi kule ilipangwa niondoke baada ya siku mbili hivi, lakini kwa haraka nikaamua kuondoka mapema, hawa watu walifahamu vipi, na mawazo hayo yalinijia usiku na usiku huo nikawasiliana na watu w ndege, na kukubaliwa kuwa nafasi ipo naweza kubadili tarehe,..yawezekana ndio, kama wana watu wao, lakini sio kwa haraka kihivyo.

 Kwahiyo hapa Dar nilifika siku mbili kabla ya ile tarehe iliyojulikana kuwa nitafika, ila hadi leo watu wanafahamu nimefika siku ile ile ya tarehe iliyokuwa imepangwa, hadi leo hakuna anayelifahamu hilo…’akasema

 Tuliteremka ngazi chache hadi chini..na kufika kwenye ghorofa ya chini ya ardhi,…tukatembea na kuingie kwenye chumba chenye kila kitu, ...ni chumba cha kifahari, nikaambiwa hapo nitakaa mimi hadi nitakapopewa maagizo mengine...’msemaji akasema na kuondoka zake.

Kitu cha kwanza nilitaka kujua ni nani yupo nyuma ya haya yote, sikujua ni nani kwa muda ule,.japokuwa kwa mtizamo wa haraka, toka awali, nilijua kuwa anayefanya haya yote huenda akawa ni Makabrasha, kutokana na maaelezo ya watendaji wangu.

Nilipoingizwa mle na kuona hicho chumba nikawa na mashaka, huenda sio makabrasha au kama ni yeye, basi kuna mtu anamtumiwa huyo Makabrasha, …maana hicho chumba ni cha kifahari, kuna gharama kubwa imetumika kukiweka vile.

 Kwanza ikabidi nijimwagie maji kidogo, na kutuliza akili, ...nikatulia na ukumbuke mtoto wangu alikuwa mikononi mwa mtu niliyemuamini, na huyo mtu alinihakikishia kuwa atamfikisha mtoto wangu kwa jamaa yangu mmoja, lakin je alimfikisha, ndio nilikuwa nawaza jinsi gani nitawasiliana naye kulihakiki hilo..

Simu yangu hawakuichukua, nikasema basi ngoja nipige simu kwa mtu mwingine yoyote kwanza nione kitakachotokea, kiukweli hakukuwa na mawasiliano ya simu, mawasiliano ukiwa humo ndani hayafanyi kazi, wamezuia namna yoyote ya kuwasiliana, kuna simu ya mezani…nikaiendea na nilipoinua tu, ujumbe ukasema

‘Kuna tatizo tunaweza kukusaidia…/’ nikaulizwa

‘Nataka kupiga simu nje…’nikasema

‘Unaweza kunitajia namba ya mtu unayempigia nikusaidia tafadhali..?’ nikaulizwa na mimi nikakata simu.

Wasiwasi wangu kwa mtoto ukawa sasa umethilika, je ni kweli kafikishwa hiyo sehemu salama, nikawa sina amani…nikaona ni lazima nifanye jambo, ni lazima niweze kujua kama mtoto wangu yupo salama au la…

Ilipofika muda fulani, nikasikia mlango ukifunguliwa, na akaingia dada mmoja akiwa kabeba vifaa ni vyakula na vifaa vingine vya kuongeza kwenye jokofu.., alikuwa kafunga uso wote, haonekani sura, kaacha  sehemu ya macho tu, inaonekana ni muhudumu, aliwekea vyakula,  hakuniangalia, alifanya hiyo kazi, na alipomaliza, akanijia, na kuniuliza

‘Una shida yoyote?’ akaniuliza

‘Ndio , nataka kutoka nje...’nikasema

‘Mhh, fuata maagizo , kama ulivyoambiwa, ..’akasema na kuondoa vyombo, akaacha kijiko, lakini ni kijiko cha plastiki, ni kama kakisahau,…mimi sikuwa na mawazo yoyote nacho, akatembea hadi mlangoni , na kabla hajafungua mlango akasema;

‘Ukweli wewe unaoufahamu,  nakushauri ufanye kama wao walivyotaka, na watakavyotaka…’akasema na kuondoka. Kwa mpelelezi ujumbe huo ulinitosha kujua ni nini kinachoendelea humo, lakini kwa muda huo, akili yangu haikuwepo, akili yangu ilikuwa kwa mtoto wangu,..mama na mtoto wake sio kitu cha kubahatisha.

Nikawa nimetulia, kwanza niliangalia zile kamera juu, nikawa nawaza jinsi gani ya kuharibu mawasiliano yao, ili wasijua kinachoendelea humo ndani, …na mara macho yangu yakigundua kitu kwenye kile kijiko cha plastiki, sikukichukua kwa haraka maana yoyote anayenichunguza juu, ataligundua hilo, nikavua koto langu na kulirusha mezani kama najisikia joto, nikajinyosha, nikatembea hatu kadhaa za mtu anayawaza.

Nikajivunga vunga na kujinyosha, halafu nikaliendea lile koti, kwa haraka nikalizoa, na kuhakikisha kuwa kile kijiko kipo mikononi mwangu

Nilienda chooni, na baada ya kuhakikisha kuwa hakuna kamera, nikachukua kile kijiko, kama nilivyohisi ilikuwa sio kijiko tu, bali kulikuwa na zaidi ay hicho kijiko…

Kulikuwa na karatasi nyepesi imekunywa vyema na kunatishwa kwenye kile kijiko, na nilipokitoa kile kikaratasi nikaona maandishi;

‘Tupo pamoja..’ nikakigeuza nyumba nikaona namba ya simu, nikaikariri halafu nikakitafuna kile kikaratasi.

Nikarudi kule ndani, …kuna hali isiyo ya kawaida nilihis hali ya hewa ni nzito, mwili ukanisihia nguvu, na kabla sijadondoka nikajirushia kitandani, ..na hapo hapo nikazama kwenye usingizi mnzito

Nilianza kuhisi hali ..nahisi nililala sana, lakini hadi hapo sikuweza hata kujiunua,ila nilihisi sipo peke yangu. Nikajipa moyo, kuwa nipo salama, ni baada ya akili kutulia.

Nililala kwa muda wa nusu saa hivi,  baadae sasa hali ikajidhihirisha kuwa kweli kuna mtu mwingine humo ndani, hapo kitandani, lakini hadi hapo, mwili wangu ulikuwa hauna nguvu hata kuinua mkono siwezi,…oh, wamenifanyia nini hawa watu

Hali hiyo ikanikumbusha siku ile nilipobakwa na ..na..mume wa familia…’akatulia kuongea na kumuangalia mume wa familia.

‘Lakini hii ilikuwa zaidi, maana hata kuwaza kitu, inakuwa vigumu, akili ni kama imefungwa hivi…’akaendelea kusimulia.

Kwa muda huo cumba kilikwua ni giza, na ni giza nene, …sijui taa ilizimwa saa ngapi,.nio nikaanza kukumbuka, nikakumbuka wakati nataka kujipumzisha chumba kilikuwa na mwanga, nikajisikia hewa ni nzito, ..na nikajirusha kitandani, nikazama kwenye usingizi mnene, nikakumbuka yoet hayo

Kwa vile mwili ulikuwa bado hauna nguvu, sikuweza kuinuka, nikawa nasubiria litakalokuja kutokea, nikasubiri, mara nikahisi kitanda kikitikisika, kuwa huyo aliyekuwa karibu yangu, akajiandaa kufanya jambo, au kama alifanya jambo anataka kuondoka,

Hapo nikawa najaribu kuvuta hisia za nguvu, nguvu ziweze kunirejea, japokuwa siwezi kuinua hata mkono, au kukunja kidole, mwili umelegea, nikahisi mkono ukinipapasa sehemu ya tumboni, nikatulia nione lengo la huyo mtu,..

Aliposogeza mkono chini zaidi, ule mkono ukasita, na mara nikaona kitu kikiletwa mdomoni, ni kijiko, kina kitu kama dawa au maji, yakawekwa mdomoni mwangu yakapenya, nikameza..nilihis mwili saa ukisimuka,. Na mara ule mkono ukawa unashika tena tumbo langu, ukielekea chini zaidi.

Nilihisi sasa nguvu zimenirejea, hasira, zikanipanda, nilisubiri, kabla mkono haujaenda mbali zaidi kwa haraka nikashusha mkono wangu ukaudaka mkono huo ulioshiaka tumbo langu, nikajirusha,..ni mbinu zetu za mapigano, nilichoskia baadae ni kilio cha maumivu, na jamaa alikuwa sakafuni akilalamika maumivu.

‘Aaah, umeniumiza mkono, ooh,, ...nini unafanya wewe, sikuwa na nia mbaya, nilikuwa nakusisimua ili damu ifanye kazi, aaah, watu wengine bwana...’sauti ikaniuliza,. Ujue humo ndani kukizimwa taa ni giza kweli,

‘Kwani wewe nani na lengo lako ni nini?’ nikamuuliza

‘Usijali sikuja hapa kwa nia mbaya, kwanza sina muda wa kufanya lolote na wewe, nimeshachoka, nilikuja kukusalimia tu, nikawa napendezewa kushika mwili wako uliojengeka kimazoezi, una mwili mzuri sana, na nilitaka kukusisimua, ili uondake na hiyo hali...’akasema

‘Wewe ni nani,…nijibu kwanza?’ nikamuuliza

‘Wala usijisumbue kutaka kufahamu mimi ni nani mimi ninachokuomba ni wewe upumzike tu, usiwe na wasiwasi upo salama...’akasema.

‘Nipo salama, wakati mumeniteka nyara, na kupulizia madawa ya kupoteza fahamu…’nikasema na kwa haraka nikawa naelekea sehemu ya kuwasha taa.

‘Wala usisumbuke kuwasha, nimekuja kukusalimia, tu, kesho asubuhi nina kikao na wewe, ajenda ni moja, kukubaliana na hayo tuliyoyapanga, wewe utatusaidia kutupa taarifa chache, na huenda tukakutuma mahali, ukimaliza kazi yetu, utaenda kuendelea na madhumuni ya kuja huku kwa dharura, unasikia sasa hii ni amri, vinginevyo....’akasema.

‘Hujanijibu swali langu, wewe ni nani…?’ nikamuuliza

‘Utanifahamu labda hiyo kesho, samahani kwa usumbufu, nashukuru kwa kuwa mvumilivu, ukifanya hivyo, na kufuata masharti yetu, ukatii yote tunayohitajia, hutapata taabu, na haya tunayafanya kwa ajili yako, na familia yako,...mwenyewe utaona, kwa hivi sasa lala,..usijali..’akasema na kuondoka, sikutaka kujishughulisha zaidi, nikarudi, na kulala huku bado nikimuwazia mtoto wangu.

‘Mtoto wangu yupo wapi…’nikawa naweweseka, maana nilihis kuzama tena kwenye usingizi mnzito

Nakatiza kidogo, tutaendelea na sehemu hii, muhimu ambayo inatupeleka kwenye mshukiwa wa mauaji

WAZO LA LEO: Maisha ya mtu yana thamani kubwa sana, na ni lazima kila mtu atafikia umauti, lakini tujitahidi sana tusiwe sisi ni sababu ya uamauti wa mwingine , dhambi yake ni kubwa sana, ni kama umeua dunia nzima…je ni nani anaweza kubeba dhambi za dunia nzima…Tuwape pole wale wote waliofikiwa na misiba, maana msiba uusikie tu kwa wengine, msiba unauma, hasa akiwa ni ndugu yako wa karibu. Ila mwisho wa yote tusema tu, yote ni mapenzi ya mungu, na mwenyezimungu anajua vipi atalilipizia hilo.


Ni mimi: emu-three

No comments :