Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, February 16, 2018

MKUKI KWA NGURUWE-82


‘Sasa mimi na huyo mnayemuita mume wa familia ni nani Malaya, niambieni ukweli wenu bila kuficha, maana katuita sisi Malaya, je mimi nikimuita yeye Malaya nina makosa, au lugha hiyo ni kwa wanawake tu…?’ aliuliza mdada

‘Je mimi na yeye ni nani anayestahiki kuitwa msaliiti, tatu mimi na yeye ni nani mbakaji, mwizi, mdanganyifu,…’

‘Je sasa mwenyekiti waniruhusu niendelee sehemu ya pili, sehemu hii ina sehemu mbili ya kwanza hitimisho ya kuzaliwa kwa mtoto, na sehemu ya pili yake ambayo ni tete kidogo, ni kuhusu yaliyotokea baadae ambayo yatabainisha, ukweli wa kifo cha Makabrasha…’akasema

‘Ina maana una jua jinsi Makabrasha alivyouwawa, lakini hilo sio swala la kifamilia, ni swala la kipolisi, au sio muheshimiwa mwenyekiti…’aliyeongea alikuwa ni wakili wa mume.

 Na wakati wakili huyo akiongea mwenyekiti alikuwa akitaka kupiga simu,...

‘Unataka kumpigia nani mume wangu…’akauliza mama, akimuangalia baba kwa mashaka

Mwenyekiti akasimama na kusema,

‘Nipeni dakika kadhaa, kuna mambo nayaweka sawa, nitarudi,…’mwenyekiti akasema na kutoka nje kidogo, na sisi tulipobakia wenyewe bila mwenyekiti,  tukawa tunaangaliana, kila mtu akiongea na yule aliyekuwa karibu naye, na kwa vile mume wangu alikuwa karibu yangu akasema;

‘Mke wangu uwe makini sana na haya mambo, haya yamepangwa ili kuivuruga ndia yetu, ninafahamu nimekosa, ..lakini ilikuwa ni bahati mbaya, na… mimi ni mume wako, na hakuna mtu atakayeweza kututengenisha, usimsikilize huyo mshenzi, huyo ni ndumilakuwili, ati anajiita rafiki yako, huyo mtu anatumiwa na watu, hata wakili wangu anamfahamu sana huyo rafiki yako, najua kabisa kakosa kote sasa hivi anataka kuharibu kabisa…’akasema na kugeuka kumuangalia wakili wake, na wakili wake akatikisa kichwa kukubaliana na yeye.

Nilimtupia macho mdada, ambaye alikuwa akihangaika na mtoto wake, alikuwa akimbadilisha nguo za ndani, na alipomaliza, akasimama na kwenda pale alipokaa mama, akawa anataka kumpa mama mtoto, na mama alikuwa kama kasinzia, akashangaa mtu kasimama mbele yake.

‘Mjukuu wako huyu…’akasema

Mama akamuangalia kwa macho ya kushangaa, hakusema neno, akawa anamuangalia yule mtoto kwa uso wa huruma, halafu akanyosha mkono kumpokea yule mtoto, akawa anamuangalia kwa makini kweli.., baadae akageuka kumuangalia mtoto yule wa bint yake wa kufikia, akatikisa kichwa na kusema;

‘Kwa haya matendo yenu mna dhima kubwa mbele ya mola, lakini hawa viumbe hawana makosa, ndio maana sitaki kusema lolote baya kuwahusu wao, vinginevyo, mimi nisingelikubali hata kumpokea huyu mtoto, yaani wanafanana kweli…’akasema

‘Ni kweli mama, lakini hayo niliyoyasema mimi ni kweli, najua mtasema, kwanini nili…kaa kimia, au kwanini ikatokea mara ya pili, na…na.. bado nikakaa kimia,..na kwanini sikuweza kuusema ukweli wote baadae, ..ni lawama kwangu kwa kweli, lakini hamjui ilivyokuwa, kiukweli baada ya hilo, nilipitia majaribu mengi sana,.. nitakuja kuyaongea hayo, yaliyotokea baadae ambayo, huenda yakasaidia kuyajibu maswali hayo…’akasema

‘Vyovyote iwavyo, huwezi kukwepa lawama kuwa na wewe ulikosea, na ulimkosea sana rafiki yako, nashangaa ukimtupia lawama kuhusu kukushauri, je ni mangapi mema alikushauri, je ni mangapi yenye kasoro alikushauri na wewe hukuyafanya, kwanini hili ukalifanya, ni kwa vile ulifahamu kuwa kuna masilahi mbele yako, huo ndio ukweli…’akasema mama

‘Mama hata sijui nisemeje…ni kweli akiri kosa, nakubali sana hilo, kuwa nimemkosea sana rafiki yangu, na sizani kama nitaweza kulilipa hilo deni.., ni yeye tu, nasubiria adhabu yake, lakini sio hiyo ya kunikamatisha watoto wa kihuni, hapana mama, huo utakuwa ni kunitaka nijiue, kaam adhabu mimi nijiue, basi iwe hivyo, sio kwa njia hiyo, …’akasema

‘Unataka adhabu gani sasa, maana sasa wewe mkosaji ndiye unayepanga adhabu gani upewe, hutaki adhabu za mkosewa, mimi nionavyo, ni kumuachia mkosewa aamua mwenyewe adhabu gani ya kukupatia, kwani hata akupe adhabu gani, sizani kama itapunguzu machungu yake moyoni, niambie kama ingelikuwa wewe ungelifanya nini…?’ akauliza mama.

‘Mama hebu fikiri, hiyo ni adhabu kweli ya kumpa mtu, tujiulize wenyewe hivi kweli hatujawahi kumkosea mtu, …ni sawa kama na wewe mzazi utaona hiyo adhabu ni sahihi…nita..oh, mama, usiombe kufanyiwa uchafu huo…’akasema

‘Nikulize umewahi kukaa ukaliwazia hilo, ni maumivu gani mwenzako kayapitia, ukizingatia kuwa wewe ni rafiki yake, ndugu wa karibu, aliyekuamini kupitiliza mpaka sisi wazazi wake akawa hatusikilizi zaidi yako, hasikii lolote kukuhusu wewe, maana sisi tulishaziona nyendo zenu wewe na mume wake, tukaambizana, je hii ni sahihi, ni kwanini binti yetu anayaruhusu haya,…yeye tulipomuuliza hilo, alisema anakuamini, wewe huwezi kumsaliti..’akasema mama.

‘Na hivyo hivyo, akamtetea mume wake kua mume wake hawezi kumsaliti kwasababu ana mkataba amabo hawezi kuuvunja, na sisi hatukuwa na ufahamu sana kuhususiana na huo mkataba, tukamuwambia, mkataba utavunjwa, na wewe utakuja kutumbia, si ndio haya yametokea…’akasema mama

‘Na tulimuambia hao hao unaowaona ni marafiki zako, ndio hao hao watakuja kukuliza, je hayajatokea…asiyesikia la mkuu, …’akasema mama.

Rafiki yangu pale akawa kainamisha kichwa chini tu, nahisi alikuwa akipambana na huo ukweli, na alipoinua kichwa, nikaona machozi machoni mwake, ..akageuka kuniangalia, na mimi nikawa nimekwepesha macho yangu tusiangaliane,..na alipoona hivyo, akawa anatembea kuja kwangu, na aliponikaribia, akataka kupiga magoti, na mwenyekiti akaingia…

‘Haya jamani tuendelee, tusiharibu utaratibu, mzungumzaji nenda kwenye sehemu yako, mchukue mtoto wako, tunataka kuendelea…’akasema mwenyekiti na huyu mdada, akaacha kitendo alichokuwa anataka kukifanya, na kwenda pale kwa mama, akamchukua mtoto wake, na kurudi sehemu yake…

Tuendelee na kisa chetu

******************
Mwenyekiti aliangalia saa, akaangalia zile ajenda mezani kwake, halafu aakgeuka kuniangalia mimi, akasema

‘Sizani kama kikao hiki kitayamaliza haya kwa leo, kuna watu wana shughuli zao, tumewasimamisha leo, kuna watu wanatakiwa kesho kusafiri, kuna mambo yangu ya kikazi, na .…’akasema

 ‘Mwenyekiti mimi naona tuendelee na kikao kwa vile tumeamua kulifanya hili jambo, basi ni vyema tukalimaliza kabisa, mimi hapa nilipo sizani kama nitaweza kuendelea kuliweka hili jambo moyoni tena, nimevuta subira kiasi cha kutosha, naona leo liwe ni hitimisho, ili maisha yaendelee…’nikasema

‘Hapo unajiangalia wewe mwenyewe, je umewauliza wajumbe kuhusu nafasi zao, je hawatathirika na hili, …’akasema mwenyekiti 

 ‘Kesho ni siku ya mapumziko ya juma,..niliwauliza wenzangu mmoja mmoja kwa nafasi yake kama leo wanaweza kuitumia nafasi hii kwa siku nzima, wengi walikubaliana na hilo, ikizingatiwa kuwa tatizo hili limewagusa kila mmoja wetu hapa,na kila mmoja anataka liishe, ..’nikasema.

‘Ndugu zanguni, ..ingelikuwa  ni vyema, tukafahamu , huenda  kuna mtu mwenye dharura, kama kuna mtu ambaye anaona tuahirishe hiki kikao aseme, ili tuone tutafanya nini, tunaweza kuahirisha hadi kesho, kama ikibidi,..’akasema mwenyekiti.

‘Kiukweli binti wangu wa kufikia, aliniambia yeye kesho ni lazima aondoke kutokana na shughuli zake huko kijijini, sasa hiki kikao ni muhimu sana kwake, ili kufahamu hatima yake…kamuacha mama yake anaumwa,…’akasema

‘Mimi naona tuendelee tu na kikao, tuyamalize, haya, ama kwa huyo binti, mimi sioni kwamba kuna jambo ambalo halijakubaliwa juu yake, kwani mtoto keshajulikana ni nani baba yake, na baba yake ni lazima awajibike juu yake, hilo halina mjadala , mengina atakuja kuambiwa tu…’akasema docta.

‘Wewe umesema hivyo, lakini ulisikia kauli ya rafiki yako, kuwa hao watu ni watu gani,…na wamefanya hivyo kwa madhumuni gani,…sitaki kumalizia kauli yake maana kwangu inanipa mashaka..’akasema mwenyekiti.

‘Hapana, hayo aliyaongea kwa hasira tu, ukweli upo wazi, hata kama dhana yake ina mantiki kwake, mimi nafikiri rafiki yangu hawezi kukwepa hilo jukumu, huyo ni mtoto wake, haijalishi walimpata kwa njia ipi, anawajibika kwa hilo,...’akasema rafiki wa mume wangu, huku akimwangalia rafiki yake

Mume wangu alikuwa kainamisha kichwa chini, hakusema neno, na wakili wake alikuwa akipitia makabrasha yake ni kama vile hawakuwepo, na kitendo hicho kikamfanya mwenyekiti kusema;

‘Hivi nyie watu wawili tupo pamoja kweli, hamuoni kuwa kikao kinaendelea au mnataka tuwaleweje, hili ni kwa manufaa yenu, je tukitoa uamuzi mtasemaje…?’ akasema mwenyekiti.

‘Samahani sana muheshimiwa mwenyekiti, kuna mambo tulikuwa tunayapitia, ili tuje kuyaweka wazi kwenye kikao, imebidi tuongee na kuona jinsi gani tutakubaliana na hilo la mtoto…sio kwamba tumekizarau kikao…’akasema wakili

‘Kwahiyo mnasemaje..tuambieni mlichokubaliana, ili ikiwezekana tumruhusu huyu binti aondoke, tatizo pia hawezi kuondoka bila kuongozana na mke wangu kuna mambo yao wanataka kuyaweka sawa, huyu tulishamchukua kama binti yetu..’akasema mwenyekiti.

‘Tumekubaliana tuendelee na kikao, ni sio lazima kiishe leo, tunaweza kuendelea na sehemu itakayobakia tupande siku ya kuiendelea nayo, isiwe nitatizo kubwa, maana hapa ni seehmu ya kuwekana sawa kama wanafamilia…’akasema wakili

‘Sawa, sizani kama tuna muda wa kuliendeleza hili tena na tena,  ni muhimu tumalizane na hili jambo ili maisha yaendelee kama kawaida, na kama kuna mengine yakufuatilia, yafautiliwe, na kama kuna kuwajibika, watu wajue ni nini wanahitajika kuwajibika nacho, naona tulimalize hili ikiwezekana leo, au mnasemaje wajumbe...’akasema mwenyekiti huku akifungua makabrasha yake.

********

‘Kwahiyo kwa sasa muongeaji wetu anaweza kuendelea na sehemu yake ya pili, kama alivyoiita yeye  mwenyemwe, ila hapo nina angalizo kidogo, kwenye utangulizi wake, kasema sehemu hiyo ya pili, pia itamgusa marehemu, hapo mimi nachelea kidogo, je wanasheria wetu mnasemaje kwa hilo,...?’akauliza mwenyekiti, akiwaangalia mawakili wetu.

‘Kwasababu ni maongezi tu, hakuna jambo linaloweza kuharibu mambo ya kisheria, sizani kama hayo atakayoongelea yataharibu mambo ya polisi na upelelezi wao, naona yeye aongee tu , akizingatia hayo ya kipolisi.., kuwa hilo swala lipo kwenye mikono ya polisi, mimi namfahamu muongeaji, yeye anafahamu wajibu wake, anafahamu mipaka ya jambo kama hilo...’akasema mwanasheria wa familia yangu, na mwenzake akakubaliana naye.

‘Sawa …’akasema wakili wa mume, akimuangalia mteja wake, mume wangu alionekana kama yupo mbali kabisa.

Mara akasimama,mke wa docta, ni kama vile alikuwa mbali, na sasa kakurupuka kutoka huko alipokuwa akasema

‘Ndugu Mwenyekiti, samahani kidogo, mimi nilikuwa na ombi, nilitaka mimi nipate nafsi hiyo kwanza, kwani nilikuwa nataka kuongea jambo moja muhimu sana,…naombe mimi  niongee mimi kwanza, kwani hata mimi kesho natakiwa kuondoka, kurudi kijijini, nataka nikajiandae,...’akasema mke wa rafiki wa mume wangu, na mume wake, akawa kama anamzuia, na wakawa wanateta na mume wake, lakini ilikuwa kama hali ya kusutana hivi, hakuna aliyesikia walikuwa wakiongea nini, na baadaye mdada yule, yaani mke wa docta akasema;

‘Basi aendelee tu,...’akasema

Mwenyekiti akawaangalia kwanza kwa uso wa shauku , lakini baadae akasema;

‘Tunashukuru sana kwa kutuelewa, kwasababu mwenzako alishaanza, itakuwa sio vizuri,tukiwa tunakatisha katisha haya mambo, mpangilio wa ajenda ni mnzuri, tu..itafikia muda wako, utaongea, au sio…? ‘akasema na kuuliza.

‘Sasa..unajua niwambie kitu, ni nini dhumuni la kuwaleta hawa mawakili wetu wawili, ilikuwa wao watusaidie kila tunachoongea hapa kiwekwe kisheria zaidi..tukianghalia mbele,…muhimu ni ili  tuwe na kumbukumbu zenye mshiko, …na hatua zikianza kuchukuliwa tuwe na ushahidi ulio kamilika,…, ..’akasema mwenyekiti.

Yule mke wa docta akasema;

‘Sawa mwenyekiti, nimekubali kusubiria, lakini akimaliza yeye, naomba mimi ndio nipewe kipaumbele,  ni muhimu sana kwakweli, sitaweza kuvumilia zaidi ...’akasema huku akigeuka kumuangalia mume wake, ambaye alikuwa akimwangalia kwa macho ya kumshangaa.

Mimi nilimwangalia huyo mdada nikahisi kweli ana jambo kubwa sana la kuongea, na kama alivyoonekana toka awali, alikuwa kama hayupo nasi kwenye kikao, na hicho alichotaka kukiongea inaonekana kakifikiria sana,..

Nikawa na mtizama kwa makini,  nikakumbuka jinsi mume wake alivyosema kuwa mke wake mara nyingi ameonekana akiwa na mawazo mengi, kitu ambacho hakuwa nacho kabla, anahisi mke wake ana tatizo kubwa, ila hataki kusema ni nini kinachomsumbua. 

Nilitamani mwenyekiti amruhusu tu huyo mdada aongee kwanza, kwani huenda inaweza ikafikia mahali, huyu mzungumzaji wa sasa akaongea mambo yakamfanya huyu mdada akaghairi hayo aliyoyataka kuyaongea na niliona kama mume wake hataki aongee jambo…huenda wamekwisha kuyaongea, na je hayo aliyo nayo yaanhusiana vipi na familia yangu

Nilipowaza hivyo, nikanyosha mkono..na mwenyekiti akaniangalia , na kusema

‘Vipi tena…’

‘Samahani mwenyekiti, huenda mwenzetu huyu ana jambo muhimu sana,kwanini tusimuachie akaongea kwanza…huenda hilo jambo halitaki kusubiriwa, au baadae akaja kughairi,...’nikasema

‘Hapana, mimi naona, tuendelee tu  kwa mpangilio wetu, kama alivyosema mwenyekiti, twende kama ajenda zinavyosema, ili tusichanganye mambo…au sio mke wangu...’akasema docta akimuangali mke wake, na mke wake hakumjibu kitu.

Mke wa docta,  akawa katulia, na alionekana kama kukerwa na maamuzi ya mume wake, akawa sasa katizama chini tu akiendelea na ile hali yake ya awali, kama hayupo vile. Na mwenye kiti akasema;

‘Basi mimi naona aliyekuwa akiongea aendelee, tusipoteze muda,… haya tuelezee sehemu yako ya pili, na sehemu hiyo kama ulivyokwisha kuonywa, isije ikagusa mambo ya kipolisi na uchunguzi wao, sisi tunahitajika kufuata sheria..’akasema

Mdada muongeaji akatikisa kichwa kukubaliana na maagizo ya mwenyekiti.

‘Ni muhimu sana , kwani hata kama hawapo hapa hao wenyewe.., lakini masikio yao ni mapana, huko walipo, wanafuatilia hiki kikao kwa ukaribu sana, wanajua humu kuna jambo ambalo linaweza kuwasaidia kwenye kesi yao, ndio maana hakuwataka kutuingilia, walitaka kuwachukua baadhi ya wajumbe, leo hii, mimi nimewatuliza kwanza….’akasema mwenyekiti

‘Mwenyekiti mbona unatutisha…’akasema docta

‘Sio kwamba nawatisha, nafahamu kilammoja  anajijua yeye mwenyewe, na hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, za mwizi niarubaini, na sisi kama wanafamilia, tutalindana pale inapobidi,lakini je kama watu wamefanyahayo nyuma ya mgongo wetu sisi tutafanyaje..’akasema mwenyekiti

Pale watu waliangaliana, kama kuhisiana, lakini hadi hapo hakuna alieymshuku mwingine..

‘Sasa jamani,  tuendelee,….ila narudia tena, muongeaji,  uwe makini na hilo, hatutaki kuja kuharibu sifa ya familia yetu, ongea yale yanayostahili kuongewa hapa...’akasema mwenyekiti.

Mdada akawa, anajikuna kuna kichwa kwanza kabla hajaanza kuongea, akawa anahangaika kidogo, na mwenyekiti akasema;

‘Sio lazima uongee ukiwa umesimama,…’akasema mwenyekiti.

‘Nashukuru sana, ndugu mwenyekiti, msiwe na wasiwasi na hilo, mimi nafahamu sana utaratibu huo, ninayotaka kuyaongea hapa ni mambo yanayoigusa familia yenu, ..oh, sijui nisema yetu,…kwa vile hata mimi nimekuwa ndani ya familia hii, na hata kutambuliakana kama mwanafamilia, nitajitahidi nisiharibu jina la familia yetu…’akasema na hapo akanitupia jicho la haraka.

‘Kwahiyo,…’akasema na kutoa karatasi fulani kwenye mkoba wake,..

‘Kuna mambo nitayaongea hapa...huenda mengi yamepotoshwa kwa masilahi fulani, lakini mimi kama mpelelezi, nimeshayafanyia kazi, na hivi ndivyo ilivyo, anayebisha, alete ushahidi wake...’akasema

‘Sehemu yangu hii ya pili, ambayo naona itakuwa hitimisho, la kila kitu kinachonihusu mimi, na walengwa, itaanzia nilipojifungua, maana hapo ndio nilianz kupata picha ya mambo ambayo nilikuwa siyajui,...’akasema na kuniangalia mimi kidogo, halafu akamwangalia mume wangu, na akatabasamu kidogo.

‘Mengi yalisemwa, hasa baada ya mimi kujifungua,  na wengi, walitaka kufahamu ni nani hasa baba wa huyu mtoto, kama nilivyosema awali, haya yaliyotokea hadi kupata mtoto, yana mlolongo wake, achilia mbali huo ushauri, kuna kuwekewa madawa ya kulevya, hayo madawa jamani ni hatari, sijui wenzangu hawa waliyapatia wapi, na kama ningeshitaki, ilikuwa ni kesi, sio mchezo....’ akasema.

‘Ningelipenda docta atuelezee kidogo kuhusu hayo madawa kabla sijaendelea..’akasema

‘Hebu tukumbushe kidogo , hayo madawa yanaitwaje… ?’ akauliza docta

‘Kifupi  chake ni PCP, na kitaalamu wamsema ni Phe, Phe-ncycline, kama nitakosea, docta unirekebishe..’akasema, na docta akasema

‘Upo sawa, ..Mhh, ni moja ya madawa yasiyorasimishwa, ni hatari sana, yanaweza yakawa ya unga unga, au vidonge, ..watumiajia wanaweza kuchanganya kwenye kinywaji, ..na yakishaingia mwilini inakuwa kama waathirika wa madawa ya kulevya, ila zaidi yake ni kuwa, mtu anaweza kufanya mambo ya ajabu, anaweza hata kuota kwa vitendo, anaweza kuona vitu ambavyo wewe huvioni, ana..jenga hisia za ajabu tu..’akasema docta

‘Mumesikia, sasa wahuni hawa waliniwekea mimi…ndio maana jamani nawaambia mimi sikuwa na dhamira hiyo, …yaliyotokea usiku ule ilikuwa nje ya uwezo wangu, najitetea tena kwa hilo,…’akasema

‘Sawa endelea, hatutaki kupoteza muda tena…’akasema mwenyekiti

‘Nafahamu kuwa rafiki yangu atanilaumu sana, na hapo alipo hataman hata kuniona, ni kweli, ilivyo, na inavyoonekana kwa sasa nimekuwa kama msaliti kwake, kwa vile niliyafanya hayo niliyoyafanya, kinyume na alivyotaka yeye ndio maana narudia seehmu hiyo…, na kiukweli nilipoongea na mama, kiukweli imenigusa sana..’akasema.

 ‘Haya tuendelee…’akasema mwenyewe hivyo.

‘Nilipojifungua, rafiki yangu alifika, na akagundua kuwa mtoto wangu anafanana sana na watoto wake, na kwa mtizamo wa haraka, kama angelikuwa hamuamini sana mume wake, angelijua moja kwa moja aliyefanya hayo ni mume wake, lakini akili yake ilifungwa kabisa, na hata alifikiria kuwa huenda ni mdogo wa mume wake, aliyefanya hivyo...’akasema na kuinama kama anasoma kitu kwenye karatasi , ilikuwa karatasi moja tu.

‘Kiukweli usiku ule uligubikwa na sintofahamu nyingi, naweza kukiri kuwa sikuwa na ufahamu zaidi ya kile nilichokiona baadae kuwa aliyenifanyia hivyo ni mume wa familia,..na kwa maelezo ya hizo dawa unaweza ukafanya kile ulichokuwa ukikiwaza, au ukamfikiria hata mfu kuwa upo naye, ni kama mashetani fulani…sasa hapo unaweza ukasema mengi … je ni kweli au si kweli, ushahidi ni huyu mtoto…’akasema

Mtoto huyu ni matokea ya yale waliyonifanyia usiku ule, sasa kama walitumwa au walidhamiria, mimi hapo sijapata ushahdi wa kulitosheleza hili, ila kama mume wa familia ana nia njema na hii familia anaweza kuliweka hili bayana, ili kuisaidia familia, na hapo itajulikana kuwa kweli yupo tayari, kujirudi..’akasema akimuangalia mume wangu.

Mume wangu alikuwa bado kainamisha kichwa , na wakili wake alitikisa kichwa kama kukubali,kwa niaba yake.

‘Baada ya kujifungua, mtu aliyekuwa karibu yangu, na kuniuliza mara kwa mara ni nani baba wa mtoto alikuwa rafiki yangu, bosi wangu, na ukumbuke yeye katika ushauri wake, alishanionya, kuwa ikitokea nikazaa na mume wa mtu basi hiyo iwe ni siri yangu…’akasema

‘Kwahiyo kumbe ni yeye alikushauri, uje uzae na mume wa mtu..?’ akauliza wakili wa mume wangu, na mwenyekiti akasema;

‘Sijaruhusu maswali…’akasema

‘Kiukweli sikuwa tayari kumwambia mtu ukweli, kwanza nilihitajia muda wa kulitafakari hilo, maana sasa nimepata ushahidi kuwa aliyefanya hivyo ni mume wa mtu,…ambaye ni shemeji yangu, ni aibu na sijui itakuwaje..’akasema

‘Rafiki yangu au bosi wangu ndiye aliyekuwa karibu sana na mimi, baada ya kujifungua, kiukweli nilitaka niwe peke yangu ikibidi, lakini kama walivyo marafiki, bosi hakutaka kulikwepa jukumu hilo,…ila sasa nafsi,ikawa inaombea huyu mtu asiwe karibu yangu, kutokana na maswali yake.

‘Na wakati tunaongea mimi na yeye, kila hatua nilianza kuhisi hatari iliyopo mbele yangu, awali nilitaka kumwambia ukweli ili yaishe,…, nikijipa moyo kuwa hakuna litakalotokea baya, yeye si rafiki yangu, rafiki wa kweli ni yule yupo tayari kumpa mwenziwe kile akipendacho, au sio…’akasema na watu wakaguna.

‘Nasemea jinsi nilivyokuwa najipa matumaini,..mnielewe hapo…’akasema alipoona watu wanaguna.

‘Kwahiyo kutokana na maneno yake kwa haraka nikamkatalia kumwambia ni nani baba wa mtoto..na hata pale alipojiwa na ufahamu kidogo ya kuhis kuwa huenda aliyefanya hivyo ni mume wake, baada ya kuona sura ya mtoto inafanana na watoto wake, nikamkatalia kuwa mume wake, sio baba wa mtoto wangu..’akatulia

‘Kiukweli.., kauli zake za vitisho, kuwa hatakubali mtu aje kutembea na mume wake, hatakubali mtu …na vitu kamahivyo, na zaidi akasema ambaye atawahi kuingilia ndoa yake kuna adhabu kubwa atakuja kupambana nayo. Niliogopa, na kuanza kujenga hisia nyingine ya kujihami.

‘Ni kweli inauma sana, lakini kinamna fulani, naweza kusema kuwa sikutarajia kabisa kuwa rafiki yangu ataumia kiasi hicho, sikutarajia kuwa hilo nililolifanya ni kosa kubwa kwake, , ikizingatiwa kuwa ni yeye rafiki yangu,na ni mtu anayependa kunipa ushahuri, na alikuwa anatamani sana na mimi nimpate mtoto...

‘Ni kweli kuwa mume wa familia nilikuwa nakutana naye mara kwa mara kwa rafiki yangu, …lakini baada ya tukio lile la pili nikawa simuamini tena, na akawa sasa anamtumia rafiki yangu awe mtu wa kutupatanisha…ili iweje basi, mtoto…mtoto akawa ni hamasa kubwa kwa mume wa familia.

‘Kama huyu mtu ndiye kanibebesha hii mimba nitakuwa na ushahidi gani baadae, nikaona nitafuta ushahid fulani, ikibidi, ili ije ijulikane ukweli ulivyokuwa, kwa vipi sasa.. kwa vile alishaona kwa rafiki yangu ndipo mahali pa kukutana naye ili kujenga suluhu, nikaweka vifaa vya kurekodi matukio, ili nipate kauli yake muhimu ya kuthibitisha kuwa yeye ndiye kasababisha haya bila dhamira yangu.

‘Sasa kumbe wakati nayafaya hayo,kumbe kulikuwa na mtu alishalifikiria hili mapema sana!!...’hapo akatulia kama anasoma kitu kwenye ile karatasi.

‘Ndugu zanguni haya nayaongea lakini naombeni muweni makini sana majumbani mwenu hasa nyie watu mashukuri..kuweni makini ..muwe mnachunguza nyumba zenu, dunia ya sasa ni kijiji…kimtandao,na mawasiliano…’akasema

‘Hadi hapo, bado sikuwa na ufahamu huyu mtu aliyefanya hivyo, alicheza huo mchezo na wanafamilia hao, au alikuwa na ajenda yake mwenyewe, na peleekni akili zenu mbali zaidi,…siwaambii hilo kwa hivi sasa, nitakuja kulifafanua baadae ili kuwaonyesha kuwa hili jambo, sivyo kama tunavyolifikiria kiraisi raisi, kuwa labda, au vile..’akatulia, na kugeuza ile karatasi upande wa pili.

***********
Siku moja, baada ya kujifungua, ni siku kama mbili hivi baada ya kutoka hospitalini, alikuja mume wa familia, kipindi hicho nipo kwenye sehemu yangu ya kwanza niliyopanga, akaniambia kuwa kuna tatizo kubwa limetokea, nikamuuliza tatizo gani, mara akatoa picha na kunionyesha, ...oh...shabashi,....’akatulia kama vile ndio anaziona hizo picha mbele yake, akijenga hisia za tukio lile.

What,..ni nini hiki, ni nani kafanya hivyo,ina maana mliyafanya haya ili …’nikawa nimekasirika kweli

‘Hapana unielewe sana, hata mimi sikulifahamu hilo, sikujua kuwa hapo kwenye nyumba yako kuna vinasa matukio,kwanza niliwazia kuwa huenda ni wewe upo nyuma ya hili jambo…’akasema

 Kiukweli zilikuwa picha chafu, zilikuwa picha zikionyesha jinsi gani walivyonizalilisha siku ile,..na anayeonekana ni mume wa familia, ndio maana baada ya pale, ukichukulia na sura ya mtoto, moja kwa moja, niliamini kuwa aliyefanya hivyo ni yeye na sio ndugu zake, kwenye picha hiyo anaonekana mume wa familia, akinizalilisha, ni ushahidi usipingika, mama kila kitu kilikuwa dhahiri…’akasema akikunja uso kuonyesha uchungu au hisia ya kukasirika.

Nilishituka sana, sikutarajia kitu kama hicho, kwanza nikaziangalia zile picha, na kwa haraka nikazichana-chana, na kuhakikisha hakuna kitu kinachoonekana na yeye, yaani mume wa familia, akaniambia;

‘Hata mimi nilipoonyeshwa hizo picha nilifanya hivyo hivyo, lakini kila siku nikawa naletewe picha kama hizo na nyingine mbaya zaidi ya hizo,...’akasema na hapo akanivuta kwenye hisia nyingine kuwa waliofanya hivyo, wana nia madhubuti ya kuniangamiza mimi.

‘Alikuwa akikuleta nani hizo pichai?’ nikamuuliza kwa hasira

‘Sijui,...ila mwishoni hapa, kuna simu nimepigiwa na mtu nisiyemfahamu, mtu huyo anasema anataka kuongea na mimi, nikamuuliza unataka kuongea na mimi kuhusu nini, akaniambia kuhusu mzigo niliokuwa nikiupokea mara kwa mara, nikamuuliza mzigo gani, akasema picha..’akatulia

‘Nikamwambia hata kwenye mitandao kuna picha, watu wanaweza kuunga unga ili kumzalilisha mtu mwingine…’nikamwambia hivyo, yeye akasema

‘Picha za kuungwa ungwa zinajulikana, na hata hivyo kuna namna ya kuhakiki kama kweli picha hizo ni za kuungwa ungwa au la,..kama nabisha nichukue hizo picha kwenye studio za wataalamu, watalithibistisha hilo kuwa hizo picha ni hakika…’akasema

‘Kwanini nifanye hayo, ..?’ nikamuuliza

‘Kwasababu ushahid halisi sasa upo , hakuna ubishi tena, picha pamojana huo ushaidi umekamilisha uchafu wako…’akasema

‘Ushahidi gani..?’ akauliza

‘Mtoto…huyo mtoto na wewe hakuna ubishi, mnafanana kama vidole vyako, …’akasema

‘Sasa unataka nini..?’ akamuuliza

‘Subiri, usiende haraka, mimi nataka kuongea na wewe…nilisubiria sana, na sasa muda muafaka umefika, nataka tuongee mimi na wewe, tutaelewana tu…’akasema na kukata simu…, ndio maana nimekuja kukuona wewe kwanza...’akaniambia hivyo

‘Ina maana huyo mtu aliyekuwa akikuletea hizo picha, mlikuwa hamuonani, naye, ulikuwa unazipata vipi hizo picha, na hayo ya kupata hizi picha yalianzia lini, na kama unavyodai umekuwa ukizipokea hizi picha mara kwa mara ina maana ni siku kadhaa nyuma sijui lini…, mbona hukuwahi kuniambia kabla, na kwanini sasa umeamua kunionyesha, ..?’ nikamuuliza

‘Ni kweli,picha hizi nilishazipata kabla,mapema tu, na sikutaka kukuonyesha mambo haya, kipindi ukiwa mja mzito, nilisubiria ujifungue kwanza, niliogopa usije ukaharibu mimba, na hata hivyo, mimi nilijua nitalimaliza mwenyewe, nikijua shida yake ni pesa, nikawa nampa pesa, lakini ikawa ndio biashara, nilitamani nionane naye ni-m-malize, maana utaishije hivyo...’akasema

‘Unahisi huyu mtu ni nani?’ nikamuuliza kabla hajaendelea zaidi

‘Kwakweli nimefikiria sana, ni nani anaweza kulifanya hili, kiukweli awali nikajua huenda ni wewe ukiwa na malengo yako, lakini kila nikipima kila nikija na kukudadisi, unakumbuka nimekuwa nikikuliza maswali awali,..ukawa unanijibu kijeuri, mimi nilikuwa na lengo langu…sasa nikirejea nyuma wewe huwezi kufanya jambo kama hili, kwa jinsi ninavyokufahamu,… sasa ni nani mwingine…, ndio nikaoana nije tuongee tuone tutafanya nini…’akasema

‘Mhh..bado hujanishawishi na majibu yako, kwanini sasa, kwanini lifanyike hivi leo, na tumekuwa tukikutana mara nyingi hapa..?’ nikamuuliza

‘Nilikuwa nasubiria wakati muafaka, maana kwanza awali ulikuwa umenikasirikia, ukawa huonekani, na baadae ndio nikakutana na wewe kule hospitalini  kiukweli, sikupenda kukuumiza zaidi, najua kilichotokea imekuwa ni mtihani kwako, na sio kwako tu, pia hata kwangu, ni- ni mtihani mkubwa.

‘Isingelikuwa huyu mtu, wa hizi picha kujitokeza sasa,  ningelisema niache mambo yaende kama yalivyo, nafahamu muda muafaka utafika, mtoto atamuhitajia baba yake…’akasema

‘Sasa kwa hili, inaonyesha tusiposhirikiana mimi na wewe..taarifa hizi zitafika sehemu ambayo haitakiwi zifike...sasa tufanyeje..’akasema

‘Tufanyeje, wewe uliponifanyia hivi, hukulifahamu hili, ..niambie ukweli ni nani alikutuma mnifanyie hivi, nahisi una njama na hujuma fulani, sema ukweli wako, maana nikija kugundua, nitafanya zaidi ya hili..?’ nikamuuliza

‘Kunituma,!!!..Hakuna aliyenituma, haya niliyafanya kwa vile ninakupenda sikuweza kuvumilia, na nilipopata nafsi hizo, nikaona nizitumie, ndio nilifanya hivyo, zaidi nikiwa nimelewa, huenda kama ningelikuwa mzima nisingeliweza kulifanya hilo, ila pombe ndio ilinihamasisha zaidi…’akasema

‘Niambie ukweli, ni pombe au ni dhamira yako, na hayo madawa mliyapatia wapi, nina mashaka na wewe..?’ nikamuuliza

‘Kiukweli mimi nakupenda, na nimekuwa nikifanya jitihada za mara kwa mara kukuonyesha hilo, wakato upo pale nyumbani, unajua, nilikuwa nahangaika sana,  ..na ilipotokea nafasi hiyo, basi..zaidi ni kwamba nimefanya hivyo ukiwa hujitambui, ..sikupenda mapenzi ya namna hiyo, nilitaka tuwe wapenzi wa kweli, na hayo madawa mbona yapo tu, ni pesa yako..’akasema

‘Hivi, nikuulize wewe si una mke wako, na mke wako ni rafiki yangu kipenzi, ina maana mke wako humpendi,..na unatarajia nini baada ya hili..?’ nikamuuliza

‘Usijali kuhusu mke wangu, hilo niachie mimi, ilimradi wewe uwe tayari, ukubali kushirikiana na mimi, ili hili tulimalize kwanza, na kuhusu mke wangu ndio nampenda kama mke wangu, huo ni upendo mwingine na wewe nakupenda kivingine usilinganishe haya mambo, nielewe tu hivyo, nakupenda…’akasema

‘Sijakuelewa, na sitakuelewa, hivi unafahamu kuwa hapo unavunja ndoa yako, na kwa hili umeshavunja ndoa yako, kutokana na mkataba wenu wa kifamilia..?’ nikamuuliza na nilipomuuliza hivyo, nikamuona akichanganyikiwa kabisa.

‘Mkataba,mkataba, mkataba….mmh, kwa kauli yako hiyo inanipa mashaka sana hivi sio wewe kweli umalifanya hili, ili uiharibu ndoa yangu..?’ akasema

‘Wewe una kicha eeh…hebu toka humu ndani kwangu, sitaki kukuona tena, na wewe na hao waliokupa hizi picha unanifahamu nilivyo,nitawatafuta,…nitawapata,..’nikasema

‘Sikiliza kwanza,…wewe ndiye pekee umesema na kulihusisha hili na mkataba wangu, na huyo aliyenitumia hizi picha kaandika ujumbe kuwa je hizi picha zikionekana itakuwaje kwenye ndoa yangu, itakuwaje, kwenye mkataba wangu wa kifamilia, na swala la mkataba lilikuwa mimi na mke wangu, ni nani.. ..’akasema, n akukatisha

‘Sikiliza, wewe na huyo mtu, mjue mumeingia sehemu isiyofaa, na kama nia yako ni kuhusu huyu mtoto, huyu mtoto hana baba, baba yake alishafiriki…’nikasema

‘Oh, kwanini unasema hivyo, mimi ndiye baba yake, huyo ni mtoto wangu tunafanana naye, nina uhakika huyo ni mtoto wangu, ni kweli , nilikufanyia vile nikiombea kuwa tupate mtoto, na niliombea atokee mtoto wa kiume, na duwa zangu zimepokelewa, kwahiyo nakuomba tushirikiane kwa hili..’akasema

‘Nakuomba utoke hapa nyumbani kwangu, sitaki nikuone ukikanyaga hapa nyumbani kwangu tena, unasikia, sitaki kusikia mambo yak ohayo..sitoshiki na huo ujinga wenu, picha zinatengenezwa, na…na sitaki kusikia.. , kuwa wewe ni baba wa mtoto wangu, unasikia,, huyu mtoto hana baba…’akasema

‘Sasa hizi picha zina maana gani, ..hujasoma ujumbe nyuma ya picha…’akasema na wakati huo nilikuwa nimeshazichana-chana  zile picha

‘Ujumbe huo unasema nini..?’ nikauliza

‘Kuwa yeye anafahamu tukio lote la kukutana mimi na wewe, na kwa jamii, wakiona kitu kama hiki sizani kama kuna cha kujitetea eti kuwa, nini na nini..’akasema

‘Bwanaee, niache..’nikasema

‘Sikiliza,..huyu aliyefanya hivi alitaka ushahidi na keshaupata, ushahidi ambao akiufiksiha kwa mke wangu anajua nitamalizwa, nitaumia, na kwa wakwe zangu hatawaweza kulivumilia hili, hii ni kashfa kubwa sana,..sizani kama walikiliona hili watavumilia, na hata kama mke wangu atanitetea vipi ..’akasema

‘Wewe unahisi ni nani huyo mtu…?’ akaniuliza

‘Bado sijaweza kumtambua, ..kiukweli nimekuwa kwenye wakati mgumu,nilipanga kuwa mimi  sitalewa tena, ulevi na mimi basi, kwa vile ulishanipatia kile nilichokitaka, lakini kwa hali kama hii…hapana nikitoka hapa nitakunwya mapaka nsipate muda wa kuwaza, …ni matatizo…’akasema

‘Kwahiyo wao wamesema wanataka nini…?’ akniuliza

‘Ndio maana nimekuja kwako, kwanza nilihisi inawezekana ukawa ni wewe ulifanya haya yote kunikomoa, mimi, ..kwahiyo kuja kwangu hapa, ilikuwa nikuulize unataka nini kwangu, mali labda, au…, lakini nilipokuona tu, akilini, nikaingiwa na mawazo ya kulipinga hilo, sio wewe, sizani kama ni wewe…na kama sio wewe ni nani basi,…mmh, huyo ni mtu asiyejulikana…’akasema

‘Naomba uondoke , na sitaki kukuona tena…’nikasema kwa hasira, na yeye akaniangalia kwa mshangao, na hakuondoka, akawa kasimama tu, baadae akasema;

‘Ina maana wewe upo tayari, taarifa hizi zifike kwa rafiki yako, ukumbuke wapi ulipotoka wewe na yeye, na ukumbuke wewe una mipango ya kwenda kusoma nje…’akasema

‘Hayo yanahusiana nini na huu ujinga wenu, ni nyie mlionifanyia haya, sikupenda iwe hivi…’nikasema

‘Una uhakika..wewe hukuwa unataka mtoto, kama ilivyo mimi, niambie ukweli wako, ..umri umekutoka, utazaa lini, ..eeh, hujashauriwa hivyo…?’ akaniuliza

‘Ni kweli nilishauriwa hivyo, ..lakini sio kwa hivi livyotokea, sikutaka iwe hivi, na sijui kwanini sikwuashitakia…’nikasema

‘Ndio..kwa vile unanipenda, au sio…?’ akauliza

‘Siwezi kupenda mume wa mtu, …wewe ni shemeji yangu, na kwa hili hata sijui jamii, itanielewaje…’nikasema.

‘Jamii, jamii..mmh, kiukweli mimi nilifikia mahali nikasema …ahsante mung, hatimaye nimepata nilichokitaka, nilijua na wewe utsema hivyo hivyo, au sio…lakini kwa hili sasa ..sijui kuna nafasi hiyo tena…’akasema

‘Mimi nakuomba uondoke ..nitajua mwenyewe jinsi gani ya kulitatua hili…unajua, natamani ni….’hapo sikuweza kumalizia, na yeye akasema

‘Kunifukuza kutasaidia nini…mimi najaribu kukumbusha tu, kuhus tatizo lilipo mbeel yako,..hebu kwanza fikiria, je hili tatizo utaweza kulitatua mwenyewe, achilia mbali matunzo ya mtoto, kumbuka,..ni nani alikusaidia na atakaye kulipia kila kitu, eeh, na ukumbuke ulipotoka, …,’akasema

‘Una maana gani..?’ nikauliza

‘Ni kuhusu hizo picha,… je yeye huyo mfadhili wako, akija kuziona, ..akiona kitu kama hicho, hivi kweli bado atakuwa na nafasi ya kukusaidia, ….na je maisha yako ya baadae yatakuwaje,…huoni huo utakuwa ni mtihani mkubwa kwenye maisha yako, utakimbilia wapi, eeh,… mimi nakuomba tushirikiane ili tuweze kulimaliza hili jambo…’akasema

‘Kwa vipi..?’ nikamuuliza, nihisi kiukweli kuwa kweli kuna mtihani mbele yangu.

‘Kwanza, …kuna mtu namshuku, lakini …sijawa na uhakika naye, wewe ni mtaalamu sana wa kuchunguza mambo, tukiwekeza nguvu zetu kwa pamoja tunaweza kumshika huyo mtu, lakini kwa hivi sasa anataka pesa, tena pesa nyingi tu..’akasema

‘Anataka pesa, mimi nitazipatia wpi hizo pesa, unajua nilivyo, au wewe unahisi nitazipataje hizo pesa…?’ nikamuuliza

‘Tukishirikiana tutazipata tu..hilo sio tatizo…,kwanza ni muhimu kupatiakane kiasi fulani, ili tuweze ku-m-poza huyu mtu…, na huku tunaendelea na uchunguzi, ujue sio kwangu tu kutaharibika lakini hata kwako pia, umeonaeeh, ..’akasema

‘Kwahiyo unatakaje..?’ nikamuuliza nikitaka kujua huyu mtu ana lengo gani, maana hadi hapo japokuwa nafahamu nimekosea, lakini sikuwa bado nimefikiria kwa hali mbaya kiasi hicho, …baada ya kuziona hizo picha ndio nikajua sasa kuna tatizo,..

‘Tushirikiane bila kujali haya yaliyotokea, pili, hili jambo liwe siri kubwa, tatu, hakikisha hata iweje rafiki yako asiweze kuliona hili, je mtoto ameshamuona..?’ akaniuliza

‘Ndio…’nikasema

‘Alipomuona kashuku jambo..?’ akaniulia

‘Anasema anafanana na watoto wako..’nikasema

‘Mhh..mtihani huo, hukutakiwa kumuonyesha yeye, sasa utafanya mambo yazidi kuwa magumu…’akasema

‘Sasa ulitaka mimi nifanye nini..?’ nikamuuliza

‘Sikiliza, kwanza cha muhimu, usije kumuambia mke wangu, fanya ufanyavyo, mke wangu asifahamu kuwa huyu mtoto nimezaa na wewe, hilo liwe siri, nakuonya hilo tena tena, humfahamu mke wangu akikasirika anavyokuwa,...'akatulia

'Sawa...'nikasema

'Sasa ni hivi, kuna wazo limenijia akilini, na..nafahamu hutamuamini huyo mtu, wengi hawamuamini, kihivyo,  lakini kwa mmabo kama haya hakuna mwingine anayeweza kupambana nayo zaidi yake, mimi namuamini sana, kwa vile huyo mtu ni rafiki yangu mkubwa sana, yeye anaweza kutusaidia kwenye hili tataizo, nakuomba kwa hili umuamini …’akasema

‘ Ni nani huyo…?’ nikamuuliza sasa nikiwa na mashaka, kila nikiwaza na kuwazua, naona hata mimi nipo kwenye mtihani.

‘Kwanza ukubali kushirikiana na mimi, ….tuwe marafiki,na hata baada ya hili..’akatulia kidogo.

'Marafiki, haaaah, ..'nikasema na kutikisa kichwa kumkatalia

‘Nakuahidi …hata kama itashindikana, japokuwa hakishindikani kitu mbele ya pesa, nakuahidi kwa hili, kwa vile mimi kweli nakupenda, natamani uwe wangu wa milele..lakini tuyaache hayo, …hayo yatakuja baadae, ila hili, kwa hili hata wewe huna ujanja kama nilivyo mimi, unasikia, na mtu peke yake wakutusaidia hili ni huyo rafiki yangu…’akasema

‘Ni nani huyo rafiki yako, sasa …?’ nikamuuliza

‘Ni jamaa mmoja hivi , ni mjumvi wa haya mambo, nimeshamtumia kwenye mambo yangu mengi, akanisaidia sana vinginevyo, ningeumbuka..na kwa hili bila yeye, hatuwezi kuponyoka,…ninachojiuliza ni kwanini mimi, maana, kila nikimaliza tatizo moja, linazuka jingine…sasa kwa hili , limenishika pabaya..’akasema

‘Ni nani huyo mtu..?’ nikamuuliza, sasa nikionyesha kukasirika, maana badala ya kunitajia anazidi kuniweka kwenye hofu, na mimi sio mtu wa hofu japokuwa hapo hofu ilishaniingia.

NB: Tutaendelea na sehemu ijayo. Msione kama tunarejea nyuma, hapa ndio tunakwenda  kufikia kwenye ukweli halisi.


WAZO LA LEO: Mara nyingi uwongo haudumu, ni swala la muda tu, wapo watu wanahisi ni wajanja kwa kuishi kiujanja ujanja,..wanahisi hali waliyo nayo, na maisha waliyo nayo, waliyoyapata kwa ujanja ujanja, watadumu nayo, na kwahiyo wataweza kuishi milele, je ni nani aliishi milele,kiukweli hakuna atakayeishi milele, walikuwepo , wamepita,…na sisi tutapita vile vile..cha muhimu ni kujiuliza huko tuendapo tumejiandaaje..niwatakie ijumaa njema.

Ni mimi: emu-three

No comments :