Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, November 15, 2017

MKUKI KWA NGURUWE-26



‘Jamani tunaomba nafasi...tunataka kumweka mgonjwa vizuri,…kuna jambo tunatakiwa kumfanyia sasa hivi, na muda umekwisha,…na hata hivyo mgonjwa hakutakiwa kuongea na watu kwa muda mrefu hivyo, docta natumai unakumbuka masharti tuliyokupatia, naona hii inatosha, samahani docta,...’akasema huyo docta, akimgeukia docta mwenzake.

‘Tunataka tufanye kazi yetu samahani…’akasema docta bingwa wa mifupa, akianz kuweka vitu vyake sawa.

‘Hamna shida, tumeshamalizana, .....’akasema docta rafiki, sasa akiniangalia mimi machoni, na kunigusa begani akasema;

‘Toa kauli yako haraka, tuondoke....’akasema na mimi nikageuka kumuangalia mume wangu, na nilivyoona vile vyuma, wanavyotaka kumuwekea mume wangu, huruma, machungu yakanishika,…nilijiuliza moyoni, ni kosa gani alilolifanya mume wangu linalostahiki hayo yote, hapana mungu anisaidie, tu, mungu amsaidie tu mume wangu

Kiukweli pale moyo wangu ukawa mweupe, nikawa sina kinyongo na lolote kwa mume wangu, haraka nikamuinamia mume wangu,  na yeye alikuwa akiniangalia kwa macho yaliyojaa huruma, ….kuonyesha kuwa anateseka moyoni na kiwili wili…tukawa tunaangaliana, niliona machoni kwake akianza kutoa machozi,…na mimi nikahisi machozi yangu yakinijia kwa kasi, kabla hayajaanza kutoka nikasema;

‘Mume wangu nimekusamehe, natamka haya kutoka moyoni mwangu, namomba mola mwenyezi akujalia upone, ili tuwe pamoja, sioni dhambi gani kubwa inayostahiki mateso hayo yote, nakupenda sana mume wangu,  pambana na haya, uyashinde, ukijua mimi mke wako nipo kwa ajili yako,..na kama kuna mengine tutayamaliza nyumbani, sawa mpenzi mume wangu....nimeshakusamehe...’nikasema na nilipomaliza kusema maneno hayo;

Nikaona tabasamu likijitokeza usoni mwake, ..uso ukapambwa na nuru ya furaha,…akawa kama anataka kuongea kitu lakini hakuweza,mdomo ukawa unatikisika tikisika,,.. na mara akaanza kutikisika hivi,…madocta hawakuwa awali wameliona hilo.

Nikawa najaribu kuwaonyeseha ishara madocta, lakini walikuwa wakiongea na yule mwingine alikuwa akiweka vitu vyake sawa..ile hali ya kutikisika haikuchukua mdua mrefu, mara akafumba macho, ...na muda ule ule,  nikasikia milio ile ya hatari ikilia chumba kizima, na wale madakitari wakamsogelea mgonjwa na kutuambia tutoke humo ndani haraka.....

‘Nini tena…’akasema docta wake, na haraka wakaanza kazi ya kumuhudumia, hata vile vyuma viliwekwa pembeni, wakawa sasa wanahangaika kumrejesha , azindukane, maana alishapoteza fahamu.

Mimi kuiona ile hali, kwanza nilibakia mdomo wazi, siamini,..nishikiwa na bumbuwazi, macho yamenitoka , nikawa sina nguvu kabisa miguu haiwezei hata kuinuka,…nikahisi maumivu makali kichwani ….maumiu makali kweli.., na pale pale nikahisi kizungu zungu, na kabla sijadondoka, giza likitanda usoni, na sikukumbuka kitu mpaka pale  nilipozindukana nikajikuta nipo kitandani.

*********

Siku mbili nilikuwa kitandani sijiwezi, japokuwa siku nile kama walivyinielezea, nililazwa na kuwekewa maji, yalipoisha, nikawa nimshazindukana, nikauliza kuhusu mume wangu, wakaniambia anahudumiwa, siwezi kumuona.

Niligoma kuondoka nikitaka nimuone mume wangu kama yupo hai au la..sijui walifanya nini, usingizi ukanijia, na nilipoamuka tena nilijikuta nipo nyumbani kwangu, kitandani nimelala mwili ulikuwa hauna nguvu kabisa,

Ilikuwa sasa ni siku ya tatu ndio  akaja docta rafiki wa mume wangu kuniangalia ninaendeleaje, nikajitutumua na kutoka, nje, kuonana naye, akasema;

‘Sasa unatia matumaini,  naona leo upo safi, siku zote nakuja hata hunitambui vyema, sasa jitahidi hivyo hivyo, ujiimarishe mazoezi, na hali hiyo itakwisha,…’akasema

‘Sawa umekuja nataka kwenda kumuona mume wangu…kama….angalau niuone mwili wake..’nikasema

‘Unasema nini wewe…uuone mwili wake, kwani mume wako amefariki, nan kakudanganya…’akasema

‘Usitake kunificha…’nikasema

‘Unajua kwa hali kama hiyo, nahisi ni vyema tukaongozana ukaenda kumuona wewe mwenyewe....’akasema

‘Docta, usitake kunifanya mimi mtoto mdogo, niliona kwa macho yangu…’nikasema, nikijua wananificha tu.

‘Usijali, tutakwenda kumuona mgonjwa, hajambo mwenzako, leo ni muhimu twenxe ukamuone ili uwe na amani ....’akasema.

‘Ina maana kweli mume wangu yupo hai,..docta, usinifichei…oh, jamani, nimekua mgonjwa zaidi ya mgonjwa, vipi anaendeleaje lakini…, mimi nilijua siku ile ndio naagana naye…’nikasema sasa nikiwa na imani, na nguvu zikaongezeka mwilini kiaina yake

‘Unajua siku ile ilikuwa kizaa zaai, maana ulipotewa na fahamu, ikabidi uhudumiwe wewe kwanza..lakini  baada ya kutolewa mle ndani maana kipindi kile ndicho mume wako naye alikuwa kapoteza fahamu, madota wake walikuwa na yeye , iakbdi mimi nipambane na wewe…’akasema.

‘Ahsante mungu wangu, kwahiyo mhh…, mungu mkubwa, mume wangu bado yupo hai…jamani hadi kwenye ndoto nikawa namuota tunaagana, hizi ndoto jamani…’nikasema

‘Hajambo kabisa, anaendelea na matibabu ya kuweka viungo vyake sawa, ile kauli yako ilitokea moyoni kuwa umemsamehe, aliihisi,…kwahiyo ila hali ya kuchanganyikiwa ikaondoka baada ya kuzindukana, akaja mtu mpya, mwenye afya yake, akawa
anaongea vizuri tu…’akasema

‘Hapo sasa umenipa nguvu …sasa naweza kwenda kumuona ila bado mimi naogopa…kwenda kuangaliana naye, unajua tangia mume wangu alazwe, anakuwa kama mgeni kwangu kabisa, sijui kwanini…’nikasema.

‘Usiogope ni lazima upambane na hiyo hali, na yeye pia, …hata hivyo baada ya kuzindukana, hali yake imeimarika sana, ..tuna imani mkikutana naye hakutakuwa na tatizo tena, na huenda akaanza kuongea tena, maana ghafla juzi alikataa kuongea kabisa na watu, hatutajua tatizo ni nini…lakini haya yatakwisha tu tu...’akasema.

‘Alikataa kuongea au ndio kule kuongea kwakwe kwa shida…?’ nikauliza

‘Ile hali ya kuongea kwa shida, ilishamalizika…na akawa anaongea vyema tu…hebu jiandae basi tuondoke, au unakwenda hivyo hivyo ulivyo…?’ akaniuliza

Baada ya kujiandaa, nikaingia kwenye gari la huyo rafiki wa mume wangu, na tukaanza kuongea maswala mengine, kwa muda ule nilitaka ninyamze tu, sikuataka kuongea kabisa,  na mara nyingi nilikuwa mtu wa kuitikia tu, lakini aliponiuliza swali hili ikabidi nishtuke na kumjibu;.

‘Rafiki yako alikuaga?’ akaniuliza.

‘Rafiki yangu gani...?’ nikauliza huku nikionyesha mshangao.

‘Usipende kuuliza swali, wakati unafahamu nakuuliza nini, una marafiki wangapi, ..na unafahamu kabisa nikisema rafiki yako nina maana gani’akasema.

‘Kwani kaenda wapi?’ nikamuuliza kwa mshangao.

‘Haah, ina maana, hujui, si kaenda kusoma ulaya, nakumbuka kuna siku uliniambia kitu kama hicho, sasa kaondoka jana usiku ...’akasema.

‘Haiwezekani, hawezi kuondoka bila ya kuniaga, ina maana kaamua kuondoka bila ya kumuona  mgonjwa, angalau angesubiria kuona mgonjwa anaendelea vipi, haiwezekani, ..hapana huyo sio rafiki yangu ninayemfahamu mimi ndio kafanya hivyo ili iweje, au unanitania..?’ nikauliza nikiwa siamini kabisa.

‘Ndiye huyo huyo rafiki yako, na kama ni swala la kumuona mgonjwa, mbona karibu siku mbili hizo, ulipokuwa unaumwa nyumbani yeye alikuwa akienda kumuona mgonjwa, alisema kwa vile unaumwa, ni wajibu wake kuchukua nafasi yako...’akasema.

‘Mimi sikuelewi, mliniambia nini mimi, kuwa mgonjwa haruhusiwi kuongea na mtu mwingine zaidi ya mimi na wewe, na hao madakitari wanaomshughulikia, ikawaje sasa mkamruhsu huyo mtu…?’ nikauliza kwa mshangao.

‘Hakuruhisiwa kumuona mgonjwa, yeye alikuwa akifika na kusimama kwenye kile kiyoo, unachoona ndani, basi, alikuwa akifanyaa hivyo kila siku ila jana, ndio akapata nafasi ya kuingia ndani, ...’akasema.

Nilitulia kwa muda, sikuweza kuongea, kwani moyo ulikuwa ukiniuma, nilihisi kuna jambo linaloendelea, na hawa watu, na wanachofanya wao ni kunichezea akili yangu,

‘Aliruhusiwa kumuona, sijui ilitokeaje, mume  wako akaulizia kuhusu huyo rafiki yako, kuwa je aliwahi kuja kumuona, tukamwambia kwa vile analea  mtoto mchanga inakuwa vigumu kwake, yeye akaomba aletwe , anataka kuonana nay eye, kama hajaondoka kwenye kusoma...’akasema na hapo nikageuka kumwangalia huyo rafiki yangu.

‘Ina maana …mbona sielewi hapo....!?’ nikauliza kwa mshangao,

‘Yaonekana mume wako akilini alikuwa anamkumbuka rafiki yako, na anafahamu kuwa atakwenda kusoma, ndio maana akaomba aje waongee naye kabla hajaondoka, na siku hiyo alikuwepo nje, sijui alijuaje kuwa yupo hapo nje, ikabidi aambiwe aingie…’ akasema.

‘Siwaelewi hapo kabisa, unazidi kunichanganya, halafu alipoingia alikuwepo nani mwingine aliyesikia wakiongea naye…’nikasema.

‘Mimi sikuwepo, nilifika wakati wameshamaliza kuongea nikaambiwa ilivyokuwa, sasa sijui waliongea nini, ..hata hivyo, kipindi wanaongea hakutaka mtu mwingine awepo , kwahiyo waliongea wao wawili tu…’akasema

‘Mhh…mimi sipendi hisia mbaya, nimejitahidi sana kulikwepa hilo, lakini kila hatua najikutwa nalazimishwa kuhisi vibaya, naanza kumshuku rafiki yangu mwenyewe ubaya, ni kwanini lakini, ni kwanini ….mimi nilimuamini sana, ..oh, hata sijui, …mungu anisamehe tu…’nikasema

‘Sio swala muhimu sana, kwa hivi sasa,…muhimu na la kuzingatia, ni ahadi kwa mume wako, kuwa umeshamsamehe au umesahau hilo?’ akaniuliza .

‘Mimi sijasahau, ila sikujua anataka nimsamehe nini, sasa , kosa gani nililomtendea, ndio maana nhitajia kumuuliza, sijui nifanyeje….’nikasema

‘Kwa hivi sasa hapana, inatakiwa wewe kuwa hivyo hivyo, kuwa umeshamsamehe, na sitaki kabisa kukulazimisha kuamini ubaya wowote dhdi ya rafiki yako na mumeo, kuwa labda kuna mahusiano ..labda…ila dalili zinajionyesha hivyo, ..’akasema

‘Hata mimi sasa naanza kuziona, lakini nafsini mwangu nashindwa kuliamini hilo, na kwanini iwe hivyo, rafiki yangu mwenyewe anifanyie hivyo, ..mume wangu mwenyewe anifanyie hivyo, hivi kweli wewe unaweza kulisamehe hilo…’nikawa nauliza

‘Kwa hivi sasa inabidi iwe hivyo, mpaka mumeo apone, mpaka, mumeo awe an nguvu za kukabiliana na wewe….naomba uwe hivyo, ujue lolote utakalolifanya kinyume na ulivyokiri kuwa umeshamsamehe, unaweza kuhatarisha maisha ya mumeo…’akasema

‘Ni vigumu sana, kama ni kweli hilo limefanyika, sizani kama msamaha huo utakuwepo, sizani,…hata kama kakimbia , nitafanya nifanyalo, akipate kile nilichoa hidi …sitamsamehe….siwezi kabisa…’nikasema

 ‘Kumbuka uliyatamka hayo mbele ya mume wako, akaamini kweli umeshamsamehe,..sasa usiwe kigeu geu wa kubadili kauli zako, unaongea vingine unakuja kutenda mengine, sio vizuri, nina imani kuwa siku ile uliyatamka hayo maneno ya kumsamehe kutoka moyoni mwako, au sio….’akasema docta

‘Ndio ilitoka moyoni, lakini sikujua kosa , sikujua nasamehe nini sasa, mlinitega tu, najua hata wewe unalifahamu hilo, na kama upo nyuma ya hili jambo sizani kama nitaweza kuwasamehe….’nikasema.

‘Mimi sijui lolote zaidi ya kufanya juhudu kuutafuta ukweli, mimi niliona hizo dalili, sikutaka kuamini hivyo, na ilichukua mud asana kuanza kuhis hivyo, japokuwa rafiki yangu alijitahidi kunificha..mimi sikupenda kabisa wewe wakufanyie hivyo, na rafiki yangu alilifahamu hilo, ndio maana hakuwahi kuniambia…’akasema

‘Rafiki yangu…siamini, bado sijaamin…’nikasema

‘Huenda ikawa sio kweli, kwasababu hata mimi pamoja na juhudi zote sijapata ushahidi wa moja kwa moja…nap engine huyo rafiki yako aliitwa  kwa jambo hilo hilo....’akasema

‘Jambo gani…?’ nikauliza

‘Kuwa labda kamkosea,..kwahiyo alitaka asamehewe, au labda,…mimi naona labda zipo nyingi sana, na sio vyme kabisa kuwa na shaka shaka hizo tena, muhimu kwa sasa tuangalia afya ya mume wako,..hilo ndilo la muhimu mengine yasubiria kwanza…’akasema

‘Ni ngumu sana…’nikasema

‘Sasa tunakaribia kufika, leo foleni imezidi sana,…tukifika ukumbuke,  ni vyema ukiingia pale uwe na uso wenye furaha, usionyeshe chuki yoyote, kuwa labda kuna jambo,  maana toka jana alipofika huyo rafiki yako wakaongea naye, alipoondoka tu tulishangaa,…’akasema

‘Alikuwaje..?’ nikauliza

‘Amekataa kuongea tena na watu, tunahisi huko kukataa kuongea kwake, kuna mahusiano na huyo rafiki yako, hatujui waliongea nini, na mgonjwa mwenyewe akiulizwa kwanini anafanya hivyo hataki kusema, basi tukasema labda ni kwa vile na wewe hujafika, lakini hilo tulimuelezea awali kuwa unajisikia vibaya, akalipokea sasa jana ndio hali hiyo ikajitokeza...’akasema.

‘Kwahiyo …sasa kwanini hakuulizwa huyo mtu kabla hajaondoka, ni kwanini anamtesa mume wangu hivyo, kuna nini kati yao wawili, …hapana mimi sizani kama nitaweza kuvumilia tena, niambie nifanye nini sasa?’ nikauliza kwa hamaki.

‘Kama nilivyokuambia mengine yasubirie, labda kama hutaki mume wako apone, na hakuna aliyefahamu kuwa kutokuzungumza kwake huko kunaweza kuwa na mahusiano na huyo rafiki yako, tumekuja kulifikiria hilo baadae, asubuhi, wakati mtu aliondoka usiku…’akasema

‘Na kuondoka kwake, ni wachache walifahamu, mimi  nimekuja kugundua nilipofika kwake asubuhi, na kuambiwa na jirani yake kuwa keshaondoka, nikauliza wapi, akasema amesafiri kwenda ulaya kusoma,....nikashangaa, mbona sikuwa makini na tarehe yake ya kuondoka, ina maana ulikuwa hujui anaondoka lini?’ akaniuliza.

‘Hapana kawahisha kuondoka, ilitakiwa akawie kidogo kwa ajili ya mtoto, sasa yeye akaamua kufuata tarehe ile ile ya awali,..tulikubaliana asubirie kidogo, na mimi nimekuwa kwenye wakati mgumu sikuwa makini kulifuatilia hilo…’nikasema

‘Basi yote hutokea ili iwe sababu, nahisi sasa utaweza kumuelewa rafiki yako ni mtu wa namna gani, kama aliyoyafanya kayafanya kwa makusudio yake mwenyewe…’akasema hivyo na kauli hiyo ikanifanya nisinyae kidogo.

‘Ok, labda,…ana sababu za kuwahi, basi angeliniambia.. ‘nikasema

‘Hapo moja kwa moja kila mtu atafahamu kuwa kuna sababu, na kuna jambo kati yake na mume wako, ..na sijui baba yako atasemaje kuhusu hilo…sasa ni wewe kupambana na hili jambo ili mumeo aweza kupona, huu ni mtihani kwako…akasema

‘Na wewe hujaongea naye, hata wewe hataki kuongea nawe…?’ nikamuuliza

‘Hata mimi ….hataki hata kuniangalia machoni…’akasema

‘Mimi siamini hilo, hata wewe rafiki yake, asiongee na wewe, akufiche mambo yake, usinitanie, nyie wawili, na sio wawili, nyie watatu, na huenda wa nne akawa mdogo wa mume wangu, nahisi nyie kuna jambo mumelifanya pamoja, na mnachokifanya ni kunizuga tu...mnanifanya mimi mtoto mdogo...’nikasema

‘Sijui kitu kwakweli, niamini hilo nakuambia zaidi ya shuku shuku tu ….’akasema

‘Mimi nawahakikishia kuwa nitaligundua hilo jambo mwenyewe, na ole wenu,...kama kuna jambo ambalo sio jema, sijui kama tutakuja kuongea, sitajali tena urafiki wetu, na huyo mume sijui,…’nikasema na kutulia.

‘Tatizo lako wewe unapenda kuchukulia mambo kihasira...na hilo ndilo litakufanya usijue mengi, na hata ukijua utakuwa hufaidiki nalo,utakuwa umeshachelewa....’akasema

‘Nimeshakuambia hivyo…’nikasema

‘Nikuambie ukweli, mimi nimejitahidi kadri ya uwezo wangu, nifahamu ni nini kinachoendelea kati ya mume wako na rafiki yako, sijaweza kukifahamu....nimejaribu kumhoji mdogo wa mume wako, .....lakini na yeye anaonekana hafahamu lolote...’akasema.

‘Mdogo wa mume wangu kasema hivyo, hafahamu kitu..?’ nikauliza kwa mshangao.

‘Ndio kama tulivyopanga, kuwa nitaongea naye, nimeongea naye, nimetumia kila mbinu, lakini inaonekana hilo jambo, ni kama tulivyo sisi anahisi hisi tu, hana uhakika, na yupo kama wewe, anamtetea sana kaka yake kuwa hawezi kufany ajambo kama hilo, …’akasema

‘Na hakukuambia kuwa zipo siku mume wangu  alilewa sana wakampeleka kwa rafiki yangu wakalala huko…?’ nikajikuta nimeongea kitu ambacho sikutakiwa kukiongea.

‘Kwahiyo kumbe unafahamu ….’akasema

‘Ilitokea, …akalewa, lakini nafahamu bado wangelilinda ndoa..’nikasema

‘Watu wamelewa chakari, wakumbuke kulinda ndoa…hapo unanificha jambo….’akasema


‘Kuondoka kwa rafiki yangu huyo bila kuniaga, kunanitia wasiwasi,..tangu siku ile nilipoongea naye, mara ya mwisho, kauli yake imekuwa kama ya kunidharau,kuna kauli zenye kujiamini zaidi, ....sasa sielewi, kuna nini kimemfanya awe hivyo....’nikasema.

‘Je kwa mtizamo wako hadi hivi sasa huwezi kuhisi kuwa huenda rafiki yako alikuwa na mahusiano ya siri na mume wako?’ akaniuliza na mimi nikamjibu kw haraka.

‘Kwa mantiki hiyo naona kuna dalili hizo, lakini nafsi na akili yangu bado ipo gizani, sawa nahisi hivyo..lakini ushahidi upo wapi, maana sitaki kuja kukosana na mume wangu wakati kweli hana kosa,..nielewe hapo, maana kama ni kweli …’hapo nikatulia.

‘Ndio sasa uanze kufunguka masikio, nimekuwa nikijaribu kukueleza uelewe, ila sikutaka kukushinikiza kwa hilo..nimefanya hivyo , isije ikawa sio kweli ukanichukia kabisa, ukafikiria labda nina nia mbaya na ndoa yako au na urafiki wenu, natumai sasa upo na mimi,unaanza kuamini hilo, japokuwa hakuna uhakika wa moja kwa moja au sio, na usikimbilie kwenye kuvunja ndoa yako, hilo usiafanye kabisa, unasikia…?’ akaniuliza.

‘Mimi nilikuwa nasubiria hiyio taarifa ya rafiki yangu, ndio niweze kuwa na maamuzi yangu, maamuzi yangu yapo moyoni, hata rafiki yangu halifahamu hilo, lakini yeye akaondoka kabla hajanikabidhi hiyo taarifa, maana yake ni nini…kanidharau, kwa vile kafahamu kuwa kanikosea, si ndio maana yake hiyo…sasa hiyo kazi  nitaifanya mimi mwenyewe ili nipate uhakika….’nikasema

‘Oh, nimekumbuka, kuna taarifa , alisema itakuwa ofisini kwako, mezani kwako, ukifika utaikuta, ila alimuambia katibu muhutasi wako asikusumbue, maana unaumwa, na ukijua kuwa taarifa hiyo ipo tayari haraka utakimbilia  ofisini badala ya kusubiria upone vyema…’akasema

‘Unasema…!!! Ina maana hiyo taarifa ipo tayari, hiyo kwangu ina muhimu sana inabidi ugeuze gari nifike ofisini kwanza, tafadhali geuza gari…’nikasema

‘Tushakaribia hospitalini hatuwezi kugeuza gari tena hapa…na hata hivyo tukifanya hivyo, tutakuwa tumechelewa , tutakuta muda wa kuona wagonjwa umekwisha,..labda kama hutaki kumuona mume wako leo, …’akasema

‘Oh….’nikaguna nikiangalia saa kumbe muda ulikuwa umekwenda sana

‘Unasemaje maana tumeshafika, je unaiona hiyo taarifa ni muhimu kuliko mume wako….’akasema sasa akiingia eneo la hospitalini...

*************
 Tulifika hospitalini, akili ikiwa imeshavurugwa,…hapa kwa upande mmoja natakiwa kuhakikisha mume wangu anapona, na ili hilo lifanikiwe, natakiwa nimeza machungu..nijifanye nipo sawa, lakini kwa upande mwingine baba ananishinikiza ili mume wangu aonekane mbaya, hafai hata kuongoza kampuni…na mpaka sasa nipo peke yangu, kwani mtu niliyekuwa nikimtegemea kwa kazi zangu nyingine ndio huyo kaondoka.

Nilitulia kimiya bila kusema neno, hadi tunakaribia kuingia chumba alicholazwa mume wangu, na hadi muda huo nilikuwa namuwazia huyo rafiki yangu, sikuwa bado nimemuwaza kwa mabaya, kwa chuki, badi nilikuwa nimempa nafasi..hapo nilikuwa nawazia tu huenda nimemtendea vibaya rafiki yangu huyo.., huenda nimemkosea ndio maana kafanya hivyo.

Hamuwezi kuamini jinsi gani nilikuwa nampenda huyo rafiki yangu, alikuwa ni kama ndugu yangu…na nilipofika hapo, nafsi ikaniuliza je ikiwa ni kweli katenda hayo yanayosemwa itakuwaje…oooh…kama ni kweli sijui kama nitaweza kuvumilia, sizani, na hata akimbie wapi…nitampata tu......atarudi, tutakutana au huko huko naweza kumtuma mtu..

‘Nilijitahidi sana nimuone mtoto wa rafiki yako, lakini mpaka anaondoka, sikubahatika kumuona sura yake....’akasema docta na kunisthua kutoka kwenye dimbwi la mawazo...

‘Sura ya mtoto wake ina umuhimu gani kwako…achana naye huyo bwana.., hana maana kabisa kwangu kaniuzi sana…’ nikasema.

‘Ingenisaidia kuwa na uhakika kuhusu baba wa huyo mtoto...yeye alijitahidi sana kufanya siri hiyo iwe siri…, dunia hii haina siri, wengi wameshaanza kuongea …sasa jiulize watu wamejuaje kuwa mtoto wake anafanana sana na watoto wako...’akasema.

‘Mhh, hata sijui …lakini hata hivyo hayo hayakuhusu au sio..labda uwe umetumwa na mtu fulani, na nafahamu kwanini unasema hivyo kuwa kama anafanana na watoto wangu basi mume wangu anahusika au sio..?’ nikamuuliza kimzaha.

‘Kwahiyo kumbe ni kweli, kuwa mtoto wake anafanana na watoto wako, nataka uhakika tu…?!’ akauliza kwaa mshangao.

‘Sijui mimi bwana, ....hata kama mtoto wake anafanana na watoto wangu, mbona watoto wakiwa wachanga wengi wanafafa tu, mimi hilo halinisumbui kichwa, na hata kama kanificha kumfahamu huyo bwana wake , mimi nitamfahamu kwa njia zangu nyingine...’nikasema

‘Ina maana wewe hujaamini hilo…’akasema

‘Nitaaminije hebu kaa kwenye nafasi yangu, jiulize ndugu yako anaweza kufanyakitu kama hicho, eeeh, sawa shuku kwenye nafsi zipo lakini nazishinda kwa kuweka hoja ya msingi, kuwa haiwezekani, yeye ni rafiki yangu, nimijitolea sana kwa ajili yake mpaka nimekosana na wazazi wake, hata huko kusoma ni juhudi zangu, je mtu kama huyo anaweza kunisaliti mimi…siamini..’nikasema

‘Mhh, hatujui lakini, hatujui, maana hata mume wako hajaliweka wazi hilo…’akasema

‘Mume wangu,…unajua mume wangu anamuheshimu sana huyo rafiki yangu, kuna kipindi aliniambia anavyomuheshimu anamuona kama mama mkwe…ndio uniambie mume wangu kafanya hivyo na rafiki yangu, hivi kweli inaingia akilini hapo, yaani siamini, siamini kabisa, hahaha, lakini lisemwalo lipo, na kama lipo, kutawaka moto, wewe subiria tu…..’nikasema.

‘Unajua ..kwanini nawashuku, sio tabia yangu kushuku watu ovyo vila vidhibiti…kama mtoto wake anafanana na watoto wako, ina maana mtoto wake anafanana na mume wako au sio, tunaangalia nadharia…’akasema

‘Mimi najua ipo siku tutathibitisha hili kivipimo, ila mimi nmefanya hivyo ili  lituame kwenye nafsi yako mapema, ili usije kulipokea kwa mshtuko baadae…, na nasema hivyo sio kwamba nafahamu kitu, unielewe hapo, hata mimi bado sijawa na uhakika ila nilidhania kuwa labda ni mipango yenu wawili, upendo wenu umefikia hapo..’ akasema na kauli hiyo ilinichefua, nikamwangalia bila kusema kitu, nikajitahdi kulimeza tu…nikajikuta nimesema hivi;

‘Pia anafanana na mdogo wa mume wangu, mbona hilo hulisemi....’nikasema.

‘Yawezekana pia… lakini  eeh, mdogo wa mume wako, angelianiambia, maana mengi yake ananiambia pia…alishaniambia jinsi gani alivyokuwa akimtaka huyo rafiki yako, na wakaishia kugombana, na tokea hapo wamekuwa hawaelewani , ni kusalimiana tu, sasa iweje leo,..lakini labda, kama alitaka mtoto na akaona haija jinsi amtumie yeey je..yawezekana pia…’ akasema.

‘Kama sio yeye, basi huyo ndugu yake mwingine…’nikasema

‘Kipindi kingi huyo ndugu yake mwingine amekuwa  hakai sana hapa Dar, ni mtu wa kutoka toka…na hana ukaribu sana na rafiki yako,…sizani kama anahusika hapo…, mtu wa kumshuku alikuwa huyu ambaye mara kwa mara wamekuwa yupo hapa ambaye hata mumeo akizidiwa ndiye humchukua kwenye gari kumrejesha nyumbani….’akasema.

‘Mhh..labda hiyo ripoti ya rafiki yangu itasema kila kitu….natamani nipae ili nifike ofisini nione alichoandika,…niliitarajia sana, hata hivyo kwanini, asingeliniletea nyumbani, sawa hamna shida kama hiyo ipo tayari, hamna shida, kazi yangu kaimaliza kwahiyo namuombea kila la heri…’nikasema

‘Kwahiyo upo radhi naye, umemsamehe….’akasema

‘Nani …? Huyo rafiki yangu…? Kumsamehe kwa lipi, maana ni sawa na hilo la mume wangu kuwa nimsamehe tu, hata kosa hulijui…’nikasema

‘Kama ni kweli,..’akasema docta

‘Ohh..,  kama ni kweli mnavyosema nyie, kama kweli anahusikana na ….na…ushetani huo, siwezi kumsamehe…katu…na..na.., hata mume wangu kwa hilo,…kama ni kweli, wote wawili kwangu watakuwa maadui… naomba, naombea sana isiwe ni kweli, maana, ohh…. nita-nita-ua mtu, wewe utaona tu…kwanini lakini, this is too much….’nikasema

Hapo docta akatulia, ..ukapita muda kidogo, halafu akasema;

‘Sasa tunaenda kukutana na mume wako, jaribu kukunjua sura yako, usije ukamuonyesha mumeo hiyo sura ya hasira, ukikunja uso wako hivyo, unakuwa kama unataka kuua mtu kweli.., mume wako akikuona hivyo anaweza kuhisi umefahamu ukweli wote...’akasema

‘Ukweli wote gani sasa, mpaka sasa sijafahamu kitu mimi, na nikifahamu,a kuthibitisha kuwa ni kweli,..hii sura itakuwa mara mbili, ok..ok..nahisi sipo vizuri....’ nikasema nikishika kichwa

‘Hebu tulia kidogo, vuta pumzi, eeeh, yes, fanya tena, haya tulia, unajisikiaje sasa…’akawa anafanyisha mazoezi ya kuvuta pumzi, nikajisikia sawa.

 Alipoona nipo tayari,  yeye akatoka kwa haraka kwenye gari na kuja kunifungulia mlango, nilisita kutoka , nikijipima kama kweli nipo tayari kukutana na mume wangu, na nikikutana naye, kweli nitaweza kujizuia.

‘Twende bwana, tumechelewa, hakikisha unaonyesha tabasamu,....usije ukamuonyesha mume wako  chuki yoyote na uwe makini kumjibu maswali kwa yake akikuuliza eeh…’akasema

‘Maswali!!…hamna shida…’nikasema

‘Kumbuka kupona kwake haraka inategemeana na wewe utakavyomtendea....kama hutaki mume wako apone haraka endelea kujenga sura ya chuki......utakuja kujilaumu mwenyewe, usije ukasema sikukukanya ...ni muhimu sana hili, mengine yapumzishe kwanza....’akasema .

‘Sawa docta…’nikasema na mara simu yangu ikaita,..nilipoangalia nikaona ni baba ananipigia….

NB: Niendelee....


WAZO LA LEO: Wengi wetu tunafurahi kutendewa mema, kujali nafsi zetu kwanza na hasa tukiwa na shida, mara nyingi tunamuona mtenda wema huo ni mwema sana, hata kama kutenda kwake huko kunamgharimu.  Lakini pindi ikatokea kuwa wema huo, au kutendewa huo hakupo tena, ni aghalabu kukubali ukweli kuwa na mwenzako anastahiki kutendewa hivyo-hivyo, huenda naye kakwama na yeye  anastahiki kutendewa.  Tujitahidi sana kulipa wema kwa jema, ili baraka ziongezeke, na maisha ya kupendana yazidi kuwepo.
Ni mimi: emu-three

No comments :