Baada
ya majadiliano kidogo, mama akaona nipewe nafasi hiyo, mimi nikae faragha na
huyo mzee, lakini sehemu ambayo naweza kuonekana ili kama akileta vurugu niweze
kusaidiwa, Nilimuangalia yule mzee, , kwasasa akawa anaona aibu hata
kuniangalia, sio kama ile awali, ni kama kabadilia, na kule kuona aibu hataki
kuniangalia moja kwa moja usoni, kukanifanya nishindwe kumtambua vyema.
‘Haya
wewe unaweza kuwepo , maana kwa hivi sasa huyu ni binti yako, au sio, sitaki
nikae naye faragha tukiwa wawili tu, walimwengu ni wengi wa kuzusha, naogopa
sana kwa sasa…” akasema huyo jamaa sasa akiongea vyema sio kama ilivyokuwa
awali, ni kama vile mtu anaigiza, kuongea kwake kwasasa sio kama awali
alivyokuja akia kama kachanganyikiwa, kama isingelikuwa hayo mavazi na
muonekano wake, usingemfikiria vibaya.
‘Sawa
lakini unaona bado tuna kazi za usafi, maana sisi, siku nzima huwa ni kazi tu, na
kazi zetu usafi ni kitu muhimu sana, na wewe sasa unatukwamisha, tumekuheshimu
tu kwa vile wewe ni mteja wetu mnzuri…’akasema mama.
‘Mimi
nitawalipa siku hii nzima, nipo tayari kwa hilo, nipigieni hesabu zenu,….,
msijali, hamuwezi kupata hasara kwasababu yangu, najua haya ni kwa masilahi yangu…samahanini
sana..’akasema akashika kifuani.
‘Pesa
utapatia wapi wewe mzee, au unaomba omba
mitaani..?’ huyo mama akamuuliza kwa utani na huyo mzee, hakukasirika akasema
kwa uzuri tu
‘Pesa
sio shida kwangu mama Ntilie,…usinione hivi…’akasema akijikagua huku akitikisa
kichwa kwa kusikitika.
‘Ukisikia
historia yangu utanionea huruma,…hadi nimefikia hii leo naweza kuongea na wewe
hivi, namshukuru sana mungu na wanaonifahamu wakiniona hivi naongea na wewe
hivi hawataweza kuamini..unajua huko nilipotoka niliondoka siku nyingi hawajui
wapi nilipo…’akasema
‘Wapi
umetokea…?’ akaulizwa
‘Huko
kwa mke wangu…nilitoka siku moja saa kumi alfajiri nikapotea, hawajui wapi
nilipo, niliwahi kuona tangazo,…kwenye gazeti, wakati akili inakuja na kupotea,
kuwa natafutwa,..lakini kwa hasira nikalichana lile gazeti, walipiga kipindi
sina midevu hii…’akasema.
‘Sasa
kwanin hunyoi…?’ akaulizwa.
‘Ningelinyoa
kama nilikuwa najitambua..sijui…kiukweli nahisi nilikuwa sijijui,..unajua hivi
sasa nahisi ni mtu mwingine kabisa…’akasema.
‘Kwani
tatizo lako ni nini…?’ akaulizwa.
‘Tatizo
langu,!!! ..labda akija mke wangu atawaambia..yeye unajua, tatizo langu
limeanzia wapi, ila hajui jinsi ya kunisaidia, mimi nilishajua lakini jinni gani
ya kumuelezea ikawa ni vgumu sana ..’akashika kichwa
‘Unajua
nikuambieni kitu,..hata kwenye njozi, nahisi hivyo, ni kuwa niliwakosea watu
wengi sana, na hilo ndio tatizo langu, hakuna zaidi…mengine sawa yawezekana
yapo,…ila nahisi , ni hayo niliyowafanyia watu , na ninayemkumbuka kwa haraka
ni huyu binti, hasa nilipomuona ndio nikakumbuka,…’akaniangalia kwa aibu.
‘Nilipomuona
tu nikamtambua, najua yeye ndiye nimemkosea sana, mke wangu nilimkosea lakini
yeye alishasema kanisamehe, iliyobakia ni huyu..najua ni huyu tu…baada ya tendo
hilo la kunisamehe..akakiri moyoni na vitendoni, nina imani mola
anatanirejeshea hali yangu, na kila mara nilikuwa naiota hiyo ndoto na
nikionywa kuwa, nispofanya haraka sitapona tena, na tumuwahi kabla hajapata
matatizo zaidi ….’akasema.
‘Kwenye
ndoto ndio unaota hivyo, sio kwa waganga wa kienyeji..?’ akaulizwa.
‘Mimi
siwajui waganga wa kienyeji, sio kwamba sijawahi kwenda, nakumbuka mke wangu
alinipeleka huko kwenye kunihagaikia…lakini nikaja kumtoroka, unajua hata
kutoroka kwangu asubuhi siku hiyo sababu kubwa ni hiyo, walipanga wanipeleke
kwa mganga wa kienyeji, kuna rafiki yake mke wangu alikuja akamshauri hivyo,
mimi alifajiri hakujapambazuka, nikatoroka mapaka leo ndio wanapata taarifa
zangu..’akasema.
‘Sasa
kwanini ukatoroka ukijua kuwa wenzako wanakuhangaikia wewe, ili uje kupona…?’
akaulizwa.
‘Mimi
sijui kwanini nilifanya hivyo…, ila kuna kitu kiliniambia toroka, huko wanakotaka
kukupeleka hutapona, watazidi kukuharibu, dawa ya maradhi yako sio hiyo, dawa
ya maradhi yako ni makosa yako mwenyewe, …’akatulia
‘Nikijaribu
kuuliza ni makosa gani nimeyafanya, basi nikijiuliza hivyo kuna watu , kelele
za watu wanalia, …wakuja kunililia, nimewakosea,..sasa kwa vipi ni nani, siwaoni
, sioni ..unajua, kichwani tu kelele za vilio, nikisikia hivyo nakiambia,
nikijaribu kuzikimbia hizo kelele, lakini wapi, kwahiyo nimekimbia wee…mpaka
wapi huko, …nilikwenda mbali sana..’akasema
‘Sasa
huku uliwezaje kurudi….?’ Akaulizwa
‘Hata
sijui, nimekua nikitembea , huku na
kule, nalala maporini, majalalani, lakini siachi kumkumbuka mungu, mimi
sijawahi kusoma dini, nahisi hili ndio kosa kubwa sana, kama ningelikuwa
nimesoma dini, huenda matatizo haya yasingelitokea, nimesoma masomo ya kawaida,
nimesoma sana usinione hivi, hadi chuo kikuu…’akasema
‘Wewe…?’
mama akauliza kwa mzaha
‘Ndio,
huamini…’akasema
‘Sawa
nikiamini aikuamini, haitasiaida kitu, muhimu ni mtu mwingine aje
kututhibtishia,…’akasema huyo mama
‘Sasa
uliambiwa ni makosa yako, hukuambiwa ufanye nini, utubu au ufanya nini…?’
akaulizwa
‘Unajua
hali hiyo ya kuchanganyikiwa, inakuja
tu, na kupotea, kuna muda nakumbuka kumbuka mambo kuna muda hali inakuwa mbaya,
wakati mwingine nahisi kama nipo kwenye njozi, ni kweli kuna muda, niliwahi
kuulizia, nitafanyaje kuhusu hayo makosa, sikumbuki jibu, lakin….ikaja hiyo
hali kuwa nitubu , kama ni makosa unatakiwaje ufanye nini, ni kutubu au sio ,
sasa kwa nani….’akatulia
‘Kwahiyo
ukafanyaje hadi ukafika huku…?’ akaulizwa
‘Kufika
huku labda niseme ni miujiza ya mungu,..sasa haivi kidogo nimeanza kukumbuka
nipo wapi, na kutoka hapa ninaweza hata kwenda nyumbani kwangu, ni mbali kidogo
na hapa, ….lakini nitafika tu….’akasema
‘Ni mke
wako unamkumbuka sasa kwa jina wapi alipo, au sio…?’ akaulizwa hapo akakaa
kimia kidogo, halafu akasema;
‘Unajua
bado, kichwani hakujakaa sawa kabisa, maana sijariskika, nahisi ..lakini
nishapona, najua kwa haya mateso, niliyopata nia dhabu tosha, sikuwahi
kuambiwa, nifanye nini, ila nahsi hivi ndivyo sahihi, ila jamani nilikuwa
nateseka, kichwani kunakuja mambo mengi hili na lile..yaani nikikaa hivi ni
kama kuna watu elifu wanaongea kwa pamoja kichwani, wengine wanalia, wengine
wanapiga makelele..yaani we acha tu…’akasema
‘Pole
sana, mungu atakujalia, utapona kabisa, mimi nimeshakusamehe japokuwa sijui
kosa ulilonifanyia ni lipi, maana sijawahi kukutana na wewe, sikukumbuki kabisa…’nikasema
na yeye akaniangalia kwa makini nikaona kama machozi yakimtoka, kiukweli
nilimuonea huruma nikasema;
‘Usilie
baba yangu, wengi tupo hivyo, tunapitia matatizo, maisha magumu, na ukifikiria
sana, unaishia kulia, na hasa ukigundua kuwa wenzako huenda …lakini sitaki
niongee zaidia, mimi namuomba mungu kama kuna ulilonifanyia mimi, hata nisipolijua
akusamehe tu, ..sina kinyongo na wewe…’nikasema.
‘Mungu
wangu…hata sijui niseme nini…’akasema.
‘Huna
haja ya kujiumiza mzee…bint huyu ni mwema, sana, katika misha yangu ya
kuhangaika sijawahi kukutana na binti kama huyu , mwenye adabu, anajua kuishi
na watu, muaminifu, ..huwezi kuamini, hata kuonja mboga jikoni mpaka aniombe
ruhusa, niliona ni mtu wa ajabu sana…’akasema huyo mama.
‘Namfahamu
sana…’akasema huyo mzee.
‘Unamfahamu
kwa vipi, unajua unatuweka kwenye mtihani mpaka watu wanatufikiria vibaya
wanafikia kuhisi labda, ni wewe ndiye
ulimpa huyu binti hiyo mimba..japokuwa tunajua sio kweli au sio…?’ akaulizwa na
hapo akanitizama tumboni, kwa uso wa huruma, akasema;
‘Ana
mimba, masikini…sikujua hilo…’akasema sasa akinitizama tumboni.
‘Wewe
si unasema unamfahamu, mbona hujui kuwa ana mimba..?’ akaulizwa.
‘Mimi
hilo sijui….ooh, yaani labda ..lakini mim isijui kabisa, nisamehe sana …sitaki
niongee zaidi hapa, nataka tuongee ukiwa huru…’akasema.
‘Kwahiyo
hiyo mimba sio ya kwako..’akasema huyo mama kwa utani.
‘Wewe
mama wewe, huko sasa…hapana, …’akasema akiona aibu
‘Niambie
ukweli, kama ni wewe ulimbaka au wewe ni baba yake, tuambie maana hata yeye
hakufahamu kabisa isije ukawa ni tapeli fulani una mambi yako…?’ mama akauliza
hivyo na jamaa akatoa jicho la kushangaa na kusema.
'Ni
hadithi ndefu, na kiukweli hivi unavyoniona na hali niliyo nay oleo ina
afadhali, nashangaa hata mimi, najikuta nipo hivi, ile hali ya awali imenitoka,
na kama mtu kanivua kofia, kofia niliyoizoea, na kuniacha kichwa, nahisi nipo
mtu mwingine kabisa…’akasema.
‘Sijakuelewa…’mama
akasema.
‘Wakati
nipo hapo nje, nililia sana, namlilia mola, kuwa nimempata mmojawapo, basi anisaidie
huyu niliyempata anisamahe…najua huyu nilimkosea, najua kwa hayo makosa
alishawahi kuinua mikono juu na kumlilia yeye, sasa nimeyaona madhambi yangu,
anisaidie huyu mtu anisamehe…nililia mpaka macho yanauma.
Kuna
muda nikahisi kama kausingizi… mara
nikahsi kitu kikipiga kichwa, taa..nikasikia nziiiiiii..hujawahi kuhisi hivyo
kichwani, mara nikajihisi kama nimetoka usingizi,…naanza kuona watu vyema,
nahisi vyema, ..na nilipojiangalia nilivyo nikashtuka, kwanini nimekuwa hivi,
unajua nilisimama najikagua kwa muda nikashikwa kichwa manywele mengi, midevu,
ohhh, sikuamini, hivi mimi ni nani , na kwanini imekuwa hivi, nikaanza sasa
kutafkari, kukumbuka imechukau muda, lakini naanza kukumbuka,…’akasema.
‘Mungu
mkubwa, kwahiyo kule kuchanganyikiwa ndio kumeondoka hivyo, nahisi mola mwingi
wa rehema kasikia kilio chako,…’akaambiwa.
‘Lakini
sijaamini mpaka nisikie kauli ya huyu mdada, najua kanisamehe moyoni ndio maana
ikatokea hivyo, natamani niskie kauli yake kuwa keshanisamehe zaidi ya hapo,
katamka na kutamka, lakini bado,ni mpaka asikia kuwa mimi nani nilimfanya nini
, hilo la mimba mimi sijui, …, najua siwezi kumlipa kwa hayo niliyomtendea,
lakini…mungu anajua jinsi gani nilivyoteseka, muulizeni mke wangu atawaambia
ukweli..’akasema
‘Sasa
mke wako tutamjuaje sisi, maana unasema mke wako mke wako, hutaki hata
kututajia jina lake…’akasema huyo mama.
‘Atakuja,…naomba
simu yako mara moja…’akasema, na huyo mama kwanza akasita kidogo, jamaa akasema
‘Usiwe
na wasiwasi nimekumbuka namba ya mke wangu, nilikuwa najaribu kuiwazia, sasa
nahis ndio hiyo, nipe nimpigie, au wewe nikutajia umpigie kama una mashaka na
mimi…’akasema na huyo akampa huyo jamaa simu,
Jamaa
akaanza kubofya hizo namba na kuweka simu sikioni, akasikiliza kwa muda mara,
haloo
Ni
mimi mume wako…’akasema
‘Ni
kweli ni mimi, umenisahau hata sauti yangu jamani…’akasema
‘Nipo..nipo..hapa
ni wapi…?’ akauliza huyo mama, huyo mama akasema
‘Nipe
hiyo simu nimuelekeze…’akasema na kupewa akaongea na huyo mke wa jamaa ana
kumuelekeza wapi walipo na huko wakasema wanakuja.
‘Wanasema
wanakuja, sijui nani na nani…’akasema mama
‘Oh,
mungu mkubwa, …’jamaa akasema huku anafuta machozi,
‘Unajua
niwaambie kitu, bila ya mke wangu kuwepo hapa hili zoezi halitakamlika, nataka
aje ashuhudulie kuwa mimi sio yule tena, mimi ni nani, na nilimkosea nini huyu
binti, yeye anajua zaidi yangu…kiukweli namuonea huruma sana mke
wangu,..kateseka kwa ajili yangu mpaka ikafika sasa hana jinsi, unajua huwezi
kujua ugumu wa jambo mpaka uwe nalo, kuishi na mtu aliyechanganyikiwa ndani ya
nyumba, ni mtihani…’akasema
‘Oh,
pole sana, sasa…mimi naona utupe muda, sitaki kukukatili na kwa vile umesema
mke wako anakuja na ni bora awepo, unaonaje ukatupa muda, tumalizie hizi kazi
au sio,…’akaambiwa
‘Sawa,
…sasa hivi nahisi nipo binadamu, najua moyoni keshanisamehe ndio maana imekuwa
hivyo, …nitawasaidia kazi, ngoja, nipeleke huu uchafu nje…’akasema na kuanza
kusaidia kazi za hapo.
Haikupita muda mara ukaingia ugeni, muda huo
tulikuwa tunapanga panga vitu, na kwa vile siku hiyo hatukuwa na kazi za
mapishi zaidi, tulikuwa tunafungasha fungasha, na ndio tukaona ugeni wa watu wa
dini, wakiwa na mavazi yao, walikuwa kundi, mpaka tukashangaa, kuna nini leo.
‘Salamu
salamu, amani iwe juu yenu nyote, hamjambo jamani…,’ mmoja wapo akasalamia na
mama alikuwa kwa ndani akatoka nje kukutana na ujumbe huo, mimi kwa muda huo
nilikuwa namalizia kazi na yule mjamaa alikuwa kapewa kiti kakaa pembeni na
muda mwingi alikuwa akinitupia jicho, sasa hivi anafanya kwa kujiiba sio kama
asubuhi alikuwa akinitizama , najisikia vibaya sijui kwanini, na hali hiyo inanifanya nasikia hata kutapika.
‘Sijui
kwanini nilikuwa nikimuangalia nahisi hivyo, hadi nilipotapika, ..na baadae
nikamuomba munu kama kuna kitu kanikosea basi amsamehe tu mja wake, maana ni
mtu mnzima, hastahili kuadhibiwa hivyo, kiukweli nilimuomba sana mungu
amsamehe, sasa sijui nilivyoomba hivyo ina mahusiano na hicho kilichotokea
anayejua ni mungu pekee.
*************
‘Jamani
wapendwa, mtusamahe kwa kuja bila taarifa kwa siku ya leo, ila taarifa mlikuwa nayo kabla , hatukuwa na jinsi, nyingine ila nikuja hivi hivi,...natumai
mliwahi kuongea na kiongozi wetu mmoja, kuwa atakuja kuwatembelea baada ya
wiki,..yeye kapatwa na dharura hakuweza kufika..., lakini hatukuona haja ya kutokufika kwa sisi,
maana viongozi wengine wapo, ndio sisi …’akasema mmoja wapo.
‘Nakumbuka
ndio…’akasema huyo mama
‘Basi
baadhi yetu hapa tumetokea huko kijijini, kama alivyokuambia huyo mzee awali,
na katika harakati zetu za kutangaza dini ya mwenyezimungu tukapungukiwa na
sehemu ya ibada, huko kijijini kwetu …na katika kuhangaika ndio tukagundua eneo
linalofaa, lipo sehemu nzuri tu, tukataka kulinunua, lakini mwenyewe akawa hayupo…’akasema.
'Mwenye eneo hilo alifahamika, eneo hilo lilikuwa la mama mmoja alikuwa akiishi na binti yake, anafahamika sana kipindi hicho cha uhai wake...'akatulia kidogo
'Sasa kuna mambo yalitokea, unajua huko vijijini kuna mambo yanakua kwa haraka, imani hizi za kishirikina, kuna mambo mengine vijana wanakuwa hawana kazi, basi yanazuka mambo mengi tu, na baya zaidi, watu wanauwana ovyo, ukiuliza sababu ya msingi hakuna, imani ya kumuogopa mungu haipo tena..
'Kwa vile watu wanalifahamu hilo eneo ni la nani, ikabidi sisi tuhangaike, ujue, kuna watu walilivamia awali,lakini hawakuweza hata kujenga, wakapata misuko suko, wakakimbia na kuliacha, wakaja wengine hivyo hivyo, mwishowe likaachwa kama lilivyo, ndio sisi sasa tukaingiwa na hamasa nalo,...'akatulia
‘Kiongozi
wetu akafanya juhudi kubwa kutembelea huku Dar, nia na lengo ni kumpata mumiliki halali wa eneo hilo, maana tulisikia mrithi huyo ni binti wa marehemu huyu mama..., na alichukuliwa huku dar, kuja kufanya kazi za ndani,
..tunasema mrithi maana mama aliyekuwa akilimiliki eneo hilo si ndio kalifariki, watu
wahuni walimfanyia kitu kibaya sana, mungu awasahemeh tu, hao watu maana nasikia nao wao wamekumbwa na matatizo makubwa, mungu huwalipa watu hapa duniani, tumuogope sana mungu…’akatulia.
‘Sasa
nyie mlikuwa wapi mpaka hali hiyo inatokea, nyie si ndio wazee wa huko, tena watu wa dini…?’ wakaulizwa
‘Unajua
sisi tuna nafasi yetu kama viongozi wa dini, kazi yetu ni kutoa imani kwa watu,
na kazi ya ulinzi ni ya serikali, tumejitahidi sana kwa upande wetu, lakini
vijana hawataki kuingia kwenye nyumba za ibada, tukiwafuata mitaani, inakuwa
kero kwa wengine, na baya zaidi ila hali ya watu kuamini mambo ya ushirikina
imeshika kasi, ni kama watu wtunarudi ujingani, hili ni tatizo kubwa sana,….’akasema.
‘Ni
vyema watu kama nyie mkiwepo…, tunashukuru kwa hilo, kwahiyo mnasemaje sasa….?’
Akaulizwa
‘Sasa
tulielekezwa hapa na huyo kiongozi wetu, kuwa kuna binti kasema anaishi na
wewe, na huenda akawa ndiye huyo tunayemtafuta, kama yupo tumuone, kama ni yeye
basi tutapanga siku ya kuja, kama hamna nafasi leo, au kama mna nafasi leo
mungu ni mwenye neema, zake, tunaweza kuongea naye, mungu akipenda…’akasema.
‘Mhh,
kiwezekanacho leo hakiwezi kusubiria, lakini nashangaa leo napata ugeni na wote
mnataa kuongea na binti yangu, kuna ugeni mwingine nao unataka kuongea na
binti, hatujajua wana nini, sasa nyie tena…’akasema huyo mama.
‘Lakini
taarifa zetu ulizipata mapema au sio, isije kuja kuazima jamvi akaja mwingine
kutaka kuliwahi, sisi tulishakuaambia na eneo hilo sisi tulisha…’kabla
hajamaliza mama akasema.
‘Wao
hawahitajii hilo eneo nijuavyo mimi, wana yao mengine kabisa, …sasa kwa vile
hao wengine hawajakamilika, basi ngoja nimuite binti, aje mumuone kwanza isije
ikawa sio yeye, nafikiri mkitambulishana itakuwa ni vyema zaidi, au sio…’akasema
huyo mama.
‘Hewala
hilo neno, …’wakasema na mimi nikaitwa kuja kuonana na huo ujumbe.
Nilitoka
nikiwa nimevaa kiheshima, na kiukweli mimi kawaida yangu ni hivyo, huwezi
kuniona nimevaa kinyume na maadili yetu, na nilipotoka kuna wazee wawili
wakatikisa kichwa kama kukubali, na wengine walibakia kimia.tu wakiniangalia.
Nikawasalimia
kama ada, na wao wakaniitikia, na yule kiongozi wao akaniuliza jina na natokea
wapi, nikawaelezea jina na jina la mama na natokea wapi, wakasema;
‘Oh
mungu mkubwa hatimaye tumekupata..ndio wewe hasa, unafanana sana na marehemu
mama yako…’akasema huyo kiongozi wao,
‘Ndio
huyu sio..?’ akauliza huyo mama
‘Ndio
yeye, bila shaka…’wakasema
‘Sasa
muelezeni shida yenu..’akasema huyo mama, na watu wale wakaelezea shida yao, na
jinsi gani walivyojpanga, na wapo tayari kunilipa pesa ya eneo hilo, wao
walikadria kutokana na bei za huko kijijini, zinajulikana, basi mimi nikawa
sina la kusema maana nilichokuwa nikihitajia ndio hicho, kwasababu sikutarajia
kabisa.
‘Wazee
wangu, nawashukuruni sana, maana sikitarajia hilo, mimi nilijua eneo hilo
limeshachukuliwa,. Na nilikuwa naogopa kabisa kurudi huko nikijua yatanipata
kama yaliyompata mama, na ujio wenu
umenipa faraja kuwa angalau wapo watu wema katika hii dunia, nimepitia machungu
mengi sana, sitaki kuelezea, lakini siku zote kama alivyoniusia mama yangu,
alinitaka nisikate tamaa na niwe na mtegemea mungu , kwani mungu pake yake
ndiye, ataniondolea mizigo hii ya mitihani..’nikasema.
‘Sawa kabisa,
imani imekuiba binti, endelea hivyo hivyo utafanikiwa hapa duniani na kesho
siku ya kiamana,…kwahiyo sasa eeh, umekubaliana na kiwango hicho.au.?’
nikaulizwa.
‘Mimi
sina zaidi,kama mumeona ni kiwango halali kwa hilo eneo, basi nimeridhia, nyie
ndio mnajua na nyie ndio mumelipima,hilo eneo, mimi yote namtegemea mungu tu ni
neema zake hizo..’nikasema.
Basi
utaratbu wa nyaraka ukapita, na nikaambiwa kwanza nifunguliwe akaunti ya benki,
tutasaidiana na wao, na malipo
yatafanyika huko huko benki, ili hizo pesa ziwe salama na niwe nachukua kwa
awalmu nikihitajia, tukakubaliana hivyo, ikabakia sehemu ya kuweka sahihi na
kupitia sehemu zote za serikali zinazostahiki ili isije kutokea migogoro
baadae, nikawa sasa na mimi tajiri, nilijihisi hivyo moyoni.
*************
Ugeni
ule baadae ukaondoka, ikabakia kesho waje tuongozane kwenda banki kukamilisha
mipango yote iliyobakia, na walipoondoka, mara ukaja ugeni mwingine , gari likasimama
nje, …na tukasikia hodi, baada ya muda,
Wa
kwanza kutoka nje alikuwa yule mzee, akasema.
‘Huyo anaweza
akawa ni mke wangu…’akasema akiwa na
furaha sana usoni.
NB
inatosha kwa leo…nipo kwenye mitihani fulani hivi, lakini nimeona nisiache siki
ipite hivi hivi
WAZO LA LEO: Tusichoke kumuomba mola wetu, kwani
mola ni mwingi wa rehema anajua ni lini atatutimizia matakwa yetu kwa wakati gani.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment