Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, August 1, 2017

DUWA LA KUKU....26


Tuligeuka kuangalia kule mlangoni, mioyo ikitudunda, ni kwanini mlango ukagongwa kwa fujo, kama ni docta anajua jinsi gani y akuufungua nlango wake...sasa ni nani huyo, ni maulizo ya sekunde kadhaaa kabla mlango hauajafunguliwa,

Lakini tendo hilo la kutaka kufunguliwa lilitaka kuzuiwa na sauti ya nguvu huku kwa mgonjwa, akisema  usifungue,..ni vitendo vilivyotokea kwa muda mfupi sana, na kitendo cha usifungue kilikuwa kimechelewa, kwani mama yule aliyekwenda kufungu amlango alikuwa ameshakinyonga kitasa cha mlango ili mlango uweze kufunguka.

Na huyo aliyekuwa huko nje, akawa keshausukuma mlango, na  kwa haraka akaingia ndani, na kitendo kile cha yeye kuingia ndani kwa haraka kikasindikizwa na mlio mwingine kwa mgonjwa, akigugumia kwa maumivu,

'Aaagh,....Aaagh....'halafu kukawa kimia

Tuendelee na kisa chetu

*******************

‘Nimesikia yote uliyokuwa ukiyasema, kumbe kweli wewe ulishiriki katika kumuua, mwanangu..’ Ilikuwa sauti ya mwanamama aliyeingia

Alikuwa mama mtu mnzima, kama sio kwa uchakavu wa maisha magumu, basi huyu mama atakuwa mtu mnzima, pamoja na hali hiyo, mwili wake ulionekana shupavu, na alipoingia, aliingia kwa kasi, akitembea pale alipokuwa kakaa mgonjwa.

Ujue vitendo hivi vilitokea kwa muda mfupi, kiasi kwamba, hakuna aliyekuwa na wazo la kumzuia huyo mama, kwani ile akili inaanza kufanya kazi, kua tufanyeje, huyo mama alikuwa tayari keshafika pale alipokaa mgonjwa na kumvamia,huyo 

Na kwa vile yule mgonjwa alikuwa kakaa kwenye kiti, na uzito wa huyo mama,  basi wote wakaporomoka chini sakafuni, mama juu, mgonjwa chini...sasa ikawa  ni kazi ya kuamulia,...lakini unaamulia nini sasa, kwani, cha ajabu kabisa,wakati huyu mama anaondolewa kwa huyo jamaa, jamaa alionekana kutulia tu.. , hakufanya juhudi yoyote ya kujitetea, au kuinu amkono wake,..japokuwa macho yalionekana kuwa na uhai yakipepesa na machozi yalikuwa yakimtoka. Yule mama akaachanishwa na huyu jamaa, na  huyu mama akawekwa pembeni, jamaa alikuwa kalala chini, hatikisiki.


‘Mhh, jamani muiteni docta…’aliyesema  hivi sasa alikuwa yule mama aliyekuwa akiiuliza maswali,..huyu mama cha ajabu yeye alikuwa karibu na hao mabondia wawili lakini yeye hakushughulika kabisa kuamualia, alikuwa kasimama kimia akiangalia hilo tukio, mimi niliingiwa na mawazo ni kwanini, nikahisi kuna jambo,...

Na hata kabla mtu hajaenda kumuita  docta, mara docta akaingia, na kwa haraka  docta akaenda pale alipokuwa kalala huyo jamaa  sakafuni, akamuweke vizuri, akawa anahangaika kumpa huduma ya kwanza.

Madocta wengine wakaja na vifaa, sisi tukaambiwa tutoke humo ndani, na yule mama aliyemvamia huyo jamaa sasa akawa kashika kichwa, hasa pale tulipotoka nje, na akaanza kwa kusema;

‘Sijui nimeua…, hata kama nimeua ni bora tu, kwanini yeye alimuaa mtoto wangu, kaua wangapi, muacheni nay eye afe…’huyo mama akasema.

‘Wewe mama kwanini umeingia bila sisi kukuita, unaona sasa umeharibu kila kitu,…’alianza kulaumiwa huyo mama, na haikupita muda tukaona kitanda maalumu kikingizwa humo ndani na baadae kikatolewa, jamaa akiwa kalazwa humo, na chupa ya kuongeza maji mwilini ikiwa inaning'inia .

Tukawa hapo nje tunasubiria, tuliambiwa tusiondoke kwanza, na haikupita muda, akaja askari, huyo alikuwa mlinzi wa hapo hospitalini, akawa anamlaumu huyo mama, kwanini aliingia huko ndani bila kibali chake, sijui huyo mama aliingiaje ndani …lakini yawezekana,  maana ilikuwa ni muda wa kuona wagonjwa,  kwahiyo huyo mama alitumia mwanya huo na kuja kuingia chumba hiki cha docta.

‘Huyu mama tulimuhitaji sisi, kwa ajili ya kutoa ushahidi, kuna tatizo lilimuhusu  mgonjwa, na mtu wake wa karibu anayemfahamu vyema ni huyu mama, kama ni lawama utulaumu sisi…’akaambiwa.

‘Lakini hakuruhusiwa kuingia chumba hicho cha docta, mimi nalaumiwa kwa hilo, hamjui , ni kosa kubwa sana limetokea linaweza kugharimi kibarua changu…’akasema huyo mlinzi.

‘Basi wanaokulaumu waelekeze kwetu, sisi tupo tayari kukutetea kuwa ni sisi tuliomuita huyo mama kwa dharura, sawa…’akaambiwa na yule mama muuliza maswali. Yule mlinzi akamuangalia huyo mama , huku akionekana kuwa na wasiwasi, yaonekana  alikuwa kafokewa na wakubwa zake, na hapo alipo ana wasiwasi na ajira yake.

Baadae docta akaja, na kutuambia…

‘Mgonjwa kapoteza fahamu…hata baada ya juhudi zote tulizofanya, jamaa hajaweza kuzindukana, inavyoonekana mgonjwa alipatwa na mshtuko mkubwa, sijui ni kitu, ilikuwaje wakati mpo naye…?’ akauliza, ikabidi aambiwe ilivyokuwa, lakini hawakusema kuwa huyo mama alimvamia huyo mgonjwa

‘Ok, bado tunahangaika naye, ngoja tuone itakavyokuwa, …ni nani ndugu yake wa karibu…?’ akauliza.

‘Huyu hapa, …?’ akaambiwa, na huyo mama, akaambiwa amfuate docta, na kabla hajaondoka na docta, yule mama muuliza maswali,akamshika huyo mama mkono, na kumnong’oneza kitu masikioni, docta hakuona kwani yeye alishaanza kuondoka.

‘Sawa nimekuelewa…’yule mama akasema na kumfuata huyo docta.

*****************

‘Hili sasa ni balaa…’akasema mama mmojawapo katika wale mama.

‘Ulimuona mgonjwa alivyokuwa, kulikuwa na damu mdomoni..mliiona hiyo damu...’akasema mwingine.

‘Mimi niliiona hata puani kulikuwa na damu…’mimi nikasema.

‘Ina maana huyo mama alimvyomvamia, alimpiga puani, mimi sikuona akiinua mkono kumpiga, tulimuwahi kabala hajaanza kumpiga…’akasema mama huyo mwingine. halafu wewe ulikuwa karibu hukuahangaika kuwatenganisha..'akasema huyo mama

‘Oh..hiyo ni dalili mbaya kwa mtu mwenye shinikizo la damu…nahisi ni kiharusi hicho…’akasema yule mama mwingine aliyeonakana kufahamu mambo ya udakitari.

‘Ngojeni tusubiria maama ni ajabu kabisa, mimi najiuliza kwanini alisema `usifungue’  kwa nguvu, kama vile alijua ni nani anakuja, hata hivyo, kama ni mkewe kwanini asema hivyo…?’ akauliza huyu mama aliyekuwa muuliza swali, hakujibu swali la kwanza aliloulizwa ni kwanini yeye hakuwaamulia wakati alikuwa karibu nao.

Baadae yule mama mtalaka, akarudi, na usoni alionekana na huzuni, akatusogelea na kusema;

‘Mhh, jamaa, yupo kwenye hali mbaya, hajazindukana, na docta naona kama ni hataki kusema tu, sizani, kama huyo jamaa atainuka, lakini wanasema bado wanajitahidi, mimi namfahamu sana huyu jamaa ana roho ya paka anaweza akainuka mkashangaa…’akasema.

‘Ndicho walichokuitia  hicho, au kuna jambo jingine wamekuambia.?’ akaulizwa.

‘Ndio hicho, ila wameniuliza maswali mengi kumuhusu mgonjwa, kutaka kujua historia yake kabla,…waliambia, mshtuko huo, umesababisha mwili kupooza, na inavyoonekana kuna damu imeingia kwenye ubongo, na sasa hivi wanasubiria vipimo walivyomchukua, kuna gharama kubwa zinahitajika kuchangia...'akasema

'Ok, hilo la gharama usijali, tutalifanikisha,...'wale akina mama wakasema.

'Kwahiyo docta akakushauri nini,...?' akaulizwa

'Alisema tuendee kusubiria, lakini mimi nikamuuliza, ina maana kwa hali kama hiyo jamaa hataweza kuinuka tena, na docta akasema;

‘Subiria vipimo, na mengine nitakujulisha baadae, …’akasema akiigiza sauti ya kiume

‘Ok, sawa, sasa usije kuchanganyikiwa hapa, sisi hatutasema wewe ulimvamia huyo mgonjwa..., najua kwenye video ya mahojiano tutakayoiomba kama ushahid ikibidi, itakuwa imeonyesha hilo tendo, lakini kwa hivi sasa, hatutaki mtu aseme wewe ulimvamia huyo mgonjwa,…’akasema huyo mama.

‘Kwanini tudanganye…?’ mimi nikauliza.

‘Wewe hujui mambo ya polisi,..ukisema hivyo polisi hawatataka kujua chanzo, huyu mama ataswekwa ndani, hadi hapo polisi watakagundua ukweli, na inaweza kachukua muda,... maana hiyo hali , inavyoonekana ilitokea ghafla, huenda baada ya kumuona huyu mkewe, akashtuka, au kabla,..mnakumbuka muda ule alibakai kimia, akawa katulia, lakini ghafla akasema ‘msifungue’ lakini hakuweza kujitikisa zaidi ya kauli hiyo, na kubakia kimia...'akasema huyo mama muuliza maswali.

'Nimekuelewa ...'akasema huyo mama

‘Mimi muda wote nilikuwa namtizama mgonjwa, sikuwa na mawazo kwingine,...huyu jamaa , hakutikisika, hata wakati anatamka maneno hayo ‘msifungue’ hapo akawa anahangaika kujaribu kutikisa angalau kichwa, lakini hakuweza, kwahiyo hiyo ‘stroke’ ilitokea kabla…au ilianza kabla huyoo mama hajamfikia, kuna wakati, nahisi kuna kitu kilitokea kipindi huyu mama nafungua mlango...'akasema

'Kwa vipi,,,,?' akaulizwa

'Muda huo ndio alionekana kugugumia, ...na uso ulionyesha kutokwa na jasho....nahisi hapo kuna kitu, sasa sijui ni nini hasa, nilimchunguza sana , na ndio maana hata wakati mnaamulia mimi nilikuwa nipo mbali ki mawazo na haikuwa na haja ya kuamua,....'akasema

'Kwanini sasa...?' tukauliza

'Kwasababu jamaa alikuwa hawezi hata kuinua mkono, huyu mama angelijua hilo asingelimvamia, unamvamia mtu ambaye alikuwa hana uwezo wa kujitetea, ....'akasema.

‘Oh, sasa hili ni nini maanake…?’ nikauliza mimi.

‘Labda tmama mjnae utusaidie maana muda nao ni muhimu, hatujui kitakachofuata huko mbele....hebu nikuulize masali mawili matatu, kuhusu huyu mtalaka wako...ilikuwaje, mpaka ukaja kuingia mle ndani bila kukuita.

 ‘Kuna mtu alinipigia simu, akaniambia niende huko chumba cha docta, nitasikia ukweli, kuhusu kifo cha mwanangu, nikamuuliza kuna nini, akasema, huko jamaa yangu anaelezea ukweli wote, kuwa,  yeye ndiye aliyemuua mwanangu, wakati awali alikuwa akikana kabisa kuwa sio yeye aliyemuua, mwanangu..mpaka tunaachana alikuwa hajakiri kosa…’akasema.

‘Ni nani huyo aliyekupigia simu..?’ akauliza.

‘Mimi sijui, ni namba tu ilionekana kwenye simu yangu…’akasema.

‘Sasa lolote likitokea,…ina maana polisi watakuita kukuhoji, uwe makini kwenye maongezi yako, usije kuongea mambo ya kuhisi,..au, nilisikia, kauli kama hizi, nilihisi, nilisikia ambazo huna uhakika nazo, nikwepe kabisa, ongea hali halisi uliyoiona na kuithibitisha, uwe makini sana na hayo….’akaambiwa.

‘Kwanini polsi wanihoji, mimi sijamfanya kitu huyo mgonjwa..., hata pale nilipomvamia, sikumpiga, nilifika pale na kumvamia, mara tukadondoka wote chini, hakunishika, na nilihsi mwili wake sio…ni wa baridi..’akasema.

‘Ndio maana nasema huenda polisi wakakuita kukuhoji, kuna dalili ya taarifa za mbaya, ni hisia zangu tu, sipenzi hivyo, na nyie mkwepe kuongea hisia zenu, nasema hapa kwa vile tupo pamoja, ..hatuombei, lakini nahisi jamaa hataweza kuamuka...'akasema

'Ni kweli, kwa hali ile,.., yawezekana akawa kwenye hiyo hali kwa mudaa mrefu, maana wengi wanaweza kuwa hivyo kwa muda mrefu, kuna wengine wanazinduka, kama damu haikugusa ubongo, lakini kama imegusa ubongo, mmh,sijui…’ akasema huyo mama mwingine.

‘Sasa hebu tuambie maisha yako na huyo mume wako, maana siku ile niliongea nawewe kwenye simu kwa haraka haraka, ndio nikakuambia ukija huku tutaongea vyema zaidi…huyu mume wako alikuwaje…?’ mama akamuuliza lakini kabla hajajibu mara akaja polisi,

****************

‘Ni nani mke wa yule mgonjwa..?’ akauliza askari , huyu alikuwa askari ambaye yaonekana kaitwa muda sio mrefu.

‘Ni mimi afande…’akasema huyo mama.

‘Twende ndani , kuna maswali tunataka kukuhoji…’akaambiwa, na hapo tukajua kuna jambo limetokea, na haikupita muda yule mama akarudi, na alionekana vile vile kuwa na wasiwasi, tukamuuliza kaulizwa nini.

‘Mhh..mimi nashindwa kuelewa, wananihoji maswali yale yale, ilikuwaje mimi na mume wangu, kwanini nimekuja huku, hawasemi kuna kitu gani kimetokea kwa mgonjwa, nahisi jamaa hayupo duniani tena…’akasema huyo mama, sasa kwa sauti ya huzuni.

‘Mhh, usiseme hivyo, …’akasema mdada

‘Sikupenda huyo jamaa haraka hivyo, nilikuwa sijamalizana naye, nilitaka apate shida kidogo,...hata hivyo jamaa ana roho ya paka,  kuna kipindi walikuwa wakitupiana makombora na huyo anayemuita adui yake,…anadondoka anapoteza fahamu masaa, lakini baadae anaamuka,….lakini ya safari hii , mhh, ...sijui , hata hivyo sikunda afe haraka hivyo...'akasema

'Lakini muda mfupu ulisikika ukisema hivyo....'akaambiwa.

'Aah, ni hasira, niliwahi kutamka hivyo mara nyingi tu, maana inauma, nyie acheni tu...mimi  nilitaka nimsikie kwa kauli yake akikiri kuwa kweli ndio yeye alimuua mwanangu..baada ya kupata mateso makali,..’akasema.

‘Lakini wewe ulisema, umesikia akisema, akikiri au…?’ akaulizwa na kabla hajaulizwa yeye akasema.

‘Pale nilipofika mlangoni nilianza kusikia pale aliposema ‘Kiukweli mimi sikujua, ningelijua nisingelifanya hilo..alinihadaa…kwanini nimuue mtoto wangu…’akasema.

‘Hebu nikuulize umesema mume wako alikuwa akitupiwa makombora, ni makombora gani hayo..?' akaulizwa

‘Unajua yeye huwa anasema eti huwa anapambana na maadui zake, mimi siwajui ni akina nani na hao anaowaita, maadui zake,wanawindana na kutupiana mashetani, ...anasema miongoni mwa hao maadui yake, mmoja wapo ndiye chanzo cha kifo cha mtoto, ndivyo anavyo jitetea hivyo...'akasema

'Huyo adui yake hujawahi kumfahamu.....?' akaulizwa

'Huwa hapendagi kumsema mtu kwa majina, ..hakuwahi kuniambia ni nani, ila wanatupiana mashetani, n ahayo masheani ndio wanaita makombora..'akasema.

'Ni kitu gani utafahamu kuwa katupiwa hayo makombora, ...?' akaulizwa

'Kuna dalili, mfano , ghafla anadondoka, na kuzimia, na ukimuangalia mdomoni, utamkuta na alama za damu, au...anaanguka na kuanza kuweweseka tu,...kama kapagawa....wenyewe wanajua...'akasema

'Na inachukua muda gani mpaka kuzindukana...?' akaulizwa

‘Inaweza ikachukua masaa hata nane, kuna siku tulijua hatazindukana, …’akasema.

‘Kwahiyo kama ulivyosema, ikitokea hivyo, kwanza anadondoka ghafla, anapoteza fahamu, na inatokea damu mdomoni na puani…si ndio hivyo?’ akaulizwa.

‘Ndio….na mara nyingi, ikitokea hivyo, nilikuwa namuita rafiki yake mmoja, yeye huyo anajua jinsi gani ya kumsaidia, basi akija kuna jinsi anamfanyia, haichukui muda, anazindukana hapo hapo au baada ya muda fulani hivi, au anaweza akachukua hata masaa kadhaa..., lakini baadae anazindukana….’akasema.

'Huyo jamaa yeye yupo wapi, huko huko kijijini, tunaweza kuwasiliana naye kwa hivi sasa..?' akaulizwa

'Mhh, hata sijui...maana hata namba yake kwenye simu...niliyo nnayo ni ya zamani, maana baada ya kuchana na mume wangu, nikaondoka huko, ..na siku nilipokutana naye huyo jamaa alisema simu ya zamani imeharibika,, na sikukumbuka kumuomba namba yake mpya...'akasema

‘Kwahiyo hili lililotokea lawezekana likawa ni kombora la huyo mwenzake..?’ akaulizwa.

‘Yawezekana, maana kweli nilipomvamia pale, sikuona akijibu mashambulizi, ndio maana nikadondoka naye, nilijua yupo sawa, kumbe alikuwa kapoteza fahamu, docta kasema alikuwa kapoteza fahamu, na pili huyu aliyenipigia simu ni nani, mbona…hata, sauti kama ni mtu namfahamu..’akasema.

‘Ni nani unahisi…?’ akaulizwa.

‘Hata sijui ni nani, ila sio sauti ngeni masikioni mwangu, ngona nitazidi kumfikiria…inaonekana ni mtu ninayemfahmu sana jamaa, na kunifahamu mimi…’akasema

'Au ni huyo raiki yake...?' akaulizwa

'Hapana, sio sauti ya huyo rafiki yake kabisa....'akasema

‘Oh, sasa itakuwaje…?’ akina mama wakabaki kuulizana

**********************.

‘Jamaa amefariki…’ilikuwa sauti ya mama , yule aliyekuwa akiongea na docta, na muda huo alikuwa kaongozana na yule mama mtalaka,…walikwenda naye kumuona docta, kujua ni nini kinachoendelea.

‘Oh, mungu wangu, …sasa itakuwaje..?’ akauliza mama mwingine.

‘Hapo sijui, ila tumeambiwa tusiondoke kwanza, tunahitajika kuhojiwa na polisi…’akasema.

‘Kwanini, kwani kauwawa, si kafa kifo cha kawaida au polisi wanashuku nini…?’ nikauliza mimi.

‘Kifo chake kinatokana na mshtuko mkubwa, na kilitokea wakati sisi tunamuhoji, maswali gani tulikuwa tunamuhoji na kwanini, na kwanini tumefanya hivyo, kwani sisi ni polisi,….ni maswali ya kawaida lakini tunatakiwa tuwe makini katika kuyajibu...'akasema huyo mama

'Sasa ni hivi, tujiandae kwa hilo, na maswali yanaweza kuwa hivyo, kwa maelezo, tutasema hivi…sisi tulimuita kwa vile tuna matatizo, na yeye ni mganga, kuna mtu alituelekeza kwake, bahati nzuri tukasikia kaja hapa dar, kuulizia, tukaambiwa kalazwa hapa hospitalini..tuakaja kumuona, tukaomba tuongee naye, …swali kwanini yeye, ..hapo sasa muwe makini kujibu…

‘Tusemeje…?’ tukauliza.

‘Hapa hatuwezi kuukwepa ukweli, kuwa matatizo hayo yanatokana na wafanyakazi wetu wa ndani, na wafanyakazi wetu wa ndani wanafahamiana na huyu jamaa, kwani huko kijijini kwao ndiye anyetambulikana kwa mambo kama hayo..hapo umemaliza.

‘Je wakati jamaa anadondoka au anapatwa na mshtuko mlikuwa mnaongea nini, mpaka ikafikia hivyo, hapo jibu ni rahisi tu, sisi tulikuwa kila mmoja anaelezewa shida zake..na mara jamaa akaanza kubadilika, na ghafla akakaa kimia, sisi tulijua ndio mambo yake y akiganga, na muda huo ndio mama mjane akaingia…'akasema

'Ok, tusubiria tu, lakini akiulizia kuhusu huyu mama alipoingia, ...?' akaulizwa

'Yeye aliingia kipindi mgonjwa yupo kwenye hiyo hali, na alipofika kutaka kuongea naye, huyo jamaa akaporomoka chini,...na ndio tukagundua kuwa jamaa hayupo sawa....'akasema

'Mhh....'mimi nikaguna hivyo

'Munielewe hivyo msije kujikanyaga, tukatofautiana maelezo, mkiingiza maneno , nahisi..nilisikia, itawapeleka segerea…na ukipelekwa huko unajua shida zake, kuingia rahisi , lakini kutoka, ...ni shida...'akasema huyo mama.

Ni kweli haikupita muda, tukaanza kuitwa na polisi

*************

 Waliitwa hao akina mama kuhojiwa, na bahati nzuri mimi na mwenzangu hatukuitwa, ikawa ni nafuu yetu

Na baaya muda, mara tukaambiwa yule mama mtalaka wa huyo jamaa akachukuliwa na polisi, kwa maelezo zaidi, kuwa yeye, anahitajika, kuisaidia polisi, ikabidi sisi tuone jinsi gani ya kumsaidia maana ni sisi tuliyemchukua huku kutoka huko kijijini kwake kwa ajili ya kuja kutoa ushahdi.

Taarifa hiyo ya kifo chake ilitugusa sana, tukikumbuka kuwa ni jamaa tuliyekwisha kumzoea kwa muda mfupi, na hata kazi tuliyotaka kuifanya na yeye ikawa haijakamilika, ikabakia swali, je itakuwaje,..hapo vichwa vikaanza kuwaka moto.

‘Kwa hilo lenu siwezi kulifanya nikiwa humu hospitalini, siwezi kuwadanganya, mimi sina tabia hiyo ya uwongo, hayo mambo yenu nitaweza kupambana nayo nikiwa majumbani kwenu, ana kwa ana, na kama kuna mtu kawaambia ataweza haya nendeni mkafanyiwe, lakini nina uhakika mtakuja kurudi hapa kwangu, na muombe mungu niwe bado sijaondoka,..'

Maneno haya yakawa yanatucheza akilini, na tulipojaribu kuulizana tufanye nini, jibu likaja, sisi twende kuonana na huyo jamaa ambaye ni mwalimi wake huyu marehemu..na kwa bahati nzuri huyu jamaa alikuwa kaja hapa dar, kwa mambo yake binafsi, tukataka kuhakikisha kuwa hajaondoka…tulipiga simu yake, ambayo huyo mama muuliza maswali alikuwa nayo, aliipata kipindi anahangaika kutafuta ukweli kuhusu mimi, na matatizo yake na mumewe.

‘Bado nipo Dar, na …hali yangu kiafya sio nzuri…’akasema, na kweli sauti iliashiria hivyo

‘Unaumwa nini..?’ akaulizwa.

‘Nina tatizo la shinikizo la damu, jana ilinikamata mpaka sasa nipo kitandani, kidogo nina nafuu, …’akasema

‘Oh, pole sana, sasa tunaweza kuja kukuona…?’ akaulizwa.

‘Kuhusu nini tafadhali, maana nahitajia kupumzika, maswala ya kazi, sitayafanya kwa hivi sasa, kwanza nataka kuachana nayo kama tulivyowahi kuongea nawe awali…’akasema.

‘Ni maswala machache tu, ni kazi ndio, unakumbuka nilikuambia kuhusu matatizo ya mfanyakazi wangu wa ndani, na baadae ukasema kuna madude yamepandikizwa kwenye nyumba yangu, sasa nataka utusaidia kuyaondoa, kama haiwezekani wewe utuelekeze kwa mtu mwingine…’tukasema.

‘Mhh..unajua siku ile hukuniamini, na mambo kama hayo yakiendelea kubakia yanazidi kuleta madhara, …na yule jamaa aliwaambiaje, hamjawasiliana naye, nasikia yupo huku Dar, …’akasema.

‘Ndio, lakini anaumwa…’akasema hivyo, hakutaka kumwambia huyo jamaa, kuwa mwenzake keshafariki.

‘Mbona …kuna taarifa,ok…..haya mtakuja lini..maana kama nilivyosema hali yangu sio nzuri, nab ado nipo kwenye michakato ya kuachana kabisa na mambo hayo…’akasema.

‘Kesho tunakuja…ni muda wako tu….’akaambiwa

‘Sawa, nitawasubiria…japokuwa kwakweli hali yangu bado sio nzuri...’akaongea kwa sauti inayoonyesha kweli anaumwa

****************
Basi kesho yake, tulifika sehemu hiyo tuliyoelekezwa kuwa jamaa huyo ndipo alipofikia, na tulipofika tulikuta watu wamekusanyika, tukauliza kulikoni, tukaambiwa jamaa mmoja amedondoka ghafla, na hali yake ni mbaya sana…

‘Ni nani huyo..?’ tukauliza

‘Ni jamaa mmoja likuja kwa jamaa yake hapa, kutokea mikoani, mara nyingi alionekana mgonjwa, akiwa ndani, wanasema muda alikuwa yupo sebuleni akiwa kapumzika, alikuwa akiongea na simu , ghafla, akadondoka, wenyeji wake walikuwa nje, na wao wanavyosema walisikia kilio kwa ndani, walipoingia wakamkuta jamaa yupo sakafuni,

‘Ikawaje sasa…?’ tukauliza

‘Ndio hivyo kakimbizwa hospitalini..’tukaambiwa,

Basi na sisi tukaona twende huko huko hospitalini,…tulipofika tukaulizia, kuhuhusu huyo jamaa tukaambiwa yupo chumba cha wagonjwa mahututi, …hatuwezi kuonana naye.

‘Hali yake ni mbaya sana…’akasema docta.

‘’Ana tatizo gani..?’ tukauliza.

‘Shinikizo la damu, …na limepelekea kiharusi, na kwa uchunguzi wa vipimo, damu imegusa ubongo,kwahiyo hali yake ni mbaya kwa kufupi…’akasema docta

Akilini tukasema; yale yale…..

***************

‘Oh, kwahiyo..?’ ikawa swali la kuulizana tena, na tukasema kwa vile tumefika pale basi tusubirie tu, ili tujue moja, na baadae tukaenda kumuona docta, docta akatuuliza sisi ni nani kwake, tukamuelezea, na docta hakutaka kutuficha akasema;

‘Huyo mzee amefariki…’tukaambiwa.

‘Kwa vipi…?’ tukauliza sasa tukichanganyikiwa kabisa, ni kwanini haya yanatokea kwa watu tuliotegemea watatusaidia kwenye hilo tatizo.

‘Mzeee kafariki kwa kiharusi,…mshtuko, shinikizo la damu, damu ikavilia kichwani, na kufariki, zaidi  labda mkamuone docta wake aliyempokea.

 ‘Sasa na hayo mauchawi jamaa aliyotuwekea itakuwaje, maana huyo mwalimu wake alisema yeye atatusaidia, nay eye ndio huyo keshafariki..?’ wakaulizana.

‘Kama wachawi waliotufanyia hivyo wamefariki , ni nani atafanikisha huo uchawi ina maana mambo hayo nayo yatakufa, kwanini tuogope uchawi na mungu yupo wa kutulinda….’wakajipa moyo hivyo

‘Lakini mnakumbuka kauli zao wote wawili ilikuwaje, kuwa hayo mambo yasipoondolewa yataanza kuleta matatizo ndani ya familia zetu..’wakasema na hapo ikawa ni mashaka kwenye nafsi za watu hawa, ikabidi sasa taarifa zifikishwe  kwa waume zao.

Mama mfadhili akawa wa kwanza kumpiga mume wake simu , alipiga simu ya nyumbani, akijua kuwa mume wake yupo nyumbani, siku hiyo alisema hajisiki vizuri, kwahiyo atapumzika , hataenda kwenye mihangaiko yake ya kila siku, na alipopiga akashangaa aliyepokea ni kijana wake, akamuuliza

‘Kwanini unaongea kinyonge hivyo..?’ akamuuliza

‘Sijisikii vizuri mama… naona mambo mawili mawili…’akasema

‘Kwa vipi,..?’ mama akaulizwa kwa wasiwasi sasa.

‘Hata sijui mama, na alitoka kidogo kununua dawa, alipokua, akawa anaongea ovyoovyo, kama mtu aliyechanganyikiwa, mimi nikaona nimpe zile dawa zake za kichwa, sasa hivi amelala, lakini alikuwa kama kapagawa…’akasema

‘Mungu wangu…na wewe umetumia dawa gani, kwanini na wewe usitumie hizo hizo dawa…?’ akamuuliza

‘Sasa tukilala wote, ni nani atamsaidia mwenzake,..na ..oh, mama kwani upo wapi, mimi naanza kuingiwa na mashaka kwanini naona watu wa ajabu..’akasema sasa mama naye miguu ikaanza kumuishia nguvu

‘Akakata simu na kuwaambia wenzake,

‘Jamani mimi naondoka…’akasema

‘Unakwenda wapi na wewe..?’ akaulizwa

‘Matatizo yameshaanza nyumbani kwangu tena….’akasema

‘Oh, ina maana ni kweli, kwangu haitawezekana, mimi namtegemea mungu wangu atatulinda..’akasema yule mama mwenye nyumba ambapo wote walikutania hapo…, lakini hata kabla huyo mwenzake hajaondoka, simu ya huyu mama ikalia.

‘Mhh, simu yangu hiyo, hata sikusindikizi, ngoja niisikilize, utatuambia kinachoendelea…’akasema akitoa simu yake kwenye mkoba, na sauti ilikuwa ya askari, ikasema

‘Samahani, mama, mume wako kapatwa na ajali, alikuwa kiendesha gari kwenye kazi za kila siku, ghafla akaona kitu mbele yake, kama alivyoniambia maana nilikuwa naye, akajaribu kukiwepa akagonga nguzo ya umeme,  sasa hivi yupo hopsitalini kapoteza fahamu..’akaambiwa

‘Ok, hospitali gani..?’ akauliza huyo mama sasa akichukua mkoba wa mwenzake akijua ndio wake

‘Mkoba wangu huo mshirika….’mwenzake akasema na simu yake nayo ikaanza kuita…

‘Bado mimi, mungu wangu wee…..’ilikuwa sauti ya huyo mama mwingine,  , mama ambaye alinipeleka hospitalini na alisema hivyo, baada ya yeye kusikia simu yake ikiita, na aliogopa hata kuipokea..

NB: Je itakuwaje sasa.....

WAZO LA LEO: Wakati mwingine matatizo yanaweza kukutokea kwa mfulululizo ya shida, mpaka unachanganyikiwa, na matatizo hayo yanaweza yakawa yana muelekeo wa jambo ulilolisikia, wewe ulilipuuzia ukasema ni mambo ya kishirikina, lakini sasa yanatokea kama ulivyoambiwa na watu, au mtu fulani, Ni muhimu kuendelea kuwa na imani yako kwa muumba wako, wala usitetereka, kwani mara nyingi,.matatizo haya yanatokea kwa minajili ya kukupima imani yako, Mungu ni mwingi wa rehema, humpima mja wake kumjua imani yake kwake, japokuwa anamfahamu . Kwa ma


Ni mimi: emu-three

1 comment :

Anonymous said...

Hey there! I'm at work surfing around your blog
from my neww iphone 4! Just wanted to say I love
reading your blog and look forward to alll your posts!
Keep up the excellent work!