Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, July 25, 2017

DUWA LA KUKU....19Tulifika hospitalini lakini muda wa kuingia watu kuwaona wagonjwa ulikuwa bado, na hata hao akina mama walipojaribu kutumia wadhifa wa waume wao ili wapate nafasi za upendeleo waligomewa , ikabidi sasa wajishushe na kuanza kubembeleza.

‘Hatuwezi kuwaruhusu kiukweli,kutokana na hali za wagonjwa, muda huu wanaonana na madakitari wao, wengine wanapata huduma mbali mbali, mkiingia mtasababisha kazi zingine zisifanyike, na wakati mwingine ni kwa afya zenu pia,kwani mlitaka kumuona nani..?’ akauliza mhusika wa wodi hiyo.

Wale akina mama hapo wakgeukiana, kwani wote walikuwa hawajui jina la mgonjwa wanayetaka kumuona,….

‘Unajua huyo mgonjwa ndio leo tumapigiwa simu, ni ndugu wa mfanyakazi wetu wa ndani, na yupo kule nje, sasa muda unatubana, tumajiiba mara moja kuja kumuona kuna maswala muhimu ya kufuatilia, nasikia anahijika dawa, na dawa hizo ni gharama sana, tunahitajika kuchangishana, sasa tusipokutana naye akatuambia vyema ni dawa gani tunashindwa kulifanyia kazi, tunataka tuongee na mgonjwa mwenyewe tusikie kauli yake,…’akasema

‘Nimewaelewa, ina maana nyie mnachotaka ni kuhakikisha kama kweli anahitajia hizo dawa, maana hawa wafanyakazi wa nyumbani wengine ni waongo ni kama watoto wadogo au sio…’akasema na ashukuru wakati anaongea hayo nilikuwa nje.

‘Ndio hivyo…’akasema mama mmojawapo

‘Oh, sasa kwa unyeti wa jambo lenyewe, mimi siwezi kuwaruhusu wote kuingia huko ndani, kwani lolote likitokea mtaniweka mimi kwenye wakati mgumu…’akasema.

‘Lolote kwa vipi,….sisi lengo letu nikupata huop uhakika, na kauli ya mgonjwa, tunakuhakikishia hakuna baya litatokea, kama mume wangu angelikuwepo hapa ..yeye ni askari basi angekuhakikishia hilo…’akasema mama .

‘Sio swala la uaskari au ubosi, ni utaratibu mama yangu, haya ingieni lakini nawaomba, msije mkafanya jambo la kunifukuzisha kazi tafadhali…’akasema na hapo, ndio wakapata mwanya wa kuingia kwa kujiiba, na sisi kwa haraka tukakimbia na kujiunga nao, msimamizi huyo alikuwa kaangalia kwingine kwahiyo hakutuona sisi tukiingia wodini.

 Ilikuwa wodi ya wagonjwa wa namna hiyo, ukianzia mlangoni, utaanza kuhisi huruma kama binadamu, kuna magonjwa yanawatesa watu, mtu wa kwanza mguu umekuwa kama umeoza, uso umeshakata tamaa ya kupona, wa pili yeye mguu wake mmoja umeshakatwa,…ukiendelea mbele, ni kila mmoja humo yupo kwenye mtihani mnzito wa maradhi haya ambayo, yanatishia amani za watu. Wakina mama hao japokuwa walikuja kwa jaziba, lakini kutokana na hiyo hali, nafsi, zikanywea.

Tulitembea hadi kitanda alicholazwa huyo mtu wetu tunayemfuatilia, nilijaribu kuwaza jinsi gani wataweza kumuongelesha hapo maana chumba kina wagonjwa,..na wapo macho, watasikia,…tukasogea hadi kwenye kile kitanda, tulimkuta jamaa kakaa kitandani akiwa kainamisha kichwa chini, hakutarajia ugeni labda maana alipotuona alishtuka, na kutukazia macho, na alipogundua ugeni huo ni wa watu gani, akainamisha kichwa chini.

‘Kumbe ndio wewe…’akasema yule mama mwenye nyumba kwa mdada.

‘Ndio mimi, karibuni wapendwa, karibuni sana, mimi sijambo kiasi, ndio nasubiria vipimo, ila mengine nimeshaambiwa, kuna dawa zinahitajika, ni aghalai kweli, kwahiyo kufika kwenu, nahisi tatizo litakwisha…’akasema.

‘Pole sana, naona umetukumbuka….’akasema huyo mama.

‘Ndio nimewakumbuka sana,  siku ile, nilikuja pale nyumbani kwako, kuonana na mdada…’ akasema.

‘Sio siku ile tu, umekuwa ukitutembelea mara kadha wa kadha, unatuona sisi tukiwa tumelala, si ndio hivyo, kwahiyo huwezi kutusahau…’akasema mama mfadhili wangu wa kwanza.

‘Kuwatembelea….mmh, hapana mimi nimelazwa hapa, tokea wiki sasa, ningekujaje nyumbani kwako…nafikiri umehisi vibaya…..’akajitetea akionyesha uso wa mashaka.

‘Kama kabla ya matatizo hayo, uliweza kutokea huko kwenu mikoani, hadi hapa Dar, na kuingia ndani kwenye majumba ya watu usiku ushindwe kuja kwangu ukiwa hapa dar…au tunaongea kwenye watu wengi usingelipenda watu wakakufahamu ..’akaambiwa na hapo akakaa kimia.

‘Tuambie, sasa lengo lako ni nini, na unapata faida gani kwa ushenzi huo…’akaulizwa na kwanza akazungusha kichwa kuangalia watu, wagonjwa walikuwa wamejilalia, wakiugulia maumivu, kwahiyo hakuona mtu mwenye dalili y akuwasikiliza, akasema;

‘Jamani mbona siwaelewi,….’akasema

‘Huwezi kujibu maswali yetu, …au unataka ukayajibie polisi..’akaambiwa

‘Jamani sikilizeni, hapa siwezi kuongea kitu, kama ingeliwezekana, nilitaka tuwe na nafasi nyingine sio hapa, nieleweni kidogo, kama kweli mna nia ya kusaidiana kwa matatizo yenu…’akajitetea

‘Kwanini unaogopa kuongelea hapa, wewe si unajiamini, huko kijijini unatamba kabisa wewe ni nani, au ?’ akaulizwa

‘Mambo mengine ni ya siri, siwezi kuyaongea hapa, na hayo uliyoyasikia kutoka huko kijijini ni uwongo na fitina za watu, tuyaache hayo tuongelee jambo la msingi, au mnataka nini kwangu…?’akasema na kuuliza.

‘La msingi kama lipi, haya tunayokuuliza kwetu ni ya msingi sana, maana yanatutesa, hatuna amani, sasa tuambie wewe ulitaka tuongelee nini kwanza..?’ akaulizwa.

Akageuka huku na kule , mara uso wake ukatua kwa mdada, ambaye ndiye chanzo cha haya yote, akakunja uso, na hakumuangalia sana, akainamisha kichwa chini na kusema.

‘Mhh, yaani, hata wewe, ….nilikuamini, nika….Ina maana, hebu jamani niambieni, shida yenu ni nini hasa….?’ Akauliza.

‘Ndio ujue kuwa mwisho wa mambo yako umefikia kikomo, si nilikuonya,…nilikuambia huko ulipokwenda utakuja kujuta, wewe tucheze sisi wanyonge lakini ipo siku utakutana na wasioingilika, uliniambia nini kuwa hujali, hata nilipolia, nakumuomba mungu akuangamize, ulisema nini, rudia yale maneno yako wayasikie hawa watu…’akasema.

‘Jamani wandugu ni hivi,…huyu ni mmoja wa watu wanaonijengea majungu na fitina, alikuja kwangu na kuanza kunilalamikia kuwa mimi ndio nimemfanya hiki na kile…nikamsaidia, nikamuambia akafanye kadha wa kadha, atapona, muulizeni hakupona huyu, sasa na nyie kama mna matatizo yenu, nitawasaidia, lakini kwanza kwa hali niliyo nayo na mimi nahitajia kusaidiwa…’akasema.

‘Utatusaidia nini, ni nani kasema anahitajia msaada wako kati yetu sisi hapa, wewe ndio wa kutusaidi sisi, au unafikiri vitisho vyako vya uchawi vinaweza kututisha sisi, watishe watu wa huko kijijini, lakini sio sisi, unasikia..’akaambiwa

‘Sasa mumefuata nini hapa..?’ akauliza sasa akionyesha jeuri yake, akawaangalia akiwa kawakazia macho.

‘Sisi kwanza tunataka kuwaita waandishi wa habari wazichukue taarifa zako zote tuna ushahidi wote kuwa wewe ni mchawi..wewe ndiye wale watu wanaowatishia watu huko kijijini, kwa imani za kishirikina, nyie ndio watu mnaotafutwa na polisi, mnaua wazee, mnaua watoto, mnawakata kata viongo vyao,..kwa imani za kishirikina, ..kweli si kweli…’mama akasema kwa nguvu na kuwafanya wagonjwa waliopo humo ndani kugeuka kuona ni nani huyo anaongelewa

‘Jamani hayo yanakujaje, una ushahidi gani na kauli yako hiyo,…kama ningelikuwa mchawi si ningelijiganga mimi mwenyewe, mbona na mimi nipo hapa hospitalini nahitajia matibabu, hizo kauli ni uzushi kabisa…’akasema sasa akiwa kainama tena.

‘Kuumwa kwako huko, ni kuwa umehangaika ukashindwa, wewe hujui ni kwanini huponi, hiyo nio adhabu ya uchawi wako, maapizo ya watu yanakurudia….’akaambiwa.

‘Ina maana wote wanaoumwa humu ndani ni wachawi…au umeniona mimi tu..?’ akauliza alipoona watu sasa wanaangalia wao.

‘Wao, sio wachawi , usitake kukwepesha mada, wewe ndio mchawi, wengine wanaumwa maradhi kama mitihani tu, mungu atawajalia watapona, hiyo ni mitihani ya mungu kwao, lakini wewe kuumwa kwako ni tofauti na wao, wewe umekuwa ukiwatesa watu, ukiwatembelea usiku ukiwanga.., kweli si kweli…muda umefika sasa tubu dhambi zako ili upone…vinginevyo utaoza mwili mzima huku unajiona…’akaambiwa.

‘Mumeharibu ndugu zanguni,..hapo mlipofikia, nawaambia wazi mumeharibu, hatuendi hivyo… nilitaka kuwasaidia lakini kwa njia hii hamtaweza kupata msaada wangu tena, na mtakuja kuniambia, mnasikia, hamnijui tu mimi ni mtu mwema sana, kwa wanataka wema wangu, lakini ukinichefua, huwezi kuamini, na ndio maana watu wananiogopa..’akasema.

‘Na sisi tukuambie hivi, hapa tumekuja rasmi, tumejiandaa kwa hilo, ulisikia mdada alivyokuambia, ulizoea kuwasumbua watu wa huko kwenu, sasa umejaribu kusipojaribiwa, umeingia choo cha kike, na utajuta kwa hilo, hatukutishi bali tunakuambia,….sasa tuambie, wewe kwanza unataka kutibiwa si ndio hivyo, sasa utatibiwaje, wakati unategemea pesa kutoka kwetu..?’ akaulizwa.

‘Nitazipata tu, hilo halina shaka,…nyie subirini muone, nina namna nyingi ya kuzipata hizo pesa, ila kwa vile mimi niliona nyie ni watu wema, mnaishi na binti wa huko kwetu na mpo kwenye matatizo, basi tusaidiane, ndio lengo langu hilo…’akasema na mara docta akaingia.

*************

‘Mbona naona kama kuna kelele hapa, kuna nini..?’ akauliza huyo docta na mmoja wa akina mama wale akamchukua huyo docta na kwenda kuongea naye pembeni waliongea kwa muda halafu yule docta akarejea na kusema;

‘Mgonjwa samahani, kwa vile nyie mna mazunguzmo nyeti, kama nilivyoambiwa, hatuna kawaida hiyo, ila kwa dharura tunafanya hivyo, ili kutokuwasumbua wagonjwa wengine, tutakuombe muende nje, au chumba …nitawaonyesha muingie huko muongee kwa uhuru, naukimaliza, utarudi hapa, sawa, upo tayari..?’ akaulizwa na yeye akabakia kimia kwa muda, halafu akasema;

‘Sawa ilimradi unihakikishie usalama wangu…’akasema huyo jamaa.

‘Usalama wako kwa vipi tena, unaogopa nini, kwani hawa sio jamaa zako?’ akaulizwa.

‘Ni jamaa zangu ndio, lakini wamekuja kwa hasira, hatuelewani ..lakini hamna shida, nitaongea nao tu, ukiwa na shdia, huna ujanja…’akasema.

‘Lakini kauli yako inanipa mashaka, kwanini unasema hivyo,…?’ akauliza docta.

‘Ndivyo alivyo huyu, tokea aanze kuumwa anakuwa hivyo anahisi kila mtu ni mbaya wake, hata kwa yale mambo ya kumsaidia, …’akasema mama mmojawapo, na docta akatikisa kichwa kuonyesha kuwa kaelewa.

‘Ndio hivyo ni kweli, haya magonjwa wengu hufikia hivyo, lakini watapona tu, ila jamani msije mkabishana hadi kuleta vurugu, kauli yake hiyo kwangu nimeipokea vingine kabisa, mnasikia….’akasema docta.

‘Kama nilivyokuambia docta kuna mambo nyeti, tunatakiwa tuongee naye, tukiwa peke yetu, hilo la usalama wake usiwe na wasiwasi, yeye ana kawaida ya kuongea hivi, kutokana na kuchanganyikiwa kwake, maradhi etna hayo docta….’akasema huyo mama.

‘Sawa mimi nawaruhusu lakini nataka uhakika wenu wa kuwa hamtafanya lolote baya..kama anavyodai yeye…’akasema docta.

‘Tunakuhakikishia hilo docta, atarudi salama..’akasema mama yule aliyenipeleka mimi hospitalini, na docta akaondoka, akisema;

‘Njooni huku na mgonjwa…’akasema

Mgonjwa kwanza akawa anasita kuondoka, ndipo mdada akajitokeza na kusema

‘Wewe ni mwanaume unatishwa na wanawake hahaha, na kujifanya kwako mchawi, nguvu za gizani kwenye mwanga unaogopa au sio, kama kweli unataka msaada wa kipesa , jitokeze uwashawishi hawa akina mama, vinginevyo, utaoza, na utazikwa kwa aibu..’kauli ile ilimfanya jamaa ajitutumie na kuinuka kitandani, akaanza kutembea kulekea huko kwenye chumba cha maongozi, kiukweli alishaanza kuwa kwenye hali mbaya hata kutemba ilikuwa ni shida.

Mama mmojawapo akawa anapiga simu kuwasiliana na watu wake na mwishoni akasema

‘Tayari..kakubali, mleteni, na kila kitu…’akasema

Mimi nilikuwa nyuma nyuma nikimuangalia huyu mtu kwa mbali, jinsi alivyo, anavyotembea, kiukweli japokuwa anaumwa na huruma za kibinadamu mtu kama huyo inabidi umuonee huruma, lakini nikiwazia yaliyonipata nilihisi vibaya, nikahisi kama kutapika!

Sikuweza kuvumilia…nikaruka kumvaa huyu jamaa..


NB: Sehemu hii iishie hapa, lakini shemu nyingine ipo tayari, kama watu watasoma kwa haraka, nitaweka sehemu nyingine jioni..Mungu akipenda..


WAZO LA LEO: Unaweza ukawa mtenda madhambi, mdhulumaji, watu wakawa wanakuhisi na hata kukuonya,lakini ukajifanya hujulikani, ukakana madhambi yako, huku unaendelea kuyatenda madhambi…, swali je unamdanganya nani, ..ukumbuke vyovyote ufayavyo, chochote ukifanyacho mwenyezimungu anakuona, na uovu wake unazidi…kwa vile umeonywa na wtu ukakaidi. Jamani tumuoge mola, dunia hii ni ya kupita, huyajui ya kesho.
Ni mimi: emu-three

No comments :