Nilifika nyumbani kwa huyu mzee, ikiwa ni makao mapya, niliyoambiwa yatakuwa ni y amuda,
na humo nikakutana na familia nyingine, ikiwa ya watu wengi kwani mzee huyu
alikuwa na watoto wengi tu, na wengi wao alikuwa akiishi nao, hawajaolewa…
Ukaribisho
wangu hapo ulikuwa wa maswali mengi, na yalianzia kwa mke wa huyo mzee, kumbe
mama mwenye nyumba wa hapo, hakuwa na taarifa na ujioa wangu, na hata kama
alikuw anao, huenda hakukubaliana nao,..na kauli yake ya kwanza naikumbuka sana
ilikuwa hivi;
'Naona umeniletea mke mwenza, maana nyie waume
hamzeeki…’akasema mke wake akiwa kashika kiuno. Alikuwa mwanamke aliyejaliwa
mwili, kwa unene, na huyu akikushika hupurukuti..tofauti na mume wake.
'Mke
wangu, ukisikia kisa na maisha ya huyu binti utamuonea huruma, hapa alipo ni
yatima, na mbaya zaidi, tokea anakuwa mkubwa maisha yao yeye na mama yake ni ya
umasikini, ya kuomba-omba, mabarabarani,
haya hilo lisitoshe, yule aliyemtegemea,kama mama yake alifariki dunia, kwa
kuchomwa moto na wezi..inasikititsiha kwa kweli…’akasema
'Mhh, na
ukaona hapa ndio kituo cha kulelea mayatima au sio, sikatai, hilo ni heri, kama
ningelijua mapema, na nikuulize tu, na
huko alipokuwa awali ilikuwaje, si ulisema yupo kwa yule bint yako unayemdekeza,
kila anachosema unamkubalia tu…na hata hili nalo umemkubalia, hata bila ya
kuomba ushauri wangu…’akasema
'Mke wangu, huko kumetokea mtihani, ndio maana
nimeamua kumleta hapa, na ni kwa muda tu, sikujua kuwa leo ninaweza kuja naye
hapa….’akajitetea mume mtu.
'Na iwe kwa muda,kweli, maana kama huko
wamemshindwa, kwa jinsi nimjuavyo yule bint, basi kuna tatizo, huyu binti
anaweza kuwa na …haya ngoja nisiseme mengi nikaja kuonekana nina gubu…’akasema
mke wake.
'Kwa
huyu kiukweli hana tatizo, ila yaliyotokea huko ni mambo juu y auwezo wao,
hayana haja kuyaselezea zaidi, tupo mbioni kulitatua hilo, najua litaisha na
likiisha huyu binti atarejea huko, au tutamtafutia njia mbadala za kumuzesha,
ili awe na maisha yake ya kujitegemea..’akasema
‘Hahaha unanichekesha kweli, wewe una watoto
hapa, hawana kazi, umeshindwa kuwatafutia njia mabadla za kujiwezesha, leo hii
uje kumtafutia huyu..mimi sijui, lakini ipo siri ndani yake, na itakuja
kujulikana tu, nawafahamu sana nyie wanaume…’akasema mama huyo.
‘Mke wangu niamini…mkaribishe mgeni, hayo
mengine tutaongea wenyewe..hiyo sio tabia nzuri ya kukaribsiha wageni…’akasema
mzee huyo.
'Mhh,..haya karibu mgeni samahani kwa lugha
yangu, inabidi unizoee, kuwa mimi sina mzaha kwenye wajibu wangu, ukikosea,
nitakupasha, na ikibidi nakutimua…na mume wangu, jingine ulisikie kabisa, mimi sitaki
kufanyiwa majaribio, maisha yenyewe haya ya kuunga unga, kama umesema ni wa
muda, na iwe hivyo,..sio kniletea mizigo humu ndani,mimi nimempokea mgeni kwa
vile wewe ni kichwa cha familia, vinginevyo, …haya karibu mgeni…’akasema na
kunipokea mzigo wangu.
Basi
nikakaribishwa kama ada, na kuanza kutambulishwa kwa wenyeji wangu, humo
kulikuwepo na wasichana wa rika langu, niliwaona wengine wakiniangalia kwa
macho ya kininyali, mpaka nikahisi vibaya, lakini niliona ni jambo la kawaida
tu , kwani maisha yangu yamekuwa hivyo toka utotoni, kudharauliwa kukashifiwa,
kunyanyapaliwa,…nikavumilia tu.
Ila mimi nilijua hali kama hizo ni kwa watu
wasiokuwa na uwezo, kumbe hata hawa watu wana tabia hizo,,…nilivumilia tu..,
japokuwa kulikuwa na visa vya hapa na pale, vya mauzi, hata wakati mwingine
nasingiziw vitu ambavyo sijavifanya mimi, niliendelea kuvumilia tu, nilijua
mvumilivu hula mbivu, mpaka wakaanza kuchoka wenyewe, na baadae ikageuka
kusifiwa tu.
Nilishangaa tangu nifike hapo ile hali ya kuota
ndoto mbaya za kukabwa, au majinamizi sikuwahi kuipata tena nikahisi huenda ni
ile duwa na maombi tuliyoyafanya siku ile kabla sijaondoka pale nyumbani, na
hata yule binti wa awali aliyetuambia mambo hayo, sikuwahi kuwasiliana naye
tena, hali yangu ilirejea kama kawaida, nikawa nalala kwa amani, hilo lilinipa
faraja sana…ila mara chache nilikuwa nikimuota mama yangu akinisihi nizidi kuwa
na uvumlivu kwani mambo bado magumu, …
‘Mambo gani magumu mama, naona sasa nina amani
licha ya hali ya hapa nyumbani, najitahidi kufany akama
ulivyonielekeza…’nikamwambia kwenye ndoto.
‘Najua hilo, lakini mitihan yako ni mingi,
uvumilivu wako ndio utakupandisha daraja, …usije kuhadaika maana mengi
yanayokutokea sio dhamira yako,…ina maana yake…’akaniambia na nilipotaka
kumuuliza swali jingine mara nikazindukana ikawa asubuhi, na asubuhi kwangu ni
mchaka mchaka wa kazi, nasahau kila kitu kazi ni nyingi, lakini sikupenda
kuziacha,…
‘Huyu mgeni ni mchapakazi kweli, hana muda wa
kuongea au kubisna na mtu, ukimuambia kitu anakubali tu, na wakati mwingine
anasingiziwa ubaya, yeye anakubali tu hata kama sio yeye aliyefanya, na kuomba
msamaha…...mmh, kweli kajaliwa ..’wengine wakaanza kusema hivyo
‘Hata hivyo muwe makini naye…’mama yao akawaasa
hivyo.
**************m
Siku moja nikiwa sokoni na wenyeji wangu mara
nikahisi mtu ananishika bega, kugeuka namuona ni yule binti wa kule nilipotoka,
akaniambia kwa ishara ni mfuate, nilishapigwa marufuku nisiwe na huyo binti,
hata wakati natoka kule, lakini kwa hapo, nikaona nimfuate nisikie anataka
kusema nini…
‘Unasemaje maana siruhusiwi kuongea na
mtu…’nikasema
‘Hata mimi, najua tu…wameshachukia sana, lakini
ukweli niwapasha,…sasa sikiliza unajua yule mjinga yupo hapa Dar…’akasema
‘Mjinga gani..?’ nikamuuliza
‘Si yule mchawi…..’akasema
‘Huyo aliyetaka kukuoa, au…?’ nikauliza
‘Ndio huyo huyo, kaja anaumwa kweli, sasa
najiuliza vipi mchawi naye akaumwa…’akasema
‘Anaumwa nini…?’ nikauliza.
‘Mguu umevimba, utafikiri ana matege…’akasema.
‘Oh, maradhi hayo, ndio umeniitia hicho,…?’
nikamuuliza.
‘Hivi hilo waliona dogo hata kama anaumwa,
hashindwi kupaa usiku na kukujia, ila kuna kitu nataka kukuambia,..’akasema.
‘Kitu gani..?’ nikamuuliza.
‘Nilikwenda sehemu,..nikaambiwa wewe upo kwenye
hatari kubwa sana, unajua na nilipokutana naye kasema wewe ipo siku utamtafuta, upende usipende….’akasema.
‘Hatari gani,..?’ nikauliza.
‘Na huyo mtaalamu kasema ukisubiria mpaka uanze kuumwa, ndio basi tena, utakwenda na maji…fanya juu chini uje tuonane kabla mambo hayajaharibika,...’akasema.
‘Ni hatari gani hiyo…?’ nikauliza na mara nikasikia
nikiitwa, na yule mwenzangu akainama chini na kupotea kwenye makundi ya watu waliopo humo sokoni,hakutaka hao jamaa zangu
wamuone, na mimi nikaguka na kuwafuta wenzangu.
‘Ulikuwa unaongea na nani..?’ nikaulizwa.
‘Yule ni msichana mmoja nilisoma naye…’nikadanganya hivyo kitu ambacho sikipendi, nilijisikia vibaya sana kudanganya hivyo nikawa natubu kimoyo moyo.
‘Achana nao, hao watakupoteza, na ukipotea
utafute pa kwenda na nakuasa siku nikisikia umeharibikiwa, wala usisubirie
kauli yangu, fungasha ondoka..maana nitakuumbua mpaka mitaa yote watafahamu…’akasema
mama mwenyeji wangu.
*************
Siku
zikaenda mwezi sasa unapita…, sikusikia lolote kutoka kwa huyo aliyekuwa
mfadhili wangu wa awali, mama mwenye nyumba awali alikuwa kilalamika lakini
siku zilivyokwenda akawa ananizoea maana niligeuka kuwa mfanyakazi wa ndani,
kila kazi naifanya mimi, tena bila kulalamika au kulipwa chochote.
Nilianza kutokujisia vyema, japokuwa
nilijitahidi kuficha hiyo hali,..ilikuwa kama kitu kigeni kuingia mwilini
mwangu, sikuzoea kuumwa umwa, na nikiwa nyumbani na mama mara nyingi nikijisia
kuumwa mama alikuwa akinipatia miti shamba, natafuna, hali inapotea, lakini hii
hali ilikuwa ngeni kwangu, sijawahi kujisikia hivyo kabla,.. siku zilivyozidi
kwenda hali ikazidi kuwa mbaya, nikaanza kuzidiwa, najisikia vibaya, siwi na
hamu ya kula, kizunguzungu…mpaka siku moja nikadondoka na kupoteza fahamu..
Nilipozindukana, wakawa wanajiuliza
‘Au ni hiyo hali aliyokuwa nayo ya kuota
majinamizi..?’ wakaulizana
‘Tumpeleke tena hospitalini..?’ wakaulizana
‘Hapo kuna mawili, …nina wasi wasi na huyu mtu,
hivi hamuoni anavyonawiri,..kunenepa gani huko, …’sauti ikasema
‘Wasi wasi wako mama, ….mimi naona …’akasita
aliponiona najitingisha, kuashiria nimezindukana, na wakanisaidia nikaa vyema,
wakaniuliza najisikiaje, niwajibu sasa nina nafuu, ni kichwa tu kinauma,
wakanipatia dawa za mauimvu ya kichwa. Baadae hali ikawa nzuri tu.
Baadae baba mwenye nyumba akafika wakamuelezea
hali iliyonitokea na yeye akauliza kwanini sikupelekwa hospitalini…
‘Kwasababu alipozindukana, akasema hajambo, na
mpaka sasa anaendelea vyema, haina haja ya kumpeleka hospitali tena, kwani bado
yupo kwenye dozi, dawa za awali bado hajazimaliza…’wakasema
‘Sawa hebu muangalieni, kama hali hiyo ikitokea
tena, basi ni muhimu tumuwahishe hospitalini…’akasema baba mwenye nyumba.
**************
Siku zilivyozidi kwenda nikawa sasa ni mgonjwa
kweli…
.
Kuumwa
kukawa tatizo sasa, hata nilivyojaribu kujificha nisionyeshe hiyo hali, lakini
ilifikia mahali sasa nashindwa, nikifanya kazi kidogo kizunguzungu, najisikia vibaya-vibaya tu, kula inakuwa ni
shida, kutapika kukaanza, nikawa sasa mtu wa kitandani hapo nikaanza kuonekana
ni mzigo.
'Mama huyu mgeni nahisi sasa ni mzigo kwetu,
kwanini haponi, mlimpima magonjwa yote..?’ akauliza binti mmoja akiongea na
mama yake, na waliongea baadae baba mwenye nyumba alipokuja mama akalifikisha
kwake, na mazungumzo yakawa hivi…
‘Huyu binti kuumwa kwake kumezidi….’akasema
mama mwenye nyumba.
'Anaumwa
kama binadamu wengine au sio, binadamu yoyote kuumwa ni kawaida au…’akanitetea baba
mwenye nyumba.
'Hapana
hii hali sio ya kawaida, mimi ni mwanamke na mtu mnzima, huyu bint tunatakiwa
tumuhoji vyema kuna jambo …’akasema huyo mama mtu mnzima.
'Kwani unahisi ana nini, nakumbuka ulishaanza
kumsifia kuwa ni mfanyakazi mnzuri wa hapa nyumbani ana Tabia nzuri tofauti na
ulivyofikiria awali, sasa imekuwaje, au watu kama hawa hawatakiwi kuumwa, mke
wangu tuwe makini na wanadamu wenzetu…’akasema baba mwenye nyumba hiyo.
'Sio swala la kuumwa tu, na siwezi kusema hisi
zangu kwa sasa, hebu jaribu kuongea naye, umuulize ana tatizo gani, labda mimi
nikimuuliza zaidi atasema ninamuonea,…jana nimejaribu kumdadisi, lakini majibu
aliyonipatia, nahisi hajielewi,..huu ni mzigo na mtihani, na mimi msimamo wangu
upo pale pale…’akasema mama huyo
‘Kwani una mashaka gani na huyo binti mke
wangu, tumempa dawa,..si alipima akaonekana ana malaria wengi tu, ana UTI,
ana…typhoid, magonjwa yote hayo yameonekana mwilini mwake,…sasa ngojeni amalize
dozi tuone matokeo yake kwanza, tukikimbilia hospitalini atazidi kupewa madawa
mengine…’akasema baba mwenye nyumba.
'Hata akimaliza dozi, tatizo hilo halitakwisha,
ndio maana awali nilikuuliza huko
alipotoka, aliondokaje huko au kuna kitu unanificha mume wangu..?’ akauliza
mama mwenye nyumba.
'Kwani
kuna nini unahisi kwanini huaniambii, mimi nitakuficha nini, huko alipotoka
tatizo ni kuwa likuwa ikifika usiku anaota ndoto mbaya, za majinamizi, watu usiku hawalali, ndio
wakaona tumlete hapa tuone kama hiyo hali itarudia au tatizo ni nini, na baadae
mambo yakikaa sawa tutamrejesha huko…’akasema.
'Una
uhakika na unachoniambia au ni mbinu za kufiachia uovu wenu, kuna nini
kilitokea huko alipotokea, mkwe wako alifanya nini,..niambie ukweli mume wangu
, maana ukinilazimisha nikagundua ukweli kwa njia nyingine kiukweli
hatutaelewana humu ndani, mimi sitkauwa na subira tena, ataondoka humu ndani,
hata kama ni usiku…’akasema huyo mama kwa ukali.
‘Mke wangu kwani kuna nini, kwanini wewe
huaniambii, una hisia gani kwa huyo binti, kwani ukiniambia mimi kutakuwa na
tatizo gani…kwani ulipompeleka hospitalini walimpima ni na nini..?’ akaulizwa.
‘Niliwaambia wampime magonjwa ya kawaida tu, kama malaria na hayo mengine,
kwasababu nilimuhoji kwanza, nijua kama anaweza kuambukizwa magonjwa mengine aliniambia hana uhusiani na wanaume, mimi
nilimuamini kwa vile ulivyosema, kuwa ni mkweli na muaminifu,…kwahiyo mimi
sikuwa na mawazo ya tatizo jingine lolote…’akasema
‘Kwahiyo kwa vile katumia dawa haponi, unahisi
kaambukizwa magonjwa mabaya,kwa muda mfupi namna hiyo unaanza kumuhisi hivyo,
kwani sisi hatujawahi kuumwa zaidi ya mwezi, na baadae tukapona, mke wangu acha
hisia mbaya hizo..?’ akauliza baba mwenye nyumba.
‘Kwa hali aliyo nayo naweza kuhisi hivyo na vinginevyo…,
mimi sijui lakini, muhimu ni vipimo vitasema, na nakuona una kwepesha kwepesha
ukweli, haya kesho tumpeleke hospitali, ukweli utagundulikana huko…’akasema
huyo mama mwenye nyumba.
‘Basi wewe umpeleke tu, utaniambia majibu
yamekuwaje,..na hata hao madakitari watakushangaa, ndio katoka kupimwa,
akaonekana ana malaria, sasa wamrejesha tena,…sawa kwa vile unataka kumjua afya
yake zaidi sio mbaya, kwanza kipimo hicho siku hizi ni bura tu…’akasema mume
mtu.
‘Mume wangu, na umri huo hujanielewa nina maani
gani…, basi kesho inabidi tuongozane, maana naona hutaniamini, hata nikija
kukuambia, hahaha, wanaume bwana mnaogopa kuumbuka eeh, hapo hapoo mtakuja
kujieleza, ni nani, …’akasema mke mtu…
‘Kwanini tuongozane mimi na wewe, ..kwani
mkienda wewe na yeye kuna ubaya gani..au hata kaam unaona anaweza kuzidiwa
unaweza kuondoka nab into yako mmoja au unasemaje?’ akauliza.
‘Nataka uwepo wewe mwenyewe, umuwakilisho huyo
anayehusika, au kama ni wewe, au mkwe wako, au yoyote, uweze kumuelezea vyema
atakavyosema docta, maana mimi sitaweza kuwa naye tena..kama ni hivyo na nin
auhakika ni hivyo, sisi tukitoka huko anakuja kufungasha virago vyake kwaheri
ya kuonana…’akasema mama mwenye nyumba.
‘Mke wangu mbona sikuelewi…’akasema.
‘Utanielewa tu hiyo kesho…, mimi sitaki mzigo
hapa nyumbani, .., unaona hawa mabinti, nilishawapa somo, na wakiona
tumelikubali hilo kwa huyi binti, wataona kumbe eeh, ni kawaida tu…, wataambukizwa,
na matokea yake tutakuwa na mizigo mingi humu nyumbani,..tuna bahati yamabinti
sasa isiwe kugeuka badala ya neema ikawa ni …aah,.. hilo mimi silitaki,
nilishawaambia atakaye fanya uchafu wake huko nje.., asije kuniletea matatizo
humu ndani, unakumbuka kila siku tunawaasa mabint zetu, …sasa wewe unataka kulianzisha, hivi utaweza
kuibeba hiyo mizigo…’akasema.
‘Mizigo gani mke wangu… atapona tu huyu, hizo
ni hisia zako tu, huyu binti kwa maelezo yake hana hata tabia chafu kama
hizo..labda awe kaambukizwa na sindano…vinginevyo, sijui…maana huwezi kumsemea
mwanadamu mwingine,..ila mimi nina uhakika ni maradhi tu ya kawaida, atapona...sizani
kama wamemuambukiza hao…’akasema.
‘Hao akina nani..?’ akauliza mke mtu.
‘Maana mle ndani alikuwa hata kutembea hana
tabia hiyo, alisema hana hata rafiki mmoja wa kiume, sasa ataambukizwa magonjwa
hayo na akina nani…au unataka kusema nini, kuwa ndugu zetu hao wana maradhi ya
kumuambukiza huyu binti, hapana wale ni watu safi kabisa…’akasema.
‘Unafikiria hayo tu eeh, maana unataka kumtetea
mkwe wako au sio..au yule kijana wao, maana yule kijana wao naye, siku hizi kabadilika
sana, suruwali zinavuka tu..hajisumbui kuzipandisha, anatuonyesha chupi yake,
hizi tabia nyingine za kuiga, hazina hata maana, wenzao wanafanya biashara za
kutangaza chupi, na mauchafu yao yaliharamishwa, wao wanaona ni fasheni…, ile
ni tabia mbobu kabisa, ..mimi humu ndani sitaki mchezo huo, wakiniletea wanaume
kama hao nitafukuza…’akasema na mara nikatokea, wakanyamaza.
‘Mhh..lakini mbona ana mwili wake tu,
hajakonda..’baba mwenye nyuma akasema nilipopita.
‘Kesho utalijua hilo vyema, mimi sikosei,…hali
hiyo ishajionyesha haina kificho tena… huyo binti kaukwaa, na …kama ni zezeta,
hatajua wapi alipoubebea huo mzigo…’akasema mama mtu na baba mtu sasa akainama
kama anawaza jambo.
‘Usiwaze sana,…kama na wewe ulipitia kidogo,
usubirie haki yako… maana baada ya vipimo, siwezi kukufanya uwe unawaza hivyo
zaidi, nataka mume wangu uwe na raha, tuwe na maisha yetu na watoto wetu, huo
ndio mzigo wetu halali, ..sio kubebeshwa mizigo mingine ambayo haipo kwenye bajeti yetu, unasikia sasa
kama ni mzigo wako, utajua mahali pa kuupeleka…’akasema.
‘Sawa kesho tutakwenda huko hospitalini kupima,
maana kwa hivi hatutaelewana…, lakini nilikuwa na mipangilio yangu mingine,
unajua kesho ndio i siku ya kwenda kuonana na huyo mkwe na binti yetu kule
alipotoka huyu binti…nataka , nijua kama wamefikia wapi, kwasababu wamekuwa
kimia, ..sijui wana mipangilio gani, lakini sio tatizo..tutakwenda na nikitoka
huko nitapitia huko mara moja.,…’akasema.
‘Utapitia au utakwenda naye…?’ akasema kama
anauliza.
‘Hapana itakuwa sio vizuri, kwa vile anaumwa,
hapan, huyu mpaka apone, na kama wameshamtafutia sehemu, bado atakaa hapa mpaka
apone, ndio ubinadamu…’akasema mume mtu.
‘Sasa hapo utaamua moja, mimi niondoke au huyo
hawara wenu aondoke…hilo sina mjadala nalo, kwetu bado kupo, unasikia, kama
ulinileta mke mwenza, umtafutie sehemu yake mpaka hapo kitakapojulikana,
unasikia, mzee wewe, utaumbuka kweli,..haya wewe jifanye msiri…’akasema mke mtu
na mara simu yam zee ikalia, na alipoangalia akasema.
‘Haya, hao wananipigia simu, nahisi wameshapata
sehemu au wameamua kumchukua tena akakae nao, subiri niongee nao…’akasema
akiweka simu hewani.
‘Hahaha ..mnajidanganya wenyewe
WAZO LA LEO: Katika maisha jitahidi sana kupende wengine,
chuki iwe mwiko kwako, usisubiri wewe kupendwa,
kwani yupo anayekupenda kwa vyovyote uwavyo, yeye kakubariki neema zote ulizo
nao.
Jitahidi
kusaidia wengine kwa kadri uwezavyo, hata kama una kidogo tu..na usitegemee
wewe kuisaidiwa na wengine, kwani ukisaidia wewe hata kidogo,… mola wako atakuzishia
barak..na utazidi kupata na kuzidi kusaidia zaidi. Kwani usiposaidia, itafika
muda utakuwa hunacho kabisa, na hapo utakosa wa kukusaidia kabisa.
Jitahidi
kusamehe hata kama wewe ndiye uliyefanyiwa ubaya, kwani kusamehe, kunavuta heri
nyingi, kamwe wewe usisubiri kusamehewa kwa wale wliokukosea, ..ukumbuke
ukisamehe, yupo yule ambaye atakusamehe, siku ambayo msamaha ni kwake tu.
Tumuombe
mola atupe iman thabit ya kumcha mola wa kweli, na kuwa mbali na unafiki, kwani
unafiki ni mbaya zaidi ya ubaya.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment