Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, July 21, 2017

DUWA LA KUKU---16Hutaamini wakati haya yanatokea hadi nafika hosp, na kuambiwa tatizo hilo, nilikuwa nimesahau kabisa yale aliyokuwa kaniambia yule mdada siku ile kule sokoni…, na baada ya tukio hilo, baada ya kutoka kwa dakitari, ndio kumbukumbu hizo zikanijia, kama vile mtu fulani ananikumbusha; …

'Unatakiwa uwahi kabla hujaanza kuumwa, ukianza kuumwa, utakwenda na maji..’maneno hayo yakaanza kunirejea akilini, lakini nilishaanza kuumwa, je kuumwa huku ndiko alikomaanisha huyo mdada, nikawa najiuliza

'Oh, kama ndio huko basi ...nimeshachelewa, ..'nikasema kwa sauti.

‘Hapana sijachelewa…hapana sijachelewa…’nikasema na kwa haraka nikasimama, sikutaka hata kusubiria tena.., sikutaka kuwasubiria wafadhili wangu hao, nilijua wakitoka humo, itakuwa kuumbuliwa, kwani huyo nikasimama alishaniambia;

 Kwa muda huo wafadhili walikuwa wakiongea na docta, na ilionekana walikuwa wakivutana huko ndani,

 'Bint, hili niachie nitajua jins gani ya kuongea nao, na watakusaidia tu, vinginevyo itabidi waeleze walichokufanyia

'Docta, hawa wazee wa watu hawahusiki lolote na haya, walinichukua kutoka kwa wafadhili wa awali, ambapo labda ndio chanzo cha tatizo hili

 'Lakini hawa ndio watasaidia haki yako ipatikane, hawa ndio nitawatumia, upate huduma zote stahiki, hilo niachie mimi

 Nilijua sitaweza kumshawishi docta zaidi, ndio nikatoka na kuwaambia wazee wanaitwa ndani

Tuendelee na kisa chetu.

*****************

 Nilimuambia mwenye bajaji nataka kwenda wapi, akanitajia gharama, sikutaka hadi kujadiliana naye zaidi, nilikuwa na akiba ya pesa zangu, nikamwambia anipeleke huko kwa haraka sana, na yeye bila ajizi akaanza kuiendesha bajaji yake kwa mwendo kasi, hapo sikujali kama anaendesha kupitiliza mwendo wa kawaida..

 Njiani niliwazia ni nini nifanye, kiukweli akili ilikuwa haijakubali kuwa kweli mimi nina mimba, sikuamini hilo kabisa lakini ndio hivyo, vipimo vimesema mimi nina mimba, tena ya karibu miezi miwili…

 'Au ndio hiyo  hatari aliyosema yule mdada, labda sio mimba halisi, labda kuna kitu kingine tumboni..labda, oh sasa iliingiaje, ina maana wale watu walikuwa ni kweli, oh, mungu wangu..nitafanyaje mie…’nikawa naongea kwa suti ya chini kwa chiini…

 Niliwazia hivyo, na jinsi nilivyozidi kuwaza ndivyo nilivyozidi kujenga hofu akilini mwangu, mpaka nafika eneo hilo ambapo mdada huyo alinielekeza siku moja, nilikuwa nawazia jinsi gani nimeipata hiyo mimba, na mpaka hapo nilikuwa hata sijui nafanya nini au nitafanya nini, akili yangu niwahi, ….niwahi nini sasa, wakati kama nikuumwa nimeshaanza kuumwa, lakini kuumwa nini…

 'Tumefika dada yangu, si ndio hapa….?’ Akasema na kuuliza.

'Sawa..'nikasema na kumpa pesa yake, na alipoanza kuniuliza maswali kuwa nina shida gani, mbona ninalia,  mimi sikumsikiliza nikaanza kutembea nikifuatilia ramani niliyoelekezwa na yule mdada, sijawahi kufika maeneo hayo kabla, ila mimi ni mwepesi sana wa kugundua maeneo ukinielekeza vizuri. Nilifika eneo hilo…ilikuwa sio sehemu iliyojificha, nikaona hiyo bara bara inayoingia kuelekea kwenye hiyo nyumba, na kwa mbele yangu nikaiona,….


Ni  jumba la maana, nikajua ni wale wale…sio kwamba nawachukia hao watu, ila nazichukia tabia zao tu, wana uwezo lakini hawana huruma na watu kama sisi,.. ndivyo akili yangu ilivyonituma hivyo.


Ilikuwa nyumba kubwa ni kama ili nyumba ya mfadhili wangu wa kwanza…, kuashiria kuwa ni mtu anayejiweza pia, moyoni nikasema;


‘Hawa watu sasa nitaachana nao, nitarudi mitaani tena…sijui itakuwaje, maana ni nani atanichukua tena na mimi nina mimba…oh …’nikajisema hivyo.
.

Nikafika mlangoni, na kabla sijagoonga nikajiuliza, hivi akitokeza mwenye nyumba, nitamuambiaje,…wakati najiuliza huku mkono upo hewani nikitaka kugonga mlango wa geti..huku akili bado inajilaumu kwa namna nyingine kuwa ni, kwanini nimefanya haraka kuchukua hatua hiyo, kwanini sikusubiria kwanza, huenda docta angeliwashawishi hao wafadhili wangu na kuafiki kunisaidia.


‘Hapana sio kwa yule mama, nahisi nikikutana naye atanitapia maneno mabaya…bora nitoweke kabisa na nisikutane no kabisa…’nikajisema hivyo,


Ndio ile nataka kugonga geti, mara geti likaanza kufunguka, kwanza nilishtuka kuwa huenda ukilishika hilo geti hujifungua lenyewe, kumbe…. hapana, kuna mtu alikuwa anafungua kwa ndani, kwa haraka nikachepuka pembeni kujificha.. ili mtu wa huko ndani asinione.


Kumbe kulikuwa na gari linataka kutoka nje, hapo nikajiingiza pembeni mwa hiyo nyumba kulikuwa na barabara inayotengenisha geti la  nyumba hiyo na geti la nyumba nyingine,..kulikuwa na miba ya miti ya michongoma, lakini nikajilazimisha hivyo hivyo na kujikuta ninachomwa na hiyo miba, sikujali, ..


Nilisubiria hadi lile gari likaanza kuondoka, na kabla halijaondoka,  nikasikia sauti ya kutoka kwenye gari, ilikuwa ni sauti ya kike, ikisema,…

‘Huenda jioni nikafika na rafiki yangu, hakikisha kila kitu kipo kama nilivyokuelekeza, sasa uanze kutanga tanga mitaani, au kuleta watu humu ndani….sitaki tabia hiyo,..unanisikia..na, nikute hujafanya hivyo nilivyokuelekeza, itakuwa ndio siku yako ya mwisho kukaa humu ndani, umenielewa….’sauti ya kike nzito ikasema, akiwa yupo ndani ya gari lake la bei mbaya.


‘Nimekusikia madamu…’sauti nyingine ikasema kutoka huko ndani ya geti,..sikumuona kwa vile nipo nyumma ya huo ukuta , ila nilihisi kutoakana na ile sauti atakuwa ni yule mdada niliyemfuata humo. Kumbe anamuita bosi wake madamu, nikatabasamu mawazoni, mimi kwangu nilizoea kuwaita mabosi wangu mama au baba.


Nilisubiria kidogo,hadi lile gari likaondoka…. halafu nikagonga mlango wa geti, kukawa kimia, nikagonga tena, baadae mlango ukafunguliwa,..na mdada akajitokeza aliponiona akashtuka, halafu akaangalia kwa ndani na kusema;


'Wewe umekuja huku, hata bila kuniarifu, hukusikia madamu alivyosema, huyo mama ni mkali kweli ungenipigia simu kwanza, ooh, halafu `sir…’  bado hajatoka, sasa wewe fanya hivi, kaa nje kidogo, ukiona gari limetoka ndio uje….unasikia, haya nenda….’akasema na mimi nikachepuka hadi sehemu nyingine inayoangaliana na hiyo nyumba, nikasubiria.


Na haikuchukua muda, gari likatoka, na nikasubiria kidogo kidogo, gari likatoka na likapit akaribu yangu, na sijui ilikuwaje, mara likasimama, na kiyoo kikashushwa, hapo nikahisi mwili kunicheza, jamaa akatokeza kichwa na kuniangalia, hakusema kitu, akapandidha kiyoo, na kuendelea na safari yake,


Alikuwa na maana gani, au aliniona wakati naongea na mdada pale getini, …nikajiuliza lakini sikuwa na muda wa kupoteza, muhimu nionane na huyo mdada, mengine yatafuta baadae.


Nikatembea hadi kwenye geti nikagonga mlango na mdada akafungua geti, akaniambia…


‘Kumbe yule sir,… kakuona, alichungulia kwa kupitia dirishani, haya madirisha ya viyoo ukiwa ndani unaona nje, ila ukiwa njehuwezi kuona huko ndani…’akasema.


‘Sasa,..’nikauliza nikionyesha wasiwasi


‘Yule mbaba, hana tatizo, nimemuambia wewe ni rafiki yangu ulikuwa unapita tu, ukaona unisalimie,  na hakuniambia kitu, zaidi ya kusema niwe makini ….hana tatizo huyo mbaba wa watu, mwenye shida ni mama, akikuona humu ndani, atakutoa kama mbwa…’akasema.


‘Sasa…’nikasema tena hivyo


‘Niambie, kwanini hukufika mapema kama nilivyokuambia…’akasema.


‘Kwani ilitakiwa nifike haraka, mimi sikukuelewa siku ile, hata hivyo si unajua hizi kazi zetu, huwezi kupata mwanya wa kutoka, labda utumwe, na huko ndio ujiibe, na …ghfala nikaanza kuumwa…’nikasema.


‘Mungu wangu, lakini nilikuambia…uwahi kuniona kabla hujaanza kuumwa…’akasema akionyesha uso wa wasiwasi.


‘Kwani tatizo ni nini, haya mfani ndio ningewahi ungelifanya nini…?’ nikauliza.


'Oh hebu twende ndani tuongee haraka, mabosi zangu wakitoka, kurudi ni jioni , labda kutokee dharura, lakini kuna kazi nyingi za kufanya ndani, tutaongea huku nachakarika, ..si unajue tena, mjibi hapa….na kuliko kukaa tu, wewe utanisaidia zile unazoweza au sio, lakini sio kwamba nakulazimisha, wewe ni mgeni wangu… ‘akasema akianza kufagia.


‘Mimi naumwa hata kukusaidia siwezi, we acha tu…’nikasema


‘Usijali, niambie sasa  imekuwaje, na umekuja kufanya nini, maana tuulizane mapema,  kama umeshaumwa mimi sina la kufanya, hilo nilikuambia mapema, usije kunilaumu…’akasema.


'Mimi hata sijui nifanyeje hapo, ulivyoniambia mimi sikuamini ..unajua mimi siamini mambo ya kishirikina, mama alinikataza,…na sasa hapa nilipo nimechanganyikiwa… huko kwenyewe nimetoroka…’nikasema.


‘Mungu wangu, umetoroka, kwanini umetoroka,…wewewe… unataka kufanya nini, hawa watu ndio wanaotufanya tuishi hapa mjini..tusiishie mitaani na kuzalilika,…, ukitoroka huko utakwenda kuishi wapi, mimi siwezi kukupokea,, ulisikia madamu alivyosema,…sasa wewe lengo lako ni nini,…unataka kuishi tena mitaani, utapaweza na sura yako hiyo, labda kama unataka kujiuza….’akasema.


'Wewe siku ile uliniambia nini, ni kutafute, sasa si ndio nimefanya hivyo….’nikasema


 'Sawa naelewa, nilikuambia hivyo… ujitahidi unione, lakini sio kwa kutoroka, maana ulivyofanya utajichongea, na kuniharibia hata mimi kazi yangu, na mimi sikubali kwa hilo..nayajua maisha ya mjini, sasa hivi hanidanganyi mtu, usipokuwa na kazi, huna kazi..utazalilika…, pili nilikupa tahdhari kuwa unione kabla hujaanza kuumwa, sasa umeshaumwa,..si ndio hivyo… na huenda ulipoteza fahamu au sio….’akasema.'Sawa sasa wewe niambie, ulitaka nikuone ili iweje, kuna maagizo, au  uliambiwa nina hatari gani itakayonipata…na kuumwa huko ni kupi, yawezekana nina tatizo ambalo halihusiania na hilo….’nikasema.'Umeumwa, una dalili za mimba, umedondoka na kupoteza fahamu, kama ni hivyo hilo ndilo tatizo lenyewe,…..’akasema.'Ndio nimeumwa, nikapoteza fahamu na sasa hivi natokea hospitalini, nimewatoroka mabosi zangu, huenda sasa hivi huko wananitafuta kama kweli wana nia njema na mimi , ila nijuavyo mimi, kwa kauli ya huyo mama mimi sitakwi tena kwenye hiyo nyumban, labda itokee miujiza, kwa baba kumshawishi mke wake…, hivi kwanini hawa akina mama matajiri wanatuchukia hivi…’nikasema'Kama ni hivyo umechelewa, hatuwezi kufanya lolote, ndivyo nilivyoambiwa,na sitakiw kukuambia la kufanya ndio miiko yenyewe,…’akasema


‘Oh, kwahiyo kumbe nimepoteza muda wangu bure kuja hapa…na wewe unaaminije hayo, ..miiko miiko…niambie nilitakiwa nifenyeje, mfano ningelikuja mapema…?’ nikauliza


‘Wewe huamini miiko, eeh, .wewe hujiulizi huyo mtu kajuaje yote hayo hata kabla hayajatokea, eti umeuliza nini, kuwa kwanini hao akina mama wanatuchukia, … hata kama ingelikuwa ni wewe, analetwa kimwana umependeza kama wewe, unafikiri yeye hawezi kuona wivu, ni wivu kwa vile wanahisi utawaibia waume zao, na waume wengine ndio hivyo, tamaa mbele…’akasema'Sasa nifanyeje…nitafanya nini mimi jamani, nitakwenda wapi masikin ya mungu, hivi nimewakosea nini hawa walimwengu jaman, kwanini wasiwafuate watu wenye uwezo wao, wanatusumbua sisi masikini ya mungu, kwani mimi nitawasaidia nini jamani, basi waniue kabisa, kama walivyomuua mama yangu…’nikaanza kulia.


'Kwani vipi….wewe unalia, mimi nililia sana tu..sasa wewe lia ukimaliza tutaendelea kuongea…’akasema


‘Inatia uchungu, kwanini ….’nikasema


‘Sasa nikuulize ,kuacha matatizo hayo kwani kuna tatizo jingine zaidi,…kama umekwenda hospitalini kutibiwa na sasa upo na afadhali, basi,…nikushauri kitu,  wewe ukitoka hapa rudi kwa mabosi zako, ukawaombe msamaha, uendelee na maisha, kwani pale wanakupia shilingi ngapi…?’ akaniuliza.


‘Hapo kwasasa silipwi kitu zaidi ya kula na kuwafanyia kazi tu….’nikasema


‘Hapo pagumu, lazima utafuta kazi ya kulipwa, ili usiishie kuomba omba, waambie wakutafutia kazi, kama wao hawataki kukulipa…’akasema.


‘Ni nani atanipokea na hali hii tena…’nikasema


‘Hali gani tena, si umesema umeshatibiwa, tatizo lipo wapi tena,…labda ilikuwa ni matatizo ya kawaida, na wewe huamini mambo ya kishirikina….’akasema


'Nimeambiwa nina mimba…’nikasema na hapo akadondosha chombo alichokuwa kakishikila, na kunitolea jicho la kuogopa, akahema, halafu akasema


'Mimba, wee..unasema ukweli…. ya nani hiyo mimba, unajua mimi nilipoambiwa nina mimba nilitafauta kile njia nisijulikane, na nashukuru, sasa nipo salama…sasa hebu niambie, …maana mimi niliambiwa utahisi dalili za mimba lakini sijaambiwa utakuwa na mimba, sasa hapo hata mimi sielewi kitu…’akasema


'Mimi sijui ya nani..hapa nimechanganyikiwa, hata sielewi nifanye nini mimi ndio maana nimekuja huku , nilijua labda ndio hicho ulitaka kuniambia, na hata hivyo mimi sijaamini kuwa nina mimba, kwani…hiyo mimba imetoka wapi, wakati mimi simjui mwanaume….’nikasema


'Yale yale..kama yaliyonikuta mimi, …sasa unajua..kama ni hivyo,…oh, kwako wewe iakwu ani ngumu,..mmh,  lakini inategemea na wewe mwenyewe..kwa hivi sasa mimi sina zaidi la kukusaidia, wakati mwingine inabidi ule matapishi yako, kwasababu aliyefanya hayo yupoo humu jijini, basi inabidi uende kwake…’akasema.


‘Kwa nani…?’ nikauliza nikionyesha uso wa mshangao.


‘Huyo mwanga, aliyekusababishia haya yote, umuone kabla hajaondoka, kama keshatibiwa…’akasema


‘Kabla hajatibiwa kwani na wao wanatibiwaga hospitalini, wao si wachawi,…?’ nikamuuliza akajifanya kama hajanisiakia, akasema;


‘Hebu nikuulize kwanza,…una uhakika kweli hujakutana na mwanaume mwingine,..usinifiche maana mtu anayeweza kukusaidia ni mimi, kama nitaujua huo ukweli wote, nitajua cha kufanya, au cha kukushauri…je hujakutana na mwanaume mwingine uwe na uhakika, maana kama umewahi kukutana na mwanaume mwingine na iwe ni mimba yake, hapo kuna mawili, kuonana na huyo mwanaume au jingine….una uhakika..?’ akaniuliza


'Uhakika gani …mimi sina mwanaume, sijawahi kukutana na mwanaume yoyote, hilo nina uhakika nalo, ndio maana siamini kuwa nina mimba kweli, huenda labda kama ulivyosema…’nikasema.


'Mhh, sasa unaanza kuamini eeh, eti kama nilivyosema, …hahaha, … sasa hapo ni tatizo, yawezekana yule jamaa kakufanyizia hivyo, ..hilo hakuwahi kuniambia,…hata hivyo kwa maelezo yake, maana ilibidi nimtoe kwa nguvu, yeye alisema utakuwa na  dalili za mimba, sasa kama umepimwa una mimba,hicho ni kitu kingine, sikuweza kumuuliza zaidi..’akasema.


'Unasema labda kanifanyizia, kanifanyizia nini sasa…?’ nikauliza na yeye akaendelea kuongea bila kujali swali langu.


'Au ni wale watu wawili mle ndani, inawezekana eeh, labda mmojawapo ndiye mimba yake hiyo,au ..hebu niambie ukweli, maana yule kijana naye, mmh, usipokuwa makini  …’akasema na kuniangalia machoni.


'Unataka kusema nini…hapana mimi likuwa ni ndoto tu, sijawahi kutembea na yoyote mle ndani, hilo sio kweli, ndio maana akilini mwangu naamini kuwa mimi sina mimba, huenda ni hayo mambo ya huyo mjamaa wako….’nikasema


'Ina maana nilichowaambia siku ile wewe hukuniamini, na huyo sio mjamaa wangu huyo ni adui yangu….’akasema.


'Mimi siwezi kuyaamini hayo kwasababu mimi nilikuwa naota tu…haiwezekani ikawa ni kweli…’nikasema


‘Hahaha, hiyo sio ndoto ile ni kweli na sababu inaweza ikawa kweli ni huyo mjamaa kuhusiana na hizo ndoto, sio kuhusiana na hiyo mimba , maana lengo lake sio ubebe mimba ya watu wengine, alikuwa makini kwa hilo, ila uzalilike tu… alichokuwa akifanya  yeye ni vile vile kama nilivyowaambia, pale baba na mtoto walikuwa wakiletwa kwako usiku, ….wanakuzalilisha, wakati huo, hata wao wenyewe hawajijui…’akasema.


‘Una uhakika gani na hilo, ….?’ Nikauliza


 ‘Jamaa alininisimuliza yote alivyokuwa akifanya…’akasema


‘Mlikutana naye..?’ akaniuliza


‘Nitakusimulia tu  , usiwe na wasiwasi chukua chai hapo jipimie kiasi chako, na vitafunio hapo kwenye kabati, ukimaliza tutaongea, ….saa hizi hakuna chakula,  sijapika…nitapika chakula maalumu cha mgeni, madamu kasema leo ana mgeni wake humu ndani, sijui ni nani….’akasema.


‘Hapana mimi sina hamu ya kula chochote…’nikasema.


‘Utakufa wewe, kula kama una mimba basi..hiyo mimba itakusumbua, jilazimishe kula wakati kipo, hujui huko mbeleni itakuwaje…’akasema


‘Sina mimba mimi jamani….’nikasema


‘Hahaha, unalo hilo, nakuonea huruma sana, lakini …pambana, usikate tamaa, tatizo je ni ya nani…’akasema


‘Nimeshakuambia mimi sina mimba, imetokwa wapi hiyo mimba, mimi sijaamini bado….’nikasema


‘Eti huna mimba, wewe si ndio umeniambia hivyo, kuwa umepimwa na vipimo vimeonyesha kuwa una mimba au,…?’ akaniuliza


‘Inawezekana ni huyo mjamaa  kaniwekezea mambo yake humu tumboni kunifanya nizalilike tu …’nikasema


‘Basi kama ni hivyo, dawa ni kuonana naye, …’akasema


‘Kwa vipi, mimi sitaki hata kumuona huyo mtu, nahisi siku nikionana naye,  nita….nita-mfanyia kitu kibaya, nitamuua…’nikasema


‘Hahaha, unakuwa kama mimi, niliapa kuwa nikikutana naye, nitamfanya  hivyo, lakini nilipokutana naye safari hii , nikagwaya…’akasema


‘Ulikutana naye safari hii, kumbe umeonana naye uso kwa uso…?’ nikamuuliza


‘Tatizo wewe umechanganyikiwa….nimekuambia nilionana naye…’akasema


‘Wapi, au usiku ..?’ akauliza


‘Alikuja hapa kwenye hii nyumba,…, karibu anifukuzishe kazi…’akasema.


‘Alijuaje upo hapa, au ulimuelekeza wewe aje hapa….?’ Nikamuuliza.


‘Hahaha, hivi hujanielewa, jamaa yule ni mchawi, usiku anatembelea majumba ya watu, hasa kwa watu wake aliowafanyizia, kama balozi wa nyumba kumi, ila hapa kashindwa…na aliposhindwa ndio, ikabidi sasa aje mguu kwa mguu kuonana na mimi….’akasema.


‘Oh….kwanini…?’ nikaguna na kuuliza.


‘Wewe subiria, niitakuelezea kila kitu, alivyokuja na mambo yake,.. alivyonielezea alivyokufanyia wewe na..mengine mengi ndio utaona kuwa wewe matatizo yako sio bure ni huyo huyu jamaa, lakini kisa kilianzia kwangu…wewe subiria kidogo nimalize usafi…’akasema na kuelekea nje.


Mara ghafla akaja mbio mbio akiwa kashikilia simu mkononi….akasema


‘Fanya uondoke….’akasema


‘Kwani vipi, kuna nini...…?’ nikauliza

'Huu sio muda wa kuuliza,....ukikutwa humu, ....utanifukuzisha kazi, na madamu anakuja na mtu ambaye hutapenda kukutana na yeye,....fanya haraka katafute sehemu, nikipata nafasi nitakuita, au nikipata mwanya nitatoka tuongee...lakini sijui kwa vipi,....'akasema sasa akinishika mkono kabisa kuhakikisha natoka nje, na wakati tunatoka nje, mara geti likagongwa, gari lilikuwa limesimama nje ya geti.


NB: Itakuwaje tena..
WAZO LA LEO: Kuna watu wanachukua dhamana za watu, wanachukua watoto wa wenza wao, iwe wa ndugu au jamaa ili waishi nao, lakini watu hao, wanakuja kuwafanyia mabaya hao watoto, wakisahau kuwa watoto hao ni sawa na watoto wao, na ya kuwa, na wao watakuja kulipiziwa kwa watoto wao. Adahabu nyingine huanzia hapa duniani. Tuweni makini sana, kama kweli tunazipenda familia zetu, basi na tuzipende familia za watu wengine.

No comments :