Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, June 14, 2017

MPENZI WA FACEBOOK-50


                                       
                                     KESI-HITIMISHO-1:

Ni siku kesi ilipangwa kusikilizwa, na siku hiyo hakukutakiwa watu wafike, lakini haikuwezekana, kila mtu alitaka kesi hiyo waione,..ni kesi ya aina yake ambapo washukiwa wanakamatwa, na kesho yake, kesi inasikilizwa….na washukiwa hao walitakiwa wawe hivyo hivyo, bila kubadili nguo.

‘Wakiruhusiwa kubadili nguo, watavuruga ushahidi…’akaambiwa hakimu.

‘Lakini mnakiuka haki za binadamu.

‘Muheshimiwa hakimu, hao watu watabadili nguo zao, mbele ya mahakama yako tukufu, na tendo hilo litakuwa ni ushahidi tosha kuwahusu hao watu ….’akaambiwa hakimu.

Mawakili wao waliruhusiwa kuongea nao, mbele ya askari…na hata mawakili walipolalamika hawakusikilizwa, na kesho yake ikafika watu hao walifikishwa mahakamani wakiwa wamefungwa kuhakikisha hawafanyi lolote kwenye miili yao.


Ilikuwa kesi ya aina yake, mashahidi mbali mbali wa kitaalamu waligizwa, wataalamu wa mitando, madocta bingwa wa ngozi, madocta wa magonjwa ya akili, ilimradi kila mtaalamu wa taaluma inahusiana na mwanadamu alitakiwa kufika hapo.

Kesi ikasomwa asubuhi, na washitakiwa hawakutakiwa kujibu lolote au kuomba dhamana, na ikatajwa kuendelea mchana…kitu ambacho sio cha kawaida, na watu hawakuondoka, na hakuna aliyekata tamaa, na watu wakazidi kuongezeka zaidi.

‘Muheshimiwa hakimu, baada ya sisi kutoa ushaidi wetu, basi utaamua mwenyewe kuahirisha hii kesi hadi siku nyingine, ndio maana tukaomba tutoe vielelezo vyote vya ushahidi hii leo bila kusubiria siku nyingine….’akaambiwa hakimu, na kesi ikaanza kwa utaratibu wake, na aliyeitwa kusaidiana na muendesha mashitaka alikuwa docta.

Docta akaelelezea kwa kirefu kuhusu kundi hilo lilivyoanzishwa, na ujanja wanaoutumia, ikiwemo kuchanganya nguvu za giza na ujanja wa kimtandao,jingine ni watu kujibadili ngozi, na kuwa sura nyingine, ‘watu hujibadili kama kinyonga…’akasema hivyo!

‘Watu wanajibadili kivipi kama kinyonga..?’ akaulizwa.

‘Kuna utaalamu wa ngozi, ngozi hizo, hunakishiwa kwa sura mtu anayoitaka, akitumia mitandao, kwahiyo kwa mfano leo akitaka sura yako, anakwenda kwenye mtandao, anaichukua sura yako kwa kuangalia picha,…na kwa kutumia komputa anaweza kuielekeza kwenye program maalumu, kuwa mimi nataka niwe hivi, au huyu awe hivi, akilinganisha na picha ya sura aliyoichukua tayari kwenye mtandao.

‘Hioyo itawezekanaje, maana wengine wana vichwa vikubwa, wengine vidogo, achilia mbali maumbile ya kiwiliwili…je wanafanyaje kuhusu hilo…?’ akaulizwa.

‘Hilo kwao walishalifanyia kazi, ndio maana anapotea mtu ambaye hana masilahi kabisa na wao, wanachotaka hapo ni wapate mtu mwenye umbile linalokaribiana na wao, usoni sio kazi kubwa sana, mtandao unaweza kurekebisha hilo,kwani ile ngozi inaweza ikatunushwa kufuatana na umbile linalotakiwa..’akasema.

‘Tutatoa mfano kwa washitakiwa, kulithibitisha hilo,..muda muafaka ukifika, na kila kitu kitakiwa hadharani, ili muone hawa watu hawa walivyoweza kuwahadaa watu,na kuwadhulumu watu wasio kuwa na hatia, kwa ajili ya kufanikisha mambo yao…ni watu walioamua kujitoa kwenye utu, wakawa ni jamii ya mashetani, wametumia mitandao vibaya na hili kwa sisi watumiaji tunatakiwa tuwe na tahadhari sana na hii mitandao…’akasema.

Baada ya kusema hayo, ndio zikaanza taratibu mbali mbali za kimahakama, kwa mujibu wa kesi kama hizo, na baadae hakimu akatoa dakika kadhaa za mapumziko, na kesi ilipoanza tena, wakili mtetezi, akatoa hoja, kuwa mshitakiwa namba moja hali yake sio nzuri, angeliomba akapate matibabu kwanza, …

Muendesha mashitaka akasema; huyo mtu atataibiwa hapa hapa, tunao madakitari tayari, …au kama ana dakitari wake, ataruhusiwa kumtibia mbele yetu, kwasababu ya kuhakikisha ushahidi wetu upo salama…’akasema muendesha mashitaka na wakili mtetezi, akajaribu kutoa vipengele vya kisheria, kuhusu haki za mshitakiwa, na muendesha mashitaka akasema;

‘Haitachukua muda muheshimiwa hakimu..ni leo tu…’akasema na hakimu akaruhusu waendelee

‘Naona imeulizwa kwanini washitakiwa wana majina bandia, hatukuwataja kwa maina yao halisi…na ni kwanini majina yao halisi mpaka sasa hayajatajwa, …’akasema muendesha mashitaka.

‘Kwa kujibu hilo swali, kwanza tungependa kuwaita watu wawili, ambao wamehudhuria hii kesi, wao watatusaidia kwa hilo…’akasema docta, mawakili utetezi wakapinga kuwa hao watu wanaitwa kama nani, je ni kama mashahidi….na hakimu akamuuliza muendesha mashitaka kuwa hao watu anawaita kama nani…

‘Ndio ni kama mashahidi, lakini sio muda wao wa kutoa ..kuthibitisha hizo aka,kwanin tukawataka washitakiwa kwa kutumia hizo aka,…’akasema muendesha mashitaka…

Hakimi akasema hao watu waitwe, na mara wakaja watu wawili, kutoka nyuma kabisa,na wlipofika pale mbele wakasimama, na kuwageukia watu waliohudhuria humo ndani,…muonekano wao, ukawafanya watu waanza kelele, kila mtu akiongea lake,, wengine walibakia midomo wazi wakiwa hawaamini, watu hao walisadikiwa kuwa ni marahemu,…lakini zaidi ya hilo,….

‘Hao watu ni mapacha wa washitakiwa..?’ akauliza hakimu akiwaangalia washitakiwa na hao watu.

‘Hapana muheshimiwa hakimu, labda tuwahoji kidogo,  wajieleze wao wenyewe..’akasema muendesha mashitaka.

Akaanza kumuhoji mmoja wapo, na huyo mmojawapo akaanza kujielezea;

‘Mimi nilikuwa mfanyabiashara wa kuagiza vitu nchi za nje, siku moja nilipokuwa nyumbani kwangu muda wa usiku, mara nikavamiwa na wat nsiowajua, wakaninusisha unga puani, ..sikuweza kujitambua tena…na ndio nikachukuliwa kusikojulikana, nikapewa madawa nikawa sijitambui, hadi nilipokuja kutolewa hivi karibu,..sijui kilichokuwa kikiendelea….’akasema.

Na mwingine akasema hivyo hivyo….na docta akawaita ndugu wa hao watu wakaulizwa je ndugu zao hao walikuwa wapi, wakaelezea kuwa ndugu zao hao,walikufa..wakawazika..na watu wakaguna.

‘Kwa vipi, ..?’ hakimu akauliza, na hapo docta ikabidi aanze kutoa maelezo.

‘Hawa watu walichukuliwa kwa kitu kinachoitwa msukule, walitekwa kimazingara, na kwenda kufichwa kusikojulikana, nia ya hao waliowafanyia hivyo, ni kutumia sura zao kwenye kazi zao kama unavyoona hapo.

‘Hao washitakiwa wanafanana sura kamili na hawa wenye sura zao, walisadikiwa wamekufa, kumbe wenzao wanatumia sura zao kwenye mambo yao.

‘Sasa ilikuwaje, kama watu hao wanajulikana kuwa wamekufa, ..ndugu zao wakija kuwaona hawa wanaotumia sura zao, si watajua kuwa ndugu zao ndio hao, au inakuwaje hapo…?’

‘Kila wanachofanya wanachukua tahadhari zote kuwa hao ndugu hawataweza kuwaona kutegemeana na kazi yenyewe…ni wajanja, na wanapochukua sura ya mtu kufanya jambo fulani , wanahakikisha hawafiki sehemu yenye hao ndugu zao, …kuna namna nyingi tu kujificha,wanaweza kutumia mawani makubwa, nk…kwahiyo tahadhari hizo wanao muheshimiwa.

Muheshimiwa hakimu akawaangalia washitakiwa halafu hao watu walioitwa alikuwa akichunguza kama kuna tofauti yoyote, akatabasamu, halafu akamuangalia muendesha mashitaka,…

‘Endelea…’akasema.

***************
 Mimi nilikuwa nikiifuatilia kesi hii kwa undani zaidi, nikakumbuka jinsi tulivyoweza kumnasa huyo mkubwa wao, ilibidi zitumike mbinu za hali,..docta alisema kwa vile huyu jamaa anamtafuta huyo mdada, basi apatikane mtu wa kwao, ambaye anaweza kumtipu huyo mjamaa kuwa mdada yupo mahali fulani…

Ikafanyika hivyo, na kwa vile huyu jamaa alikwua akimuamini sana huyo aliyemtumia ujumbe, akaharakisha kuelekea sehemu hiyo, na docta alikuwa na laptop yake iliyokuwa na mtandao, wao, jamaa alipofia sehemu hiyo, akakuta mlango upo wazi.

Kwanza alisita kuingia, akasimama kwa muda, baadae akataka kugeuka kuondoka,..lakini akasita, kwa haraka akaingia kwenye chumba hicho akiwa na silaha zake za kutoka moshi, hakutaka kuzitumia kwa muda huo, hakutaka kumdhuru huyo mdada, kwani anamuhitajia kwa mambo yake..

Alipoingia tu, mimi nilikuwa nimejificha pamoja na mpelelezi, na nilitakiwa kwa haraka nimrushie huyo jamaa huo unga niliokuwa nao, jamaa alijiandaa kwa hilo , alikuwa kava maski….kwahiyo, isngeliwezekana..sasa tufanyeje.

Jamaa alipoingia akawa na simu yake, simu hiyo kumbe inaonyesha maeneo,..hilo docta alishalijua, akahakikisha kaharibu namna yoyote ya mtandao kuweza kunasa matukio humo ndani, kwahiyo simu ya jamaa ikawa hainyeshi ramani ya humo ndani, hapo akajua kanaswa, akageuka, akisubiria…

Mdada alikuwa kalala, …bado tulikuwa hatujamzindua tuliogopa tungeharakisha kufanya hivyo, ingelileta uzito fulani….jamaa alipoona hakuna mtu, akasogea taratibu kumfuata mdada…alipofika, pale akataka kutoa vitu vyeka,…ambavyo angempaka mdada na mdada angmfuata yeye kama zezeta fulani.

Hapo hapo mpelelezi akacheza, wakati jamaa anainama kutaka kumpaka huyo mdada hizo dawa zake, mpelelezi kwa haraka sana, akamvamia kwa nyuma, akitumia kitako cha bunduki, na kumpiga nacho jamaa kichwani..jamaa alitaka kugeuka na silaha zake, mimi nikatokeza na kumpiga mikono yake…na sekunde chache askari wakishajaa wakamzunguka.

Alipata kipigi kidogo,…cha kumlegeza, na docta alipokuja akamtoa hiyo maski, na akapa ule unga wa kumlegeza, ikawa ndio mwisho wa nguvu za huyo jamaa, ..baada ya kuhakikisha vitu vyote alivyokuwa navyo vimechukuliwa.


Akiwa kalegezwa viungo, lakini anaweza kuona, na kutambua , na hata kuongea , ila anaongea kilevi levi, akajaribiwa kuhojiwa kuwa yeye ni nani, lakini hakutoa sauti hata kidogo, akafungwa kama alivyofungwa msaidizi …na gari maalumu ikaletwa , kila mmoja na gari lake, wakafikishwa kituo maalumu, chenye ulinzi mkali, na ilihakikishwa hawabadili nguo au kufanya lolote, zaidi walilishwa kwa kutumia mipira maalumu.

‘Hawa watu wanatakiwa kufikishwa mahakamani kama walivyo…’akasema tena docta, na yeye na mkuu hawakuondoka eneo hilo hadi watu hao walipofikishwa mahakamani.

**************

Mimi , docta, na mpelelezi, tulibakia pale ndani, wakati jamaa huyo anaingizwa kwenye gari maalumu, na docta akawa analifuatilia hilo gari, kwa kupitia laptop yake, na baadae akanigeukia mimi na kusema;

‘Nataka hili zoezi la kumzidnua huyu mtu lifanyike mahakamani, kama litakavyofanywa kwa hao washitakiwa ili iwe ni moja ya ushahidi,..unaonaje..?’ akaniuliza mimi.

‘Aaah, docta ya kesho anajua nini, kwanini nisimuone huyu mdada…kama kweli yupo sahihi, huenda sio yeye, huenda wamemvika ngozi..mwenyewe hayupo…’nikasema.

‘Usijali tutamuomba mungu, maana haya sio kwa mapenzi yetu, na haya hatuyafanyi kwa kujionyesha, lakini yanahitajika mahakamani kama ushahidi na ukweli kuhusu huyu mdada ndio utaonyesha jamii, ubaya wa hawa watu, yeye ana mambo mengi sana, ambayo jamii inatakiwa iyajua,…’akasema docta.

Mimi niligeuza kichwa na kumuangalia huyo mdada pale alipolala, kiukweli sura aliyo nayo hapo, huwezi ukasema ni binti wa mzee…kuna utofauti kidogo, na anafanana fanana na yule binti wa facebook, lakini sio saana, kitu ambacho kilifanya nihisi huenda sio yeye, huenda walitaka kutumia sura yake.

‘Lakini docta huyu sio yule msichana wangu wa facebook..’nikasema.

‘Hilo utakuja kuliona huko mahakamani, kama sio yeye, huyo msichana wako wa facebook, atatokea..usijali..’akasema docta.

Ikawa ni kazi ya kumchukua huyo binti kwenye gari maalumu na kupelekwa sehemu ya kiusalama zaidi..na jengo hilo, sehemu hiyo ya kundi hilo, ikafungwa na kuwa chini ya ulinzi, hadi hapo itakatolewa amri nyingine.

Mimi na wenzangu tukaondoka kurejea majumbani kwetu, na wakati nataka kuondoka, docta akanisogelea na kusema;

‘Sasa kuna jambo moja nataka ukalifanye..’akasema.

‘Jambo gani…?’ nikauliza.

‘Nataka uende kule kwa mzee, ukajaribu kuongea na bint wa mzee, usikie ana kauli gani dhidi yako, nataka umweke sawa, maana kwa hivi sasa yupo na kimuhe muhe cha kumuona dada yake..kiukweli hata mimi paka sasa sijawa na uhakika kama dada yake ndio huyo au huyu ni mtu mwingine…sijaweza kuingia zaidi kwenye komputa na kumsoma, lakini nina imani kuwa ndio yeye…’akasema docta.

‘Docta, ina maana…’nikataka kusema.

‘Nishakuambia mimi sio docta wa ramli, mimi ni docta wa vidhibit, ni mpaka nifanye utafiti kwanza nichukue vipimo halisi nione matokea yake, ..vipimo halisi kwa sasa ni huyo mdada, huko mahakamani ndio tutapata majibu yake…’akasema docta.

‘Sasa huko kwa huyo mdada, nitasema nini,ukumbuke huyo mdada amekuwa kinichukia sana, ….kuwa mimi ndiye chanzo cha haya yote…’nikasema.

‘Sasa hivi ni tofauti, nia ni kutaka kujua, yeye, anakupenda,…’docta akasema.

‘Docta..’nikalalamika.

‘Nina maana yangu kubwa, ukumbuke kama huyo ndugu yake , ndio huyo, ..yeye alikuwa ni mchumba wako, ukamkana, je akisema hakutaki tena…’akauliza docta.

‘Docta, hayo ni ya zamani, nilishakuambia moyo wangu upo kwa mtu mwingine, siwezi kulazimisha kupenda mtu….’nikasita.

‘Una uhakika…?’ docta akauliza.

‘Uhakika gani docta…?’ akauliza.

‘Ndio maana nataka ukaongee na huyo mdada, ili haya mambo yamalizike kwa amani, ukumbuke wewe ndiye kwa namna moja uliyehusika na hiyo familia, wazazi, na familia nzima ilikuchukia wewe, ..ndio kwa hivi sasa hawatakuchukia kama awali, lakini bado una dhima, ya kuwaomba msamaha..umenielewa hapo…’akasema docta.

‘Lakini nilipenda wewe uwepo…’nikasema.

‘Nitakuwepo sana, lakini kwa sasa siwezi kuwaamini hawa watu, nataka hawa watu wabakia hivyo hivyo hadi kesho mahakamani, kama kuna dharura za kibinadamu, nitahakikisha nazifanya mimi mwenyewe kama docta…’akasema.

‘Docta na kuhus vile vifaa…?’ nikamuuliza.

‘Hahaha..usijali, hilo tuliweke kapuni kwanza…nitakuja kukuambia ni kwanini,naikibidi titavikabidhi mbele ya mahakama,..kwanini unaviulizia, …?’ akauliza.

‘Naulizia je bado mimi nitahitajika …kuvifanya vifanye kazi , nikiwa na bint wa mzee..?’ nikauliza na docta akainama kama anawaza, baadae akasema;

‘Tutaongea…’akasema na mimi nikaelekea huko kwa mzee, wakati huo docta akielekea huko walipopelekwa hao watuhumiwa!

*************

Sasa ikafikia muda muafaka, kuwatambua hao watu wawili mashukuri, watu walitikisa jiji, na kuweza kuleta tishio kubwa kwa jamiie eneo kubwa la sehemu inayojulikana kama makaburini.

Je hawa watu ndio hao kama walivyo..kama wanavyoonekana…, au ni akina nani hasa…maana majina yao yaliyoandikwa kama washitakiwa yanasomeka, kwa aka zao,...yaani kwa majina ya bandia,..na muda huo ulipofika muendesha mashitaka akamuomba muheshimiwa hakimu amuite docta aendelee kwenye shughuli hiyo muhimu.

‘Muheshimiwa hakimu, kama tulivyoomba awali, watu hawa wamekuja kama walivyo, ili kupata ushahidi halisi, mawakili watetezi, wamesema tunakiuka haki za kibanadamu kwa kuwashikilia watu hivyo hivyo kama walivyo,..lakini sisi hatukutaka tuwe na ushahidi wa video, unaonyesha shughuli zao nyingi walizokuwa wakifanya kwa sura tofauti tofauti, lakini sasa tunataka muwaone wenyewe walivyo, kutoka sura hii ya sasa hadi sura zao asili.

Labda kama wamejikosha, na kuwa tayari kutubu madhambi yao,tungeliomba mahakama yako tukufu iwasikie wakitamka wenyewe kwa kauli yao, kuwa wao ni akina nani,..maana sisi tumejaribu kuwahoji, wamekataa kuongea, labda muheshimiwa hakimu unaweza kutusaidia hilo..’akasema muendesha mashitaka wakati huo docta alikuwa akiwema mambo yake vizuri.

Hakimu aliwauliza hao watu wao ni akina nani..lakini watu hao walikuwa kama bubu, hawakutaka hata kuongea neno moja na muheshimiwa hakimu akatoa amri kuwa watu hao waondelewe hizo ngozi bandia walizojivika, ili uhalisia wao ugundulikane.

Wa kwanza alikuwa kiongozi…ambaye alikuwa ndiye muendeshaji wa shughuli za kila siku kwenye hilo kundi, lakini kawaida yake alikuwa hapatikani kazini muda wa mchana, yeye hupatikana huko kazini saa za usiku tu,…ni kwanini…..’ akasema muendesha mashitaka kama anauliza na docta akakohoa kidogo , na kusema;

‘Jibu lake tutalipata wakiwa kwenye uhalisia wake, jibu litajieleza lenyewe….’akasema docta.

‘Haya waondoeni basi hizo sijui mnasema ni ngozi, ili tuwaone hao ni watu gani,…’hakimu akatoa amri.

‘Tunaomba dakika chache tuweke mambo vizuri….’akasema docta, akiwasha laptop yake, akatoa waya ambayo aliupachika kwa mmoja wapo..na kuanza kulisha laptop yale, ….

Kwa muda ule watu walikuwa kimia wakitaka kuona kitakachoendelea, …
‘Tafadhali…, kwa vile ngozi hiyo anajivika sehemu ya juu, kichwni hadi mabegani, nyingine inaweza ikawa ya mwili mzima, kama itakuwa ni ya mwili mzima, basi hatuna budi kuficha baadhi ya sehemu ili kuhifadhi utu wa mtu…’akasema docta.

‘Sawa endelea…’akasema hakimu.

NB: Tutamalizia sehemu iliyobakia sehemu ijayo;


WAZO LA LEO: Tusikimbilie kuhukumu jambo kabla ya kupata ushahidi wake, maana hukumu huja baada ya kuthibitisha, unapohukumu jambo, kumbe likawa ni kinyume chake, sio kweli, utakuwa umemdhulumu huyo uliyemuhukumu, huyo ulisema kafanya, kumbe hajafanya,…ni vyema tukajiuliza je ningelifanyiwa mimi hivyo ingekuwaje!
Ni mimi: emu-three

No comments :