Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, June 12, 2017

MPENZI WA FACEBOOK-49


‘Ehee, wewe ndiye nakutafuta kwasasa, nashukuru umeniletea kitu muhimu sana kwangu, japokuwa vingine bado sijavipata hawa washenzi wameshindwa kazi, lakini nitavipata hivi karibuni, kwako wewe nataka hicho ulichovaa mguuni mwako…’akasema akimuangalia mdada mguuni.

Mdada akainama kidogo kujikagua, kabla hajainua uso, akawa keshavamiwa na kuinuliwa juu kwa juu.

‘Nataka hivi viatu, unasikia, baada ya kuvipata hivi viatu…, sidhani kama utakuwa na faida kwangu…mwenye faida kwangu ni dada yako…na sheria na utaratibu wangu utafuatwa, nitahakikisha, unabakia huku huku kuzimu..ukiwa miongoni mwa mizimu, unasikia…’jamaa akawa anaongea huku akiendelea kumzungusha mdada hewani.

Mdada hakujua ni kwanini anafanya hivyo, kumzunguisha hewani, badala ya kumvua viatu, yeye akaendelea kuziba mdomo na pua,…akichelea huo moshi usije kumuingia, moshi ulikuwa sio mwingi sana, lakini alishajua madhara yake, alipomuona huyo msaidizi wa mtandao, alivyofanywa na huo moshi!

Wakati bado anamzungusha hewani mara wakaingia askari, wakiwa na silaha, wakawa wanamuelekezea.

Huyo jamaa hakusituka, alichofanya, kwanza ni kumweka mdada chini, halafu kwa haraka sana, akawa kama ananyosha mikono juu, na kwenye koti lake sehemu ya viwiko vya mikono, kulitokea vibomba viwili, vikatoa moshi…na kwa haraka akawa kaam anakunja mikono mara mbili, kikatokea kibomba kingine cha ziada kikawa kinatoa moto…

Ule moshi, ukageuka kuwa moshi wa moto, ukaanza kuungiza vile vifaa walivyovaa askari, ni kitendo cha haraka sana, hata askari hawakupata muda wa kujihami, na mara askari hao wakadondoka sakafuni na kazimia…

Mdada kwa muda ule alikuwa anarudi kinyume nyume, kutafuta upenyo wa kukimbia, na alipoupata tu…akageuka na kuanza kukimbia…

‘Simama, nitakumaliza kwa risasi…’huyo jamaa akasema lakini mdada hakusimama, akawa anakimbia kama anapaa…hata mdada mwenyewe alishangaa kwa jinsi alivyokuwa akipaa hewani,  kwani vile viatu vilikuwa kama vinampaisha,akiinua mguu, anarushwa kwenda hewani…mbio mbio, na kutokezea sehemu ya ukumbi mwingine ambao ulikuwa umapangishwa na watu wengine.

Hapo akasimama, kwa mbali akamuona jamaa akimtafuta,….hakutaka kupoteza muda, akaanza kukimbia kuelekea nje ya jengo, na mara akajikuta uso kwa uso na Mkuu…

‘Wewe ulifuata nini huku…mbona mnatupa wakati mgumu kutekeleza majukumu yetu..?’ mkuu akamuuliza

‘Nilikuja kumfuata dada yangu…’akasema

‘Dada yako, dada yako yupi….?’ Akauliza

‘Ndio bado yupo hai..lakini huyo shetani kanizuia…’akasema

‘Shetani gani huyo..?’ akauliza

‘Huyo mkuu wao, manenda huko eeh, haya nendeni mkafe, kama hamjitaki…mimi huko sirudi tena,…’mdada akasema akigeuka nyuma kwa mashaka.

‘Nenda kakae kwenye lile gari pale,….’akaambiwa

‘Hapana mimi narudi nyumbani…’akasema sasa akiangalia usawa wa kupata bajaji, na mkuu msaidizi hakumzuia, …

****************

Mzee na mkewe walifika nyumbani, na wakaanza kuongea, maana huko njiani hawakuweza kuongea, kwa vile walikuwa kwenye gari la askari, ambalo lilitakiwa kuwafikisha hapo nyumbani, na ulinzi mkubwa uliwekwa kwenye nyumba yao.

‘Hivi ulimuelewa binti yako…’akasema mzee

‘Kuhusu nini,kuwa huyo dada yake yupo hai…?’ akauliza mama.

‘Ndio…nahisi bado akili yake haijamkaa sawa…’akasema mzee

‘Akili yake ipo sawa, sio yeye tu aliyewahi kusema hivyo,..hata huyo kiongozi wao, aliniambia hivyo,…’akasema

‘Ukamuamini, hujui kuwa alikuambia hivyo ili kukuteka mawazo yako…’akasema

‘Aaah, hata sijui,….kama yupo hai tutampata tu, ilimradi wawakamate hao watu, maana sitakuwa na amani mpaka nisikie wote wamekamatwa, hasa hao watu wawili wakubwa zao....nasikia mzee , kafariki, maana huyo naye,..mmh, hata siamini kuwa nay eye alikuwa miongoni mwa hilo kundi…’akasema mama.

‘Kwanini usijue na wewe ulikuwa mwanachama…?’ akauliza mumewe

‘Ina maana hujaniamini..mimi niliingizwa kichwa kichwa kwa ajili ya kuwapata hao mabinti, lakini mambo yao ya ndani mengi nilikuwa siyajui…nimeipata hiyo taarifa wakati wananiachia huko gerezani, nikasema kama alikuwa miongoni mwao, afadhali iwe hivyo….’akasema mke

‘Basi sasa nimesikia…maiti yake ilikuwa haishikiki…ilioza kwa siku moja…’akasema mzee.

‘Alikuambia nani..?’ akauliza

‘Kuna docta mmoja aliyekuwa akishughulia maiti yake…’akasema

‘Ndio watu waone, jinsi gani wachawi wanavyoadhibiwa hapa hapa duniani, unajua wakati wanafanya mambo yao wao hujisahau wakajiona wataishi milele, kumbe ipo siku watarejea kwa mola hakimu wa mahakimu,..…’akasema mama.

‘Huyo docta anasema wakati wanakwenda kumchukua, walipompima, awali kabisa, walimuona hajakara roho, lakini mwili umeshaanza kuoza,  alikuja kukata roho baadae, na wanasema kwa hali aliyokuwa nayo, alikuwa anapata maumivu makali sana…’akasema.

‘Hata sitaki kumuwazia, maana siwezi kuamini mtu tuliishi naye vyema, alikuwa kama ndugu yetu , halafu anakuja kutufanyia hivyo, siwezi hata kuamini..’akasema mke.

‘Halafu sikiliza sasa, kutokana na hali yake, walitaka kumzika haraka haraka,..maana sio kumzika tena, ni kumfukia,….nasikia hata kaburini lake, lilikuwa na vituko, kwani waliposhusha kaburini tu….wakiwa wamemuweka madawa makali ya kupunguza harufu, lakini harufu ya uozo, ilikuwa haiishi..na wakati wanaanza kumfukia, mara kutokea nyoka kutoka aridhini wakamzunguka,….’akasema

‘Oh, watu hawajakimbia…?’ akauliza mke

‘Walifukia kwa haraka haraka wakaondoka, hakuna aliyetaka hata kukaa humo zaidi…’akasema

‘Mungu, kweli adhabu ya dhalimu, huanzia hapa hapa duniani…’akasema mama

‘Sasa hawa watoto, maana mimi nimeshaanza kusema watoto, kama vile kweli huyo binti yetu mkubwa bado yupo hai…’akasema

‘Yupo hai bwana…’akasema mama, na mara mlango ukagongwa

‘Ni nani huyo tena, ni askari au ni mgeni..?’ akauliza mama

‘Ngoja niwapigie simu askari tuwe na uhakika, …

‘Fungua ni mimi mama, ni mimi baba…’sauti ya kike ikasikika nje.

*********************

Mkuu akaanza kuwasiliana na watu wake wa ndani lakini hakupata jibu, na mara docta akampigia simu.

‘Vijana wangu hawapatikani..’akamwambia docta

‘Wamelishwa moshi wa huyo jamaa, kama nilivyokuambia wawe makini sana na huyo mtu, ukasema wamevaa kinga, hizo kinga hazifui dafu na huo moshi wa moto wa huyo jamaa, na kwasasa ….mkichelewa hamtamuona tena huyo mtu, …’akasema

‘Kwani kwasasa hivi yupo wapi..?’ akauliza mkuu msaidizi

‘Anarudi ndani, nahisi anataka kumfuata msaidizi wangu, au bado anamtafuta mdada, binti wa mzee….’akasema docta

‘Wa nini…?’ akauliza

‘Wa nini, kwani kilichomleta humo unafikiri ni nini, yeye anamtaka huyo binti, awakutanishena msaidizi wangu, ..wakati akiwa keshavipata hivyo vifaa vitatu,,..akimali hilo basi hatawezekana tena…’akasema

‘Sasa atavipataje na wewe unavyo huko?’ akauliza

‘Kuna mzindiko yao walitarajia watayafanya, lakini huyo jamaa hajui kuwa nimeshayamaliza nguvu, kama mzee angelikuwa hai angeliweza kumsaidia,,lakini kafanya haraka kumua, msadizi wake wa nguvu za giza.

‘Oh, sasa unafikiri atafanyaje..?’ akauliza

‘Zaidi ni kutumia nguvu, lakini hana ujanaj kwa hizi sasa, muhimu ni kujitahidi kuwa mbali naye hadi tumtege kiaina..’akasema docta.

 ‘Kwahiyo unataka tufanye nini huku, maana sisi tulitaka tumuingilie tumshike…’akasema.

‘Mtamshikaje, huoni, ilivyotokea kwa askari wako, hapo hajataka kuwamaliza angelitaka angewaua wote…’akasema docta.

‘Kuna mbinu nyingi za kumkamata, sema nakusikiliza wewe kwa sasa…’akasema huyo mkuu msaidizi.

‘Ni kumtega tu….tumsubirie akiingia kumfuata huyo kiongozi, basi tutafunga mlango,..tatizo ni kuwa askari watakao kuwa humo wanaweza kuuwawa…’akasema

‘Siwezi kuruhusu askari wangu wauwawe….kama ni hatari kihivyo ni bora tutumie nguvu.

‘Mkuu ukutumia nguvu, hutafanikiwa, ushahidi wote wa harakati hizi utapotea, na huyo jamaa ni mjanja, akitoka nje, hutampata tena…naonelea mimi nije huko, najua jinsi gani ya kuzi-zimisha nguvuu za giza za huyo jamaa.

‘Lakini ukija huku sisi tutapataje taarifa za ujumla, wewe ukiwa huko ndio unatuona mbashara kila mtu na katika sehemu tofauti tofauti…’akasema mkuu msaidizi.

‘Usijali, kazi iliyobakia sasa ni ndogo, muhimu kwasasa wasiliana na muendesha mashitaka muambie kazi imekamilika, awasiliane na hakimu , kesi hii ifanyike haraka iwezekanavyo, …’akasema.

‘Hakimu aliyekuwa akisimimia hii kesi kapatwa na dharura, ..kasafiri, labda tuombe hakimu mwingine…’akasema.

‘Itakuwa vyema, …hakimu yule wa kwanza ataikwamisha hii kesi, hakikisha unampata hakimu mwenye msimamo, maana kesi hii imegubikwa na sintofahamu nyingi…’akasema docta.

‘Hilo litafanyika, nawasiliane naye tukimaliza mawasiliano na wewe…’akasema.

‘Sawa vinginevyo, hawa watu watayeyuka na hatutaweza kuwapata tena, na hii inaweza kuleta balaa kubwa baadae,…’akasema.

‘Kwanini watayeyuka….sioni ni kwanini tukiwamakata wanakwenda jela kwenye mikono yetu hawawezi kutoroka tena…’akasema.

‘Mkuu, haya mambo yasikie tu, hawa watu ni wajanja sana, na daa yao ni hiyo usiwape muda,..kesi ifanyike haraka iwezekanavyo,..maelezo zaidi ….utayapata huko huko..kwa hivi sasa siwezi kukupa jibu la uhakika, tusipoteze muda, wewe unaweza kuendelea na vijana wako, ila wasifanye haraka kutumia nguvu…mimi nakuja huko huko…’akasema docta.

‘Na huyo binti wa mzee,…tutamfanyaje…maana askari wanasema bado hajiwezi, anahitajiak huduma za haraka….kwanini tusimuwahishe hospitalini?’ akauliza huyo mkuu.

‘Huyo atapona tu,… tiba yake sio ya hospitalini, hapo alipo kalegezwa na madawa ya mzee marehemu…’akasema docta.

‘Kama ni madawa ya huyo mzee marehemu, ataponaje na wakati huyomzee mwenyewe hayupo duniani tena…?’ akauliza

‘Ndio maana nataka kuja huko..’akasema docta

‘Ok, sawa ngoja nifanye ulichoagiza…nina hamu sana ya kukutana na hao watu wawili , wamenisumbua sana akili yangu, najua wapo wengi, lakini yeye atakuwa ni funzo kwa wengine wote…’akasema mkuu msaidizi.

‘Ni kweli,… utakutana nao tu mkuu,…, hutaamini macho yako…’akasema docta,na kukata mawasiliano

**************

 Msaidizi wa docta, akachukua leso yake, akaziba mdomo na puani, huku sasa akiukimbia ule moshi, ulikuwa kama unamkimbiza, alipofika mbele akaona mlango wa chumba ukifunguka, nay eye bila kujiuliza akaingia kwenye hicho chumba ule moshi, ukapita..yeye akafunga mlango….na wakati anajiuliza;

Mara akashtuka mtu anamshika begani, akageuka kwa haraka, akakutana uso kwa uso na askari.

‘Usijali upo mahali salama….nimepewa taarifa unakuja..pole na majanga…’askari akasema, na msaidizi akageuka na kuwaona askari kama watano wapo humo ndani, na pembeni alikuwepo yule kiongozi aliyekamatwa awali, aliyeweza kupata bastola na ufunguo kwake, ..na jamaa alimuangalia kwa macho yaliyojaa hasira,

Akakumbuka jinsi gani alivyoweza kumshinda ujanja huyu jamaa…na kuvichukua hivyo vitu kwa kirahisi akimuacha akikamatwa na polisi….hakutaka kuliwazia hilo sana, akageuka na kusema kimoyo moyo;

 ‘Oh..hii maana yake ni nini…’akatulia kwa muda.

Wakati yupo na hao askari humo ndani, ndio wazo likamjia, akaamua kuwasha simu yake, ambayo muda mwingia alikuwa kazima, ilipowaka tu, akakutana na mlio wa siku anapigiwa,..

‘Wewe hebu zima simu yako….’akasema askari mmojawapo.

‘Oh, samahani napokea taarifa muhimu kutoka kwa docta na mkuu msaidizi…’akasema na yule askari kabakia kimia…

‘Docta hapa….sasa fanya hivi …rudi pale ulipotoka, kamuokoe mpelelezi, kabla hajavamiwa na hao watu, kuna wasaidizi wameitwa wa huyo jamaa kuja kumkomboa kiongozi wao,yeye mwenyewe anaonekana hataki kujionyesha, kajificha kwenye chumba kimojawapo, hakikisha ukienda kumchukua mpelelezi uwe umeziba mdomo na pua..’akaambiwa

‘Kwanini wasiifanye hiyo kazi hawa maaskari

‘Sina uhakika nao, wewe fanya nilichokuambia, nina maana yangu…’akaambiwa na msaidizi hakupoteza muda, akatoka mle,..askari hawakumzuia inaonekana walishaambiwa wamruhusu atoke..

Haraka haraka msaidizi, akatoka mle, hakukuwa na moshi tena, akarudi kule, na kweli alimkuta mpelelezi kalala sakafuni, akamshika, ..akajitahidi mpaka akamuweka begani, akaanza kutoka naye, kwa haraka hadi kule kwenye chumba alichokuwa awali..na alipofika tu, docta akampigia simu
‘Sasa chukua huo unga kidogo aliokupa huyo mzee, mpake puani…’akaambiwa akafanya hivyo, na mara mpelelezi akazindukana,…

‘Kuna nini…’mpelelezi akauliza

‘Mapambano yameanza, …’akasema msaidizi na mpelelezi, kwa haraka akasimama na kujinyosha, akageuka kuwaangalia maaskari waliokuwemo, nahisi alitaka kuwamba silaha, lakini akajizuia

Simu ikapigwa tena alikuwa ni  docta akamwambia,…

‘Sasa jitahidini mtoke hapo, waacheni hao askari, wataendelea kufanya yao, sisi hatuingiliani na wao, …mkitoka hapo, tembeeni hatua chache, karibu na chumba mlipokuwa awali, mkifika hapo, nitawafungulia chumba, mtaingia humo, na humo mtapata maelekezo zaidi,fanyeni haraka kidogo, kabla hao watu walioitwa hawajaingia huko.,…’akasema.

 ‘Sawa bosi…’akasema msaidizi, yeye na mpelelezi wakatoka na kunza kurejea kule walipokuwa awali, na kabla hawajasogea hatua chache…, mara kwa mbele wakaona askari wakija.

‘Hawa wanaonekana kama sio askari…’akasema msaidizi, na mpelelezi, akaguna kwanza halafu akasema;

‘Ni kweli, hawa watakuwa watu wao wamevaa sare za usalama…sasa hapa hatuna muda wa kupoteza tugeuka turudi kwa haraka…’akasema mpelelezi.

Wale watu waliovalia ki-askari walipowaona hawa watu wawili wakaanza kuwafuata, ikawa sasa kazi ya mpelelezi na msaidizi kurudi mbio, hadi chumba kile walipotokea, walipofika tu mlango ukafunguliwa wakaingia.

‘Mnakuja kuvamiwa…’wakasema , kuwaambia askari waliokuwemo humo ndani.

Askari wakajiweka tayari, na mara docta akapiga simu,…

‘Ni kweli hao sio askari, ni watu wa huyo jamaa, mumefanya vyema kukimbia kurudi , sasa ni kazi ya hao askari kupambana nao,…sasa wewe fanya hivi, kwenye hicho kichupa chenya unga mwekundu ulichopewa, nenda kampake huyo kiongozi wao,aliyeshikiliwa na polisi, fanya haraka,..’akaambiwa, na msaidizi akafanya hivyo.

Alipomsogelea huyo jamaa, alikuwa kafungwa imara kabisa, na alipomuonamsaidizi anakuja akiwa kashikilia kichupa , akajua ni nini anafanyiwa, akainamisha kichwa kuficha uso wake, lakini akisaidiwa na askari akainualiwa uso, na alipopakwa huo unga puani, akalegea,… na kupoteza fahamu.

Docta, akasema,

‘Kwahivi sasa huyo sio tishio kwenu kwa muda,…ni mtu hatari sana huyo akipata mwanya, na ilivyo, anatakiwa kufikishwa mahakamani akiwa hivyo hivyo…’

Huko nje kukawa kunasikika milioa ya risasi,na haikupita muda, askari wakaja na kusema,

‘Tumeshawamaliza,..iliyobakia, sasa ni kumtoa huyu mtu hapa ndani…’akasema kiongozi wa kundi hilo linalomlinda huyo mshukuwa ambaye alikuwa kiongozi wa shughuli nyingi za hilo kundi.

‘Wasimtoe mpaka nifike..’docta akasema kwenye simu akiongea na msaidizi na msaidizi akamuambia mpelelezi.

Mpelelezi akasogea mbele ya huyo jamaa na kusema;

‘Huyu mtu hatoki hapa kwa hivi sasa.

‘Kwanini…mnazuia..?’ akauliza askari mmojawapo

‘Afande huyu ni lazima tumtoe humu, ni hatari akiendelea kukaa humu ndani,..’akasema

‘Nimesema huyu hatoki humu, …nieleweni hivyo..’akasema mpelelezi na kukawa na kubishana fulani hivi hadi mkuu alipopiga simu, kuwa huyo mtu asitolewe humo ndani.

Na haikupita muda, kiongozi wa kikosi hicho cha humo ndani akaamriwa atoke akaonane na mkuu….alionekana kakasirika, lakini amri ya mkuu ni moja, …

‘Huyu atakuwa ni kibaraka…’akasema msaidizi wa docta

‘Wapo wengi…’akasema mpelelezi

‘Unawafahamu…?’ akauliza msaidizi

‘Sio rahisi kuwafahamu, watu hawa wana mtindo wa kuhakikisha watu walichukuliwa kwenye usalama, hawajuani…ni siri ya mtu mwenyewe…’akasema

‘Kwanini sasa umekuja huku na wewe bado unaumwa…?’ akaulizwa

‘Ninataka kusafisha jina langu, ..najua sitaeleweka, lakini nilifanya mengi kwa masilahi ya familia yangu, nikakiuka amri za kazi yangu…’akasema

‘Mimi sioni kosa lako, maana ulifanya kwa masihali ya familia, usingelifanya hivyo familia yako ingedhurika, au sio…?’ akasema msaidizi.

‘Kwako wewe hulioni hilo kosa, lakini ndani ya sheria za kazi yetu ni kosa kubwa, kuna makosa nimeyakiuka, na sizani kama itakuwa rahisi kwangu kusamehewa…’akasema

‘Usijali , tutakusaidia,…’akasema msaidizi, na mara simu ikalia, alikuwa ni docta tena

‘Nimeshafika nipo huku nje, …na namuona jamaa yao, anatoka kwenye kile chumba sasa hivi kavalia kama askari, keshajua kuwa kazungukwa, sasa muwe makini sana…nilitaka mfike kwa mdada lakini haitawezekana kwasasa.

‘Sasa tufanyeje,…?’ akauliza.

‘Nakuja huko huko ndani, TUMALIZE KAZI….’akasema docta kwa kujiamini kabisa.


NB: Tutamalizia sehemu ijayo... kama hitimisho la kisa hiki!

WAZO LA LEO: Mtu anapokalia kiti cha dhuluma, hujisahau akaona yeye ni yeye tu, na watu kama hawa ukiwagusa wanasema ‘Unajua mimi ni nani…’ mimi ni nani maana keshajitolesha kuwa yeye ni juu ya sheria, lakini wapi , hata siku moja dhuluma haidumu,…

Jamani tusijisahau kihivyo, hata kama tunazo, tunautawala, au sisi ni mabosi kwenye ofisi, tukaanza kuwanyanyasa wenzetu , tukawadhuluma wengine haki zao, kwa kutumia ubosi wetu...

Hala hala ndugu bosi...kumbuka hili,...hata kama utafanikiwa sasa hivi, ukawanyamazisha hao wanyonge, ukafanya ulichofanya, ...wanyonge wakakosa haki yao, wewe ukaonekana bosi mwema, kwa tajiri wako, hujashinda, maana huo sio mwisho wa dunia..., haki, ya mtu ipo pale pale…, na mungu atairejesha kwa huyo mnyonge kwa namna ambayo huwezi kutegemea kabisa..na wewe utalipwa mabaya kutokana na dhuluma yako hiyo, wangapi wangapi tumewaona.... Tumuombe mungu atulinde, na atuongoze kwenye njia sahihi, anayoirizia yeye mwenyewe,…Aamin.

Ni mimi: emu-three

No comments :