‘Ni
nini hicho…?’ akauliza mdada baada ya kuona alama nyekundu ikitokea kwenye
komputa na ikifuatiwa na herufi nyingi zilizojipanga kwa pamoja, hadi zikaajaa
kwenye uso wa hiyo komputa..,
‘Ni
ishara ya hatari…’akasema huyo jamaa akihangaika kudonoa batani za haiyo
komputa ilikuwa ni desk top…, lakini pamoja na utaalamu wake haikuwezekana
kufany alolote,…akaishia kusema;.
‘Hatari,
hatari..hatari….mungu wangu ….’akasema hivyo na kushika kichwa
‘Hatari
gani hiyo…..?’ mdada akauliza mdada, naye akihisi mashaka, akilini mwake isije
ikawa ni bomu likaja kulipuka na kuwamaliza wote humo ndani, hakuwa na mawazo
mabaya mengine,.. na jamaa sasa akijaribu hata kuzima komputa huku akisema;
‘Mtandao,
umekula mzinga,…hapa sina ujanja tena,….umeharibika kabisa…oh, sasa hili ni balaa
jingine, hawa jamaa sijui kama watanielewa….’akasema
‘Kwani
ni kosa lako, si utawaambi ukweli ulivyo….’akasema mdada.
‘Wewe
huwajui hawa watu, wao wanajua kuwa mtu hakosei, ..na hata sio kwamba nimekosea
mimi, hii ni virus, imetumwa na…, najua huyu atakuwa ni docta tu, …’akasema
‘Docta,
docta atahusikanaje na hilo tatizo, msimsingizie mtu wa watu,…hayo ni mambo
yenu mabaya, sasa yanaaza kuwarudia wenyewe…’akasema mdada.
‘Oh,
sasa nitafanya nini, na huyu bosi akisikia hivi, na..unaona hii alama hapa,…sasa
hii ni hatari, na kiongozi hayupo, …mtaalamu ndiye alikuwa anaweza kupambana na
hawa watawala wa hili kundi,…sasa mimi nitasema nini….’akatulia akiangalia
alama nyingine ya kama kitaa chekundu, inawaka na kuzimika.
‘Mh….jamaa
huyo …keshaingia ndani ya ….jengo, ..unaiona hii, hii ndio alama ya huyo bosi mkubwa,
ikialika hivi, ujue yupo karibu, na sio karibu, yupo humu ndani,…’akasema
‘Itakuwa
afadhali na mimi nimuone, huyo shetani, na nikikutana naye, sijui..ataniambia
wapi dada yangu alipo, na kwanini walimfanyia hivyo,na kwanini wanaifuata fuata
familia yangu…aje mimi nipo tayari kukutana naye..’akasema mdada
‘Mungu
wangu, wewe dada wewe, hapa ni kuomba tu, dua yako ya mwisho, ilivyo, huyu mtu
akikutana nawe, hataki uje umkumbuke, ina maana akija kwako, akimalizana na
wewe anakuacha ukiwa maiti…haonekani ovyo ovyo kikazi, …’akasema
‘Kwani
yeye, mungu, yeye ni malaika mtoa roho, acheni imani zenu za kishetani…’akasema
mdada.
‘Hata
sijui nikuambieje..unaona, ni kama anakuja huku….haonekani, anaonekana kwa alama
hii,..yupo,na sio mbali..anakuja huku..huyu, oh, sasa mdada, mimi sikai hapa
tena…’jamaa akasema akijaribu kusimama, akaanguka, alikuwa kasahau kuwa
kafungwa miguu..
‘Unataka
kwenda wapi….?’ Mdada akamuuliza akimsaidia kusimama
‘Wewe
tuondoke hapa, ..huyu mtu akiingia humu, sizani kama atatuacha hai,….’akasema
‘Usiogope
mimi nitapambana naye, na isitoshe, polisi wapo, watamkamata ….’akasema mdada
‘Hawa
polisi wenu, hahaha..nisiseme mengi, unajua, hapa walikuwa wakimuogopa
mpelelezi, huyo mpelelezi akaja kuwekwa sawa, …akaja huyo msaidizi wa mkuu, …nay
eye utasikia, vumbi lake, anajifanya haingiliki, wamesha muanza kwenye familia
yake..’akasema
‘Kwa
vipi…?’ akauliza
‘Utamuuliza
mwenyewe….’akasema akijaribu kujifungua hizo kamba, na mdada hakutaka kumzuia,
akawa anamuangalia tu.
‘Dada
tafadhali, hii alama inaashiria kuwa huyu jamaa anakuja huku…mimi nakuomba sana
unisaidie,…tuondoke hapa, haraka…’akasema, na akageuka kuangalia mlangoni na
mdada naye akageuka kuangalia huko……
Tuendelee
na kisa chetu
**************
Wakati
huo huo mzee na msaidizi wa docta walikuwa wakikodoa macho kuangalia mlangoni,
wakisubiria hicho kitakachoingia, ….na mzee akawa anahangaika, ni kama vile mtu
anahisi pumzi kumuishia mwilini, …
‘Mzee
vipi una nini…?’ akauliza msaidizi.
‘Jamaa
akanitupia kombora…ooh,,,kokoko..oohhh…’akawa anahangaika kuzuia kitu , ni kama
kameza kitu anajaribu kukitoa lakini hawezi.
‘Kakutupia
saa ngapi, na kwanini afanye hivyo, wakati anataka kuonana na wewe ili muweze
kufanya mambo yenu….’akasema
‘Si-s-jui
kwanini anafanya hivi, nahisi haniamini tena….’akaweza kuongea lakini sasa
akawa anatoa jasho jingi,
‘Sasa
mzee tufanyeje, maana mimi siwezani na mambo yenu ya kishirikina..?’ akauliza
lakini mzee alikuwa kimia akitoa jicho kama vile kaona kitu cha kutisha mbele
yake, kijana aangalia huko anapoangalia mzee, lakini yeye hakuona kitu.
‘Mzee,
sema..sema kitu nikusaidie, …’akasema, na mara wakasikia sauti ya mtu anatembea
kuja muelekeo wa mlangoni, lakini kukatulia hakuonekana mtu, ..ila baada
kidogo, kukaanza kuonekana dalili ya moshi…ulianza kidogo kidogo sasa ukawa
unakuja kwa kasi.
‘Wewe
una leso…?’ akauliza
‘Leso…leso
ni moja ya nguo zangu siwezi kutembea bila leso,…!?’ akauliza msaidizi n
akuongeza maneno hayo
‘Ziba
mdomo wako na pua, hakikisha hufungui, huo moshi ukiingia ndani ya mwili wako
unapoteza fahamu, …’mzee akasema na yeye akaziba mdomo wake kwa shida, maana
mikono ilikuwa ikimtetemeka…na msaidizi akafanya hivyo hivyo,…ule moshi,
ukaanza kutulia kidogo kidogo baadae ukaisha.
Mzee
akiwa bado anatetemeka mikono, akatoa vitu ..ilikuwa vichupa viwili vyenye unga
unga ndani yake..akatoa unge kwenye kichupa kimojawapo na kumuambia msaidizi,
paka hii puani…
‘Hapana
mzee, sijawa tayari na mambo yenu, mpaka mtimize masharti yangu…’akasema
‘Paka
hii puani, na machoni…sasa hivi hakuna muda tena na mambo hayo, huyu mtu kaja
kwa shari, ..keshanichokoza, nataka hizo sumu zake zisikuathiri na wewe…’akasema
akihema kwa shida, na msaidizi akafanya hivyo kwa kusita sita, akajipaka, na
baadae akauliza..
‘Hivi
huyo ni nani, mpaka umuogope hivyo..?’akauliza
‘Ni
mwenyewe, yeye hutumia moshi kuzimisha watu…’akasema
‘Oh,
kwahiyo…keshafika au sio, safi kabisa huyo huyo ndiye wakumkamata atuambie
mdada yupo wapi, la sivyo tunawaita polisi….’akasema.
‘Polisi..hahaha..hivi
hujanielewa…sikiliza nikuambie kitu, usitamani kukutana na huyo mtu, ni bora
uonekane muogoa, sas ahivi kaja kama yeye, akiwa huko duniani, aah, ni mwema
sana,..mimi sijawahi kukutana naye uso kwa uso,..labda akiwa huko duniani,
maana huko huwezi kujua yeye ni nani…’akasema.
‘Una
maana gani huko duniani, kwani sisi tupo wapi…?’ akauliza.
‘Hahaha..kohokohokoho…aah,….’mzee
akawa anakohoa kwa shida, na ikaonekana damu zikitoka mdomoni.
‘Mzee
upo sawa kweli, unahitajika ukamuone docta….tutoke hapa, utakufa mzee….’akasema.
‘Tumeshachelewa
hapa,..sina dawa ya kunisaidia, ningelikuwa kwangu, huko duniani, ningeliweza
kujisaidia, hapa,..hata mizimu imekaa kimia,..nahisi imenisusa, nimeshindwa
kutimiza makafara yao..’akasema.
‘Sasa
mbona haji…’akasema msaidizi, na mzee akainua uso kumuangalia , uso
ulishabadilika,macho yameshabadilika, ..yanatisha..hadi msaidizi akasogea nyuma
‘Mbona
umekuwa hivyo, kama shetani….’akasema na mzee akawa kimia.
‘Hawezi
kuja hapa kwasasa hivi anajua huku keshamaliza kazi, nahisi sasa hivi anakwenda
kwenye mitambo, kuhakikisha kila kitu kipo sawa, …atahakikisha kaharibu kila
kitu ili kuondoa ushahidi, au kuna kitu muhimu kakigundua ambacho ni cha maana
zaidi ya sisi hapa…..’akasema.
‘Kama
nini..kaona nini….?’ Akauliza.
‘Siwezi
kujua, labda..kati ya vile vitu vitatu, au yule binti ambaye ni muhimu sana
kwake, wewe atakufuata baadae, ….’akasema.
‘Binti
gani, huyo ambaye alikuwa marehemu,…safi kabisa,.. kama ni yeye mzee huoni kuwa
atatusaidia, akija hapa mimi nitajificha,a kitokeza tu, namvamia kwa nyuma,
unaonaje hiyo plani..usiogope mzee, upo kijana ngangari..mimi sasa hivi nina
miaka,..ooh, mzee, ishirini tisa…ningelishaoa zamani, lakini ndio hivyo tena.
‘Na-nakujua
sana, ni zaidi ya hiyo miaka…sa-sa hatuna mu-da…’mzee akawa anaongea kwa shida..
‘Mzee
twende ama tutoke humu, au twende tukapambane tumuokoe binti mikononi mw huyu
shetani,…naona na wewe …unatisha mzee, sura imekua kama sio yako….’akasema.
‘Sikiliza
kijana sasa sio muda wa kunibishia, nataka nikuokoe kwenye hili janga, najua
huko mbele utakuja kunikumbuka na kuniombea, najua nimefanya mengi mabaya,
lakini hata zuri moja jamani..haaa, naona wahenga wananiita…unawaona wale….’akasema
mzee akiashiria kwa kichwa na msaidizi akaangalia hakuona kitu.
‘Mzee,
vipi mbona unaanza kunitisha, mimi sioni kitu …nahisi mwili unasisimuka
tu..nywele zinanisimama.
‘Si
umesema wewe huogopi…’mzee akasema.
‘Aaah,
ni kuhusu afya yako mzee, kwangu usijali..nakuogopea wewe, ila nahis mwili
unanisisimuka, ni kama kuna kibaridi fulani hivi….’akasema.
‘Na
mimi najalimaisha yako kwa sasa…sasa hivi, sina mdua, sikiliza,…unaona hicho
kinapita hapo,…’akasema mzee akiashiria kwa kichwa.
‘Mbona
sioni kitu mzee…’akasema akiangalia huku na kule.
‘Sawa
subiria utakiona …hicho hicho….ndio yeye, kapita, anaelekea huko juu, nahisi
anajua keshatuzimisha, na kwa vile hana umuhimu na sisi kwasasa ndio maana
kapita, ila akirudi, atahakikisha kanimaliza na wewe atakuchukua…’akasema.
‘Oh,
sasa mambo gani, kwahiyo unasemaje, maana mimi sasa nachoka, lengo letu
halijatimia, haya huyo mshenzi keshafika, ..na huyo, nikikutana naye mzee, mimi
simpi muda, …chochote nitakachookota ni saizi yake, ..humu ndani kuna
nini…’msaidizi akasema akigeuka huku na kule, akaona chuma …ilikuwa nondo fupi
iliyokatwa.
‘Sasa
mzee mimi nina silaha sema tufanyaje…tutoke nje ukatibiwe au tukapambane
kiume..mimi sijali, …kama kufa, tutakufa tu, lakini tusikubali,…tupambane
kiume..’akasema msaidizi.
‘Kijana,
kijana,…hapa silaha ni nguvu za giza, mwenzko huyo atakuwahi hata kabla
hujamkaribia, uliuona huo moshi, akiupilizia…, kama anataka kuku-ua mara moja,anauwasha
moto, ..sasa ule moshi unakujia huku unawaka moto…ukikuingia unaunguza vitu
vyote ndani ya mwili wako…’akasema.
‘Hatari…’msaidizi
akasema, ni kama vile haamini, na mzee akatikisa kichwa, kusikitika, akasema.
‘Kijana…hujui
upo wapi, hujui hatari gani ipo mbele yako, upo upo tu, sawa, sio kosa lako,
lakini sasa…sikiliza kwa makini, wewe si huogopi…’ mzee akauliza.
‘Kwanini
niogope mzee, huo moshi, ukija wa moto, nitaiba mdomo, au sio nitamuomba mungu
wa wote, atatulinda, kama siku imefika, basi mungu atupe mwisho mwema, ndio
hivyo tu mzee kufa tutakufa sote, siku ikifika haina mjadala, ..ndio maisha ni
mzuri, lakini hatuna mamlaka ya kuzuia kifo,..mimi nimeshaanza kuogopa
kidogo..sijui kwanini…’akasema.
‘Sasa
sikiliza lolote laweza kutokea, kwa hivi sasa …’akasema na akaanza kutoa vitu
mfukoni, akatoa vichupa viwili,…
‘Hiki
chenye unga mweupe, ni kwa ajili ya kumzindua yule mdada …tuliyekuja kumuona,
amehamishwa hapa sijui kapelekwa wapi, nahisi huyo jamaa ndio
anamtafuta,..akimpata atakuja kukuchukua na wewe..mimi sizani kama nitaweza
kupambana naye tena, keshaniwahi….sasa sikiliza usiongee sana…’akasema
alipooana msaidizi anataka kuongea.
‘Huyo
mdada hataweza kuzindukana kwenye hiyo hali, ni mpaka umrushie huu unga, huku
ukisema maneno haya….’akawa anaghani maneno , kama anaimba vile.
‘Hebu
yarudie,….’akasema na msaidizi akayarudia yale maneno vile vile kama alivyokua
akisema huyo mzee, uafikiri ndio huyo mzee anayaghani.
‘Safi
kabisa, wewe una akili sana…ningelikuwa mzima, ningekufundisha mambo mengi,
lakini sitaweza kuwa nawe tena…sikiliza kwa makini maagizo yangu haya, huyo
mdada hataweza kuinuka mpaka umtupie huu unga na wakati unafanya hivyo, ughani
hayo maneno, halafu umuombe mungu wako, unachokusidia, kwanza kuwa huyo mdada
azindukane, halafu hilo lililo moyoni mwako, …muda ukiomba chochote unafanikiwa…’akatulia
akichukua kichupa kingine.
‘Na
hiki nyekundu rangi nyekundu,..ni silaha, akija adui yako mrushie usoni,
ataishiwa nguvu atadondoka…na na- na-…’ mzee akashindwa kuendelea, akaanza kutetemeka.
‘Vipi
mzee, ndio mziimu hiyo nini, ….’akasema msaidizi akishangaa kumuona mzee anatoa
macho kweli kweli…
‘Si-si-s-kiliza..wewe
ondoka hapa mara moja…., akikuona hapa atakuzidi na akivichukua hivyo vitu ndio
basi tena….o-o-ndoka, haraka…’
‘Mzee,
usiogope, mimi siwezi kufa kabla ya muda wangu…’alipomaliza kusema hivyo tu,
yule mzee akadondoka, chini na mara akaanza kutoa mapofu mdomoni yakichanganyikana
na damu,..akatikisika kwa muda halafu akawa kimia.
Msaidizi
kuona vile,…akageuka kushoto na kulia, alipoona hakuna mtu, huyo akatoka
nje,…mara anakutana na moshi,..unakuja kwa kasi, akakumbuka alivyoagizwa,
haraka akaziba mdomo, huku anakimbia kukwepa ule moshi…..moshi ukawa unakuja
kwa kasi kweli…
Akafika
kwenye sehemu ina chumba,akakipiga teke kikafungua na kwa haraka akaingia humo
na kufunga mlango, ..akatulia, na kabla hajakaa sawa akashikwa begani…
*************
Sasa
huku alipo mdada…
Mlango
ukafunguliwa…lakini hakutokea mtu mara moja, kulitangulia moshi…ukawa unatanda
kuingia ndani, na mdada akakumbuka jambo, akachukua leso yake akaziba mdomo na
…..ule moshi uliingia ndani kwa kasi, akageuka kumuambia huyo jamaa ajifunge
mdomoni, lakini akawa kachelewa, ule moshi ukamuingia jamaa akaanza kukohoa na
mara, akalala,…..kapoteza fahamu.
Mdada
kule kuziba mdomo, na pua, pumzi inamuwia, shida, akaona ni bora atoke mle, maana ukiwa ndani unaweza kufungua mlango
kutoka nje..na mlango ulipofunguka tu,i anakutana na jamaa akiwa kavalia koti
refu, usoni kajifunika,,,na kabla hajasema kitu, mdada akainuliwa hewani..kama
katoto kwa huyo jamaa, mdada hakuachia pua na mdomo…
Na
huyo jamaa akasema;
‘Wewe
ndiye nakutafuta kwasasa…nataka hiki kitu…kimoja kwako, baada ya hili
sitakuhitaji tena, na huhitajiki tena kwenye hii dunia…utabakia huku huku
kuzimu..ukiwa miongoni mwao…’jamaa akawa akawa anaongea huku anamzungusha mdada
hewani.
Mara
wakaingia askari, wakiwa wameziba midomo yao kwa vifaa maalumu, mikononi wana
silaha, jamaa kafanya mambo yake, ule moshi ukaanza kuwaka moto…ukawa uanunguza
vile vifaa walivyo vaa hao maskari, na mmoja mmoja akawa anadonoka sakafuni
kazimia…
NB:
Naishia hapa kwa leo, wikiend njema.
WAZO LA LEO: Sisi wana-damu, ni
wakosaji, tunafanya madhambi mengi tu, kwa hiari na mengine kutokana na
mitihani tunajikuta tumeyafanya , ikiwa ni pamoja na kuwadhulumu wengine. Mtu
anaweza kusema mimi sijamdhulumu mtu, lakini jiulize mambo haya, je hakuna haki
ya mtu niliyowahi kuichukua, kwa kudanganya, au kwa namna ya kutaka kupata
faida ukamwambia mtu hiki kitu ni kizuri, hakina tatizo lakini kumbe kina
tatizo, ili tu upata faida,..hujapunguza kibaba, hujakopa na mpaka leo
hujarudisha, au umekopesha kwa riba, hujamuhadaa mdada, au mkaa ili ukidhi haja za
matamanio ya nafsi yako, ukijua unadanganya,..yapo makosa mengi tu! Yote hayo
ni dhuluma!.
Ndani
ya mwezi huu, tumepewa nafasi ya kutubia madhambi yetu, tutubie kwa kiukweli
toba ya kweli, ili iwe ni sehemu ya kujisafisha, na hata mwezi huu wa toba
ukiisha tuwe kama nguo safi iliyotoka kufuliwa.
Tumuombe mola wetu atusamehe makosa yetu, na atuongoze njia iliyonyooka,
Aamin
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment