Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, June 9, 2017

MPENZI WA FACEBOOK-47
Hata docta hakuamini,….!
‘Hata huyu mzee yumo ndani ya hili kundi.., haiwezekani!,..’akasema
Docta japokuwa alipokutana naye alihisi nafsi ikimtilia mashaka, lakini sio kihivyo kuwa ana uhusiano na kundi hilo haramui.
Docta akataka kumpigia simu mkuu-msaidizi, ili kumuelezea lakini akaona ngoja aone kinachoendelea, akaendelea kuwafuatilia, hawa watu wawili, na baadae docta akajisema;
'Huyu mzee, kumbe ndiye Kigagula wao, ndiye amewafundisha jinsi ya kuwteka watu kimazingara,….ndio wanaita msukule, oh…hii sasa hatari, unaishi na mtu kumbe mtu huyo huyo usiku anakugeuka….’akajisemea huku akiendelea na kazi yake kwenye komputa yake.
Docta akawa makini hasa pale alipoona msaidizi wake na yule mzee wamefika kwenye kile chumba,..chumba ambacho alikuwa kawekwa yule mdada, ambaye kwasasa inasadikiwa kuwa ndio huyo binti wa mzee, …aliyetambulikana kuwa ni marehemu,…docta kwanza akasogeza mtambo wake na kukikagua vyema hicho chumba chote, na kuhakikisha kuwa hakuna kitu cha zaidi au hatari.
Na ni pale, hamasa yake ilipovutika na tukio jingine, alikuwa huyo mdada aliyeingia, kutoka nje, akiwa kavalia kama hao watu waliokuwa wakitokea ndani, na yeye akatembea kuelekea sehemu ya hilo kundi,…maana wao walikuwa na sehemu yao tofauti na watu wengine waliowekeza humo…
'Huyu, ….atakuwa ni binti wa mzee, ...najiuliza na yeye anataka nini humo ndani, mbona anajitumbukiza kwenye matatizo, keshapona, sasa anataka nini tena, oh, ngoja nione anataka nini ...'akasema na kumpigia simu mkuu, kuwa humo yupo binti wa mzee, na kwahiyo kunahitajiwa mlinzi mwingine karibu yake bila ya yeye kujua.
'Hakikisha unamuwekea mlinzi wa ziada…huyo binti…’docta akasema.
'Kwanini…?’ mkuu msaidizi akaulia.
'Nina uhakika hao watu wakimuona hawatamuachia tena, unajua kupna kwake ni juhudi zetu, hawakutaka hawa watu wapone, waliwataka wawe kwenye miliko yao, wawafanya watakavyo.....'akasema docta, hakutaka kumuambia kuwa huyo bint kavaa viatu vya ajabu. Viatu vinavyotafutwa na hilo kundi
Docta, akamfuatilia kidogo huyu binti…, kwa muda huo alikuwa kaingia chumba cha mitambo, na aliingia kwasababu alishafahamu namba ya siri ya kuingilia humo,.. docta hakutaka kuizuia, na kama angelitaka angezuia watu wasiingie humo, kwa vile kwasasa yeye ana mamlaka na mitambo yote ya hilo jengo.
**************
Binti aliingia kwenye hicho chumba cha mitambo, akionyesha ana lengo lake maalumu, maana alipoingia tu, akaelekea idara ya muendesha mitambo, inayochunguza kila kitu homo ndani,…na mle ndani kwa hivi sasa alikuwepo mtu mmoja tu, wengine wote walikuwa wameshikiliwa na polisi na wengine wameamua kucha kazi.
Binti, alipoingia haraka akamuendea huyo jamaa aliyeachiwa kazi ya kuendesha mitambo, …na haa kabla huyp jamaa hajasema kitu, binti akatoa kitu kwenye pocho yake, ilikuwa kirungu..au kitu kizito, akamgonga huyo jamaa kichwani, na huyo jamaa akadondoka chini.
Binti akachukua majukumu ya kuendesha mitambo yeye mwenyewe akawa anakagua kwenye vyumba mbali mbali, sijui alikuwa akitafuta nini,…kuna sehemu nyingien zikawa hazifanyi kazi, akaina kumuangalia huyo jamaa alikuwa kapoteza fahamu.
Binti akaacha ile kazi, akatembea humo ndani kutafuta kitu, …akaona hicho anachokitafuta, ..ilikuwa ni kamba, …akaichukua ile kamba na kuanza kumfunga huyo mtu miguuni na mikononi, halafu akawa anamburuza hadi chumba kingine.
Docta akaendelea kumfuatilia huyo binti huku akijiuliza ni kitu gani huyo mdada anakitaka kukifanya, maana hiyo mitambo inahitajia mtu anayeiwezea vyema, na hana uhakika kama huyo mdada ana utaalamu kihivyo.
Huyo mdada alipomfikisha huyo jamaa kwenye hicho chumba kingine, akatoa kitu kwenye pochi yake akampulizia, huyo jamaa puani, na mara huyo jamaa akapiga chafya,…na ikanonekana kuwa huyo jamaa keshazindukana, na mdada akaanza kumgonga gonga huyo jamaa kwenye vifundo vya miguu.
‘Unaniumiza,..unataka nini wewe…’huyo jamaa akawa analalamika.
‘Sawa kabisa, nilitaka uulize hivyo, unanikumbuka mimi ni nani..?’ mdada akasema akivua ile miwani na kofia kichwani, akabakia uso wazi, na huyo jamaa akamtolea macho ya kushangaa
‘Oh….umefuata nini tena huku,…?’ akauliza
‘Kwahiyo umeshanikumbuka sio…?’ akauliza
‘Ndi-ndio, …lakini mimi sijakufanyia kitu kibaya,…’akasema
'Wewe ulitumika kunifanya niwe mtumwa wa hawa watu, sasa wewe utakuwa badili yangu, utafanya yale nitakayokuambia uyafanye,….’mdada
'Lakini dada yangu, usione hivi, sikupenda kuja kuyafanya haya, nilijua wameniajiri kutokana na utaalamu wangu wa komputa kumbe kuna mambo yao mengine,..
'Usinifanye hasira zangu zikanijia,…ulikuwa unafurahia kila kitu nilichokuwa nafanyiwa na wewe ukawa unawaongoza, na kuwaelezea kila hatua yangu..siku moja nilitaka kutoroka na wewe ukaawaambia je hukuona kuwa mimi nipo hatarini…?’ akauliza.
‘Dada mengine ni katika kutafuta riziki,…si unajua tena,….’akajitetea.
‘Rizki ndio uhatarishe maisha yangu, haya nikuulize, dada yangu yupo wapi..?’ akauliza
'Dada yako gani huyo…?’ akauliza
'Unajifanya humjui au sio nikukumbushe,…’akaanza kumgonga gonga tena, na jamaa maumivu yalipozidi akasema;
'Yupo kule kwenye chumba alipokuwa kafungiwa…’akasema huku akiendelea kulalamika maumivu.
'Una uhakika kweli yupo huko….?’ Akauliza
‘Ndi-ndi..o, nenda huko-uko… utamkuta….’akasema, akionyesha kuhisi maumiu makali
‘Kumbe na nyie mnaumia, mimi nilijua nyie miili yenu imeumbwa kwa chuma, …unajua jinsi gani, nilivyoteseka, hukunionea, huruma, wazazi wangu , baba sasa hivi yupo hospitalini kisa ni wewe…’akasema.
‘Sio kusudio langu, nielewe tu dada yangu…’akasema
'Sasa ni hivi, mimi ninataka unionyeshe kwa kupitia mitandao yenu, nimuone huyo dada yangu, la sivyo….nitakugonga mpaka nihakikishe hutaweza kutembea tena…’akasema huyo mdada.
'Lakin mitandao imegoma, haifanyi kazi za kihivyo…unaweza kufanya kazi za ndani za kawaida…’akasema.
‘Kama zipi, huwezi kukagua miendendo ya kwenye vyumba kuwa mtu fulani yupo…?’ akaulizwa.
‘Kuna muda inakubali, wakati mwingine inagoma….’akasema.
‘Sasa mimi ninataka unionyeshe huko alipokuwa anawekwa dada yangu, nionyeshe haraka….’akasema.
'Lakini….’akataka kulalamika, na alipoona mdada anainu akile kichuma mkononi, akasita kuongea.
‘Huo mtambo unafanya kazi gani kwa sasa…?’ akauliza
' Za kawaida tu..nasema hivi, ulivyonifunga hivi nitainukaje, na mikono…’akasema
'Haya twende unionyeshe…’mdada akasema akimlegeza kamba miguuni, wakatembea hadi kwenye ile meza ya awali, halafu,
'Haya anza kazi, mimi nipo nyuma yako….’mdada akasema akiwa kasimama nyuma ya huyo jamaa.
Jamaa akaanza kuonyesha vyumbani..na wakati anaendelea hivyo, mara simu ya mitambo hiyo ikaita, mdada akamsogezea huyo jamaa, na kumuashiria apokee hiyo simu..mdada akahakikisha kaweka spika ya nje, ili na yeye asikie kinachoongewa.
Alikuwa yule mzee anampigia huyu jamaa…, kuulizia kwanini vyumba vipo wazi, alipomaliza kuongea, mdada akaiondoa hiyo simu, na kumuambia,;
'Haya onyesha hapo alipo dada yangu…’akaambiwa na jamaa akajaribu lakini haikukubali kuonyesha.
‘Unaona sasa imegoma….’akasema
‘Hebu jaribu kuonyesha matukio ya nyuma ya kile chumba alichokuwa huyo dada, ..’
‘Kwa hivi sasa mitambo haikubali kufanya kitu kama hicho, si umeona mwenyewe….’akasema
'Kwanini…? Akauliza
'Mimi sijui mambo yao hayo…’akajitetea.
'Unajua sana, nilikuona ukisaidiana na mareheme, mtaalamu wenu, unajua kila kitu, kama hujui nitakufanya ujue…’akasema mdada
‘Ni kweli, ngoja nikuonyeshe….’akasema na kujaribu kufanya ili irejeshe matukio ya nyuma, lakini ikatokea ujumbe kuwa taratibu hizo haziwezekani,…
‘Sasa nikuulize dada yangu ilikuwaje,…walimfanya nini, mpaka akawa hivyo….?’ Akauliza.
‘Mimi hayo siyajui dada yangu…kweli nakuambia, zaidi ni pale ninaposikia makiongea yule mtaalamu…’akasema.
‘Kwanini usijue na wakati ndio nyie mlikuwa mnaendesha mitambo ya kutufanya hivyo, kutuharibu akili …na sasa dada yangu sijui yupo wapi, nisipompata ninakuala sahani moja na..wewe…’akasema mdada akimgonga gonga jamaa kichwani na kile kirungu cha chuma.
‘Oh, sikiliza dada…ukitaka kujua zaidi, wewe nenda kamuuliza huyo mzee…’akasema.
'Mzee gani huyo…?’ kauliza mdada
'Huyu aliyepiga simu sasa hivi, yupo ndani ya hili jengo, kwenye hicho chumba,…’akasema.
'Sasa ulijuaje kuwa wapo humo…?’ akamuuliza.
‘Nimekuambia kuna muda inakubali kuna muda inakataa…’akasema
‘Ulipoangalia muda huo mzee alikuwa na nani…?’ akauliza
‘Alikuwa na mtu mwingine…’akasema
‘Ni nani..mbona unaongea kama unaogoa, nitaanza kukuharibu miguu yako , au nivunje hiki kichwa chako…’akamgonga kichwani.
Basi jamaa akajaribu, tena na tena lakini haikuonyeha kitu…na mdada akasema;
‘Nikimleta mtu wangu akafanya ikakubali, nitakuharibu ….’mdada akasema;
‘Kweli haiwezekani, labda itokee….lakini kwa hivi sasa haikubali kabisa…’akasema.
'Umesema huyo mzee alikuwa na mtu gani mwingine..?’ akauliza
'Na yule …nahisi ni msaidiz wa docta…’akasema
'Kumbe na yeye ni mshirika wenu…nilijua tu, mimi hawa watu wawili siwaamini kabisa…’akasema.
'Hapana…sio mshirika wa mzee kabisa, mzee nahisi ana hitaji kitu kwa huyo mtu…’akasema.
'Kitu gani…?’ akauliza.
‘Nijuavyo, kuna vitu ambavyo huyo jamaa alivipata akavipeleka kwa docta, sasa mzee anataka kumtumia ili virejee kwao…’akasema.
‘Kwa vipi?’ akauliza.
‘Anajua huyo mzee, na mtaalamu, ..mimi hayo ni mambo siyajui, utaalamu wangu ni komputa tu,….’akasema.
'Hebu jaribu tena…’ akaambia na yeye akajaribu tena na ukaja ujumbe ule ule,
'Maana yake nini…?’ akauliza mdada.
'Ina maana kuna mtu kateka huu mtandao, kwahiyo kazuia baadhi ya taratibu zake, na mimi sina uwezo wa kurejesha kama ilivyokuwa awali, kunahitajika ufunguo wake, na mwenye ufunguo huo,….keshakamatwa…’akasema.
'Ni nani alikuwa na ufunguo huo…?’ akauliza
‘Kiongozi ….’akasema
‘Ok, tuyaache hayo,…unahisi ni nani kauteka huo mtandao wenu, na kufanya mshindwe kufanya shughuli zenu..?’.
'Atakuwa ni docta…’akasema.
'Well done,...’akasema bint.
'Sasa, nikushauri kitu, unajua wewe sasa hivi ni mhalifu, na utakwenda kufungwa kwa kazi hizi, wengi wamekamatwa, nashindwa kuelewa ni kwa nini hawajakukumata na wewe, mimi nakufahamu sana kuwa wewe ni miongoni mwao..’akasema mdada
'Tafadhali dada yangu usiwaambie, nipo chini ya miguu yako…mimi kujiunga kwao, sikupenda, walinilazimisha kwa kunitishia kuiua familia yangu.
'Hayo utayaongea mahakaman, lakini mimi naweza kukusaidia, kama utafanya nitakayo ufanye….’akasema mdada.
‘Niambie nitafanya kama ninaweza lakini…’akasema.
'Mimi ninataka unionyeshe wapi dada yangu kapelekwa, na je yupo salama…’akasema
‘Nimekuambia mtambo huu hauna uwezo huo tena, ukitaka hilo, labda uwasiliane na docta…’akasema.
'Mimi sio kundi moja na docta, mimi nipo na familia yangu tu…hao watu siwaamini, wapo na polisi, hawajui kuwa polisi wengi wapo na nyie, kweli si kweli…?’ akauliza
‘Ndi-o…lakini sio wote…’akasema
‘Sasa mimi nitajuaje…’akasema
‘Hata mimi siwezi kujua ni nani na nani yupo, labda itokee mtu anatakwia kukaguliwa kumbukumbu zake, ndip naweza kujua nani ni nani..ujue kazi nyingi alikuwa akifanya yule mtaalamu, akishirikiana na mzee…’akasema.
'Ok,a basi mimi nataka kwenda kuonana na huyo mzee…’akasema mdada.
'Wewe …dada yangu, nakushauri, kutoka moyoni mwangu, huyo mzee ni hatari, kuliko unavyomfaham nje,..anapokuwa kazini, usiombe ukutane naye au ufanye makosa, ..anageuka kuwa kama shetani,…sijui..lakini kwasasa hivi, yupo humu ndani, na humu ndio masikani yake,…ndio ufalme wake, humuwezi kwa lolote akiwa humu ndani…’akasema.
'Mimi simuogopi, hawezi kunifanya lolote..ninajua hilo, na kama ni mfalme humu ndani ajua kuanzia sasa ameshapundiliwa, shetani katekwa, hana amri tena kwetu…’akasema mdada.
‘Na isitoshe huyo mzee, hana ubaya na sisi….’akaongezea mdada.
'Kwanini unasema hivyo, …!’jamaa akauliza kwa kushangaa
'Wazazi wangu waliwahi kupanga kwenye nyumba yake, na yeye alimchukulia mzee kama ndugu yake, sasa iweje atufanyie ubaya kama huo…’akasema mdada.
'Sasa wewe hujiulizi, kwanini huyo mzee akamchukua dada yako msukule…’akasema jamaaa.
'Msukule ndio nini..?’ akauliza mdada
'Wanamchukua mtu kimazingaumbwe, nyie jamaa zake, mnajua kuwa huyo mtu kafa kumbe katekwa kinguvu za giza…’akasema.
'Ndivyo mlivyomfanyia dada yangu hivyo au sio…?’ akauliza.
'Ndio walivyomfanyia…lakini tofauti na wengine,dada yako hakufanyiwa hiyo yenyewe ambapo, huwezi kurudia hali yako ya kawaida tena, dada yako alichukuliwa kivingine kabisa…’akasema.
'Kwanini yeye alifanyiwa hivyo…?’ akauliza.
'Kuna stori ndefu ndani yake, imefungamana na mambo ya kurithi vitu vya kale..’akasema.
'Vitu gani hivyo…?’ akauliza.
'Bastola , ufunguo na viatu…’akaambiwa.
‘Aaah, hayo nimeshayasikia, hayana maana, ni mambo ambayo siyaoni umuhimu wake, kwani wangelivitaka hivyo vitu si wangelisema tu..na hata hivyo, sisi hatukwua navyo…vimekuja baadae, …na sasa hata sijui vipo wapi…’akasema mdada.
‘Walivipata vitu viwili, bastola na ufunguo,... ikabakia viatu, na viatu yasemekana bado vipo kwa baba yako…vingelipatikana vyote wangelisha maliza kazi yao.., ila kuna tatizo kuwa ili hivyo vitu vifanye kazi damu yenu ilikuwa inahitajika...'akasema
'Damu yetu,....kwa vipi ndio huko kutuua, au...?' akauliza
'Ukisema damu ina maana nyingi, kuna mambo yao ya matambiko, kafara...mimi sio mtaalamu wake,..ila dada yako damu yake ilikuwa ni muhimu sana,...'akasema
'Mhh....nimeshajua,..sasa na mimi je,...?' akauliza
'Wewe ni katika kufanikisha,...nikuembie kitu, ..mimi sijui sana ukiniuliza ni kama unanionea tu...'akasema.
'Haa,h, sasa ndio ujue, kuwa kujiingiza kwenye mambo, bila ya kutafuta uhalali wake, ndio hivyo, utafungwa, utaozea jela..na kama hutafanya jambo la kuniridhisha, ooh, ndugu yangu, mimi mwenyewe kama ni mahakamani nitasimama kutoa ushahidi kuwa na wewe ulikuwepo...'akasema
'Unajua dada yangu, ingelikuwa mimi ndio nyie, ningelishirikina nao, tu, kama wanahitajia viatu, sijui, bastola, mungewapa tu..mkafanya watakavyo, basi, ..mngekuwa matajiri, na ...'akasema
'Nani ashirikiane nao, ushirikiana nani anautaka siku hizi...'akasema mdada
'Sasa ndio hivyo mambo yameharibika hivi, najua wataanza kufanya mauaji, kila aliyehusika, watamuua, mpaka wabakie wenyewe wanaojuana, na dada yako hawawezi kumuua, kwasasa ni mpaka wakamilishe utaratibu wote.…’akasema
huyu mdada aliposikia hivyo akahisi mwili ukimsisimuka, akijua viatu alivyovaa ni miongoni mwa vitu vinavyotafutwa, alivivaa ili aje awakabidhi lakini kwa makubaliano kuwa wamrejeshe dada yake...sasa kumbe dada yake ni mtaji kwao, na hata hivyo wakimalizana naye wanamuua...!
‘Kwahiyo unasema ..kuwa vitu hivyo viwili anavyo docta au…?’ akauliza
‘Ndio, kwa hivi sasa lakini..mzee akikutana na huyo jamaa yao, watavirudisha ni watu hatari hao,…’akasema.
‘Huyo jamaa yao ni nani..’ akauliza.
‘Mhh, sijawahi kumuona hata picha yake haijawahi kuonekana hata kwenye mitandao yetu huwa hapatikani,..ni mtu wa ajabu sana….wanasema anajibadili kama kinyonga, na aana mazindiko ya kila aina…hata huyo mzee haoni ndani…’akasema.
‘Kama ana ubavu huo, kwanini kashindwa kuvipata hivyo vitu mpaka anapitia kuua watu,…na dada yangu au sisi tuna umuhimu gani na hivyo vitu…?’ akauliza na mara kukatokea kitu kwenye huo mtandao.
‘Ni nini hicho…?’ akauliza.
‘Ni ishara ya hatari…’akasema.
‘Hatari gani…..?’ akauliza .
‘Mtandao,….umeharibika kabisa, na pili….kuna..unaona hii alama hapa,….ikitokea ina maanisha, huyo jamaa yupo ..karibu, na akitokea, huyo atakayeonana, naye, ajue siku zake,….
Mara mlango ukafunguliwa…
NB: Tunaishia hapo kwasasa....mhhhh maana hata mimi mwenyewe naogopa!
WAZO LA LEO: Uwongo umekuwa ni jambo jepesi, kama ilivyo kusengenya, mtu kudanganya ili apate masilahi anaona ni jambo la kawaida tu au kumdanganya mwenzake kuwa nipo mahali fulani kumbe sio kweli…tunaona ni kawaida tu, lakini hatujiulize athari zake kwa huyo uliyemfanyia hivyo…na je mwenyezimungu atakwua radhi na wewe uliyetenda kosa hilo…!
Uwongo ni uwongo tu hata uwe mkubwa au mdogo, uwongo hushusha thamani ya mtu, na uaminifu wake huondoka.., na kuwa kwenye daraja la mnafiki.sasa hebu tujiulize mnafiki ana hukumu gani mbele ya mungu…!
Tumuombe mungu atusaidie katika mitihani hii ya maisha, maana kusema au kutenda uwongo, imekuwa ni jambo la kawaida kwetu, kutokana na maisha yenyewe yalivyo, maisha yamegibikwa na mitego mingi..wakakati mwingine inabidi useme uwongo, ili upate, au uokoke na janga fulani.
Ni mimi: emu-three

No comments :