‘Umekuja…nilijua
utakuja tu, nilikuwa na kusubiria, …’sauti hiyo ilinishitua na kunifanya
nisimame kwa haraka, na kwa haraka nikageuza kichwa kumtizam huyo mtu
aliyeongea kutoak nyuma yangu….
Tuendelee
na kisa chetu….
*************
Nilishtuka pale niliposikia sauti
hiyo nyuma yangu, na haraka nikakumbuka kauli ya docta;
'Shetani hatakuweza kamwe..hata mchawi hakuwezi, kama nafsi yako utaijengea
udhibit wa kuondoa hofu..hofu ndio silaha ya shetani,..na Ili shetani akuingie..au
hata hata mchawi, akitaka kukuloga kitu cha kwanza anachokufanyia ni
kukuingizia hofu, hofu ambayo, itakufanya uondokane na imani yako ya kumtegemea
mungu.
Nilipoyawazia hayo, nikasema kwa ujasiri;
‘Ndio mzee…. nimekuja, nataka nikamuone huyo binti, uliyesema yupo hai....’
nikasema.
'Sawa kama upo tayar, ..hebu sogea pembeni,…ngoja nikuonyesha jinsi ya kufungua
huu mlango wa kuzimu…’akasema na kuinama akagusa pembeni akawa kama
anakandamiza, halafu akasimama,
‘Sasa unasukuma hivi…’akasukuma,
na hiyo sehemu ya juu ya kaburi, ikasogea na kucha uwazi….
‘Umesema huu ni mlango wa
nini….?’ Nikamuuliza, na akajifanya kutabasamu , alipogundua. Nahisi
alipogundua kuwa kaongea neno ambalo hakutaka kuliongea akasema;
'Wewe huoni hili…kwa kawaida, mtu utaingiaje huku,..hapa watu wengi wanafahamu
kuwa ni kabur, lakini kumbe ndani kuna maajabu…eeh, wewe hulioni hili,..humu
kuna maajabu…utakuja kujaona, na kawaida mtu ukiingia huku, eeh, kama zio
kuzikana, basi wewe ni mfu au sio…’akasema.
'Mzee mbona lugha yalo ni ya kuogofya,...ina maana sisi ndio tunajipeleka
kuzimu..au ..’akasema msaidizi, akisita kuingia ndani.
'Usiogope kijana, wewe lengo lako si kukutana na huyo binti, au umeghairi
tena…’akasema huyo mzee.
'Mimi sanasana lengo langu ni kukutana na mrembo wa facebook, lakini yeye
sizani kama ni marehemu, huku tunakwenda kuhakikisha kama huyo binti wa mzee
yupo hai au la, si ndio hivyo…’nikasema.
'Haaah, kumbe...hahaha, haya, ngoja ukajionee mwenyewe, hapo ndio namvulia
kofia huyo mtaalamu, masikini wameshamuua, hawa watu bwana…’akasema.
'Unamvumilia kofia Mtaalamu gani huyo…?’ nikamuuliza.
'Tatizo lako wewe unakuwa na hamasa kupitiliza, unisikie… mengine naongea tu,
haya zama ndani jizike mwenyewe….’akasema akinisukumia ndani, na yeye
akafuatilia, halafu akasema
‘Unaona hicho hapo juu, ni kamba,
lakini hii ndio itatusaidia mambo mawili, italifunga hili kaburi,..na sisi
tutajizika,…mambo ya duniani, tutatachana nayo, kama tutajaliwa tutaoka nje,
kama ndio hivyo, useme dunia bya bye…’akasema
‘Sijakuelewa mzee…’nikasema
‘Wewe kivute hicho kitu usiogope,
upo na mimi, haya unaona limejifunga, haya kivute tena,…huoni sasa tutashushwa
kwenda chini, kama lifti, utaalamu huo.
Tulishushwa kidoo tu,, tukawa tupo
sehemu ya chini, ndani kwa ndani..
'Sasa…hapa ndio pa kuamua, tunakwenda wapi, huku kuna chumba alipowekwa
bosi,..au tuelekee moja kwa moja alipowekwa huyo binti…. kuna mawili chagua
moja..’akasema, na mimi nikasema;
‘Unajua tokea awali kuwa mimi lengo
langu kwasasa ni huyo binti,..kama kweli yupo hai…’nikasema
'Swadakta,…..umenena vyema kijana,..huku sasa usije ukashangaa nakuita
marehemu, hahaha..usiogope,….lakini kwanza kabla hatujaenda huko, nina ombi
langu kwanza,....'akasema, huku akisimama.
‘Ombi gani tena mzee….?’
Nikamuuliza
‘Kule duniani, nilikugusia, kuwa
….eeh, ni hivi….unajua mimi nimekuwa nikitaman sana kuvipata vitu vitatu,...
' Vitu gani hivyo mzee…?’ nikamuuliza.
'Ehee,… kuna bastola ya ajabu,…hiyo ni muhimu sana kwangu, kwanza nikuulize,
uliionaje hiyo bastola, ile uliyompa, Docta,… ushawahi kuisikia siri yake
kabla,…?’ akauliza.
'Hapana….’nikasema
' Ndio maana, maana ungelijua siri yake, sizani kama ungemkabidhi mtu kama
yule,…Ile silaha ukiwa nayo, umeshajiandikishia kuwa wewe ni mtawala, ile siri
yake toka awali na nembo ya mtawala…enzi za mamabu zetu waliamini hivyo..ili
ina mkono wa shetani,…na…amani…’akatulia.
' Kwahiyo wewe unavihitajia hivy vitu kwa vile unataka kuwa mtawala…lakini wewe
si mumbe tayari, unataka uwe nani, mbunge, raisi, au….?’ Nikamuuliza.
'Sio lazima niwe mimi..unielewe hapo,…. tunaweza kuiuza kwa mtu tunayefikiria
anafaa…huyo keshapatikana, na huyo akiipata ikiwa tayari, basi…dunia itakuwa
mkononi mwetu…’akasema
' Kwahiyo kuna mtu unafikiria anafaa kuwa mtawala na ana pesa nyingi za
kukulipa..au sio, na huyo ndiye unatak kumkabidhi hiyo bastola….?’ Nikamuuliza.
'Kwa kiifupi ndio...’akasema.
'Ni nani huyo…?’ nikamuuliza.
'Huyo, kwa hivi sasa siwezi kukuambia, wakati muafaka utafika, na huenda ukaona
naye, mimi sijawahi kumuona uso kwa uso, namsikia tu….’akasema.
'ndio huyo mkuu nini…?’ nikamuuliza na yeye akatabasamu na kusema.
‘Huyo hatajwi tajwi ovyo….sema
kwa vile wewe hujui sifa zake, ….’akasema.
‘Mhh, mnamuabusu au…ni mtu au ni
shetani….?’ Nikamuuliza
'Kwanza sikiza,..usipoteze muda wako kunidadisi, ukitatarajia kuwa nitakuambia
mambo ukamsimulie docta,au polisi, ujue umeshaingia humu, wewe sasa ni mtu
wangu, ninaweza kukufanya nitakavyo…’akasema akipangusa pangusa mikono kama
alishika uchafu.
‘Sasa sikiliza, kwa vile wewe
lengo lako ni jema tu, wewe unamtaka nani…binti mrembo…na mimi nahitajia nini,
hivyo vitu vitatu, kwasasa viwili anavyo, docta,au sio….mimi navihitaia hivyo,…
unasemaje, nitavipata au...na kama nilivyokuambia awali, ukiingia humu,
umeingia kuzimu, na kila ukiahidi, kitu, nikaumbie ukweli, huwezi kuvunja
ahadi, ukivunja mizumu itakuandama…. ukihin, utakuwa mfu…
'Ndio imani zenu hizo….’mimi nikasema.
'Nikuulize tena wamtaka huyo binti au la…., na hii ndio nafasi yako ya mwisho,
ukiwa bado hujazama kwenye dimbwi la umauti, na kuusahau ubinadamu…’akasema ,
nahisi alijua mimi nitaogopa,…mimi nikasema;
'Mzee tumekuja kote huku nia ni hiyo, hayo mengine, siwezi kukuahidi, kwa vile
hivyo vitu havipo mikononi mwangu tena…’nikasema.
'Ninafahamu hilo, lakini..nina namna naweza kukuwezesha, ukaenda kuvichukua, ni
wwewe tu, ukubaliane na mimi…sitaki kutumia nguvu, ….’akasema.
'Kwa vipi, ina maana unaweza kutumia nguvu kunilazimisha niende kuvichukua, au…?’
nikauliza.
'Wewe nijibu tu, kama upo tayari, kunipatia hivyo vitu, kama upo tyari ukikuali
basi nitajua la kufanya, na wewe utakuwa na huyo rafiki yako,…ni mpenzi wako au
sio, basi wewe kubali, kuw upo tayari, ….’akasema.
'Mzee mimi siwezi kukubali wakati, sina namna ya kuvipata hivyo vitu, unajua
fika, kwa hivi sasa siwezi kwenda huko alipoweka huyo mtu, ….na kama nikienda,
muda, mpka niende nikutane naye, sijui nitamshawishije hadi akubali, ni kitu
kigumu sana….’nikasema.
'Mimi ninajua umemkabidhi docta, na wwewe ndiye anayeweza kwenda na kuvipata
hivy vitu, kirahisi,….wewe kubaliana na mimi, kuwa upo tayari, mengine niachie
mimi…’akasema na nikashindwa kumuelewa,anawezaje kufanya hadi nikavipata hivyo
vitu na kumkabidhi yeye,…
Mimi nikawazia, nimdanganye tu, kuwa kama kuna njia hiyo ya kuvipata, basi,
nitajua huko mbele kwa mbele, muhimu mimi niweze kumuona huyo binti.
'Mzee, kwanza ni kwanza, ahadi yetu, ni mimi kwanza niweze kumuona huyo binti,
ili niweze kusadikisha maneno yako, hili la hivyo vitu limekuja baadae, kwanza
timiza ahdi yangu au….na mimi,...nikimuona,…’nikasema na yeye akaangalia juu,
halafu akasema
‘Ina maana huniamini…..’akasema
‘Mzee,… kwanza nikuulize, una
uhakika, kuwa kweli huyo binti yupo hai au na wewe unakisia tu, huenda ulimuona
binti mwingine aliyefananishwa naye, hawa watu wanaweza kumabdili mtu akawa
kama yeye….’nikasema.
‘Kijana, hayo ninayokuambia, nina
uhakika nayo, na mimi nisingechukua
hatua hii ya hatar, nina uhakika huo..ujue kijana kuingia huku ni hatari..huku
ni kuzimuni…’akasema akiangalia juu.
'Ok, …mzee, lakini nilishakuambia awali, mimi sitakiw atu wafu…mimi namtaka
huyo binti, ninayemfahamu mimi, mpenzi wa facebook, sio huyo mfu…najua
nitamuona lakini kumbe yupo huku kuzimuni hafai huko duniani…’nikasema.
'Sawa, wewe si ndio hivyo,
unatamka mpenzi wako wa facebook, wote hao nakuhakikishia utawapata, lakini
kwanza ni wewe kutimiza masharti yangu, hayo ni muhimu sana, ..umenielewa,…’akasema
sasa akiongoza tuanze kutembea;
'Sawa, twende…’akasema.
‘Haya twende mimi nikimuona, basi
nitaangalia namna ya kwenda kuvipata hivyo vitu….’nikasema;
'Aaah..unajua ni hivi, wewe, unakwenda kuvileta, hivyo vitu kwa vile hivyo vitu
ndio ufunguo wa kupata mahitaji yako…huyo mdada ili aweze kuongea, ..anahitajia
nguvu ya hivyo vitu….’akasema.
‘Sikuelewi mzee, ina maana ni
maiti, mnataka kuihuisha au…?’ nikauliza
‘Hakuna mwanadamu wa kuhuisha…labda
awe amepewa miujiza na mungu…sisi ni ..mimi ni mtaalamu wa kuagua, ..unajua,
nafahamu huyo binti hajafa, ila kafanyiziwa tu, sasa mengina nitakuambia…’akasema.
'Mzee, nikaumbie ukweli, kwangu mimi, hivyo vitu havina thamani kabisa kwangu,
sina haja navyo, na wala sijui umuhimu wake. Mimi ninachotaka ni kumuona huyo
bint, ambaye alisadikiwa kuwa kafariki…au sio, halafu unielekeze jinsi ya
kumpata huyo mpenzi wangu wa facebook,…sawa….’nikasema.
'Huyo binti hajafariki,…hilo liweke akilini mwako, siri ya yote hayo hadi akawa hivyo, naifahamu
mimi, ngoja nikueleweshe sasa, ...'akasema.
'Siri gani hiyo…?’ nikamuuliza.
'Hiyo, nitakuambia ukitimiza makubaliano yetu….unasikia,…’akasema
'Kwahiyo, tukubaliane kitu kimoja uniweke wazi, wewe ni miongoni mwa hao watu,
au sio…?’ nikamuuliza.
'Usiniulize maswali ya kunitega, kuwa labda unatafuta ukweli wa kuja kunifunga,
hutaliweza hilo, maana kuanzia sasa upo hapa…’akaonyesha kiganja chake cha
mkononi…
‘Na unielewe kijana, mimi haya
yote ya kuwa na hawa watu, kama nilivyokuelezea awali, kazi yangu ni ujanja, nauma
na kupuliza…, ila kiukweli kama huyu jamaa wahili kundi, akibahatika kuupata
utawala, …lakini kuweza kwake ni mpaka aipate hiyo bastola, na hivyo vitu
vingine….’akasema
' Kwahiyo wewe kumbe, nia na
lengo lako ni kuwasaidia, au kumsaidia huyo mtu, ili aupate utawala, sio wewe
haswa… au sio...?’ nikauliza
‘Kijana..unauliza sana maswali,
unajua hata nikikujibu, ..huna namna nyingine, ushaingia humu ujue utakubaliana
na mimi, ..kuna namna nyingi, lakini mimi sitaki kukuumiza, najua wewe sasa ni mtu
wangu…nikuulize kitu, unajua ni kwanini ukaja mwenyewe huku…?’ akaniuliza.
‘Nilitaka mwenyewe ndio..nina
hamu sana ya kumuona huyo binti…ndio lengo langu…’nikasema
‘Na docta hakupenda kabisa wewe
uje huku, unalielewa hilo…’akasema
‘Mimi nimekuja mwenyewe kwa
utashi wangu…’nikasema
‘Sawa tusibishane kwa hilo…utakuja
kugundua kuwa mimi ndiye nimekuvuta hadi ukaja, na docta hakuweza kukuzuia,
maana nina nguvu zangu za kuweza wewe kufanya nitakavyo, lakini sitaki kwa hivi
sasa kuzitumia, haina haja, nataka wewe ukubali kwa utashi wako, maana nina
imani wewe utakuja kumuona utmakaye, na nyie wawili mtafanikisha jambo, ambalo
hata wewe utakuja kulifurahia,….’akasema
‘Sawa mzee, mimi sina
shaka,..kwasabau hata ukinisimulia mambo yenu ya kuzimu, uchawi, mimi siujui,
na wala siuamini, na …hivyo vitu kama unavihitajia, eeh, kama kuna namna, basi
nitavileta, lakini kwanza nimuone huyo binti, hilo ndilo sharti langu…’nikasema
‘Sawa sawa, kwahiyo umekubali…..’akasema
‘Kwa sharti hilo…..unielewe hapo,
kwanza kwanza..sio uniletee ujanja ujanja wako wa nguvu za giza, mzee,
nikuambie kitu, mimi ..anyaway, twende huko,..ukanionyesha, halafu, uniambia na
namna ya kuvipata hivyo vitu, mimi nitakueletea, .havina maana kwangu…’nikasema.
‘Hapo sasa tupo sawa, mizimu
wamekusikia,…twende kijana….napenda sana watu wa namna yako majasiri,
wanaojiamini,..hahaha.. unampenda sana huyo binti, hata yeye alikuwa anajiamini
hivyo hivyo, nikamuambia, haya….sasa hivi watu wanamtambua kama marehemu,
lakini….’akatulia, alihisi kitu akatikisa kichwa…
‘Nahisi kuna kitu hakipo sawa….’akasema
‘Unaona , mzee wewe umeanza
ujanja ujanja wako…’nikasema
‘Sio kuhusu hilo….mizimu..inaniashiria
jambo, hebu kidogo, akasugua mikono yake, ahalafu akanusua, ..halafu akasugua
tena, akaniambia
‘Hebu nusa….’akaninyoshea mikono
yake
‘Hapana ….mzee, mimi sitaki huo
ujanja wako, sitaki uniharibu akili yangu, tuelewane wewe unataka hivyo vitu
sawa, kuna namna ya mimi kuvipata , sawa..kama ni hivyo, nionyeshe huyo binti,
kama ni ujanja, na mimi nitatumia ujanja wangu, wa asili, …’nikasema
‘Hahaha, huo ujana wao hauna kazi
humu ndani..humu eeh, ni milki ya mababu zangu, na hata hao watu,
wamekodi..wanalipa pesa nyingi sana, makafara ..ndio usiombe, ni lazima wafanye
hivyo, la sivyo, hawatafanikiwa, na wewe upo kwenye miliki yangu, utafanya
nitakavyo mimi….’akasema
‘Mzee, unataka kusema nini…’nikasema
‘Sikiliza bwana mdogo, mimi
nakupeleka kiungwana, sitaki nikupeleke kinamna ya kukupumbaza, nataka haya
yatendeke ukiwa na akili zako, ili baadae tuwe marafiki au sio,…sasa kuna
jambo, nataka ulielewe,..twende,, ..usiogope, siwezi kukufany akitu, wewe ni
mtu muhimu sana kwenye haya mambo…’akasema na tukaanza kutembea kuelekea huko
kwenye sehemu anayosema ndipo huyo binti yupo…
***************
Mpelelezi
akamdaka yule mdada kabla hajadondoka…alijitahidi kufanya hivyo kwa mkono mmoja,
na kuhakikisha anamuweka chini salama, huku akiangalia huku na kule kuhakikisha
hakuna mtu anayemgundua, na pia kuangalia kama kuna mtu atakayeweza kumsaidia,
ili akaendelee na kazi yake iliyomleta hapo…wakati hayo yanatendeka, docta
anaona, akayasoma mawazo ya mpelelezi,
Docta
akapiga simu kwa haraka kwa mkuu-msaidizi , kuwa mpelelezi anahitajia msaada wa
haraka. Na mkuu akamjibu;
‘Kijana
wangu yupo karibu yake keshaiona hiyo…usijali endelea kunipa habari…
Na
wakati huo,…wakati mpelelezi, sasa anageuka huku na kule kutafuta msaada, mara
akajitokeza mtu karibu yake,na huyu mtu, akasogea kumkagua huyo mdada, mdada,
wakati huo yupo kalala sakafuni, hajitambui,..huyu akasema, kwa kuuliza;
‘Kuna
nini, huyu mdada kafanya nini…?’ akauliza akimuinamia kumkagua
‘Huyu
dada naona anahitajia msaada, sijui ana tatizo gani!
‘Ok,
ok, hebu subiria,…ninapiga simu kumtafuta docta wangu, atashughulikiwa mara
moja,au….?’ Akauliza huyo mtu.
‘Sawa,
sawa itakuwa vyema, ila…’akasema mpepelezi, na huyo jamaa akamkatisha kwa
kusema;
‘Usijali,..bosi,…nimeshapiga
simu kuna docta anakuja kumshughulikia…’akasema huyo mtu, na mpelelezi,
alijitahidi asiangaliane na huyo machoni ili asije kutambulikana kuwa yeye ni
nani,..hata hivyo, kwa tahdhari, akataka kuhakikisha kuwa huyo mdada yupo
mikono salama,.. akasema
‘Huyo
docta anatokea wapi…?’ akauliza
‘Yupo
hapa jirani, ana hospitali yake, lakini kama una docta mwingine, mimi naweza
kumzuia huyo asije, unasemaje…?’ akaulizwa na mpelelezi, akaona haina haja,
akamuamini huyo mtu, na kusema;
‘Haya,
mimi nina mtu namfuata huko ndani, …umesoma hiyo hospitali inaitwaje..?’
akauliza na huyo jamaa akamtajia jina la hospitali ambayo huyo mdada, ikibidi
atapelekwa huko…
‘Ok,
sawa,..naifahamu, haya nikitoka huko nitakuja huko, …’akasema mpelelezi, na
kuanza kuondoka.
‘Lakini
bosi si ingekuwa vyema, kama ungesubiria, na ikibidi uongozane na huyo docta,
maana hata mimi, sina shughuli, si unajua tena ,au..?’ akauliza huyo jamaa.
‘Mhh..hapana
kuna mtu namtafuta huko ndani,..huyu hakikisha yupo salama, mwambie docta mimi
nitakuja,..nikitoka huko ndani, ..kiukweli mimi simjui huyo mdada…’akasema
mpelelezi, akiona asipoteze muda hapo nje, na akiendelea kubakia hapo
atashindwa kufanya kazi yake na anaweza kutambulikana.
Mpelelezi
alipoondoka, tu, huyo jamaa akampigia bosi wake simu, kuwa mtu wake, anahitajia
mtu mwingine wa kumfuatilia, yeye kabakia na mdada, na akajibiwa kuwa, sawa
ahakikishe kuwa huyo mdada yupo salama, mpaka atakapopewa taarifa nyingine.
Huku
kwa mpelelezi, yeye kwa haraka…akaendelea na lengo, lakini hakujua kuwa kuna
mtu anamfuatilia kwa kutumia mtandao…yeye, akili yale sasa ilikuwa kumtafuta
mbaya wake, au wabaya wake, na kukamilisha dhamira yake, huyo mdada akaomba
mungu awe kwenye mikono salama, ila akilini alitamani amfahamu huyo mdada,
anahisi kama anamfahamu, japokuwa hakupata nafasi ya kumchunguza vyema;
‘Huyu
dada nahisi ndio yule …niliyewahi kumuona kule…yawezekana, sina uhakika lakini,
hata hivyo nitalijua hilo nikiingia huko ndani,..’akajisemeza hivyo, na kwa
haraka akawa anatembea kuelekea ndani , hakukuwa na mtu wa kumzuia,..watu
walikuwa wakitembea wengine kuingia, wengine kutoka, ila alishangaa kuona watu
waliokuwa na sare kama ile yam dada, na watu walikuwa wakiwashangaa.
‘Sasa
nitaingiaje humu..?’ akajiuliza, mara alipofike kwenye mlango ambao ukiingia
ndio unaweza kwenda vyumba vya chini,.. na mara ghafla, mlango ukafunguka…mara,
akatoka jamaa mmoja akiwa na haraka,
Huyu
jamaa wala hakusema neno alipomuona mpelelezi, alimpita huku akiangalia saa
kuonyesha kuwa ana jambo muhimu analiwahi, na keshapoteza muda, …mpelelezi,
bila kupoteza muda , yeye akaingia ndani, na mlango ukajifunga kwa nyuma yake..hakuangalia
nyuma yeye, mbio mbio, kumtafuta mbaya wake..
‘Kwanza
kabla ya kukabiliana na huyo, kwanza niende nikahakikisha jambo moja, je kweli
huyo mdada ndio yule niliyemuona kule….kama ni yeye,..kuna tatizo,…kama ndio
yeye, ..lakini hata kama yeye, mimi sina shughuli na yeye, mimi nataka kuonana
na huyo jamaa aliyetaka kuniua na kundi lake….hao..ndio wabaya wangu…
Akafika
kwenye kile chumba,…anakuta mlango upo wazi…..
NB:
Sehemu ijayo
WAZO LA LEO: Tumemaliza kumi la
kwanza, la mfungo, hebu tujikague je kuna chembe ya imani imeongezeka, …jana au
juzi uliweza kumsaidia nani, uliweza kujitolea kwa jambo gani, je hukugombea
kitu na wenzako, ukasema basi mpeni huyu…nasema hili kwani tulikuwa tunagombea
dala dala, kuingia ndani, niliona watu wanavyosukumana kuingia ndani , hakuna
aliyejali kuwa kuna watoto, wazee, na
wasiojiweza, kisa wanakimbilia kiti…
Haya
sasa tumeingia ndani, umeonyesha umahiari na ubabe wako,...umekaa huku unawaona, wazee, kuna akina mama wamebeba watoto wadogo, kuna
wagonjwa, wamesimama, kwenye viti, umakaa , kwa vile wewe umewahi kuingia kwa ubabe, wao si vijana, wana nguvu..hapo wanatabasamu kuwa wameshinda...wameshinda nini..,kupata
viti, hawa wamefunga, kumi la kwanza limeisha,....Huu ni mfano mdogo tu, wa kupima imani zetu kama kweli zimeshaanza kutakasikia, kuna chembe ya upendo ndai yetu,….kiukweli, imani
ya kweli sio kitu cha mchezo…
Tunaambiwa imani ya kweli ni mpaka pale
utakapokuwa radhi kumpa mwenzako kitu unachokipenda haswa, ukasema aah chukua
wewe kwanza kwa kutoka moyoni..pia, nafsi yako ikajenga kukinai,.... ukarizika na kidogo ulicho nacho,...pia ukawasaidia
masikini na wanaohitajia, nk...….
RAMADHANI KAREEM, tumshukuru mungu kwa kulifikia, kumi hili la pili.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment