Docta,
alipokea ujumbe kutoka kwa mtu wake, kuwa kafanikiwa kutengeneza namna kwa
kutumia herufi za kikomputa, itakayomuwezesha kurejesha ule mtandao ufanye kazi
tena kama awali…
'Sawa
ni vyema, hata hivyo nimeshaupata ufunguo wake tayari…’akasema docta
‘Umeshaweza
kuufungua huo mtandao..?’ akauliza
‘Bado
sijapata muda huo…’akasema docta
‘Ufungue,
ukishaufungua uweke hivyo vielelezo vya herufi za kikomputa nilivyokutumia,
visaidia kujilinda, na kuulinda huo mtandao usiingiliwe tena…’akambiwa.
'Kwahiyo,
...’docta akataka kuuliza lakini simu ikakata mawasiliano.
Mawasiliano
yakakatika, na docta,akahisi kuna tatizo mahali,…lakini hakusubiria, kwa haraka
akafungua ule mtandao wa awali, ulipogoma akaingiza ule ufunguo, ni aina ndogo
sana ya kitendea kazi cha komputa cha nje(external drive) alipokichomeka tu
kwenye komputa, ilijiandika, ..kuwa huo ni ufunguo tawala, unaweza kuingia
sehem yoyote iliyifungwa, ikauliza unataka kufanya nini sasa…!
Docta alichagua kwenye namna mbalimbali
zilizoorodheshwa, kuwa anataka mtandao uliofungwa, urudie kufanya kazi, na
alipochagua hivyo, mtandao ukaanza kufanya kazi, ukiuliza ushehenezwe habari za
zamani na sasa, akasema ndio..ikawa sasa inajaza habari, hadi ikafika mia, na
hapo hapo ikasema mtandao upo tayari kutumiwa,…sasa ndio akaweka zile herufi,
za kujikinga, ili asiingiliwe, na zilipokamilika, akaweza kuwa mtawala wa
mitandao.
'Sasa tunamaliza kazi...'akasema docta
akionyesha tabasamu usoni.
'Cha
kwanza ni kuharibu mitandao yao yote mibaya, yenye kuathiri
wanadamu,....akazitafuta sehemu hizo, ambao kulifichwa kumbukumbu za watu,
akahakikisha kila mmoja karejeshewa kumbukumbu zake, halafu ndio akaziharibu
sehemu hizo, zisiweze kufanya kazi tena.
'Chapili
ni kuwafungulia wale wote waliofungwa akili zao, warejee kwenye akili zao
sahihi, kwa amani na salama..’akasema na kuanza kufungua, na ikasema tayari hao
watu wameshafunguliwa na kumbukumbu zao zote..wapo salama.
Na
kila mtu anapohakikishiwa kuwa yupo salama, kumbukumbu na picha yake hutokea,
na kuonyesha sasa yupo wapi…
Alizifuatilia
hizoo picha na majina yao… aliona picha mbali za wahanga wa hao wakubwa kwa
wadogo..na ni wale waliopo hai, kama mtu amefariki inaonyesha alama nyekundu
kuwa huyo mtu ni marehemu.
Akawa anafuatilia watu na majina yao, hadi
mwisho!
'Mhh,…. ina maana ni kweli, mbona sijamuona..’akasema
akiendelea kutafuta majina tena na tena kwa wale waliofariki, na alipohakikisha
kuwa hilo jina halipo, akaona arejee kwenye majina ya waliopo hai,..hayupo,....hii
sasa ni ajabu!
‘Mbona
huyu mtu hayupo popote, kwanini…?’ akajiuliza sasa akilini akijaribu kuwaza
hilo lina maana gani…kama hajafariki alitakiwa awe kwenye majina ya watu
waliopo hai…., lakini huko hajaonekana jina lake, na kwenye hata waliofariki
pia jina lake halipo...hii ina maana gani…, akajiuliza na hakuweza kupata jibu
la uhakika.
Alipojirizisha,..na kinachoendelea kwenye
mtandao, ndio akaanza kumtafuta huyo mtu yupo upande gani, na kwanini
hajawekwa kwenye huo mtando, kulikuwa na
watu wengi kwenye hilo jengo, na wingi wao ukaongezeeka, kutokana na hao watu
waliotokea ndani, hao waliokuwa wafungwa, hawakuwa wanaonekana huko nje,..na
cha ajabu wote walikuwa na vazi la aina moja, kutokana na vazi lao walilovaa, watu
waliokuwemo kwenye hilo jango, kwa shughuli zao mbali mbali walihisi labda,
hilo ni vazi rasmi la wafanyakazi wa hilo jengo.
Cha
ajabu hata wafanyakazi wa humo, waliokuwa kwenye shughuli zao mbali mbali,
walijikuta wakiwashangaa hao watu pia, na walishindwa kufanya lolote maana hao
watu, walikuwa wakitokea ndani, na hali hii
ikazidisha hamasa kwa wateja, na hao wafanyakazi pia, kubakia kuwaangalia hao
watu waliokuwa wakitokea ndani.
Hakuna
aliyewatambua hao watu kwa haraka, maana miongoni mwao, kuna ambao walikuwa
wamepotea siku nyingi, na ndugu zao walishafikiria kuwa huenda wameshafariki,
lakini kuna wale ambao walitambulikana kuwa wamefariki wakazikwa, sasa
wanatokea, hao ndio itakuwa ni balaa kwa jamaa zao,…je wakionekana na jamaa zao
itakuwaje..
Docta
hakuwa na muda wa kuwadadisi zaidi yupo ni yupi , inagwaje majina yao yalikuwa
yakitokea, kila anamgusa na kiashiria cha komputa….na wakati anawakagua mmoja
baada ya mwngine mara macho yake yakatua, kwa mtu mmoja aliyekuwa akiwashangaa
hao watu wanatoka ndani…
‘Mpelelezi…’
**************
Docta
hakutajia kabisa kumkuta mpelelezi eneo hilo, kwa vile alikuwahajapna vyema, na
haitakutakiwa afike eneo hilo tena,kwani jamaa walikuwa wakimtafuta ili
wamuue,kwa vile wanahisi ataweza kuongea mambo mengi kuhusu hilo kundi, ndio
maana ilitakiwa kama inawezekana aendelee kuumwa hivyo hivyo, mpaka hilo kundi
lisambaratishwe, sasa huyu anaonekana yupo kwenye eneo la maadui.
Docta
akahisi mwili ukimsisimuka kwa woga,..huyu mtu akipatikana sizani kama watampa
hata nafasi ya kujitetea, na hata binti yake ambaye naye yupo kwenye ulinzi
mkali, akiwa na mama yake walitakiwa na wao wafichwe seehmu nyeti, lakini
wameachiwa kama mitego, ili jamaa wakitaka kuwasogelea tu wakamatwe!
'Huyu
mpalelezi kafuata nini huku, na iweje, ina maana keshapona, haiwezekani,..lakini
huyu mtu alikuwa hospitalini, kafikaje hapa…’ aliposema hivyo ndio akaitisha
namna ya kufuatilia nyendo za huyu mtu, kwa kutumia mtandao, na ndio akagundua
kuwa huyu mtu alitoroka hospitalini, na kuja maeneo hayo akitumia bajaji,…
‘Sasa
kafuata nini huku kwenye hatari hivi, na bado anaonekana mkono wake haujawa
sawa..?’ akajiuliza, na kabla hajapata jibu, simu yake ikawa ainaita, na
alipoangalia akakuta ni mkuu anampigia;
‘Naona
kuna mambo yanaendelea jumba la biashara ni wewe umefanya vitu vyako nini,
mboan hujaniambia kuwa umefanikiwa kurejesha huo mtandao, je ni wewe au kuna
namna hawa watu wanatutega,…au kuna nini…maana hata walinzi wangu wameshindwa
kujua ni nini kinachoendelea, na walinzi wa ndani wanasema milango yote ya
ndani imefunguka..’akasema mkuu.
‘Waambie
watu wako wa kule makaburiini, wawe stand
by, lolote linaweza kutokea, na wale wa ndani karibu na sehemu hiyo ya
makaburini wawe wepesi kuwakagua hao watu,…wanaotoka ni lazima upate taarifa
bila kujali ni nani, ama kwa wanaoingia, wawaruhusu tu, lakini wakujulisha kuwa
ni nani…’akasema docta
‘Sawa
ndivyo wanavyofanya, kwani kuna jambo gani jipya…?’ akauliza mkuu.
‘Kuna
watu wawili wameonekana wakiingia kwenye njia ya kupitia kaburini,…ndio nataka
kuwafuatilia, sijawagundua bado, je watu wako hawajawaona watu kama hao..?’
akauliza
‘Sijapata
taarifa yoyote, ngoja niwaulize, wewe je umeona nini huko…’akasema mkuu.
‘Sawa
waambie wawe makini, najua wanaotumia eneo hilo watakuwa watu wanaofahamu sana
kundi hilo…’akasema
‘Ni
kweli…’akasema mkuu
‘Na
huyo mtu wetu wa ndani muwe makini naye, anaweza kutafutiwa njia za kutoroka…ama
kwa kupitia kwa wako au..akanbaweza kuja mtu ambaye watashindwa kumzuia…’akasema
docta.
‘Lakini yupo kwenye kifungo, ..kafungwa vyema
mikononi na miguuni,..hawezi kufanya lolote, na nimehakikisha mle ndani kuna
kifaa cha kuangalia mienendo yote na hivi sasa namuona, yupo, anaonekana hana
raha kabisa…’akasema
‘Sawa…..,.
najua hilo…lakini naona kuna ugeni unamfuata hapo, hao watu wawili msiwazuie,
tuone wanadhumuni gani, ila uwe …walindwe,…’akasema doctacta
‘Mgeni,
gani..ooh, nimekuelewa,… ndio maana hata mimi nataka nielekee huko, sasa wewe
fanya hivi, endelea kuwepo hapo kwenye mtandao wako, halafu utanipa habari za nini
kinachoendelea huko,ngoja mimi nielekee huko..’akasema
‘Kuna
kitu nimeona, mpelelezi katoroka hospitalini yupo huko..’akasema
‘Oh,
kwa vipi, katokaje, ..ndio hapo nashindwa kuwaelewa hawa walinzi wangu, kuna
uzembe au kuna ndumilakuwili… , inakuwaje wanamuachia mtu…lakini sina shaka
naye, ila ninacho-ogopea kwa sasa ni usalama wake, kwa vile hajapona vyema , na nachelea asije
kuharibu mitego yetu..’akasema
‘Ninamfuatilia
kwa karibu,..akili yake kwa hivi sasa ipo safi , ila anaonekana na huzuni
usoni..kuna kitu kinamsumbua, na hali kama hiyo inaweza ikawa ya kutaka kufanya
jambo, likaharibu kila kitu, naona ni bora ukamtuma mtu wako mmoja awe karibu
naye, hatua kwa hatua..’akasema docta.
‘Sawa
hilo litafanyika mara moja..na vipi uliweza kuvipata vile vitu..salama..?’
akauliza mkuu
‘Vitu
gani,…oh, bado, ngoja kwanza kuna kitu kimetokea, …’docta akasema na kukata
simu.
**************
Docta
alikata simu baada ya kuvutiwa na mtu…alimuona mdada mmoja, mrefu kiasi, ana
umbile nzuri kutokana na vali alilovaa kuonyesha kwa nje hivyo, japokuwa halionyeshi
kwa ndani yupoje, maana linafunika sehemu zote kutoka juu hadi chini, alikuwa
miongoni mwa watu walitokea ndani na inaonyesha hivyo kutokana na mavazi yake….akawa
anatembea mwendo wa pole pole, tofauti na wengine ambao walikuwa wakitembea kwa
haraka.
‘Yaonyessha
huyu bado afya yako haipo sawa,..ni mdada gani huyu,.. au hayupo kwenye orodha
ya watu waliokuwepo kwenye huo mtandao hatari, ambao walihitajia kurejeshewa
kumbukumbu zao, na ili warejee kwenye afya zao, sasa huyu kulikoni…’akasema
docta.
Docta
, akavuta sehemu ya kuuliza, je huyo mtu ni nani…lakini ombo hilo
halijakamilika, kukatokea tukio jingine lilimfanya asiendelee kuperuzi huko…,
huko upande wa makaburini, kuna kitu kikaashiria kuna tukio, akaona ngoja aangalai
huko kwanza....akaona jambo, lililomfanya aachane na kumtafuta huyo mdada, kuwa
ni ni nani.
Alipovuta
seehmu hiyo ya makaburini, akahisi mwili ukihisi hali ya mashaka makubwa, ndio
akasema;
‘Huyu
sio ooh,..’ akakunja ngumi kuashiria
hasira!
‘Msaidizi
wangu..’
‘Huyu
mtu kafuata nini huku, mbona hakuniambia anakuja, huku…na hajui kuwa
anajipeleka kwenye hatari, huyu mtu kachanganyikiwa nini…’ na mara akaona kuna
mtu mwingine nyuma yake…
‘Hii
sasa ni hatari…na hapa kwasasa siwezi kumsaidia kwa lolote,, hivi anaelewa ni
kitu gani kipo mbele yake,..na huyu mtu anayeongozana naye ni nani huyu,..’akasema
na kuchukua simu yake na kumpigia msaidizi wake, lakini simu ya msaidizi wake
ikawa haipatikani, akawapigia walinzi wa huko.
‘Huyu
msaidizi wangu yupo wapi?’ akauliza
‘Ndio
mkuu…eeh, ngoja, maana mimi nilitoka kidogo…’akasema mlinzi na docta akakata
simu kwa hasira, akampigia msaidizi wa mkuu wa kituo, akamuulizia kuhusu hilo,
na msaidizi akasema.
‘Niajuavyo
mimi yupo mle ndani na watu wengine, tuliwaambia wakae hapo kwa usalama wao,
sasa sijui kama anaweza kutoka,….kama kafanya hivyo, walinzi watafahamu ..ngoja
niwapigia.
‘Wala
usihangaike kuwapigia, ..huyu jamaa keshatoka humo, sijui kwanini kafanya
hivyo, namuona, na…watume watu wako wawe karibu naye ila wasifanye lolote la
kuwazua, kuna kaongozana naye, ..simuamini…’akasema.
‘Ni
nani huyo kaongozana naye..?’ akauliza.
‘Sijamtambua
bado,..ngoja, ..oh, nitakuambi-a, baadae…..kuna kitu nimekiona ..ok, baadae,
nakata simu mara moja..…’docta akakata simu.
Huku kwenye jengo, akaingia mdada mmoja.., huyu
anatokea nje, ni kama pacha wa yule wa ndani , hata kuvalia kwao,ila huyo yupo
tofauti usoni..
‘Huyu
mdada alikuwa kavaa sawa sawa na hao watu waliotokea ndani, kavalia vazi jeupe refu, lenye mikono mirefu,
na vazi hilo lina kitu kama kofia,..inayoshikiliwa kwa nyuma kutoka kwenye
gauni, kofia hiyo ni kama mtandio wa wanawake lakini ni duara, kama kofia,
inaonekana inavutoka, unaweza kuivuta hadi sehemu ya shingo, ila sehemu ya
mbele usoni inakuwa wazi.
Sasa
kwa huyu mdada aliyetoka nje, yeye kavaliwa mawani makubwa ya rangi nyesu ya
kufika sehemu kubwa ya usoni, ili mtu usitambulikane sura yake….kilichomvutia
docta zaidi ni sehemu ya miguuni, kavalia viatu vya aina yake..
‘Oh..hivi
viatu,…vinaonekana vya aina yake, ok…labda, lakini nahisi kuna kuna kitu hapa,..’
akasema hivyo, na hakuataka hisia zake ziwe za kutoka akilini, akawa anaiuliza
komputa kw..na kabla jibu halijatokea…mara simu yake ikalia, aliyekuwa akipiga
simu alikuwa ni mkuu, msaidizi wa kitup
cha polisi
‘Docta,
docta….kuna mtu kafika, na gari na sasa anaelekea eneo la makaburini yawezekana
ni yule mtu wetu,..kaja na taxi ya kukodi,walinzi wamejaribu kutafiti kuwa ni
nani, lakini hawajaweza kumtambua,kwa jinsi alivyovalia,…nahisi kavalia hivo
kuficha sura, kavalia koto refu …kichwani kofia pana, na mawani makubwa ya
rangi nyeusi, unaweza kumtafuta kuwa ni nani kwa haraka…’akaambiwa
Ikabidi
docta kwanza afanya hiyo kazi, ya mkuu , maana ni muhimu, huyo kwasasa ndiye
mkuu wake wa kazi, la sivyo angemkatalia kuwa kuna jambo jingine analifanya,…akawa
anamtafuta huyo mtu kwenye mtandao, kweli ..akamuona sasa hivi alikuwa kasha fika
maeneo ya mkaburini,…
‘Huyo
mtu ni nani…?’ akajiuliza docta
akimkagua kwanza huku akiweka sawa seehmu ya kuuliza,
‘Huyu
mtu anaweza kuwa ni miongoni mwa hawa watu …’akasema.
Huyo
mtu alichofanya kwanza hakuonyesha wapi anapoelekea, ila ni makaburini,
alichofanya yeye, ni kujifanya ni mmoja wa watu waliofika kuzika, kwani
kulikuwa na shughuli za mazishi zinaendelea, yeye akafika hapo na
kujichanganya, baadae akatoka hiyo sehemu na kuelekea kule kwenye kaburi,..kaburi
la binti wa mzee, akaangalia huku na kule alipoona hakuna mtu, akainama na
kushika upande wa lile kaburi
Halafu akainama na kuanza kusukuma,..likawa
lile mlango wa juu linasogea kirahisi tu,..na hapo docta akangiwa na hamasa
kiasi kwamba alisahau kumpa taarifa mkuu wake, kuwa huyo mtu ni nani, ni kwa
jinsi alivyoweza kutambua ni sehemu gani ya kugusa kwenye huo .mfuniko wa juu
wa hilo kaburi, na kuweza kuusukuma kwa kirahisi kabisa,..ina maana analijulia
hilo kaburi lilivyo.
Haikupita
muda, huyo mtu akazama ndani ya hilo shimo la kaburi…, na akawa anavuta ule
mfuniko kwa ndani ukajifunga,....sasa hapo docta akawa na hamu ya kumtambua huyu
mtu vyema ni nani, akaangalia sehemu aliyoulizia, na maelezo yakaja hivi;-
‘Huyo
mtu ni mgeni kwenye mtandao, ila anavyoonekana kajibadili sura,kwa kuvalia kitu
cha ziada, na kuficha sura yake halisi,…, ila yawezekana akawa kati ya hawa
watu hapa chini; ikatokea orodha ya majina ya watu, na docta hakuwa na nafasi
ya kuyakagua, kuwa hao watu ni akina nani huenda akampata mtu anayemfahamu.
Ilichukua
muda kuonyesha orodha ya watu, na docta akaachana nayo…akaamua kumuelezee mkuu wake
hicho alichokipata…na huku anavuta sehemu za kufuatilia nyendo za huyo mtu,
sasa alikuwa kwa ndani, na wakati anafanya hivyo, mara akaona ishara kuwa kuna
jambo muhimu kule kwenye jengo la biashara;
Akaacha kwanza huko makaburini na kuelekea
huko kwenye jengo la biashara.
************
Huku napo alimuona mpelelezi akiwa anamfuatilia
yule dada aliyetokea ndani….na yule dada alionyesha kama anataka kutoka nje ya
hilo jengo,…na mpelelezi sasa akawa nyuma yake, na huyo mdada hakuonyesha
ishara ya mashaka, ila bado alionekana akitembea kwa kuyumba yumba..
‘Itakuwa ni hatari kwa huyu mdada akifika barabarani, anaweza hata kugongwa, anavyotembea ni kama...ok,...'akasema na kumpigia simu mkuu, na wakati
anataka kufanya hivyo yule mdada akawa anayumba yumba anataka kudondoka, na
mpelelezi akamuwahi na kumdaka.
NB:
Nimechelewa kuanza kuandika hii story, lakini kwa matukio, ilikuwa hivyo,
najaribu kuyaweka matukio mengi kwa pamoja, japokuwa kila tukio lilikuwa na
taarifa yake ndefu tu yenye kutosheleza sehemu nzima ya kisa kwa siku
WAZO LA LEO: Utofauti wa
binadamu na wanyama wengine ni tabia, hulka yake ya kutambua baya na zuri. Ukiona
mwanadamu anafanya mambo mabaya kinyume na utu, kinyume na mienendo ya wanadamu
wenzake, ujua kuna walakini. Sasa iweje sasa mwanadamuu huyo huyo awe anafanya
mambo wanayofanya wanyawa wengine wasiojua kutofautisha zuri na baya,
wakajizalilisha, wakavaa uchi…eti kwa vile wameofanya hivyo ni wasanii
mashuhuri, wenye pesa na kujulikana
Je
kama kwa hao wao labda ilitokea bahati mbaya tu, nguo ikawavuka, tutaiga tu, au
wakitembea uchi, sisi tutaiga tu, au je kama kwao ni namna ya kutangaza propaganda
mbaya zenye muelekezo wakutangaza mauchafu yao, tabia zao chafu,kinyume na
maumbile ya mwanadamu, sisi tutaiga tu, kwanini hatutumii akili zetu kutafakari
mambo kabla ya kuyafanya, umhimu wake kwa jamii na muonekano wetu ..ni aibu na
fedhaha, kama tutakuwa tunaiga bila kutumia akili zetu…itafika sehemu wanyama wataonekana ni bora zaidi yetu…Tumuombe
mola wetu atuepushie na tabia hizo chafu.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment