Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, June 2, 2017

MPENZI WA FACEBOOK-42


Mpelelezi alijiinua pale kitandani, akajinyosha, bado alihisi mwili ukiwa na maumivu kila sehemu hasa sehemu ya mkono wa kushoto, bado mkono ulikuwa haukubali kunyoshwa,… bado kulikuwa na matatizo. Alipojaribu kumuuliza docta,…docta akasema;

 'Itachukua,muda kupona kabisa, cha muhimu kwa sasa uwe makini, usijitoneshe, na ingelifaa ukapata mapumziko ya muda mrefu, …yaani ukiona upo sawa, sisi tutakuruhusu, hata hivyo bado utahitajia kupumzika nyumbani kama miezi mitatu hivi kabla hujaweza kwenda kazini, jitahidi sana kufuata masharti, utapona kabisa….’akasema docta.

 ‘Nikae nyumbani miezi mingine mitatu!!..hapana…haiwezekani, …?’ akasema Mpelelezi akijikagua

‘Ndio,…inahitajia kupumzika, kwa kipindi hicho au hata zaidi itategemeana na kupona kwako…hiyo sehemu ni sehemy nyeti, hiyo risasi iligusa mfupa, na una bahati sana, lakini utapona kabisa, ni swala la muda tu..’ndivyo docta alivyomuambia, na alipoambiwa hivyo, akajua sasa kazi basi.., na ndoto zake za kujitahidi afikie cheo kikubwa zimekwisha..na huenda akizidi kukaa nyumbani, atalipwa nusu mshahara, mshahara wenyewe ni mdogo!

 Aliiwazia familia yake, akawazia watoto wake, ambao baadae alikuwa ameamua kuwahamisha na kuwapeleka, shule za kulipia,…na japokuwa imekuwa kazi kubwa kwake kuwalipia wote, na sasa alipojiunga na hilo kundi, waliweza kumpa pesa akawa analipia,..hakupenda ….

'Unajua haya maisha ni lazima uwe na malengo, ya mbali,…kwa hivi sasa tutakusaidia kulipia ada watito wako, tutakuanzishia miradi mbali mbali…miradi hiyo ni kwa maisha yako ya keshi,…unajua nikuambia kitu,.. hizi kazi zina leo na kesho, ukitegemea ajira tu…, ipo siku itatokea tatizo….’akaambiwa, kiukweli hakupenda na huyo mtu hakuchoka, akaendelea kumuelezea.

‘Hizi kazi zenu hizi , kwanza ni za hatari,..inaweza ikatokea, ukapatwa na matatizo makubwa ukashindwa hata kujilisha, huku familia inakutegemea,… na hao unaowatumikia hawatakujali tena, maana umuhimu wako ni pale unapoishika silaha, ukapambana na wahalifu au sio, hebu fikiria umefikia sehemu huwezi hata kuishika silaha, itakuwaje ndio maanaa mimi nakushauri hivyo,…utafuta njia nyingine ya kuingiza kipato...na njia ndio hii…’akaambiwa.

‘Tatizo njia yenu sio halali, ni haramu…’akamwambia

‘Ni tafsiri tu….na maneno ya watu, wewe ukifika kwa jamaa yetu, yupo jamaa mtaalamu anajua jinsi gani y a kukupa mawazo ya kuwekeza, mbinu za kupata pesa, ….mwenyewe utafurahi,…yeye huyo nina uhakika,… atakuonyesha njia mbali mbali, za kuwekeza wewe utachagua ipi inakufaa, au sio…kama hupendi hii, kuna nyingine,na…wanaweza kuutumia utaalam wako..ikibidi..’akaambiwa.

‘Utaalamu wangu!!!!....hahaha, mimi ni askari na utaalamu wangu ni wa kuitumikia nchi yangu kwa mambo yahusuyo usalama wa nchi..watautumiaje utaalamu wangu…’akamuuliza huyu mtu.

‘Wewe kubali tu …kujiunga…utajulishwa, nina uhakika hutajutia…na sio hivyo, watu wanavyosema, viitu kma hivyo havipo…lakini kama hutaki haya, usije kunilaumu!

 Akamkumbuka jinsi jamaa huyo alivyojitahidi kumshawishi, ili ajiunge na hilo kundi, na mpelelezi alipoonyesha msimamo wake, …na baadae ndio wakaanza kumfanyia vitimbwi…mwanzoni hakujua kuwa ni hao watu, lakini siku moja wakaamwambia waziwazi…, na wakati wanamuelezea hivyo binti yake yupo mahututi…hana pesa, …ana madeni…

Aliyakumbuka hayo kwasababu jana usiku alimuota huyo jamaa, jamaa ambaye litumwa kwake kumshawishi, alijua kuwa huyo jamaa alitumwa kwake , baada ya kulazimishwa kujiuna na hilo kundi bila hata kupenda, sasa jamaa huyo huyo akamjia kwenye ndoto,…sasa anaongea kwa kumkebehi...,

'Unaona sasa wewe, hapo ulipo ni sawa na kilema,… unafikiri nini, wewe ni kilema, mkono huo mmoja hautafanya kazi maisha mwko tena,..utaalamu wako wa shabaha hautakuwepo tena….ujasiri wako wa kupigana, wa kufanya mambo kwa haraka, kwa mikono yako miwili hautakuwepo tena..na kwa namna hiyo, thamani yako kama askari itakuwa zero…nani atakuthamini kwa hali kama hiyo tena, hakuna.

Hata wewe mwenye unaujua ukweli huo…umuhimu wa mtu…, muajiriwa ni pale akiwa kazini na ana afya , ukiwa mgonjwa, muajiri wako atakuona ni hasara, sasa wewe hapo ni hasara.. watakuvumilia kidogo baadae watakuambia ukapumzike nyumbani, na kukulipa nusu mshahara, baadae unastafishwa….’akaambiwa na huyo jamaa akiwa kwenye ndoto.

‘Nilikuambia haya awali,   hukutaka kunisikiliza ukafikiri mimi nataka kukuchuuza, haya ukaja kuingia kichwa kichwa, wakakutumia, lakini bado hukutimiza yale yaliyotakiwa ina maana ulikuwa ndumilakuwili au sio..… ungelikubaliana na mimi, ukajiunga kistaarabu, haya yote yasingelitokea,…

Na hata kama ingetokea hivyo…maana kazi yako ni ajali mkononi…, ukaumia,..bado usingelikuwa kwenye hali kama hiyo …mawazo na kujuta,..ukisema ningelijua….maana sasa ungelikuwa na miradi yako, inajiendesha yenyewe…, hata ukiwa unaumwa, , hata ukiwa kitandani…

‘Hebu sasa, muangalie binti yako alivyo sasa hivi hana raha, mkeo hana raha, watoto wengine halikadhalika, au wale sio watoto wako ehe……, binti yako hataki, hata,kuja kukuona,  unafikiri ni kwanini…mkeo anakuja lakini akikuangalia hana raha, unafikiri ni kwanini, na watoto wengine, wamefukuzwa shule, hawana ada, unafikiri watakuaonaje wewe, ni  baba gani wewe…

'Kwasababu wewe ni baba, asiye na malengo ya mbali,..chukulia mfano binti yako alikuambia nini, unakumbuka, alikuomba sana, umsomeshe..anataka kusoma awe docta, kufeli kwake kwa mara ya kwanza sio tatizo, angerudia tena, angelifanya vizuri… , ukamwambia, huna pesa za ziada, eti kwa vile hakufaulu kidato cha nne, huku unajifanya unampenda,…hahaha

‘Wewe kumpenda mtoto ni kumpa elimu bora…au … angalia watoto wa wenzako wanasoma shule za fedha,…wana cheo kama chako, kwanini…wanatumia akili ya kuona mbele…sasa wewe  kwann, huna akili yakufikiria..unafikiria kuua watu kwa risasi tu, au kuwakamata wahalifu au sio…sasa zawadi yake ndio hiyo…au utasema ulikuwa unaishi kwa jasho lako, su sio…haya wasomeshe hao watoto, jiulize ni kwanini, utasema mshahara wako ulikuwa hautoshi au…, kwann usitoshe,...kwasababu hutaki kufikiria mbali, sasa utakula jeuri yako…’akaambiwa na huyo jamaa akimkebehi kwa ulimi…

 Alijaribu kuikwepa hiyo ndoto,lakini kila akipatwa na usingizi , hiyo ndoto inamrejea tena na tena, na mwishowe akamuota sasa bint yake mwenyewe kamjia, akiwa kitandani, yeye hajiwezi, binti kaja kusimama kitandani kwake…hapo anaota , binti yake anasema;

'Baba, nimejua sasa wewe hunipendi,..hutupendi sisi watoto wako,… kama ungelikuwa unanipenda, kwanini hukukubaliana na hao wenzako werevu…ukawekeza biashara,…sasa umeacha mimi nateseka, umeacha mpaka hao wtu wananichukua na kunitesa, haya wewe ni jabari, askari shupavu, mbona ulishindwa kuniokoa kwenye mikono ya hao watu...’huyo binti akasema akiwa hana nguvu, mwili umelegea,

‘Sasa unaniona nilivyo, nipo kama zezeta, sijitambui, sijijui...’ Na aliposema hivyo, mate yalikuwa yakimtoka kama mlemavu, asiyeweza hata kuzuia mdomo wake….mate yanajitokea ovyo
 Ndoto hiyo ilimfanya Mpelelezi azindukane, na kukaa kitandani,,,japokuwa macho yaliashiria kuwa bado aan usingizi, madawa anayotumia yanamchosha…lakini kwa hali aliyoona kwa mtoto wake, na kwa hali aliyo nayo kwasasa…, akajikutaanashika kichwa,…na bila hata kutegemea akaanza kulia…hakujua ni kwanini machozi yamemjia ghafla hivyo…akalia sana…, hata alipochoka , akaanza kujipiga piga na mkono mmoja kifuani…, maana mkono mwingine hauwezi kuuinua,..mkono huo kwenye kwapa ndipo risasi ilipitia,….

 Baadae akatulia, akatuliza mawazo na kuanza kutafakari, ni nini hatima yake, ni nini amekipta baada ya haya yote,…haya ukiangalia , kikazi, sasa hivi hataaminika tena, maana, ataonekana alijiingiza kwenye makundi haramu,..hakuna atakayemuamini tena, hata akielezea ni kwanini…kwani wanamuuliza kama kulikuwa na tatizo kama hilo kwanini, hakusema...kwann, kwann, hizi kwann zinamfanya aonekane sio mtiifu tena, hakuweza kutekeleza majukumu yake vyema kiapo chake cha utii hakukitimiza.

 Na sasa akigeukio huko kwa hao watu waliomshawishi aliangalia kama kuna lolote amepata, amepata nini hakuna…ilikuwa ni ahadi tu…, utakuwa hivi, tutakufanyiwa hivi,  na zaidi alikuwa akipewa pesa,..lakini cha ajabu hizo pesa, japokuwa zilikuwa nyingi, zilikuwa kama pesa hewa, ni nyingi, lakini hazishikiki…, ni pesa chafu, unapata leo, siku kadhaa zimekwisha, pesa gani hizo...alifikia hatua akawa anamshuku mkewe kuwa labda ndiye anamuibia, lakini haikuwa hivyo, kumbe zile zilikuwa ni pesa chafu!

 Mawazo yakamzidi..akitaka kulala labda atatuliza kichwa, hakulaliki, kwni akilala anaandamwa na ndoto mbaya….sasa alitaka atoke nje,  angalau akajipe mazoezi, lakini sasa maumivu yalizidi kwasababu ya kujipiga piga…, akainamisha kichwa, lakini moyoni akasema, hakuna machozi tena…, hakuna kuwaza tena…, iliyobakia sasa ni vitendo, akakumbuka usia wa babu yake alipomuambia kuwa ameamua kujiunga na jeshi la polisi

'Sawa sawa mjukuu wangu, uwe jasiri kama mimi…, na hata ukienda huko vitani, usikubali kufa kikondoo, ufe kiume, ..ufe kama chui, au ufe kama paka, unajua siri ya paka, paka akiona hana upenyo wa kukimbia, anakurukia wewe mwenyewe..unasikia, usikubali kuwa msaliti, usikubali kuwa mnyonge ukatekwa, pambana kiume…’.

 Alipowaza hivyo akajitutumua..akahisi sasa mwili ukisisimuka, akitamani atoke nje,…na hakutaka kupoteza nafasi hiyo tena…., hakujali maumivu tena, hakujali maagizo ya docta tena…akasimama,  akajitutumua…akaangalia viatu vyake vipo wapi…akaviona akainama , akahisi maumivu lakini hakuijali  tena, akavivaa viatu vyake…, akavua zile nguo za hosp, akavaa nguo za kwake… , akaanza kutoka nje.

‘Sasa naenda kupambana na hao watu,…ama zangu ama zao…nitakufa ki—ki…, nitaenda kutimiza wajibu wangu…liwalo na liwe….’akasema lakini akilini akahis kama anajisuta

‘Utakwenda kupambana na nani, ….na una silaha gani,….jifikirie kwanza kabla ya kuchukua hatua..wewe ni askari shupavu, huwezi kuanza jambo bila ya mpangilio…utakufa kizembe wewe…’alipowaza hivyo, akatulia na kuwaza,

‘Kweli lazima kwanza niwe na mpango…natakiwa niende wapi, naenda kukutana na adui yangu wapi, kwanza adui yangu ni nani..hilo lipo wazi, …akakumbuka, sehemu ile ile alipojeruhiwa na silaha ndipo walipo wabaya wake, hasa huyo aliyemfanya hivyo, huyo ni lazima ajibu mapigo…jino kwa jino..huyo ndiye wa kwanza,….wengine watafuta, …’alipofikia hapo hakupotezea muda, ….akaanza kutembea kuelekea nje, ….

 Alipofika mlangoni,mara  akakutana na mkewe na bint yake…!

Oh….hatimaye wamekuja, lakini wamekuja kufuata nini…akawaangalia usoni…nyuso zao hazikuonyesha furaha kabisa,hwakuonyesha kuwa wamekuja kumuona mgonjwa, …maana yake ni nini, nyuso zao zilionyesha ajenda nyingine,..wanataabika, wana maisha magumu, hawana matumizi.

Akamuangalia binti yake…usoni hana furaha, hana furaha kwanini, kwasababu baba anaumwa, hapana, ni kwasababu anafikiria kuwa , sasa hatima yake imekwisha hatasoma tena…lakini hata hivyo, kwanini hafanani kma ilivyokuwa kwenye ndoto,…kuwa kawa kilema wa mwili…yupo salama, lakini usoni , nyoyoni hayupo salama…, kwanini, kwasababu ana baba asiyejua muelekeo wa mbele….sasa, nitawaonyesha kuwa mimi ni baba gani…’akataka kuanza kuondoka, lakini akataka kumuangalia na mkewe..

 Mkewe kama kawaida, hana furaha..usoni, tokea awali, hana furaha, atakuwa na furaha gani wakati kila anachokitaka, kinahusu pesa, na sasa ..na kabla, pesa ilikuwa haishikiki…haya kashauriwa na wenzake ajiunge na kikundi chenye muelekeo wa kuwekeza, kakataa…..imefika hatua, ….watoto wanafukuzwa shule…ada hakuna….wewe ni mume gani, …unajiita jasiri, askari shupavu, mbaona ushupavu wako hausaidiii familia yako…..hayo mawazo yalimfanya azidi kuchanganyikiwa…akaanza kutembea kutoka nje, hakuna kurudi nyuma hiyo….

Mama na binti yake wakawa wamesimama, sasa wameshikwa na mshangao huyu mtu anakwenda wapi, lakini nani ainue mdomo,….wanamuogopa…huyooo, anaelekea nje…huyoo, akachukua bajaji, huyoo, anaelekea huko huko walipomjeruhi…

**************

 Mimi nikiwa sehemu maalumu ambayo tumeambiwa tukae kwa muda kwa ajili ya usalama wetu, sikuwa na raha baada ya tukio lile….hadi sasa siwezi kula, nikihisi kile kilichotokea, damu, ....ubongo vilivyonirukia usoni, vilinifanya nijihisi vibaya…nahisi kama vile

 Kiukweli kama kuna tukio litanisumbua sana akili yangu, ni hilooo..hivyo ulishaona mtu anpigwa riasi kichwani…mbele tobo, lakini huku nyuma, kichwa kinafumuka…hao atu ni wanyama….Tukio hilo limenifanya nisiwe na hamu ya kula nyama kabisa, mawazo yakaniandama, hata ule ujasir wangu wa awali ukawa haupo tena.

Imenisumua sana hiyo hali, na wakati nawaza hayo, nikakumbuka jambo, nilitaka niongee na docta, lakini nikasita, nikaona labda, nifuate mawazo ya huyo mzee, labda kweli anaweza kunisaidia, nikakumbuka jinsi tulivyokutana naye hapo kwenye hilo tukio..jinsi alivyobadilika pale aliponiona nipo nyuma yake, na alikuwa akijiuliza je nimesikia yale aliyokuwa akiyaongea, ....

 Mimi akilini nikawa nawaza na kujiuliza inawezekanaje huyu jamaa aliyekuwa rafiki wa karibu wa mzee mwenzake…

'Siamini, yule mtu anajifanya yupo karibu na mzee mwenzake, kwa vile alikuwa mpangaji wake kumbe alikuwa na ajenda ya siri, alikuwa akimchunguza na  kupeleka taarifa huko kwenye hilo kundi. Ama kweli adui ya mtu ni mtu…

Yule mzee alipogeuka na kuona namuangalia kwa macho ya mshangao, akashtuka, lakini kwa ujanja akajifanya kuniongelesha kwa kusema;

'Hawa watu bwana wasumbufu kweli…, inabidi niwadanganye, kihivi umesikia nilivyowaambia hizo ni kamba za kuwaingiza kwenye mkenge, …mimi ni kiongozi muadilifu,..lazima nifanye kazi y akuwasiaidia polisi, wakifika tu,…wanakutana na polis,umeona ujanja wangu ee….'akasema na mimi sikumjibu kitu, alipoona nipo kimia akaendelea kusema:

'Unajua nilikuwa nakutafuta sana…kuna kitu nilitaka nikuambie, aheri, nimekuona,..unakumbuka kipindi kile mlipokuja awali, wewe na docta, eeh, mkasema mnamtafuta yule binti …niliwaza sana, nikajua wewe ulikuwa na mahusiano na yule binti,..nikaunga na kuunga,nikakumbuka, wale wazee walikuwa wakimtafuta mtu aliyempa…unakumbuka, …na nikajua, ni wewe, unabisha..’akasema na mim nikabakia kimia japokuwa moyoni nilianza kushtuka.

Sasa..unajua tena, hata mimi nilipitia huo ujana,…kama alijiua si yeye, bwana,…huwezi kumlaumu mtu wakati sio yeye aliyempa sumu au sio…..nikamezea, nikaacha kama ilivyo,kwanza mumejitolea sana kuisaidia hiyo familia, …lakini muhimu sio hilo…kuna kitu kingine nilitaka kukuambia…

Akamsogelea sasa akawa anaongea kwa kunong’ona

‘Unajua nimegundua kitu,kumbe yule msichana hajafa..yupo hai..niamini mimi nimemuona mimi kwa macho yangu, ndio hicho nilikuwa nakutafutia, sasa nimekuona, ..unasema tukaliongee hili sehemu tukiwa wawili, maana …unasikia, ni siri…hawajui watu, na wakijua huyo binti anaweza kuuwawa,..’akasema.

'Unasema nini….huyo binti yupo hai..'nikamjibu na hapo akapumua akijua keshaniteka mawazo wangu

'Unajua hayo matukio yote, yamegubikwa na ushirikina, sasa kama nilivyosikia, huyo bint hakufa...kuna mazingaumbwe yalichezwa….unataka nikuambie kila kitu…’akasema na mimi nikakaa kimia, kwanza nikiona kama ni mzaha, au huyu mzee anataka kuniteka mawazo, ili nisahau hayo niliyosikia akiyaongea, lakini…hapana kuna kitu, …nakumbuka hata yule kiongozi alipokuwa akiongea na yule mama, kuna kitu aliongea, lakini ….sio kuwa huyo bint yupo hai….

‘Haiwezekani,hawezi kuwa hai…’nikasema


‘Kama huamini, basi nitakwenda mimi na wewe mguu kwa mguu, hadi huko..ila kwa sharti moja….’akasema huyo mzee

NB: Hapo sasa...k

WAZO LA LEO: Moja ya fundisho la swaumu, ni kuijua njaa ilivyo,...ili ukimuona mwenzako ana njaa ujue jinsi gani anavyojisikia...kuna wenzetu wanaishi maisha ya shida, vita vimewazunguka, mabwana wakubwa wanashusha mabomu kila kona! Wahanga hawa wa vita, hawana sehemu ya kukimbilia, kisa nini...watu wanagombea mali...kisa nini..ubabe., na mengi wanayoyafahamu wao, kuuza silaha nk...sasa hawa watu wasio na hatia, wanakufa kwa njaa,..hawana amani tena, ndani ya nchi yao wenyewe.... sisi huku tunakula na kusaza, na kumwaga, hatujali tena mayatima, hatujali tena wazee, wajane, masikini...tunajaza vyakula vya kila aina mezani, ...je yule yatima, je yule ambaye hana hata cha kufuturia, hata maji, ..umewahi kumfikiria...sasa hivi hata maji ni gharama, mali ya asili ya mungu inauzwa,,...tuikumbuke njaa, ili tuwakumbuke na wenzetu wenye njaa...Ramadhani kareemu, na Ijumaa njema.

Ni mimi: emu-three

No comments :